Kama woote
tunavyofahamu kuwa Duniani ziko dini nyingi sana na zote zina vitabu vyake
vitakatifu vinavyodaiwa kuwa ni neno la Mungu na kuwa ndio mamlaka ya mwisho ya
dini hizo wahindu wana kitabu chao kiitwacho (Vedas),na sikhiism(Adigranth),Confusian(Analets),Shinto (Nihong),Na Budha (Dharma),Judaism(Torati),Islam(quran) na sisi wakristo Biblia
agano jipya na Kale,na Kila mmoja anaamini kuwa ni neno la Mungu katika eneo
hili tutakuwa tukijiuliza swali je Quran ni neno lu Mungu na tutafanya upembuzi
yakinifu kwa kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-
·
Jinsi quran ilivyopatikana
na muundo wake
·
Jinsi quran inavyopotosha kweli za kibiblia
·
Jinsi quran inavyomuelezea
Yesu masihi
·
Jinsi quran
inavyojikanganya yenyewe
Jinsi
quran ilivyopatikana na muundo wake.
Kabla ya kuchambua jinsi quran ilivyopatikana ni muhimu
kujikumbusha kwamba quran ni nini? Quran ndio kitabu kitakatifu na mamlaka ya
mwisho kwa waislamu,qurani ni neno la kiarabu cha kikuresh lanye maana ya “recitation” yaani yaliyo
kaririwa,quran ilitokana na aya alizokuwa akizitoa Muhamad kwa madai kuwa
zilitoka kwa Allah kupitia malaika Jibril,tangu alipomkaba na kumuamuru
kuikariri kwa Kumwambia “Iqraa-bism-rabik”
yaani soma na ukariri,Muhamad aliendelea aliendelea kutoa aya hizo kwa miaka
23, Waislamu huamini kuwa aya hizo zilitolewa kipandekipande toka katika kitabu
halisi kilichoko mbinaguni,Muhamadi alitoa aya hizo kwa kuzisema kwa Maswahaba
wake ambao walizikariri kichwani (Hawakuwa wanajua kusoma wala kuandika) baada
ya kifo chake Muhamad aya hizo zilikusanywa toka kwa maswahaba mbalimbali na
kuwa kitabu kimoja kiitwacho quran leo,Maswala mengine kuhusu Muhamad na maisha
yake yamekusanywa katika vitabu vya hadithi ambavyo pia hutumika katika
kutafasiri quran
Muhamad
alipokea aya hizo za Quran kwa namna zifuatazo (aya au wahyi)
Kwa mujibu
wa vyanzo vya kiislamu Muhamad alipokuwa anapokea aya hizo alikuwa anavamiwa na
nguvu za kigeni zilizomuathiri sana na kumpa shida sana kama inavyokua kwa
mgonjwa wa kifafa, aliunguruma kama mtoto wa ngamia huku akitoa povu
mdomoni,Alitisha na kutia huruma hali hizi zilikuwa zikimpata kila alipokuwa
anataka kutoa aya hizo,wanasema wakati mwingine alikuwa anaanza kusikia mlio
kama kundikubwa la nyuki likimjia vinaeleza vyazo hivyo vya kiislamu! Jambo
lililopelekea watu waliomuona kumpa majina yafuatayo
Ø
Walimuita
aliyepagawa au mwendawazimu (Surat
as-saafat 37:35-36,dukhan
44:13-14,at-tur 52:29,qalam 68:1-2,Takwyr 81:22).
Ø Walimuita mchawi (Yunus 10;2,surat
sad 38;4,az-Zumar 39:41)
Ø
Wengine
walifikiri amerogwa (Ban Israel
17:47-48,fur-qan 25:4-5,8)
Ø Aliitwa pia mpiga ramli au mtunga Mashairi (Tur 52;29, haqqah 39;41)
Muhamad
alidai pia kuletewa aya hizo na malaika Jibril ambae kwa mujibu wa quran ndie
malaika mkuu, wakati mwingine alidai kusikia sauti ikimpa aya, na wakati
mwingine alitoa aya hizo moyoni mwake au alioteshwa ndoto au kupewa ufunuo (Surat nasm 53:1-11)
Muhamad
alihubiri quran na mafundisho yake na kupata matokeo hafifu sana hali hii
ilimkatisha tama hususani pale makka ambapo watu walimpinga sana akiwemo baba
yake mdogo Abu Lahib na hivyo
alimlaani na kumtaja kama mtu wa motoni kwa muongozo wa Allah soma kitabu
maisha ya nabii Muhamad uk 19 kifungu cha mwisho n auk 20 kifungu cha kwanza na
cha pili.Baada ya upinzani mkali Muhamad ili apatane na watu wa makka alibadilisha aya na kuleta aya inayoitambua miungu ya ndugu
zake aya hiyo husomeka hivi “…….Je mumewaona lat.uzza na manta? Hawa watatu
maombi yao (wanayo waombea) ni ya kutumainiwa (Surat sad 38;5-7).Miungu
hiyo ni ile iliyoabudiwa na wapagani wa pale Makka na kufanyiwa
hijja,alipoulizwa kuhusu kigeugeu chake cha kubadilisha aya mara kwa mara alidai kuwa Zilitoka kwa
shetani hivyo jibrili aliiondoa sehemu ya pili ya aya hiyo hivyo sasa inasomeka
hivi(Surat nasm 53:19-20) Hivyo
ndani ya quran ziko aya nyingi sana zinazopingana na nyingine zimebadilishwa na
watu kama tutakavyoona mbeleni.
Mungu wa
Muhamad mwenyewe alikuwa na kigeugeu kwa kumletea aya na kuzibadili baadae
mfano (al-baqara 2;106,an- nahil 16;101)
hivyo Muhamad alibadili aya za quran katika maeneo mengi na kubadili
nyingine,aya zilizoondolewa ziliitwa “Mansukh” na zile zilizokuja kubadili
nyingine ziliitwa “Nasikh” Hizi ni
aya zilizo karabatiwa “the law of abrogation” bahati mbaya aya zoote hizi
zimo katika quran na zilizobadilishwa zinakadiriwa kufikia kati ya “5-500” kwa
mujibu wa mwanazuoni wa kiislamu Jalalud-din baadhi ya aya hizi ni pamoja na
Ø
……Asilazimishwe
mtu kuingia dini (Baqara 2;256)ilibatilishwa
kwa (Surat as saf 61:10-12)
Ø
…....Muelekeo
wa wakati wa kusali (Baqara 2:142)
ilibatilishwa kwa(Baqara 2;147)
Ø
……Amri
ya kuomba usiku (al Muzzamil 73;2)
ilibatilishwa kwa (al Muzzamil 73:20)
Ø
…..Adhabu
ya wazinzi (an Nisaa 4;15-16)
ilibatilishwa kwa (an-Nur 24:2)
Hizi ni baadhi tu ya aya zinazo jikanganya zenyewe Muda
usingeweza kutosha kuandika na nyingine zinazopingana zenyewe kwa zenyewe.
Muundo wa quran.
Qurani imeundwa na baadhi ya mila na tamaduni
mbalimbali za kiarabu na mchanganyiko wa dini mbalimbali,na mambo mengine
yametoka katika vitabu vya tamaduni za kiyahudi za kiyahudi kama Talmud na Mishna,pia kuna tamaduni za kiajemi hii ni kwa sababu Muhamad
alikuwa na rafiki wa kiajemi aliyeitwa Salman,pia kuna vihistoria toka kwenye
Biblia ingawa vimepinda huenda ni kwa sababu ya Makosa ya kukariri au kwa sbabu
ya kutokujua kusoma kwa Muhamad na maswahaba wake au kazi ya shetani kupotosha
ukweli,aidha kuna tamaduni nyingi za kipagani hasa za pale arabuni makka na
mawazo ya Muhamad mwenyewe.
Jinsi quran inavyopotosha kweli za
kibiblia .
Quran ni kitabu kilichojaa hadithi za
kudandiadandia toka kwenye biblia na
ambazo nyingi haziko sahihi na zinapingana
na kupotosha kweli zilizomo katika biblia,Hadithi nyingi katika qurani
ni tofauti na zile zilizomo katika biblia, Biblia ina masimulizi
yanayojitosheleza yenye mwanzo mpaka mwisho,ni rahisi kujua kipi ni kipi na
kipi utakipata wapi,lakini sivyo ilivyo katika quran hadithi zake ni za
kudandiadandia hiki au kile wakati mwingine bila kujua mwanzo wala mwisho au
kupata habari kamili labda ndio maana Muhamad alirejea mara kwa mara kuwataka
waislamu kutuuliza sisi tuliopewa vitabu kabla yao hapa chini Tutachambua mambo
ambayo qurani imepotosha au kudanganya tofauti na biblia;-
Ø Q. Nuhu
alikuwa na mtoto mmoja aliyekufa kwa gharika(hud 11;40-45).
Ø B. Nuhu
alipata neema machoni pa bwana yeye na uzao wake yaani watoto wake woote watatu
(Mwanzo sura ya 6-7).
Ø
Q. Baba wa Ibrahimu ni azar (al anam 6:74)
Ø B. Baba wa Ibrahimu ni Tera (Mwanzo11;31)
Ø
Q. Musa aliokotwa na mke wa
Farao (ak qasas 28;9).
Ø
B. Musa aliokotwa na binti wa Farao (kutoka 2;5-10).
Ø
Q. Farao alimwambia Haman
ajenge mnara wa Babel (al qasas28:38)
Ø
B. Mnara wa Babel ulijengwa
na Nimrod (Mwanzo 10:32,11:4) pia
habari hizi Quran imezungumza uongo kwani kuna tofauti Farao aliishi miaka 800
baada ya Mnara wa babel na Haman aliishi miaka 900 baada ya Farao hivyo kuna
tofauti ya miaka 1700 tangu mnara wa babel na kuishi kwa Haman.
Ø
Q. Inafundisha kuwa mariam
mamayake Yesu ni dada wa Haruni mtoto wa Imran (surat Maryam 19;17-28).
Ø
B. Huu ni uongo,Je hii ina
maana Musa ni mjomba wa Yesu masihi kama Mariam ni dada wa Haruni kakaye na
Musa? Naona hapa Muhamad na Allah wali Comfuse yaani walichanganya mada, Habari
za Mariam mama wa Yesu na habari za Mariam (Miriam) dada wa Haruni na Musa zina
tofauti ya miaka kama 1400 hivi k.k.
Ø
Q. Yesu alizaliwa chini ya
mtende (Maryam 19:23)
Ø
B. Yesu alizaliwa katika
hori ya Ngo’mbe (Luka 2;8-18)
Ø
Q. Zekaria alikuwa bubu siku
tatu (Maryam 19:10-11).
Ø
B. Zekaria alikuwa bubu mpaka alipozaliwa mtoto
(Luka 1;8-22,57-64).
Ø Q. Roho
mtakatifu ni malaika Jibril (al baqara
2;87).
Ø B. Roho mtakatifu ni Mungu ni tofauti na malaika
(Luka 1:26-35, Matendo 5:3-4).
Ø Q. Ishmael ndiye aliyetolewa sadaka na Ibrahimu
( as saafat 37:99-111)
Ø B. Isaka ndiye aliyetolewa sadaka na Ibrahimu (mwanzo 22:1-19).
Q……Inawakilisha Quran.
B……Inawakilisha Biblia.
Yako mambo mengi sana ambayo quran
inapingana na biblia ambalo ndio neno la Mungu,ndio maana tunaona kuna dosari
nyingi katika quran zinazotuthibitishia kuwa si kitabu cha kuaminika sana kwani
kilikuja baadae sana kuliko Biblia ambayo ni ya zamani zaidi lakini imetunza
kweli kwa usahihi
Jinsi quran
inavyo Muelezea Yesu kristo.-
Qurani na
waislamu huwa wanapinga kuwa Yesu si Mungu huku quran yenyewe inamuelezea
Kristo katika viwango vya juu na vya kipekee kuliko vya nabii yeyote na vya
kipekee kuliko hata Muhamad, namna quran inavyomuelezea Kristo inamaanisha wazi
kabisa kuwa Yesu ni Bwana.
- Yesu alikuwa ni Muujiza kwa ulimwengu (al-Nabbiya 21;91)
- Alizaliwa na Bikira (surat Maryam 19;20-21) kukubali hilo ni sawa na Kukubali kuwa biblia inasema kweli (luka 1;28-35,Isaya 7;14,9:6).
- Alifanywa Ishara (muujiza waziwazi) surat az-zukhuf 43:63) hii ni sawa na kusema alifanywa ishara ili watu wamuamini yeye (Yohana 20;30-31,5;36)
- Alikuwa mtakatifu hakuwa na dhambi (Maryam 19;21,21;19) sifa ya utakatifu ni ya Mungu peke yake.
- Ni ishara kwa wanadamu woote(surat Maryam 19;21 al anbiyaa 21;19)Hivyo Yesu ni muujiza kwa watu woote ili wapate kumuamini ( Yohana 6;25-35)
- Qurani inamkiri Yesu kuwa ni Masihi (Surat an Nisaa 4;171-172),mtu yeyote anaekubali kuwa Yesu ni masihi maana yake amekubali kuwa Yesu ndie ufunuo wa mwisho kabisa wa mambo yote na kuwa ndie ambae watu walikuwa wakimgojea (Yohana 4;15-26).
- Amejazwa roho mtakatifu (al Baqara 2;87) kwa kawaida waislamu hudai kuwa roho ni jibril (Luka 1;28-35)Roho ni tofauti na jibril lazima waislamu wajue kuwa Roho mtakatifu ni Mungu.(Mdo 5;3-7)
- Alipaa Mbingini (surat an Nisaa 4;158)
- Alilisha watu mikate (al Maida 5;112-115) kukubali Ishara hii ni kukubali kuwa Yesu ni nabii yule ajae ulimwenguni aliye tabiriwa na Musa (Yohana 6;1-14)
- Ni alama ya kiama (Ishara) (al Zukhuf 43;61) maana yake mpaka yeye aje ndipo mwisho utakapokuja,yeye ndiye atakayehukumu na ndiye atakayefufua wafu soma ufafanuzi wa ayahii,atawafufua wafu akiwamo Muhamad( Yohana 5;22-23) soma pia injili ya barnaba uk 11.
Quran na aya za shetani.
Kama
tulivyoona hapo juu kuhusu kuweko kwa kigeugeu kati ya mungu wa muhamad ambaye alimletea aya na kasha kuzibadili baadaye Al-Baqara 2; 106 na an nahil 16;101 hivyo
Muhamad alibadili aya Mansukh na kuleta
aya nyingine Nasikh ambazo nyingi zilikuwa zinagusa mahitaji yake kama kuoa
wanawake aliojitakia hata wakiwamo wake za watu, kuna wakati ambapo Muhamad
mwenyewe aliulizwa kuhusu kigeugeu alicho nacho na alidai kuwa shetani alikuwa
amemdanganya na kumletea aya
zisizostahili Mwandishi maarufu wa Novel wa kiingerezamwenye asili ya kihindi
bwana Salman Rushdie aliweza kukosoa
kiasi kikubwa cha aya hizo katika novel; yake iliyopewa jina la Aya za
shetani (The Satanic Verses)
Pichani Bwana Salman Rushdie Mwandishi
maarufu wa Novel nchini uingereza ambaye alilazimika kukaa mafichoni baada ya
kuandika kitabu chake kiitwacho Aya za shetani mwaka 1988 Jambo lililopelekea
Ayatollah Khomein Kiongozi wa kidini wa Iran kuagiza kuwa bwana huyu auwawe,
wengi wa waislamu walifikiri kuwa kitabu chake kinaushambulia uislamu.
Ukweli kuhusu kitabu hiki unaweza kubaki
palepale nasema unaweza kubaki palepale hasa unapoangalia mfumo mzima wa Quran
na uislamu na tamaduni zake na maisha ya nabii Muhamad kwa ujumla utaweza kuona
zinaa ikihalalishwa kwa visingizio vya kuletewa aya, uchawi, uhusiano na majini,
msisitizo wa ugaidi, mfumo wa kukubali kuua au kuuawa kwaajili ya mwenyezi
Mungu hata ingawa anatajwa kuwa mwingi wa rehema lakini mfumo mzima wa kiislamu
hauonyeshi kivitendo kama kweli Mungu ni wa Rehema na badala yake sisi tunaona utendaji mkubwa wa
shetani ukitenda kazi kwani Kristo alisema kazi ya ibilisi ni kuvunja, kuiba,
kuchinja na kuua Yohana 10;10 “Mwivi haji ila aibena kuchinja na kuharibu mimi
nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele”Kazi ya Yesu Kristo na agizo
lake katika injili ni kuleta uzima na sio kuua kama yalivyo maagizo katika
Quran.
Kama wewe ni Muislama ukishaifahamu kweli hii Okoka haraka acha kupoteza Muda!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni