Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Nabii Hosea



A.       Mwandishi wa kitabu cha Hosea.

-          Alikuwa Nabii kwa Israel katika Dakika za mwishoni kabla kidogo sana Israel kuanguka katika mikono ya waashuru mwaka 722 K.K
-          Ni Nabii maarufu kama Nabii wa Upendo na uaminifu jina lake Hosea ni la Kiebrania Hoshea ambalo maana yake ni wokovu au msaada,jina kama Yoshua na Yesu yanatokea katika mzizi wa jina kama hilo.
-          Ni wazi kuwa Hosea alikuwa Mwiisrael alizungumza kama ndugu na aliyataja mataifa kama Lebanon,Tabori, Bethel na Samaria
-          Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa alikuwa na asili ya ukuhani kutokana na kutaja kwake maswala mengi yanayohusiana na ukuhani
-          Alikuwa na Mambo mengi ya kukatisha tamaa aliyokutana nayo katika familia yake, Huduma na hali halisi ya Taifa lake.
-          Hosea anazungumza na kuonyesha kwa nguvu upendo wa Mungu kwa Israel licha ya kuwa na uovu mwingi, Dhuluma, mateso, udanganyifu, Rushwa, kukosa uvumilivu, ulevi na maisha ya anasa, Mungu aliwataka warejee kwake.

B.       Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Hosea.

Inakisiwa kuwa kati ya Mwaka wa 750-725 wakati wa utawala wa Uzzia, Jothamu, Ahazi na Hezekia Mfalme wa Yuda na Yeroboamu ii mfalme wa Israel Inaonekana Nabii ananukuu Wafalme wa upande wa Yuda kwa sababu kwanza alikuwa anaamini kuwa walikuwa wafalme wa kweli na warithi halisi wa kiti cha enzi cha Daudi pili wafalme wengi wa Israel waliomfuta Yeroboamu wa ii walioishi muda mfupi sana na kuuawa hivyo huenda majina mengi yangeorodheshwa mfano ni orodha hii ifuatayo;-                            

                                                    Utawala wa wafalme wa Israel 2Falme 14-18

Yeroboamu
Miaka 41
2  Falme 14;23-29
Alikufa
Zekaria
Miezi 6
               15;8-12
Aliuawa
Shalumu
Mwezi 1
               15;13-15
Aliuawa
Manahemu
Miaka 10
               15;16-22
Alikufa
Pekaiya
Miaka 2
               15;23-26
Aliuawa
Peka
Miaka 20
               15;27-31
Aliuawa
Hoshea
Miaka 9
               17;1-41
Alifungwa.

                                    Mwisho wa utawala wa Israel wakachukuliwa utumwani Ashuru

-          Watu wa Israel walikuwa wamekataa kurudi kwa Mungu Pamoja na mahubiri ya Nabii Amosi na matokeo hali ilizidi kuwa mbaya
-          Badala ya kumrudia Mungu watu waliendelea kuwa waasi huku wakiwaua wafalme wakifanya mapinduzi kwa mapinduzi Mafalme Tiglath – Pileser wa Ashuru aliishinda mashariki ya kati na kupanua mipaka yake mpaka Misri na mataifa yoote  yaliyotawaliwa yalitakiwa kulipa kodi kwa waashuru
-          Syria na Israel waliamua kuishambulia Yuda kwa sababu walikataa kuungana nao katika kuasi kulipa kodi kwa Ashuru
-          Hivyo Mfale Hoshea aligoma kulipa kodi na akaomba msaada Misri kuungana nae katika kujitoa chini ya utawala wa Waashuru jambo hili lilisababisha uvamizi wa majeshi ya waashuru huko Israel na kuwahamisha ambapo Hoshea mfalme aliwekwa kizuizini.

C.       DHAMBI YA ISRAEL ZILIKUWA  SURA YA  4-10

*      Kukosa maarifa ya kumjua Mungu Hosea 4;6,11
*      Kiburi 5;5
*      Kutokuridhika 6;4
*      Udunia na kuwa kama mataifa  7;8
*      Rushwa 9;9
*      Kurudi nyuma 11;7
*      Kuabudu sanamu 13; 2,4;11-12.

D.      Upekee wa kitabu cha Hosea na ujumbe wake.

-          Hosea ni mojawapo ya kitabu kirefu ukilinganisha na vingine katika Manabii wadogo na kinakaribiana kidogo na cha Zekaria
-          Ujumbe wake unawezekana ulitolewa kwa muda mrefu kiasi kwani kitabu kinaonyesha Upendo wa Mungu kwa Taifa lisilo na uaminifu la Israel na kinatumia maisha ya Mwandishi yaani Nabii Hosea kama mfano hai wa jinsi Mungu anavyojisikia kuhusu watu wake
-          Hosea anaonya  juu ya hukumu inayokuja ambayo inaweza kuepukika kwa kumrudia Mungu tu

E.       Mstari mkuu na mistari ya Msingi.

-          Kiini kikuu cha kitabu hiki ni Pendo la Mungu kwa Israel na hukumu dhidi ya dhambi
2; 19, 4;1, 4;6, 6;6, 7;8, 8;7.

F.       Mgawanyo wa kitabu cha Hosea

-          Zinaa ya Israel ilikuwa ni kukosa uaminifu kwa Mungu sura ya 1-3
-          Hoja za kinabii kutokumcha Mungu na hukumu ijayo isiyoepukika 4-13
-          Kuamini kwa Israel na kusamehewa sura ya 14;

G.      Mchanganuo wa kitabu cha Hosea

a.       Familia ya Hosea na Israel sura 1-3
i.                     Mungu alimuagiza Hosea kuoa mwanamke kahaba hata hivyo kuna mjadala wa kitheolojia kuhusu ukahaba wa mke wa Hosea kuwa ulikuwa ni ukahaba wa aina ipi Zinaa au kuabudu miungu ambako nako kuliambatana na ibada za zinaa? Katika Israel wazinzi walipigwa mawe je ni zinaa ya aina gani?
ii.                    Mungu alitaka kuwafundisha Israel kitu  kwani walikuwa wazinzi kiroho na Hosea alikuwa ndio somo lenyewe
iii.                  Mungu huihesabu tabia ya kuabudu miungu kama zinaa ya kiroho na kwa kuwa Hosea alikuwa mwaminifu kwa mkewe Gomeri ambaye Yeye hakuwa mwaminifu ndivyo na Mungu alivyokuwa mwaminifu kwa Israel.
iv.                  Hosea aliwaita wanawe majina yaliyokuwa yakiashiria unabii.
1.       Yezreel jina hili lilikuwa na maana ya kuwa Mungu “ametawanya au Muangu atapanda” hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha watu wa mji wa Yezreel juu ya mauaji yaliyofanyika Yehu alipokuwa mfalme,Yehu aliagizwa na Mungu kuwashughulikia watoto wa Ahabu lakini aliwashughulikia zaidi ya kiwango kwa sababu ya ubinafsi aliwaua watoto70 wa Ahabu huko Yezreel, Mungu alimwambia Yehu kuwa wanawe kizazi cha nne watamiliki kiti cha enzi, Yeroboamu wa pili alikuwa ni uzao wa tatu na Zekaria mwane ndipo unabii ulikuja kutimia 2Falme 10;30,1-8,Zekaria alitawala miezi sita tu kisha akauawa
2.       Lakini hata Hivyo Yezreel walikuwa na ujumbe mzuri pia  kuwa Mungu hupanda 1;45 yaani pamoja na kuwa wana wa Israel walichukuliwa mateka utumwani Mungu angewarejeza tena katika inchi yao
3.       Lo-Ruhama 1;6-7 mtoto mwingine wa Hosea jina hili maana yake Hakuna rehema
4.       Lo-Ammi maana yake sio watu wangu 1;8-9 majina haya mawili yanatufundisha na kuwakumbusha wana wa Israel na Gomeri juu ya dhambi zao na jinsi walivyolivunja agano lao na Mungu
v.                    Kwa mujibu wa sheria ya Musa wazinzi walitakiwa kuuawa kwa mawe lakini Hosea alimpenda mkewe na Mungu aliipenda Israel hivyo Gomeri na Israel walikuwa wanapewa Muda ili kwamba waweze kubadilika lakini haikuwezekana na hivyo talaka iliwakumba wote
vi.                  Mwishowe Hosea aliamua kumrudia tena mkewe na Mungu alikusudia kuwarejeza tena Israel matukio haya yana mambo ya kutufundisha sisi wa kizazi hiki cha leo
vii.                 Kwa ufupi sura ya 1-3 Inazungumzia maisha ya kielelezo ya Nabii Hosea ambaye anamwakilisha Mungu  Hosea alimuoa mwanamke kahaba anayefanya zinaa kwa sababu hatosheki na mume mmoja hatosheki ashiki zake ni Malaya anafanya zinaa pia kwa ajili ya kupata faida mapato, Huyo ni Gomeri mke wa Hosea anayeiwakilisha Israel, Baada ya kuwa amezaa watoto watatu alimwachia Hosea watoto hao na kwenda kuishi na mwanaume mwingine, wanaume wengine wakamgombea na ikalazimu wamuuze mnadani ndipo Hosea akamnunua  kwa upendo akamrudisha nyumbani.

b.       Ujumbe wa Nabii Sura ya 4-14

i.                     Kuanzia sura ya nne hadi ya 14 Nabii analeta mashtaka ya Mungu kwa wana wa Israel
1.       Anaonyesha jinsi ambavyo hakuna rehema, Hakuna kweli, hakuna kumjua wala kumjali Mungu katika Israel
2.       Kwa kusudi walijiingiza katika Ibada za sanamu na kuabudu miungu mingine
3.       Nabii anatoa wito wa kutubu lakini Israel wanakataa na kuendelea na dhambi zao
ii.                    Kwa kukataa kwao kutubu Nabii analeta ujumbe wa adhabu kwao anaitabiria Samaria kuanguka na Yuda pia wataadhibiwa
iii.                  Mwisho Nabii anatabiri kurejezwa upya kwa Yuda na Israel kuwa taifa moja na nchi moja na kuwa baadae watamtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao bila shaka huu uatakuwa wakati wa utawala wa miaka 1000 ya Kristo Duniani.

Nabii Amosi


AMOSI: NABII WA UTAKATIFU

A.      UTANGULIZI
-          Amosi alikuwa miongoni mwa wanamapinduzi wakubwa katika Isarael huduma yake ilifanyika kipindi ambacho Israel walikuwa wameharibika vibaya  na walikuwa katika wakati wa mafanikio na starehe ambazo ziliwafanya Israel  kuishi maisha ya dhambi
-          Jina lake maana yake ni “Mbeba mzigo” alikuwa na mzigo wa kutimiza agizo Mungu alilokuwa amempa kulitangaza neno la bwana wakati wa ukengeufu mkubwa wa Israel alizaliwa katika kijiji kiitwacho Tekoa miles 12 hivi kutoka Yerusalem
-          Alikuwa Mchungaji wa Kondoo na mtunzaji wa miti ya mikuyu hakuwa Nabii aliyesomea  7;14 lakini alikuwa mnenaji Hodari “Great orator”Asili ndiyo ilikuwa shule yake na anga ubao wake 5;8 Neno lake linaonyesha historia yeke 3;8
-          Amosi alikuwa mtu wa Yuda ingawa alitumwa kwa Ufalme wa Israel

 
Pichani Juu wachungaji wakichunga kondoo katika uwanda wa mashamba ya ngano huko Tekoa mahali alikotokea Nabii Amosi Tekoa iko mail 12 hivi kutoka Yerusalemu katika tawala za Yuda Picha kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote 

B.     TAREHE YA UIANDISHI.
-          Kitabu kiliandikwa mwaka wa 755 K.K. wakati wa utawala wa Yeroboamu II mfalme wa Isarael na Uzziah Mfalme wa Yuda


C.     WASIFU WAKE.
-          Amosi alikuwa Mnyenyekevu na wala hakijaribu kuficha maisha yake ya huko nyuma 7;14
-          Alikuwa na Hekima  katika kupeleka kwake ujumbe alimtumia misamiati amabayo ilikuwa wazi na ya kivitendo
-          Alikuwa mtu Imara thabiti alikataa kugeuzwa na Amazia kuhani mwakilishi wa Yeroboamu huko Betheli 7; 10-17.

D.     HISTORIA YA WALENGWA.
-          Wakati huu Israel walikuwa wanaishi maisha ya anasa na mafanikio makubwa sana hata hivyo baadhi ya matajiri waliupata kutokana na dhuluma
*      Masikini walikandamizwa Amosi 5;7,11
*      Mahakimu au Waamuzi walikuwa wakipokea Rushwa Amosi 5;12
*      Wafanya Biashara hawakutumia mizani za halali Amosi 8;5-6
*      Wenye haki waliuzwa utumwani amosi 2;7
*      Kulikuwa na uashaerati usio wa kawaida hata Baba na Mtoto waliweza kutembea na mwanamke mmoja Amosi 2;7.
*      Waliwakataza Manabii kuhubiri Amosi 2;7.
*      Watu walioishi maisha ya Stareha na anasa Amosi 6;1
*      Uasi wa kidini ulitawala Amosi 4;4-5, 5;21-23
-          Utawala ambao ungeiangamiza Israel ingawa haujaelezwa ni Ashuru.

E.     WAZO KUU NA MISTARI YA MSINGI.
-          Wazo kuu katika kitabu hiki ni Samaria Inavuna hukumu,amosi alikuwa  ni Nabii wa kwanza kutamka anguko la Samaria au Israel ambalo lilitimia miaka 40 baadaye ujumbe wake ulikuwa hukumu ya Mungu kwa sababu ya Kukosekana kwa haki katika jamii
-          Mstari mkuu au wa msingi ni
-          Amosi 3;3 Je wawili waweza kutembea Pamoja isipokuwa wamepatana?
-          Amosi 4;11-12 “Jiandae kukutana na bwana Mungu wako”
-          Amosi 6;1 ole wao wanaostareha katika Sayuni

F.      MGAWANYIKO WA KITABU CHA AMOSI.
-          Hukumu ya mataifa sura ya 1-2
-          Hukumu ya Israel sura ya 3-6
-          Uchanganuzi wa hukumu 7-9;10
-          Ahadi ya kurejeshwa upya 9; 11-15.

G.     MCHANGANUO WA KITABU CHA AMOSI
-           Kabla ya kutangaza hukumu  dhidi ya Yuda na Israel Nabii anachagua mataqifa kama sita hivi  ambayo pia aliyatangazia hukumu ya Mungu
-          Matatu kati ya hayo ni Dameski Syria,Gaza kwa wafilisti na Tiro ambao hawa hawakuwa na uhusiano wa kindugu na Israel bna yuda
-          Mataifa mengine matatu ambao walikuwa na uhusiano wa kidugu na Israel na Yuda ni Edomu, Ammoni na Moabu.
-          Kila tamko la hukumu kwa mataifa ya jirani na Israel na Yuda ilianza na “Haya ndiyo asemayo Bwana kwa makosa matatu naam kwa makosa manne sitazuia adhabu….”
-          Mtindo huu unamaanisha maovu yaliyopita kiasi na ya kuwa maovu hayo yaliongezeka mwaka kwa mwaka
-          Amosi ndiye mwanzilishi wa mtindo wa kuliita taifa kupitia jina la mji mkuu wake mfano anapoizungumzia Yuda anaitaja kama Yerusalem na Israel kama samaria.

A.      HUKUMU DHIDI YA DAMESKI SYRIA 1;3-5
-           Dameski ulikuwa ni mji mkuu wa Syria na hapa Syria inatangqaziwa hukumu kwa sababu ya kulitendea vibaya Gileadi Gileadi ulikuwa mji wa kale wa kabila ya nusu ya Manase ambao walibaki ng’ambo ya Yordani watu walipokuja kuitamalaki inchi ya mkanaani,
-          Dameski waliwachukuwa watumwa au mateka kwa vyombo vya chuma na kuwaburu za kama mtu avunaye ngano mungu anahaidi kushusha moto na kuwateketeza

B.      HUKUMU DHIDI YA GAZA 1;6-8
-          Gaza ulikuwa mji mkuu wa wafilisti  kusini magharibi ya Yerusalem,Dhambi yao ilikuwa ni kusafirisha watumwa waliwachukuwa watu walioishi vijijini  hususani waisreal na kuwauza huko edomu kama watumwa
-          Mungu anaahidi kuwaletea hukumu ya kuwateketeza kwa Moto na kuuchoma mji na majumba yake.

C.      HUKUMU DHIDI YA TIRO 1;9-10
-          Tiro iko kaskazini mwa pwani ya Israel na mji uliokuwa kutuo kikuuu cha bahari au bandari Isaya ,Yeremia na Ezekiel waliitangazia hukumu maalumu ulikuwa mji mkuu sana wa kibiashara  na kajhba mkuu wa wakati ule
-          Inaonekana waliwachukuwa watu fualni kabila nzima huenda Waisrael na kuwatia mikononi mwa Edomu hivyo dhambi yao ilikuwa ni kufanya biashara ya utumwa na Edomu na walisahau agano la undugu huenda hili lilikuwa ni agqano walilolifanya Daudi na Hiramu katika 2samuel 5;11
-          Hukumu yao ni moto na kuharibiwa majumba yake na ni kweli Nebukadneza alijaribu kuuteka tiro lakini si kwa mafanikio sana na mwishoni  uliharibiwa vibaya na Alexander mkuu.

D.      HUKUMU DHIDI YA EDOMU 1;11-12
-          Hwa walikuwa ni uzao wa Esau pacha wa Yakobo na walioishi kusini mwa bahari iliyokufa  sehemu iliyoitwa araba, wao wanahukumiwa kwa Matendo yasiyo ya kindugu,alimtumia upanga na mateso hawakuwa na huruma na walikuwa na kisasi cha hasira kwa siku nyingi na wanatangaziwa hukumu nya moto juu ya temmani na Borsa  miongoni mwa miji yao mikubwa na kuiteketeza.

E.       HUKUMU DHIDI YA WAAMONI 1;13-14
-          Waamoni na wamoabu ni Watoto,wajukuu wa Lutu waliozaliwa kutokana na zinaa ya baba na watoto wake wa kike  Mwazno 19;30-38
-          Wao wanahukumiwa kwa sabau ya ukatili wao kwa Gileadi ,waliwapasua wanawake wenye mimba wa Gileadi wanatangaziwa hukumu dhidi ya mji wao mkuu  Raba au Raboth-ammoni
-          Inaaminika kuwa huko ndiko Daudi alikoagiza Yoabu kuhakikisha Uria anauwa vitani 2Samuel 11.

F.       HUKUMU DHIDI YA WAMOABU 2;1-3
-          Hawa walikuwa na kosa la kuichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu  hata ikawa chokaa inaonekana hawakumpata akiwa hai hivyo kwa hasira walilipa kisasi kwa mifupa ya mfalme Isaya 15;5,16;11 Yeremia 48;36
-          Wamoabu walihukumiwa kwa moto ,na kuuawa kwa Viongozi ,Waamuzi na watu wakuu
-          Mungu anafuatilia sio tu mataifa wanavyolifanyia taifa la watu wake bali hata kila taifa linavyolifanyia lingine.

G.      HUKUMU DHIDI YA YUDA 2;4-5
-          Tofauti na mataifa haya mengine ya kidunia sita Nabii anaigeukia Yuda ambao ni ufalme wa kusini lakini hawa wanahukumiwa kwa kutokishika Sheria ya Mungu hivyo wao wanahukumiwa kwa maswala ya kidini yaani walikengeika na kuiacha Shetia ya Bwana
-          Waliishi kama watu wa dunia  nao watahukumiwa kwa moto na majumba yao kuteketezwa

H.      HUKUMU DHIDI YA ISRAEL 3;1-6
-          Pamoja na matangazo yoote hayo ya hukumu mungu alikuwa akiilenga Israel wao ndio wanaoonekana kuwa na dhambi nyingi zaidi kuliko mataifa mengine mlomlongo wa msururu wa dhambi kwa Israel ni mkuu sana  walionea masuikini,waliwauza watu wenye haki ,waliabudu sanamu,waliifanya biashara ya utumwa, waliwafanya wanadhiri kuvunja nadhiri zao na kulitii unajisi jina la bwana
-          Amosi aliorodhesha dhambi nyingi za Israel kuliko za mataifa mengine huenda ili kuonyesha hatia kubwa waliyokuwa nayo na pia kwa sababu alikuwa akiihubiri Israel na kuwaonyesha uhakika ya kuwa Mungu angewahukumu wao.
-          Mungu anaihukumu Israel na kuwatangazia hukumu hivyo akisisitiza katika matangazo makuu matatu yoote yakianzia na neno lisikieni 3;1,4;1,5;1 na katika 3;3 anauliza je wawili waweza kutembea Pamoja isipokuwa wamepatana? Mungu alikuwa anahoji anawezaje kutembea na Israel na kukubaliana nao huku wanatembea dhambini
-          Amosdi alimtumia hata mifano kama simba na mawindo,Mtego na tarumbeta  ili kuwaaamsha Israel kutoka katika usingizi wa maovu na starehe
-          Mungu hawezi kutuma hukumu kwanza kabla hajaifunua siri hiyo kwa watumishi wake Manabii amosi 3;8
-          Israela walikuwa wameingia katika ile dhambi ya kuabudu miungu 1Falme 12;25-33 na dhambi za starehe 3;15
-          Katika Sura ya 4 amosi aliendelea na ujumbe wake wa hukumu aliwaita Israel Ng’ombe za bashani Bashani palijulikana sana kwa  utajiri wa mifugo na mafuta na wanyama waliolishwa vizuri sana  Kumbukumbu 32;14-15, Wanawake matajiri waliokuwa wabinafsi waliitwa ng’ombe za bashani walijali maswala yao ya starehe na anasa na waliwatia moyo waume zao kujitajirisha na kuwaonea masikini 4;4 inaonekana kulikuwa na shughuli nyinfgi za kiibada na za kidini lakini  hakukuwa na kujitoa kwa kweli kwa Mungu
-          Mungu alihaidi kuwatumia Mapigo makuu matano  4;6-11 yaani njaa ,ukavu dhuruba,nzige,magonjwa
-          4;6 Lugha ya kimafumbi inatumika “Euphenism language” nimewapa usafi wa meno maana yake njaa. 4;12 wanaambiwa wajitayarishe kukutana na Mungu.
-          Katika sura ya 5 nabii anaomboleza kwa ajili ya dhambi ya Israel, wako watu ambao hudhani kuwa kuudhuria kwao ibada ni kwa muhimu zaidi au kunaweza kuwapa kibali kwa mungu na kusahu wajibu wa kujitoa kwake.

H.    UFAFANUZI WA HUKUMU AMOSI 7;-9;10
a.       Eneo hili lina ufafanuzi wa hukumu tano ambazo Mungu alimuonyesha Amosi katika maono
i.        Nzige- Mungu wakati mwingine hutimia majanga ya asili  katika kuhukumu amosi aliomba kwa niaba ya taifa likasamehewa pigo hilo 7;1-3
ii.   Moto Mungu alikusudia uteketeze na kuangamiza lakini pia amosi alimuomba    Mungu asamehe na ikawa hivyo  7;4-5
iii.      Timazi kilikuwa kipimo cha kuonyesha kuwa wamepotoka kiasi gani Bwana alimuonyesha amosi na wakati huu ikawa ndio mwisho wa kusamehewa mungu ana kipimo chake kwa ajili ya maisha yetu
iv.      Kikapu cha mavuno ya wakati wa hari 8;1-3 kuonyesha kuwa wanvuna kile walichokipanda
V. Kuvunjwa kwa madhabahu 9;1-10 huku ni kuharibiwa kwa hekalu lililokuwako huko Betheli kwa ufalme wa kaskazini
·         Amazia ambaye alikuwa ni kuhani mkuu kwa upane wa Betheli 7;10-17 alishutumu Amosi na kumshutumu kuwa amafanya uongo fitina juu ya Israel na hivyo hawawezi kustahimili Maneno yake na Amosi alisisitiza kuwa wito wake ni kutoka kwa Mungu

I.  AHADI YA KUREJEZWA TENA 9;11-15.
- Amosi anamalizia kitabu chake kwa ahadi ya kurejezwa tena kwa Israel
- Kwamba watatawanywa hukona huko kati ya mataifa lakini mabaki watarejezwa
- Nchi itastawi na hawataweza kutawanywa tena 9;11-15