Warumi 8:32 “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?”
Utangulizi:
Moja ya sifa kubwa sana ya Mungu
wetu ni pamoja na kuwa Mkarimu, Maandiko yanatufunza sisi nasi kuwa wakarimu,
Waebrania 13:2 “Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Lakini hata hivyo yanamfunua kuwa Mungu ni zaidi ya Ukarimu, hii inapimwa na andiko hili katika Warumi 8:32 Mstari huu unaakisi kinabii tendo lililofanywa na Abrahamu aliyekuwa na upendo mkubwa sana kwa Mungu kiasi cha kuwa tayari kumtoa Isaka.

Kimsingi na kinabii Ibrahimu
alikuwa anamwakilisha Mungu na Isaka anamwakilisha Yesu, Tendo la Ibrahimu kuwa
tayari kumtoa mwana wake wa pekee Isaka kwa Mungu, Hali kadhalika ni picha
halisi ya namna na jinsi Mungu alivyokuwa mkarimu kiasi cha kuwa tayari kutoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwetu, na kwa
ulimwengu mzima kwa ujumla Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele.” Mungu yu aonyesha zaidi
ya ukarimu kwa kumtoa mwanae wa Pekee Yesu Kristo kuja ulimwenguni kwa watu
wasiofaa ili awaokoe huu ni zaidi ya ukarimu Yesu Kristo ni zawadi ya juu na
kubwa mno ambayo tumepata kupewa kama wanadamu Isaya nabii anaielezea zawadi
hii namna na jinsi Yesu alivyo zawadi kubwa mno na yenye thamani na nguvu ona!
Isaya 9:6-7 “Maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele,
Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa
hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio
utakaotenda hayo.”
Tumepewa Isaya anasema
tumekarimiwa ni zawadi ya mtoto wa kipekee mwanamume, ni mfalme serekali iko
mabegani mwake ni mshauri wa ajabu, ni Mungu mwenye nguvu na baba wa milele na mfalme
wa amani, hana mwanzo wala mwisho ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, Huyu
ni Yesu Kristo ni zawadi kubwa mno ni zawadi ya kipekee sana ni zawadi kubwa
Mungu kutupa Yesu ameonyesha zaidi ya Ukarimu
Huu ni upendo mkubwa mno kwa
kupewa Yesu Kristo kuwa zawadi kubwa kwetu:-
·
Hakuna wa kutushitaki
·
Hakuna wa kutuhukumu
·
Hakuna wa kututenga na upendo wa Mungu ulio
katika Kristo Bwana wetu
Orodhesha chochote unachoweza
kuorodhesha hakuna kinachoweza kulinganishwa na upendo wa Mungu kwetu na
ukarimu wake wa kupita kawaida
Warumi 8:33-39 inasema “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Sasa basi ikiwa upendo wa Mungu
kwetu ni mkubwa namna hii Paulo mtume anasema kwamba Kama Mungu alimuachilia
mwana wake wa pekee kwaajili yetu atashindwaje kutukirimia na mambo mengine?
Atatukarimia mambo yote pamoja naye, kama ametupa Yesu Kristo ni rahisi,
kupewa Mume, ni rahisi kupewa mtoto, ni
rahisi kupewa ufaulu katika mitihani yako, ni rahisi kupewa gari, ni rahisi
kupewa nyumba, ni rahisi kupewa Hekima
1Wafalme 3:5-13 “Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.”

Suleimani aliomba Hekima lakini
Mungu alimuongezea Utajiri na heshima kubwa sana, Mungu alidhihirisha kuwa yeye
ni zaidi ya ukarimu, yeye anaweza kutupa lolote tuliombalo na tulitakalo kwa
kadiri ya wingi wa rehema zake na neema yake, Yesu ni zaidi ya Hekima, Yesu ndio Hekima
yenyewe kutoka Mbinguni unapokuwa naye unakuwa na kila kitu, Ukimtafuta yeye
mambo mengine yote utazidishiwa, Yesu ndio zawadi ya juu kabisa ambayo Mungu
amepata kuwapa wanadamu, nyingine ni ndogo Yesu ni zawadi kubwa mno sasa Kama Mungu ametupa Yesu Kristo ni wazi kuwa
ametupa kila kitu hatatuzuilia maswala mepesi tuyaombayo kwa kuwa amekwisha
tenda jambo zito kuliko yote kutupa Yesu Kristo kama zawadi ya pekee ni
kwaajili ya sababu hii nzito Paulo mtume anahoji kuwa kama Mungu hakumuachilia
Yesu Kristo mwana wake wa pekee alimtoa kwaajili yetu, atakosaje atashindwaje
atasitaje kutukirimia mambo yote pamoja naye kumbuka kuwa mambo yote pamoja
naye yaani ukisha kuwa na Kristo ambaye ndiye mfalme wa Ufalme wa mbinguni
hutakosa kamwe kupewa mengineyo huu ni zaidi ya ukarimu!
Warumi 8:32 “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa
ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?”
Ni zaidi ya Ukarimu
Na Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
Rev. Innocent Kamote
0718990796.
Maoni 1 :
Amina Mchungaji
Chapisha Maoni