Zaburi
37:37 “Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu
mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.”
Utangulizi:
Moja ya njia ya kujihakikishia kuwa tunasonga
mbele katika safari ya imani, ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunasahau yaliyo
nyuma na kuyachuchumilia yaliyo mbele, Hii ilikuwa njia mojawapo ya mafanikio
kwa Mtume Paulo ona
Wafilipi
3:12-13 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha
kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa
ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba
nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma,
nikiyachuchumilia yaliyo mbele;”
ukimuuliza mtu ni nani anaweza kuwa mtu wako wa
mfano au shujaa wako, kila mmoja anaweza kuwa na watu kadhaa ambao anavutiwa
nao na anawaiga kiimani, Binafsi katika maswala ya imani navutiwa sana na
Bishop Zachary Kakobe kwa kuwa ndiye aliyekuwa Mchungaji wangu wa kwanza mara
baada ya kuokoka niliokokea katika kanisa lake nilipoikuwa nasima Makongo
Secondary Jijini Dar, Lakini pia navutiwa sana na mafundisho ya Muhubiri
Mwalimu kutoka Ghana anayeitwa Mensa Otabil napenda anavyofundisha neno la
Mungu, naweza kuwa na watu wa mifano katika siasa, uongozi, watumishi na
kadhalika Katika Biblia ukimuacha Yesu Kristo navutiwa sana na Paulo Mtume
katika agano jipya na Daudi katika agano la kale, watu tunaowafanya kuwa mfano
wetu wa kuigwa, huwa tunawaiga imani zao na kuwafuata kama vile wanavyomfuata
Yesu Kristo, kuwakumbuka wale waliotuongoza, waliotuambie neon la Mungu ni
agizo la kibiblia ona
Waebrania
13:7 “Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza,
waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao,
iigeni imani yao.”
Hata hivyo maandiko yanatuasa pia kuwafuata wao
na kuwaiga wao kama vile wanavyomfuata Kristo kwa sababu wao ni wanadamu
1Wakoritho
11:1“Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.” Wanadamu wote katika maandiko ambao tunaweza kuvutiwa nao na wakawa
mifano kwetu walikuwa na mambo mengi na sifa nyingi njema lakini vilevile
walikuwa na madhaifu ya aina mbalimbali ya kibinadamu kwa mfano:-
1. Adamu na Eva – Ndio wazazi wetu wa kwanza, hawakuzaliwa waliumbwa kwa sura na mfano wa
Mungu, walikuwa na ushirika wa karibu na Mungu wakizungumza naye usokwa uso,
Mungu alikuwa muumba kwao na baba kwao, aliwadekeza na kuwamilikisha kila
walichokitaka. Walipewa mamlaka mna utawqala dhidi ya kila kitu Duniani,
wanyama waliwaogopa, hata hivyo walimkaidi Mungu na kumuasi kwa kula matunda
waliokatazwa na Mungu, wakawa sababu ya
kuleta kifo na mauti duniani, leo hii wote tunapata tatizo la kifo kwa sababu
yao ona:-
Mwanzo 3:11-13 “Akasema,
Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza
usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa
matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili
ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.”
2.
Nuhu aliyetajwa kuwa mtu wa haki mkamilifu katika
vizazi vyake na kwamba alikwenda au kutembea pamoja na Mungu na katika
ulimwengu uliokuwa umeoza kwa uovu yeye pekee na familia yake walipata neema
Machoni pa Bwana ona
Mwanzo 6:8-9 “Lakini Nuhu
akapata neema machoni pa BWANA.Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa
haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.” Pamoja
na ukamilifu wake wote baadaye maandiko yanatutaarifu kuwa ndiye mgunduzi wa
kwanza wa Pombe na ndiye mtu wa kwanza kujihushisha na ulevi na sio hivyo tu
alikunywa divai akalewa na kusababisha
aibu kubwa
Mwanzo 9:20-22
“Nuhu
akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi
katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza
ndugu zake wawili waliokuwa nje.”
3.
Ibrahimu anayetajwa kuwa baba wa imani na rafiki wa
Mungu, Baada ya miaka mingi sana ya ukimya tangu Mungu alipozungumza na Nuhu,
hakuwa amezungumza na mwanadamu awaye yote kwa Karne nyingi sana mpaka
alipozungumza na Abrahamu na kufanya maaganio naye Ibrahimu anaitwa mtu wa
kwanza kuwa na uhusiano na Mungu aliye hai baada ya karne nyingi, Ni baba wa
imani kwelikweli Imani ya kiyahudi na Kikristo na Uislamu zinaitwa Abrahamic
Religions yaani ni imani ambazo mizizi yake imeanzia kwa Ibrahimu Warumi 4;16 “Kwa
hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe
imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya
Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote;”
Mungu
alikuwa na urafiki wa Karibu na Ibrahimu kwatika ushirika wa ajabu sana kiasi
cha kumuita rafiki yake ona Isaya 41:8 “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua;
mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;” Lakini hata hivyo maandiko yanatutaarifu kuwa yeye alisema uongo zaidi ya mara moja, kwa sababu
ya woga na kutokumuamini Mungu kwaajili ya ulinzi wake,
Mwanzo 12:18-19 “Ndipo
Farao akamwita Abramu, akasema, N'nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya
kuwa huyo ni mkeo? Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke
wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako.”
Mwanzo 20:1-5 “Ibrahimu
akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye
akatembea katika Gerari. Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu.
Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. Lakini Mungu
akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa
sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu. Basi Abimeleki alikuwa
hakumkaribia, akasema, Ee BWANA, Je! Utaua hata taifa lenye haki? Je!
Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema,
Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono
yangu, nimefanya hivi.”
Isaka na Yakobo wanaotajwa na Mungu pale anaposema mimi ni Mungu wa
Ibrahimu Isaka na Yakobo
Kutoka 3:15-16
“Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa
Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa
Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele,
nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.Enenda, ukawakusanye wazee wa
Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu
wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona
mnayotendewa huko Misri;” wote
tunafahamu kuwa Isaka alisema uongo vilevile Mwanzo 26:6-7 “Isaka akakaa katika Gerari.
Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu
maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya
Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.” Yakobo ndiye aliyekuwa
muongo zaidi na mwenye hila zaidi akijifanya kuwa ni Esau na wanawe pia
walimdanganya kuhusiana na habari za Yusufu kuwa aliuawa na mnyama ilhali
walimuuza kwa hiyo hawa wote walikuwa ni wanadamu na walikuwa na udhaifu wao!
4.
Musa anayetajwa kuwa mpole au mnyenyekevu kuliko watu
woote wakaao juu ya uso wa nchi Ona katika
Hesabu 12;3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa
mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.” Biblia
inatuambia kuwa Musa ndiye aliyekuwa mtu mpole, myenyekevu kuliko watu wiote
wakliokuwa juu ya uso wanchi” yeye naye kuna wakati alikasirika sana
na kunena Maneno yasiyotegemewa na hata hatimaye kushindwa kumstahi Mungu pale
Meriba jambo lililomkosesha kuingia katika nchi ya Kanaani, Hesabu 20:10 “Musa na Haruni
wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi;
je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? ”
Kumbukumbu 3;23-26 “Nikamnyenyekea
Bwana wakati huo, nikamwambia, Ee Bwana Mungu, umeanza kumwonyesha mtumishi
wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au
duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye
nguvu? Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng'ambo ya
Jordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni. Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa
ajili yenu, asinisikize; Bwana akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi
jambo hili.”
5.
Daudi mtu anayetajwa na Mungu kuwa ni mtu
aliyeupendeza moyo wake, Matendo
13;21-22 “Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu
akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka
arobaini. Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye
alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo
wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.” Wote tunafahamu ushujaa wa
Daudi, mtu aiyependa uonevu, mtu mwenye kumcha Mungu, kiongozi mkuu sana wa
ibada lakini maandiko nayo yanasema yeye naye alifanya dhambi ya zinaa na mke
wa Uria, alimpa na mimba, alimuua na mumewe kisha akajioza yeye mke huyu wa
uria ona 2Samuel 11;2-5 “Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani,
akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona
mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je!
Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka
wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke
amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke
akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito.,
2Samuel 14-27 “Hata ikawa
asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria. Akaandika
katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha
ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe. Ikawa, Yoabu alipokuwa akiuhusuru mji,
akamweka Uria mahali alipojua ya kuwa pana mashujaa.Watu wa mji wakatoka,
wakapigana na Yoabu; na baadhi ya watu, watumishi wa Daudi, wakaanguka; Uria
Mhiti naye akafa. Ndipo Yoabu akapeleka na kumwarifu Daudi habari zote za vita;
akamwagiza yule mjumbe, akisema, Ukiisha kumpa mfalme habari zote za vita, itakuwa,
hasira ya mfalme ikiwaka, akakuambia, Kwani mliukaribia mji namna ile ili
kuupiga? Je! Hamkujua ya kuwa watapiga mishale toka ukutani? Ni nani aliyempiga
Ahimeleki, mwana wa Yeru-beshethi? Je! Si mwanamke aliyemtupia jiwe la kusagia
la juu kutoka ukutani? Hata akafa huko Thebesi? Kwani kuukaribia ukuta namna
ile? Ndipo utakaposema, Mtumishi wako Uria, Mhiti, amekufa naye. Basi yule
mjumbe akaenda, akafika na kumwonyesha Daudi yote aliyomtuma Yoabu. Yule mjumbe
akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani,
tukashindana nao hata mahali pa kuingilia langoni. Wapiga mishale wakatupiga
sisi, watumishi wako, toka juu ya ukuta; na baadhi ya watumishi wa mfalme
wamekufa, na Uria, Mhiti, mtumishi wako, amekufa naye. Basi Daudi akamwambia
yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni
pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako
juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo. Na yule mke wa Uria alipopata habari ya
kuwa Uria mumewe amekufa, akamwombolezea mumewe. Hata maombolezo hayo
yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa
mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza Bwana.”
6.
Suleimani alikuwa mwenye Hekima
kuliko watu wote, aliwaonya watu wajiepushe na maswala mbalimbali ya uovu
katika kitabu cha mithali, lakini pia aliwataka watu wamkumbuke Mungu tangu
siku za ujana wao, Mungu alizungumza na Suleimani wazi wazi, na kumtaka aombe
lolote, alikuwa mtoaji kwa rekodi ambazo hazijawahi kuvunjwa 1Falme 4;29-34 “Mungu
akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko
pwani. Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima
zote za Misri. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani
Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake
kati ya mataifa yote yaliyozunguka. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo
zake zilikuwa elfu moja na tano. Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko
Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege,
na vitambaavyo, na samaki. Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya
Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima
yake.” lakini aliangukia katika tamaa ya wanawake iliyokuwa ya
kutisha sana akaoa wanawake wengi sana na wanawake zake wakamgeuza moyo
akaabudu miungu ona 1Wafalme 11;1-4 “Mfalme Sulemani
akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa
Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,na wa
mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie
kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana
nao kwa kuwapenda.Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu;
nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake
wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu
kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake”
7.
Mtume Petro alikuwa mtu wa kwanza
kudai kuwa yuko tayari kwenda na Bwana Yesu gerezani na aliapa luwa hatamkana
Yesu kamwe! Mathayo 26:31-33 “Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili
yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi
watatawanyika.Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.
Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi
sitachukizwa kamwe.” Petro aliahidi mbele za Yesu kuwa yeye atakuwa
tayari hata kwenda naye gerezani lakini wakati wa majaribu Petro alimkana Yesu
mara tatu ona Mathayo 26:69-75 “Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja
akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana
mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. Naye alipotoka nje hata ukumbini,
mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo
pamoja na Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.Punde kidogo,
wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja
wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha. Ndipo akaanza kulaani na kuapa
akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.Petro akalikumbuka lile neno la
Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje,
akalia kwa majonzi.”
Nini
cha kujifunza?
Sisi wote ni wanadamu tu, manabii na mitume nao
ni wanadamu, wachungaji walimu , wazee mashemasi na washirika wote ni wanadamu
tu, katika namna fulanifulani za uanadamu wetu tunajikwaa Yakobo ambaye alikuwa
mtume na askofu mkuu wa kanisa lililokuwako Yerusalem Ndugu yake Yesu wa
kunyonya aliyeitwa James the Just alikuwa muombaji na mtu wa haki alisema katika
Yakobo 3:2 “Maana
twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo
ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.” Sisi sote kama binadamu tunajikwaa katika
mambo mengi hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, Mungu hututumia kwa sababu ya
mambo mazuri ya upande wa jambo zuri analotaka kulitimiza kwetulakini kama
Mungu angelikuwa anaangalia ukamilifu wetu hakuna amabaye angeweza kusimama
mbele zake sio Musa wewe wala mimi, tunapoona madhaifu kadhaa wa kadhaa kwa
viongozi wa kidini, tunapaswa kukumbuka kuwa wao sio kielelezo chetu, wao ni
binadamu tu, udhaifu wao hauondoi ukweli kuwa wokovu upo, Mungu anaokoa, na
kielelezo chetu ntulichopewa kukifuata ni Yesu Kristo pekee, wao walitolewa ili
kutumia vipawa walivyopewa na Mungu kutuelekeza kwa Kristo Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa
mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa
wachungaji na waalimu;kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WA KRISTO;” Yesu Kristo
ndiye Mwanzilishi wa imani yetu, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamfuata yeye
katika mwenendo wetu wote Waebrania 12:2
“tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye
kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake
aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha
enzi cha Mungu.” Maandiko yanatutaka tumtazame yeye kwa sababu yeye
alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi ona Waebrania 4:15 “Kwa
kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu;
bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.”
Imani yetu haisimami kwa mtu inasimama katika Kristo Yesu, hatuna budi
kuhakikisha kuwa tunaacha kuwaangalia wanadamu na kumtazama mtu mkamilifu
ambaye mwisho wake utatupa amani, Ni Yesu pekeee aliye mkamilifum, ni Yesu
pekee aliye kielelezo chetu, tutawafuata wengine na kujifunza kutoka kwao kama
vile wanavyomfuata Yesu lakini wakikengeuka haiwi sababu ya sisi kulaumu, au
kuacha wokovu au kurudi nyuma kwa sababu Yesu hajawahi kurudi nyuma, acha
kuwatazama wanadamu mtazame Yesu, mtazame Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai
acha kuwashutumu wanadamu, acha kuwaangalia wao, wao ni watu tu tunaye kuhani
mkuu aliyejaribiwa katika mambo yote bila kufanya dhambi, Baba mtakatifu he is
not our hero he is not our rolemode, askofu mkuu, wa jimbo waangalizia, mapadri
na mashemasi na kdahalika wao sio kielelelzo chetu Yesu Kristo pekeee ndio
kielelezo chetu kikuuu, yeye ndiye aliyetuita tumfuate 1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita
alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa
maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Never
compromise becase someone somewhere sheor he has compromise he/she is not our
example our real example is Jesus Christ the son of the living God!
Rev.
Innocent Samuel Kamote
Mkuu
wa Wajenzi mwenye Hekima!.