Msatari wa
Msingi Genesis 25:29-34
Utangulizi:
1. Esau ni moja ya watu muhimu katika Biblia lakini habari zake zinatupa
masikitiko Makubwa
a. Alikuwa Mzaliwa wa Kwanza wa Isaka na Rebeka na Pacha la Yakobo Mw
25:21-26
b. Alipendwa na baba yake Isaka sana na alibarikiwa kuwa Mwindaji Hodari Mw
25:27-28
2. Alikuwa ni Mtu mwema sana
a. Alionyesha wema wake kwa ndugu yake aliyemdanganya Mw 33:1-16
b. Alisaidia wakati wa Mazishi ya Baba yake Isaka Mw 35: 29
3. Lakini Mara mbili bila Huruma alitendewa visivyo haki na Ndugu yake
Yakobo
a. Yakobo alimuuzia Esau ndugu yake haki ya uzaliwa wa kwanza alipokuwa na
njaa kali Mw 25:29-34
b. Mara ya pili wakati Isaka amekusudia kumbariki Esau Yakobo alijiingiza
kwa hila Mw 27:1-41
Katika somo hili tutaangalia zaidi katika eneo la Kwanza ambalo kwalo
linaweza kutufunza maswala kadhaa katika maisha.
I.
Esau auza Haki ya mzaliwa wa kwanza.
Katika mila na desturi za Israel Uzaliwa wa kwanza
kilikuwa ni cheo chenye faida kadhaa za kimwili na Kiroho, Neno la kiyunani
kuhusu Mzaliwa wa kwanza ni Prototokos “Prototokos” Ambalo maana yake ni wa kwanza katika Cheo cheo hiki kilikuwa na maana pan
asana! Na faida zifuatazo
a.
Faida za Kimwili
-
Kupata Urithi Maradufu kutoka katika urithi wa baba
yako Mwanzo 36:6-7
-
Kuwa kiongozi wa Familia na mtunga sheria wa familia
Mwa 27:29
b.
Faida za Kiroho
-
Kuwa mrithi wa ukuhani wa kifamilia baba yako
anapofariki
-
Mrithi wa matamko yote ya Baraka juu ya ukoo wako
-
Kurithi Baraka zote ambazo Abraham alikuwa
ametamkiwa Mw 28:4:12:1-3
-
Kupata haki ya kutamkiwa Neno la Baraka kubwa na
mzazi wako anapokaribia kufa.
-
Hili ndilo Jambo kubwa ambalo kila mmoja katika
Familia alikuwa analitamani. Kwa Esau na Yakobo.
II.
Mtazamo wa Esau na Yakobo:-
Mtazamo wa Esau
-
Esau alitazama haki ya uzaliwa wa kwanza kwa mtazamo
wa mwilini kuliko wa Rohoni.
-
Alikuwa na mtazamo wa sasa kuliko wa baadaye,
alizarau haki ya msingi kwaajili yam lo mmoja tu na kwa sababu hii aliitwa mtu
asiyemcha Mungu Waebrania 12:16, haki ya Uzaliwa wa kwanza
inakuunganisha na Mungu moja kwa moja.
-
Esau alipuuzia jambo hilo kwa kujumuisha kiapo
wakati anakubali kumuuzia Yakobo.
-
Alipuuzia umuhimu wa Baraka za wakati ujao, aliweza
kujali mlo mmoja tu ambao ungeondoa njaa ya siku moja na kusahau kuwa kesho
angehitaji tena hivyo anafananishwa na Muasherati, waashetari hutamani
kuitimiza shuku ya mwili kwa wakati huo tu bila kujua madhara na matokeo ya
matendo yao na kusahau kuwa kesho watahitaji tena tendo la jinsi ileile.
-
Alifananishwa na mtu aliyetaka kupata raha ya muda
na nafuu ya muda tu, akasahau kuwa anajitia katika tatizo kubwa litakalogharimu
maisha yake, Viongozi wengi sana wa bara la Afrika wana mitazamo kama ya Esau
wanaingia mikataba ya kushangaza wakifikiri watatatua matatizo ya wananchi wao,
baadaye wanakuja kugundua kuwa wamejiingiza pabaya na kuwa mikataba hiyo
itagharimu maisha ya waafrika wengi, si vema kuingia katika mikataba ya aina
yoyote eti kwa sababu una njaa tu, wengi wameoa au kuolewa kwa mitazamo ya
kuona karibu, anafikiri kuwa kwa maisha ya ndoa atafurahia ulimwengu, atakuwa
ameuchinja lakini wengi sasa wanajuta kwa kufanya maamuzi yanayogharimu maisha
yao na umilele wao, huolewi tu kwa sababu wengine wanaolewa wala huoi tu kwa
sababu wengine wanaoa, ni lazima ufikiri kwa kina na kumuhusidha Mungu kwa vile
maamuzi hayo yatagharimu maisha yako.
-
Wengi tunaingia katika chuki na wivu na kuwapiga
vita wengine kwa sababu tunaangalia vichache walivyo navyo na tunasahau kuwa
Mungu amekusudia kuimbariki kila mmoja wetu. Katika kristo sote ni wazaliwa wa
kwanza, tunazo ahadi na Baraka za Mungu tusijaribiwe kwa kuanza kupiga vita
wengine.
III.
Somo kuu la Kujifunza kwetu
-
Sisi nasi ni warithi wa ahadi zilezile pamoja na
Ibrahimu kwa njia ya Imani Galatia 3:29
-
Tuwarithi pia pamoja na Kristo Warumi 8:16-17
-
Tu warithi wa tumaini lile la milele Tito 3:7
-
Tu warithi wa ufalme ule tulioahidiwa Yakobo 2:5
na 2Petro 1:11
-
Katika Kristo vitu vyote ni vyetu 1Koritho
3:21-23 na Ufunuo 21:7
-
Tuna urithi usioharibika mbinguni uliotunzwa
kwaajili yetu 1Petro 1:4, Marko 10:28-30.
Tahadhari:-
-
Sisis nasi tunaweza kuuza Urithi wetu wa Mzaliwa wa
Kwanza kwa kufuata anasa na raha ya dhambi za dunia hii Waebrania 11:24-26
-
Kwa tamaa ya maswala ya dunia hii bila kumtanguliza
Mungu 1Yohana 2:14, Yakobo 4:4
-
Kwa kuufuata Mwili na kukataa kuongozwa na Roho wa
Mungu Wagalatia 5:16-26
-
Ni lazima tuhakikishe tunashika nafasi yetu ya
uzaliwa wa kwanza kwa gharama yoyote
Tunawezaje
kupoteza haki zetu za Uzaliwa wa Kwanza?
1. Imarisha uhusiano wako na Mungu na tafuta kuwa na amani na watu wote Waebrania
12:14
2. Usikubali kuipungukia Neema ya Mungu Waebrania 12:15
3. Ishi maisha ya utawa na kumtegemea Mungu wakati wote 1 Koritho 9:24-27; 1 Tito 4:7-8.
Kumbuka !
-
Esau hakuangalia mbali aluidharau Baraka za Mungu
zilizokusudiwa kwake
-
Alisikiliza tamaa za mwili na kutekeleza maswala ya
Muda mfupi
-
Sisi nasi tunaweza kumpuuzia Kristo, tunaweza
kufanya makosa yaleyale
-
Mungu atusaidie tusije tukajisahau na ikawa ngumu
kwetu kupata tena neema ile hata tujapolia kwa machozi Waebrania 12:17.
Tuitimishe ujumbe huu kwa kuimba Tenzi hii Mungu
amenihurumia
Wimbo:
Mungu amenihurumia
1. Mungu ametuhurumia, tendo hili
kubwa sana,
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake
2. Nalistahili kupotea, lakini
nahurumiwa,
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.
3. Mungu mwenye huruma nyingi,
usininyime huruma,
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni