Waefeso 6:10-13. “Hatimaye, mzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate
kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”
Utangulizi:
Tuko vitani, uwe unapenda au
hupendi lakini ni muhimu kwako kuwa na ufahamu kuwa tuko vitani, hii sio vita
kama zile za kawaida za dunia hii, ni muhimu wote kukumbuka kuwa tunazungukwa
na maadui wa aina mbalimbali kila siku na kila wakati katika ulimwengu wa roho
kila mmoja kulingana na kiwango chake
cha kiroho, uwe umeona au hujawahi kuona lakini uko katikati ya vita, uchaguzi
ni wako uweke silaha chini na ukimbie au uvae silaha na kupambana, kwa wale
ambao wako tayari kupambana, ufahamu kuhusu somo hili utakusaidia kuweza
kufahamu yale yanayokukabili na ukajipatia ushindi, kule kuwa na ujuzi tu
kuhusu adui zako unaopambana nao ni nusu ya ushindi kwa sababu kunatusaidia
kujua namna shetani na malaika zake wanavyofanya kazi katika ulimwengu wa roho 2Wakorintho 2:11 “Shetani
asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia vipengele kadhaa vifuatavyo:-
·
Ufahamu
kuhusu kuwepo kwa pepo wa mahaba.
·
Makusudi
ya utendaji wa pepo wa Mahaba.
·
Namna
tunavyokaribisha pepo wa mahaba.
·
Jinsi ya
kuwashinda Pepo wa Mahaba.
Ufahamu kuhusu kuwepo kwa pepo wa Mahaba.
Maandiko yanatueleza wazi juu ya
kuwepo kwa Pepo wabaya, shetani na mamlaka zake, jambo hili ni halisi, na sio
dhana na ndio maana Yesu alitupa mamlaka ya kushughulika na pepo wabaya Luka 10:18-20 “Akawaambia,
Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri
ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini
kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”
Kama uwepo wa shetani na pepo
ungekuwa sio halisi Yesu asingelisema lolote kuhusu hao wala asingetupa mamlaka
dhidi yao, lakini kitendo cha kutajwa na Kristo na huduma nzima ya Masihi
ilijihusisha pia na kutoa pepo ni swala lililowazi kuwa Pepo wapo na wanafanya
kazi katika Nyanja mbalimbali, jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa ukimuamini
Yesu na kutokumpa ibilisi nafasi ushindi dhidi yao ni Dhahiri. Sitaki kuchukua
Muda mwingi leo kuzungumzia uwepo wa shetani na mapepo na namna wanavyofanya kazi,
na historia yao lakini leo nataka
tuchukue muda kuzungumzia kuhusu pepo wa mahaba wakiwepo pepo wa mahaba wa
ngazi ya juu wajulikanao kama Incubus
and Succubus ambao mimi nitawaita Inkubi na Sakubi kwa Kiswahili pepo hao ni wabaya zaidi katika aina ya pepo
hao wa kawaida wa mahaba.
Pepo wa mahaba ni roho maalumu
wachafu wanaohusika na kuwatesa wanadamu kwa tamaa ya kingono, wakipandikiza
mawazo machafu ya zinaa na kuathiri maswala kadhaa katika maisha na utendaji wa
kila siku wa wanadamu pamoja na kuwafanya waishi maisha dhaifu ya kiroho,
wadumae kiroho na hata kushindwa kuendelea na tabia ya uchaji wa Mungu kwa
sababu tu ya tamaa ya ngono. roho hawa wachafu wanaweza kumuingia mtu mwanaume
na mwanamke kwa kujificha na kukaa katika akili zao na kuwasumbua kwa tamaa ya
ngono, pepo hao wako katika makundi makuu mawili wako wanaofanya kazi kama
wanaume na wako wanaofanya kazi kama wanawake na kusababisha ndoto za kingono,
tamaa ya kingono, na mashambulizi ya kingono, watumishi wengi wa Mungu
wanaojihusisha na utoaji wa Pepo watakuwa wanaufahamu wa kutosha kuhusu kuwepo
kwa pepo hao wa mahaba.
Lakini hata hivyo ni muhimu
kufahamu kuwa Pepo hao wachafu wa mahaba pia wako kwenye ngazi mbalimbali za
kiutendaji na ngazi ya juu zaidi ambao wao huweza kushambulia na kuondoka zao
wakiacha athari kubwa sana katika maisha ya mwanadamu huitwa Inkubi na Sakubi
kwa kiingereza [Incubus and Succubus]
wenyewe hujulikana sana kama pepo wa usiku wa mapenzi ambao hushambulia
wanadamu wakiwa wamejitokeza katika umbile la kiume au umbile la kike na
kuwanajisi kwa kuwafanyia vitendo vya kingono vilivyo na msisimko mkubwa kuliko
wa binadamu.
Inkubi [Incubus] – hawa ni roho wachafu wa mahaba wanaomtembelea
mtu wakati wa usiku hususani wanawake na kufanya nao mapenzi.
Sakubi [Succubus] – hawa ni roho wachafu wa mahaba wanaomtembelea
mtu wakati wa usiku hususani wanaume na kufanya nao mapenzi.
Pepo hawa hufanya mapenzi na
wanadamu hususani wanapokuwa usingizini au katikati ya usingizi na kuamka hawa
ni pepo wa ngazi ya juu wa mahaba wanaofanya ngono na wanadamu na wanajulikana
kama pepo wa usiku, tofauti ya pepo wa mahaba wa kawaida inkubi na sakubi wao
wanahusika zaidi ya upotoshaji wa kingono huo ndio msingi wao mkubwa,
tunapozungumzia upotoshaji wa kingono maana yake pepo hawa ni wakali na ni wabakaji
lakini hupenda kuhakikisha kuwa wamekuacha umekasirika na kukosa amani ya
kiakili na utulivu, pia husababisha mgandamizo mkubwa na mateso ya
kisaikolojia, pepo hawa pia wanaweza kuleta tamaa ya kufanya ngono kinyume na
maumbile, wanaweza kuwa na majina tofauti tofauti kulingana na jamii mbalimbali
duniani, sehemu nyingine hujulikana kama popo bawa na kadhalika, pepo hawa
wamepewa majina mbalimbali kutokana na namna wanavyojidhihirisha katika jamii
mbalimbali duniani, Pepo hawa sio wa kawaida wako katika ngazi ya juu zaidi na
ni wenye nguvu tofauti na pepo wa kawaida wa mahaba, wakorofi na wakali na
wanaweza kuchukua nguvu zako! Wao ndio viongozi wa ngazi ya juu zaidi katika
maswala yote ya ngono.
Pepo hawa wanauwezo wa kuvaa
mwili [Incarnation] sio lazima uwe
mwili wa kibinadamu lakini hawa wana kiwango Fulani kinachowaruhusu kuvaa mwili
wa kiume au wa kike na kufanya ngono na wanadamu sawa tu na shetani ambaye ni
roho lakini aliweza kujitokeza kwa Eva katika umbile la nyoka kama unavyoweza
kuona katika kitabu cha:-
Mwanzo 3:1-4 “Basi nyoka alikuwa mwerevu
kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati!
Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke
akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya
mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije
mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,”
Nyoka huyu maandiko yanamtambua
kama Shetani (Joka) Ambaye yeye pamoja na pepo wengine wachafu yaani malaika
zake walitupwa duniani baada ya kufukuzwa huko mbinguni, kwa hiyo katika lugha
ya kinabii Nyoka na nge humaanisha Shetani na malaika zake, katika pepo wenye
gazi inayowaruhusu kutwaa mwili kwa muda na kutekeleza jambo Fulani Sakubi na Inkubi
wana ngazi ya aina hiyo kwa hiyo ndio maana wanapofanya uhalifu wa kingono
utaweza kuona au kuhisi kuwa unapata hisia za kuhisi kuwa kuna kiumbe kisicho
cha kawaida kimefanya jambo linalofanana na uhalisia katika mwili wako na
kuacha athari za kisaikolojia, kiroho na mateso. Pepo hawa pia wanahusika na
swala zima la kupooza kwa wanadamu [impotance] and [inability of an erection]
pamoja na kuua shauku ya kimapenzi kwa wanawake na wanaume.
Ufunuo 12:7-10 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake
wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka
akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.”
Inaweza kuwa ngumu kuelewa namna
roho hawa wachafu wanavyoweza kujipachika mwili lakini wale ambao wamewahi
kushambuliwa nao wanajua ukweli halisi wa namna roho hawa wanavyofanya kazi
yao, akili yako na nafsi yako itakuhakikishia tukio lisilokuwa la kawaida la
kukandamizwa na msisimko mkali na halisi, watakaokuachia au utakaojisikia
wakati wamekuingilia. Lakini wakati mwingine wengi huwa wasiri wanaficha
yanayowakuta na ni ngumu kuelezea yaliyokukuta kwa sababu Pepo hawa wanabaka au
kukuingilia bila ridhaa yako.
Pepo hawa hujidhihirisha wakati
wa usiku, ingawa wanaweza pia kujitokeza wakati mwingine hata mchana, wengi
wanaeleza kuwa wakati mwingine unawahisi pepo hawa wakiwa na miili yao ya
kiroho wanakuja na kufanya nao mapenzi, lakini inkubi na sakubi, mara nyingi ni wakorofi na waasi na wanavamia
na kukukandamiza na kukubaka, wanaweza kukupiga, na kukuzuia wanaweza pia
kusumbua na hata kuvunja vitu, unapofikiri kuhusu wao na utendaji wao hauna
tofauti na mpenzi mwenye fujo anayebaka au kulazimisha kufanya mapenzi na
anayetumia nguvu nyingi katika ngono tofauti tu ni kuwa hali ya hisia kali za
ngono yao utakaousikia unazidi ule wa wanadamu wa kawaida.
Pepo hawa watakuachia mbegu mbaya
ya kuitamani kufanya ngono kupita kawaida, au wataucha mwili wako ukiwa na
athari za kutaka sana ngono na utajua kabisa kuwa umepata mashambulizi ya pepo
hao, uhitaji wako wa kingono unakuwa wenye nguvu ya kupita kawaida na unatawala
akili yako hali hii itatokea wakati wowote lakini zaidi sana unapokuwa
mwenyewe, au unapokuwa peke yako au unapokuwa umelala, au kupumzika, unaweza
kujisikia kutokufanya lolote, au kufikiri lolote, unapatwa na uzito hujisikii
kuoga, kwenda kazini, au hata kuchangamana na watu utaona tu kuwa unachokitaka
wewe ni ile testi ladha ya ngono waliokuachia hawa viumbe, wakati mwingine
utasikia hamu na tamaa ya kufanya ngono ambayo ni kali zaidi kuliko ya kawaida
ya kibinadamu, mahitaji yako ya kingono hayawi ya kawaida wakati mwingine
uhitaji wako wa ngono unakuwa mkubwa kupita kawaida, ni muhimu tu kufahamu sio
kila uhitaji mkubwa wa kingono na wa nguvu unatokana na pepo hawa, kwani
unaweza kuwa na uhitaji mkubwa wa kingono, kihisia na ukashiriki ngono hiyo kwa
nguvu tu lakini na mpenzi wako au mkeo halisi au mumeo halisi, kwa wakati
halisi, hii inakuja tu bila kujali ni wakati gani na wakati mwingine hata bila
msisimko kutoka nje na ni tamaa ambayo huwezi kuidhibiti, hii ndio nguvu na
athari inayosababishwa na pepo hao na ni rahisi kuijua kwa sababu sio ya
kawaida! Kama umeokoka na ikatokea
ukavamiwa na roho hizi utatambua kuwa pepo hawa ni halisi, na utajua wazi
kabisa kuwa umepatwa na shambulizi, kwa ujumla Inkubi na Sakubi wanawasumbia na
kuwashambulia waamini pia katika nyakati
Fulani Fulani.
Inkubi na Sakubi pia hujihusisha
na ndoto zinazohusisha kulowa mbegu au majimaji
ya kutoka via vya uzazi au ndoto zinazohusisha kuleta mwamko mkubwa sana wa
kingono yaani nyege za kupita kawaida na inapokutokea usiku kama ndoto hizo
utaweza kuona umeamka ukihisi uhalisia wa tukio kupoteza usingizi, moyo kwenda
mbio na wakati mwingine kuachwa katika hali ya hofu.
Makusudi ya utendaji
wa pepo wa Mahaba.
Incubi na Sakubi ni pepo ambao
kazi yao ni kuharibu uzao wa kiungu, wote tunakumbuka habari ya wana wa Mungu
na wana wa wanadamu iliyotokea katika Mwanzo 6 ambapo wana wa Mungu waliwaona
hao binti za wanadamu kuwa ni wazuri wakajitwalia wake wowote waliowachagua na
kukazaliwa majitu hodari, hii sio lazima kuwa andiko hili liendane na kazi ya
inkubi na sakubi kwani wao ni viumbe wa kiroho na hawana uwezo wakuzaa na
wanadamu lakini matokeo yao yanafanana na tukio lile la Mwanzo 6 yaani kubadili
kabisa mwenendo wa watu wachamungu na kuharibu mwenendo mzima wa kifikra na
kiutendaji na kitabia wa binadamu.
Mwanzo 6: 2-4. “wana wa Mungu waliwaona hao
binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye
ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili
walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia
kwa binti za binadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari
zamani, watu wenye sifa.”
Kama ilivyo katika tukio hilo
wana wa Mungu walipooa binti za wanadamu kukazaliwa watu hodari ambao kimsingi
walianzisha tabia nyingine tofauti na kawaida za kibinadamu na ikalazimu Mungu
kuleta gharika, ni katika mtazamo kama huo Mapepo ya mahaba sakubi na inkubi
wanapofanya ngono na wanadamu, hawawezi kuzaa nao watoto lakini wanazaa nao
watoto wa kiroho,yaani kuna matokeo mabaya sana ya kiroho yanayotokana na
athari za pepo hawa, watoto hao wa
kiroho ni nini ni tabia chafu za kingono ambazo ziko nje ya asili ya tabia ya
kawaida ya kibinadamu, wao wanataka kuzalisha hali mbaya ya kiroho kwa mtu, wanaamsha
hitaji la kingono na kuiharibu dhamiri yako na kuvunjilia mbali ukuta wa
kingono na kuzalisha uovu katika ubongo wako wakikuachia mbegu ambayo wanaamini
itakuja kuota au kujitokeza, kwa hiyo wanapokuingilia wanaacha athari kubwa
sana, kama vile mwanamke mwenye hisia kali za kimapenzi anavyojiachia kwa mwanaume
na kumruhusu mwanaume huyo kumtawala kila eneo na kupandikiza lolote
analolitaka linalotokea kwake, au kama
mwanamke anayesumbua akihitaji ngono anavyoweza kujiachia kwa mtu aliyemsumbua,
mbegu zinapoingia hajui zinaenda wapi zitafanya nini na hajui kama
zitambadilisha,au kumpa mimba au magonjwa na yanaweza kujitokeza kwa sasa au
baadaye.
Inkubi na Sakubi halikadhalika
watakuacha ukiwa na hisia kali sana za kingono na hali ya ukavu wa kiroho,
baada ya kukuibia tabia njema na kukupandia mimba ya tamaa mbaya, lengo kubwa
ni kutaka kukuchepusha, kukutawala la kukuacha ukijiona hufai, pepo hawa wana
ujuzi mkubwa sana wa kukuachia msisimko mkubwa sana wa utamu wa kingono lakini
watakuachia hali ya kujiona duni usiyefaa kwa vyovyote vile, raha
watakayokuachia hawa roho wabaya kwa kawaida inazidi sana ile ya kawaida na
inakufanya uwe teja wa hiyo raha, hali hii inaleta hatia, kwa sababu ya raha
ambayo mwili wako umeisikia na inashusha chini nguvu yako ya kukataa jambo hilo
tena, kama utaumbiwa tamaa ya kuwataka pepo hao wakutembelee tena na tena
utakuwa mshirika na mashetani.
Jambo lingine wanalotaka
kuliingiza kwa kazi za pepo hawa wa usiku ni kuchepusha Imani, wanakuachia
mgandamizo wa mawazo utakaokupa nguvu ya kutafuta faraja, watakuingiza kwenye
shughuli za kingono, kupiga punyeto, kujipa raha zizizo halisi, kuangalia
mikanda ya ngono, sinema na picha za ngono, kwa ujumla kila aina ya jambo la kingono
linalokupa raha na zaidi ya yote kupoteza uadilifu na Imani kwa Mungu na
kujikuta umeacha kumpendeza Mungu, pepo hawa watafanya kila juhudi na bidii ya
kuhakikisha unaikana Imani kivitendo:-
Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani
haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba
yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
Wakifanikiwa kukupandikizia hayo
maana yake wamefanikiwa kuharibu uhusiano wako na Mungu na unapoteza kusudi la
kuishi kwako, kama kila kitu
kinawezekana kwake aaminiye kinyume chake ni kuwa kila kitu hakiwezekani kwake
asiyeamini, kwa msingi huo kila kitu kinaanza kuharibika, watu wanaoathiriwa na
pepo hawa huanza kuharibikiwa akili, lakini kila kitu katika maisha yao huanza
kwenda kombo na unaweza kudhani umerogwa au umelaaniwa, au u mtu mwenye bahati
mbaya sana lakini ukweli ni kuwa mfumo wako wa kiimani umeingiliwa na
kuharibiwa na kunajisiwa kwa kuchepushwa
na pepo hawa inkubi na sakubi. Sakubi na Inkubi wanajihusisha pia na maswala ya
migogoro katika ndoa, ugomvi hasa unaotokana na tendo la ndoa
kutokujitosheleza, wanakausha raha ya ndoa, wanaleta ukavu na kuondoa nyege kwa
wanawake na wanaume, wanaiba nguvu za kiume na nguvu za kike, wanaiba hata mbegu za kiume, wanazuia watoto
wasizaliwe, wanazuia ndoa zisifungwe, na ikifungwa ni kivumbi kwa migogoro,
wanapandikiza mawazo machafu unapofanya tendo la ndoa na mkeo au mumeo mawazo
yako yanakuwa kwa mwanaume mwingine au mwanamke mwingine, kusudi likiwa
lilelile la kukutoa katika wazo la kiungu kukuchepusha, wanajihusisha na kusinyaza uume na
uke, wanaweza kusinyaza uke au uume hata kati kati ya tendo la ndoa, wanajihusisha na kuzuia uzazi, yaani ugumba na utasa, au idadi ndogo ya
watoto usiowatarajia, unaweza kupata watoto wachache sana au ukakosa au ukapata
wa aina moja tu kusudi likiwa lilelile la kukutoa nje ya ndoa na nje ya Mungu, pale unapotaka kupata mtoto au watoto wa aina
nyingine, unaweza kuumbiwa wazo la kutafuta mtoto unayemaka nje ya ndoa yako, wanajihusisha na kupiga punyeto za aina zote ikiwa ni pamoja na kutumia
vifaa vya ngono kama uume wa bandia, na aina nyingine za vifaa au nyenzo zinazofanana
na hizo, mizozo na mafarakano, na zinaa zinazolenga wake za watu na waume za
watu watoto wadogo, ndugu na kadhalika vitendo hivi vyote na hata ubakaji na
udhalilishaji wa kijinsia na vinavyofanana na hivi vina ushawishi wa uwepo wa
pepo wa mahaba na pepo wa usiku na hasa hawa majini makubwa Sakubi na inkubi,
aidha Inkubi pia anauwezo wa kumuingilia mwanaume kinyume na maumbile na Sakubi
kujihusisha na maswala ya usagaji yaani kumuingilia mwanamke mwenzake kwa namna
ya kusagana, na inkubi pia anaweza kumuingilia mwanamke kinyume na maumbile
wakati wote huo watasababisha msisimko mpya na mkubwa usiokuwa wa kawaida ili
kukupandia mbegu ya kukuchepusha kutoka katika mapenzi ya Mungu, wanaweza
kusababisha kununiana na kugombana sana bila sababu hata kwa vitu vidogo
vidogo, kuharibika kwa mahusiano unashangaa tu kama ulichumbia mchumba wako
anakukimbia au anavunja uhusiano bila sababu ya msingi, kutokushika mimba, au
kutokuweza kumpa mtu mimba, kukosa hamu ya kufanya tendo la ngono na mkeo au
mumeo, wakati mwingine kwa muda mrefu tu, kulala mzungu wa nne au kuhama chumba, au kuamua kulala mbali na mwenzako, kwa ujumla wao wanailenga sana ndoa ili iweze kuharibika bila kujali ni mwaka gani watafanikiwa kufanya hilo, na wakati mwingine kuota unaoa au
unaolewa, kutokuolewa, au kutokuoa huku ukiwa na umri ambao watu wanatarajia
utaoa au kuolewa, wanawafanya vijana wanaume kuogopa kuoa na kubaki mabachela
kwa muda mrefu huku maisha yao ya ndoa yakiwa hayaeleweki, pia wanasababisha
watu kuachana na kupeana talaka, hii ni kwa sababu pepo hao pia wana wivu, na
hawapendi uwe na uhusiano mzuri na mwenzi wako mwanadamu, wanaleta hamu za
ngono zisizoweza kutoshelezeka, lengo kuu la pepo hawa ni lazima kukuchepusha
ili kutoka katika njia za kawaida za kingono za uumbaji na sheria za
Mungu, Katika maandiko pepo hawa wanaitwa
kiebrania LILITH AU LILIT ambayo tafasiri yake ni viumbe wa usiku kwa kiingereza “night creatures”
Isaya 34:14 “Na hayawani wa nyikani watakutana na mbwa-mwitu, na
beberu anamwita mwenziwe; naam, BABEWATOTO anakaa huko na kujipatia raha.”
Ukitazama vizuri mstari huo kwa
makini utaweza kuona neno BABEWATOTO nadhani
ni Kiswahili ambacho hakitumiki sana siku hizi lakini Biblia ya kiingereza
imetumia neno NIGHT CREATURE mfano
mzuri unapoangalia katika biblia ya kiingereza ya New International Version
yaani NIV maneno hayo yanasomeka hivi:-
Isaiah 34:14 “Derset creature will meet
with hyenas, and wild goats will bleat to each other; there the NIGHT CREATURE
will also respose and find for themselves places of rest.”
Unaona kimsingi hapa anazungumzwa
mnyama mweusi mkubwa kama bundi au popo lakini kwa kiebrania anaitwa “LIYLIYTH” Kwa kiingereza NIGHT SPECTRE yaani mzushi wa usiku au
mnyama wa usiku kwa kawaida hapa yanazungumziwa majini ya usiku yaani Majini
mahaba au mapepo wa mahaba au inkubi na sakubi ambayo ndio majinamizi ya usiku. Kwa kawaida biblia ina tabia ya
kujitafasiri yenyewe kama kuna sehemu imetumia neno gumu eneo lingine
linakusaidia kuweka sawa na hivyo ni
rahisi kuelewa kile ambacho kilikuwa andiko hilo limekusudia kupitia andiko lingine ona
sasa:-
Isaya 13:19-21 “Na Babeli, huo utukufu wa
falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu
alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake
tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji
hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani;
na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na MAJINI WATACHEZA HUKO.”
Andiko hili sasa linatusaidia
kufafanua andiko lile la mbele kwamba viumbe wanaozungumziwa hapo ni majini,
ndio maana huitwa jini mahaba, au pepo la mahaba, na ngazi ya juu zaidi ya pepo
hao ndio sakubi na inkubi, pepo hawa licha ya kuonekana kuchochea raha ya
kingono kwa wanadamu lakini wana madhara makubwa sana na maudhi makubwa sana
kwa wanadamu kiujumla sio wazuri hata kidogo, unaweza kufurahia utamu wa ngono
unaoshirikiana nao lakini unaweza kuwajibika kulipa gharama kubwa sana kwa
uharibifu mkubwa watakaosababisha katika maisha yako, shetani hana urafiki na
wanadamu ni adui wa wanadamu kwa hiyo ni muhimu kukataa hali hiyo vinginevyo
athari watakazozisababisha au wanazozisababisha zimewatesa wanadamu wengi sana
na kuwafanya watafute msaada baadaye na kama utakwenda kwa waganga wa kienyeji
utasababisha majanga makubwa zaidi hizi ndio athari zinazoweza kusababishwa na
majini hawa au pepo hawa wa mahaba:--
- Pepo hawa huwa wanaharibu sana uhusiano kabla ya ndoa chumba kadhaa zinaweza kuvunjika kama mtu analo pepo hili halitaki mahusiano hata kama mpenzi wako hujamkosea lolote unaweza tu kushangaa amesitisha uhusiano na wewe na labda akabaki anakula tu pesa zako, hata kama ishu sio kula pesa zako lakini ni pepo hawa wamesababisha uhusiano huo ufe bila sababu na baada ya ndoa kama watashindwa kuvunja uchumba wanaleta mafarakano na chuki ya kufa mtu ili mahusiano hayo yaharibike, unaweza kushangaa unamchukia mumeo au mkeo kana kwamba ndiye adui namba moja duniani wakati ulimpenda mwenyewe mtagombana na kususiana na kulala mzungu wanne na wakati mwingine kuvunjiika kwa ndoa.
- Kama ni kwa mtumishi anayemtumikia Mungu hasa waliotoa mwanya Fulani kushambuliwa na Inkubi au Sakubi basi ujue majini haya yanaharibu kiwango cha upako na huduma ya utumishi wako usishangae wahubiri wengi sana waliokuwa na upako mkubwa sana wamejikuta wakiangukia pua kwani kadiri unavyoongeza kiwango cha upako nao wanaiongeza tamaa ya zinaa mpaka ugundue na kufunguliwa au kufanya kazi ya kujikomboa wewe mwenyewe, kumbuka inkubi na sakubi hawaogopi ngazi yako ya kitumishi, watakuacha utumike na kutoa pepo lakini watahakiklisha unakuwa dhaifu sana linapokuja swala la ngono, huwezi kabisa kufurukuta, utafunga na kuomba, utahubiri, utatoa unabii, utatoa pepo lakini utajikuta u mzinzi mzuri sana na unaweza usielewe sababu zake lakini ni kama uliwapa mwanya sehemu fulani jambo hili litakufanya ukataliwe na Yesu wakati wa hukumu ona;-
Mathayo 7:21-23 "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
-
Wanaharibu Baraka za Mungu ambazo zimekusudiwa
kwako, wanaweza kupandikiza roho ya kukataliwa
-
Wanasababisha kufilisika na kuleta umasikini
mkubwa na wa hali ya juu, kila unavyopambana na kuinua kiwango chako cha
kiuchumi wao huharibu na kukushusha kwa kasi ili uwe masikini wa kutupwa!
-
Wanapandikiza chuki kubwa mnashangaa unamchukia
mkeo au mumeo kwa chuki kubwa sana kana kwamba ulilazimisha kumuoa hii inatokea
baada ya muda mfupi tu wa kufurahia ndoa yenu na kuendelea mfululizo mpaka
ufunguliwe, au wanaweza kusababisha talaka katika umri wowote wa ndoa yenu.
-
Wanasababisha kutokewa na matukio mabaya
yasiyoeleweka elewekaeleweka, kama mikosi, kuharibikiwa kazini nk.
-
Wanasababisha utasa kama yako kwa mwanamke na
ugumba kama yako kwa mwanaume mayai hayakomai na mbegu hazizalishi, au kiwango
kidogo cha mbegu za mwanaume na kusababisha kukosekana kwa watoto
-
Wanasababisha mimba kuharibika kama zinashika,
au kutokushika kabisa, au kuzaa watoto wawili au mmoja ama watoto kadhaa wa kike tupu au kadhaa wa kiume tupu.
-
Wanafunga siku zako za kuona mwezi na
kusababisha ugomvi mkubwa katika siku za hatari au za kufurahi tendo la ndoa,
wanasababisha kuweko kwa maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na uvimbe
katika kizazi
-
Wanaleta mawazo mabaya ya kutoa mimba, kuikataa
na hata kuharibika, kwa ujumla hali ya uzao inakuwa ngumu. Pepo hawa pia
wanaweza kuleta mvurugiko wa mzunguko wa siku zako za mwezi kwa wanawake.
-
Wanavuruga sana tendo la ndoa na hawataki mtu
aoe au aolewe unaweza kushangaa mtu wa miaka 40 mwanaume wala hana mpango wa
kuoa, au dada mwenye sifa za kuolewa lakini haolewi.
-
Wanasababisha maumivu makali sana wakati wa tendo
la ndoa kiasi cha kuhatarisha ndoa na sababu mbali mbali za hovyo hata
kununiana na kunyimana bila sababu mtu anaweza kupoteza hamu ya kulala na wewe,
maumivu chini ya kitovu na kwenye mji wa uzazi, wakati mwingine kuwa na uvimbe
unaohatarisha uzazi.
-
Wanaleta fadhaa kubwa, hali ya kujiona duni, kudhalilisha,
kukataliwa na hata kujiona hufai au kutaka kujiua na kukuumbua kuchukiwa na
ndugu, jamaa na marafiki, kukufanya ukasirike kasirike na kuharibu mipango yako
yote na mambo yako hasa ya maendeleo na kushindikana kwa kila unalolifanya hata
kama utasaidiwa.
-
Wanaharibu nguvu za kiume na za kike na
kuwafanya washindwe kufanya tendo la ndoa na wenzi wao na hatimaye wanaweza
kufunga ndoa na wewe ya kiroho jambo ambalo ni baya zaidi kwani litaongeza kifungo, Inkubi anaweza kuchukua nguvu za mwanaume mara baada ya kumuingilia kinyume na maumbile na kufunga nguvu zake za kiume kwa kusudi la kumuharibu na kumuingilia mwanamke kinyume cha maumbile ili kumuharibu pia
-
Ukiota ndoto za kufunga ndoa kuna uwezekano
wakawa wamekuoa katika ulimwengu war oho, na ukiota unanyonyesha mtoto kuna
uwezekano umezaa nao katika ulimwengu war oho, lakini kimwili hutapata watoto,
wala ndoa na kama ikiwepo itakuwa ni ndoa iliyo kwenye mashaka makubwa sana ni
ndoa ya moto
-
Kuwakwa sana na tamaa ya ngono ma mambo machafu
unapokuwa peke yako, lakini unapokuwa na mwenzi wako unakuwa huna hamu ya ngono
kabisa, na unaweza kupoteza nguvu, mwenzio akiwa mbali unatamani sana awepo
lakini akiwepo, unachukizwa naye bila sababu za msingi na unatamani asingekuwepo!
-
Pepo hawa wanaweza kuwapo ndani yako kwa muda
mrefu na usigundue tatizo, kama wapo ila dalili zake na majanga yote
niliyoelezea hapo juu, ufunuo wa juu kabisa kuwa wako nawe ni siku inkubi na
sakubi watakapo fanya shambulio la kimapenzi litakalokupa wakati mgumu sana hii
ndio dalili mbaya na ya juu zaidi ya kujidhihirisha kwao, na ukiifurahia watakutembelea tena na tena!
Kuna maswala mengi yanayoweza
kuonyesha utendaji wa pepo hawa lakini mengi yanapatikana kupitia watu
waliowahi kukutana na hali hizo na wakamua kuweka wazi. Sasa ni namna gani pepo
hawa wanapata nafasi za kupita na kuwasumbua wanadamu katika maisha yao tunaliangalia
hilo katika kipengele kifuatacho:-
Namna tunavyokaribisha pepo wa mahaba.
Inkubi na Sakubi pamoja na pepo
wote wa mahaba kama ilivyo kwa shetani hawatuwezi kibinadamu, kama umemuamini
Bwana Yesu na kumfanya kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, pepo wa mahaba
huondoka haraka au mara moja tu mtu anapookoka, lakini inkubi na sakubi
wanaweza kushambulia kutoka nje sio lazima wawe wamekupagaa, hata hivyo kama
ilivyo desturi ya pepo huwa kuna vitu vinawavutia kuja na kusababisha waweze
kutushambulia;-
Mathayo 12:43-45 “Pepo mchafu, amtokapo
mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu
husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa,
na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu
kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya
mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho
kibaya.”
Pepo hupata nafasi kama mioyo
yetu iko tupu, imefagiwa na kupambwa, kama hatutaruhusu Roho Mtakatifu kuwapo
katika mioyo yetu, kama hatutaruhusu maombi na maisha matakatifu kama
hatutaruhusu kujaa neno la Mungu na kama tutaruhuru uasi na ukiukwaji wa amri
za Mungu watapata nafasi ya kutushambilia lakini inkubi na sakubi huvutiwa
Zaidi na maswala yafuatayo:-
1. Tamaa ya raha ya zinaa na uasherati
Pepo hawa ni
pepo wa tamaa ya ngono na hivyo moja ya pambo lao kubwa wanalovutiwa nalo ni
tabia ya kutamani kupenda ngono na misisimko ya kingono isiyokuwa ya kawaida, kwa
kawaida iko haja ya kawaida ambayo mwili wa kibinadamu unahitaji lakini inapotokea
kuwa haja hiyo inazidi mipaka inakuwa dhambi, mfano kula sio tatizo lakini kula
kupita kawaida kwa ulafi ni dhambi, Hakuna shida wala tatizo kuwa na hamu ya
ngono ambayo Mungu ametujalia lakini kutimiza mahitaji hayo ya kingono kwa
kupiga punyeto, kujitia vidole, kutumia vifaaa vya kujitimizia raha ya kingono
kwa vifaa vya bandia, na kila aina ya maasi ya kingono hayo ni mapambo
yanayowapa pepo nafasi ya kuichezea miili yetu na kuitumia, wokovu haufanyi
kazi na uasi.
Kama unataka
kweli kuwa mbali na pepo hawa basi lazima uwe umekasirishwa na tabia mbaya za
kwako mwenyewe na kufanya maamuzi ya kutubu na kuacha viashiria ngono vya iana
zote ambavyo vitawavutia hawa pepo na hivyo unawajibika kwa uzembe wa kuwaruhusu
kukufikia na hata kukudhaklilisha na kukushambulia kupitia matendo yako, kwa
hiyo ni lazima ujiangalie moyo wako na kujipima katika mtindo wako wa maisha
sawa na neno la Mungu kama uko mlango ulifungua unapaswa kuufunga na kujiweka
huru kupitia jina la Yesu
Milango ambayo
inaweza kuruhusu pepo wa usiku inkubi na sakubi ni pamoja na
a.
Uzinzi na
Uasherati – kila tendo la kingono lisilo halali ikiwemo zinaa, zinaa na
ndugu, ushoga, usagaji, na mambo yote yanayofanana na tendo hilo yanafungua
mamlaka ya pepo hao kukufanyi lolote.
b.
Kupiga
punyeto – Punyeto ni mlango mzuri sana wa kuwaruhusu pepo wabaya wa usiku
hususani inkubi na sakubi kutuvamia, kwa sababu kupitia punyeto unafanya dhambi
dhidi ya mwili wako mwenyewe na kuutoa ushughulikiwe na pepo wabaya, hata hivyo
tendo la punyeto lenyewe linatawaliwa kwa kiwango kikubwa na pepo hawa wa
mahaba kutokana na tamaa inayokuwa imepandikizwa ndani yako na wao.
c.
Kuangalia
picha za ngono – Ni mlango mzuri sana unaotuharibu akili na kutoa kibali
cha kushughulikiwa na pepo wa usiku, picha na sinema za ngono zimeundwa maalumu
kufanya kazi sawasawa na utendaji wa pepo wa usiku inkubi na sakubi na hivyo
kile ambacho wangekupandikizia kinapandikizwa vema na sinema hizo na hivyo wao
kutengenezewa njia nzuri ya kukushughulikia na kutawala na kukudhoofisha na
kujiweka katika nafasi dhaifu ya kuupinga uovu huo unapokuja ki halisia, chochote
tunachoingiza akilini mwetu wakati wa mida ya kawaida kinaweza kutawala wakati
wa usiku na kuzalidha uovu ndani yetu ,
usikubali kuingiza uchafu katika ubongo wako pepo wa ngono wako karibu na kila
picha ya ngono.
Zaburi 101:3-4
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi
yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami. Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,
Lililo ovu sitalijua.”
d.
Kuwa na
hisia kali za kingono (Tamaa)
– Moja ya mambo ynayowavitia sana pepo
hawa inkubi na Sakubi ni pamoja na kuweko kwa hisia kali za kingono, uhitaji
wako mkubwa wa kingono na nguvu kubwa ya uhitaji wa kingono aliyonayo mtu
huwavuta pepo hawa na kuja kuweka jiwe la msingi, wana wanavutiwa na mtu mwenye
hisia kali za kingiono na wanataka kuja kumsaidia mtu mwenye hisia kali za
kingono ambazo hazijatoshelezwa au kutimiziwa mahitaji yake, hisia kali za
kimapenzi zinatumika kama sumaku ya kuwavutia maviumbe haya na kukuza uwepo wao
na uhitaji wao. Wito wa Mungu na mapenzi yake ni kila mmoja aishi maisha
matakatifu na kujihadhari na uasherati hata katiika hatua ya mawazo na
kujifunza kuiweza miili yetu katika nnjia ya utakatifu na heshima ona 1Wathesalonike 4:3-5 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu,
mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika
utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua
Mungu.”
e.
Mtu aliye
katika hali ya upweke – Inkubi na Sakubi pia wanapendelea au kuvutiwa na
mtu ambaye ana hisia kali lakini anayezungukwa na mazingira ya upweke huku
akiwa na uhitaji wa kingono, yaani ni kama mtu aliyepeke yake anayetamani mtu
Fulani atokee, wanamuwinda mtu wa namna hiyo mtu anayehitaji ngono anayetamani apate mwanaume au mwanamke wa
kushirikiana naye ngono, au aliye katika hali ya kusumbuka kwaajili ya ngono,
au aliyevunjika moyo, au upweke watu wa aina hii huwavutia viuomba hawa wa
kiroho kuja kumshambulia
f.
Watu
walioumizwa sana kihisia – watu waliumizwa mioyo kihisia wako katika nafasi
kubwa sana ya kuwavutia inkubi na sakubi, hususani watu wenye histiria ya
kupoitia majanga mazito kama kukataliwa kisaikolojia maumivu makali ya kihisia
na kujeruhiwa moyo kunaitwa (Trauma) yaani watu waliopita mateso, vitisho na
matukio ya kukataliwa na yenye kuwakandamiza kihisia, changamoto za
kisaikolojia zilizokosa majibu, hofu na mateso ya kiakili yaliyodumu kwa muda
mrefu, mawazo mabaya, tabia haribifu, au kuvutiwa sana na maswala ya kiroho,
watu wa namna hii wanaweza kutengeneza mazingira yenye nguvu za kuruhusu kuja
kwa viumbe hawa.
g.
Mazingira
yenye giza na yenye nguvu – Mazingira yenye giza na nguvu yanaweza pia
kutengeneza uwanja mzuri kwa inkubi na sakubi kuweza kuvamia, yaani mazingira
ambayo yana historia kali za kihisia kama vile nyumba zulizojengwa na kuwachwa
kwa muda mrefu, mapagala, Majengo ya zamani, au eneo linalohusika na matambiko,
au mawasiliano ya rohoni, yanaweza kuwavutia hawa pepo, au eneo lenye mabaki ya
kale na eneo lenye rutuba au uwanja
ambao unatumika kwa dua na maombi, au mazungumzo na viumbe wa kiroho eneo hilo
linaweza kuwa na mvuto mzuri kwa viumbe hao pia
h.
Watu
waliowahi kupambana na maswala ya rohoni – watu waliowahi kupambana na
ulimwengu wa kiroho wa mzizimu, roho, au watu wa rohoni mara nyingi wao wenyewe
wanakuwa ni mawindo makubwa ya inkubi na sakubi, madhara ya kirpoho yanayoachwa
na viumbe hivi vya rohoni yanaweza kuwa sababu ya viumbe vingine jirani navyo
kujihusisha, kwa hiyo ni muhimu kutambua na kupambana na uzoefu huo wa zamani
ili kujikinga na uvamizi na mashambulizi ya haya majamaa.
i.
Kuwaalika
kwa kujua au kwa kutokujua – Yako mazingira ambayi kway yanaweza kuwapoa
nafasi pepo hawa kufanya uvamizi, kupitia mawazo yako na matendo yako, hii
inaweza kutokea endapo mtu Fulani kwa kujua au kwa kutokujua anatamani viumbe
hao wakutane nae au kuzalisha nguvu zenye kutengeneza mazingira ya kuwavutia,
kwa hiyo ni muhimu wakati wote kuwa na dhamiri safi na mawazo masafi
Zaburi 19:14 “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate
kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.”
2. Uchungu na kutokusamehe – uchungu na
kutokusamehe unafunga kabisa mlango wa neema ya Mungu kwetu na hivyo
kutuondolea ulinzi na hivyo kila iana ya pepo anaweza kupata nafasi ya
kulivamia hekalu na maisha yako yakaharibikiwa Yesu alionya ya kuwa
kutokusamehe humweka mtu kifungoni
Mathayo 18:21-34 “Kisha
Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami
nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata
saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja
aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu
mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru
auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile
deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami
nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe
ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona
mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata, akamshika koo,akisema
Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie,
nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata
atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika
sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake
akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote,
uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi
nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata
atakapoilipa deni ile yote.”
Unapoacha
kusamehe unaachiwa kwa watesaji gerezani maana yake pepo wanapewa kibali cha
kukutesa kwa msingi huo ni lazima usamehe, ili kutoa mlango wa wewe kuwa huru
mbali na mashambulizi na mapepo yote wakiwepo pepo wa mahaba na sakubi na
inkubi maandiko yanasemaje linapokuja swala la mtu kuwa na uchungu na kupaswa
kusamehe ni kuhakikisha unaachia kabla jua halijachwa ona Waefeso 4:26-27 “Mwe na hasira, ila
msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe
Ibilisi nafasi.” Uchungu, hasira hali ya kutokusamehe inapaswa
kumalizwa mapema kabla jua halijachwa vinginevyo shetani atapata nafasi
wakiwemo pepo hawa hatari wa mahaba inkubi na sakubi.
3. Kufuata kawaida ya ulimwengu – Waefeso 2:1-3 “Nanyi
mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa
kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga,
roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi
tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili
na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.”
Ni jambo la
hatari sana kuishi kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, yaani kuishi maisha
ya kawaida unaweza kuwa uliokoka lakini ukawa huna hata haja ya kuendeleza hali
yako ya kiroho badala yake unaishi maisha ya kawaida sana unatumia muda mwingi
sana kwenye maswala ya kawaida na yasiyo ya kiroho, inaweza ikawa sio dhambi
lakini yanakunyima muda wa kujijenga na kujikuza kiroho au kukuza uhusiano wako
na Mungu, kumbuka kuwa tunajiweka katika mazingira magumu katika wakati wa
usiku akili zetu na miili yetu inapokuwa imechoka, huu ni wakati ambapo
tunategemea sana nguvu za roho zetu kutulinda dhidi ya uovu, kama hatujamjenga
mtu wa ndani yaani roho zetu na zikawa dhaifu na kama hatujampa Roho Mtakatifu
nafasi roho wabaya wanaweza kuifikia miili yetu na kufanya wayatakayo. Kwa
msingi huo ni muhimu kujiendeleza kiroho, wako watu ambao wanampenda Mungu
lakini hawaombi, hawasomi neno, hawasikilizi hata kwaya, wanaishi maisha ya
kawaida tu, hawana utumishi wa aina yoyote kanisani na wakati mwingine hata
hawahudhurii ibada yaani wanaishi kawaida hali kama hiyo inahatarisha ustawi
wako wa kuwa mtu wa rohoni na hivyo ibilisi na malaika zake wanaweza
kukukushambulia watakavyo kwa sababu wao wako kazini na hawana muda wa kupoteza
kosa lako moja tu wao wanajitengenezea ushindi.
4.
Msinyimane
– 1Wakorintho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa
kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume
wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe
haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana
amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda,
ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa
kutokuwa na kiasi kwenu.”
Moja ya kazi
kubwa sana ya pepo wa mahaba wakiwepo inkubi na sakubi ni pamoja na kuharibu
ndoa, wote tunajua kuwa moja ya lengo kubwa la pepo hawa kuchepusha, kupotosha
kuwaondoa watu katika kusudi na mpango wa Mungu, kuwafanya watu hawa waende
mbali kabisa na mpango wa Mungu, sasa jaribu kuwaza kuwa ninyi ni waamini
waaminifu na mnamcha Mungu lakini mnanyimana tendo la ndoa au mnakomoana katika
tendo hili kwa vyovyote vile kama Paulo mtume alivyosema ngono ni hitaji
mojawapo la muhimu la mwanadamu, na mpaka mtu anaoa au kuolewa moja ya kusudi
kuwa ni ili aweze kutimiziwa mahitaji yake ya kimwili, na sasa anakutana na
hali ya kukosa tendo hilo, jambo hili linafungua mlango wa tamaa ya zinaa,
linafungua mlango wa mawazo mabaya, linafungua mlango wa mafarakano, linafungua
mlango wa kuvunja agano la ndoa maana kila mmoja aliapa kuwa atampa mwenzi wake
haki yake,tendo la kunyimana linapoteza
umaana wa ndoa, nadhani umewahi kuwasikia wakristo wanaosema afadhali ndoa za
mitala, au afadhali wenzetu waislamu wanaona kama ndoa ya mke mmoja ambayo ndio
mpango wa Mungu unaonekana mpango huo kama ndio wa hovyo zaidi na hivyo
kuwafikisha watu kwenye hali ya kulidharau neno la Mungu, tendo la kunyimana
unyumba ukiacha tu kuwa linamchukiza Mungu lakini linampa shetani nafasi ya
kuharibu na pepo wa mahaba hufanya kazi hiyo lakini inkubi na sakubi wanapata
mlango wa kuidhalilisha miili yenu na kuongeza mpasuko mkubwa na uharibifu
mkubwa katika ndoa, pepo hawa pia hufanya usimamizi huu wa kunyimana ili
kuwachepusha kwenye neno la Mungu lililoagiza msinyimane na hivyo zinaa inaweza
kutokea, watu wengi wanajua kuwa ndoa ni agano na agano hili kabla ya talaka
linavunjwa na kukiukwa pale watu wanapoanza kunyimana. Kama ulimyima mwenzi
wako mpaka akatioka nje ya ndoa fahamu na kukumbuka kuwa kabla hujamlaumu wewe
ndio unawajibika kwa kuvunja agano:-
Malaki 2:14-16 “Lakini
ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya
wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako,
na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja
aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja
atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye
yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia
kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa
udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije
mkatenda kwa hiana.”
Kwa msigi huo
kama hakuna sababu za msingi zinazosababisha usimtimizie mwenzi wako haja zake
za kimwili basi ni vema kuhakikisha kuwa hatuendi na uchungu kitandani na
kuhakikisha kuwa wanandoa wanapeana huduma sahihi na toshelevu za kindoa ili
kutokumpa ibilisi nafasi kumbuka maneno yale ya mtume Paulo “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda,
ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa
kutokuwa na kiasi kwenu” ni kwambie shetani na mapepo yanapata
nafasi aidha kwa kusababisha mnyimane au kwa sababu wewe umeamua kumnyima
mwenzi wako na kutokujali hali yake ya kutaka kutimiza hitaji lake kupitia wewe.
5.
Hofu
na Mashaka – Kuwa na hofu na Mashaka katika maisha yako kunafungua mlango
wa pepo wabaya wakiwepo inkubi na sakubi na pepo wengine na pepo wa usiku au
pepo wa mahaba kushambulia maisha yako kwa kusudi la kuongezea hofu na mashaka
katika maisha yako, wanataka uwe na hofu, ukiondoa hofu na mashaka kwa kawaida
utakuwa mbali na kuonewa lakini ukiruhusu hofu na mashaka ukaogopa utaonewa Isaya 54:14 “Utathibitika
katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu,
kwa maana haitakukaribia.” Ukikubali kuogopa na ukajaza moyo wako
hofu na mashaka pepo hawa huja kuongezea hali hiyo ili kuchepusha Imani yako na
kuidhoofisha kwa kusudi la kuiba uhusiano wako na Mungu.
6.
Uchawi
na kutokutii au uasi – Uchawi na kutokutii au uasi katika maandiko vinawekwa
katika kiwango kimoja kwa sababu uchawi na kutikutii vyote vinahusisha uasi, au
kwenda kinyume na njia za Mungu, lakini kwa ujumla kujihusisha na unajimu,
kupiga ramli, kuangalia nyakati mbaya, kuwaendea wenye pepo wa utambuzi, na
aina zozote za uchawi hata mawasiliano na wafu ni maswala yanayoweza kuharibu
kabisa uhusiano wetu na Mungu
1Samuel 15:22-23 “Naye
Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa
na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia
kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni
kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye
amekukataa wewe usiwe mfalme.”
Mambo ya walawi 19:31 “Msiwaendee
wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi
BWANA, Mungu wenu”
Kumbukumbu 18:10-14 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake
kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati
mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga
mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa
maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo
Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.
Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na
kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.”
Tunaweza
tusijihusishe na maswala yaliyoidhinishwa hapo juu lakini kama hatuwatunzi vema
na kuwatendea haki watu tunaoishi nao, na kuwonea watoto, wenzi wetu na wote
wanaoishi katika nyumba zetu, na wote waliokaribu nasi yaani kutokuwa na amani
na watu wote kunaweza pia kufungua mlango kwa pepo wa usiku kutushambulia.
7.
Unyanyasaji
– Unyanyasaji ni moja ya mlango mzuri sana wa kuwaruhusu Pepo wabaya wa usiku
kutushughulikia, kwa kuwa pepo wenyewe ni wanyanyasaji, unaponyanyasa watu
unajiweka katika njia yao ya kukuingia, lakini pia unaiweka akili yako kuwa
chini ya mashambulizi ya pepo, kumbuka kuwa pepo wa usiku Sakubi na inkubi ni
wanyanyasaji kwa msingi huo ukiwa na tabia ya unyanyasaji unawapa nafasi ya
kukunyanyasa nawe usiku, mtu mnyanyasaji ni mtu asiyejiamini, uko unyanyasaji
wa aina nyingi sana, kunyanyasa mke, kunyanyasa mume, kunyanyasa wafanyakazi,
na unyanyasaji wa kijinsia, Unyanyasaji huu unahusisha tabia ya kuwaingilia
watoto wadogo kingono na vitendo vya aina hii huwaacha watoto walioingiliwa
kimwili katika hali ya aibu, hatia na msongo wa mawazo sawa kabisa na utendaji
wa pepo wa usiku Dini iliyo safi ni dini inayohusisha kujali “Caring” watu wanyanyasaji huwa
hawajali angalia
Yakobo 1:26-27 “Mtu
akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali
akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.Dini iliyo safi, isiyo na
taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika
dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”
Neno kuwatazama
kwa kiyunani ni episkeptomai yaani
hali ya kwenda kutafuta nafuu ya wengine caring
au go to see relieve. Hali ya kuhakikisha wengine wananufaika
kinyume cha hapo ni unyanyasaji, Pepo wa usiku huvutiwa sana na matukio ya upweke,
unyanyasaji, msongo wa mawazo, hatia, huzuni mtindo wao wa kimateso unafanana
na mwanadamu anayefanya unyanyasaji hivyo kufanya unyanyasaji kunawapa wao
mlango wa kuja kuchochea jambo hilo na kukunyanyasa. Swala hili pia linahusisha
kujeruhiana mioyo kimsingi kila aina ya udhaifu pepo hawa huititumia kama
nafasi ya kufanya wayatakayo.
8.
Kuchokana
– hii inahusiana zaidi na wana ndoa watu wanapoishi muda mrefu sana katika
ndoa hufikia wakati wakazoeana sana na kama ndoa yao ilipita katika majaribu
mbalimbali hasa ya kugombana nasfi zao
zinachokana na hivyo wanandoa hutamani
kujaribu mfumo mpya wa kujipatia raha ya nafsi kwa mtindo huu unaweza kufikia
ngazi ya kuamua kuchepuka, jambo hili nalo linaweza kufungua mlango wa Pepo
hawa wa usiku kukuvamia mawazo yako yatakuwa yanatamani kujaribu jambo jipya, penzi
jipya changamoto mpya mwanaume mpya au mwanamke mpya na kadhalika hali na mna hii inapendwa na pepo hao.
9.
Miungu
ya kifamilia – Miungu ya kifamilia yaani Mizimu nayo inamchango mkubwa sana
katika kusababisha uvamizi wa pepo wakiwepo pepo wa usiku, miungu ya kifamilia
ina usumbufu mkubwa sana miungu hii au mizimu ni miungu ya mababa iliyokuwa ikimilikiwa
na viongozi wa ukoo fulani zamani ambao hufanya mawasiliano kwa njia ya ndoto
na ramli au maono na kupanda kwa pepo ni pepo wa ngazi ya juu miongoni mwa pepo
ambao hujihusisha na kutoa taarifa kuhusu sababu ya janga fulani, au ugonjwa,
kifo, na majanga mengineyo na wakati mwingine hutoa maelekezo yanayoweza kusaidia
kuleta ufumbuzi wa aina fulani katika familia, Pepo hawa kama wako kwenye ukoo
basi wataweza kurithiwa kutoka kizazi hata kizazi, Mjomba wa Yakobo Labani
alikuwa na miungu na Raheli alipokuwa anaondoka na Yakobo mumewe aliiba miungu
ya baba yake ona
Mwanzo 31:19 “Basi
Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba
vinyago vya babaye.”
Watoto waliozaliwa
na Raheli ni Yusufu na Benjamini, tunafahamu kuwa Yusufu alikuwa mcha Mungu
lakini siku za mbeleni watoto wa Yusufu yaani Eframu na Manase, hasa Efraimu
alijihusisha sana na kuabudu sanamu kuliko kabila zote katika Israel Hosea 4:17 “Efraimu
amejiungamanisha na sanamu; mwache.”
Athari
za kuabudu miungu hata pamoja na kuwa ilitekeketezwa na Yakobo lakini ilikuja
kujitokeza katika wana wa Yusufu miaka mingi baadaye hii ni athari ya miungu ya
kifamilia roho hizi zinaweza kuwafuatilia hasa wale ambao watakuja kuwa watu wa
rohoni na kuwasumbua na kuwatesa ziko familia nyingine shangazi alikuwa tasa na
baadhi ya watoto wa ndugu zake wanakuja kuwa tasa hizi ni dalili zinazoashiria
kuwa huko nyuma kuna mtu alikuwa na roho wachafu aliokuwa akiwafuga kwa niaba
ya familia sasa Pepo wa mahaba wanaweza pia kuingia na kushambulia kwa njia hii
hii ya kufuata hali kiroho ya familia na
ndio maana utaweza kuona kuwa kuna familia nyingine wanaathiriwa na maswala
kadhaa wa kadhaa yanayofanania kutoka mababu mpaka mababu wakati unapotafuta ukombozi
ni muhimu kuhakikisha kuwa unakata kitovu za kiroho cha familia yako kutoka
pande zote upande wa baba na mama babu na bibi wa pande zote na kujitangaza
kuwa huru huku ni kukata kitovu kwa
jinsi ya rohoni yaani kuvunja makataba wa mambo mabaya ya kifamilia na kuruhusu
yale mazuri tu.
Ezekiel 16:2-4 “Mwanadamu,
uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu
hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori
alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa
kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji
usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.”
Kitovu ndicho
kinachohusika kuunganisha mtoto tumboni mwa mama yake na kuumbika na kumkuza
muunganiko huo hukatwa mara baada ya mtoto kuzaliwa huu ni muunganiko wa
kimwili, lakini uko muunganiko wa kiroho ambao nao unatakiwa kushughulikiwa ili
roho za kifamilia zisiweze kukuandama na kukuonea na kukutesa wakiwepo pepo
hawa wa usiku inkubi na sakubi kama waliwahi kuwa na umiliki dhidi ya mtu
katika familia yenu, zamani. Kata kwa kutumia maombi na kukataa mabaya na
kukubali mazuri.
10. Kujihusisha na mambo ya kiroho au nguvu za
giza – kujiingiza katika maswala ya kufanya mambo ya kiroho ua ya kichawi
pasipokuwa na ufahamu wa kutosha kunaweza kukaribisha mambo yasoyohitajika
katika maisha yako, mfano unafanya tambiko au jaribio la kuwasiliana na ulimwengu
war oho bila kufuata maelekezo kwa usahihi au bila kuchukua tahadhari, kuna
uwezekano mkubwa ukafungua mlango wa inkubi na sakubi, kwa hiyo ni muhimu
kufuata maelekezo ya kiroho kwa tahadhari, au kutafuta muongozo kutoka kwa watu
wenye uzoefu, ili kukulinda au kujilinda na roho wasiotakiwa na ukajikuta
unanaswa nao. Pepo hawa pia wanaweza kutumwa kwa nguvu za giza za kichawi au za
kiganga kwa kusudi la kumdhuru mtu au kumuharibia, kwa sababu ya wivu wa mfumo
wa maisha yako.
11. Vita vya kiroho – kunaweza kukawa na
sababu nyingi lakini kwa wale wenye kiwango cha utumishi ikitokea unashambuliwa
na pepo wa usiku ufahamu kuwa ni vita vya kiroho, Pepo hawa kwa kawaida
wanatumia nafasi yoyote ile ya kutaka kuathiri
na hivyo inapotokea umelala ni lazima ukumbuke kuwa tunavita, vita vya
kiroho tulivyo navyo katika maisha yetu ya kiola siku wakati mwingine
vinadhoofisha hali yetu ya Rohoni na ndio maana wakati mwingine wanaweza kupata
nafasi ya kushambulia ili walete uharibifu wa kiroho ikiwa ni pamoja na
kukuingizia roho ya uzinzi na ndio maana wakati mwingine unaweza kuona sio
jambo la kushangaza kuona watoaji pepo waombaji
manabii na wainjilisti watu ambao wako Mstari wa mbele katika vita vya
kiroho na huduma unashangaa wanaingiziwa tamaa kubwa Zaidi ya kingono n ahata kuathiriwa Zaidi kwa
sababu ya vita za kiroho kusudi kubwa ni ili wakataliwe na kwenda motoni.
Mathayo 7:21-23. “Si
kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali
ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku
ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa
pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri,
Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
Kila muhubiri wa
injili na watu wote wanaojihusisha na maswala ya kuimarisha wengine kiroho wako
katika ngazi ya juu Zaidi ya kushambuliwa na pepo wa ngazi ya juu Zaidi, kwa
msingi huo kwaajili ya ulinzi lazima kanisa lijifunze kuomba na kuwaombea watu
walioko katika ngazi za utumishi, lakini sio hivyo tu nao hawana budi
kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutokujiachia lakini waweke bidi ya kutokufanya
kazi ya kuwahubiri wengine kisha wao wakawa wakukataliwa
1Wakorintho 9:25-27 “Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote;
basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji
isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana
ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na
kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa
kukataliwa.”
Wimbo uliobora 1:5-6 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za
Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze
kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu
walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba
langu mwenyewe sikulilinda.”
Ni wajibu wa
kila mkristo na wakristo, watumishi kuhakikisha kuwa wanajilinda wanapolinda
hali ya kiroho ya wengine wasisahau kulinda na mioyo yao wenyewe ili
wasishambuliwe na mapepo haya ya usiku na aina nyingine za pepo ili wao wawe
mstari wa mbele katika kuwasaidia.
12.
Dhambi
yoyote isiyotubiwa kwa haraka – Pepo hawa wanaweza kuitumia nafasi yoyote
ya dhambi isiyotubiwa kukuadhibu, maandiko yanasema wala msimpe ibilisi nafasi Waefeso 4:27 “wala msimpe Ibilisi nafasi.”
Kumbuka kuwa kazi za shetani ni kuharibu kuchinja na kuua tendo la kumpa
ibilisi nafasi linaweza kuleta majuto makubwa sana katika maisha yetu, tunaweza
kupata shambulizi la ghafla, haichukui muda mrefu kwa Inbubi na sakubi
kusababisha majuto na huzuni katika maisha yako kwa msingi huo tunajua kuwa
kila mkristo aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, yaani hadumu katika dhambi,
lakini ukikosea na ukatenda kosa moja tu lisilotubiwa hata hasira na uchungu wa
muda mrefu unaweza kuleta haribiko kubwa sana katika maisha yetu. Hivyi ukihisi
hauko sawa hakikisha kuwa unatubu haraka na usilale na dhambi ambayo hujaitubia
hasa wakati wa usiku, hakikisha unatubu, unaishi maisha matakatifu, unafunga na
kumuomba Mungu akusaidia na kukuokoa na pepo hawa wa mahaba kwa maelekezo
mengine tuzingatie kipengele kinachofuata jinsi ya kuwashinda pepo wa mahaba.
Jinsi ya kuwashinda Pepo wa Mahaba.
Ni muhimu kufahamu na kukumbuka
kwamba moja ya funguo muhimu sana ya kufunguliwa kutoka katika changamoto
yoyote ile ya adui kwanza ni maarifa au ujuzi Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa
kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe,
usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami
nitawasahau watoto wako.”
2Wakorintho 2:11 “Shetani asije akapata
kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Kama tumepata
uelewa wa kutosha na ufahamu wa kutosha
kuhusu utendaji wa pepo hawa na jinsi adui yetu shetani anavyotenda kazi katika
kiwango hicho sasa tunaweza kutumia mbinu za ushindi ambazo maandiko yanatupa
ili pepo hawa wawe mbali nasi na tukaishi kwa ushindi, furaha na amani
Lengo kuu la inkubi na sakubi ni
kutuchepusha kutoka katika mapenzi ya Mungu, kutuumiza na kutuletea fadhaa, lakini
hawa huacha mimba au mbegu ambayo wanaamini itaona katika akili zako na mawazo
yako, kwa msingi huo lazima kuhakikisha kuwa tunavunja mkataba nao kwa jina la
Yesu na kung’oa kabisa mbegu zao na mimba zao kuzitoa na kuua kila kitu kibaya
wanachokikusudia lazima kuhakikisha kuwa kila aina ya kazi za kipepo ambazo
zimeainishwa kufanywa ndani yetu zinaharibiwa na kusambaratishwa na kuondolewa
na kuuawa kabisa katika maisha yetu, na kuhakikisha kuwa tunakuwa vizuri kiroho
ili hayo yatendeke ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:-
1.
Kama
hujaokoka hakikisha ya kuwa unamkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozo wa maisha
yako, hakikisha kuwa umesamehewa dhambi zako na unaanzisha uhusiano mwema
na Mungu naye atakuhamisha katika nguvu za giza na kukuingiza katika ufalme wa
mwana wa pendo lake jambo litakaloleta usalama katika maisha yako ya kimwili na
kiroho ona Waefeso 2:1-6 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata
mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu,
tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa
hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa
mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya
makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho,
katika Kristo Yesu;”
2.
Hakikisha
unafunga milango yote ya dhambi ambazo pepo hawa huzitumia kama nafasi ya
kupita na kutushambulia - baada ya
kuwa umeokolewa usiruhusu mlango wa dhambi hata kwenye mawazo dhambi
zishughulikiwe kwenye nia na mawazo hata kabla hayajakomaa na kuzaaa dhambi na
dhambi kuzaa mauti kila mtu aliyeokolewa
anapaswa kujua wazi kanisa kuwa usalama wake ni kukaa ndani ya mji wa
makimbilio ambao ni Yesu nje ya Kristo utaumizwa, kushuka kiwango cha kiroho
kunakuweka katika hatari ya kuumizwa usitende dhambi tena Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta
ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena,
lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”
3.
Watangazie
pepo wote na mapepo yote ya mahaba na inkubi na sakubi kuwa unakataa kazi zao
katika maisha yako na huwezi kuwa na ushirika na mashetani- kama walikuvamia au kukushambulia au wako ndani yako kwamba
kazi zao zinavunjwa na kuharibiwa na kusambaratishwa katika jina la Yesu, kila
mbegu waliyoipanda ndani yako na kusababisha madhara iharibiwe na wakome kabisa
kukufuatilia tumia jina la Yesu na damu yake kuharibu roho na kujikinga, endapo
wamekutokea mara moja anza kushughulika nao mara moja kabla hawajakurudia tena
na tena, usikubali roho hawa wakutawale bila kuwakatalia kwa nguvu na kuwaamuru
kuacha mambo yao katika jina la Yesu. Kama hutafanya dhambi tena na
kuwafungulia mlango basi hawatapata nafasi ya kukushambulia tena
4.
Hakikisha
kuwa unamuomba Mungu na kuwakemea kabla hujalala na kama utaota ndoto zao
tena unapoamka anza mara moja na usiruhusu mbegu zao kuota katika maisha yako,
kumbuka kutamka yale usiyoyataka kwa sababu mauti na uzima uko katika uweza wa
ulimi wako, kuitamka kuna nguvu kubwa sana maneno utakayoyasema yatakupa uzima
na kuua kila kitu kilichopandwa na usijaribu kuikumbuka ndoto ile hata kama
ilikuwa na mvuto kiasi gani. Angusha mawazo yote mabaya kwa jina la Yesu!. Mithali 18:21 “Mauti
na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
5.
Hakikisha
ya kuwa unajitakasa na kujiweka wakfu, na kuharibu kila roho chafu iliyopata
nafasi katika maisha yako, na usikubali kujihusisha tena na matendo yoyote yasiyo
ya kiungu, na ikitokea umekosea hakikisha ya kuwa unatubu haraka, haimaanishi
kuwa wewe ni mkamilifu wala hakuna mtu mkamilifu lakini kumbuka kuwa kila aina
ya dhambi na tendo lolote lisilotokana na imani lazima lishughulikiwe kwa
kiwango cha juu, hii lazima iwe hivyo hawa wakati unashughulika kujikomboa
kutoka kwa pepo hawa. Wakati mwingine husisha kufunga na kuomba lakini
hakikisha unajiokoa na kila ushawishi, wa aina yoyote wenye uhusiano na maswala
ya ngono na dhambi nyinginezo.
6.
Kumbuka
kila udhaifu na uovu ndani yako unawaalika hawa pepo kukushambulia, lazima
ujifunze na kuwa na ufahamu kuwa pepo hawa pia wanaweza kukushambulia kwa njia
ya zinaa, hivyo kila unapofanya zinaa uwe na uelewa kuwa unajiungamaisha nao,
pia pepo hawa wanapofanya ngono na wewe ni kama unakuwa mwili mmoja nao.hivyo
usikubali kuchepushwa kifikra na majini haya
7.
Kumbuka
pepo hawa ni pepo wa tamaa mbaya na tamaa yao huwa sio ya kawaida na
nitamaa isiyo ya kidunia kwa hiyo huwezi kusema kuwa hutajaribiwa tena
utajaribiwa kila mmoja hujaribiwa na shetani katika tamaa mbalimbali Shetani yeye
ni mungu wa dunia hii atatujaribu tu kwa kusudi la kudhoofisha roho zetu hivyo
kumbuka kuishi maisha matakatifu na usikubali kulegea uwe mwenye nguvu.
8.
Omba
kwa kutumia zaburi za ukombozi kila siku tumia Zaburi 9, 31, 38, 39, 68, na 46 zaburi
hizi zitaimarisha misuli yako ya kiroho utakayoitumia kuvunja daraja la uovu na
kupandisha Imani huku ukiomba dua za kushughulikiwa kwa adui zako wakiwepo pepo
hawa, katika maisha yetu ni Imani yangu kwamba pamoja na maombezi utakuwa huru
kutoka katika mashambulizi ya roho hawa wabaya
9. Waone watumishi wa Mungu – watumishi wa Mungu wenye uzoefu wa kukemea pepo hawa na weka ahadi ya kupata maombezi kwa kusudi la kufunguliwa, tubu, omba, kemea, funga, jitoe kwa Mungu, ishi maisha ya kumpendeza Mungu utaelewa kwanini Mungu anatoa wito wa kila mmoja wetu kuishi maisha matakatifu na kuwa makini au kukesha kwaajili ya umakini dhidi ya adui, Mungu ni mwingi wa rehema atafanya.
Endapo utakuwa umesumbuliwa na pepo hawa na wamesababisha madhara kadhaa katika mwili, nasfi na roho yako usisite kunitafuta kwa namba zangu za Whatsapp nitakusaidia, nitakupa maelekezo ya kufanya, kama ni wewe na mkeo msiogopa nitawapa maelekezo hukohuko mliko na mtakuwa huru Mungu ni mwema kwa sababu kwa kila jaribu ameweka na mlango wa kutokea!
Na. Rev. Innocent Mkombozi Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Whats’app +255 718 99 07 96