“If today you will be a servant to these People, they will always be your servants”
Lengo: kufanya maamuzi yenye Busara.
Andiko: 1Wafalme 12:1-15 “1.
Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekwenda Shekemu, ili
kumfanya mfalme. 2. Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati alipopata habari (maana
alikuwa akaliko Misri, huko alikokimbilia awe mbali na mfalme Sulemani;
Yeroboamu akakaa huko Misri, 3. wakapeleka watu kwenda kumwita); basi Yeroboamu
na jamii yote ya Israeli wakaenda, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 4. Baba
yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito
tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi
tutakutumikia. 5. Akawaambia, Enendeni zenu hata siku ya tatu, kisha mnirudie
tena. Watu wakaenda zao. 6. Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee waliokuwa
wakisimama mbele ya Sulemani, baba yake, alipokuwa hai, akasema, Mwanipa shauri
gani ili niwajibu watu hawa? 7. Wakamwambia wakasema, Ukikubali kuwa mtumishi
wa watu hawa leo, na kuwatumikia, na kuwajibu, na kuwapa maneno mazuri, basi
watakuwa watumishi wako daima. 8. Lakini
akaliacha shauri lile la wazee, walilompa, akataka shauri kwa wale vijana
waliokua pamoja naye, na kusimama mbele yake. 9. Akawaambia, Mwanipa shauri
gani ili tuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakinena Utufanyie jepesi kongwa
lile alilotutwika baba yako? 10. Na wale vijana waliokua pamoja naye
wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliokuambia, wakisema, Baba
yako alilifanya zito kongwa letu, bali wewe utufanyie jepesi, uwaambie hivi,
Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11. Basi kama
vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba
yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 12. Basi,
Yeroboamu na watu wote wakamfikia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme
alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 13.
Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa;
14. akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya
zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa
mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 15. Basi mfalme hakuwasikia wale
watu; maana jambo hili lilitoka kwa Bwana, ili alitimize neno lake, Bwana
alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.”
Utangulizi.
Somo letu leo linahusu tukio hili
kubwa kabisa la kusikitisha ambalo lilitokea mapema sana mara baada ya utawala
wa Rehoboamu mwana wa Sulemani kuingia Madarakani!
Jina Rehoboamu maana yake “Mwenye
kuwaongeza watu” Lakini hata hivyo maisha yake yalijawa na wingi wa majanga
yenye kuhuzunisha na kusikitisha sana, na Moja ya janga kubwa ni kugawanyika
kwa Ufalme wa Israel na kujitenga kutoka kabila la Yuda, jambo hili
linatupelekea leo kuchukua Muda mfupi ili kujifunza mengi kutoka kwa Rehoboamu.
Katika kujifunza somo hili
tutaangalia mambo muhimu yafuatayo:-
1. Ushauri
kutoka kwa wazee 1Falme 12:6-7
2. Ushauri
kutoka kwa vijana 1Falme 12:8-11
3. Muitikio
wa watu baada ya Uamuzi 1Falme 12:13-14a, 16
Ushauri kutoka kwa wazee IFalme 12:6-7
Inaonekana mfalme Rehoboamu
alisikiliza ombi la watu, na jamii kubwa ya watu waliomshauri katika kundi la
Kwanza walikuwa ni wazee, hawa walikuwa ni Makuhani, makamanda, washauri na
magavana, hawa walikuwa ni watu wenye ujuzi na ufahamu kuhusu utaratibu wa
Israel na tamaduni zake. Lakini pia walifahamu athari za utawala wa kifalme
hasa wakati wa Sulemani na jinsi utawala wake ulivyoacha athari mbaya kwa raia
wake.
Wazee hawa walichokifanya kwa
Rehoboamu ilikuwa ni kuweka wazi udhaifu wa Mfalme aliyetangulia, Ufalme wa
Sulemani ambaye aliitwa mwenye hekima kubwa kuliko watu wote Duniani katika
nyakati zile, ulikuwa umeacha athari kubwa na makovu makubwa sana kwa watu wake
na hata kwa Mungu pia, Sulemani alikosa muda wa kushughulika hata na familia
yake, alikuwa akishughulika na mambo ya watu wengine Wimbo uliobora 1:5-6, Sulemani katika utawala wake alijishughulisha
kushauri wafalme wa maytaifa mengine, alijishughulisha kujenga utukufu wake na
sifa zake, aliiigeuza jamii yote kuwa watumwa wake, alisahau hata kumuweka
Mungu mbele, alioa wanawake wengi ambao waliingiza ibada za miungu katika
Israel, Mahitaji ya Sulemani yalikuwa makubwa sana kiasi ambacho aliongeza kodi
kwa raia wake na kila mmoja alijihisi kuwa ni mtumwa, watu walikaa kimya,
waliojaribu kumpinga walitaka kuuawa na hivyo walikimbia uhamishoni, Mungu
alikwisha kukusudia mapema kuwa atausambaratisha utawala wa Sulemani na kuugawa
na atabakiza kabila moja tu kwaajili ya Daudi mtumishi wake, Mungu
alikwishakuupima moyo wa Sulemani nakuona kuwa ameshindwa kuiendea njia ya
Daudi baba yake.
Wazee waliona nafasi ya magezi
ilikuwa moja tu, ni Mara alipotawazwa Rehoboamu kuwa mfalme, hapo ndipo
walipojua kuwa watapata Nafuu hivyo walimsihi mfalme.
1. Utupunguzie
utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako
2. Kubali
kuwa mtumwa wa watu hawa ( hapa wazee walikuwa wanamaanisha Unyenyekevu,Utu,
Huruma na kujali)
3. Wape
maneno mazuri (Jibu watu vizuri, jali watu ona watu kuwa wathamani, kuwa mwema
kwao na wakati mwingine wasikilize na kuwajibu watu vizuri) “Mithali 15:1-4”
4. Watu
watakutumikia daima, walikuwa tayari kumtumikia mfalme anayejali
Rehoboamu alifanya maamuzi ya
busara, alitulia na alitoa siku tatu kuwa atatoa jibu ni maamuzi gani atafanya.
Ushauri kutoka kwa vijana 1Falme 12:8-11.
Hata hivyo ilikuweko nafasi
nyingine, hii ilikuwa ni kuwasikiliza vijana wanasema nini? Na hata hivyo
hakuweza kuukubali ushauri wa wazee mapema kwani aliona hawezi kuwa mnyenyekevu
na kuwatumikia watu wanaostahili kutawaliwa tu majibu ya Rehoboamu yalikuwa ya
Ujeuri zaidi
1. “Kidole
changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu” “loins – sex organ”
Haya yalikuwa ni
majivuno na kiburi cha hali ya juu, Rehoboamu alitaka kuonyesha kuwa ana nguvu
kuliko aliyemtangulia, utawala wake ni superior kuliko ule wa Sulemani yeye ni
super power
2. Rehoboamu
alishauriwa kuongeza utumwa na kodi na kuifanya nzito zaidi, alisema kama Baba
aliwapiga kwa mijeledi mimi nitawapiga kwa nge (Scorpion) hiki ni chombo chenye vipande vya chuma vyenye uwezo wa
kukatakata, ujumbe aliokuwa akiutoa hapa ni wazi kuwa nitaongeza machungu yenu
hasa kuliko ilivyokuwa kwa Sulemani
3. Alizungumza na watu kwa ukali sana Mstari 13.
Hakuna kubembeleza mtu,Hakuna maneno mazuri wala ya Heshima
4. Watu
wakaasi na kumuacha Rehoboamu.
Muitikio wa watu baada ya Uamuzi 1Falme 12:13-14a, 16
1. Watu
waliona kuwa hawana urithi wowote katika Yuda waliamua kujitenga 15-16
2. Watu
waliamua kuangalia maisha yao wenyewe na nyumba zao wenyewe 16
3. Watu
waliingiwa na roho ya ukatili, walimuuamsimamizi wa utumwa 18
4. Na
Israel waliasi 19. Sio tu waliasi ufalme wa Yuda bali pia walimchukia Mungu wa
Israel na katika utawala wao waliona waabudu miungu mingine (watu
wakikasirishwa nawe hata Mungu unayemuamini hawatamuamini)
5. Rehoboamu
alitaka kupigana na Ndugu zake Mungu akamkemea 1Wafalme 12:21-24
Hitimisho.
Nini cha kujifunza kutoka katika somo hili.
1. Kuzaliwa
na mwenye Hekima hakukufanyi uwe na Hekima, wengine wameshindwa kupata japo
nusu ya akili za Baba zao
2. Tukiisha
kumuacha Mungu na kumdaharu utukufu wake unaondoka
3. Namna
yoyote ile ya kutaka kuwa na nguvu na utukufu bila kutanguliza Mungu na utu
utatupa kuishia kwenye wakati mgumu
4. Bila
uongozi wa kiroho au wa Roho wa Mungu hatuwezi kufanya maamuzi ya Busara
5. Ni
lazima tuwe na huruma kwa wanadamu, na kuonyesha kujali ubinadamu kwanza kabla
ya mambo mengine
6. Manabii
walikuweko na makuhani, ambao waliweza hata kuepusha vita kati ya ndugu na
ndugu, walitakiwa kusikilizwa kwanza
7. Rehoboamu
alilijua wazi kabisa tatizo lakini, alikataa kabisa kulishughulikia na hivyo
watu walimuasi na Mungu aliruhusu
8. Mgawanyiko
na udhaifu huu uliwapa nguvu maadui wa Israel kuwamaliza na kupelekwa utumwani
9. Lazima
wakati wote tufanye maamuzi yenye busara na kukataa ushauri mbaya, lakini pia
kama wazazi wetu hawakufanya vema tusiiifuate njia yao.
Mkiyajua hayo
Heri ninyi mkiyatenda! Yohana 13:17
Na mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent
Kamote.