A. MWANDISHI
WA KITABU CHA YOELI
Ø Mwandishi ni Yoel baadhi ya wasomi wanaamini
alikuwa mwana wa Samuel (Samuel 8;1-2.) lakini Maandiko yanamtaja kama mwana wa
Pethuel yaani uaminifu wa Mungu ingawa hatuna taarifa alizaliwa wapi na
historia yake si kubwa sana ingawa inaonekana ya kuwa alikuwa kuhani Yoel
1;13-14,2;1 na 14-17.
Ø Jina lake maana yake ni Yehova ni Mungu wasomi wengi wanaamini kuwa alikuwa kuhani hii
labda huenda inatokana na kujishughulisha kwake zaidi na maswala ya hekalu na
kushughulikia na majukumu ya kikuhani
1;13-14, 2;1, 14-17.Na mkazo wake katika kitabu chake chote unawafanya
wasomi kuamini hivyo.
Ø Inaonekana pia kuwa alikuwa anaishi Yudea na ni
maarufu sana kama Nabii wa Pentekoste.Kwa sababu ya kuzungumzia swala la ujio
wa Roho Mtakatifu katika Yoel 2; 28.
B.
TAREHE YA UANDISHI.
Ø Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Yoel
Haijulikani hasa ni lini Baadhi wanaamini kuwa huenda kiliandikwa wakati wa
baada ya Uhamisho wa Babel kwa sababu Yoel hajawataja waashuru wala wakaldayo
wala maswala ya kuabudu sanamu.
Ø Ingawaje baadhi ya wasomi wanaamini kuwa
uchanganuzi wa wadudu kama tunutu, Madumadu n.k ni Lugha ya mafumbo
inayohusiana na uvamizi wa majeshi ya kigeni hivyo kama hivyo ndivyo Basi
tarehe ya uandishi inaweza kuwa ni kabla ya utumwa na moja ya jambo
linalothibitisha kuwa hakikuandikwa wakati wa utumwa ni kwa sababu kinagusia
maswala ya ukuhani na hekalu hivyo kunauwezekano kikawa kimeandikwa 830 k.k.
kwani hekalu liliharibiwa mwaka wa 586 k.k.
C. HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA YOEL
2Falme 11; 1-12;3.
Ø Ukweli kuwa Yoeli anashughulika na makuhani
zaidi na sio wafalme unashuhudia ya kuwa kitabu huenda kiliandikwa wakati wa
Yehoiada kuhani mkuu ambaye ni mtu mkubwa aliyechaguliwa kusimamia maongozi kwa
sababu mfalme alikuwa mtoto hivyo Yoel hajazungumzia maswala ya mfalme katika
kitabu chake.
Ø Malkia wa Yuda Athalia alikuwa amewaongoza watu
katika kuabudu mabaali. Lakini Yehoiada aliwaongoza kurudi kwa Mungu Na huduma
ya Nabii Yoel ilichangia kuwarudisha watu kwa Mungu
Ø Athalia alikuwa mtoto wa mchawi malikia
Yezebeli aliyeolewa na Ahabu na aliolewa na Yehoramu mwana wa Yehoshafati
mfalme wa Yuda. Athalia aliwaongoza Yehoramu na Yuda kuenda mbali na Mungu kuabudu
baali na kufanya dhambi nyingine Yehoramu aliwaua nduguze 6 ili kujihakikishia
anabaki kwenye kiti cha kifalme na alipokufa mwanae Ahazia akawa Mfalme Badala
yake, Athalia alimchochea Ahazia katika kuabudu miungu na baada ya mwaka mmoja
aliuawa na Athalia alitawala na kutoa amri kuuawa kwa watoto woote wa Ahazia
yaani wajukuu wake na warithi wa kiti cha ufalme.
Ø Dada wa Ahazia alikuwa ni mke wa kuhani mkuu
Yehoiada na kwa neema ya Mungu aliweza kumuokoa moja ya wana wadogo
aliyeitwa Yoashi na kwa kuwa alikuwa na
umri mdogo miaka 7 Yehoiada aliongoza
makuhani na wazee wa Yuda kisiasa kufanya mapinduzi na kumfanya Yoashi kuwa
mfalme na Athalia akauawa.
Ø Yehoiada aliendelea kusaidia kuongoza mpaka
Yoashi alipofikia Umri wa kuweza kutawala.
D. UPEKEE
WA KITABU CHA YOEL NA UJUMBE WAKE
a.
Yoeli alisisitiza
kuhusu Siku ya Bwana, majukumu ya makuhani ambao ni muhimili wa dini na
kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mapigo yanayohusiana na nzige ni vitu
maalumu sana katika kitabu hiki.
b.
Kitabu
chote kialenga katika siku ya Bwana, huku Yoeli akitumia mifano ya Nzige
kuwaonya dhidi ya hukumu ya Mungu itakavyokua isipokuwa kama watatubu. Jambo
hili ingawaje linaenda zaidi ya hali halisi ya siku hizo kwani pia inazungumzia
juu ya dhiki ile kuu siku za mwisho ambapo hasira ya Mungu itashuka ulimwenguni.
Nzige (Locust)
Moja ya wadudu waharibifu wakubwa wa mazao kwa mujibu wa Yoel ni miongoni mwa
Majeshi ambayo Mungu angeyatumia kuwashambulia watu wasipotubu uovu wao Picha
na Maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.
E. MSTARI
WA MSINGI AU MISTARI YA MUHIMU
Yoeli
2;1 - Siku ya Bwana inakuja
Yoel
2;13. - Rarueni mioyo yenu
Yoel
2;28 - Nami nitawamwagia watu wangu Roho
yangu
Yoel
3;10 - Yeye aliye dhaifu na aseme mimi
ni Hodari
F. MGAWANYO
WA KITABU
Kitabu cha Yoeli kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
a. Nabii
anazungumza 1;2-2;17
b. Mungu
anazungumza 2;18-3;21
G. MCHANGANUO WA KITABU CHA YOELI
·
Hukumu
na toba Yoel 1;1-2;27
Yoeli
anatoa kwanza sababu za ujumbe 1;1, Neno la Bwana lilimjia, mara nyingi kile
ambacho Bwana aliwapa Manabii walitakiwa kuwaambia watu na Mungu alizungumza
wazi kulingana na mazingira yao nini cha kukifanya ili waepuke hukumu zake na kufurahia Baraka
zake zaidi
·
Mapigo
ya Nzige 1;2-0
Mapigo
ya nzige kulikuwa kitu cha kawaida katika mazingira yale lakini nzige hawa anaozungumza
Yoel ni wa Tofauti na hawajawahi kuonekana mstari 2-3 ilikuwa ni kitu ambacho
wazazi wangewasimulia kizazi kijacho cha watoto wao, kule kuonyesha kuwa wazazi
hawatasahahu ni wazi kuwa watu wanapomuacha Mungu kwa hakika hukumu ya Mungu
huwa inakuja juu yao bila mzaha, 2-4, Mstari wanne unaashiria labda vipindi vinne
vya uvamizi wa nzige au hatua zao za kukua
·
Baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa adhabu ya
aina hii ya nzige inawakilisha falme nne zilizoigandamiza Yuda na Israel kwa
miaka mingi
Ø Tunutu
– wanawakilisha Babeli
Ø Nzige
– wanawakilisha Waajemi na Waamedi
Ø Parare
- wanawakilisha Wayunani
Ø Madumadu
- wanawakilisha Warumi.
Hata
hivyo baadhi ya wanatheolojia wanasema hawa walikuwa ni wadudu halisi na
hawakuwakilisha falme yoyote I; 4 na 2;25-26
H. WITO WA KUTUBU 1;2-2;17
Ø Yoeli
aliwaita watu woote kutubu kuanzia na Viongozi 1;2,3,14, 2;15-16 na wote
walioishi juu ya nchi 1;2,3,14, Watoto wachanga na wanyonyao 2;16, Walevi 1;5 wakulima
na watunzaji wa mizabibu 1;11 makuhani 1;13,14,2;15,2;1,15,17.bwana harusi na
bibi harusi 2;16,8 walitakiwa kuomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mume wa
ujana wake, walitakiwa kufunga na kuomba na kuitakasa siku ya bwana hili lilikuwa linadhihirisha nini watu
wanatakiwa kukifanya ili kuepuka hukumu ya Mungu
Ø Yoeli
aliwahakikishia watu kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na huruma na neema na si
mwepesi wa hasira na kuwa hughairi mabaya
Ø Uamsho
lazima uanze na Viongozi wa kidini hivyo
makuhani waliagizwa kuomboleza kati ya patakatifu na madhabahu
I. KUREJESHWA KWA BARAKA ZA MUNGU 2;18-27
Ø Yoeli
2;18-27 Inatoa majibu ya Mungu kwa maombi ya Nabii, makuhani na watu wote, toba
ya kweli inapofanyika Mungu Huiheshimu na kuikubali, hivyo Mungu alihaidi
kuwaondolea Mbali nzige na kuwa angerejesha mazao na mavuno yangepatikana, miti
ya matunda ingezaa na mashamba yangezalisha mavuno mengi
Ø Baadhi
ya wasomi wanatafasiri kuwa Yoel 2;20
jeshi la kaskazini kuwa kama ni Ashuru lakini mstari wa 25 unaweka wazi
kuwa Mungu anamaanisha ni nzige halisi
Ø Ingawaje
namna atakavyo wafukuza nzige hao kungewatia moyo watu wake kumuamini kwa wokovu dhidi ya
majeshi ya wageni
Ø Yoeli
2;21-27 inakazia maswala ya kiroho na Baraka ambazo zingewajilia watu wa Mungu,Baraka
hizo za kimwili na kiroho zingeipata Yuda kama wataamua kumgeukia Mungu na hii
pia iliwakilisha Baraka ambazo zingewapata kwa kumuamini Yesu wakati wa miaka
1000 ya Utawala wake duniani.
J. SIKU ZA MWISHO 2;28-3;21
Ø Kwa
Maneno Hata itakuwa baada ya hayo 2;28 Nabii alimaanisha kuhusu wakati ujao
mbali kutakuwa na utembeleo maalumu na hukumu
A.
Kumwagwa
kwa Roho Mtakatifu 2;28-29
Ø Watu
woote wa Mungu wangejazwa Roho Mtakatifu na kuna makundi sita yanatajwa kama
ambao wangetembelewa na Roho Mtakatifu Wana wenu, binti zenu, vijana, wazee
wanaume na wanawake.
Ø Hiki
alicho kitabiri Yoeli kilitimia kuanzia siku ya Pentecost Matendo 2;17-18 Petro
aliitumia tafasiri ya siku za mwisho na kuendelea kwa kawaida siku za mwisho
zilianza na Kuzaliwa kwa kanisa siku ya
Pentecost na kuendelea katika kipindi chote cha kanisa, Mungu aliwajaza watu wa
chache Roho wake kwa kusudi maalumu lakini sasa anasema kwa watu woote kila mtu
atakuwa na sehemu katika utumishi wa kazi yake Sehemu hii pia ya unabii wa
Yoeli unaeleza nini kitatokea kutokana na kumwagwa huko kwa Roho wa Mungu, watu
watatabiri, wataota ndoto, na kuona maono
Ø Ishara
hizi zoote zinafunua ushahidi wa Agano la kale
Mungu angaeendelea katika namna kama hiyo iliyokuwa wazi wakati wa Agano
la kale kujifunua mwenyewe lakini kwa
upana zaidi katika Agano jipya
B.
Dhiki
kuu 2;30-32.
Ø Ishara
na maajabu yanayotajwa katika mstari wa 30-32 yatatukia mwisho wa kipindi
cha kanisa, Danieli alisema kutakuwa na kipindi cha dhiki ambayo
haijawahi kuweko tangu kuumbwa kwa ulimwengu
lakini katika wakati huo watu wako kila atakayeonekana jina lake
limeandikwa katika kitabu cha uzima wataokolewa Daniel 12;1, Tunaona katika
Ufunuo 6;12-14 kile ambacho Yoel alitabiri lakini kwa undani zaidi
Ø Tetemeko
kuu jua kutiwa Giza na kuwa jeusi mwezi kuwa mwekundu kama damu lakini wale
watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.
C.
Hukumu
ya Mataifa 3;1-16 Isaya 2.
Ø Mwishoni
mwa dhiki ile kuu kutakuwa na hukumu kubwa kwa kuanziwa na vita vya Armageddon
watu wa Mungu watakapokuwa wamepatwa na maangamizo makubwa mwishoni wataliitia
jina la Bwana kwa wokovu 5;15
Ø Maombi
ya Israel wakati huu yatakuwa watelemshe
mashujaa wako ee Bwana Yoel 3;11 na Isaya 64;1
Ø Yesu
atakuja na watakatifu wake na jeshi la malaika
na atamshughulikia mpinga Kristo na Israel watakapomuona watatubu na
kumtambua kama Bwana na mwokozi wao, Kisha hukumu ya mataifa itachukua nafasi
yake na mataifa yoote yatahukumiwa katika msingi wa namna wanavyoshughulika na
Israel na kanisa.
D.
Utawala
wa Yesu Kristo wa Miaka 1000. 3;17-21 Isaya 35
Ø Ujumbe
wa Yoeli unamalizikia na Baraka kubwa iliyohaidiwa kwa watu wa Mungu
o
Bwana atakuwa kimbilio lao na Ngome yao kuu sana
3;16
o
Bwana atakaa katika Sayuni 17,21
o
Yerusalemu watakuwa watakatifu na haitovamiwa tena mstari
wa 17
o
Israel itapata chemuchemu za maji na nchi itakuwa
yenye kuzalisha sana mstari wa 18 na Yuda itadumu milele mstari wa 20. Mungu
atawasamehe Israel Mstari wa 21.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni