Andiko: 2 Timotheo 4:16-18
“16. Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu,
bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17. Lakini
Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe
utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika
kinywa cha simba. 18. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata
nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina”
Kuokolewa katika kinywa cha Simba
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa Nyakati
za kanisa la kwanza wakristo walipitia vipindi mbalimbali vya Mateso na
kulikuwa na aina kuu mbili za maadui, walikuweko maadui wa nje wa kanisa na wa
ndani, wote walikuwa ni hatari sana, katika mwaka wa 54-68 baada ya Kristo Mateso ya Kanisa yaliongezeka sana na ndugu
wengi katika Kristo waliuawa, kwani mfalme katili zaidi kuliko wote alitawala
aliyejulikana kama “NERO CLAUDIUS” wakati
huu ulikuwa wakati mgumu sana na hasa kwa viongozi wa Kanisa na washirika pia,
Paulo mtume wakati huu aliandika waraka wake wa mwisho ili kumtia moyo Timotheo
kuendelea kusimamia kanisa la Mungu bila kuogopa Mateso.
Licha ya Paulo mtume kumtia moyo
Timotheo lakini vilevile alijitia Moyo yeye mwenyewe ingawa wakati huu
alifahamu kuwa atakufa na kuwa huduma yake ilikuwa imefika mwisho, lakini
aliandika waraka huu akiwa kifungoni Rumi na mtawala Nero akiwa hataki kabisa
kusikia Injili ikihubiriwa, lakini hata wakristo na ndugu waliokuwa pamoja na
Mtume Paulo walikimbia na hakuna mtu alitaka kusimama upande wake hivyo wakati
huu Paulo alivunjika moyo na kukata tamaa lakini katika mistari hii hapo juu
kuna mambo Muhimu ya kujifunza kutoka kwake
·
Lakini Bwana alisimama Pamoja nami
·
Kuokolewa katika kinywa cha Simba
·
Kuokolewa na kila neno baya.
Lakini Bwana alisimama Pamoja nani
Paulo ingawa alikuwa anajua kuwa
mwisho wake umekaribia na kuwa sasa anamiminwa "2Timotheo 4:6-7" hakutaka Timotheo akate tamaa
yeye alikuwa na ujuzi kamili ya kuwa Bwana angesimama pamoja naye, Mungu
kusimama pamoja naye halikuwa jambo geni katika maisha ya huduma yake, Mara
kadhaa kila alipokutana na jambo gumu hata kukaribia kutaka kufa Yesu alikuwa
Pamoja naye, Neno KUWA PAMOJA, AU KUWA
KARIBU kwa Kiyunani ni “PARISTEMI”
kiingereza chake place beside, put at disposal, to present, to stand before,
to provide, or come to aid or present offer
na standing near, tafasiri rahisi ya
Kiswahili ni “KUWEPO KWA KUSUDI LA
KUSAIDIA” Neno kama hilo limetumika mara kadhaa katika huduma ya Paulo
Matendo 23:11 “Usiku ule
Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama
ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo
Rumi nako.”
Matendo 27:23 - 25 “23.
Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye
ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,
24. akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena,
tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. 25. Basi, wanaume,
changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama
nilivyoambiwa.
Ni kawaida ya Mungu kuwepo karibu
nasi na kutoa msaada pale tunapohitaji msaada wake ama pale watu wengine
wanapokuwa wameshindwa kutoa msaada, Inaonekana wazi kuwa alipokuwa Gerezani
Bwana alimtia nguvu, Mungu ataendelea kututia nguvu mpaka dakika ya mwisho
Kuokolewa katika kinywa cha Simba
Paulo mtume anazungumza jambo
lingine lililokuwa likiwakabili watu wa nyakati za Kanisa la kwanza na Bwana
pia alimuokoa nalo na hii ilikuwa ni kuokolewa katika kinywa cha samba, Nyakati
za Kanisa la kwanza wakati wa mateso kulikuwa na samba wa aina tatu waliokuwa
wakilisumbua kanisa
·
Simba wa
kawaida wanyama – Hawa walikuwa wakitumika kuwatesa wakristo kila mtu
aliyesimama kuihubiri injili na kumkiri Yesu kuwa ni Bwana kama akikamatwa
auwakikamatwa walitupwa viwanjani na kufunguliwa simba wenye njaa na kuwatafuna
wakristo, watu wengi katika maombi yao waliomba waokolewa na simba hao, huenda
Paulo mtume pia alimuomba Mungu akaokolewe na simba wakristo wengi waliomba
muujiza utokee kama Daniel lakini walitafunwa hivyo hofu kubwa iliingia
·
Simba
aliwakilisha mtawala wa Rumi – Nero Claudio alikuwa ni mtawala katili
aliyeuawa wakristo wengi bila Huruma na hivyo wakristo wengi walimuogopa na
walitumia jina simba pia kama lugha ya mficho dhidi ya mtawala katili
·
Simba aliwakilisha
Shetani - katika wakati huu kwa
kweli shetani alikuwa amekasirika kama simba akipania kabisa kuisambaratisha
injili kwa kulisambaratisha kanisa sura ya shetani ilionekana wazi kupitia Nero
na simba halisi waliokuwa wakitumiwa kama njia ya mateso 1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na
kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” Kukesha ni kuomba Yesu alisema
Ombeni ili msije mkaingia majaribuni
Kuokolewa na kila neno baya
Ni muhimu kufahamu kuwa mitume kamwe hawakuwa wanaogopa kufa lakini
walikuwa wanaogopa kusalitiwa na watu wa baya ndani ya injili “deliver me from every evil work” Neno baya au evil katika kiyunani
ni “PONEROS” ambalo kiingereza chake ni “The
negative moral quality of a person or action opposed to God and his goodness”
Paulo alijiombea kuwa asije akamkosea Mungu akapoteza Ufalme wa mbinguni, Paulo
alijiombea kumaliza vizuri mwendo wake, kuvipiga vita vilivyo vizuri vya imani,
alijiombea asinenwe vibaya asichafuke kwaajili ya injili, Mungu na awe karibu
na kila mmoja wetu na kutupa msaada na kutuokoa na kinywa cha simba na
kutuokoka na kila neno baya.
Na. Rev.
Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima