MALACHI:
NABII WA SIKU ZA UAMSHO
A. Mwandishi
-
Malaki aliishi katika nusu ya
pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo, baada ya ujenzi wa hekalu kumalizika.
Malaki ambalo ni neno la Kiebrania ‘‘Malaki’’ kama lilivyo kwenye
Kiswahili, maana yake ‘‘Mjumbe
wangu.’’. Jina hili ni kifupi cha ‘‘Malakia’’
ambalo maana yake ni ‘‘Mjumbe
wa Bwana‘’ (1:1).
-
Jina hili la kitabu limetumika
vivyo hivyo kwenye maandiko ya Kiebrania na Kiyunani likionyesha kwamba hili likuwa
jina la nabii ambaye ujumbe wake umenukuliwa humu. Hakuna habari nyingine zo
zote za kibinafsi zinazofahamika za huyu nabii. Maisha ya kidini ya Wayahudi
yalikuwa mabaya :
-
Walikuwa wamekengeuka, wakawa wameoa wanawake
wa mataifa mengine, wakaacha kutoa zaka (fungu la kumi) na dhabihu ambayo na
sehemu ya Mungu, hata wakawa wamemwacha Mungu, hali ambayo ilifanana sana na
ile iliyokuwepo wakati wa Nehemia (444-432 K.K.).
B. Kiini cha ujumbe wa kitabu cha
Malaki
-
Masikitiko makubwa ya Malaki ni uhusiano kati ya Waisraeli na Mungu
haukuwa kama ulivyopaswa uwe. Walimwacha Mungu na kumdharau, wala
hawakumheshimu inavyostahili, wakashindwa kufuata yale Mungu aliyowaagiza.
Matokeo yake hukumu ikawa inawangoja, lakini watu wanaomcha Mungu
wamehakikishiwa kuwa wameandikwa kwenye kitabu cha Mungu, nao watafuhia wokovu
wa Mungu milele.
C.
Kusudi
-
Kuwahimiza watu wafanye
mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao, kwa kuwakumbusha upendo wa
Mungu (1:1-5) na pia kwamba
adhabu yake iko karibu (2:17; 3:13)
D. Mchanganuo wa kitabu cha
malaki
-
Kitabu hiki kinaonyesha
kuwa:(1)Hekalu lilijengwa tena (516/515 K.K.), dhabihu na sikukuu zilirudishwa.
(2)Ufahamu wa jumla wa sheria ulirudishwa tena na Ezra (kama 457-455 K.K. ; tazama Ezra 7 :10, 14, 25-26) na
(3).Kurudi nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea miongoni mwa makuhani na mwa
watu pia (kama mwaka 433K.K.). Kutokana na hali hii hali ya kiroho na upuzi
Malaki anaouzungumzia kwa karibu vilifanana sana n aile hali aliyoikuta Nehemia
aliporudi kutoka uhamishoni Uajemi (kama 433-425 K.K.) ili kuwa mtawala wa
Yerusalemu (ling. 13 :4-30).
E.
Mahali
-
Yerusalemu. Malaki, Hagai na
Zekaria walikuwa manabii katika Yuda (Ufalme wa kusini) baada ya watu kurudi
kutoka uhamishoni.. Hagai na Zakaria waliwakemea watu kwa kutokumalizia ujenzi
wa hekalu. Malaki alipambana nao kwa sababu walipuuzia hekalu na kutokumjali
Mungu.
F.
Tarehe
-
Yale yaliyomo kwenye kitabu
hiki yanaonyesha kwamba huduma ya Malaki ilikuwa kwenye utendaji mnamo sehemu
ya pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo. Hekalu lilikuwa tayari limeshajengwa
tena upya. Kutokana na wakati alioishi Malaki na yale yaliyomo kwenye kitabu
hiki, inawezekana kiliandikwa 557- 525 K.K.
G.
Wahusika
wakuu
-
Malaki na makuhani
H.
Mgawanyo
-
Upendo wa Mungu kwa Israeli.
(1:1-5)
-
Israeli yamtukana Mungu.
(1:6-2:16)
-
Hukumu ya Mungu na ahadi yake.
(2:17-4:6)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni