Andiko:
Matendo 4:36.
“Na Yusufu,
aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake
ni mtu wa Kipro,”
"Ndani ya Yesu Kristo kulikuwa na huduma ya Faraja, watu walifurahi kumsikia kumgusa na kumuona, ilikuwa Huzuni kwa wanafunzi wake alipowaambia kuwa ataondoka, lakini aliwaahidi kuwaletea mfariji yaani Roho Mtakatifu, ambaye hufanya kazi ya kuwahudumia watu waliomuamini"
UTANGULIZI:
Kufariji maana yake ni tendo endelevu la kuendelea kutia
moyo, kutia matumaini, kutia nguvu, kila mtu duniani anahitaji kutiwa moyo,
kuishi kwa matumaini, na kutokukata tamaa katika maisha yetu ya kila siku,
Tunaishi katika ulimwengu wenye changamoto nyingi sana na bila huduma ya
kutiana moyo ulimwengu hauwezi kuwa mahali pa kupendeza sana kuishi, Tunahitaji
watu wenye huduma ya kutia moyo wawepo kila mahali, Nyakati za Kanisa la Kwanza
Mungu alilipa Kanisa zawadi ya mtu mwenye karama ya kutia moyo wengine, Mtu
huyu alijulikana kama Yusuphu Mlawi
mzaliwa wa Cyprus.
·
Mitume walimuita mtu huyu “Barnabas” kuonyesha umuhimu wa
huduma hii ya faraja
·
Tunawezaje kutiana moyo kila mmoja na mwingine?
Ni kwa kujifunza kutoka kwa “Barnaba” na kuangalia kila alichokifanya:-
Huduma ya Barnaba.
I. Alitia moyo kanisa kwa kuonyesha mfano wa
matendo yake.
·
Aliuza shamba lake na kutoa fedha Matendo 4:37 alionyesha mfano katika kanisa, Kutoa kwake ulikuwa ni
moyo wenye kuonyesha kuwa anawajali wengine, lilikuwa ni jambo gumu sana kuuza
shamba Yerusalem kwa ajili ya umuhimu wa kumiliki ardhi katika jiji hilo lakini
Barnaba alifanya akionyesha kujali wengine.
·
Aliwatia moyo waliokataliwa katika jamii na
kanisa Matendo 9:26-30, Paulo mtume
ambaye ndiye Sauli alipookoka na kujiunga na wanafunzi pale Yerusalem watu
walikuwa na mashaka naye Lakini Barnaba alikuwa na ujasiri wa ajabu alimchukua
Sauli na kumtambulisha kwa mitume, Je tufanyeje kwaajili ya watu wanaokataliwa
katika jamii au kanisani lazima wawepo wenye huduma ya kufariji na kutia moyo
kama Barnaba.
·
Aliwatia moyo washirika kukaa katika kweli kwa
Bwana Matendo 11:22-24, kudumu kwetu
katika wokovu pia kunahitaji watu wa kukujenga na kukutia Moyo Barnaba alikuwa
mtu wa namna hiyo alilitoia moyo kanisa la Antiokia kudumu katika imani
·
Alimtia moyo Muhubiri mwenye kipawa na kuhudumu
naye Matendo 11:25-26, wakati jamii
inawapiga vita watu wenye vipawa the talented people na wakati mwingine
kuwachukia ni rahisi kuwapoteza watu wa aina hii kama hakuna huduma ya kutia
moyo Paulo mtume alikuja kuwa muhubiri mkubwa sana na mwenye huduma kubwa sana
lakini ilifanyiwa malezi na kutiwa moyo na Mchungaji Barnaba, watumishi wengi
wa Mungu wameshindwa kulea watu wenye vipawa kwa kuhofia kuwa watameza huduma
zao, au wameshindwa kuwasaidia waimbaji kwa kufikiri kuwa ni watu
wasiochungika, kama tukiwaelewa na kuwatia moyo na kuwajenga watakuwa wenye
kufaa sana katika kazi na ujenzi wa ufalme wa Mungu
·
Alitumika kuyatia moyo makanisa yaliyopata shida
kwa kupeleka zawadi Matendo 11;27-30, Wakati
kanisa la Uyahudi linapitia shida Kanisa la Antiokia lilimtuma Barnaba kupeleka
msaada na kanisa likafarijiwa kwa nini Barnaba kwa sababu alikuwa na moyo wa
kweli wa kujali na kuwajenga wengine.
·
Alilitia moyo Kanisa kwa ibada za kufunga na kuomba
pamoja na mafundisho Matendo 13:1-3, Namna nyingine ya kulitia moyo kanisa ni kukaa
katika maombi, kufunga na kuabudu na kufundisha Barnaba alikuwa mstari wa mbele
kufanya hayo mimi naamimi kwa vyovyote vile aliutafuta uso wa Bwana na
kuwaombea wengine, alitumiwa na Mungu pia kwa ishara na miujiza maana yake
aliwaponya watu wengine na pia kujitoa katika kazi ngumu sana ya umisheni.
II. Alilitia moyo kanisa kwa kutumia neno la
Mungu
·
Alilitia moyo waamini kukaa katika imani bila
kujali dhiki Matendo 14:21-22 Barnaba
na Paulo walilikumbusha kanisa kuwa imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu
kwa njia ya dhiki nyingi, waliwakumbusha kuvumilia na kuwatia moyo, fikiria
kama unapitia majaribu ya aina mbalimbali na hakuna wa kukutia moyo, je
ungedumu katika imani?
·
Alilitia moyo kanisa kwa kutafuta suluhu ya
kanisa la mataifa kuhusu tohara Matendo
15:1-2 Injili mbaya ya kutahiriwa kwanza ndipo uokoke ilipolivamia kanisa
Barnaba akiwa na Paulo walibishana na waalimu hao wa uongo, lakini pia
walikwenda Yerusalem kwaajili ya kutafuta suluhu ili kanisa liweze kufarijika
·
Alilitia moyo kanisa kupitia shuhuda za matendo
makuu ya Mungu Matendo 15:12
·
Alilitia moyo kanisa kupitia waraka na maneno Matendo 15:31-32 baada ya maamuzi ya
mitume waliyarudia makanisa yaliyosumbuliwa na fundisho baya na kuyaimarisha
kwa misimamo ya mafundisho sahii na maamuzi ya kanisa kutoka mkutano wa
Yerusalem
III. Alilitia moyo
kanisa kupitia kuwepo kwake
·
Ulimwengu huu ni ulimwengu wa changamoto
mbalimbali una dhiki nyingi Yohana 16:33
·
Ayubu ni moja ya mfano wa watu waliokutana na
mambo magumu sana kiasi ambacho hata waliokuja kumfariji walikaa kimya kwa siku
saba Ayubu 1;13-19,2;7-11-13
·
Kuwa na watu kama kina Barnabas ni kwa muhimu
sana kwa sababu ziko nyakati ambazo kama wanadamu tunahitaji faraja kwani yako
mambo yanatuelemea Majukumu ya kifamilia, watoto wasiosikia na kutii, mikwaruzo
katika ndoa, Hofu za kupoteza ajira, mishahara isiyotosheleza mahitaji yetu,
hasara za kibiashara, kazi nyingi nyumbani, upweke, kuvunjika kwa uchumba, lawama
kutoka kwa ndugu, lawama kazini, lawama kwa bosi, mahitaji ya ada za wanafunzi,
Bili za umeme, bili za maji, kodi ya mwenye nyumba mahitaji ya wazee kijijini,
mahitaji ya palizi au maandalizi ya mashamba kupanda kwa bei ya vyakula, nguo za
watoto, kusengenywa, mafarakano, visa vya majirani, mashambulizi ya wachawi, kuuguliwa,
madeni ya vikundi vya mikopo saccos, kupigwa nyundo Kanisani, shida za
washirika na wachungaji hali kama hizi na nyinginezo nyingi ndizo zinazopelekea
Kuweko na hitaji la kufarijiwa au kutiwa moyo hili ni jambo muhimu sana na
linahitajika sana katika wakati huu tulionao kuliko nyakati nyingine zozote,
Huduma za watumishi kama Barnaba zinahitajika sana wakati wa maswala mzito kama
hayo.
Hitimisho:
Tafadhali kuwa mtu
mwenye kutia moyo wengine na kuwafariji, usiwe mtu wa kuwaponda tu na kuwasema
wengine vibaya utakuwa mwana wa uharibifu, Mungu anataka kina barnaba wawepo
kila mahali , katika taifa, familia, mashuleni, majumbani na katika taasisi
mbalimbali
Jihadhari kuwa mkosoaji na mvunjaji moyo watu
yako maswala mazuri ambayo wanadamu wanayo hayo ndio vema yakajadiliwa kwa
mujibu wa fundisho la kibiblia “Wafilipi 4:8”
Uwepo wetu uwe na thamani kwa sababu kupitia
kuwatia moyo wengine na kuwafariji dunia itakua mahali pazuri pa kukaa salama,
utakumbukwa duniani kutokana na mchango wako mkubwa kwa jamii na dunia itaona
ni afadhali umeondoka endapo utakuwa mtu mwenye kuharibu wengine
·
Barnaba
alikuwa mwenye kujali wengine Caring
·
Barnaba
alikuwa mwenye kutia matumaini wengine wasikate tamaa Consoler
·
Barnaba
alikuwa ni mwenye kuwahurumia wengine Compassionate
·
Barnaba
hakuwa mtu wa kubadilika badilika katika huduma aliyokuwa nayo Consistent
· Alikuwa jasiri
katika kile alichokiamini kuwajenga wengine na kuwatetea kwa gharama yoyote ile
Convictions
Katika
kuhudumia kwangu kanisa la Mungu mtu anayefanana na Barnaba ambaye mimi
nimewahi kumuona ni rafiki yangu mmoja anaitwa Raphael Sallu Yeye ni Mchungaji
wa TAG Mkanyageni huko Muheza huyu jamaa ni kama Barnaba siongei kumtetea kwa
sababu ni rafiki yangu hapana lakini ndivyo alivyo.
Na
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.