Adniko la Msingi: Zaburi
27:13. “Naamini
ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai”
Utangulizi:
Zaburi ya 27 ni wazi kabisa kuwa
ni zaburi ya Daudi, Zaburi hii ina mambo mengi sana ya kutafakari, Muda hauwezi
kutosha kutafakari mambo yote, lakini leo nataka tutafakari tumaini kuu la
ajabu alilokuwa nalo Daudi, kuhusu ndoto yake na ahadi za Mungu kwake, Haikuwa
wazi kabisa kuwa Daudi hapa alikuwa anapigana vita ya aina gani, au bwana
alikuwa amempa ushindi wa namna gani ama bado adui walikuwa wakimtishia na
ulifikia wakati akaogopa lakini bado
alisalia na tumaini moja tu kwamba yeye anaamini kuwa atauona wema wa Bwana
katika nchi ya walio hai! Ni kitu gani kinampa Daudi moyo wa imani hii
1. Mstari
1-3
Alikuwa na ujuzi kuwa Bwana ni Nuru yake. Kwamba hakuna giza mbele kama
unamtumainia Mungu, hofu yote inaondoka na unaweza kuiona future ( kuwa na
Maisha mazuri na ya furaha) hata kama kuna kila aina ya hila, wazushi, waongo,
watenda mabaya, watesi, adui, majeshi ya maadui, hivi vyote haviwezi kumtisha Daudi
kwa sababu Bwana ni Nuru yake, mtu asiye na Mungu yumo gizani, ataishi maisha
ya hofu kuu sana kwa sababu.
·
Watenda mabaya, wenye dhambi, waovu, wicked or
evil doer
·
Watesi, waonezi, wasengenyaji, wanyanyasaji
·
Adui, foes, enemies, wapinzani, wasiotaka
ufanikiwe
·
Jeshi, wanaopigana nao kimwili na kiroho,
kisaikolojia, kiakili na vyovyote vile
Daudi alisema
hawaogopi hao kabisa kwa sababu Bwana ni ngome ya uzima wake, Huu ulikuwa ni
uthibitisho ulio dhahiri kuwa Daudi alidumisha uhusiano wake na Mungu, mtu
yeyote yule atakayedumisha uhusiano wake na Mungu hawezi kutembea gizani, hawawezi
kupoteza tumaini hata kama wataogopa watajitia moyo, na Mungu kwa hakika
atawapigania na kuwalinda hakuna adui anaweza kufanikiwa kwako kama ilivyokuwa
kwa Daudi ndivyo itakavyokuwa kwa kila anayemtanguliza Mungu mbele
2. Mstari
4-5 Daudi anaeleza sababu kubwa ya
kumtegemea Mungu ni kwamba pia akipewa uhai na kulindwa na Mungu atautumia uhai
huo kukaa nyumbani mwa Bwana, ana kiu na shauku ya kutaka kuendelea kumuabudu
Mungu, ni kama anaweka Nadhiri kwa Mungu mradi Bwana atanisitiri siku ya Mabaya
na kuniinua, basi katika maisha yangu nitamuabudu, nitamtafakari, hekaluni
mwake nitamuimbia, Daudi aliongeza aina nyingine ya Mapito na maombi aliyotaka
mungu amtendee lakini kubwa zaidi anahitimisha kwa imani kuwa
3. Anaamini
kuwa atauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai, katika eneo hili Daudi
alimuomba Mungu Mstari 12, asimtie
katika nia ya adui zake, nia ya adui zake ni kumuangusha ni kuona kuwa
hafanikiwi, ni kutoa ushahidi wa uongo na maneno ya Jeuri sana, Lakini Daudi
anaamini atauona wema wa Bwana katika inchi ya walio hai
Mstari 13 jambo
gani kubwa tunajifunza, hapa Daudi alielewa wazi kuwa kuna maisha baada ya
kufa, alijua kuna kuishi milele, alijua kuna kwenda Mbinguni, lakini
hakufurahia kuishi kwa shida Duniani, hapa alimuamini Mungu kuwa hatamuacha afe
bila kumuonyesha mema katika nchi ya walio hai yaani hapa Duniani,
Kuingia mbinguni
sawa kupo, kula vizuri mbinguni sawa kupo, magari ya farasi mbinguni sawa yapo,
maisha ya matanuzi huko mbinguni sawa yapo lakini Daudi aliomba auone wema wa
Mungu hapa Duniani kwenye nchi ya walio hai, kuna nchi ya wafu sawa, lakini
kabla ya kwenda huko je nisionje mema ? kuna kufaulu kule mbinguni sawa, lakini
ndo nifeli na Duniani, kuna majumba mbiguni sawa lakini ndo niishi katika
kijinyumba cha nyasi Duniani? Kuna magari ya farasi za moto mbinguni sawa
lakini je hapa duniani nisiendeshe hata toyo?, kuna hali ya hewa nzuri Mbinguni
sawa lakini ndio nisipigwe hata na kiyoyozi duniani Daudi alimuomba Mungu
kwamba ni lazima ufikie wakati vita vimalizike, mapambano yaishe, awe na wakati
wa starehe, afanye kazi ya kuabudu
ndugu
ulivyopambana duniani inatosha sasa mwambie Mungu akufurahishe akuonyeshe wema
wake sasa, lazima ufikie ndoto zako na kuepushwa na kila aina ya mabaya ya
dunia hii na Mungu atakupa kustarehe Hatimaye daudi alistarehe
2Samuel 7:1-2 “1. Ikawa, mfalme alipokuwa
akikaa katika nyumba yake, hapo Bwana alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake
waliomzunguka pande zote, 2. mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa,
mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya
mapazia.
Uko wakati wa
Mapambano lakini pia uko wakati wa kustarehe Mungu na akufanikishe katika vita
vyako na pia akujaalie wakati wa Kustarehe kama ilivyokuwa kwa Daudi
Naamini ya kuwa
nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai
Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni