A.
UTANGULIZI.
Ø Je
umewahi kusikia habari za Mwinjilisti ambaye amekasirika kwa sababu wenye
dhambi aliowahubiri wametubu na kuokolewa? Yona ni miongoni mwao
Ø Yeye
anaitwa Nabii asiyetii au Mmishionari
Mzalendo yeye alikuwa na uchungu dhidi ya watu ambao Mungu alikuwa amemtuma
akawahudumie, alikuwa mbishi muasi na mwenye ubinafsi wa hali ya juu alikosa
upendo na huruma na kama ungekuwa wewe na mimi Tusingelimtuma Yona kuwa Nabii
Ø Jina
lake Yona ni la kiibrania ambalo maana yake ni “Njiwa” Ni mwana wa Amittai ambaye maana yake ni kweli ya Mungu kutoka
Gath-Hepher ambayo ni kana ya wakati wa Agano jipya na ilikuwa karibu na Nazareth mahali
alipokulia Bwana Yesu
Ø Kitabu
kinahusu kufanya umisheni katika nchi ngeni na Mungu anamtumia Nabii asiyependa
kufanya umisheni wa kigeni kukiandika, Kitabu kinatufundisha jinsi Mungu
anavyojihusisha na mataifa mengine pia na kuwa hana upendeleo.
B. MWANDISHI
Ø Wanatheolojia
wengi wanaamini kuwa huenda kitabu kiliandikwa kati ya 780- 753 K.K mapema wakati wa utawala wa Yeroboamu wa pili
Ø Kuna
uwezekano kuwa alianza huduma yake wakati wa Nabii Elisha mwishoni kwani
kulingana na Tamaduni za Israel inasemekana kuwa ndiye mtoto wa mwanamke mjane
wa Sarepter ambaye Eliya alimfufua kutoka kwa wafu tarahe kamili inakisiwa ya
uandishi kuwa 780 K.K.
Ø Yesu
alinukuu Matukio ya Yona katika Mathayo 12; 39-41 Jambo linalothibitisha kuwa
kitabu chake kimevuviwa na sio hadithi tu kama watu wengine wanavyofikiri Yona
pia anatajwa katika 2Falme 14;23-25 kama mtu anayetambuliwa kuwa alikuwa Nabii
katika ufalme wa kaskazini wakati wa Yeroboamu wa pili mwaka 792-753 K.K.
C. HISTORIA YA WAASHURU WALENGWA.
Ø Watu
wa Ashuru walijulikana sana kwa ukatili wao baadhi ya watu waliochukuliwa
mateka na wafalme wa kiashuru waliwekwa katika visanduku vidogo vya chuma na
misumari na kupelekwa nje ya mji wa
Ninawi mji wao mkuu
Ø Visanduku
hivyo vilikuwa vidogo kiasi ambacho mtu hakuweza kukaa wala kusimamia waashuru
waliwaua wafungwa wengi kwa kuwakata miguu kila siku mguu moja na siku nyingine
mguu mmoja ili kuwafanya wasikie maumivu makali
Ø Wengine
walilazimishwa kuwachinja rafiki zao waliowafahamu zamani watu wengi waliona ni
afadhali kujiua kuliko kuwa kwenye mikono ya waninawi Nahumu 3;19
Ø Wanawake
waja wazito waliwapasua tumboni ili kuona ni jinsi gani kitoto kinakaa ndani ya
tumbo la mama zao.
Ø Inawezekana
hii ndio ilikuwa sababu iliyomfanya Yona kuchagua kufa kuliko kuwahubuiri watu
hawa katili aliokuwa amesikia habari zao na huenda pia Yona alifahamu kuwa
wangetumiwa na Mungu kuwaadhibu wa Israel. kwani mnamo mwaka wa 722 K.K. yaani
miaka 38 baada ya mahubiri ya Yona Waashuru waliivamia Israel na kuwachukua
mateka huko Ashuru
D. UPEKEE WA KITABU CHA YONA
Ø Kitabu
cha Yona ni Tofauti na Vitabu vingine vya kinabii kwa sababu ya maswala ya
msingi yafuatayo;-
1. Kimeandikwa
katika mtindo wa kihistoria kuliko Vitabu vingine vya kinabii ingawa kina kweli
nyingi ambazo zinaweza kuwa ni changamoto kubwa na kweli kuu ambazo zaweza
kufanya kazi katika maisha yetu leo.
2. Matendo
ya Mungu kwa asili katika kitabu hiki kina kweli kuu kuhusu Mungu kwa asili hii
inafundisha wazi kabisa kuwa Mungu yuko kila mahali na ni vigumu kukimbia au
kujificha mbali na uso wake Zaburi 139;7-12, kinafundisha pia kuwa Mungu ni
Bwana wa Historia, mataifa na Viumbe vyote na kuwa anahukumu kila jamii
inapokosea na anaweza kutumia asili kwa mfano alimtumia upepo, samaki mkubwa
mmea wa mtango, mnyoo Jua n.k. katika kukamilisha mpango wake kwa Yona kwenda
ninawi.
3. Kitabu
hiki kipekee sana kinasisistiza Umisheni
na kufunua Upendo wa Mungu na mpango wa Mungu wa wokovu sio kwa wayahudi
pekee bali kwa watu wote wa mataifa Yoote Matendo 10;34-35
4. Unabii
unaotegemea Conditional natural Prophecy Yona alitangaza kuwa Ninawi
utaharibiwa katika siku arobaini lakini haukuharibiwa mji kwa sababu watu
walitubu Yeremia 18;7-10
E. MGAWANYO
Ø Yona
kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
1. Wito
wa kwanza na upinzani wa Nabii sura ya 1-2
2. Wito
wa mara ya pili na Manung’uniko ya Nabii 3-4
F. MSTARI MKUU AU MISTARI YA MSINGI
Ø 2;9
Wokovu unatoka kwa Bwana
Ø 3;9
Nani ajuaye ya kuwa Mungu ataghairi na kusamehe
Ø 4;2
Najua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma si mwepesi wa hasira u
mwingi wa rehema nawe wagahiri mabaya.
G. MCHANGANUO
WA KITABU CHA YONA
Kukimbia wito wa Mungu sura ya 1-2.
Ø Yona
hakuwa na mshaka kuhusu nini Mungu alikuwa anataka kukifanyaalipokea ujumbe kwa
Mungu kabla na hivyo alifahamu sauti ya Mungu lakni kile ambacho mungu alikuwa
amemtuma kilikuwa kimemshagaza kumbuka wakati Mungu alipomwambia Petro aende
kwa Kornelio Matendo 10;1-29
Ø Ninawi
ulikuwa mji wa kipagani na mji mkuu wa Ashuru Utawala ambao ulikuwa ni adui
mkubwa wa Israel kwa miaka Mungu alisema
uovu wao umepanda juu mbele zangu Mwanzo 18;25 Kwa hivyo yona aliitwa kwenda
kuhubiri dhidi ya Ninawi lakini yona hakutaka kulitimiza Jukumu hilo hivyo
alikimbia kwenda mbali ingawa alijua wazi kuwa Mungu yuko mahali kote
Ø Kumbuka
Ninawi ilikuwa karibu kuluiko alikokuwa anakimbilia yaani Trshishi ambayo
inaaminika kuwa ni sehemu za Hispania ya leo Mbali sana kutoka Yaffa
Ø Kilichofuata
ni adhabu kwa ajili ya kutokutii kwa Yona lakini kwa upande mwinginie ni Rehema
za Mungu ni upendo wake kumrejeza Yona katika hali ya utii Waebrania 2;10-11.Mungu
alituma upepo mkali na mabaharia walifikiri kuwa meli ingevunjika.
Ø Katika
hali hizo zote za dhuruba Yona alikuwa amelala usingizi na hakuwa anajua nini
kinaendelea 1;6 matoleo mengine ya Biblia kama Septuagint inasema alikuwa
anakoroma
Ø Yona
alipoamsahwa alitoa ushuhuda wa ajabu kuwa anamwabudu “Mungu wa mbingu aliyeumba
bahari na nchi kavu …. Na ya kuwa ninakimbia mbele zake” jambo la kushangaza ni
kuwa zaidi ya kuasi kwake Yona alikuwa anashuhudia kuhusu Mungu wa kweli na
kabla ya kutupwa watu hao waliomba sasa si kwa miungu yao bali kwa Mungu wa
Yona 1;14 walitoa sadaka na kuweka nadhiri kwa Mungu huyo huenda waliahidi
kumtumikia Ushuhuda wa Yona ulileta matokeo na watu walitubu ingawaje yeye
alikuwa akielezea kukimbia kwake
Ø Yona
aliyatoa maisha yake kwa hiyari yake mwenyewe ili wale walikuwa kwenye meli
waweze kuokolewa 1;12
Ø Huenda
Yona alijua wazi kuwa kama Ninawi watatubu Mungu atawasamehe na kuwaokoa lakini
la kushangaza Yona mwenyewe hakuwa tayari kutubu na badala yake alikuwa tayari
kufa kuliko kwenda Ninawi hii inaonyesha jinsi ambavyo kuna hatari katika kuasi
mapenzi ya Mungu na na jinsi chuki dhidi ya wengine inavyoweza kutenda kazi
ndani ya mtu.
H.
KUHIFADHIWA
NA KUOKOLEWA.
Ø Mungu
hakuwa amemsahau mtumishi wake na bado alikuwa na mpango naye na huduma yake
kwa ajili ya watu wa Ninawi aliandaa samaki mkubwa Nyangumi na kummeza Yona
baadhi ya matoleo ya Biblia yanasema Mungu akaandaa au akachagua samaki mkubwa
hii inaonyesha uweza wa Mungu dhidi ya mambo ya asili kuwa Mungu aweza
kuyatumia mazingira au Viumbe katika kutimiza mpango wake,wengine wana fikiri
kuwa labda swala la kumezwa na nyangumi ni hadithi lakini kumbuka kuwa ni
mpango wa Mungu, Mungu aliandaa samaki mkubwa hii imerudiwa mara nne katika
kitabu cha Yona
Ø MAOMBI
KWA AJILI YA WOKOVU.
Yona
alifanya maombi na kujiuhukumu mwenyewe ndani ya samaki, lakini Mungu kwa
huruma yake na Neema wakati mwingine anaruhusu sisi kupitia hukumu zake ili
kwamba tumlilie yeye na kumtegemea yeye na kwa wakati huu sasa Yona alikuwa tayari
kwenda Ninawi na kumtii Bwana
alithibitisha kujitoa kwake kwa Mungu na
Furaha ikaujaza moyo wake.
I.
KUTII
WITO WA MUNGU MARA YA PILI.
-
Hakuna ajuaye ya kuwa Samaki alimpeleka wapi Yona
huenda alimtapika huko Ninawi hata hivyo hili si la muhimu hapa la muhimu ni
kuwa Yona alikubali wito wakati, Mungu alipomtuma mara ya pili.
-
Watu wengine hukataa wito wa Mungu na hawapati
nafasi ya pili ya kumtumikia Mungu wengine hufikiri ya kuwa huenda Mungu hata
watumia tena,Yona alitii neno la Bwana lilipomjia mara ya pili na alikwenda
Ninawi
-
Inakisiwa watu wapatao 600,000. Waliishi Ninawi na
vitongoji vyake ilimgharimu siku tatu Yona kuihubiri Ninawi ingawa alipewa siku
39. Ujumbe wake ulikuwa katika siku tatu ninawi utaangamia, kwa mujibu wa Luka
11;30 tunajua kuwa huenda Yona alimtumia
uzoefu wake wa kumkimbia Mungu na kuokolewa na hii ilikuwa ishara kwa watu wa
ninawi kutubu mji mzima na kumrudia Mungu
J. KUMFAHAMU MUNGU NA MTAZAMO WAKE SURA YA NNE
-
Mwinjilisti anakasirika kwa sababu wenye dhambi
wametubu hiki nacho ni kioja ni wazi
kuwa alijua kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na ya kuwa atawasamehe waninawi na
ndio maana alikimbia wala hakutaka waninawi waokolewe
-
Wakati waninawi wanatubu kwa kufunga, Yona alikuwa
anajijengea kibanda cha mapumziko kwa ajili yake nje ya mji akisubiri kwa
tumaini kuwa Mungu atawaangamiza na siku arobaini zikapita patupu!
-
Yona alikasirika alikuwa na tatizo Kiburi,Ubinafsi
na kukosa upendo alijihusisha sana na heshima yake kama Nabii ametabiri na Mungu
ataitimiza unabii wake alikuwa tayari kufa kuliko kurudi Israel na kusimulia kuwa
mahubiri yake yamewafanya Waninawi watubu na kuokolewa
-
Mungu ana namna yake anavyoweza kuyaangalia mambo
na kutuonyesha makosa yetu na kutufundisha mtazamo wake aliandaa mtango kumpa
Yona kivuli na Nabii wake mwenye hasira
akapumzika kisha akaandaa mnyoo upepo na jua kali vikaharibu kile kivuli Yona
akakasirika zaidi
-
Kumbuka kuwa mungu alimuuliza yona unaona vema
kukasirika hatupaswi kulaumu kile mungu anachokifanya Yona alijibu kuwa
anafanya vema kukasirika hata kufa Hasira husumbua watu wengi na husababisha
kifo au kupooza Srtokes
-
Mungu alikuwa akimfundisha Yona na sisi kuwa Yeye
ni mwingi wa Rehema Yona alifurahia
faraja zake na starehe zake kuliko
maisha ya watu 120,000 watoto wachanga na wanyonyao Mungu aliwajali wao kwani
anaupenda ulimwengu mzima Yohana 3;16.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni