Ni
muhimu kufahamu kuwa yako mambo yaliyokuwepo kabla ya uislamu na ambayo
waislamu huyaamini na kuyaabudu hata sasa umuhimu wa kuyajua haya ni kupata
uthibitisho ulio dhahiri kuwa uislamu ni upagani ulioboreshwa tu na kuwa
Muhamad hakuleta jambo jipya
Mungu
anayeabudiwa na waislamu aitwae allah.
Mungu huyu
anayeitwa allah kwa asili sio Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo aliyewatoa
Israel huko Misri kwa mkono wa nguvu na kujitambulisha kwa Musa kwa jina la Yehova katika (Kutoka 6;2-3)Kinyume na huyu allah
alikuwa ni mungu wa wapagani ambae awali alikuwa na mabinti zake watatu au wakeze watatu ambao
waliitwa al- lat (mungu jua),al-manat (mungu sayari venus au nyota)
na al-uza (mwenye nguvu)Mkuu wao
aliitwa Hubal ambae baadae alikuja kujulikana kama allah na ndiye aliyekuwa
mungu wa mji wa makka (Surat an
najim-nyota 53;19-20)Mungu huyu
ndiye anayeabudiwa na waislamu leo na jitu lililomtokea Muhamad lilimuamuru
kumuabudu mola huyu wa nji wa makka soma(surat
Naml-sisimizi 27;91) miungu hii ilikuwa maarufu pale makka wakati Muhamad
anazaliwa (Najm 53;21-23)na huyu
allah alikuwa mungu mwezi,inaaminika na baadhi ya wasomi kuwa jina allah au
al-llah linatokana na jina Ilah ambae alikuwa mungu mwezi wa Arabia ya kusini
ambao waliamini mungu mmoja bila kudharau mingine hivyo kwa asili waislamu
wanaabudu mwezi na nyota hata Muhamad mwenyewe alipotaka kuapa aliapa kwa Nyota
soma (Najm 53;1) miungu mingine iliyokuwepo ni pamoja na wadd (pia mungu mwezi) suw’a,yaguth na nasr
soma (surat Nuhu 71;23)
Jiwe jeusi
katikati ya msikiti wa makka “Hajar al aswad”.
Jiwe hili
jeusi hajar al aswad ni nyota au kimondo kilichoanguka zamani sana,Jiwe hili
ndilo lilikuwa al kaaba ya wapagani, Ambao waliliabudu na kulisujudia soma kitabu maisha ya nabii Muhamad ukurasa wa 15-16 kifungu h. mahali hapa
muhamad alipozaliwa tu alifanyiwa duwa na babu yake soma kitabu hicho uk wa 5
kifungu cha mwisho.Hapa ndipo wanapoabudu waislamu woote duniani huelekea hapo
wakati wa sala na huenda hapo kufanya hija na hulisujudia jiwe hili na
kuliabudu kama unabisha soma kitabu vipi
uhiji uk 29 cha shehk A.Suleman.Lazima ulisogelee jiwe hilo uweke mkono na
kulibusu na kulisujudia mara tatu.Muhamad alipofikisha miaka 35 kabla hajapewa
utume aliitwa kutatua ugomvi wa jamii ya makuresh kugombea kuliweka jiwe hili
baada ya ukarabati wa al kaaba yeye akaliweka jiwe hili na ugomvi ukaisha soma
kitabu maisha ya nabii muhamad cha sheikh abdulla Saleh Fars uk 15-16 kifungu
h.
Pichani juu mahali lilipohifadhiwa jiwe
jeusi katikati ya msikiti wa makka kama linavyoonekana leo baada ya kuboreshwa
mahali hapa inaaminika ni kamsikiti kadogo ka kwanza kalikojengwa na nabii
Ibrahimu na mwanae Ishimail kwa ajili ya kumuabudu Mungu wakitumia jiwe
lililotumiwa na nabii Adamu Picha kwa
hisani ya maktaba ya Mwalimu wa somo Mchungaji Innocent Kamote
Ibada ya
Kutufu.
Ibada hii pia
kwa asili ilikuwa ya wapagani ambao walikuwa wakitufu uchi wa mnyama kabisa
kutufu ni ibada ya kuzunguka al-kaaba hufanywa na waislamu wanapokwenda hija
kwa sasa waislam wameiboresha ibada hii kwa kuwa huvaa migolole miwili bila
kuvaa chupi ndani kwani nguo zilizoshonwa ni najisi soma kitabu hija na
maamrisho yake cha sheikh awam shaaban kaifta uk wa 27 mambo yanayo harimishwa
point namba mbili. Ili kuthibitisha kuwa ibada hii ilifanyika uchi soma Maisha
ya nabii Muhamad
uk 4 kifungu a mwishoni. Unapokwenda kwenye jiwe hili
jeusi hajar al aswad unaligusa na kuliabudu na kulisujudu mara tatu na kusema
allh akbar (yaani mungu mkubwa) huku ukiliashiria lile jiwe kwa mikono yote
kisha unasema maneno yafuatayo “Allah
humma imana bika watasdika bikita bika biadhika watiiba lisunnat nabiyyika
salla ilaahu wassalim” yaani “Ewe mola kwa imani yangu juu yako na kwa
kuthibitisha kitabu chako na kwa kutekeleza ahadi yako na kuufuata mwenendo wa
nabii wako natekeleza sala hii” kumbuka sala hii huelekezwa kwenye jiwe lile
jeusi upo?
Ibada ya
hijja ifanywayo na wislamu.
Ibada hii
pia ina asili ya Kipagani,wapagani walikuwa wakifanya hija pale al kaaba kwa
kuzunguka wakiwa uchi wa mnyama wanaume kwa wanawake wakiamini kuwa nguo ni
kitu kinachopata uchafu yaani najisi na hivyo haistahili kuvaliwa ibadani soma
kitabu maisha ya nabii muhamad uk 3-4 kifungu a. pia inaeleza jinsi mahujaji wa
kipagani (majahili) walivyofanya ibada hizo na jinsi Makureshi kabila ya
muhamad walivyokuwa wakifanya huduma mbalimbali kwa mahujaji.makuresh walikuwa
na jamii 12 tano kati yao walifanya huduma hizo jamii hizo ni
Ø
Siqaya-Kutengeneza maji ya
wanaokuja kuhiji
Ø
Rifad-Kutengeneza chakula kwa
wale wasiojiweza
Ø
Hijaba-Kushika funguo za al-kaaba
Ø
Liwaa-Kupigana vita na kusaidia
kuongoza misafara
Ø
Nad-wa- Kuongoza vikao vya
makureshi
Hivi leo waislamu wanapokwenda kuhiji huelekea palepale
na hufanya yaleyale ambayo wapagani walikuwa wakiyafanya na quran imewaamuru
wakahiji hapa (surat Imran 3;96-97).Mwenye
masikio ya kusikia na asikie!
Mwezi wa
mfungo wa Ramadhani.
Funga ya
ramadhani pia ilikuwa funga ya wapagani,iliadhimishwa hata kabla ya Muhamad na
uislamu soma kitabu maisha ya nabii muhamad uk 16 kifungu cha 3 sura ya 4
“….Hata siku moja mwezi wa ramadhani 17 jumatatu mwaka wa 40 unusu wa umri wa
Muhamad alienda pangoni…..”Hii ina maana funga ya ramadhani ni ya wapagani na muhamad aliifunga kama
mpagani kabla ya utume na ndiyo funga hii ambayo waislamu wameamuriwa kuifunga
katika quran soma (Surat al Baqara 2:183)
al baqara-ng’ombe jike, soma pia ufafanuzi katika al-Bukhar vol 16 no;-28….
“walikuwa wakifunga majahili kabla ya Muhamad pale makka” majahili ni majinga
inashangaza ibada hizi za majinga ndio alla anawaamuru waislamu kuzifuata.!
Msikiti wa
Mecca.
Msikiti wa Mecaa kama
unavyoonekana katika pichani leo msikiti huu ni maarufu kama al-Haram uko Saud
Arabia ndio mahali panaposadikiwa kuwa patakatifu zaidi katika misikiti ya
waislamu al –kaaba iko katikati ya
msikiti huu, mji wa mecca ndio mji aliozaliwa Muhamad mwanzilishi wa Uislam na
ndio mji ambao waislamu wanapaswa kufika kwaajili ya kuhiji japo mara moja
katika maisha kama wana uwezo na ndipo mahali ambapo wakisali wanatakiwa
kuelekea Kibla .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni