Mstari
wa Msingi Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in
Greek, means FIGHT) kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Utangulizi:-
Ni
muhimu kufahamu wazi kuwa kila mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu
awe ameokoka au hajaokoka yuko katika vita na mapambano na shetani pamoja na
majeshi yake katika ulimwengu wa roho, Kwa wale waliookoka vita hii huwa kali
zaidi. Biblia inatufundisha wazi kuwa shetani ni adui yetu mkuu Mathayo 13:38-39, “lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme;
na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno
ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika”. Yesu anamtaja
shetani kuwa ni adui ni adui wa Mungu na ni adui wa wana wa Mungu, Kama shetani
hakusumbui na kukupiga vita wewe unapaswa kujiangalia sana kwamba uko upande
gani. Yesu anamtaja tena shetani kuwa ni adui katika Luka 10:17-19 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa
furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia,
Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri
ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru”. Kwa msingi huo katika somo hili tutachukua muda
kuchambua na kujifunza kwa undani kuhusu mapepo na jinsi ya kuwashinda kwa
kuzingatia maswala ya msingi yafuatayo:-
·
Ufahamu kuhusu Ulimwengu wa roho
·
Ufahamu kuhusu asili ya Mapepo na
nyadhifa zao
·
Ufahamu kuhusu vita vya kiroho.
·
Jinsi ya kuwashinda Pepo.
Ufahamu
kuhusu Ulimwengu wa roho.
Ni muhimu kufahamu
kwamba nguvu za Mungu ziko; lakini vilevile nguvu za giza zipo, na nimuhimu
kufahamu kuwa nguvu hizo zinatenda kazi katika ulimwengu usioonekana, ulimwengu
huu usioonekana ndio unaitwa ulimwengu wa roho Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, Pale in
Greek, means FIGHT) kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Kwa msingi huo
basi maandiko yanatufunulia wazi kuwa uko ulimwengu huu wa asili unaoonekana na
uko ulimwengu war oho usioonekana, ni katika ulimwengu huu usioonekana ndiko
aliko Mungu, lakini vilevile ndiko aliko shetani, ulimwengu huu tunaouona ni wa
muda tu, na ule usioonekana ni wa milele 2Wakoritho
4:18 “tusiviangalie
vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu;
bali visivyoonekana ni vya milele” kwa msingi huo tunao ulimwengu
huu unaoonekana ulimwengu ambao tunaweza kuona kila kitu kwa macho,tunaweza
kuhisi, tunaweza kusikia, tunaweza kunusa na kuonja huu ndio ulimwengu
tunaoishi siku zote, Lakini vilevile kuna ulimwengu war oho, ulimwengu huu una
Mungu na Malaika zake, ulimwengu huu una shetani na malaika zake waovu ambao
ndio tunawaita pepo, Na biblia imetaja hivyo nasi tunaamini, Biblia
tunayoitumia yenye vitabu 66
imewataja malaika mara 300, imemtaja
shetani mara 40, na imewataja pepo
mara 50 na neno roho chafu mara 40 pia limetajwa likimaanisha pepo. Kwa
msingi huo tunapozungumzia vita katika ulimwengu wa roho maana yake tunapambana
na malaika waovu yaani pepo ambao wanafanya kazi nyingi sana za kuwapinga
wanadamu katika ulimwengu huu unaoonekana kwa vyanzo kutoka ulimwengu
usiioonekana.
Ufahamu
kuhusu asili ya Mapepo na nyadhifa zao
Ni muhimu
kujiuliza sasa hawa pepo wanatokea wapi? Wakoje na wanatendaje kazi, Pepo kama
wanavyotajwa katika biblia vilevile ndio Majini kama wanavyotajwa katika quran
hawa kwa asli walikuwa Malaika
Malaika
ni nani?
Neno
au jina malaika lina asili ya kiyunani
ambayo ina maana pana kadhaa jina hilo kwa kiingereza ni Angel ambalo limetokana na jina la
kiyunani Angelos (Angelos)ambalo
lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) kwa Kiarabu Malakat au Malik ambalo pia maana yake ni
mjumbe(Messenger) wa Mungu, Hawa ni
roho watumishi wanaotumwa na Mungu kuwahudumia watu wake Waebrania
2:14 “Je!
Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”
lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa kumaanisha maswala kadhaa
yafuatayo;-
·
Neno
hili angelos lilitumika pia
kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa”
na matumizi kama hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika Matendo 12;15 ambapo wanafunzi
walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga mlango hii ni kwa sababu kimsingi
wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na isingeliwezekana kutoka gerezani
na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama vile hii ni kwa sababu
walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa Yakobo pamoja na kuwa
waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro kuweza kuwa hai. Jambo
lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa kama malaika kwa
msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia ilimaanisha wazi
kutumiwa kama neno malaika.
·
Neno
malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe
wa Mungu aliye mwanadamu” mfano katika Ufunuo
2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu inakisiwa
kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani
wajumbe ambao wanabeba gombo la
chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa ambayo Yohana alikuwa
akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa na Ufunuo
1;11, ambapo agizo linaonyesha kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo
ukayapeleke kwa hayo makanisa saba Efeso,
na Simirna, na Pergamo na Thiatira, na
Sard na Filadelfia na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano
wale waliopeleka magombo hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa
inamaanisha viongozi wa kila kanisa ambao husimamia makanisa na huwasomea watu maandiko kama
ilivyokuwa wakati wa matumizi ya masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza
kazi ya kiongozi ilikuwa ni kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo
walikuwa ni watu wanaowajibika kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo
viongozi hao pia waliitwa malaika yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha viumbe wa kiroho wa Mungu
ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa yale na imani hii ina mzizi
katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa malaika wa kila eneo, na pia
kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya mbinguni hapa duniani.
·
Malaika
ambao tunajifunza habari zao ni viumbe wa kiroho wenye maadili na uwezo mkubwa wa Ufahamu
ambao hawana miili ya kibinadamu na wale wa aina hiyo lakini wakaasi na kuitwa
mashetani kwa msingi huo somo hili halitahusu aina nyingine za malaika zile ambazo
zimetwajwa hapo juu kama roho ya waliokufa, wanadamu, wasomaji maandiko ,
wasimamizi wa kanisa au sinagogi au wachungaji ama kanisa lenyewe ambalo
humwakilisha Mungu duniani
· Malaika
pia wana majina kadhaa katika maandiko kama vile Wana wa Mungu Ayubu 1;6,2;1,Watakatifu Zaburi
89;5,7. Roho Waebrania 1;14,
Walinzi Daniel 4;13,17,23,Enzi,
Falme, mamlaka na usultani Wakolosai
1;16 na nguvu Waefeso 1;21.
Pepo ni Nani?
Neno
hilo pepo (Demons evil spirit) maana yake ni roho chafu au malaika walioasi,
malaika wabaya majini, au malaika waliofanya dhambi.
Asili yake ni nini?
Mungu
alipouumba ulimwengu aliumba kwanza ulimwengu wa roho, katika ulimwengu huo
Mungu aliwaumba malaika, hatuambiwi kuwa ni wakati gani malaika waliumbwa
lakini bila shaka ni miaka milioni nyingi sana, Mungu alipowaumba malaika
aliwaumba wakiwa na uhuru wa kuchagua mema au mabaya, la kusikitisha ni kwamba
Mungu alipowaumba wanadamu ndipo ilipofunuliwa kwetu kwamba kundi kubwa la
Malaika walichagua uovu, walimuasi Mungu wakiongozwa na Shetani ambaye
alijulikana kama LUCIFER yaani nyota
ya alfajiri Isaya 14:12-14 “ Jinsi ulivyoanguka
kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa
kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka
mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu
ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo
vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” Ezekiel 28: 13 -18 “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la
thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na
zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani,
na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku
ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa
mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu,
umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako
tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa
uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa
sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho
najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya
moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa
sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate
kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia
unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao
umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote
wakutazamao.” Baada ya anguko hili la shetani theluthi moja ya
malaika walijiunga naye na kupoteza nafasi yao mbinguni kwa Mungu Baba na hawa
ndio Mashetani, majini au mapepo au roho chafu au majeshi ya pepo katika
ulimwengu wa roho sasa basi kazi yao kubwa ni ipi?
Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za
baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa MWUAJI tangu mwanzo; wala
HAKUSIMAMA KATIKA KWELI, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo,
husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu YEYE NI MWONGO, na baba wa huo.”
Yohana 10:10 “Mwivi haji ila AIBE na KUCHINJA na KUHARIBU;
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa
kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake;
kwa maana ametupwa chini MSHITAKI wa ndugu zetu, yeye AWASHITAKIYE mbele za
Mungu wetu, mchana na usiku.”
Hizo
ni kazi kuu za shetani na sifa zake, katika somo langu hili tutajadili pia kazi
azifanyazo shetani na malaika zake au mapepo.
1. Kuongoza ulimwengu katika uasi “Misleading the
Entire Inhabited Earth”
Ni muhimu kufahamu kuwa shetani pamoja na mapepo wana nguvu ya ushawishi
katika akili na maisha ya watu, shetani na mapepo yake wanamamlaka ya kuuongoza
ulimwengu katika kuasi au kufanya maasi Ufunuo 12:9 “Yule
joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.” Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za
mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote
kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”
Ziko njia
nyingi sana ambazo ibilisi huzitumia katika kufanikisha njia zake pamoja na
mapepo yake na moja ya silaha yake kubwa ni kutumia UONGO, atatumia mafundisho
ya uongo na dini za uongo 1Timotheo 4:1 “Basi Roho
anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”
unaweza kuona kwamba kumbe shetani na mapepo wanaweza
kutumia mafundisho na ushawishi usio wa kiungu kuupotosha ulimwengu, wakitumia
dini za uongo pia Mashetani wamefanikiwa kuzipofusha fikra za watu wengi ili
isiwazukie Nuru ya injili 2Wakoritho 4: 3-4 “Lakini
ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao
mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili
ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”
a.
Mafundisho
kuhusu mawasiliano na wafu “The teaching that the dead are still alive and you
can communicate with them” Shetani anaweza kutumia sauti na uwezo wa kichawi
kupitia mapepo kuwadanganya watu kuwa unaweza kuwasiliana na wafu, Biblia
inatufundisha kuwa baada ya kifo ni hukumu na kuwa hakuna mawasiliano na wala
tusiwasiliane na watu waliokufa Kumbukumbu 18:9-13 “Utakapokwisha
kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa
machukizo ya mataifa yale. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti
yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye
nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga
mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa
Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele
yako.Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.”
Mungu alikataza maswala hayo kwa sababu alijua kuwa
mashetani yanatumia njia hizo hapo juu, kuharibu uhusiano wetu na Mungu na
kujikuta tukipoteza ibada, wote tunakumbuka Jinsi Sauli alivyowaendea waaguzi
na kupiga bao hii ilikuwa kinyume na Torati na hivyo alikufa
1Samuel 28:1-25,
“Ikawa siku zile hao Wafilisti
wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi
akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na
watu wako. Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda
mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe
kuwa mlinda kichwa changu daima. Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao
Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake
mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na
wachawi katika nchi. Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko
Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika
Gilboa. Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo
wake ukatetemeka sana. Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala
kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. Ndipo Sauli akawaambia watumishi
wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza
kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa
utambuzi huko Endori. Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha
akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku;
akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja
kwako. Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi
alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona
basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?
Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema,
Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke
aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia
kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya?
Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule
mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. Naye akamwuliza, Ni
mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli
akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi,
akasujudia. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata
kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti
wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala
kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.Samweli
akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui
yako? Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana
amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa
sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu
ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. Tena pamoja na wewe
Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao
mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa
Wafilisti. Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa
sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana
hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha. Ndipo yule mwanamke akamwendea
Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako
ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami
nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia. Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize
sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu,
utakapokwenda zako. Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila
watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza
sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda. Naye yule mwanamke
alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na
unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo; kisha akamwandalia Sauli
na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.”
1Nyakati 10:13-14
“Basi Sauli alikufa kwa sababu
ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na
tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa
Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.”
Mtu awaye yoye anayekwenda kwa waganga na kutaka
shauri, kupiga ramli anafanya kosa kwani Neno la Mungu liko kinyume na ibada za
kishetani
b.
Mmomonyoko
wa Maadili “Anything-goes morality”
Ulimwengu mzima uko chini ya yule mwovu 1Yohana 5:19 “Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa
katika yule mwovu.” Shetani na mapepo yake wanatumia nguvu zao katika
vyombo vya taarifa Media na njia nyingine zote kuinua kiwango cha uovu, ili
kwamba wanadamu waone ni sahii na kufuata tamaa za dunia na kusababisha
mmomonyoko mkubwa wa uadilifu Waefeso 2:1-3 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata
mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza
mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao
wengine”. Kwa sababu hiyo leo
tunashuhudia mmommonyoko mkubwa wa uadilifu, ushoga, tamaa, na kila aina ya
uharibifu huku viwango vya utakatifu na uadilifu vilivyowekwa na Neno la Mungu
vikionekana kuwa ni ushamba.
c.
Kuinuka
kwa roho za uaguzi (Uganga) “The promotion of spiritism.”
Maandiko yanaonyesha jinsi Paulo mtume alivyokutana na
mwanamke mwenye roho ya uaguzi au pepo wa auaguzi, na aliyekuwa akijipatia
fedha au faida nyingi kwa sababu yanuaguzi Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi
mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida
nyingi kwa kuagua.” Watu wengi hudhani kuwa waganga wako kwaajili ya
kutoa msaada lakini waganga wote ni maajenti wa shetani na wanakuwa na pepo wa
uaguzi kwaajili ya kuwasaidia kuagua na kutafuta dawa kwa nguvu za kipepo na
hivyo kuwapotoshwa watu wa Mungu katika ushirikina, Paulo akitambua kuwa ni
dhahiri chanzo cha uaguzi ni pepo au shetani alikataa kusikiliza sifa za
kishetani na kulikemea pepo hilo na likaondoka
d.
Kuinua
watu wenye kufanya Uchawi “The promotion of witchcraft”
Wachawi ni njia nyingine ya utendaji kazi wa kishetani
na kipepo, Mungu alikataza uchawi na alitaka wachawi wauawe Kutoka 22:18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” Wachawi walikuwa ni
maadui wakubwa wa kazi ya Mungu wakati Mungu alipomtuma Musa na Haruni, wachawi
wa Farao huko Misri walipingana na Musa na Haruni wachawi hao walijulikana kama
Yane na Yambre 2Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na
Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni
watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.” Kutoka
7: 10-13 “Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao,
wakafanya vivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini
mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Ndipo Farao naye akawaita
wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni
ikazimeza fimbo zao. Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama BWANA
alivyonena.
Ni kazi za wachawi ambao pia ni maajenti wa shetani
kuwafanya watu wasiokoke, wasiiamini injili na wawe na mioyo migumu kama
ilivyokuwa kwa farao, wachawi hufanya kazi za shetani na ndio maana Paulo
alimkemea Mchawi
Matendo 13:8-12 “Lakini Elima,
yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia
yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa
Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote,
mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana
zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione
jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta
mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.Ndipo yule liwali, alipoyaona
yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana”
Unaweza kuona hizi ni baadhi ya kazi za waziwazi za
kimapepo, ni kazi za shetani na majeshi yake, yako na mambo mengine mengi
ambayo mapepo huyafanya na ni vigumu kuorodhesha moja baada ya jingine lakini
hata hapo umepata picha dhidi ya utendaji wa Ibilisi.
2.
Tabia
za pepo.
Pepo kwa vile ni roho wachafu waasi ambao walikuwa
malaika wana tabia zinazofanana na za malaika na pia kwa kiwango Fulani wana
tabia zinazofanana na wanadamu, popo wana nafsi kwa sababu hiyo wana sifa
kadhaa vilevile ambazo tunaweza kuzipata katika maandiko matakatifu
a.
Pepo
wana Hisia
Pepo wana hisia na utambuzi, Yesu alipokutana na mtu
aliyekuwa amepagawa na mapepo mengi sana katika inchi ya wagerasi pepo waliweza
kuonyesha hisia zao na utambuzi wao kuhusu Yesu, walimuogopa Mathayo 8:28-29 “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili
wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze
kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana
wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?”
b.
Pepo
wana uwezo wa kufundisha.
Kwa ujumla wataalamu wote wa uganga na uchawi na
wapunga pepo huwa wanafundishwa na mapepo, Hali kadhalika pepo huweza kupotosha
ukweli na kusababisha ukengeufu, wanauwezo wa kutumia watumishi wa uongo na
kufundisha mafundisho yao, biblia inasema wazi kwamba roho hizi zidanganyazo
zaweza kutoa mafundisho, ambayo biblia inayataja kama mafundisho ya Mashetani 1Timotheo
4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za
mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na
mafundisho ya mashetani;”
c.
Pepo
wana vurugu na wanapiga.
Wakati mwingine ni muhimu kuwa na ufahamu hususani
endapo utajihusisha na kazi za kutoa pepo, kwamba pepo wanavurugu wanafanya
fujo na wanaweza kupiga, Matendo 19: 13-16. “Baadhi ya
Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la
Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu,
yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani
mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na
Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu
akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile
hali wa uchi na kujeruhiwa”
d.
Pepo
hupokea ibada.
Katika namna ya kijanja sana shetani na mapepo hupenda
na hutamani kuabudiwa, hivyo kila mtu anapaswa kuwa na ufahamu ni namna gani na
jinsi gani atajilinda na utendaji wa mapepo asije akayaabudu, wanao hujificha
nyuma ya sanamu, wakipokea ibada, hujificha nyuma ya waganga wa kienyeji na
wachawi wakipokea ibada na hujificha nyuma ya dini za uongo wakipokea ibada
uwezo wote na nguvu zote za waganga na wachawi na makuhani wa dini za uongo
hutegemea nguvu hizi za kimapepo nyuma yake ni muhimu kujihadhari tusiwasujudie
mashetani Ufunuo 9:20-21 “Na wanadamu waliosalia,
wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata
wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za
mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakuutubia
uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.”
e.
Pepo
wana uwezo wa kufanya ishara na miujiza
Tuliona tangu wakati wa Musa na Haruni jinsi
walivyofanya ishara na wachawi wakaigiza sihara zile, Biblia iko wazi kuwa pepo
nao huweza kufanya ishara lengo lao likiwa ni kupotosha watu kupitia siashara
zao Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani,
zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya
kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”
f.
Pepo wanawajua watu wa Mungu na wokovu.
Kama unamtumikia
Mungu kwa dhati na kuhubiri njia sahii ya wokovu pepo wanafahamu, ingawa wakati
wmingine wao ni waongo lakini wakati mwingine husema ukweli. Tunapaswa kuwa makini
na kuwa na karama ya kupambanua hasa wakati unapotoa nafasi ya kuwasikiliza
Pepo Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja
aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa
kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi
wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.”
g. Pepo wanaamini kuwa
yuko Mungu mmoja na wanatetemeka.
Pepo wanafahamu
ukweli kuhusu Mungu na wanajua wazi kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, wanatambua
kuwa anapaswa kuabudiwa na wanatetemeka, na ndio maana tunapowakemea kupitia
jina la Yesu, kwa ufahamu walio nao kuhusu Mamlaka hiyo wanatii na kuondoka. Yakobo
2:19 “Wewe
waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na
kutetemeka”
h. Pepo wanaweza
kuwapagaa wanyama
Biblia inatuonyesha
kuwa uko uwezekano wa pepo kuwapagaa wanyama, na hii inatupa ushahidi ulio wazi
kuwa wachawi na waganga wanaweza kufanya mambo ya kichawi na kusumbua watu
kupitia wanyama mbalimbali Mathayo 8:28-31. “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya
Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali
mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema,
Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Wale pepo wakamsihi, wakisema,
Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe”
i.
Pepo wanaweza kuwa wengi ndani ya mtu mmoja.
Biblia inatufundisha
kuwa tabia ya pepo katika kuwatesa wanadamu kwamba pia wanauwezo wa kupagaa mtu
mmoja huku wao wakiwa wengi na kusababisha madhara makubwa zaidi Luka 11:24-26 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali
pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitairudia nyumba
yangu niliyotoka. Hata afikapo, akaiona
imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu
kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho
huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
3. Nyadhifa na mamlaka
za mapepo.
Biblia inaonyesha
wazi kuweko kwa mamlaka za kipepo kama zilivyo mamlaka za Malaika kwamba mapepo
kuanzia na shetani yana protokali zake Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu”Wakolosai 2:15 Biblia
inaonyesha kuwa ziko enzi na mamlaka “akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na
kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.” Kwa msingi huo
unaweza kuona kuwa biblia inagusia kuwepo kwa enzi na mamlaka za kipepo katika
namna isiyokuwa ya kawaida Nabii Daniel pia anasaidia kujua namna na jinsi
mamlaka za kipepo zilivyojipanga kwamba kuna pepo linalotawala kwa kila Taifa
au ufalme na uko wezekano mkubwa kuwa pepo hao wakawa wamejipanga mpaka katika
kiwango cha mkoa, wilaya, tarafa kata, kijiji, kitongozi na hata kifamilia
(Family spirit) kwa msingi huo unaweza kuona kuwa katika mpangilio wa Mapepo na
utawala wa shetani hali hii inawezaikawa inafanana na mpangilio wa uongozi wa
shetani.,Daniel 10:13,20-21
1. SHETANI
(Mungu wa Dunia hii,
na Mfalme wa Uweza wa Anga, Mkuu wa ulimwengu huu)
2Wakoritho 4:4,Yohana
12:31
“ambao ndani yao mungu wa dunia hii
amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru” ya injili ya utukufu wake
Kristo aliye sura yake Mungu.
“Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu
wa ulimwengu huu atatupwa nje.”
2.
WAKUU WA NCHI FALME AU MAMLAKA
Waefeso 6:12,
Daniel 10:13,20
“Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in
Greek, means FIGHT) kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho.
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga
siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele,
akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata
nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka
huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.
3.
MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA
ROHO
Waefeso 6:12,
Kwa
maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means
FIGHT) kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
4. MAAJENTI WA
SHETANI NA MAPEPO
Waefeso 6:12 c “juu ya majeshi
ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Hawa ni
binadamu ambao wanafanya kazi kwa niaba ya shetani, kundi hili ni pamoja na
waganga, wachawi, wanga na wengineo
Majeshi haya ya Pepo
hufanya kazi mbalimbali za uharibifu na wamejipanga vema katika kuhakikisha
utaratibu wao wa uharibifu unafanikiwa
5.
MAPEPO WALIOFUNGWA
Yuda 1:6
“Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe,
lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele
chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.”
Mungu Katika hekina
yake amewaweka kifungoni baadhi ya Mapepo kutokana na uwezo wao mkubwa wa uharibifu,
aidha baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa aina hii ya mapepo inaweza
kuruhusiwa wakati wa dhiki kuu na watahusika kipekee katika kuleta mateso na
uharibifu mkubwa kwa binadamu wakati wa dhiki kuu.
Majina ya Mapepo na
kazi zao
Mapepo yana majina mengi
tofauti tofauti kutokana na tabia, vyeo na kazi zao, waislamu wanasema kuna
majina yapatayo 99 ya majini, Katika ukristo Shetani ametajwa kwa majina
kadhaamachache kulingana na tafasiri ya kazi zake lakini kwa mujibu wa Mtandao
wa unexplained-mysteries.com ambao unafundisha kuhusu Mapepo na vyeo vyao
tunafunuliwa kazi kadhaa za mapepo kupitia majina yanayotumika katika jamii
mbalimbali
Apollyon (Abaddon)
: King of Demons- Mfalme wa Mapepo
Abigor: Horseman
with a scepter and lance, commanding 60 legions, Kiongozi wa kikosi cha farasi
anayeongoza Majeshi 60 ya mapepo, kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000
Adremelech:
Chancellor and High Council of Demonds – Kiongozi mkuu wa halimashauri kuu ya
Mapepo
Aguares : Grand
Duke of Eastern region, commanding 30 legions- Mtawala wa Mashariki anayeongoza
Majeshi 30 ya mapepo kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000
Alocer : Grand
Duke , commanding 36 legions - Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36 ya mapepo
Amduscius : Grand
Duke, commanding 29 legions, -Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 29 ya mapepo
Andras : Marquis
, commanding 30 legions- Mtawala anayeongoza Majeshi 30 ya mapepo
Asmodeus (Asmoday)
: Head of Casinos, Mkuu wa anasa za Makasino na Majumba ya Starehe
Astaroth : Grand
Duke of Western region, Lord Treasurer, Mtawala wa Magharibi na Mtunza hazina
wa mapepo
Aym : Grand Duke
, commanding 26 legions, Mtawala wa kati anayeongoza majeshi 26
Ayperos :
Prince, commanding 36 legions- Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36
Azazel :
Standard Bearer of Armies, also known as Satanael.Mpambe wa Majeshi
Baal :
Commanding General of the Infernal Armies, Mkuu wa Majeshi ya Mapepo yanye
makelele sana ya kuzimu
Baalberith :
Chief Secretary and Archivist (second order demon, Berith)Katibu mkuu wa
mipango ya kipepo
Balan : Prince,
Mfalme
Bearded Demon :
Remains nameless to avoid his use in search of the Philosopher's Stone (King
Solomon)Mfalme wa maswala ya ujenzi wa kutumia mawe
Beelzebub (Beelzebuth) : Prince of the Demons, Lord of the Flies, second only to Satan
Mfalme
wa Mapepo, Mungu wa mainzi ni mamlaka ya pili kutoka kwa Shetani
Belial : Prince
of Trickery, Demon of Sodomy- Mfalme wa Hila na mtawala wa maswala ya ulawiti
na ufiraji na mapenzi ya jinsia moja
Belphegor : Demon
of Ingenious discoveries and wealth, Pepo la maarifa na ugunduzi na utajiri
Buer : Second
order demon but commands 50 legionsMamlaka ya kipepo inaongoza vikosi vya
majeshi ya pepo 50 kumbuka kila jeshi au kikosi ni pepo 6000
Caym : Grand
President of the Infernal Rais wa kuzimu
Charon : Boatman
who ferries souls across the river Styx-Pepo la maji na mito
Chax : Grand
Duke- Pepo dume mkuu
Cresil : Demon
of Impurity and slovinliness- Pepo la uchafu na kutokujali, uvivu na
uhovyohovyo
Dagon : Baker
and member of the House, Pepo la mapishi na nyumbani
Eurynomus :
Prince who feeds on corpses,
Furfur : Count ,
commanding 26 legions
Geryon : Giant
centaur, guards hell
Jezebeth : Demon
of Falsehoods
Kasdeya :
According to the "Book of Enoch", the fifth Satan
Kobal :
Entertainment Director, patron of Comedy
Leonard :
Inspector General of Black Magic and Sorcery
Leviathan :
Grand Admiral: androgynous ( Christian myth says he seduced both Adam and Eve)
Lilith : Princess
of Hell. ( Hebrew myth is that she is a succubus)
Malphas : Grand
President, commanding 40 legions
Mammon : Demon
of Avarice
Mastema : Leader
of the offspring of fallen angels by humans
Melchom :
Treasurer of the House
Mephistopheles :
Some versions a servant of Lucifer, others Satan himself
Merihim : Prince
of Pestilence
Moloch : Another
demon of Hebrew lore
Mullin : Servant
of the House of Princes, Lieutenant to Leonard
Murmur : Count,
Demon of Music
Naburus :
Marquis, connected with Cerberus
Nergal : Chief
of Secret Police, second order demon
Nybras : Grand
Publisist of Pleasures, inferior
Nysrogh : Chief
of the House of Princes, second order demon
Orias : Marquis,
Demon of Diabolic Astologers and Diviners
Paymon : Master
of Ceremonies
Philatanus :
Demon assisting Belial in furthering sodomy and pedophile behaviors
Proserpine :
Princess of Hell ( some say, close to Persephone of Pagan traditions)
Pyro : Prince of
Falsehoods
Raum : Count,
commanding 30 legions
Rimmon :
Ambassador from hell to Russia, also known as Damas
Ronwe :
Inferior, yet commands 19 legions
Samael : Angel
of Death, Prince of Air
Semiazas : Chief
of Fallen Angels
Shalbriri :
Demon that strikes people blind
Sonneillon :
Demon of Hate (Michaelis )
Succorbenoth :
Chief Eunuch of the House of Princes, Demon of Gates and Jealousy
Thamuz :
Ambassador of hell, Creator of the Holy Inquisition, Inventor of Artillery
Ukobach :
Stationary Engineer
Uphir : Demon
physician
Valafar : Grand
Duke
Verdelet :
Master of Ceremonies of the House of Princes
Verin : Demon of
Impatience
Vetis : demon
who specializes in corrupting and tempting the holy
Xaphan : Stokes
the furnace of hell, second order demon
Zaebros : Animal
- human combination
Zagan : Demon of
Deceit and counterfeiting
Ufahamu
kuhusu vita vya kiroho.
Ni
muhimu kufahamu kuwa katika nyakati za agano jipya biblia inaonyesha wazi
kabisa kwamba kila mtu aliyemwamini Yesuyuko katika mapambano, tunapambana wazi
kabisa na nguvu za yule muovu Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye,
mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote
za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa
sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu,
na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Biblia inaonyesha wazi kabisa
kwamba tuko katika mapambano yasiyoonekana, ni mapambano dhahiri kati ya ufalme
wa giza na ufalme wa Nuru, ufalme wa shetani na ufalme wa Mungu.
Linaendelea.....................................................................
Jinsi
ya kuwashinda Pepo.
1. Lazima
uwe Hodari Yoshua 1:6 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe
utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.”
Biblia
inazungumzia Uhodari, kwa kuwa kuwashinda Pepo ni vita vya kiroho basi jambo la
kwanza ni kuwa Hodari, kuwa hodari maana yake ni kuwa na uzoefu wa vita
mbalimbali za kiroho, uwe mpambanaji, kama unaytaka kuwa huru au kuweka wengine
huru kutoka katika nguvu za giza basi huwezi kuepuka kuepuka agizo la kuwa
Hodari, popote biblia inapozungumzia vita inazungumzia UHODARI, Angalia Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye,
mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote
za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa
sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu,
na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Mashujaa wote wa Imani katika
Biblia wanatajwa kuwa walikuwa Hodari katika vita angalia Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena?
Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na
Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao
kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi,
walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza
majeshi ya wageni.” Unapotaka kuwashinda maadui na kufukuza majeshi
ya wageni unapaswa kuwa hodari, neno Uhodari katika kiibrania linatajwa kama
neno “Mashal” ambalo maana yake ni kufanya zaidi ya jinsi ulivyofundishwa, ni
weledi katika kupambana na maadui, lazia kila anayetaka kupambana na shetani
ajue kuwa anapaswa kuwa na ujuzi na ukomavu katika imani, ni lazima uwe na
mamlaka na ujuzi wa mamlaka ya kupambana na majeshi ya mapepo na uhodari huu
unafichwa katika uzoefu wa vita na imani.
2. Ni
lazima uwe na Mafuta ya Roho Mtakatifu. Luka 4:18- 19 “Yesu
alisema maneno haya muhimu sana Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na
kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”. Yesu Kristo anaonyesha wazi kuwa
ili kuweka watu huru tunahitaji Upako yaani tunahitaji kupakwa mafuta na Roho
Mtakatifu, Roho wa Bwana akiwa juu yetu na kutupaka mafuta tuaweza kuwafungua
waliofungwa, tutaweza kuwaweka watu huru kutoka katika upofu,tutaweza kuwaweka
huru waliosetwa yaani wanaoonewa wote hao ni kutoka katika vifungo mbalimbali
na uonevu wa Ibiblisi, Nabii Isaya anaonyesha wazi kuwa njia ya kuwashinda
maadui na kujilipiza kisasi na kuondoka katika mizigo yao ni kwa kupitia mafuta
angalia Isaya 10:24-27 24. Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu
mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua
gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri. Maana bado kitambo kidogo tu
ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza.Na Bwana wa majeshi
ataamsha mjeledi juu yake, kama vile alivyopiga Midiani karibu na jabali la
Orebu; na fimbo yake itakuwa juu ya bahari, naye ataiinua kwa namna ya Kimisri.
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake
shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta”.
3. Ni
lazima umfunge kwanza yule mwenye nguvu. Mathayo 12:28-29 “Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa
Mungu umekwisha kuwajilia. Ama awezaje mtu
kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake,
asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.” Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu
alizungumza nini katika eneo hili, kwa uwazi wote tunajua kuwa miili yetu ni
nyumba Biblia inasema kwa wale waliookoka kuwa waoa ni Hekalu la Roho Mtakatifu 1Wakoritho 6:19 “Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;” Kama mwili wa
mtu aliyeokoka ni Hekalu au nyumba ya roho Mtakatifu ni wazi kuwa mtu
asiyeokoka ni nyumba ya pepo angalia
Mathayo 12:43-45 “43. Pepo mchafu, amtokapo mtu,
hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu
husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa,
na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu
kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya
mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho
kibaya.” Kumfunga yule mwenye Nguvu basi kwa maana ya Yesu ni kushughulika
na mwenye nyumba zaidi yaani ni kumshughulikia Shetani na kupindua ufalme wake
na kumuingiza mmiliki mwingine yaani Yesu Kristo ili atawale maisha ya mtu
huyo, ili pepo wasiweze kummiliki mtu ni lazima shetani afungiwe kabisa na
kutupwa nje, ni rahisi sana mapepo kuondoka yenyewe ikiwa ufalme wake
umepinduliwa, mapepo hufanya kazi chini ya utawala wa shetani, mtu akimpokea
Yesu anapewa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu na hivyo ufalme wa giza
hupinduliwa na Yesu huchukua nafasi yake na hivyo wajumbe wa shetani yaani
mapepo huondoka bila shida Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa
Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
4. Shugulikia
kiti cha enzi cha Shetani Ufunuo 2:12-13 “Na kwa
malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo
upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI
CHA SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata
katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, HAPO
AKAAPO SHETANI”. Ni
muhimu kufahamu kile anachokizungumza Yesu hapa Pergamo, Pagamo ndio ulikuwa
mji mkuu wa kisiasa katika ugiriki ya zamani nyakati za leo ni uturuki, mjii
huu ulikuwa na hadhi ya kipekee kwa kuwa hali ya ushawishi wote ilianzia hapo
katika asia ndogo ya zamani, ulikuwa ni mji wenye wagunduzi na waanzilishi wa
maswala ya mambo mbalimbali, lakini hata mauaji ya wakristo yalianzia kwa kasi
katika mjii huu, Lugha anayoitumia Yesu kutaja kiti cha Enzi cha shetani
ilikuwa inamaana kuwa wakati huu ushawishi mkuu wa ibilisi ulikuwa unatokea
katika eneo hilo, hivyo Pagamo palikuwa ni makazi ya Ibilisi, hii inatupeleka
mbali zaidi kuwa shetani anaweza kufanya makao ndani ya mtu, ndani ya familia,
ndani ya ukoo, ndani ya kijiji, ndani ya kitongoji, ndani ya kata, nadani ya
tarafa, ndani ya wilaya ndani ya mkoa na ndani ya taifa, bara na kadhalika, ni
muhimu kumfunga na kuharibu kila kinachoonekana kuwa ni utawala wa ibilishi na
kusimamisha utawala wa Mungu kama ilivyo katika kipengele kilichopita
Angalia shuhuda hizi kutoka kwa
Joseph Ntandu alipokuwa akifundisha kuhusu umiliki na kuwashinda wakuu wa giza
Nanukuu..
Mchungaji
Yonggi Cho
apambane
kwa maombi na mkuu yule giza. alipomshinda kwa maombi kupitia jina la YESU
ndipo huduma yake ilistawi na huduma hiyo imefikia hatua ya sadaka zinahesabiwa
kwa zaidi ya siku 2 na sadaka hiyo kuipeleka bank ni kwa msafara mkubwa kukiwa
na ulinzi mkubwa wa Polisi wengi.
Ndugu,
ukishinda katika ulimwengu wa roho hata katika ulimwengu wa mwili utashinda
pia.
#Askofu
Moses Kulola kabla ya kuanza kuhubiri injili ya mafanikio makubwa katika
Tanzania aliingia katika maombi ya kufunga siku 4 mlimani. Katika maombi hayo
akiwa katika siku ya mwisho ya maombi aliona jitu kubwa la kutisha likija alipo
na lilipokaribia lilimwambia kwanini anataka kulichukua eneo lake huyo mkuu wa
giza, yaani
Tanganyika
kwenye ulimwengu wa roho wa giza kulikuwa na mtawala wake ambaye ndiyo huyo roho
ya kuzimu, kwa maombi Askofu Moses Kulola alimshinda yule mtoto wa shetani ndio
maana akaanza kuhubiri injili ya mafanikio sana. Kila Eneo huwa lina utawala wa
aina tatu. Kuna utawala wa kibinadamu, kuna utawala kutoka ulimwengu wa roho wa
giza na utawala wa MUNGU hutawala pote na una mamlaka ya mwisho.
Kumbe ili
ulipate eneo fulani kwa ajili ya kitu fulani chako chema inabidi kwa maombi
umpige mkuu wa giza wa eneo husika. Mwisho wa kunukuu.
Kumbe
basi ili kuweza kuyashinda mapepo hatuna budi kuhusika kipekee katika
kushughulikia viti vyao vya enzi na kuvisambaratisha.
5. Tumia
jina la Yesu. Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi
kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.” Pepo wanaweza kutii pale unapolitumia
jina la Yesu, kumbuka kuwa ni Yesu ndiye aliyetoa amri na agizo la kutoa pepo,
hivyo huwezi kutoa pepo kwa namna nyingine yoyote kanuni ni lazima ulitumie
jina la Yesu Marko 16:15-18 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa
kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara
hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa
lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha
kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao
watapata afya”
6. Hakikisha
kuwa unamtii Mungu na kumpinga shetani Yakobo 4:7 Biblia inasema “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Utii kwa Mungu unaongeza Mamlaka
yetu dhidi ya pepo waovu na maasi mengine yote ya ibilisi, Utii wetu na uchaji
wetu kwa Mungu hutupa nafasi na kibali cha juu sana cha kusikilizwa na Mungu, Waebrania 5:7-9. Yeye,
siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika
mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi
alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo
yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa
watu wote wanaomtii” Ni kutokana na utii aliokuwa nao Yesu
alisikilizwa sana na Mungu, Yesu mwenyewe alishuhudia kuwa Mungu anamsikia siku
zote yaani mara zote Yohana 11:41-42 “Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu,
akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia Nami nalijua ya kuwa
wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema
haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma” Utii na ushirika na Mungu utakufanya
usikilizwe siku zote na shetani akukimbie tunaona jinsi maisha ya Yesu
yalivyojaa utii na unyenyekevu jambo lililopelekea kuadhimishwa mno na kila
kitu kuwekwa chini yake Jina lake limekuwa juu ya majina yote na ameadhimishwa
sana kama maandiko yasemavyo lakini sababu kuu ikiwa ni utii Wafilipi 2:8-11 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena
Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa
jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya
chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa
Mungu Baba.” Biblia inaonyesha wazi kuwa kuna viwango tofautitofauti
vya kusikiwa na Mungu na si kila mtu anaweza kusikilizwa tu ziko ngazi ambazo
unaweza kuzifikia kwa utii na Mungu akakusikiliza na katika kiwango hichohicho
cha utii mamlaka yako dhidi ya Ibilisi ikawa kuu mno Yeremia 15:1 “Ndipo Bwana akaniambia, Hata
wangesimama mbele zangu MUSA NA SAMWELI, moyo wangu usingewaelekea watu hawa;
watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.” Unaona Kumbe
biblia inaonyesha wazi kuwa Musa na Samuel walikuwa na ushawishi mkubwa kwa
Mungu hii ina maana Mungu aliwasikiliza sana watu hao, Katika Ezekiel Mungu
anawataja watu wengine ambao yeye huwasikiliza Ezekiel 14:14 “ wajapokuwa watu hawa watatu,
NUHU, NA DANIELI, NA AYUBU, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu
kwa haki yao, asema Bwana MUNGU” Biblia
pia imewataja Nuhu, Daniel na Ayubu kwamba ni watu ambao Mungu angeweza
kuwasilikiza Kama utajongea katika kujiongeza kutii ndivyo ulimwengu war oho
unavyoweza kukusikiliza na kutii na ndivyo mamlaka yako inavyoweza kuongezeka
juu zaidi.
7. Isipokuwa
kwa kufunga na Kuomba
Ni
muhimu kufahamu kuwa kutokana na ngazi na mamlaka walizonazo pepo ambazo ni
sawa na mamlaka za kijeshi, kila mtoa pepo anapaswa kukumbuka kuongeza mamlaka
yake kwa kutii, lakini kama Yesu anavyotufundisha ni wazi kuwa aina nyingine za
pepo hawatoki kwa mtu anayeomba maombi ya kawaida tu, wakati mwingine ziko aina
nyingine za Pepo watatoka kwa kujumuisha maombi na kufunga angalia mfano wa
aina hizo za pepo kama pepo wanaohusika kuleta kifafa Mathayo
17:14-21 “Nao
walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, Bwana,
umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi
huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze
kumponya.Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka,
nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku
kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi
hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa
maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia
mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno
lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”
Unaweza
kuona pia katika Marko 9:17-29 “Mtu mmoja katika
mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila
ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema
na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Akawajibu, akasema, Enyi kizazi
kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni
kwangu. Wakamleta kwake; hata
alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa,
akitokwa na povu. Akamwuliza babaye,
Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa
katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote,
utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake
aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie
kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio,
akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi
nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata
wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.
Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi
hatukuweza kumtoa? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote,
isipokuwa kwa kuomba.”
8.
Ni
lazima kuharibu kazi zake 1Yohana 3:8
“atendaye dhambi
ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili
Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi” Ilikuwa
mbali na nguvu za giza ni lazima kazi zote za ibilisi zivunjwe na kuharibiwa
hapa kuna jambo pana sana la kujifunza, Kazi ya kwanza ya ibilisi ni
kuhakikisha watu wanafanya dhambi, kuishi katika dhambi ni kuishi katika
uharibifu, ni ugonjwa mkubwa wa kiroho unaoweza kuruhusu magonjwa mengine ya mwili
naya kipepo pia Marko 2:17 “Yesu aliposikia
aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita
wenye haki, bali wenye dhambi.” Kusudi kuu la Yesu Kristo kuja ni
kuleta uzima na sio hukumu Yohana 3:17
“Maana Mungu
hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe
katika yeye”. Tunaposhughulika
na kuharibu kazi za ibilisi maana kuu ni pamoja na kuhakikisha watu wanaondolka
katika dhambi, ama tunaacha dhambi ili tuwe mbali na utendaji wa shetani,
lakini vilevile kuharibu kazi nyingine za ibilisi ni pamoja na kuhakikisha kuwa
tunajiepusha na shughuli zote za utendaji wa ibilisi au kazi zile ambazo nyuma
yake shetani anaweza kujificha na kuzitumia kuleta madhara ya kiroho
-
Ushishiriki
ibada za kimila/kimapepo/kishetani 1Wakoritho10:20-21
“. Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa
kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.
Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi
kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani”
-
Ikimbieni
ibada ya sanamu 1Wakoritho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.”
Ni wazi kuwa ibada ya sanamu ni kazi nyingina ya ibilisi, biblia ilikwisha
kukataza kuabudu au kutengeneza au kuzitumikia sanamu za aina yoyote ile Kutoka 20:2-6 “Mimi
ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya
utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala
mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala
kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi,
BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao,
hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri zangu”. Vijana kama Shedrak, Meshack na
Abednego wanaotajwa katika Daniel walikuwa tayari hata kuangamiza maisha yao
kuliko kuabudu sanamu hii ilitokana na msimamo ulio wazi kwao kwamba kuabudu
sanamu kungemaanisha wazi kuwa wanaabudu miungu mingine na kuabudu miungu
mingene ni uhalisia ulio wazi kuwa ni kuabudu mashetani hivyo walimtumaini
Mungu naye akawaokoa Daniel 3:1-18 “Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu
wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika
uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Ndipo Nebukadreza akatuma watu
kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na
mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa
kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. Ndipo maamiri, na
manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili,
na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme
Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza
aliyoisimamisha. Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila
zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na
filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma,
lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza
aliyoisimamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo
katika tanuru ya moto uwakao. Basi
wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na
kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na
mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza
aliyoisimamisha. Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu
ya Wayahudi. Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza, Ee
mfalme, uishi milele. Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu
atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na
zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya
dhahabu; na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto
uwakao. Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya
Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme,
hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya
dhahabu uliyoisimamisha. Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu,
waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele
ya mfalme. Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na
Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia
sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia
sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna
zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali
msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani
Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? Ndipo Shadraka, na Meshaki, na
Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu
katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na
tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si
hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala
kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha” Ni lazima watu
wakatae kuabudu sanamu kwa gharama yoyote nyuma ya sananu yako mashetani
yakitafuta kuabudiwa, yako mapepo, Vijana hawa alikataa kazi hizi za ibilisi
kuabudu sanamu kungeweza kuleta laana ya Mungu kwa kizazi cha wanadamu hata cha
tatu na cha nne, lakini Rehema za Mungu yaani kama tutamcha zinaweza kudumu pia
kwa vizazi vyetu
-
Choma
moto vifaa vyote vya uganga na uchawi Matendo19:18-20
18. “Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama,
wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya
uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya
hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.
Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu”Unaweza kuona Biblia inasema
watu wa Efeso walidhihirisha matendo yao, yaani walionyesha wazi kuwa wao na
kazi za ibilisi basin a hivyo waliamua kuziharibu kabisa ona kwamba vitabu
hivyo viligharimu fedha 50,000/- yaani sawa na shilinga 34,000/- ya mwaka 1952,
Mji wa Efeso walikuwa wakiabudu sanamu na miungu na walishiriki uchawi na
uganga lakini walipoiamini injili walaiharibu kabisa kazi za ibilisi, ni muhimu
kwa kila mtu anayetaka kuwa huru kuharibu kabisa, Hirizi, kuharibu tunguli,
kuharibu na kuchoma mapembe na kuacha kabisa ushirikina, achana na wapunga pepo
na wapiga madogoli na ibada zote za mizimu na kishetani, achana na misa za wafu
kabisa, achana na ubashiri wa nyota, kupiga bao na ramli, ngoma za
mashetani,kujizindika, kuchanjia muku, kupandisha mapepo, sadaka za kuchinja,
makafara ya watoto au ndugu,kunuiza, namba za kichawi, kwenda kwa waganga wa
kienyeji, ulaji wa nyama za binadamu,kushiriki bahati nasibu, kucheza kamari,
maswala ya kuondoa nuksi na mambo yanayofanana na hayo hizi zote ni kazi za
shetani ambazo zinapaswa kuharibiwa.
9.
Usiwaruhusu
peo kuzungumza Marko 1:34 “Biblia inasema Akaponya wengi waliokuwa na maradhi
mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.”
Yesu hakuwaruhusu pepo kuzungumza biblia inasema kwa sababu walimjua, hata
hivyo ziko sababu nyingi ambazo zinaweza kujumuishwa hapa kwanini Yesu hakuwaruhusu
Pepo kuzungumza Luka 4:41 “Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye
maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja
akawaponya. Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u
Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye
Kristo”. Kama tulivyosema awali kuwa ziko sababu kadhaa kwanini Yesu
hakuwaruhusu Pepo kuzungumza
a.
Shetani
anaitwa baba wa uongo angalia katika Yohana 8:44 na Mwanzo 3:4 ni wazi kuwa
Mashetani au mapepo yana tabia sawa na ile ya shetani hakuna kweli ndani yake
hata siku moja Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo
mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika
kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake
mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Kama shetani ni
muongo asemapo uongo hujihakikishia tabia yake hivyo hakuna pepo mkweli, pepo
wanaweza kusema kweli mara kadhaa lakini hatuhitaji ukweli wao hata kidogo,
Mapepo yalikuwa yanamjua Yesu kuwa ndio Masihi lakini Kristo hakukubali
kudhihirishwa na Mapepo watu wapinzani walishamsema kuwa anatoa pepo kwa mkuu
wa pepo, na hivyo kuyaruhusu mapepo kuzungumza hata kama yangesema kweli,
ilikuwa ni kutia mafuta ya petrol katika moto, lakini tukijifunza kutoka kwa
Yesu Kristo hii inamaanisha wazi kuwa hatupaswi kuwasikiliza Mapepo, wako
watumishi mbalimbali hasa wenye karama za kinabii huchukua mud asana kuwahoji
pepo, kufanya hivi wakati mwingine kunaweza kuruhusu fitina na mafarakano
miongoni mwa watu
b.
Kuwaachia
pepo kuzungumza kungemaanisha kuwa huna mamlaka dhidi ya pepo, pepo wameumbwa
kijeshi, jeshini hakuna mazungumzo na muhalifu ni amri, hatujapewa nafasi ya
kuzungumza na pepo tumepewa amri ya kutoa pepo, kwa msingi huo ni muhimu kwetu
kuwafunga na kuwaamuru kutoka tu Marko
8:33” Akageuka, akawatazama wanafunzi wake,
akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya
Mungu, bali ya wanadamu.” Yesu hakutoa muda hata kusikiliza mawazo ya
shetani, kuwanyima pepo kuzungumza kunaonyesha jinsi ambavyo pepo hao wanatii
mamlaka iliyokuu kwa jina la Yesu Luka
10:17”Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha,
wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.”
c.
Kuwahoji
pepo ni kupoteza Muda, angalia huduma zifanywazo na wanaotoa pepo katika mtindo
huo huku wakiwa na umati mkubwa wa watu wanaohitaji huduma kumbuka Yesu alikuwa
na watu wengi sana aliokuwa akiwahudumia angalia biblia inavyosema Marko 1:34 “Biblia
inasema Akaponya wengi waliokuwa na
maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu
walimjua.” Je watu wengine wanaohitaji huduma watafunguliwa saa ngapi
kama bwana yesu angehusika kuhoji waliopagawa mmoja mmoja nafahamu kuwa kuna wakati Yesu aliliuliza
pepo jina lako nani Luka 8:30 “Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni
Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”Katika kifungu hiki Yesu
aliuliza jina la pepo kwa kusudi la kutufundisha kuwa pepo wanaweza kuwa wengi
katika mtu mmoja katika mstari wa habari hii hii katika injili nyingine neno
Jeshi limatajwa kama neno Legion angalia Marko
5:9 “Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina
langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.”jina hilo la kilatini Legion
lilikuwa na maana ya kikosi cha askari wapatao 6000 kusudi kuu la Yesu ni
kuonyesha jinsi ambavyo mapepo hao wakiokuwa juu nya mtu mmoja walivyokuwa
wengi na kwa kusudi hilohilo aliwaruhusu kwa nguruwe 2000 kumaanisha au
kuonyesha mateso makubwa alivyokuwa nayo mtu yule, hivyo pepo wanaweza kuulizwa
swali kwa kusudi tu lakini si kila wakati
d.
Yesu
hali kadhalika hakutaka kudhihirishwa kuwa yeye ni Masihi kupitia roho wa uongo
hata kama walisema kweli, Miujiza aliyoitenda Kristo pekee ilikuwa inatosha
kuonyesha wazi kuwa yeye ni masihi Mathayo 11:4-6, Luka 7:21-23 na miujiza yake
yote ilitabiriwa katika Isaya 29:18, 35:4-6 kwa sababu hiyo hakupenda
kudhihirishwa na mapepo, ni jambo kama hili ndilo lililomuudhi Paulo, hatupaswi
kuthibitishwa ubora wa utumishi wetu kupitia mapepo, tusifurahi kwa sababu pepo
wanatutii bali kwa sababu tunajulikana mbinguni yaani majina yetu yameandikwa
mbinguni.
10. Watu wengi wasikemee pepo mmoja
au kwa pamoja
Kumekuweko
na tatizo kubwa sana kwa jamii ya wapentekoste au watu wenye kuhusika na
kuwafungua wenye pepo, kumbuka pepo wameumbwa katika mfumo wa kijeshi na hivyo
hupokea amri kijeshi, unapokuwa jeshini kisha ukaamriwa na kila kamanda kufanya
jambo Fulani unaweza kujikuta unachukua muda mwingi kutafuta yupi wa kumtii
kwanza, Pepo hawatatii kwa haraka watu amabao hawajajipanga katika utoaji wa
pepo, tunatofautiana viwango vya amri na mamlaka na utii ni muhimu mtu mmoja
anapokemea pepo wengine wakawa kimya kinyume na hilo itawachukua muda mrefu
sana kumfungua mtu anayeteswa na Mapepo.
Jinsi ya kutoa Pepo
Kazi ya kanisa ni kuhubiri
injili, kazi hii ya ufalme wa Mungu katika agizoa lake kwa ujumla pia
inahusisha kutoa pepo, Marko 1:21-27, Kutoa pepo pia ni ishara ya kila mtu
anayelitimiza agizo kuu na aliyemwamini Yesu Kristo Marko 16:17
Lengo kuu la Mapepo ni kutimiza
Mapenzi ya kiongozi wao amabaye ni ibilisi, kama ilivyo kwa wakristo wanapenda
kutimiza mapenzi ya Mungu, mashetani hutimiza mapenzi ya baba yao ibilisi,
wakijua wazi kuwa hawamwezi Mungu wanataka kumuuzi Mungu kwa kuwaonea wanadamu
ambao Mungu anawapenda upeo
Wanataka mkuiba ibada 1Wakoritho
10:19-21
Wanataka kuwaweka wanadamu katika
utumwa wa hofu magonjwa na tabia mbaya ili kuharibu sura ya Mungu ndani yao.
Wanawapiga watu upofu ili
wasiikubali injili Matendo 10:38, 2Wakoritho 4:4, 2Timotheo 2:25 na Waebrania
2:14
Mapepo hudanganya Yohana 8:44,
1Timotheo 4:1 2Patro 2:21
Mapepo yanaua na kusababisha
machafuko na kudhuru wanadamu Yohana 8:44
Mapepo yanatesa Mathayo 12:22,
Luka 13:11-17,Ayubu 12:22
Mapepo yanatia watu ukichaa Luka
8:27-29
Mapepo yanaongoza katika uchafu
wa kingono Mathayo 10:1, Marko 1:23,3;11
Mapepo huzuia kazi ya injili
1Thesalonike 2:18
Mapepo yanafundisha uchawi Torati
32:16-17 ISamuel 15:23
Mapepo yanaongoza kuabudu Mizimu
1Wakoritho 10:19-20
Mapepo hupagaa watu
Kupagaa
ni kitendo cha kudhuru na kutawala kwa namna mbalimbali, Mapepo yanapokuwa
yamempagaa mtu maana yake huingia ndani ya mtu na kutawala maisha yake kwa
sehemu au yote, hii inaweza kutokea pia mtu huyo akawa anafanya vitu nje ya
akili zake za kawaida, mtu anapokuwa amepagawa kunaweza kuwekokwa dalili
zifuatazo
1.
Mabadiliko
ya mtu huyo Marko 9:26
2.
Nguvu
za kupita kawaida Luka 8:29
3.
Ufahamu
usioweza kuelezeka Matendo 16:16-17
4.
Mateso
ya kupita kawaida ikiwemo upofu, uziwi au ububu Marko 1:26, Mathayo 12:22-30, 9:32-34
5.
Kujichukia
kujiua na kujifanyia vitendo vya ukatili Marko 9:22,5:5
6.
Kuogopa
jina la Yesu au kumuogopa Yesu mwenyewe Marko 1:24
Mapepo hayawezi
kumpagaa Mkristo wa kweli
Inagawa
mapepo hayawezi kumpagaa mkristo wa kweli bado mapepo yanaweza kumjaribu, au
kumtia majaribuni, kumdanganya, kumshambulia, na kumtesa kutokea nje lakini ni
vigumu kumpagaa kupagaa ni kudhibiti kabisa ufahamu na maamuzi ya mtu hivyo kwa
mkristo aliyezaliwa mara ya pili yaani aliyeokoka ni vigumu na haijawahi
kuthibitika kuwa anaweza kuwaliwa na Mapepo, lakini uwezekano wa Mkristo
kupagawa na pepo unaweza kutokea kwa Mkristo aliyerudi nyuma au kukengeuka
Na
mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.
Still
underconstructions / bado linamatengenezo!