Jumanne, 29 Machi 2022

Na sisi je tufanye nini?


Luka 3:2-14wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi, kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa; Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu. Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi?  Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi?  Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.”

Utangulizi:

Moja ya manabii wa ajabu sana ambao unaweza kujifunza habari zao na ukashangaa ni pamoja na na Nabii Yohana mbatizaji, Huduma yake ya kinabii ilikuwa imejawa na kuwaandaa watu watubu, kwaajili ya kumpokea Masihi, Ni wazi kuwa Masihi kwa namna anavyoelezewa na maandiko ni kiongozi wa ngazi ya juu mno na ambaye sio wa kawaida na hivyo Mungu aliona kuwa hawezi kupokelewa kienyeji bila mioyo ya watu kuandaliwa ili iweze kustahimili ujio wa Masihi, kwa hiyo Mungu katika mpango wake alikusudia kumtuma Yohana Mbatizaji nabii, Hili linadhihirishwa wazi na nabii Isaya miaka 700 kabla ya ujio wa Yesu, alitabiri juu ya ujio wa Yohana mbatizaji na huduma yake ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa sana katika kuandaa mazingira ya kumpokea Yesu Duniani ona:-  

Isaya 40:3-5 “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.”

Unaweza kuona umuhimu wa nabii huyu ulikuwa mkubwa mno, kwani alitumwa kuwaandaa watu watubu kabla ya huduma ya masihi kwa kuwa masihi mwenyewe ndio wokovu wa Bwana utakaofunuliwa kwa watu kwa jinsi ya Mwili, Masihi mwenyewe ni utukufu wa Mungu, na kwa sababu watu wangemuona kwa macho yao ya mwili ilikuwa ni muhimu kuandaa mioyo yao ili macho yao yauone wokovu wa Bwana na utukufu utakaofunuliwa kwa watu wote ona:-

Luka 2:25-32 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, Uliouweka tayari machoni pa watu wote;Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.”

Kuja kwa Masihi kuliambatana na mahubiri mazito yaliyokuwa yakiwataka watu wawe na toba ya kweli iliyoambatana na kuzaa matunda na kubatizwa ili kudhihirisha kuwa kweli watu wamebadilika na wako tayari kumpokea Masihi, ilikuwa ni lazima jamii iwe na usafi wa moyo na kuwa mioyo yao ilikuwa lazima iwe tayari kwaajili ya Mungu na kwaajili ya wanadamu, Ili Yesu akute na atembelee jamii ilikuwa ni lazima njia isafishwe, palipo na kilima pasawazishwe na kila mahali ambako hakuko sawa sawa ilikuwa ni lazima pawe sawa, kila kikwazo ilikuwa ni lazima kiondolewe ili watu waweze kuishuhudia neema ya Mungu maishani mwao, ilikuwa ni lazima watu wawe mbali na uchungu, waondoe chuki dhidi ya Mungu, na maudhi na kero zote walizokuwa wakiwafanyia wanadamu wenzao, Yohana aliwaonya juu ya hukumu ya Mungu itakayokuja endapo kizazi kile hakitatubu, Hata hivyo ujumbe wa Yohana mbatizaji ulikuwa na mtindo wenye kufurahisha sana kwa sababu watu walimwendea wakitubu kwa kupitia kazi zao (professional), Mtindo wake wa kimaonyo na kimahubiri unaonyesha wazi kuwa ni watu ndio walimuendea wenyewe wakitubu, na kuuliza maswali, lakini sio hivyo watu walienda kimakundi kutokana na uhalisia wa kazi zao na kila mmoja akitaka kujua kuwa afanyaje ili asimkwaze Mungu na jamii na ndio maana swali kubwa la ujumbe huu ni *Na sisi je tufanye nini?*

1.       Kwa Jamii (Makutano) – Yohana mbatizaji alishangaaa kuona jamii kubwa ya watu wakikimbia kwenda kutubu na hivyo aliiambia jamii waziwazi, Kwamba waondoe uchungu mioyoni mwao Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?Kitendo cha kuwaita makutano kizazi cha nyoka kilimaanisha kuwa watu wengi walikuwa upande wa shetani ambaye ndiye nyoka, lakini sio hivyo tu jamii ilikuwa na uchungu na malalamiko ya kila aina, na sio hivyo tu ilikuwa ni jamii iliyojaa hila na dhuluma na vilio vya kila aina, manung’uniko na hali ya kujiona kuwa hawakufanyiwa sawa, watu ambao wakati wote hawana jema Yohana aliwaonya watu wa namna hii Kuwa kamwe hawatafurahia uwepo wa Masihi, Na ujio wa Masihi hautakuwa na maslahi wa jamii yenye uchungu, jamii yoyote yenye uchungu hata uwafanyie nini hawatakuja kuridhika hata siku moja, hawatakuja kutoa shukurani, wakati wote watalalamika, uwepo wa Mungu na Baraka za Mungu na Hazifanyi kazi kwa jamii ambayo imejaa uchungu, Na ndio maana Yoaha nanakiita kizazi cha nyoka!Uchungu wakati wote katika maisha unapunguza sana neema ya Mungu, Maandiko yanatuonya kutokuwa na uchungu!

 

Waebrania 12:15 “mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”

 

Yohana alikuwa anaiona hukumu ya Mungu na kuwa mafanikio hayawezi kuja kwa jamii ambayo wakati wote inalalamika tu au kwa jamii ambayo haitendeani mema au kwa jamii iliyojaa dhuluma, wizi, ubabaishaji, na hila za kila aina au jamii ambayo hairushusu hofu ya Mungu kutawala! Kama jamii ina uchungu wa aina yoyote hicho ni kizazi cha nyoka!

 

Waefeso 4:31-32 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”

 

Kizazi cha nyoka ni jamii iliyojawa na uchungu na uchungu ni sumu, ghadabu, hasira ni lazima iondoke katika jamii, uovu na ubaya wa kila namna ni lazima uondoke katika jamii ambayo inamtaka Masihi awe kiongozi wao, apite katikati yao aweze kuwa Baraka na kuleta uponyaji, ni lazima iwe jamii inayojaliana na kufadhiliana jamii ambayo imeacha umimi ubinafsi na uchoyo, Maandiko yanaitaka jamii kuondoa uchungu kwa kujilinda na choyo na kufadhiliana ona

 

Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.”

 

Si vema Yesu akaja katika jamii na kuikuta ina sumu, ina uchungu, na hasira, ina ubaya ina uovu, ina hali ya kutokusameheana au  isiyosamehe, jamii inayosingiziana, Yesu anaitaka jamii iwe na fadhili na ndio maana Yohana mbatizaji aliiiambia jamii kama una cha ziada gawia wasio nacho !

 

Luka 3:10-11 “Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo

 

Jamii isiyo na umimi itajifunza kutoa na kufadhiliana na itaachana na ubinafsi na kuangaliana wao kwa wao, leo hii jamii haiko hivyo kila mtu ana uchungu na kila mtu yuko kwenye kujikusanyia, kila mtu anangalia mambo yake na tumekuwa na jamii isiyo na shukurani na bingwa wa kulalamika na kujenga hoja za malalamishi ndio anaonekana shujaa katika jamii! Kama jamii ikiwa katika hali hiyo kweli hicho ni kizazi cha nyoka na hakina budi kubadilika na kutoka katika hali ya kuwa wana wa ibilisi na kuwa wana wa Mungu!

 

2.       Mafarisayo na Masadukayo (Madhehebu mbalimbali) – Wakati wa Yohana mbatizaji na Yesu pia kulikuwa na watu wa Madhehebu ya aina mbalimbali, madhehebu makubwa ya watu waliokuwepo nyakati hizo walikuwa ni pamoja na Mafarisayo na masadukayo, hawa walikuwa madhehbu maarufu sana nao waliposikia huduma ya Yohana mbatizaji walimwendea na wakatubu kwa wingi lakini Yohana hakuwaacha bila maonyo watu wa Madhehebu aliwaonya kuwa ni lazima waache kiburi cha kidini na kidhehebu, lakini lazima waache kujihesabia haki, Mafarisayo na Masadukayo walijifikiri kuwa wao ni madhehebu bora kwa sababu Ibrahimu ni baba yao Mbatizaji aliwaonya kwa manenio haya ona:-

 

Mathayo 3:7-10 “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

 

Mafarisayo na masadukayo yalikuwa ni madhehebu makubwa nyakati za Yohana na Masihi, Mafarisayo katika theolojia yao walikuwa wakiamini katika ufufuo wa wafu, waliamini katika malaika na maono na walikubaliana na vitabu vya Musa na manabii, lakini Masadukayo wao hawakuamini katika ufufuo, wala hawakuamini katika malaika na maono na waliamini vitabu vitano vya Musa tu na hawakujali vitabu vya manabii, kila mmoja alikuwa akijiona bora kutokana na madhehebu yake aliyokuwa nayo,Lakini zaidi sana walidhani ya kuwa Mungu anawahesabia haki kwa vile wao ni wana wa Ibrahimu, hata leo katika jamii zetu watu wanadhani kuwa kuwa na madhehebu ndio kuuchinja, wananadi sana madhehebu yao kuliko kumnadi Yesu, Yohana Mbatizaji aliwakazia akawaambia sikiliza Mungu anataka matunda yatokanayo na toba, Mungu anataka watu waliotubu na kugeuka na kuacha dhambi, ishu sio kuwa mtoto wa Ibrahimu kwa sababu Mungu anaweza kumuinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe, Hivyo Dhehebu lako sio ishu wala sio dili, dili ni Yesu, Dili ni Masihi, dili ni toba ya kweli na mabadiliko, Mungu anataka matunda mazuri, hakuna matunda mazuri mti huo utakatwa na kutupwa motoni:-

 

Wagalatia 5:19-24 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.”

 

Wakati Yohana akikazia kuwa shoka limekwisha kuwekwa tayari na ni moto tu unahusu watu wasio na toba Paulo anaongezea kuwa watu wenye matunda yasiyofaa hawatauona ufalme wa Mungu, Kama una dini nzuri watu wanataka kuona matendo yako na sio vinginevyo, kama una dhehebu zuri watu wanataka kuona mabadiliko dini au dhehebu lako halitusaidiii katika jamii Mungu anataka matunda kinyume cha hapo ni hukumu tu. Wayahudi na waislamu na wakristo wanatokana na Imani ya Ibrahimu na wote wanakiri kuwa Ibrahimu nabii ni baba yao wa imani, Ni muhimu kufahamu kuwa dini na madhehebu hayatatusaidia kama hakuna matunda ya kweli na toba ya kweli

 

Yakobo 1:26-27 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”

 

Kwa msingi huo Yohana aliionya jamii kuacha kujivunia dini zao na Madhehbu yao, wako watu ambao wako tayari kufa kwaajili ya dini zao wanazing’ang’ania kama chapati na hawana mpango na Yesu, na sio hivyo tu wanakiri ya kuwa wana dini lakini matunda hayaonekani, kama watu wana dini ya kweli chuki inatoka wapi, majungu yanatoka wapi, kiburi na dharau kinatoka wapi, fitina na majungu na kujipendekeza kunatokea wapi?  Mbona watu hawajilindi na mawaa, mbona hawajilindi na dunia, mtu anakiri kuwa na dhehebu safi lakini amejaaa viwango vya kidunia. Ni lazima watu watubu na kuzaa matunda.Vinginevyo hukumu itamhusu kila mmoja bila kujali ana dhehebu au dini nzuri kiasi gani!

 

3.       Watoza ushuru - Luka 3:12-13 “Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi? Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa.”

 

Kundi hili nalo wakati wa Yohana mbatizaji lilijitokeza kutubu, hawa walikuwa ni watoza ushuru, kundi hili liliagizwa kuacha dhuluma na kutoza zaidi ya kiwango kilichowekwa, kundi hili lilikuwa ni kundi la watu wenye tamaa ya fedha na waliojilimbikizia mali ka njia ya dhuluma, Dhambi yao kubwa ilikuwa ni kuzidisha na kutoza zaidi ya jinsi ilivyoamuriwa  ni watu waliokuwa wamejaa dhuluma sana, waliwadhulumu wananchi lakini pia hawakufikisha mapato serikalini, jamii ya watoza ushuru walihesabika kuwa hawana uzalendo na wala wakati mwingine sio waaminifu na hawafikishi kile kiwango cha fedha wanachokusanya au wakati mwingine walitoza juu ya kiwango kwa faida zao wenyewe! Hwa pia waliongezea manung’uniko katika jamii na kwa wayahudi watu hawa waliwekwa katika kundi la watu wenye dhambi sana, Kundi hili pia lilitakiwa kuacha uovu wake na kujiandaa kumpokea Yesu

 

 Luka 19:2-10 “Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

 

Watoza ushuru walikuwa wamejitajirisha kupitia mali za dhuluma, na kuzidisha kiwango cha fedha kilichowekwa, hawa Yohana mbatizaji aliwajibu walipo uliza na sisi je tufanye nini aliwaambia wasitoze zaidi ya kiwango kilichowekwa, sehemu nyingi sana leo hii kumekuweko na watu ambao wanatoza zaidi ya kiwango kilichowekwa, unadhani kwanini serikali inapiga marufuku swala la twisheni kwa walimu? Kwa sababu tayari ada zipo zimewekwa, lakini kwanini walimu wanafanya twisheni, kwa nini wanachukua fedha ili wakufundishe pembeni pembeni, ada unayolipa haiwatoshi? Kuna namna nyingi sana watu wanatoza zaidi ya kiwango kilichowekwa,  wako pia wafanya biashara ambao wanatoza zaidi ya kiwango kinachokusudiwa na ukitaka kuwaweza we sema tu unadai risiti, watakuambia kuna bei ya kuandika kwenye risiti na bei ya bila risiti, Kristo hawezi kukubaliana na jamii ya watu yenye dhuluma ili aweze kuweka makazi anahitaji watu watubu kama alivyofanya Zakayo, aliamua kutubu na kurudhisha kwa jamii kile alichokusanya, wako watu wanakusanya na hawarudishi kwa jamii, lakini vilevile hawafikishi serikalini kama kila aina ya ushuru ungekuwa unafika inakotakiwa serikali ingekuwa imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo, watu wangeweza kunufaika na mataifa yao na nchi zao na huduma za kijamii bila kuhitaji kukopa katika mataifa au mabenki, hakungekuwa na sababu ya kuinamia mataifa mengine, kuhitaji msaada, watoza ushuru hali kadhalika walifanya kazi za kubambikizia watu kodi nzito, kutishia kufunga biashara ugomvi na wafanya biashara dhuluma na mambo mengine ya kusikitisha lakini hata hivyo wakitubu Yesu atawapokea.

 

4.       Askari – Luka 3:14 “Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu

 

Maandiko hayaonyeshi kuwa kazi ya uaskari kuwa ni kazi mbaya au isiyofaa kwani ni wazi Askari waliomjia Yohana mbatizaji hapa ilikuwa ndio mahali pa kuwaambia waache kabisa kazi hiyo kama ingekuwa haifai, katika ulimwengu huu ulioharibika askari ni wa Muhimu na wanahitajika kwa sababu kuna watu ni waizi, na bila kuweko askari wakati mwingine ni ngumu kuitunza amani inayokusudiwa, Lazima askari wawepo ili kukomesha umwagikaji mkubwa wa damu na kuzuia uhalifu, kulinda taifa raia na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo kila eneo, hivyo nabii hakusema waache kazi hii lakini aliwaonya wasidhulumu mtu na wala wasishitaki mtu kwa uongo kubambikizia watu kesi na kuwa watosheke na mishahara yao,Jaribu hili ndilo lililokuwa likiwakabili askari na hasa jeshi la polisi ambao walikuwa wakilinda usalama wa raia na mali zao katika mswala haya matatu kuna mambo ya ksingi ya kujifunza kwetu kwa kila kitu walichojibiwa askari kupitia Yohana mbatizaji.Sisi ni aksari tufanye nini:-

 

1.       Msimdhulumu mtu.

 

Dhuluma kwa kiingereza maana yake ni “unrighteousness” au KAKIA kwa kiyunani yaani ni hali ya kutokutenda haki, kutenda kwa ubaya, kutenda kwa kuumiza, kutenda bila kujali, watu wengi sana hawatendi haki hususani askari na hata watu wasio askari, lakini hata hivyo neno la Mungu linamtaka kila mtu atende haki kutokutenda haki kunaondoa neema ya Mungu

 

Tito 2:11-12 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;”

 

Kutokutenda haki sio mpango wa Mungu, Mungu alimwita Abrahamu ili awafundishe watu wake kutenda haki, na hii ndio sababu kubwa kwa nini Mungu alimchagua Ibrahimu, Mungu mwenyewe anaeleza:-

 

Mwanzo 18:17-19 “BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.”

 

Mungu hukasirishwa sana wanadamu wanapoacha kutenda haki na kufadha udhalimu

 

Warumi 2:18 “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;     na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu;”

 

Na ndio maana sasa katika mahubiri ya Yohana Mbatizaji aliwataka askari kuhakikisha kuwa hawadhulumu mtu na hii ilikuwa ni agizo la kwanza kwao haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya taifa zima !

 

2.       Wala msimshitaki mtu kwa uongo:

 

Kushitaki watu kwa uongo ni moja ya dhambi kubwa sana zinazofanywa na askari Katika Biblia mara kadhaa tumewahi kushuhudia watu wakiuawa na kuhukumiwa kwa kusingiziwa makosa yasiyokuwa yao, siku hizi unaweza kupewa kesi nzito kama Uhaini, unaweza kubambikiziwa ugaidi, au utakatishaji wa fedha au uhujumu uchumi na kadhalika kesi ambazo zinaweza kukunyima dhamana na ukajikuta unasota rumande Moja ya amri katika amri za Mungu ni pamoja na kutokushuhudia uongo

 

Kutoka 20:16 “Usimshuhudie jirani yako uongo”. Ni wazi kuwa kwa mujibu wa sheria za Musa kushuhudia uongo lilikuwa ni moja ya makosa mazito na kama mtu anagebainika kutaka kumsingizia mtu uongo adhabu yake ilipaswa kuwa sawa na kile alichokuwa akimshitaki mwenzi wake, waamuzi walitakiwa kuchunguza ka makini sana kama mtu anatoa ushuhuda wa uongo kisha yeye anayeshuhudia uongo alipaswa alipaswa kuhukumiwa katika kosa lileliole analolishuhudia ili mwenzake ahukumiwe

 

Kumbukumbu la torati 19:18-19 “nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye;ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako          

 

Agizo la torati liliwataka waamuzi vilevile kutokumhurumia mtu aliyewashitaki wengine kwa uongo yaani aliyetoa ushahidi wa uongo alitakiwa asihurumiwe

Kumbukumbu la torati 19:21  Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.”

 

Awaye yote ambaye angemshitaki mtu kwa uongo au kutoa ushahidi wa uongo kama alikuwa ana lengo la kumuumiza mwenzake waamuzi wangebaini wangetakiwa kutokumhurumia mtu huyo na angehukumiwa sawa na kosa alilokuwa akilitolea ushaidi wa uongo bila huruma, kwa hiyo unaweza kuona kwa nini Yohana mbatizaji alikuwa mkali kwenye swala hili ni wazi kabisa ilikuwa ni kosa kubwa na zito mbele ya macho ya Mungu kushuhudia uongo dhidi ya mtu mwingine.

 

Ukiacha maamuzi yanayoweza kutolewa na waamuzi au serikali, Mungu pia huingilia kati pale askari na watu wengine wowote wanapoacha kutenda haki na kujaribu kumshitaki mtu kwa uongo, Kitabu cha Esta ni mfano uliowazi wa mtu aliyeitwa Haman ambaye alikuwa mshauri wa Mfalme Ahasuero alimshauri vibaya kwa makusudi ya kuwaangamiza wayahudi, hususani kwa sababu ya chuki yake dhidi ya Mordekai, hii ikitokana na wivu mkubwa aliokuwa nao dhidi yake unaweza kuona

 

Esta 5:9-14 “Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai. Walakini Hamani akajizuia, akaenda zake nyumbani kwake; akatuma kuwaita rafiki zake na Zereshi mkewe. Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, nayo mambo yote pia ambayo mfalme amemfanikisha katika hayo, na jinsi alivyompandisha juu ya maakida na watumishi wa mfalme. Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme. Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme? Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.” Unaweza kuona pia.

 

Esta 6:4 “Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari.”

 

Esta 7:9-10 “Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.”

 

Maandiko yanaonya kuwa wote wanaoshitaki wengine kwa uongo wako chini ya hukumu ya Mungu na hukumu ileile wanayoikusudia kwa wenzao itawapata wenyewe, wale waliomshitaki Daniel ili atupwe kwenye tundu la simba walitafunwa wao, maandiko yanasema kila aliyechimba shimo aliingia mwenyewe pia, Mungu hafuirahii udhalimu hata kidogo

 

Zaburi 5:4-6 “Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya; Mtu mwovu hatakaa kwako; Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; Bwana humzira mwuaji na mwenye hila

 

Jambo la kushangaza ni kuwa wakati mwingine unaweza kuona kuwa hata makanisani na sehemu zenye watu wanaodhaniwa kuwa watu wa Mungu watu husingiziana, hubambikiziana kesi za uongo na kusababisha madhara makubwa wakati mwingine unaweza kuumizwa na watu wanaoshuhudia uongo lakini Mungu anajua na atakufariji kwa namna yake, Yesu alitambua kuwa wako watu wanashitakiwa kwa kubambikiziwa kwa uongo kwa kutokusimama katika haki au kuisimamia kweli

 

Mathayo 5:11-12 “Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu”.

 

Haijalishi watu watatuzushia nini kwa uongo tumtegemee Mungu, Mungu atatulipia tu unaweza kuzushiwa uongo na kubambikiziwa kesi mbaya sana na ukaumia na kupata hasara lakini Mungu atakuja kufanya kitu

 

Zaburi 119:69-72 “Wenye kiburi wamenizulia uongo, Kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako. Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Mimi nimeifurahia sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.”

 

Ni jambo la kusikitisha sana kuona jamii ikiwa imejaa watu ambao wanaweza kutunga jambo zito na gumu dhidi ya watu wengine na kuwaharibia maisha, wahubiri wa haki ya Mungu kama ilivyo kwa Yohana mbatizaji, asingeweza kuvumilia dhuluma katika jamii wala asingetaka Yesu Kristo aikute dhuluma lakini kutokana na jamii iliyokuwa imejaa uovu hata Yesu mwenyewe alishitakiwa kwa uongo na mafarisayo na Yesu Kristo aliposhutumiwa uongo alinyamaza kimya wala hakujibu neno

 

Isaya 53:7-8 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.” 

 

Unajua kwanini Yesu hakufunua kinywa chake kujitetea dhidi ya washitaki wake, maandiko yalionyesha katika Torati kuwa ni jukumu la Waamuzi kuamua na kuchunguza kwa makini kama mtu analeta ushahidi wa uongo na ni jambo la kusikitisha kuwa Pilato pia alishindwa kufanya maamuzi ya hali na kuachilia Yesu auawe huku ushahidi ukiwa wazi kuwa ni ushahidi wa uongo

 

Mathayo 27:22-26 “Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe. Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe. Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. Ndipo akawafungulia Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa ili asulibiwe.”             

 

Kama unadhani kubambikizia mtu kesi na kumshitaki mtu kwa uongo ni jambo jepesi ni lazima ujiohoji na uhoji kuwa ukiacha kusudi la Mungu la mwokozi kufa pale msalabani kesi ya kubambikiziwa Yesu ilimwachaje Mariamu mama yake? Na je ndugu zake Yesu na wanafunzi wake hii maana yake wale wote waliomshitaki Yesu kwa uongo nao vilevile kwa sharia ya Musa walitakiwa kusulubiwa lakini Yesu alitangaza sharia mpya ya msamaha ndio maana akawaombea baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo ni kwaajili ya haya mahubiri ya Yihana mbatizaji na makatazo yake yalikuwa ni ya muhimu sana kwa wanadamu na jamii sio tu ya wakati ule bali hata naya wakati wa sasa.

 

3.       Kutokutosheka na Mishahara –

 

Yohana aidha aliwajibu na kuwataka askari vilevile kutosheka na mishahara yao, ni wazi kuwa kutokuridhika ni tatizo kubwa sana la mwanadamu tangu anguko la mwanadamu lilipotokea hakuna kitu kinatosha wanadamu wamekuwa na tamaa na miongoni mwao wakiwa askari kwa sababu wao kama walinda usalama katika jamii wana nafasi ya kuona fursa mbalimbali na hivyo ni rahisi kwao kama ilivyo vilevile kwa watu wengine kuingia katika mlango wa tamaa hususani katika fedha na kuwa na roho ya kutokutosheka

 

1Timotheo 6:7-10  Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

 

Hali ya kutokuridhika na kuwa na tamaa kwa vyombo ambavyo vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa haki au kwa mwanadamu awaye yote ni tatizo la siku nyingi katika jamii mbalimbali hali hii huharibu uhusiano wetu na Mungu na wanadamu na kuharibu hali ya kiroho, Mungu angehukumu vilevile hali hii kwani hata zamani katika Israel ilikuwa ni njia ya matajiri kujipatia utajiri kwa njia zilizoharamu maswala haya yalikemewa na manabii kama Amosi, Mika na Yeremia Mfano katika kitabu cha Amos watu waliweza kuuza utu wa watu kwa sababu ya jozi za viatu tu 

 

Amosi 2:6b “Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu;”

 

Kwa msingi huo Yohana katika mahubiri yake alikuwa akiitaka jamii hususani askari kuwa na shukrani kuridhika kwani moja ya matunda ya ukomavu wa ubinadamu ni pamoja na kuridhika Lakini Mungu anawataka watu wake kuitenda haki ili Baraka za Mungu ziweze kumiminika katika maisha yetu

 

Mika 6:8 “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Lazima jamii ikubaliane na maandiko kuwa unapaswa ufike wakati turidhike na maandiko yanatufundisha kuwa kuridhika kuna faida kubwa sana

 
1Timotheo 6:6-19 “Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli

 

Kwa mtindo huu utakubaliana nami kuwa Nabii Yohana mbatizaji alikuwa Mtu aliyeibhubiri haki ya Mungu kwa konyooka bila kujali cheo cha mtu yeye aliwaonya watu wote masikini kwa matajiri, wafalme na hata watumwa akiwataka wote kuandaa njia ya masihi na kuwa tayari kwa mioyo iliyotubu mbele za Mungu.kila mmoja  hana budi kujiuliza nay eye je anafanya nini katika nafasui yake! Na afanye ulio wajibu wake

 

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima

Jumapili, 6 Machi 2022

Ngazi ya Yakobo:-


Mwanzo 28:10-19Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.”


Utangulizi:

Habari ya Ngazi ya Yakobo ni moja ya unabii ulio wazi kabisa kwamba kupitia Yakobo Mungu anakwenda kufanya jambo la maana sana kwa Dunia, ni ndoto iliyo wazi ya kuwa Mungu anakwenda kufanya njia ambayo kwa hiyo kutakuwa na uhusiano ulio wazi wa Mungu kwa watu wake kupitia Israel, Ni unabii ulio wazi kuwa Mungu amekusudia kupitisha jambo kwa Yakobo na kumfanya kuwa Baraka kwa dunia bila kujali kwamba amefanya nini katika maisha yake, Mungu katika maono haya au ndoto hii anamthibitishia Yakobo kwamba yuko pamoja naye na kuwa mapito yake sio mwisho wa kila kitu, Hatima ya maisha yetu haiamuliwi na nini tunakutana nacho katika maisha bali inaamuliwa na uhusiano wetu na Mungu, na ile kiu na hamu na shauku iliyoko ndani yetu inayotudhihirishia wazi kuwa tunampenda Mungu!, Kwa msingi huo basi leo tutachukua Muda kujifunza kwa undani na kwa kina na mapana na marefu, kuhusiana na somo hili Ngazi ya Yakobo, tukiwa na hamu na shauku ya kutaka kujua umuhimu wa Ngazi hii na maana yake kwa Yakobo na ujumbe wake kutoka kwa Mungu, tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo:-

·         Maisha kabla ya ndoto

·         Ndoto ya Yakobo

·         Maana ya ngazi ya Yakobo 


Maisha kabla ya Ndoto:

Kabla ya Ndoto yake Yakobo ambaye baadaye alikuja kuwa baba wa Taifa la Israel, alikuwa anakimbia kutoka mbele za uso wa ndugu yake Esau, sababu za kukimbia kwake zilitokana na makosa kadhaa aliyoyafanya kwa kaka yake, iko wazi kuwa wao walikuwa na ugomvi tangu tumboni

Mwanzo 25:21-23 “Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.”

Ni wazi kuwa Mungu alikwisha kuonyesha mpango wake Tangu mwanzo ya kuwa atamtumia Yakobo katika mapenzy yake na Sio Esau, Hata hivyo watoto hawa walikuwa na mafarakano tangu tumboni, walikuwa ni kapacha wasiofanana na wenye mitazamo tofauti, ingawa Mungu alionyesha wazi kuwa atamchagua na kumtumia Yakobo, hata hivyo kulinganisha na tabia zao, Yakobo alikuwa mwenye hila na tabia mbaya sana ukilinganisha na Esau kaka yake kwani katika maisha yake baadaye alinunua kwa hila haki ya mzaliwa wa kwanza kutoka kwa ndugu yake ambaye naye alikuwa na mtazamo usiokuwa wa maana wa kutiokujua umuhimu wa Haki ya mzaliwa wa kwanza na kuuza kwa bei ya hovyo 

Mwanzo 25:27-34 “Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani. Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo. Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.”

Licha ya kununua kwa hila haki ya mzaliwa wa Kwanza, bado Yakobo aliendelea na tama yake ya kutamani maswala Muhimu ya kiungu ambayo esau alionekana kuyadharau, na hivyo Yakobo kwa mara nyingine alisaidiwa na mama yake walijaribu kwa kila namna, kumlaghai mzee Isaka na kufanikiwa kuchukua Baraka za Mzaliwa wa kwanza kutoka kwa Isaka ambaye yeye alikuwa amemkusudia Isaka, Yakobo tena na mama yake kwa hila walifanikiwa kumlaghai mzee Isaka na kuchukua Baraka hizo ambazo zilikuwa na umuhimu wa maswala ya kimwili na kiroho kwa Familia nzima  ona

Mwanzo 27:30-36 “Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake. Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki. Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa. Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako. Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?

Tukio hili japo lilikuwa ni mpango wa Mungu lakini namna lilivyofanyika liliharibu kwa kiwango kikubwa mahusiano katika Familia ya Isaka, ambaye naye kimsingi ni mwana wa Ibrahimu na mrithi wa ahadi ile ya Abrahamu kufanywa taifa kubwa na Baraka kubwa sana kwa UlimwenguMwanzo 12:2 Kwa tendo la Yakobo kufanya hila hizo, kulipelekea uadui mkubwa kati ya Esau na Yakobo na kwa kweli Esau alikuwa amekusudia kumtenda mabaya Yakobo na kuwa angemuua mara tu baba yao atakapokuwa amekufa

Mwanzo 27:41 “Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.”

Jambo hili lilipelekea Isaka na Rebeka  kumruhusu Yakobo akimbie uhamishoni kwa mjomba wake Labani ili kwamba akajipatie mke huko lakini vilevile kuanza maisha mapya, Yakobo aliondoka katika hali ya wasiwasi mwingi na majonzi akiwa hana uhakika kuwa Mungu atafanya jambo, ama atatuimiza neno lake au atakuwa mwaminifu  kwa mtu ambaye kwa namna moja ama nyingine yeye mwenyewe amepoteza uaminifu, wote tunafahamu pale tunapokuwa tumefanya makosa makubwa sana wote tunajua kuwa japo tunampenda Mungu lakini wakati mwingine tumemkosea Mungu na kufanya mambo ya aibu na makubwa na mabaya ambayo kwayo tunaweza kudhani kuwa kila kitu kimeishia hapo, na kuwa yale yote ambayo tuliyatamkani na kuyafanya kwaajili ya Mungu huenda tusiyaone tena katika maisha yetu, wakati mwingine tunadhani kuwa hatuwezi tena kustahili Baraka za Mungu, tukiangalia mambo mabaya tuliyoyafanya, tunaweza kudhani kuwa tumepoyteza kibali kwa Mungu, tumepoteza upako, Mungu hatatutumia tena wala hatujali na wala hawezi kuzungumza na sisi, inaweza kuwa tumemkana Bwana tumefanya kinyume kabisa na neno lake, Yakobo alisababisha huzuni kubwa kwake, kwa kaka yake Mpendwa na pacha wake wa pekee, kwa baba yake ambaye ni mzee na yuko katika hali ya kufa, na mama yake aliyempenda sana sasa atamkosa na kukaa uhamishoni, ilikuwa ni hali ya kukatisha tamaa, kwamba badala ya kuona Baraka ambazo Mungu alizikusudia sasa yakobo anageuka kuwa mkimbizi na mtumwa anapoelekea kwa mjomba wake, akiwa njiani alichoka nadhani sio tu kwa sababu ya safari lakini pia kwa kuhuzunishwa na tafakari ya matendo yake ya kuhuzunisha na huzuni aliyowaachia wengine! Akiwa katika hali hii ndipo akapitiwa na usingizi mzito wa mawazo na kulala ! Hapa ndipo Mungu aliposema naye kwa njia ya Ndoto!

Ndoto ya Yakobo

Akiwa katika hali ya kufikiri na kutafakari, bila shaka utakubaliana nami kuwa haukuwa usiku mzuri kwa Yakobo hata kidogo, wewe na mimi tunafahamu tangu tulipokuwa wadogo pale tulipofanya makosa makubwa wakati mwingine baada ya kuadhibiwa au hata kabla ya kuadhibiwa tunafahamu usiku wetu unavyokuwa majuto mkaubwa yanavyotujia, mashaka makubwa yanavyotuvaa, na unajua kuwa unaweza usilale au unaweza kulala na usitamani kuamka na kama utaamka kosa lako linakuja na linakuwa la kwanza kulitafakari, majuto yanakuja unawaza  kwa nini nilifanya ujinga ule mkubwa, na unawaza kwa nini nimefanya vile laiti ningelijua, jaribu kuwaza na kukumbuka usiku ambao ulifanya makosa makubwa sana hutatamani jambo hilo ulikumbuke uatatamani hata kulifuta katika historia ya maisha yako, hiki ndio kilikuwa kinaendelea katika maisha ya Yakobo usiku ule, Yakobo alikuwa peke yake alikuwa anaelekea uhamishoni, usiku ule ulikuwa mzito na wenye kutisha usiku uliojawa na nyota nyingi na hakuna pa kupumzika Yakobo aliamua kuchukua jiwe ili ajipumzishe katika jiwe hilo kama ndio mto wa kulalia

 

Mwanzo 28:10-11 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale

Usingizi mzito ulimkabili Yakobo tena usingizi wa haraka ulikuwa ni usiku wa huzuni sana lakini ghafla usiku ule ulibadilishwa na kuwa usiku wa matumaini makubwa na usiku wa kipekee, usiku huu ulibadilishwa na Ndoto kutoka mbinguni na ndoto hii ilikuwa ndoto ya ajabu sana ndoto hii ilibadili mwelekeo wote wa mawazo ya Yakobo, ilikuwa ndoto ya matumaini makubwa sana ndoto hii ilikuwa hivi  

Mwanzo 28:12-15. “Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.” 

Ilikuwa ni ndoto iliyoleta uamsho mkubwa na matumaini makubwa katika maisha ya Yakobo yaliyokuwa muda mfupi uliopita amegubikwa na huzuni na kukosa matumaini lakini ndoto inabadili mwelekeo wa maisha yake, kila mmoja wetu katika maisha yake anapaswa kuacha kulalamika na kuhakikisha anakaa katika zamu yake akiisubiri ndoto yake itimie na ndoto hiyo haitasema uongo na itatimia kwa wakati wake, Yakobo alikuwa tu na muda wa kuisubiri ndoto hiyo itimie  kwa sababu ilikuwa ni ahadi ya Mungu mwenyewe ambaye ana sifa ya uaminifu!

Habakuki 2:1-3 “Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”

Kila mmoja wetu anasubiri ndoto yake kutokana na majanga anayoyapitia ndoto itakayobadilisha mwelekeo wa maisha yako, maandiko yanatuahidi kuwa iko ndoto ambayo itakujia kwa wakati uliomariwa na ndoto hiyo inakuja hatraka, haisemi uongo wala haitakawia inafanya haraka kufika mwisho wake  ni lazima itakuja tu

Maana ya ngazi ya Yakobo

Ndoto kuhusu Ngazi ya Yakobo inahusu nini hasa?  Wana theolojia wengi sana wametafakari sana kuhusu maana ya ndoto hii lakini wameshindwa kupata majibu muafaka na kamili, Aidha katika commentary za Marabi wa Kiyahudi nao pia hawana tafasiri nzuri nay a kujitosheleza kuhusu ngazi hii, na wengine wamefikiri kuwa ngazi hii ni Yesu Kristo, Lakini ni wazi kwanza kabisa hili lilikuwa ni agano kati ya Mungu na Yakobo ya kuwa atamtumia na kuwa pamoja naye na kuwa kupitia yeye Mungu atafanya uhusiano na Yakobo na uhusiano huo utawaunganisha wanadamu wote na Mungu kupitia taifa la Israel  unaweza kuona, Hivyo ngazi ya Yakobo inafunua Neema ya Mungu inayotuunganisha na Yesu Kristo, isiyotokana na matendo yetu, lakini inatupa kibali cha kumdfikia Mungu kwa neema tu! Ona  

Mwanzo 28:12-15. “Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.” 

Ngazi ya Yakobo katika ndoto hii ilikuwa inawakilisha muungano “Connection” Kati ya Mungu na wanadamu, inaonyesha wazi kuwa Mungu anatamani katika maisha yake kuwa na uhusino maalumu na mwanadamu bila kujali kuwa mwanadamu huyo yukoje yeye anatamani sana angekuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mwanadamu, uhusiano huo haungeweza kuanzishwa na mwanadamu mwenyewe bali ni Mungu tu, Ni Mungu pakee awezaye kuuanzisha uhusiano huo, Uhusiano huo ni wa kiagano ni uhusiano wa neema hautokani na matendo yetu ya nyuma tuliyotena kwamba tulikuwa wema au wabaya lakini tunaokolewa kwa neema ona

Waefeso 2:1-9Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. nKwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”

 

Yakobo alikuwa anajua wazi kuwa ameharibu uhusiano na Mungu na wanadamu, ameharibu usiano wake na familia alikuwa akijifikiri kuwa yeye ndio basi tena lakini Hakujua kuwa iko ngazi inayoweza kumuunganisha yeye na Mungu, hii ilikuwa ngazi ya neema inayoweza kumuunganisha mwanadamu na Mungu, ambayo haingalii historia yetu ya nyuma bali inaangalia moyo wenye kiu na hamu na shauku ya kumtaka Mungu, Yakobo anaona wazi kabisa Mungu amesimama juu ya ngazi hiyo  huku malaika wake wakipanda na kushuka hii ilikuwa ni ahadi iliyowazi kuwa Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake hata pale inapotokea kuwa sisi tumepoteza tumaini na kuacha kumuamini yeye hubaki wa kuaminiwa

2Timotheo 2:13  Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.”

Hakuna mwingine anayeweza kuwa mpatanishi, kiunganishi, daraja lenye kuweza kumfukia Mungu isipokuwa Yesu Kristo yeye pakee ndiye anayeweza kumpatanisha mtu mwenye dhambi na Mungu na kufufua tena matumaini yaliyopotea kwa sababu ya makosa na dhambi zetu

1Timotheo 2:5 “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;

Ngazi ya Yakobo inawakilisha upatanisho kati ya Mungu na wanadamu, Ki msingi upatanisho huu ulifanywa na Yesu Kristo kristo pale msalabani hivyo kimsingi ngazi hii ya matumaini inayounganisha uhusiano wetu na Mungu inayosimama kama daraja au mahali palipobomoka kutupatanisha sisi na Mungu bila kujali historia yetu kuwa tulifanya nini huko nyuma ua tumeharibu kwa kiasi gani, NGAZI HII NI NEEMA YA MUNGU INAYOTUUNGANISHA KWAKE KUPITIA KAZI ALIYOIFANYA YESU PALE MSALABANI Kupitia Yakobo ambaye ndiye baadaye Israel kulitokea kabila 12 na mojawapo ikawa kabila la Yuda ambalo lilimleta maishi kwetu Mathayo 1;1-17  Yakobo ambaye alikuwa na makosa mengi katika familia yake kupitia ngazi hii anapewa ahadi na Mungu kuwa Mungu atamtumia kuwa Baraka kwa ulimwengu, ngazi hii ni ya kwetu sote haijalishi kuwa tumeharibu kiasi gani, Mungu wetu ni mwaminifu, Mungu ni kama alikuwa hajali Yakobo amefanya nini lakini Mungu alikuja kuonyesha ya kuwa amemkubali Yakobo kwa neema tu,  haijalishi anaweza kujikosoa kiasi gani lakini ahadi ya Mungu kutoka kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo iko juu yake na kuwa Mungu atamlinda na kumuongoza  na kupitia yeye jamaa zote za Dunia watabarikiwa, Ngazi ya Yakobo ni uhusiano  wa neema ulioimarishwa kati ya Mungu na wanadamu kupitia Yesu Kristo, Huyu ndio njia na kweli na uzima ! Mungu anasema nasi na kuwasiliana nasi kwa njia ya Yesu Kristo na kwa neema yake, Pamoja na matendo yake Maovu Yakobo alipata neema ya kulibeba kusudi la Mungu na hata hivyo kwa kuwa Yakobo alipata neema ya kulibeba kusudi hilo Mungu hakumuacha awe na tabia mbaya bali alimbadilisha yeye mwenyewe baadaye na kuondoa jina la hila na kumuita Israel.

Waebrania 1:1-2 “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu

Usinione hivi nilivyo mwenzio nina ngazi, ni ngazi hii inayoniunganisha na Yesu ndio inayonifanya niwe tofauti na wanadamu wengine, Ngazi hii ni neema ya Mungu, Roho Mtakatifu aliniambia Bwana alikuwa amesimama mwishoni juu ya ngazi hii na malaika wa Mungu walikuwa wakipanda na kushuka, na kwa vyovyote vile Ngazi hii sio Kristo, Bali ngazi hii ni nyenzo inayotuunganisha na Kristo na akaniambia ngazi hii ni neema ya Mungu! Yakobo hakuwa mzuri, kimtazamo kama Esau, hakuna na akili kama Esau, hakuwa na nguvu kama Esau, tofauti zao ilikuwa Yakobo alitamani sana mambo ya Mungu na esau aliyadharau mambo ya Mungu na kwa kuwa Mungu hutazama moyo Yakobo alipata neema ya Mungu, na Mungu akafanya naye agano la neema, mwambie mwenzio nina ngazi na ngazi hii ni neema ya Mungu neema hii inaniunganisha na Kristo kule Mbinguni, ninalindwa nina ahadi nina nguvu kwa sina stresses tena siogopi kwa sababu nina neema!

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote



Alhamisi, 24 Februari 2022

Katika habari ya Madhehebu hiyo inanenwa vibaya!


Matendo ya Mitume 28:17-22Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu. Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa. Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako. Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali.”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Paulo mtume alitamani sana Kufika Rumi kwa miaka mingi, Mji wa Rumi ndio ulikuwa makao makuu ya Utawala wa waroma wakati wa ufalme mkubwa wa Kaisari, watu wengi sana waliishi katika mji mkuu wa Rumi, na wayahudi wengi sana, hivyo Paulo alitamani kuwa katika safari zake za injili vilevile aweze kufika Rumi, na alimuomba Mungu ili aweze kufika huko nako, unaweza kuona katika

Warumi 1:9-12Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu, nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu. Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara; yaani, tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.”

Unaweza kuona kwa hiyo kuwa kiu kubwa ya Mtume Paulo ilikuwa siku moja aweze kuonana na wayahudi walioko Rumi ili aweze kuonana nao, iliposhindikana kufika Rumi kwa wakati aliotamani aliwaandikia waraka, Paulo aliamua kuwaandikia waraka huu ili kuweka mafundisho Muhimu sana kuhusu Wokovu na ukombozi wa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini vilevile kanisa la Rumi na wayahudi walioko huko na wale walioamini wapate kujua injili aliyokuwa akiihubiri, Rumi ndio ulikuwa mji mkuu wa ulimwengu wa wakati ule na ulikuwa ni mji wenye watu wengi sana wakiwepo wayahudi, Paulo aliutamani mji huu kwa kuwa ulikuwa ni hazina ambayo baadaye ilikuja kutumika kueneza injili ya Kristo Duniani kwa kujua ubora wa mji huu na umuhimu wa huduma ya Paulo Mtume kwa watu wa Rumi, Shetani alijaribu kwa kila hila kuzuia injili kupitia Paulo mtume  na kupingana naye kwa namna na mazingira Magumu sana asifike katika mji wa Rumi na hivyo kulikuwa na mazingira magumu sana 

Matendo 27:1-44 “Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi. Siku ya pili tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa. Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho. Tulipopita bahari ya upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira, mji wa Likia. Na huko yule akida akakuta merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri kwenda Italia, akatupandisha humo. Tukasafiri polepole kwa muda wa siku nyingi, tukafika mpaka Nido kwa shida; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete, tukaikabili Salmone.Tukaipita kwa shida, pwani kwa pwani, tukafika mahali paitwapo Bandari Nzuri. Karibu na hapo pana mji uitwao Lasea. Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya, akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia. Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo.Na kwa sababu bandari ile ilikuwa haifai kukaa wakati wa baridi, wengi wao wakatoa shauri la kutweka kutoka huko ili wapate kufika Foinike, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi; nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki. Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani. Baada ya muda mchache ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani, uitwao Eurakilo, merikebu iliposhikwa, na kutoweza kushindana na upepo, tukaiacha tukachukuliwa. Na tukipita upesi karibu na kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida. Walipokwisha kuikweza wakatumia misaada, wakaikaza merikebu kwa kupitisha kamba chini yake, nao wakiogopa wasije wakakwama katika fungu liitwalo Sirti, wakatua matanga wakachukuliwa vivi hivi. Na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka. Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii. Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa. Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja.  Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu. Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano. Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche. Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo, Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. Na kulipokuwa kukipambauka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea. Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Ndipo wakachangamka wote, wakala chakula wenyewe. Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita. Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini. Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana. Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo. Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.  Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu; nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi

Hatimaye Paulo mtume alifika katika mji huu wa Rumi akiwa mfungwa lakini vilevile kwa shida kubwa sana wakinusurika kifo kwa njia zote dhoruba njaa na majanga makubwa sana mwishoe Paulo aliingia Rumi akiwa mfungwa wan je katika nyumba mojawapo chini ya ulinzi wa akida aliyeitwa Julius, akiwa katika vifungo vya minyororo. Na ndipo wazee wa kiyahudi walipokuja na kumsalimu lakini wakitaka kujua kwanini dhehebu hili linanenwa vibaya! Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vikuu viwili vifuatavyo:-

·         Katika habari ya Madhehebu hiyo inanenwa vibaya!

·         Kwa nini Dhehebu hili linanenwa vibaya!

Katika habari ya Madhehebu hiyo inanenwa vibaya!

Kwa bahati njema kama tulivyoona katika utangulizi wazee na viongozi wakuu wa wayahudi waliokaa Rumi walikuja kumtembelea na kumjulia hali, na kukutana naye katika nyumba aliyokuwa amefungwa, Naye aliwaelezea mkasa mzima wa namna alivyo singiziwa maneno ya uongo na jinsi alivyotaka kuuawa na akaamua kuyaokoa maisha yake kwa kukata rufaa kuja Rumi kwa kaisari hata hivyo wazee wa kiyahudi kule Rumi hawakuwa na taarifa yoyote kuhusu kesi yake na kile kilichokuwa kimeendelea juu yake

Matendo 28:17-21 “Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu. Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa. Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.”

Wazee wa kitahudi pale Rumi hawakuwa na neno lolote kuhusu Paulo Mtume na walikiri kuwa hawakuwahi kupata hata barua kuhusu Paulo mtume zilizotoka uyahudi, na hawa wayahudi waliosafiri kutoka Israel hawakuwahi kmzungumzia Paulo Mtume lakini jambo moja tu walitaka kujua habari ya dhehebu, kitu walichotaka kukisikia kutoka kwa Paulo na kutaka uhakika kutoka kwake ni habari ya dhehebu lake kuwa linanenwa vibaya kila mahali

Matendo 28:22 “Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali.”

Wazee wa kiyahudi walikuwa wamechoshwa kusikia kuwa kuna mamdhehebu mengi yametokea miongoni mwa wayahudi na yanajulikana kila mahali lakini katika habari ya Madhehebu hii habari imetukfikia kuwa inanenwa vibaya kila mahali, Wazee walimuuliza Paulo mtume swali hili kwa sababu yeye hakuwa maarufu na watu walimchukia kiasi cha kutokutaka kuzungumza habari zake, yeye alikuwa ni mtu aliyechukiwa na Wayahudi wote kila mahali hata huko Asia uturuki ya leo, kila mahali alikokwenda sio yeye tu watu wote waliomuhubiri Kristo walichukiwa na kuuawa wayahudi walifikiri kuwa ukristo unaondoa taratibu zao na desturi zao

Matendo 6:8-14 8. “Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati; maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa.”

Wayahudi walimuua Stefano kwa sababu alimuhubiri Kristo akiyatumia maandiko kuthibitisha kuwa Yesu ni Masihi, wayahudi walimshitaki Paulomtume pia kuwa ameingiza watu wa mataifa Hekaluni

Matendo 21:27-29 “Basi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimia, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata,wakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu. Kwa maana walikuwa wamemwona Trofimo, Mwefeso, pamoja naye mjini, ambaye walidhania ya kuwa Paulo amemwingiza katika hekalu.”          

Pia unaweza kuona kuwa wayahudi kutoma Asia walimfanyia fujo kubwa Paulo mtume kule Thesalonike Wakati Paulo mtume na Sila walipoihubiri injili, wayahudi walijaa wivu kuiona mafanikio ya injili na wakawafuatia kwa ukaribu na kufanya ghasia kubwa sana ona

Matendo 17:1-14 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano. Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko.”         

Ukristo na wahubiri wa kweli hawakuweza kukubalika kirahisi, Paulo mtume na washirika wake walipingwa kila mahali, nyakati za kanisa la kwanza injili haikuwa rahisi, ibilisi aliwatumia wayahudi kuhakikisha kuwa wanafanya fujo na kuharibu kabisa mpango wa Mungu hata kwa kukodi,  watu wasio na sifa njema ili mradi tu kuharibu haklinya hewa, na kuuahribu Ukristo, Wayahudi kutoa sehemu mbalimbali duniani walikuwa wamekwenda Yerusalem mara kadhaa katika siku kuu mbalimbali  na inawezekana walikutana na Wayahudi kutoa Asia ambao waliwatahadharisha kuhusu Ukristo kuwa ni madhehebu yasiyofaa kuna wakati ambapo hata Kaisari aliwafukuza wakristo waondoke Rumi kwa sababu ilifikiriwa kuwa wana imani tofauti mwaka wa 49AD Baada ya Kristo ona

Matendo 18:1-2 “Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao;”

Hata hivyo habari njema ni kuwa Wayahudi wa Rumi na hawakumpokea Paulo kwa fujo na hivyo walimsikiliza na hawakumshutumu kwa lolote lakini walitaka kusikia kutoka kwake, kuwa hawa watu wayahudi wanaomuhubiri Yesu kuwa ni masihi awathibitishie maana kila mahali hawa wanaomuhubiri Kristo kwa dhati wananenwa vibaya kila mahali hu ni uzushi au ni ukweli, huyu Masihi mnayemuhubiri ni kweli au ni uzushi? Hivyo walitaka kusikia Kutoka kwa Paulo Mtume kwamba hiki sasa ndio chanzo cha ukweli wa habari zote ambazo tumekuwa tukizisikia tunataka kusikia kutoka kwako hii ikoje katika habari ya madhehebu hii inanenwa vibaya

Kwa nini Dhehebu hili linanenwa vibaya!

1.       Walimuhubiri Christo.

 

Kristo Yesu, mateso yake kufa kwake na kufufuka kwake ilikuwa ndio kiini kiku cha ujumbe wa wahubiri wa nyakati za kanisa la kwanza, Nyakati za kanisa la kwanza wahubiri waliwaelekeza watu kwa Yesu, wakliwathibitishia wayahudi kwa wayunani kuwa Kristo ni Bwana, mahubiri yenye nguvu kupita yote ni yale ambayo kiini cha ujumbe wake ni Yesu, waelekeze watu kwa Yesu, sio dhebu lako, sio kwa mchungaji wako, waimarishe watu wasimame imara katika imani wakimtegemea Yesu, Paulo mtume na timu yake ya umisheni na uinjilisti hawakupeleka khadithi kwa watu walipeleka neno la Mungu, hawakupeleka hekima za wanadamu, walilihubiri neno lililothibitishwa kwa ishara na miujiza ya jina la Yesu  jambo hili liliwafanya kunenwa vibaya kila mahali. Ona;-

 

1Wakoritho 1:22-24 “Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta HEKIMA; BALI SISI TUNAMHUBIRI KRISTO, ALIYESULIBIWA; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu

 

Dhehebu au mtu awaye yote anayemuhubiri Kristo hawezi kufurahiwa, shetani hawezi kufurahi watu wamuhubiri Kristo shetani anataka mahubiri ya aina nyingine anataka watu wahubiri uponyaji na wa mwilini ambao ni wa kitambo na  mafanikio ya mwilini ambayo pia ni ya kitambo, lakini ile injili ya kweli ya kuwaelekeza watu kwa Yesu, na kubadilisha desturi za watu waache tabia mbaya, waishi maisha matakatifu, waache uchawi, waache ushirikina, wabadilike biashara ya uaguzi iharibike kamwe shetani haitaki injili ya aina hiyo wala hawezi kuikubali, unapomuhubiri Kirsto Kuzimu hakuwezi kufurahia na ndio maana nyakati za Kanisa la kwanza waliigundua siri kwamba nguvu ya kweli iko katika kumuhubiri Kristo, hivyo kila Muhubiri wa nyakati za kanisa la kwanza alipohubiri Kristo ndio ilikuwa kiini cha somo lake  na matokeo yalikuwa makubwa sana nay a kushangaza ona

 

Matendo 5:42 “Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za YESU KWAMBA NI KRISTO.”

 

Matendo 8:4-5 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO.”         

 

Matendo 4:18-20 “Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha KWA JINA LA YESU. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.”

 

Mahali popote au dhehebu lolote au taasisi yoyote ambapo Yesu anatajwa na kuelezewa vema, shetani hawezi kukubali mahali hapo panenwe vizuri, Jina la Yesu lina nguvu uwezo na mamlaka ya kuokoa na kuwaelimisha watu na kuwastaarabisha na kuwaponya na kuwaleta katika kiwango kikinge, kwa sababu hiyo kila mahali ambapo Kirtso anahubiriwa kwa dhati mahali hapo hapawezi kunenwa vema! Wapanene vema kwa lipi ilihali biashara zao zinaharibiwa, biashara ya tabia mbaya na ukahaba, na wizi, na ulevi na mapinduzi makubwa yanatokea watafurahishwa vipi, ni kwaajili ya haya katika habari ya madhehebu hiyo inanenwa vema!

 

2.       Walikazia kuwa viwango visivyo vya ulimwengu huu.

 

Kanisa au dhehebu tamu ni lile ambalo wahubiri wake wanakazia viwango, wanawaelekeza watu kuishi kwa viwango vya juu zaidi vya kibiblia, hawalichuji neno la Mungu wala kulighoshi wanakaza, injili za kina Paulo mtume zilikaza wazi wazi wala msiifuatishe namna ya dunia hii ona

Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

 

Watu au wakristo wanaoishi kwa viwango vya juu anavyovitaka Kristo na wahubiri wakikazia viwango anacvyovotaka Kristo shetani hawezi kufurahia, dunia haiwezi kukuinena vema, utasikia wanajifanya watakatifu sana sio wanajifanya maandiko yanatuita sisi ni watakatifu, hatupaswi kuishi chini ya kiwango  sisi sio wa ulimwengu huu na hivyo usufikiri kuwa dunia itakukubali, ikukubali kwa lipi, ikuunge mkono kwa lipi lazima unenwe vibaya

 

Yohana 15:18 -19 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.”

Sisi tumechaguliwa na Yesu, na sisi sio wa ulimwengu huu, hatuwezi kukubaliwa na ulimwengu, Mkristowa kweli ukiona unakubalika tu kila mahali lazima ujihoji, sisi sio wa kawaida Yesu ametuambia lazima ulimwengu utuchukie na kama utatuchukia utatunena vizuri kwa lipi ? sisi ni ukuhani mteule, taifa takatifu watu wa miliki ya Mungu, tumeitwa kutoka gizani sisi ni nuru giza hakliwezi kuwa na furaha na sisi hata kidogo, hivyo kama wanasengenya wasengenye sana, kama wanaroga waroge sana, kama wanakosoa wakosoe sana katika habari ya madhehebu hii inanenwa vibaya hii

 

1Petro 2:9 -10 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.”

 

Unaona kumbe kama dhehebu au kanisa au wahubiri na waamini wataishi maisha ya kiwango kile Mungu alichotuitia ulimwengu hauwezi kufurahia hata kidogo, watufurahie kwa lipi kama hatuna urafiki na dunia

 

Yakobo 4:4 “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.”            

 

Unaona nyakati za kanisa la kwanza watu walikuwa serious hawakuwa na mchezo walivunja urafiki na dunia, hawakuwa na mahusiano ya kijinga na watu wasioamini, unadhani dunia ingewakubalije, unadhani wangesifiwa unadhani wangenenwa vema?

 

2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike

Yesu alieleza wazi kuwa kwa kumfuata yeye na kumuamini hali haiwezi kuwa nzuri kwa dunia lazima watatuchukia, watatutesa, watatuua, na tunaweza kuchukiwa na mataifa yote kwaajili ya Kristo,

 

Mathayo 24:9 “Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.”

Moyo wangu unalibeba jina la Yesu unamuamini Yesu, nimejitenga na dunia, nimevunja urafiki na watu waovu, naishi maisha ya mfano nakazaia utakatifu naonyesha namna tunavyotakiwa kuvaa kwa nidhamu, naonyesha namna inavyotupasa kuabudu kumuheshimu Mungu naelekeza watu kwa Yesu, naishi maisha ya kiwango kisha unatarajia dunia inipende inipende kwa lipi?  Katika habari ya madhehebu hii imejulikana kwetu kuwa inanenwa vibaya kila mahali!

 

3.       Waliihubiri kweli!

 

Wanadamu huwa wanachukia ukweli, watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, ukitaka kuchukiwa wewe uwe tu msema kweli, utaona, watu wana mambo yao na wanataka wasiambiwe, ukiwaambia tu tayari unakosana nao kwa sababu watu wanapenda uongo na wanataka kudanganywa na ndio maana utaina imani za ajabu ajabu zenye usanii mwingi zinakubalika na kujaza watu wengi, wewe nyoosha maelezo utaona kimsingi tunapomuhubiri Yesu tunahubiri ukweli yeye ndio njia na kweli na uzima Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Tunapolihubiri neno la Mungu na kulitumia kwa halali tunaihubiri kweli Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Kwa msingi huo unapotaka kuwa na uadui na watu na ukitaka watu wakuchukie wewe uwe msema kweli, moja ya sababu ya Ndugu zake Yusufu kumchukia na hata kutaka kumuua ukiacha ndoto zake ni kwa sababu Yusufu alikuwa mkweli alipopeleka ripoti ya mambo yao kwa baba yake aliipeleka kama ilivyo

Mwanzo 37:2-4 “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.”

Nyakati za Kanisa la kwanza wahubiri hawakuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa walipeleka injili kavukavu na ukweli wake wote bila kuichuja jambo hili liliwafanya waonekane kuwa maadui ona Wagalatia 4:16 “Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?   watu katika ulimwengu huu wana mambo yao na yana faida klatika akili zao na hivyo sio rahisi kukubali mabadiliko anapotokea mtu kuwaambia ukweli wanachukia, dunia ya leo inahitaji kuhubiriwa kweli, mitume walihubniri ukweli, manabii walisema ukweli, wengine waliuawa kwa sababu ya kusema ukweli madhahebu haya yalinenwa vibaya kila mahali kwa sababu watu hawataki kuambiwa ukweli ona

 

Warumi 1:16-22 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;” Pale stefano alipowaambia watu ukweli walimsagia meno na wakamuua kwanini basi dhehebu linalohubiri kweli lisinenwe vibaya kila mahali.

 

4.        Shetani amepofusha fikra zao:

 

Kuna mambo mengi sana yanayowafanya watu wawe vipofu wa kiroho, wakati mwingine shetani, wakati mwingine kiburi, wakati mwingine ujinga, wakati mwingine kupuuzia, wakati mwingine kuongozwa na viongozi vipofu, wakati mwingine kufuata mkumbo, wakati mwingine kurithi na kadhalika, au kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu,  unapkuwa kipofu kwa sababu yoyote ile kati ya hizo huwezi kuona Yesu katika ubora wake kwa sababu maarifa yako na ujuzi wako unapigwa upofu ili usihifahamu kweli ambayo inatabia ya kukuweka huru

 

Yohana 8:31-32 “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Kazi mojawapo kubwa anayoifanya shetani pamoja na nyenzo zake nyingine ni kupofusha fikra na hivyo kuwafanya watu wawe wagumu na wawe vipofu ili wasimjue Yesu na nuru ya injili isiwazukie

 

2Wakoritho 4:3-4 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”  Unaona watu ambao fikra zao zimepofushwa na ibilisi hawawezi kuona utamu wa injili ya Bwana Yesu wao wataipinga tu wao ni vipofu hawawezi kuona ni watu wa dunia hii wanafuata kawaida ya ulimwengu huu wako chini ya mkuu wa anga hili ambaye anatenda kazi kwa wana wa kuasi waefeso 2:1-2 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;” unaona kwa msingi huo hawawezi kamwe kuisifia kazi ya injili na badala yake itanenwa vibaya kila mahali, wengine kwa sababu ya kiburi na wengine kwa sababu ya kukaa chini ya viongozi wasioifahamu kweli na kupata mafundisho potofu Mathayo 15:14 “Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.” Kwa msingi huo wakati mwingine sio rahisi mtu wa kawaida kujua maswala haya ya muhimu ya kiroho ni kwaajili ya haya utaweza kuona katika habari ya madhehebu hii inanenwa vibaya kila mahali.

 

5.       Kwa sababu ya tabia ya mwilini                .

 

Kristo Yesu amekuja kuwakomboa watu kwa jinsi ya Rohoni, ukiisha kusamehewa dhambi pia unaponywa kwa msingi huo asili ya ukombozi wetu inaanzia rohoni, neno linapohubiriwa ni mpaka mtu wa rohoni asikie ndipo na wa kawaida anaweza kuelewa kwa msingi huo mtu wa mwilini hawezi kuyatambua mambo ya Roho wa Mungu

 

1Wakoritho 2:13-15 “Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.”

 

Injili ni swala la kiroho, hivyo uwezo wa kufasiri maswala ya rohoni unamuhitaji Mungu ambaye ni Roho unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu, ni vigumu kwa ulimwengu kuitambua haya nan i vigumu kwa watu wa mwilini kuyatambua haya, ulimwengu haujui kuwa Mungu Roho Mtakatifu yupo, haujui kuwa Roho Mtakatifu yuko kazini, haujui kuwa yeye ni roho wa kweli, na hawawezi kumpokea maana hawamuoni 

 

Yohana 14:16-20 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.”

 

Kuifahamu injili, na kumfahamu Yesu kristo hakuji kwa akili za kibinadamu ni hekima inayotoka kwa Mungu hivyo wanadamu wa kawaida huona kuwa ni ujinga na upuuzi swala zima la injili na kwa sababu hiyo hawawezi kuzungumza jema kuhusu Ukristo sahihi

 

1Wakoritho 1:18-20 “     Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

 

6.       Dunia inamchukia Mungu

 

Kwa kawaida dunia iko kinyume na Mungu na inamchukia Mungu, Nyakati za kanisa la kwanza waliwaelekeza watu kwa Mungu na kulitangaza jina la Mungu, Dunia haimtaki Yesu na inamchukia Yesu na inachukia jina lake nyakati za kanisa la kwanza walimtangaza Yesu na walitii agizo lake la kuipeleka injili, Yesu alikwisha kuonya kuwa wale waifanyao kazi hiyo kwa dhati na kwa moyo watachukiwa udhihirisho wa chuki hiyo ni pamoja na kunenwa vibaya Mathayo 10:22 “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka,” unaona ni wazi kuwa Yesu alijua kuwa wanafunzi wake wa kweli watachukiwa  na watachukiwa kwaajili ya jina lake ni wazi kabisa kuwa Yesu anajua kuwa kwa chuki hizo watu hawawezi kulinenea vizuri kanisa la kweli nah ii ni kwa sababu ulimwengu unamchukia Mungu na hivyo sio ajabu kuchukia mali yake

 

Yohana 15:18 -19 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia                 

 

Maandiko yako wazi kuwa watu wa ulimwengu huu ni waovu, wenye tama, wenye chuki, wenye wivu, wauaji, wagomvi, wadanganyifu, matapeli, wachawi, wasengenyaji, wambeya, wenye kumchukia Mungu, wenye kiburi na majivuno, wenye kujisifu, wasiotii wazazi wao, wenye nia mbaya wenye ujuzi wa kutenda maovu kuliko mema, wenye kuvunja mapatano, wasio na huruma wenye mioyo mibovu wasiotii wazazi unategemea watu kama hawa watalipenda kanisa ambalo liko kinyume na  njia zao, linakemea uovu na kuonyesha njia ya haki sio rahisi

 

Warumi 1:28-30 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao  na maandiko yanaonyesha wazi kuwa pia huenda  wako watu wengi wanaomchukia Mungu pasipo sababuna pia wanaowachukia watu wa Mungu pasipo sababu ni wengi Daudi alichukiwa pasipo sababu alikuwa na maadui wengi ijapokuwa hakuwa mtenda maovu ona  Zaburi 69:4 “Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua”. Dunia inamchukia Mungu na neno lake kwa sababu linawashuhudia kuwa ni waovu Yohana 7:7 “Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovuunaona kanisa la kwanza hawakukubali kukalia kimya uovu waliukemea waliushuhudia kuwa haukuwa sahihi waliwaonyesha njia, hali kadhalika kazi hii ndio aliyoifanya Yesu alikema unafiki wa kidini, alionya na kuelekeza ibada sahihi na namna sahihi ya kumuabudu Mungu je unatarajia kama kanisa au dhebu litayatenda haya au mimi na wewe tutayafanya haya je tutanenwa vizuri kila mahali? Katika habari ya madhehebu hiyo imejulikana kwetu kuwa inanenwa vibaya.

 

7.       Kumfuata Yesu sio rahisi.

Nyakati za kanisa la kwanza mafundishi kuhusu dhiki nha udhia yalikuwa ni mojawapo ya nguzio muhimu sana ya Ukristo, wakristio waliteseka kwa namna na kwa njia mbali mbali ilikuwa kama kuchagua injili ni kuchagua njia ya mateso na mitume waliweka wazi hili kama msingi wa mafundisho yao na ya Kristo

 

Matendo 14:21-22 “Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.”

 

1Petro 1:6 -7 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.

 

Unaona tangu mwanzo Yesu alikuwa amekwisha kuonya kuwa kufuata yeye sio lele mama nyakati za leo injili zilizojaa mitaani ni za mafanikio na vitu vya duniani, injili za nyakati zetu  mkazo ulikuwa ni huu hapa IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI, injili  za leo ni kutesa duiniani na mbinguni ahaaaa tunapoteza muelekeo sio kuwa naunga mkono mateso hakuna mtu anapenda mateso lakini sisi ambao tumepata rata commitment zetu ni tofauti sana na zile wanazopata watu wanaopitia shida kwa ukweli Yesu hakuonyesha kuwa kazi ya injili ni lele,mama Luka 14:26-27 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.  Lakini watu wengi sana leo wanajihurumia na wanapoutazama Ukristo wa kweli na kuona msimamo wa aina hii ni wazi kabisa kuwa hawawezi kuzungumza mazuri kwa kuona watu ambao wana misimamo mikali na wanasonga mbele bila kujali kuwa wanapitia changamoto gani watu ambao wako tayari kuzipoteza nafsi zao kuliko kuziokoa Mathayo 16:24-26 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?   

 

Misimamo hii na misingi hii ndio ilikuwa misimamo ya Paulo mtuma na ilikuwa ni misimamo ya injili waliyoihubiri na ilikuwa misimamo ya kanisa la nyakati za kanisa la kwanza ni kwaajili ya haya watu wa ulimwengu ule walichukizwa na misimamo yao na kuona kuwa watu hawa wanaupindua ulimwengu na kubadili desturi za kilimwengu na kuuleta umayi kwa Yesu hivyo shetani alitumia silaya ya kuinena vibaya lakini wazee wa kirumi waliomfuata Paulo wao walikuwa waungwana na wenye hekima hawakutaka kusikia tu walimuuliza Paulo mtume mwenyewe wakitaka kusikia kutoka kwake kwanini katika habari ya madhehebu hii inannenwa vibaya ?

 

Bwana atupe neema kanisa la leo ili tusinenwe vibaya kwa ubaya badala yake tunanene vibaya kwa sababu ya viwango vya kujitoa kwetu kwa Mungu kuwa vya hakli ya njuu kiasi cha kuuchanganya ulimwengu, ni maombi yangu kuwa tutasimama imara na kuendelea kuipeleka injili mpaka Yesu afurahi barikiwa!

 

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote