AMOSI: NABII WA UTAKATIFU
A.
UTANGULIZI
-
Amosi alikuwa miongoni mwa wanamapinduzi wakubwa
katika Isarael huduma yake ilifanyika kipindi ambacho Israel walikuwa
wameharibika vibaya na walikuwa katika
wakati wa mafanikio na starehe ambazo ziliwafanya Israel kuishi maisha ya dhambi
-
Jina lake maana yake ni “Mbeba mzigo” alikuwa na mzigo wa kutimiza agizo Mungu alilokuwa
amempa kulitangaza neno la bwana wakati wa ukengeufu mkubwa wa Israel alizaliwa
katika kijiji kiitwacho Tekoa miles 12 hivi kutoka Yerusalem
-
Alikuwa Mchungaji wa Kondoo na mtunzaji wa miti ya
mikuyu hakuwa Nabii aliyesomea 7;14
lakini alikuwa mnenaji Hodari “Great orator”Asili ndiyo ilikuwa shule yake na
anga ubao wake 5;8 Neno lake linaonyesha historia yeke 3;8
-
Amosi alikuwa mtu wa Yuda ingawa alitumwa kwa
Ufalme wa Israel
Pichani Juu wachungaji wakichunga kondoo katika
uwanda wa mashamba ya ngano huko Tekoa mahali alikotokea Nabii Amosi Tekoa iko
mail 12 hivi kutoka Yerusalemu katika tawala za Yuda Picha kwa hisani ya
maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote
B. TAREHE YA UIANDISHI.
-
Kitabu kiliandikwa mwaka wa 755 K.K. wakati wa
utawala wa Yeroboamu II mfalme wa Isarael na Uzziah Mfalme wa Yuda
C.
WASIFU
WAKE.
-
Amosi alikuwa Mnyenyekevu na wala hakijaribu
kuficha maisha yake ya huko nyuma 7;14
-
Alikuwa na Hekima katika kupeleka kwake ujumbe alimtumia
misamiati amabayo ilikuwa wazi na ya kivitendo
-
Alikuwa mtu Imara thabiti alikataa kugeuzwa na
Amazia kuhani mwakilishi wa Yeroboamu huko Betheli 7; 10-17.
D.
HISTORIA
YA WALENGWA.
-
Wakati huu Israel walikuwa wanaishi maisha ya anasa
na mafanikio makubwa sana hata hivyo baadhi ya matajiri waliupata kutokana na
dhuluma
Masikini walikandamizwa Amosi 5;7,11
Mahakimu au Waamuzi walikuwa wakipokea Rushwa Amosi
5;12
Wafanya Biashara hawakutumia mizani za halali Amosi
8;5-6
Wenye haki waliuzwa utumwani amosi 2;7
Kulikuwa na uashaerati usio wa kawaida hata Baba na
Mtoto waliweza kutembea na mwanamke mmoja Amosi 2;7.
Waliwakataza Manabii kuhubiri Amosi 2;7.
Watu walioishi maisha ya Stareha na anasa Amosi 6;1
Uasi wa kidini ulitawala Amosi 4;4-5, 5;21-23
-
Utawala ambao ungeiangamiza Israel ingawa
haujaelezwa ni Ashuru.
E.
WAZO
KUU NA MISTARI YA MSINGI.
-
Wazo kuu katika kitabu hiki ni Samaria Inavuna
hukumu,amosi alikuwa ni Nabii wa kwanza
kutamka anguko la Samaria au Israel ambalo lilitimia miaka 40 baadaye ujumbe
wake ulikuwa hukumu ya Mungu kwa sababu ya Kukosekana kwa haki katika jamii
-
Mstari mkuu au wa msingi ni
-
Amosi 3;3 Je wawili waweza kutembea Pamoja
isipokuwa wamepatana?
-
Amosi 4;11-12 “Jiandae kukutana na bwana Mungu
wako”
-
Amosi 6;1 ole wao wanaostareha katika Sayuni
F.
MGAWANYIKO
WA KITABU CHA AMOSI.
-
Hukumu ya mataifa sura ya 1-2
-
Hukumu ya Israel sura ya 3-6
-
Uchanganuzi wa hukumu 7-9;10
-
Ahadi ya kurejeshwa upya 9; 11-15.
G. MCHANGANUO WA KITABU CHA AMOSI
-
Kabla ya
kutangaza hukumu dhidi ya Yuda na Israel
Nabii anachagua mataqifa kama sita hivi
ambayo pia aliyatangazia hukumu ya Mungu
-
Matatu kati ya hayo ni Dameski Syria,Gaza kwa
wafilisti na Tiro ambao hawa hawakuwa na uhusiano wa kindugu na Israel bna yuda
-
Mataifa mengine matatu ambao walikuwa na uhusiano
wa kidugu na Israel na Yuda ni Edomu, Ammoni na Moabu.
-
Kila tamko la hukumu kwa mataifa ya jirani na
Israel na Yuda ilianza na “Haya ndiyo asemayo Bwana kwa makosa matatu naam kwa
makosa manne sitazuia adhabu….”
-
Mtindo huu unamaanisha maovu yaliyopita kiasi na ya
kuwa maovu hayo yaliongezeka mwaka kwa mwaka
-
Amosi ndiye mwanzilishi wa mtindo wa kuliita taifa
kupitia jina la mji mkuu wake mfano anapoizungumzia Yuda anaitaja kama
Yerusalem na Israel kama samaria.
A.
HUKUMU
DHIDI YA DAMESKI SYRIA 1;3-5
-
Dameski
ulikuwa ni mji mkuu wa Syria na hapa Syria inatangqaziwa hukumu kwa sababu ya
kulitendea vibaya Gileadi Gileadi ulikuwa mji wa kale wa kabila ya nusu ya
Manase ambao walibaki ng’ambo ya Yordani watu walipokuja kuitamalaki inchi ya
mkanaani,
-
Dameski waliwachukuwa watumwa au mateka kwa vyombo
vya chuma na kuwaburu za kama mtu avunaye ngano mungu anahaidi kushusha moto na
kuwateketeza
B.
HUKUMU
DHIDI YA GAZA 1;6-8
-
Gaza ulikuwa mji mkuu wa wafilisti kusini magharibi ya Yerusalem,Dhambi yao
ilikuwa ni kusafirisha watumwa waliwachukuwa watu walioishi vijijini hususani waisreal na kuwauza huko edomu kama
watumwa
-
Mungu anaahidi kuwaletea hukumu ya kuwateketeza kwa
Moto na kuuchoma mji na majumba yake.
C.
HUKUMU
DHIDI YA TIRO 1;9-10
-
Tiro iko kaskazini mwa pwani ya Israel na mji
uliokuwa kutuo kikuuu cha bahari au bandari Isaya ,Yeremia na Ezekiel
waliitangazia hukumu maalumu ulikuwa mji mkuu sana wa kibiashara na kajhba mkuu wa wakati ule
-
Inaonekana waliwachukuwa watu fualni kabila nzima
huenda Waisrael na kuwatia mikononi mwa Edomu hivyo dhambi yao ilikuwa ni
kufanya biashara ya utumwa na Edomu na walisahau agano la undugu huenda hili
lilikuwa ni agqano walilolifanya Daudi na Hiramu katika 2samuel 5;11
-
Hukumu yao ni moto na kuharibiwa majumba yake na ni
kweli Nebukadneza alijaribu kuuteka tiro lakini si kwa mafanikio sana na
mwishoni uliharibiwa vibaya na Alexander
mkuu.
D.
HUKUMU
DHIDI YA EDOMU 1;11-12
-
Hwa walikuwa ni uzao wa Esau pacha wa Yakobo na
walioishi kusini mwa bahari iliyokufa
sehemu iliyoitwa araba, wao wanahukumiwa kwa Matendo yasiyo ya
kindugu,alimtumia upanga na mateso hawakuwa na huruma na walikuwa na kisasi cha
hasira kwa siku nyingi na wanatangaziwa hukumu nya moto juu ya temmani na
Borsa miongoni mwa miji yao mikubwa na
kuiteketeza.
E.
HUKUMU
DHIDI YA WAAMONI 1;13-14
-
Waamoni na wamoabu ni Watoto,wajukuu wa Lutu
waliozaliwa kutokana na zinaa ya baba na watoto wake wa kike Mwazno 19;30-38
-
Wao wanahukumiwa kwa sabau ya ukatili wao kwa
Gileadi ,waliwapasua wanawake wenye mimba wa Gileadi wanatangaziwa hukumu dhidi
ya mji wao mkuu Raba au Raboth-ammoni
-
Inaaminika kuwa huko ndiko Daudi alikoagiza Yoabu
kuhakikisha Uria anauwa vitani 2Samuel 11.
F.
HUKUMU
DHIDI YA WAMOABU 2;1-3
-
Hawa walikuwa na kosa la kuichoma moto mifupa ya
mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa
inaonekana hawakumpata akiwa hai hivyo kwa hasira walilipa kisasi kwa mifupa ya
mfalme Isaya 15;5,16;11 Yeremia 48;36
-
Wamoabu walihukumiwa kwa moto ,na kuuawa kwa
Viongozi ,Waamuzi na watu wakuu
-
Mungu anafuatilia sio tu mataifa wanavyolifanyia
taifa la watu wake bali hata kila taifa linavyolifanyia lingine.
G.
HUKUMU
DHIDI YA YUDA 2;4-5
-
Tofauti na mataifa haya mengine ya kidunia sita
Nabii anaigeukia Yuda ambao ni ufalme wa kusini lakini hawa wanahukumiwa kwa kutokishika
Sheria ya Mungu hivyo wao wanahukumiwa kwa maswala ya kidini yaani walikengeika
na kuiacha Shetia ya Bwana
-
Waliishi kama watu wa dunia nao watahukumiwa kwa moto na majumba yao
kuteketezwa
H.
HUKUMU
DHIDI YA ISRAEL 3;1-6
-
Pamoja na matangazo yoote hayo ya hukumu mungu
alikuwa akiilenga Israel wao ndio wanaoonekana kuwa na dhambi nyingi zaidi
kuliko mataifa mengine mlomlongo wa msururu wa dhambi kwa Israel ni mkuu
sana walionea masuikini,waliwauza watu
wenye haki ,waliabudu sanamu,waliifanya biashara ya utumwa, waliwafanya
wanadhiri kuvunja nadhiri zao na kulitii unajisi jina la bwana
-
Amosi aliorodhesha dhambi nyingi za Israel kuliko
za mataifa mengine huenda ili kuonyesha hatia kubwa waliyokuwa nayo na pia kwa
sababu alikuwa akiihubiri Israel na kuwaonyesha uhakika ya kuwa Mungu
angewahukumu wao.
-
Mungu anaihukumu Israel na kuwatangazia hukumu
hivyo akisisitiza katika matangazo makuu matatu yoote yakianzia na neno
lisikieni 3;1,4;1,5;1 na katika 3;3 anauliza je wawili waweza kutembea Pamoja
isipokuwa wamepatana? Mungu alikuwa anahoji anawezaje kutembea na Israel na
kukubaliana nao huku wanatembea dhambini
-
Amosdi alimtumia hata mifano kama simba na
mawindo,Mtego na tarumbeta ili
kuwaaamsha Israel kutoka katika usingizi wa maovu na starehe
-
Mungu hawezi kutuma hukumu kwanza kabla hajaifunua
siri hiyo kwa watumishi wake Manabii amosi 3;8
-
Israela walikuwa wameingia katika ile dhambi ya
kuabudu miungu 1Falme 12;25-33 na dhambi za starehe 3;15
-
Katika Sura ya 4 amosi aliendelea na ujumbe wake wa
hukumu aliwaita Israel Ng’ombe za bashani Bashani palijulikana sana kwa utajiri wa mifugo na mafuta na wanyama
waliolishwa vizuri sana Kumbukumbu
32;14-15, Wanawake matajiri waliokuwa wabinafsi waliitwa ng’ombe za bashani
walijali maswala yao ya starehe na anasa na waliwatia moyo waume zao
kujitajirisha na kuwaonea masikini 4;4 inaonekana kulikuwa na shughuli nyinfgi
za kiibada na za kidini lakini hakukuwa
na kujitoa kwa kweli kwa Mungu
-
Mungu alihaidi kuwatumia Mapigo makuu matano 4;6-11 yaani njaa ,ukavu dhuruba,nzige,magonjwa
-
4;6 Lugha ya kimafumbi inatumika “Euphenism
language” nimewapa usafi wa meno maana yake njaa. 4;12 wanaambiwa wajitayarishe
kukutana na Mungu.
-
Katika sura ya 5 nabii anaomboleza kwa ajili ya
dhambi ya Israel, wako watu ambao hudhani kuwa kuudhuria kwao ibada ni kwa
muhimu zaidi au kunaweza kuwapa kibali kwa mungu na kusahu wajibu wa kujitoa
kwake.
H.
UFAFANUZI
WA HUKUMU AMOSI 7;-9;10
a. Eneo
hili lina ufafanuzi wa hukumu tano ambazo Mungu alimuonyesha Amosi katika maono
i. Nzige- Mungu wakati mwingine hutimia
majanga ya asili katika kuhukumu amosi
aliomba kwa niaba ya taifa likasamehewa pigo hilo 7;1-3
ii. Moto Mungu alikusudia uteketeze na
kuangamiza lakini pia amosi alimuomba
Mungu asamehe na ikawa hivyo
7;4-5
iii. Timazi kilikuwa kipimo cha kuonyesha kuwa
wamepotoka kiasi gani Bwana alimuonyesha amosi na wakati huu ikawa ndio mwisho
wa kusamehewa mungu ana kipimo chake kwa ajili ya maisha yetu
iv. Kikapu cha mavuno ya wakati wa hari 8;1-3
kuonyesha kuwa wanvuna kile walichokipanda
V.
Kuvunjwa kwa madhabahu 9;1-10 huku ni kuharibiwa kwa hekalu lililokuwako huko
Betheli kwa ufalme wa kaskazini
·
Amazia ambaye alikuwa ni kuhani mkuu kwa upane wa
Betheli 7;10-17 alishutumu Amosi na kumshutumu kuwa amafanya uongo fitina juu
ya Israel na hivyo hawawezi kustahimili Maneno yake na Amosi alisisitiza kuwa
wito wake ni kutoka kwa Mungu
I. AHADI YA KUREJEZWA TENA 9;11-15.
- Amosi
anamalizia kitabu chake kwa ahadi ya kurejezwa tena kwa Israel
- Kwamba
watatawanywa hukona huko kati ya mataifa lakini mabaki watarejezwa
- Nchi
itastawi na hawataweza kutawanywa tena 9;11-15
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni