Jumanne, 8 Machi 2016

Jinsi Quran Ilivyopatikana



      Kama woote tunavyofahamu kuwa Duniani ziko dini nyingi sana na zote zina vitabu vyake vitakatifu vinavyodaiwa kuwa ni neno la Mungu na kuwa ndio mamlaka ya mwisho ya dini hizo wahindu wana kitabu chao kiitwacho (Vedas),na sikhiism(Adigranth),Confusian(Analets),Shinto (Nihong),Na Budha (Dharma),Judaism(Torati),Islam(quran) na sisi wakristo Biblia agano jipya na Kale,na Kila mmoja anaamini kuwa ni neno la Mungu katika eneo hili tutakuwa tukijiuliza swali je Quran ni neno lu Mungu na tutafanya upembuzi yakinifu kwa kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-

·         Jinsi quran ilivyopatikana na muundo wake
·         Jinsi quran inavyopotosha kweli za kibiblia
·         Jinsi quran inavyomuelezea Yesu masihi
·         Jinsi quran inavyojikanganya yenyewe

Jinsi quran ilivyopatikana na muundo wake.
     Kabla ya kuchambua jinsi quran ilivyopatikana ni muhimu kujikumbusha kwamba quran ni nini? Quran ndio kitabu kitakatifu na mamlaka ya mwisho kwa waislamu,qurani ni neno la kiarabu cha kikuresh lanye maana ya “recitation” yaani yaliyo kaririwa,quran ilitokana na aya alizokuwa akizitoa Muhamad kwa madai kuwa zilitoka kwa Allah kupitia malaika Jibril,tangu alipomkaba na kumuamuru kuikariri kwa Kumwambia “Iqraa-bism-rabik” yaani soma na ukariri,Muhamad aliendelea aliendelea kutoa aya hizo kwa miaka 23, Waislamu huamini kuwa aya hizo zilitolewa kipandekipande toka katika kitabu halisi kilichoko mbinaguni,Muhamadi alitoa aya hizo kwa kuzisema kwa Maswahaba wake ambao walizikariri kichwani (Hawakuwa wanajua kusoma wala kuandika) baada ya kifo chake Muhamad aya hizo zilikusanywa toka kwa maswahaba mbalimbali na kuwa kitabu kimoja kiitwacho quran leo,Maswala mengine kuhusu Muhamad na maisha yake yamekusanywa katika vitabu vya hadithi ambavyo pia hutumika katika kutafasiri quran 

Muhamad alipokea aya hizo za Quran kwa namna zifuatazo (aya au wahyi)
      Kwa mujibu wa vyanzo vya kiislamu Muhamad alipokuwa anapokea aya hizo alikuwa anavamiwa na nguvu za kigeni zilizomuathiri sana na kumpa shida sana kama inavyokua kwa mgonjwa wa kifafa, aliunguruma kama mtoto wa ngamia huku akitoa povu mdomoni,Alitisha na kutia huruma hali hizi zilikuwa zikimpata kila alipokuwa anataka kutoa aya hizo,wanasema wakati mwingine alikuwa anaanza kusikia mlio kama kundikubwa la nyuki likimjia vinaeleza vyazo hivyo vya kiislamu! Jambo lililopelekea watu waliomuona kumpa majina yafuatayo

Ø  Walimuita aliyepagawa au mwendawazimu (Surat as-saafat 37:35-36,dukhan 44:13-14,at-tur 52:29,qalam 68:1-2,Takwyr 81:22).
Ø  Walimuita mchawi (Yunus 10;2,surat sad 38;4,az-Zumar 39:41)
Ø  Wengine walifikiri amerogwa (Ban Israel 17:47-48,fur-qan 25:4-5,8)
Ø  Aliitwa pia mpiga ramli au mtunga Mashairi (Tur 52;29, haqqah 39;41)

  Muhamad alidai pia kuletewa aya hizo na malaika Jibril ambae kwa mujibu wa quran ndie malaika mkuu, wakati mwingine alidai kusikia sauti ikimpa aya, na wakati mwingine alitoa aya hizo moyoni mwake au alioteshwa ndoto au kupewa ufunuo (Surat nasm 53:1-11)
  Muhamad alihubiri quran na mafundisho yake na kupata matokeo hafifu sana hali hii ilimkatisha tama hususani pale makka ambapo watu walimpinga sana akiwemo baba yake mdogo Abu Lahib na hivyo alimlaani na kumtaja kama mtu wa motoni kwa muongozo wa Allah soma kitabu maisha ya nabii Muhamad uk 19 kifungu cha mwisho n auk 20 kifungu cha kwanza na cha pili.Baada ya upinzani mkali Muhamad ili apatane na  watu wa makka alibadilisha aya  na kuleta aya inayoitambua miungu ya ndugu zake aya hiyo husomeka hivi “…….Je mumewaona lat.uzza na manta? Hawa watatu maombi yao (wanayo waombea) ni ya kutumainiwa (Surat sad 38;5-7).Miungu hiyo ni ile iliyoabudiwa na wapagani wa pale Makka na kufanyiwa hijja,alipoulizwa kuhusu kigeugeu chake cha kubadilisha  aya mara kwa mara alidai kuwa Zilitoka kwa shetani hivyo jibrili aliiondoa sehemu ya pili ya aya hiyo hivyo sasa inasomeka hivi(Surat nasm 53:19-20) Hivyo ndani ya quran ziko aya nyingi sana zinazopingana na nyingine zimebadilishwa na watu kama tutakavyoona mbeleni.
     Mungu wa Muhamad mwenyewe alikuwa na kigeugeu kwa kumletea aya na kuzibadili baadae mfano (al-baqara 2;106,an- nahil 16;101) hivyo Muhamad alibadili aya za quran katika maeneo mengi na kubadili nyingine,aya zilizoondolewa  ziliitwa “Mansukh” na zile zilizokuja kubadili nyingine ziliitwa “Nasikh” Hizi ni aya zilizo karabatiwa “the law of abrogation” bahati mbaya aya zoote hizi zimo katika quran na zilizobadilishwa zinakadiriwa kufikia kati ya “5-500” kwa mujibu wa mwanazuoni wa kiislamu Jalalud-din baadhi ya aya hizi ni pamoja na

Ø  ……Asilazimishwe mtu kuingia dini (Baqara 2;256)ilibatilishwa kwa (Surat as saf 61:10-12)
Ø  …....Muelekeo wa wakati wa kusali (Baqara 2:142) ilibatilishwa kwa(Baqara 2;147)
Ø  ……Amri ya kuomba usiku (al Muzzamil 73;2) ilibatilishwa kwa (al Muzzamil 73:20)
Ø  …..Adhabu ya wazinzi (an Nisaa 4;15-16) ilibatilishwa kwa (an-Nur 24:2)

Hizi ni baadhi tu ya aya zinazo jikanganya zenyewe Muda usingeweza kutosha kuandika na nyingine zinazopingana zenyewe kwa zenyewe.

  Muundo wa quran.
     Qurani imeundwa na baadhi ya mila na tamaduni mbalimbali za kiarabu na mchanganyiko wa dini mbalimbali,na mambo mengine yametoka katika vitabu vya tamaduni za kiyahudi za kiyahudi kama Talmud na Mishna,pia kuna tamaduni za kiajemi hii ni kwa sababu Muhamad alikuwa na rafiki wa kiajemi aliyeitwa Salman,pia kuna vihistoria toka kwenye Biblia ingawa vimepinda huenda ni kwa sababu ya Makosa ya kukariri au kwa sbabu ya kutokujua kusoma kwa Muhamad na maswahaba wake au kazi ya shetani kupotosha ukweli,aidha kuna tamaduni nyingi za kipagani hasa za pale arabuni makka na mawazo ya Muhamad mwenyewe.

Jinsi quran inavyopotosha kweli za kibiblia .
     Quran ni kitabu kilichojaa hadithi za kudandiadandia toka kwenye biblia  na ambazo nyingi haziko sahihi na zinapingana  na kupotosha kweli zilizomo katika biblia,Hadithi nyingi katika qurani ni tofauti na zile zilizomo katika biblia, Biblia ina masimulizi yanayojitosheleza yenye mwanzo mpaka mwisho,ni rahisi kujua kipi ni kipi na kipi utakipata wapi,lakini sivyo ilivyo katika quran hadithi zake ni za kudandiadandia hiki au kile wakati mwingine bila kujua mwanzo wala mwisho au kupata habari kamili labda ndio maana Muhamad alirejea mara kwa mara kuwataka waislamu kutuuliza sisi tuliopewa vitabu kabla yao hapa chini Tutachambua mambo ambayo qurani imepotosha au kudanganya tofauti na biblia;-
Ø  Q. Nuhu alikuwa na mtoto mmoja aliyekufa kwa gharika(hud 11;40-45).
Ø  B. Nuhu alipata neema machoni pa bwana yeye na uzao wake yaani watoto wake woote watatu (Mwanzo sura ya 6-7).
Ø  Q. Baba wa Ibrahimu ni azar (al anam 6:74)
Ø  B.  Baba wa Ibrahimu ni Tera (Mwanzo11;31)
Ø  Q. Musa aliokotwa na mke wa Farao (ak qasas 28;9).
Ø  B.  Musa aliokotwa na binti wa Farao (kutoka 2;5-10).
Ø  Q. Farao alimwambia Haman ajenge mnara wa Babel (al qasas28:38)
Ø  B. Mnara wa Babel ulijengwa na Nimrod (Mwanzo 10:32,11:4) pia habari hizi Quran imezungumza uongo kwani kuna tofauti Farao aliishi miaka 800 baada ya Mnara wa babel na Haman aliishi miaka 900 baada ya Farao hivyo kuna tofauti ya miaka 1700 tangu mnara wa babel na kuishi kwa Haman.
Ø  Q. Inafundisha kuwa mariam mamayake Yesu ni dada wa Haruni mtoto wa Imran (surat Maryam 19;17-28).
Ø  B. Huu ni uongo,Je hii ina maana Musa ni mjomba wa Yesu masihi kama Mariam ni dada wa Haruni kakaye na Musa? Naona hapa Muhamad na Allah wali Comfuse yaani walichanganya mada, Habari za Mariam mama wa Yesu na habari za Mariam (Miriam) dada wa Haruni na Musa zina tofauti ya miaka kama 1400 hivi k.k.
Ø  Q. Yesu alizaliwa chini ya mtende (Maryam 19:23)
Ø  B. Yesu alizaliwa katika hori ya Ngo’mbe (Luka 2;8-18)
Ø  Q. Zekaria alikuwa bubu siku tatu (Maryam 19:10-11).
Ø  B.  Zekaria alikuwa bubu mpaka alipozaliwa mtoto (Luka 1;8-22,57-64).
Ø  Q. Roho mtakatifu ni malaika Jibril (al baqara 2;87).
Ø  B.  Roho mtakatifu ni Mungu ni tofauti na malaika (Luka 1:26-35, Matendo 5:3-4).
Ø  Q.  Ishmael ndiye aliyetolewa sadaka na Ibrahimu ( as saafat 37:99-111)
Ø  B.   Isaka ndiye aliyetolewa sadaka na Ibrahimu (mwanzo 22:1-19).
Q……Inawakilisha Quran.
B……Inawakilisha Biblia.
     Yako mambo mengi sana ambayo quran inapingana na biblia ambalo ndio neno la Mungu,ndio maana tunaona kuna dosari nyingi katika quran zinazotuthibitishia kuwa si kitabu cha kuaminika sana kwani kilikuja baadae sana kuliko Biblia ambayo ni ya zamani zaidi lakini imetunza kweli kwa usahihi 

Jinsi quran inavyo Muelezea Yesu kristo.-
     Qurani na waislamu huwa wanapinga kuwa Yesu si Mungu huku quran yenyewe inamuelezea Kristo katika viwango vya juu na vya kipekee kuliko vya nabii yeyote na vya kipekee kuliko hata Muhamad, namna quran inavyomuelezea Kristo inamaanisha wazi kabisa kuwa Yesu ni Bwana.
  • Yesu alikuwa ni Muujiza kwa ulimwengu (al-Nabbiya 21;91)
  • Alizaliwa na Bikira (surat Maryam 19;20-21) kukubali hilo ni sawa na Kukubali kuwa biblia inasema kweli (luka 1;28-35,Isaya 7;14,9:6).
  • Alifanywa Ishara (muujiza waziwazi) surat az-zukhuf 43:63) hii ni sawa na kusema alifanywa ishara ili watu wamuamini yeye (Yohana 20;30-31,5;36)
  • Alikuwa mtakatifu hakuwa na dhambi (Maryam 19;21,21;19) sifa ya utakatifu ni ya Mungu peke yake.
  • Ni ishara kwa wanadamu woote(surat Maryam 19;21 al anbiyaa 21;19)Hivyo Yesu ni muujiza kwa watu woote ili wapate kumuamini   ( Yohana 6;25-35)
  • Qurani inamkiri Yesu kuwa ni Masihi (Surat an Nisaa 4;171-172),mtu yeyote anaekubali kuwa Yesu ni masihi maana yake amekubali kuwa Yesu ndie ufunuo wa mwisho kabisa wa mambo yote na kuwa ndie ambae watu walikuwa wakimgojea (Yohana 4;15-26).
  • Amejazwa roho mtakatifu (al Baqara 2;87) kwa kawaida waislamu hudai kuwa roho ni jibril (Luka 1;28-35)Roho ni tofauti na jibril lazima waislamu wajue kuwa Roho mtakatifu ni Mungu.(Mdo 5;3-7)
  • Alipaa Mbingini (surat an Nisaa 4;158)
  • Alilisha watu mikate (al Maida 5;112-115) kukubali Ishara hii ni kukubali kuwa Yesu ni nabii yule ajae ulimwenguni aliye tabiriwa na Musa (Yohana 6;1-14)
  • Ni alama ya kiama (Ishara) (al Zukhuf 43;61) maana yake mpaka yeye aje ndipo mwisho utakapokuja,yeye ndiye atakayehukumu na ndiye atakayefufua wafu soma ufafanuzi wa ayahii,atawafufua wafu akiwamo Muhamad( Yohana 5;22-23) soma pia injili ya barnaba uk 11.
Quran na aya za shetani.

Kama tulivyoona hapo juu kuhusu kuweko kwa kigeugeu kati ya mungu wa muhamad  ambaye alimletea aya  na kasha kuzibadili baadaye  Al-Baqara 2; 106 na an nahil 16;101 hivyo Muhamad  alibadili aya Mansukh na kuleta aya nyingine Nasikh ambazo nyingi zilikuwa zinagusa mahitaji yake kama kuoa wanawake aliojitakia hata wakiwamo wake za watu, kuna wakati ambapo Muhamad mwenyewe aliulizwa kuhusu kigeugeu alicho nacho na alidai kuwa shetani alikuwa amemdanganya  na kumletea aya zisizostahili Mwandishi maarufu wa Novel wa kiingerezamwenye asili ya kihindi bwana Salman Rushdie aliweza kukosoa  kiasi kikubwa cha aya hizo katika novel; yake iliyopewa jina la Aya za shetani (The Satanic Verses)


Pichani Bwana Salman Rushdie Mwandishi maarufu wa Novel nchini uingereza ambaye alilazimika kukaa mafichoni baada ya kuandika kitabu chake kiitwacho Aya za shetani mwaka 1988 Jambo lililopelekea Ayatollah Khomein Kiongozi wa kidini wa Iran kuagiza kuwa bwana huyu auwawe, wengi wa waislamu walifikiri kuwa kitabu chake kinaushambulia uislamu.

      Ukweli kuhusu kitabu hiki unaweza kubaki palepale nasema unaweza kubaki palepale hasa unapoangalia mfumo mzima wa Quran na uislamu na tamaduni zake na maisha ya nabii Muhamad kwa ujumla utaweza kuona zinaa ikihalalishwa kwa visingizio vya kuletewa aya, uchawi, uhusiano na majini, msisitizo wa ugaidi, mfumo wa kukubali kuua au kuuawa kwaajili ya mwenyezi Mungu hata ingawa anatajwa kuwa mwingi wa rehema lakini mfumo mzima wa kiislamu hauonyeshi kivitendo kama kweli Mungu ni wa Rehema  na badala yake sisi tunaona utendaji mkubwa wa shetani ukitenda kazi kwani Kristo alisema kazi ya ibilisi ni kuvunja, kuiba, kuchinja na kuua Yohana 10;10 “Mwivi haji ila aibena kuchinja na kuharibu mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele”Kazi ya Yesu Kristo na agizo lake katika injili ni kuleta uzima na sio kuua kama yalivyo maagizo katika Quran.
Kama wewe ni Muislama ukishaifahamu kweli hii Okoka haraka acha kupoteza Muda!

Mambo yaliyokuwako kabla ya Uislamu



     Ni muhimu kufahamu kuwa yako mambo yaliyokuwepo kabla ya uislamu na ambayo waislamu huyaamini na kuyaabudu hata sasa umuhimu wa kuyajua haya ni kupata uthibitisho ulio dhahiri kuwa uislamu ni upagani ulioboreshwa tu na kuwa Muhamad hakuleta jambo jipya

Mungu anayeabudiwa na waislamu aitwae allah.
   Mungu huyu anayeitwa allah kwa asili sio Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo aliyewatoa Israel huko Misri kwa mkono wa nguvu na kujitambulisha  kwa Musa kwa jina la Yehova katika (Kutoka 6;2-3)Kinyume na huyu allah alikuwa ni mungu wa wapagani ambae awali alikuwa  na mabinti zake watatu au wakeze watatu ambao waliitwa al- lat (mungu jua),al-manat (mungu sayari venus au nyota) na al-uza (mwenye nguvu)Mkuu wao aliitwa Hubal ambae baadae alikuja kujulikana kama allah na ndiye aliyekuwa mungu wa mji wa makka (Surat an najim-nyota 53;19-20)Mungu huyu ndiye anayeabudiwa na waislamu leo na jitu lililomtokea Muhamad lilimuamuru kumuabudu mola huyu wa nji wa makka soma(surat Naml-sisimizi 27;91) miungu hii ilikuwa maarufu pale makka wakati Muhamad anazaliwa (Najm 53;21-23)na huyu allah alikuwa mungu mwezi,inaaminika na baadhi ya wasomi kuwa jina allah au al-llah linatokana na jina Ilah ambae alikuwa mungu mwezi wa Arabia ya kusini ambao waliamini mungu mmoja bila kudharau mingine hivyo kwa asili waislamu wanaabudu mwezi na nyota hata Muhamad mwenyewe alipotaka kuapa aliapa kwa Nyota soma (Najm 53;1)  miungu mingine iliyokuwepo ni pamoja na  wadd (pia mungu mwezi) suw’a,yaguth na nasr soma (surat Nuhu 71;23)

Jiwe jeusi katikati ya msikiti wa makka “Hajar al aswad”.
    Jiwe hili jeusi hajar al aswad ni nyota au kimondo kilichoanguka zamani sana,Jiwe hili ndilo lilikuwa al kaaba ya wapagani, Ambao waliliabudu na kulisujudia soma kitabu maisha ya nabii Muhamad  ukurasa wa 15-16 kifungu h. mahali hapa muhamad alipozaliwa tu alifanyiwa duwa na babu yake soma kitabu hicho uk wa 5 kifungu cha mwisho.Hapa ndipo wanapoabudu waislamu woote duniani huelekea hapo wakati wa sala na huenda hapo kufanya hija na hulisujudia jiwe hili na kuliabudu  kama unabisha soma kitabu vipi uhiji uk 29 cha shehk A.Suleman.Lazima ulisogelee jiwe hilo uweke mkono na kulibusu na kulisujudia mara tatu.Muhamad alipofikisha miaka 35 kabla hajapewa utume aliitwa kutatua ugomvi wa jamii ya makuresh kugombea kuliweka jiwe hili baada ya ukarabati wa al kaaba yeye akaliweka jiwe hili na ugomvi ukaisha soma kitabu maisha ya nabii muhamad cha sheikh abdulla Saleh Fars uk 15-16 kifungu h.


     Pichani juu mahali lilipohifadhiwa jiwe jeusi katikati ya msikiti wa makka kama linavyoonekana leo baada ya kuboreshwa mahali hapa inaaminika ni kamsikiti kadogo ka kwanza kalikojengwa na nabii Ibrahimu na mwanae Ishimail kwa ajili ya kumuabudu Mungu wakitumia jiwe lililotumiwa na nabii Adamu  Picha kwa hisani ya maktaba ya Mwalimu wa somo Mchungaji Innocent Kamote

Ibada ya Kutufu.
    Ibada hii pia kwa asili ilikuwa ya wapagani ambao walikuwa wakitufu uchi wa mnyama kabisa kutufu ni ibada ya kuzunguka al-kaaba hufanywa na waislamu wanapokwenda hija kwa sasa waislam wameiboresha ibada hii kwa kuwa huvaa migolole miwili bila kuvaa chupi ndani kwani nguo zilizoshonwa ni najisi soma kitabu hija na maamrisho yake cha sheikh awam shaaban kaifta uk wa 27 mambo yanayo harimishwa point namba mbili. Ili kuthibitisha kuwa ibada hii ilifanyika uchi soma Maisha ya nabii Muhamad
uk 4 kifungu a mwishoni. Unapokwenda kwenye jiwe hili jeusi hajar al aswad unaligusa na kuliabudu na kulisujudu mara tatu na kusema allh akbar (yaani mungu mkubwa) huku ukiliashiria lile jiwe kwa mikono yote kisha unasema maneno yafuatayo “Allah humma imana bika watasdika bikita bika biadhika watiiba lisunnat nabiyyika salla ilaahu wassalim” yaani “Ewe mola kwa imani yangu juu yako na kwa kuthibitisha kitabu chako na kwa kutekeleza ahadi yako na kuufuata mwenendo wa nabii wako natekeleza sala hii” kumbuka sala hii huelekezwa kwenye jiwe lile jeusi upo?

Ibada ya hijja ifanywayo na wislamu.
       Ibada hii pia ina asili ya Kipagani,wapagani walikuwa wakifanya hija pale al kaaba kwa kuzunguka wakiwa uchi wa mnyama wanaume kwa wanawake wakiamini kuwa nguo ni kitu kinachopata uchafu yaani najisi na hivyo haistahili kuvaliwa ibadani soma kitabu maisha ya nabii muhamad uk 3-4 kifungu a. pia inaeleza jinsi mahujaji wa kipagani (majahili) walivyofanya ibada hizo na jinsi Makureshi kabila ya muhamad walivyokuwa wakifanya huduma mbalimbali kwa mahujaji.makuresh walikuwa na jamii 12 tano kati yao walifanya huduma hizo jamii hizo ni 
Ø  Siqaya-Kutengeneza maji ya wanaokuja kuhiji
Ø  Rifad-Kutengeneza chakula kwa wale wasiojiweza
Ø  Hijaba-Kushika funguo za al-kaaba
Ø  Liwaa-Kupigana vita na kusaidia kuongoza misafara
Ø  Nad-wa- Kuongoza vikao vya makureshi
Hivi leo waislamu wanapokwenda kuhiji huelekea palepale na hufanya yaleyale ambayo wapagani walikuwa wakiyafanya na quran imewaamuru wakahiji hapa (surat Imran 3;96-97).Mwenye masikio ya kusikia na asikie!

Mwezi wa mfungo wa Ramadhani.
      Funga ya ramadhani pia ilikuwa funga ya wapagani,iliadhimishwa hata kabla ya Muhamad na uislamu soma kitabu maisha ya nabii muhamad uk 16 kifungu cha 3 sura ya 4 “….Hata siku moja mwezi wa ramadhani 17 jumatatu mwaka wa 40 unusu wa umri wa Muhamad alienda pangoni…..”Hii ina maana funga ya ramadhani  ni ya wapagani na muhamad aliifunga kama mpagani kabla ya utume na ndiyo funga hii ambayo waislamu wameamuriwa kuifunga katika quran soma (Surat al Baqara 2:183) al baqara-ng’ombe jike, soma pia ufafanuzi katika al-Bukhar vol 16 no;-28…. “walikuwa wakifunga majahili kabla ya Muhamad pale makka” majahili ni majinga inashangaza ibada hizi za majinga ndio alla anawaamuru waislamu kuzifuata.!

Msikiti wa Mecca.


Msikiti wa Mecaa kama unavyoonekana katika pichani leo msikiti huu ni maarufu kama al-Haram uko Saud Arabia ndio mahali panaposadikiwa kuwa patakatifu zaidi katika misikiti ya waislamu al –kaaba  iko katikati ya msikiti huu, mji wa mecca ndio mji aliozaliwa Muhamad mwanzilishi wa Uislam na ndio mji ambao waislamu wanapaswa kufika kwaajili ya kuhiji japo mara moja katika maisha kama wana uwezo na ndipo mahali ambapo wakisali wanatakiwa kuelekea Kibla .

Huzuni ya kuuza Haki yako ya Uzaliwa wa Kwanza !



Msatari wa Msingi Genesis 25:29-34

Utangulizi:
1.      Esau ni moja ya watu muhimu katika Biblia lakini habari zake zinatupa masikitiko Makubwa
a.       Alikuwa Mzaliwa wa Kwanza wa Isaka na Rebeka na Pacha la Yakobo Mw 25:21-26
b.      Alipendwa na baba yake Isaka sana na alibarikiwa kuwa Mwindaji Hodari Mw 25:27-28
2.      Alikuwa ni Mtu mwema sana
a.       Alionyesha wema wake kwa ndugu yake aliyemdanganya Mw 33:1-16
b.      Alisaidia wakati wa Mazishi ya Baba yake Isaka Mw 35: 29
3.      Lakini Mara mbili bila Huruma alitendewa visivyo haki na Ndugu yake Yakobo
a.       Yakobo alimuuzia Esau ndugu yake haki ya uzaliwa wa kwanza alipokuwa na njaa kali Mw 25:29-34
b.      Mara ya pili wakati Isaka amekusudia kumbariki Esau Yakobo alijiingiza kwa hila Mw 27:1-41
Katika somo hili tutaangalia zaidi katika eneo la Kwanza ambalo kwalo linaweza kutufunza maswala kadhaa katika maisha.


I.                   Esau auza Haki ya mzaliwa wa kwanza.
Katika mila na desturi za Israel Uzaliwa wa kwanza kilikuwa ni cheo chenye faida kadhaa za kimwili na Kiroho, Neno la kiyunani kuhusu Mzaliwa wa kwanza ni Prototokos “Prototokos” Ambalo maana yake ni wa kwanza katika Cheo cheo hiki kilikuwa na maana pan asana! Na faida zifuatazo
a.      Faida za Kimwili
-          Kupata Urithi Maradufu kutoka katika urithi wa baba yako Mwanzo 36:6-7
-          Kuwa kiongozi wa Familia na mtunga sheria wa familia Mwa 27:29
b.      Faida za Kiroho
-          Kuwa mrithi wa ukuhani wa kifamilia baba yako anapofariki
-          Mrithi wa matamko yote ya Baraka juu ya ukoo wako
-          Kurithi Baraka zote ambazo Abraham alikuwa ametamkiwa Mw 28:4:12:1-3
-          Kupata haki ya kutamkiwa Neno la Baraka kubwa na mzazi wako anapokaribia kufa.
-          Hili ndilo Jambo kubwa ambalo kila mmoja katika Familia alikuwa analitamani. Kwa Esau na Yakobo.

II.                Mtazamo wa Esau na Yakobo:-
Mtazamo wa Esau
-          Esau alitazama haki ya uzaliwa wa kwanza kwa mtazamo wa mwilini kuliko wa Rohoni.
-          Alikuwa na mtazamo wa sasa kuliko wa baadaye, alizarau haki ya msingi kwaajili yam lo mmoja tu na kwa sababu hii aliitwa mtu asiyemcha Mungu Waebrania 12:16, haki ya Uzaliwa wa kwanza inakuunganisha na Mungu moja kwa moja.
-          Esau alipuuzia jambo hilo kwa kujumuisha kiapo wakati anakubali kumuuzia Yakobo.
-          Alipuuzia umuhimu wa Baraka za wakati ujao, aliweza kujali mlo mmoja tu ambao ungeondoa njaa ya siku moja na kusahau kuwa kesho angehitaji tena hivyo anafananishwa na Muasherati, waashetari hutamani kuitimiza shuku ya mwili kwa wakati huo tu bila kujua madhara na matokeo ya matendo yao na kusahau kuwa kesho watahitaji tena tendo la jinsi ileile.
-          Alifananishwa na mtu aliyetaka kupata raha ya muda na nafuu ya muda tu, akasahau kuwa anajitia katika tatizo kubwa litakalogharimu maisha yake, Viongozi wengi sana wa bara la Afrika wana mitazamo kama ya Esau wanaingia mikataba ya kushangaza wakifikiri watatatua matatizo ya wananchi wao, baadaye wanakuja kugundua kuwa wamejiingiza pabaya na kuwa mikataba hiyo itagharimu maisha ya waafrika wengi, si vema kuingia katika mikataba ya aina yoyote eti kwa sababu una njaa tu, wengi wameoa au kuolewa kwa mitazamo ya kuona karibu, anafikiri kuwa kwa maisha ya ndoa atafurahia ulimwengu, atakuwa ameuchinja lakini wengi sasa wanajuta kwa kufanya maamuzi yanayogharimu maisha yao na umilele wao, huolewi tu kwa sababu wengine wanaolewa wala huoi tu kwa sababu wengine wanaoa, ni lazima ufikiri kwa kina na kumuhusidha Mungu kwa vile maamuzi hayo yatagharimu maisha yako.
-          Wengi tunaingia katika chuki na wivu na kuwapiga vita wengine kwa sababu tunaangalia vichache walivyo navyo na tunasahau kuwa Mungu amekusudia kuimbariki kila mmoja wetu. Katika kristo sote ni wazaliwa wa kwanza, tunazo ahadi na Baraka za Mungu tusijaribiwe kwa kuanza kupiga vita wengine.
III.             Somo kuu la Kujifunza kwetu
-          Sisi nasi ni warithi wa ahadi zilezile pamoja na Ibrahimu kwa njia ya Imani Galatia 3:29
-          Tuwarithi pia pamoja na Kristo Warumi 8:16-17
-          Tu warithi wa tumaini lile la milele Tito 3:7
-          Tu warithi wa ufalme ule tulioahidiwa Yakobo 2:5 na 2Petro 1:11
-          Katika Kristo vitu vyote ni vyetu 1Koritho 3:21-23 na Ufunuo 21:7
-          Tuna urithi usioharibika mbinguni uliotunzwa kwaajili yetu 1Petro 1:4, Marko 10:28-30.
Tahadhari:-
-          Sisis nasi tunaweza kuuza Urithi wetu wa Mzaliwa wa Kwanza kwa kufuata anasa na raha ya dhambi za dunia hii Waebrania 11:24-26
-          Kwa tamaa ya maswala ya dunia hii bila kumtanguliza Mungu 1Yohana 2:14, Yakobo 4:4
-          Kwa kuufuata Mwili na kukataa kuongozwa na Roho wa Mungu Wagalatia 5:16-26
-          Ni lazima tuhakikishe tunashika nafasi yetu ya uzaliwa wa kwanza kwa gharama yoyote
Tunawezaje kupoteza haki zetu za Uzaliwa wa Kwanza?
1.      Imarisha uhusiano wako na Mungu na tafuta kuwa na amani na watu wote Waebrania 12:14
2.      Usikubali kuipungukia Neema ya Mungu Waebrania 12:15
3.      Ishi maisha ya utawa na kumtegemea Mungu wakati wote 1 Koritho  9:24-27; 1 Tito 4:7-8.
Kumbuka !
-          Esau hakuangalia mbali aluidharau Baraka za Mungu zilizokusudiwa kwake
-          Alisikiliza tamaa za mwili na kutekeleza maswala ya Muda mfupi
-          Sisi nasi tunaweza kumpuuzia Kristo, tunaweza kufanya makosa yaleyale
-          Mungu atusaidie tusije tukajisahau na ikawa ngumu kwetu kupata tena neema ile hata tujapolia kwa machozi Waebrania 12:17.


Tuitimishe ujumbe huu kwa kuimba Tenzi hii Mungu amenihurumia
Wimbo: Mungu amenihurumia
1. Mungu ametuhurumia, tendo hili kubwa sana,
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake
2. Nalistahili kupotea, lakini nahurumiwa,
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.
3. Mungu mwenye huruma nyingi, usininyime huruma,
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!