Jumapili, 13 Juni 2021

Hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena Milele !


Msatri wa Msingi: Kutoka 14:14-14Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.”




Utangulizi:


Siku moja Bwana Mungu aliviita viungo vyote katika mwili wa mwanadamu na akataka kuwauliza ili kujua wanafanyaje kazi? Kichwa kilielezea yote, Moyo, mikono miguu na kila kiuongo kwa jinsi yake, Lakini kiungo kimoja kilikuwa na malalamiko dhidi ya kiungo kingine, kiungo kilichokuwa na malalamiko kilikuwa ni *Ulimi* na mlalamikiwa alikuwa ni *Meno*, Kesi iliposikilizwa, ulimi ulisema kuwa mimi ni laini sana Mzee na umeniweka na Meno ambaye kwaasili yeye ni mgumu, tunapokuwa katika kazi ya kulainisha chakula mara kwa mara Meno huning’ata na kuniumiza na hivyo nachukua siku kadhaa kupona na kuendelea na kazi zangu, Mungu alimwambia ulimi usilalamike, ulaini wako haumaanishi kuwa wewe ni dhaifu kuliko meno, wewe ni mgumu sana, kuliko unavyojifikiri utaumizwa na utapona, na utaendelea kuwepo,  lakini sivyo ilivyo kwa meno ambaye anaonekana kuwa mgumulakini ukweli yeye ni dhaifu, baada ya miaka kadhaa utahesabia meno na utakubaliana nami kuwa mengine yataliwa na wadudu na hutayaona tena na yatang’olewa, lakini wewe ulimi utadumu hata mwisho wa dahari, ni kweli ulimi ulivumilia na kutoa muda kwa meno na wakati wa uzee, ni ulimi pekee aliyeonekana kudumu na kutokuchoka tena ukiwa na nguvu zake vilevile!


Lolote lile linalokusumbua katika maisha yako, na kukuumiza lipe muda tu, iko siku litang’oka, Wamisri waliwaonea wana wa Israel na kuwatumikisha kama watumwa kwa miaka mia nne na thelathini, Lakini siku moja wakati Israel wakiivuka bahari ya shamu, Musa alitabiri kuwa hawa wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele, unabii huu ulidumu kwa muda mfupi tu, kwani hata Musa aliusema akiwa kama kiongozi na mwenye kuwatia moyo watu wake kama mchungaji, lakini yeye mwenyewe alimlilia Mungu kwa hali aliyokuwa anaiona, Mkono wa Mungu ulikuwa mwema kwani aliwafutilia mbali Wamisri wale waliokuwa wakiwaandama wana wa Israel ili kuwaonea.


Leo nakutangazia kwa jina la Yesu, Magumu yote yanayokukabili na changamoto zote unazozipitia hautakuja uzione tena milele, Bwana atakupigania nawe hutanung’unika milele, Bwana atakustarehesha, Bwana atakupigania nawe utanyamaza kimya, kila changamoto unayokutana nayo katika maisha yako na inayoonekana kuwa ngumu au tishio kwako, hayo ni kama magego tu na wewe ni kama ulimi wewe ni imara zaidi kuliko wao na kuliko changamoto zako, Mungu anayejua kuwa uko katikati ya magumu atakutetea, Changamoto hizo kwa mamlaka niliyopewa kama mtumishi wake natangaza  leo ziwe mwisho na usizione tena katika jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai, Natangaza kuwa changamoto zinazokukabili hautaziona tena, sema amina

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Alhamisi, 3 Juni 2021

Ni mizuri kama nini miguu yao, wahubirio habari ya mema!


Isaya 52:7 “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!



Utangulizi:

Ujumbe huu wa Nabii Isaya ulikuwa ni ujumbe wa maono ya siku ya ukombozi wa Yerusalem ambao vilevile huitwa sayuni, Ni ujumbe unaohusiana na Israel (Wayahudi) kuletewa ujumbe wa amani kutoka kwa mfalme Koreshi ya kwamba Mungu amemtuma awatangazie uhuru wayahudi waliokuwa utumwani huko Babel kwamba warejee kwao na kuujenga tena mji wao na Hekalu la Mungu wao baada ya kuwa utumwani kwa miaka mingi, Nabii anaona maono ya ukombozi anawaona wajumbe juu ya milima ya Yudea wakiiletea Yerusalem habari za kufunguliwa kwake! Ona


Isaya 40:9-11 “Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake. Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Nabii Isaya hakupata nafasi ya kuona kile kilichowapata wana wa Israel (Wayahudi) waliochukuliwa utumwani wakati wa Mfalme Nebukadreza, lakini aliweza kuona na kutabiri katika ulimwengu wa kiroho na kuwaona wayahudi wakipelekwa utumwani lakini vilevile wakirejea, Unabii wake huu hasa unatoa matumaini kwa Wayahudi ambao wangechukuliwa utumwani na kuwatia moyo ya Kwamba Mungu angewatokea tena na kuwarejeza.

Wayahudi walichukuliwa utumwani na Mfalme aliyeitwa Nabukadreza kimsingi mfalme huyu wa wakaldayo, alikuwa ni mwana wa Nabopolassar na alipata utawala mwaka wa 604 Kabla ya Kristo baada ya kuanguka kwa utawala wa waashuru, Jina lake kamili hasa linaandikwa na kutamkwa kama Nebuchadrezzar ambalo kwaasili ni “Nabu-Kudurri-usur” ambalo maana yake ni Nebo linda mipaka yangu (Nebo ni mungu wa wakaldayo) Mfalme huyu aliyekuwa katili sana na aliyekuwa dikteta mkubwa mno ametajwa zaidi ya mara tisini katika agano la kale.

Wayahudi wanamkumbuka Mfalme huyu kama moja ya wafalme katili sana ambaye wao wanamuhesabu kuwa aliwafanya wayahudi kama moja ya wanyama, alipopata utawala alikuwa na kampeni ya kupanua mipaka yake ya kuitawala Dunia mpaka Misri na kuhakikisha kuwa kila mfalme anamtii yeye na akawa mfalme wa wafalme, Wayahudi pia walitawaliwa na mfalme huyu, na Yehoyakimu mfalme wa wayahudi alitakiwa kujinyenyekesha chini yake na alipoasi jamaa alimuharibu ona

2Wafalme 24:1-3 “Katika siku zake akakwea Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Yehoyakimu akawa mtumishi wake muda wa miaka mitatu;kisha, akageuka,akamwasi.Naye Bwana akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii. Hakika kwa amri ya Bwana mambo hayo yalimpata Yuda, ili waondoshwe kutoka machoni pake, kwa sababu ya dhambi zake Manase, kadiri ya yote aliyoyafanya;


Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Nebukadreza vilevile aliliharibu Hekalu la Yerusalem na kuchukua vyombo vitakatifu na kuvipeleka katika hekalu lake huko Babeli wakati wa mfalme Yehoyakimu

2Nyakati 36:5-7 “Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake. Juu yake akakwea Nebukadreza, Nebukadreza akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya Bwana mpaka Babeli, akavitia katika hekalu lake huko Babeli.”
Aidha alimuua mfalme wa wayahudi na kuutupa mwili wake bila kuuzika sawa na alivyotabiri nabii Yeremia ona

Yeremia 22:18-19 “Basi, Bwana asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake. Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.” Ona pia

Yeremia 36:30-32 “Basi, Bwana aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hari, na wakati wa usiku upigwe kwa baridi. Nami nitamwadhibu yeye, na wazao wake, na watumishi wake, kwa sababu ya uovu wao, nami nitaleta juu yao, na juu ya wenyeji wa Yerusalemu, na juu ya watu wa Yuda, mabaya yote niliyoyatamka juu yao, lakini hawakukubali kusikiliza. Ndipo Yeremia akatwaa gombo lingine, akampa Baruku, mwandishi, mwana wa Neria, naye akayaandika maneno yote yaliyotoka katika kinywa cha Yeremia, ya kitabu kile alichokiteketeza Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika moto; tena maneno mengi zaidi kama yale yakatiwa ndani yake.
Licha ya kumuua mfalme wa wayahudi na kumtupa bila kuzikwa, Nebukadreza pia alichukua utumwani kundi la wayahudi wapatao 4,600 ona

Yeremiah 52:27-30 “Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake. Watu hawa ndio wale ambao Nebukadreza aliwachukua mateka; katika mwaka wa saba, Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu; katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza aliwachukua toka Yerusalemu watu mia nane na thelathini na wawili;katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.” 

Mfalme huyu ambaye hakuwa na huruma aliamuru mateka watembee moja kwa moja bila mapumziko mpaka Ukaldayo bila kupumzika hata hatua moja, akiamini kuwa wayahudi wakipewa nafasi tu watapata muda wa kusali na kuomba na kutubu kwa Mungu wao na wanaweza kupata rehema, hivyo ili wakose pumzi ya kupata kanafasi ka toba na kusababisha Mungu wao kubadili mawazo alihakikisha kuwa wanakula kibano sawia, alipofika ukaldayo alifanya sherehe kubwa sana ya kufurahia ushindi wake na kuwalazimisha wayahudi waimbe nyimbo za Sayuni kwa miungu yake huko


Zaburi 137:1-3 “Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.”


Vijana wazuri wenye nguvu na hekima walihasiwa ili wawe watumishi wa mfalme yaani walifanywa kuwa matowashi, akiwepo Daniel, Hanania, Mishael na Azaria, walikuja kujulikana baadaye kama Shedrack, Meshak na Abednego ona Daniel 1:1-4 “Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli,alikwenda Yerusalemu akauhusuru. Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.”                

Licha ya mateso haya ya kiutu na kisaikolojia Mateka wengi waliachwa na njaa, walipigwa na jua kali, walitembezwa wakiwa uchi mpaka wakawa weusi, njaa ilisumbua watu wazima mpaka vitoto vichanga, ilifikia  hatua hata wanawake waliokuwa na huruma walikula watoto wao kwa zamu Maombolezo 4:8-10 “Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba. Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.” Kuna maswala mengi sana ya kikatili yaliyofanywa na Mfalme huyu mkubwa sana na dikteta wa hali ya juu aliyekuwa amejaa kiburi mpaka aliponyenyekeshwa na Mungu, ukweli ni kuwa hata wayahudi walipofika utumwani hawakuwa na maisha salama waliendelea kutumikishwa katika shughuli ngumu na kali na mateso. Aidha kiimani walilazimishwa kuabudu na kuitumikia miungu migeni ya Ukaldayo kwa ujumla waliishi Maisha ya wasiwasi na kutokuelewa kuwa kesho yao itakuwaje jambo hili liliwafanya waikumbuke Sayuni, wakumbuke Yerusalem wawe na tamaa ya kurudi kwao, Kwa hiyo nabii Isaya licha ya kuona mateso haya kinabii vilevile alitabiri kuwa anawaona malaika wa Bwana wanashuka juu ya milima ya uyahudi wakitangaza habari njema, ni habari ya kuwekwa huru, ni habari ya kuamuriwa kurudi Yerusalem, ni habari ya kurudi nyumbani, ni habari ya kwenda kuwa na ushirika na Mungu wao ni habari ya kwenda sehemu ambako unabii wa kuja kwa masihi ungetimizwa ni habari ya kurejeshewa kwa matumaini yao, ni habari ya kuelezewa ya kuwa mambo yatakuwa mazuri, Nabii isaya anasema ni Mizuri kama nini Miguu yao juu ya milima ya uyahudi waletao habari za amani, waenezao habari njema wasemao habari za wokovu waambiao watu Mungu ndiye anayetawala yaani ufalme wa Mungu u karibu  hii ilikuwa ni kauli ya furaha kwa watu waliokata tamaa, kila mmoja anaweza akawa yuko katika hali ya mateso na hali isiyofurahisha wala kuridhisha kila mmoja anahitaji ukombozi, anahitaji kusikia habari njema Baada ya kutimizwa kwa unabii huu wa Isaya Mungu alimuinua mfalme mkuu Koreshi wa uajemi ambaye alitoa habari njema kwa kuwaruhusu Wayahudi warejee Yerusalem ili kulijenga tena hekalu na vilevile kukomesha utumwa wa wana wa Israel na mateso yao ona Isaya 44:28 “nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.” Isaya 45:1-5 “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;” Unabii Isaya wa isaya ulitimizwa miaka 180 baadaye Isaya alikuwa na maono ya ajabu sana mpaka ya kutaja jina la Mfalme huyo mabaye Mungu alimuita Mtumishi wake na mpakwa mafuta waka na Mchungaji wake, hii ni wazi kuwa mtumishi awaye yote wa Mungu atakayetenda mapenzi halisi ya Mungu ni yule mwenye miguu mizuri anayetangaza habari njema na za amani na za wokovu na za kuwaweka watu huru, katika namna nyembamba kiongozi huyo ni Koreshi bali katika namna pana Kiongozi huyo ni Yesu Kristo, lakini wale wanaoihubiri habari njema yaani injili pia wanaitwa ni wenye miguu mizuri kwa sababu wanafanya yale mapenzi ya Mungu kwa watu wake.

Paulo anaitumia kauli hii ya Nabii Isaya katika Warumi 10:15b “Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya memaWahubiri katika agano jipya wanapaswa kuwatangazia watu habari njema za matumaini ya Kwamba Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai ndiye aliyekuwa anatabiriwa kutuletea habari njema ya ukombozi ya kuwekwa huru sio tu kwa Israel bali na kwa mataifa mengine, watu wameteseka vya kutosha chini ya utawala wa mfalme asiyekuwa katika mikono ya Mungu, shetani ni mfalme wa wafalme aliye katili sana mwenye kuwatesa watu na kutokuwapoa pumzi ya uhuru wala nafasi ya toba, Lakini Yesu ni Mfalme wa wa falme mwenye rehema, Wahubiri katika agano jipya hawapaswi kuwatisha watu, wala kuwabebesha watu mizigo, bali wanapaswa kuwafungua watu kutoka katika vifungo vyao, watu wa Mungu wana mahitaji ya aina mbalimbali na wanahitaji ukombozi wa kweli wala sio vitisho na migandamizo kutoka kwa watu waovu wanajipa mamlaka kubwa na kusahau kuwa yuko Mungu wa mbinguni na kuwa Mungu huyo ndiye anayetawala, Mungu anachokitaka kwa watu wake ni kuwatangazia habari njema huu ndio mpango wake Israel wote walikuwa wakiusubiri mpango huu ona Isaya 58:6 “ Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?       

Mungu anapenda watu wake wasamehewe, walegezewe mizigo yao inayowaelemea, wajisikie huru kutika kila aina ya uonevu na kila aina ya magereza inayowatesa hata kama ina nguvu kiasi gani nira yake ivunjwe mtu anayefanya hayo ndiye mwenye kuleta habari njema ndiye ambaye miguu yake ni mizuri kama nini, ndiye anayetangaza habari za kweli za wokovu, ni ujumbe kama huu ndio tunayaita maneno ya neema na nitangazo la namna hii ndio Yesu Kristo alikuja kulitimiza na kulifanya Luka 4;16-22 16. “Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? unaona Masihi Yesu Kristo mwenyewe alipoianza kazi ya kuhubiri injili yaani habari njema alitangaza kufunguliwa kwa watu na jamii ya watu wa kwao WALISTAAJABIA MANENO YA NEEMA YALIYOTOKA KINYWANI MWAKE. Huyu ndiye ambaye kila mtu alikuwa anamgoja anayetangaza habari ya mema, habari za amani habari za kuwaweka huru waliosetwa, habari za kuwafungua waliofungwa, habari za vipofu kuona habari ya kutangaza jubilii yaani mwaka wa bwana wa neema, Mtu wa namna hii ndiye ambaye tunasema ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari njema, kutana sasa na wale wasiotangaza habari njema miguu yao ni mibaya utasikia Leo tunamtangaza dada fulani au kaka fulani kuwa tumemkabidhi kwa shetani, leo natangaza kumtega fulani, leo namfukuza fulani kutoka katika kanisa letu, leo tunaanza mfungo wa siku miamoja, leo ni siku ya kumtolea Bwana Isaka wako, leo ameondoka katika kanisa hili habari zake ndio kwishinei, leo nalaani wanaopingana nami, dhehebu hili ndilo bora kuliko lile, muhubiri yule anahubiri mafundisho potofu na yasiyofaa, yule ndio mzinzi namba moja, huyu jamaa si aliwahi kufumaniwa, yule hanizidi mimi kwa maombi,  sisi ndio waanzilishi wa imani, sisi tunauzoefu, mimi sibabaishwi na hiki ama kile, mimi nimetembea sana nimezunguka nchi nyingi sana duniani, mimi utaniambia nini, mimi nina miaka mingi sana katika wokovu au nimekutangulia sana katikla huduma na kadhalika nisikilize, watu hawahitaji kujua umezunguka nchi ngapi, hawahitaji kujua umesoma kiasi gani watu wanahitaji kustaajabia maneno ya neema yanayotoka kinywani mwako, watu wanahitaji kutangaziwa msamaha wa dhambi,  wanahitaji wokovu, wanahitaji utawala na ufalme wa Mungu, wanahitaji kufundishwa na kuwekwa huru kutoka katika vifungo mbalimbali, wanahitaji kuelekezwa kwa masihi ili awaponye na kuwaweka huru, watu wanaotangaza habari za namna hii ni adimu sana kuwapata siku hizi, watu watamleta Isaka wao na hata Yakobo kama tu watahudumiwa vema na kutangaziwa utawala na malamaka ya kiungu hawa ndio Isaya anawatabiri kuwa ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari njema, wanaoleta habari njema wanaotangaza amani, wanaotangaza mambo mema, wanaotangaza wokovu na kuwaambia watu uko ufalme wa Mungu na kuwaelekeza watu kwa Yesu!

Ni Mizuri kama nini miguu yao, wahubirio habari ya mema!

Isaya 52:7 “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumatatu, 24 Mei 2021

Jinsi ya kutupilia mbali aibu!!


Isaya 54:4 “Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.”



Utangulizi:

Moja ya changamoto kubwa inayotukumba wanadamu tangu anguko la mwanadamu kutokea  katika bustani ya Edeni ni pamoja na changamoto ya aibu, au kuona aibu, au kutahayari. Aibu ni moja ya fedheha kubwa sana katika maisha ya mwanadamu, Hakuna mtu awaye yote anayependa kuaibishwa, Mpango wa shetani wakati wote ni kutuleta katika aibu, na kwa sababu hiyo kuna changamoto nyingi sana ambazo ibilisi huzifanya ili kutuleta katika aibu!, moja ya changamoto inayotuleta katika kuona/Kupata aibu ni pamoja na dhambi kama maandiko yasemavyo ona


Mwanzo 3:9-10 “BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.”


Adamu na Eva wazazi wetu wakubwa sana waliokuwa karibu sana na Mungu walipofanya dhambi, walijisikia aibu, kule kujiona kuwa wako uchi na kujificha ilikuwa ni ishara ya aibu kwao kwamba wamevunja sheria ya Mungu wao, ni ukweli usiopingika kuwa dhambi ni aibu ya watu wote ona


Mithali 14:34 “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.”tunapofanya maovu kwa njia ya siri tunaweza kujifikiri kuwa ni wajanja na washindi, lakini dhambi zetu zinapofuniliwa na wengine wakazijua kwetu linaweza kuwa jambo la aibu, kwa msingi huo ni wazi kuwa aibu inaleta fadhaaa kubwa!. Na hakuna mwanadamu anayependa kuaibishwa!


Aibu hasa ni nini? Aibu ni tatizo la kisaikolojia na kisosholojia (Kijamii)- (Psychosocial-Problem) linaloendeshwa na hisia, hasi zinazotokana na dhamiri ya mwanadamu kujihuhukumu kuwa hajaenenda sawa na jinsi alivyopaswa kuenenda, ni hali ya kujitathimini kihisia na kujithaminisha katika hali ya chini na hivyo kupelekea kujitoa, kujificha, kujihukumu, kukosa furaha, kutokujitokeza, kutokujiamini, kukosa nguvu na kujiona hufai! Ni hofu ya kuogopa kuwekwa wazi kwa mambo yetu yasiyofaa tuliyoyafanya sirini, na wakati mwingine hutupelekea kuwashutumu wengine kwa kusudi la kuficha mambo yetu! Neno aibu kwa kiyunani ni Aischuno ambalo maana yake ni kuvuliwa nguo hadharani Yesu analishughulikia swala hilo la mtu kuvuliwa nguo kwa kutoa ushauri wa kutoa mavazi yatakayo ficha aibu hiyo ya kuwa uchi ona “Ufunuo 3:18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Hakuna mwanadamu awaye yote mwenye akili kamili na timamu ambaye atafurahia kuwekwa uchi hadharani, jambo kama hili ni aibu kwetu na kwa kila mwanadamu mwenye akili timamu.


Aibu ni moja ya tatizo linalohitaji kutatuliwa kiroho, Mungu katika Hekima yake na mpango wake wa ukombozi alikusudia pia kutukomboa kutoka katika aibu.  Yeye kama Muumba wa Mbingu na sisi anatujua vema namna na jinsi tunavyoteswa na aibu na hivyo aliwasaidia wazazi wetu wa kwanza kuwa mbali na aibu kwa kumwaga damu ya Mnyama ili awatengenezee mavazi ya ngozi na kuwavika hii ilikuwa ni ishara ya kinabii ya kuvikwa vazi la kutuondolea aibu yetu ona Mwanzo 3:21 “BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.Kwaajili ya hayo nabii Isaya anatupa ujumbe kwamba tusifadhaike wala tusiogope na kwamba hatutatahayari wala kuaibishwa na kuwa Mungu mwenyewe ataifutilia mbali aibu yetu, hakuna wa kutushutumu wala hatutakumbuka tena aibu! Milele! Kwa hivyo ni ahadi ya Mungu kutuondolea Mauti, ni ahadi ya Mungu kutufuta machozi lakini vilevile ni ahadi ya Mungu kuiondoa aibu ya watu wake milele angalia Isaya 25:8-9 “Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.”  

             

Yesu alikuja kuiondoa aibu yetu!

Moja ya majukumu makubwa ya waamuzi,wafalme na manabii nyakati za agano la kale ilikuwa ni pamoja na kuwaondolea watu aibu, kuna aibu za aina nyingi sana, kushindwa vita ni aibu, kufungwa magoli mengi ni aibu, kufeli ni aibu, ndoa kuvunjika ni aibu, kuziniwa mkeo au mumeo ni aibu, kufukuzwa kazi ni aibu, kufanya uzembe ni aibu, kuomba omba ni aibu, kufumaniwa ni aibu, kuugua magonjwa mabaya ni aibu, kufiwa na mtu mnayemtegemea sana ni aibu, kusemwa vibaya ni aibu, kuvuliwa nguo ni aibu, kusutwa ni aibu, kudhalilishwa ni aibu, kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni aibu, kushindwa vita ni aibu, kutengwa kanisani ni aibu na maswala mengi kadhaa wa kadhaa yenye kuumiza moyo, kwa ujumla hakuna mwanadamu anayependa aibu, Na ndio maana watakatifu waliotutangulia nyakati za agano la kale walimkimbilia Mungu ili wasiabike milele Zaburi 31:1 “Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye,” Tunapokuwa tumefunikwa na aibu tunakosa ujasiri wa kufanya mambo kwa ufasaha hata katika kumtumikia Mungu, vijana wengi sana hunifuata kwa siri na kwa kuwa mimi pia ni mkuu wa shule na mchungaji, hivyo wanafunzi wengi wa kiume hunifuata na kunieleza wazi wazi, kuwa mchungaji mimi napenda sana kumtumikia Mungu na ni kweli unaweza kuona ni vijana wenye vipawa mbalimbali vya utumishi na lakini unaweza kuwaona wanakwepa kufanya huduma zao walizopewa na Mungu nao huniambia tunasumbuliwa na tatizo la kupiga punyeto na ingawa tatizo hili linafanyika kwa siri lakini dhamiri zao zinawafanya wajisikie aibu na kukosa ujasiri wa kutumika ipwaswavyo, nami huwa ninawajibu na kuwasaidia katika namna na hekima ile ambayo Mungu hunipa niwahudumie, lakini Napata jibu kuwa kama tuna mambo ya aibu hata kama watu hawajayajua, ni ya sirini yanapunguza ufanisi wetu kwa kiwango kikubwa, kuna changamoto nyingi mno zinazofanana na hizo ambazo huwanyima watu kuutumia uwezo waliopewa na Mungu kwa kuwa ndani ya mioyo yao wana hisia za aibu, na zinakuwa mbaya zaidi zinapofunuliwa katika jamii na hivyo wengi wanashindwa kujiamini, Habari njema ni kwamba Yesu ndiye mwamuzi mkuu, ndiye nabii, mkuu na ndiye mfalme mkuu, Yeye ukiacha kushughulika na maswala mengine pia alikuja kwaajili ya kutuondolea aibu, tunapokuwa na aibu tunashindwa kufanya mambo lakini tunapokuwa na ujasiri tunaweza kufanya mambo makubwa sana, Nisikilize Mungu anataka tumuone Bwana wetu Yesu Kristo kama sababu ya ujasiri wetu, wakati mwingine vilevile tunaogopa kukosea, tunatetemeka hatujiamini kwa sababu ya mambo ya aibu ya sirini au kwa sababu tunaogopa kuwamba tutakosea hatutafanya kwa ufasaha na kusababisha aibu hivyo tunaona aibu hata kabla hatujajaribu, huu ni uonevu wa ibilisi kwetu, Biblia inatuita kwamba tunapokuwa na hali kama hiyo na 

unapolemewa na aibu Mtazame Yesu –  Waebrania 12:2-3 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”


Unapolemewa na aibu Kisogelee kiti cha rehema  - Waebrania 4;15-16 “Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”


Ujasiri wetu ni katika kumtumainia Kristo – Waefeso 3:11-12 “kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.”


Kumbuka kuwa sisi wenyewe hatutoshi – 2Wakoritho 3:4-6 “Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.”   

     

Mtumaini Bwana – Warumi 5:3-4 “Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;  na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.” Tunapoweka tumaini letu kwake Mungu wetu hatatuacha tuaibike wala hatawaacha adui zetu wafurahi Zaburi 25: 1-3 “Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.”


Tumuombe yeye atufunike – Mwanzo 3:21 “BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.Mungu anaijua aibu yetu anaelewa kioa kitu tuko wazi mbele zake hatuwezi kujificha Adam hata kabla hajaomba Mungu alijua fedhea ya Adamu alieleza wazi kuwa amejificha waliposikia sauti ya Mungu kwa sababu yuko uchi, Mungu alifanya mavazi kwaajili ya Adamu na mkewe akawavika, Yesu kama mwokozi anajua kwamba anawajibika kutufunika , tukimwamini hatutaaibika kamwe Warumi 10:11 “Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.” Yaani kila amwaminiye hataaibika unaona


Tumtumikie yeye wala tusiache yeye atatusitiri – Zaburi 91:1-4 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.” na Zaburi 27:4-5 “Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake. Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.”


Hakuna wa kukushitaki Yesu ndiye mtetezi wetu – Zakaria 3:1-4 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni? Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika. Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.”    

          

Jinsi Yesu alivyoiondoa aibu yetu!

Maandiko kadhaaa hapo yametutia moyo kwamba hatupaswimkuogopa, na kuwa tunapaswa kuwa na ujasiri, kwa nini kwa sababu Kama Mungu alivyoshughulika na aibu ya adam na Eva na vilevile malaika wa bwana alivyoshughulika na aibu ya Yoshua kuhani mkuu ni ufunuo wa kimaandiko ulio wazi kuwa Yesu Kristo anashughulika na mambo yetu yote ya aibu na dhambi, Yeye alipoishughulikia dhambi pale msalabani na kuaibishwa aliaibihwa kwa niaba yetu, na kwa mateso yake akaimwaga damu yake pale msalabani ni wazi kuwa damu yake inafunika dhambi zetu na sio kufunika tu inaziondilea mbali kabisa, Yesu aliwaendea watu waliokuwa ni aibu kabisa katika jamii, wasio na matumaini wala kufikiri mkwamba itakuja itokee siku kuna mtu atawajali lakini wote aliwavuta kwake na kuwaingiza katiia mpango wake wa ukombozi, tunapozungumza wiokovu wetu ni pamoja na kufutiwa aibu yetu, hatupaswi mkuogopa wala kujidharau na kufikiri kuwa sisi hatufai hata kidogo, wala hatupaswi kuwalaumu watu, tunaye Mungu ambaye anajua kushughulika na aibu zetu kwa huruma zake na rehema zake atatufunika tunachotakiwa ni kumjia na kumueleza kuwa Bwana Yesu mimi sifai hata kidogo, nisamehe nisafishe kwa damu yako na kwa kazi yako uliyoifanya pale msalabani, na kwa njia rahisi sana weka imani kuwa amekusamehe na kukuelewa Mungu anatuelewa vizuri kuliko kiongozi yeyote wa kidini, hatupaswi kujificha, hupaswi mkuaxcha kuimba, hupaswi mkuacha kuhudhuria ibada na kumtumikia Mungu, Mwambie Bwana Yesu afanye kazi na wewe kwa utukufu wake akufiche chini ya ushindi wake akufunike kwa neema yake, usitishiwe na mtu yeyote kwa sababu wote biblia imesema wote ni wenye dhambi, wote tunaokolewa bure kwa neema kwa njia ya imani, asikutishe mtu kazi ya ukombozi sio mya mwanadamu wala haifanywi kwa vitisho vya kidini na viongozi wa kidini, wala kwa kukutenga imefanywa na Yesu pale msalabani nani yeye ndiye anayeweza kutuhukumu na kutuhesabia haki na sio mwingine, hakuna mamlaka yoyote inayoweza kukutenga na upendo wa Kristo, hata malaika hawawezi, viongozi wa dini hawawezi,  wako watu wanajipa mamlaka hata za kutenga au kukabidhi mtu kwa shetani, ni wajinga tu mwana akiwaweka huru mnakuwa huru kwelikweli watafunga hewa watatenga hewa mimi na Yesu tunaendelea kuwasiliana milele anaendelea kunibariki anaendelea kunitumia na wataisoma namba viongozi vipofu wa vipofu,  majoka wana wa majoka kuta zilizopakwa chokaa hakuna mtu wa kututenga na upendo wa Kristo, hakuna mtu mwenye hati miliki ya Mungu, ni watu waliojaa kiburi na jeusi wanaochukua nafasi ya Mungu tu wanaoweza kujifanya wana mamlaka ya kufunga lolote au kufungua lolote, nataka ujue ya kuwa mamlaka hiyo umepewa wewe na mimi, wakifunga nafungua mwenyewe wakifungua nafunga mwenyewe, wakikufukuza kwenye dhehebu lao na kuweka zengwe nenda linguine, wakikukataa anzisha la kwako liite hata kwa jina lako Muhubiri Yesu anza hata na mkeo na mwanao ahaaaaa, mpaka walalamike kuwa madhebu yamezidi utawajibu na vilabu vimezidi, acha kusikitika wanapokuaibisha kata aibu Yesu yuko kutupilia mbali uonevu Warumi 8:33 -35 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? ” kisha 38-19 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima !    

Mtu wa kumwangali


Zaburi 37:37 “Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.

 

Utangulizi:

 

Moja ya njia ya kujihakikishia kuwa tunasonga mbele katika safari ya imani, ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunasahau yaliyo nyuma na kuyachuchumilia yaliyo mbele, Hii ilikuwa njia mojawapo ya mafanikio kwa Mtume Paulo ona

 

Wafilipi 3:12-13 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;”

 

ukimuuliza mtu ni nani anaweza kuwa mtu wako wa mfano au shujaa wako, kila mmoja anaweza kuwa na watu kadhaa ambao anavutiwa nao na anawaiga kiimani, Binafsi katika maswala ya imani navutiwa sana na Bishop Zachary Kakobe kwa kuwa ndiye aliyekuwa Mchungaji wangu wa kwanza mara baada ya kuokoka niliokokea katika kanisa lake nilipoikuwa nasima Makongo Secondary Jijini Dar, Lakini pia navutiwa sana na mafundisho ya Muhubiri Mwalimu kutoka Ghana anayeitwa Mensa Otabil napenda anavyofundisha neno la Mungu, naweza kuwa na watu wa mifano katika siasa, uongozi, watumishi na kadhalika Katika Biblia ukimuacha Yesu Kristo navutiwa sana na Paulo Mtume katika agano jipya na Daudi katika agano la kale, watu tunaowafanya kuwa mfano wetu wa kuigwa, huwa tunawaiga imani zao na kuwafuata kama vile wanavyomfuata Yesu Kristo, kuwakumbuka wale waliotuongoza, waliotuambie neon la Mungu ni agizo la kibiblia ona

 

Waebrania 13:7 “Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.”    

 

Hata hivyo maandiko yanatuasa pia kuwafuata wao na kuwaiga wao kama vile wanavyomfuata Kristo kwa sababu wao ni wanadamu

 

1Wakoritho 11:1Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.” Wanadamu wote katika maandiko ambao tunaweza kuvutiwa nao na wakawa mifano kwetu walikuwa na mambo mengi na sifa nyingi njema lakini vilevile walikuwa na madhaifu ya aina mbalimbali ya kibinadamu kwa mfano:-

 

1.       Adamu na Eva – Ndio wazazi wetu wa kwanza, hawakuzaliwa waliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, walikuwa na ushirika wa karibu na Mungu wakizungumza naye usokwa uso, Mungu alikuwa muumba kwao na baba kwao, aliwadekeza na kuwamilikisha kila walichokitaka. Walipewa mamlaka mna utawqala dhidi ya kila kitu Duniani, wanyama waliwaogopa, hata hivyo walimkaidi Mungu na kumuasi kwa kula matunda waliokatazwa na Mungu,  wakawa sababu ya kuleta kifo na mauti duniani, leo hii wote tunapata tatizo la kifo kwa sababu yao ona:-

 

Mwanzo 3:11-13 “Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

 

2.       Nuhu aliyetajwa kuwa mtu wa haki mkamilifu katika vizazi vyake na kwamba alikwenda au kutembea pamoja na Mungu na katika ulimwengu uliokuwa umeoza kwa uovu yeye pekee na familia yake walipata neema Machoni pa Bwana ona

 

Mwanzo 6:8-9Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.Pamoja na ukamilifu wake wote baadaye maandiko yanatutaarifu kuwa ndiye mgunduzi wa kwanza wa Pombe na ndiye mtu wa kwanza kujihushisha na ulevi na sio hivyo tu alikunywa divai akalewa  na kusababisha aibu kubwa

 

Mwanzo 9:20-22 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.”

 

3.       Ibrahimu anayetajwa kuwa baba wa imani na rafiki wa Mungu, Baada ya miaka mingi sana ya ukimya tangu Mungu alipozungumza na Nuhu, hakuwa amezungumza na mwanadamu awaye yote kwa Karne nyingi sana mpaka alipozungumza na Abrahamu na kufanya maaganio naye Ibrahimu anaitwa mtu wa kwanza kuwa na uhusiano na Mungu aliye hai baada ya karne nyingi, Ni baba wa imani kwelikweli Imani ya kiyahudi na Kikristo na Uislamu zinaitwa Abrahamic Religions yaani ni imani ambazo mizizi yake imeanzia kwa Ibrahimu Warumi 4;16 “Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; Mungu alikuwa na urafiki wa Karibu na Ibrahimu kwatika ushirika wa ajabu sana kiasi cha kumuita rafiki yake ona Isaya 41:8 “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;” Lakini hata hivyo maandiko yanatutaarifu kuwa yeye alisema uongo zaidi ya mara moja, kwa sababu ya woga na kutokumuamini Mungu kwaajili ya ulinzi wake,

 

Mwanzo 12:18-19 “Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N'nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo? Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako.”

 

Mwanzo 20:1-5 “Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari. Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu. Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee BWANA, Je! Utaua hata taifa lenye haki? Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi. 


Isaka na Yakobo wanaotajwa na Mungu pale anaposema mimi ni Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo 


Kutoka 3:15-16 “Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri; wote tunafahamu kuwa Isaka alisema uongo vilevile Mwanzo 26:6-7 “Isaka akakaa katika Gerari. Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.Yakobo ndiye aliyekuwa muongo zaidi na mwenye hila zaidi akijifanya kuwa ni Esau na wanawe pia walimdanganya kuhusiana na habari za Yusufu kuwa aliuawa na mnyama ilhali walimuuza kwa hiyo hawa wote walikuwa ni wanadamu na walikuwa na udhaifu wao!

               

4.       Musa anayetajwa kuwa mpole au mnyenyekevu kuliko watu woote wakaao juu ya uso wa nchi Ona katika Hesabu 12;3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.” Biblia inatuambia kuwa Musa ndiye aliyekuwa mtu mpole, myenyekevu kuliko watu wiote wakliokuwa juu ya uso wanchiyeye naye kuna wakati alikasirika sana na kunena Maneno yasiyotegemewa na hata hatimaye kushindwa kumstahi Mungu pale Meriba jambo lililomkosesha kuingia katika nchi ya Kanaani, Hesabu 20:10 “Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?             

 

 Kumbukumbu 3;23-26 “Nikamnyenyekea Bwana wakati huo, nikamwambia, Ee Bwana Mungu, umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu? Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng'ambo ya Jordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni. Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, asinisikize; Bwana akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo hili.”      

5.       Daudi mtu anayetajwa na Mungu kuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wake, Matendo 13;21-22 “Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.” Wote tunafahamu ushujaa wa Daudi, mtu aiyependa uonevu, mtu mwenye kumcha Mungu, kiongozi mkuu sana wa ibada lakini maandiko nayo yanasema yeye naye alifanya dhambi ya zinaa na mke wa Uria, alimpa na mimba, alimuua na mumewe kisha akajioza yeye mke huyu wa uria ona 2Samuel 11;2-5 “Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito., 


    2Samuel 14-27Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria. Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe. Ikawa, Yoabu alipokuwa akiuhusuru mji, akamweka Uria mahali alipojua ya kuwa pana mashujaa.Watu wa mji wakatoka, wakapigana na Yoabu; na baadhi ya watu, watumishi wa Daudi, wakaanguka; Uria Mhiti naye akafa. Ndipo Yoabu akapeleka na kumwarifu Daudi habari zote za vita; akamwagiza yule mjumbe, akisema, Ukiisha kumpa mfalme habari zote za vita, itakuwa, hasira ya mfalme ikiwaka, akakuambia, Kwani mliukaribia mji namna ile ili kuupiga? Je! Hamkujua ya kuwa watapiga mishale toka ukutani? Ni nani aliyempiga Ahimeleki, mwana wa Yeru-beshethi? Je! Si mwanamke aliyemtupia jiwe la kusagia la juu kutoka ukutani? Hata akafa huko Thebesi? Kwani kuukaribia ukuta namna ile? Ndipo utakaposema, Mtumishi wako Uria, Mhiti, amekufa naye. Basi yule mjumbe akaenda, akafika na kumwonyesha Daudi yote aliyomtuma Yoabu. Yule mjumbe akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani, tukashindana nao hata mahali pa kuingilia langoni. Wapiga mishale wakatupiga sisi, watumishi wako, toka juu ya ukuta; na baadhi ya watumishi wa mfalme wamekufa, na Uria, Mhiti, mtumishi wako, amekufa naye. Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo. Na yule mke wa Uria alipopata habari ya kuwa Uria mumewe amekufa, akamwombolezea mumewe. Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza Bwana.”  

6.       Suleimani alikuwa mwenye Hekima kuliko watu wote, aliwaonya watu wajiepushe na maswala mbalimbali ya uovu katika kitabu cha mithali, lakini pia aliwataka watu wamkumbuke Mungu tangu siku za ujana wao, Mungu alizungumza na Suleimani wazi wazi, na kumtaka aombe lolote, alikuwa mtoaji kwa rekodi ambazo hazijawahi kuvunjwa 1Falme 4;29-34 “Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.” lakini aliangukia katika tamaa ya wanawake iliyokuwa ya kutisha sana akaoa wanawake wengi sana na wanawake zake wakamgeuza moyo akaabudu miungu ona 1Wafalme 11;1-4Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake              

7.       Mtume Petro alikuwa mtu wa kwanza kudai kuwa yuko tayari kwenda na Bwana Yesu gerezani na aliapa luwa hatamkana Yesu kamwe! Mathayo 26:31-33 “Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya. Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.” Petro aliahidi mbele za Yesu kuwa yeye atakuwa tayari hata kwenda naye gerezani lakini wakati wa majaribu Petro alimkana Yesu mara tatu ona Mathayo 26:69-75 “Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha. Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

 

Nini cha kujifunza?

 

Sisi wote ni wanadamu tu, manabii na mitume nao ni wanadamu, wachungaji walimu , wazee mashemasi na washirika wote ni wanadamu tu, katika namna fulanifulani za uanadamu wetu tunajikwaa Yakobo ambaye alikuwa mtume na askofu mkuu wa kanisa lililokuwako Yerusalem Ndugu yake Yesu wa kunyonya aliyeitwa James the Just alikuwa muombaji na mtu wa haki alisema katika Yakobo 3:2 “Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. Sisi sote kama binadamu tunajikwaa katika mambo mengi hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, Mungu hututumia kwa sababu ya mambo mazuri ya upande wa jambo zuri analotaka kulitimiza kwetulakini kama Mungu angelikuwa anaangalia ukamilifu wetu hakuna amabaye angeweza kusimama mbele zake sio Musa wewe wala mimi, tunapoona madhaifu kadhaa wa kadhaa kwa viongozi wa kidini, tunapaswa kukumbuka kuwa wao sio kielelezo chetu, wao ni binadamu tu, udhaifu wao hauondoi ukweli kuwa wokovu upo, Mungu anaokoa, na kielelezo chetu ntulichopewa kukifuata ni Yesu Kristo pekee, wao walitolewa ili kutumia vipawa walivyopewa na Mungu kutuelekeza kwa Kristo Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WA KRISTO;” Yesu Kristo ndiye Mwanzilishi wa imani yetu, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamfuata yeye katika mwenendo wetu wote Waebrania 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” Maandiko yanatutaka tumtazame yeye kwa sababu yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi ona Waebrania 4:15 “Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” Imani yetu haisimami kwa mtu inasimama katika Kristo Yesu, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaacha kuwaangalia wanadamu na kumtazama mtu mkamilifu ambaye mwisho wake utatupa amani, Ni Yesu pekeee aliye mkamilifum, ni Yesu pekee aliye kielelezo chetu, tutawafuata wengine na kujifunza kutoka kwao kama vile wanavyomfuata Yesu lakini wakikengeuka haiwi sababu ya sisi kulaumu, au kuacha wokovu au kurudi nyuma kwa sababu Yesu hajawahi kurudi nyuma, acha kuwatazama wanadamu mtazame Yesu, mtazame Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai acha kuwashutumu wanadamu, acha kuwaangalia wao, wao ni watu tu tunaye kuhani mkuu aliyejaribiwa katika mambo yote bila kufanya dhambi, Baba mtakatifu he is not our hero he is not our rolemode, askofu mkuu, wa jimbo waangalizia, mapadri na mashemasi na kdahalika wao sio kielelelzo chetu Yesu Kristo pekeee ndio kielelezo chetu kikuuu, yeye ndiye aliyetuita tumfuate 1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Never compromise becase someone somewhere sheor he has compromise he/she is not our example our real example is Jesus Christ the son of the living God!

 

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!.

Jumapili, 9 Mei 2021

Wewe u mwana wa mwanamke mwingine!

Waamuzi 11:1-2 “Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.”



Utangulizi:


Wewe u mwana wa mwanamke mwingine! Yalikuwa ni maneno ya kukatisha tamaa yaliyotolewa kwa kijana shujaa aliyejulikana kama Yeftha, Mwandishi wa kitabu cha Waebrania katika agano Jipya anamtaja kama mojawapo wa mashujaa wa imani ona Waebrania 11:32-34Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.”

Yeftha ni moja ya waamuzi wakubwa miongoni mwa waamuzi wanaotajwa katika Biblia, waamuzi walikuwa ni viongozi wa mpito waliotumiwa na Mungu, kuwasaidia Israel walipokuwa hawana mfalme tangu kufa kwa Yoshua mpaka kupakwa mafuta kwa mfalme wa Kwanza aliyeitwa Sauli, Jina Yeftha maana yake ni ni Bwana atafanya njia, au Bwana atafungua.

Yeftha alikataliwa na ndugu zake, baada ya kifo cha baba yake kwa sababu eti alizaliwa na mwanamke Kahaba, sababu hii inawezekana kabisa ilitokana na sifa zake kuwa alikuwa mtu mwema tene mwenye ujuzi kuhusu Mungu na hodari sana, alikuwa ni shujaa, kuzaliwa kwake na mwanamke kahaba haikuwa sababu yay eye kukata tama katika maisha yake, alijiendeleza kitabia na kuwa mtoto mwema sana kuliko wenzake kwa wivu walimkataa kwa maneno mabaya ya ubaguzi kuwa yeye ni mwana wa mwanamke mwingine hii haikuwa sababu ya kumzuia Yeftha ambae aliamua kwenda kuishi katika mji mwingine ulioitwa Tobu, watu wote hohehahe walimkusanyikia na kuishi Pamoja naye,  Israel walipoonewa na wana wa Ammoni na kuteswa vibaya walimkumbuka Yeftha na wakatuma wazee kumuomba Yeftha aje kuwa shujaa wao, naye kwa neema ya Mungu akijazwa Roho Mtakatifu, na kuonyesha ujuzi wake katika Torati na historia ya wana wa Israel alikubali kuja na kuwatetea na kuwaokoa dhidi ya wana wa Amoni ona


Waamuzi 11:4-11 “Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu; wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni. Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?  Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena, ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi. Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi Kwamba mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu? Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya sawasawa na neno lako. Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa.”


Licha ya kufanywa kiongozi na mwamuzi wa Israel ni wazi kuwa Yefhta aliijua sharia alitenda haki na hata vita yake na namna alivyokuwa anajenga hoja alijenga kwa haki, akiitumia torati, Yeftha hakuwa na makosa ni baba yaka ndiye aliyezaa na mwanamke kahaba, lakini kigezo hiki cha kilitumiwa na ndugu zake kumkataa na kumbagua, huenda jambo hili pia liliingiliwa na wazee kwa kuwa katika Israel maamuzi yasingelifanyika bila wazee kuingilia kati wote wakiwa wametiwa upofu na wivu tu, uwezo wa Yeftha katika kulijua neno la Mungu unaonekana wazi kwa hoja anazozijenga dhidi ya mfalme wa wana wa Amoni kabla hajampa mkon’goto ona

Waamuzi 11:11-28 “Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa. Basi Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una nini nami, hata umenijilia kupigana juu ya nchi yangu? Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea kutoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena pasipo matata. Yeftha akatuma wajumbe mara ya pili waende kwa huyo mfalme wa wana wa Amoni; akamwambia, Yeftha akuambia hivi; Israeli hakuitwaa nchi ya Moabu, wala nchi ya wana wa Amoni; lakini hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walienenda katika bara hata kuifikilia Bahari ya Shamu, na kufikilia Kadeshi; ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hakusikia. Ni vivyo wakampelekea wajumbe mfalme wa Moabu; wala yeye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi. Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga marago upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu. Kisha Israeli wakatuma wajumbe waende kwa Sihoni mfalme wa Waamori, mfalme wa Heshboni: Israeli wakamwambia, Twakuomba utupe ruhusa tupite katika nchi yako, mpaka mahali pangu. Lakini huyo Sihoni hakuwaamini Israeli ili wapite ndani ya mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, nao wakapanga kambi katika Yahasa, wakapigana na Israeli. Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawapiga; basi Israeli wakaimiliki hiyo nchi ya Waamori, wenye kukaa nchi hiyo. Nao wakaumiliki mpaka wote wa Waamori, tokea Arnoni hata Yaboki, tokea hiyo bara hata Yordani. Basi sasa yeye Bwana, Mungu wa Israeli, amewapokonya Waamori watoke mbele ya watu wake Israeli, na wewe wataka kuwatamalaki? Je! Wewe hutakitamalaki hicho ambacho huyo Kemoshi mungu wako akupa kukitamalaki? Kadhalika, awaye yote ambaye Bwana, Mungu wetu, amemfukuza atoke mbele yetu hao ndio tutakaowatamalaki. Na wewe sasa, je! U mwema kuliko Balaki mwana wa Sipori, huyo mfalme wa Moabu, kwa lo lote? Je! Yeye alishindana na Israeli, au kupigana nao? Wakati Israeli waliokuwa wakikaa Heshboni na miji yake, na katika Aroeri na miji yake, na katika miji hiyo yote iliyo huko kando ya Arnoni, muda wa miaka mia tatu; mbona ninyi hamkuipata tena katika majira hayo? Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye Bwana, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni. Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuyasikiza hayo maneno ya Yeftha aliompelekea.”



inaonyesha wazi jinsi alivyokuwa mtu wa haki na mwenye ujuzi wa neno la Mungu, Mungu alimjaza kwa Roho wake na kusikiliza dua yake na maombi yake akamuwezesha kuwaokowa wana wa Israel kwa kuwapiga wana wa amoni ona 


Waamuzi 11:29-33 “Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni. Naye Yeftha akamwekea Bwana nadhiri, akasema, Kwamba wewe utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu kweli, ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa. Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye Bwana akawaua mkononi mwake. Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.”


Ni dhahiri kuwa Yeftha alikuwa amekubalika na Mungu, sio lazima wakati wote tukubalike kwa wanadamu, lakini Mungu akikukubali na kuweka mkono wake lazima mlango uliofungwa na wanadamu utafunguliwa tu , lazima bwana atafanya njia, Kujitoa kwa Yeftha kwa Mungu na uaminifu wake kwa Mungu hakujawahi kufikiwa na myahudi wala mkristo awaye yote yeye ni mtuwa pekee aliyeweka nadhiri ngumu sana na kuitimiza, japokuwa kuna mgogoro mubwa wa kimjadala kuhusu Nadhiri yake, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mwana huyu wa kahaba, mtoto wa mwanamke mwingine alikuwa vizuri kwa Mungu wake kuliko wana wengine, Ni kitu gani tunaweza kujifunza kutoka kwake ni kuwa hatupaswi kukata tama katika maisha,  kila kikwazo katika maisha yetu tunaweza kukitumia kuwa nafasi ya kipekee kutupeleka katika hatua nyingine:- Hatupaswi kukatishwa tamaa na jambo lolote!


Mwanzilishi wa Kampuni ya kutengeneza injini za aina mbalimbali ikiwemo magari, pikipiki, jenereta na mashine za pump za kumwagilia na kuoshea magari Chini Japan aliyejulikana kama SOICHIRO HONDA alizaliwa mwaka 17 November 1906  na alifariki mwaka 5 August 1991 akiwa na miaka 84 Kampuni yake iliitwa Honda Motor Company ltd. Aliondoka nyumbani akiwa na miaka 15 tu na akaanza kuwa fundi wa kutengeneza magari na kuuza vifaa nya magari vilivyotumika, alikuwa nimmtu mchapakazi sana na alipenda sana magari, na kutamani kuwa fundi wa kuyatengeneza, lakini hata hivyo alikataliwa kwa sababu na mambo yalikuwa magumu kwa sababu hakuwa na Elimu yeyote, wenzake walimpa kazi ya kuwapikia chakula na kusafisha duka la spea za magari. Aliamua kujiendeleza mwenyewe ili kuendeleza kipawa chake alijiunga na timu ya mbio za magari, lakini wakati Fulani alianguka na kupata ajali ambayo ilimjeruhi mwili wake na hakuweza kuendelea tena,  na akaachana na swala la mbio za magari, Baada ya kupona Soichiro alianza kutengeneza Piston rings kwa uwezo wake, alizipeleka kwa kampuni ya TOYOTA ili awauzie, lakini walimfukuzilia mbali kwa aibu, walikataa kabia uvumbuzi wake wakisema ni wa hali ya chini, kukataliwa kwake hakukumfanya ake chini aliendelea kukazana na kuamua kuanzisha kiwanda chake hatimaye aliweza, leo hii ndio mtu mwenye pikipiki imara sana kuliko aina nyingine ya pikipiki duniani.

Mungu hamtupi mja wake, Hijalishi umetiokea katika ukoo gani, au jamii gani au una historia mbaya kiasi gani, wala haijalishi watu wanasema nini juu yako, jambo kubwa la kuuliangalia ni Mungu anasema nini juu yako, tunaweza kupitia katika hali ya kukataliwa, Lakini hilo lisitutishe tumpe Mungu nafasi ya kutuonyesha nini kiko mbele yetu, Na kwa neema na uweza wa Roho Mtakatifu Bwana atakufanya uwe kimbilio la Ndugu zako na jamaa zako wote walipokupuuzia  na kukudharau watakuja wakuinamie kumbuka jiwe walilolikataa waashi hilo limekuwa jiwe kuu la msingi Yeftha aliambiwa wewe u mwana wa mwanmke mwingine, ni kama wanamwambia wewe sio ndugu yetu halisi, lakini baadaye walikwenda kumuhitaji na kuhitaji msaada wake!


Na Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.