Mstari wa Msingi: Isaya 53:1 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
Kware kama wanavyoonekana Pichani ni ndege watamu sana na wenye afya ya ajabu
Utangulizi:
Neno mkono linapotumika katika
maandiko humaanisha utendaji au uweza, Na tunapoona neno Mkono wa Mungu moja
kwa moja humaanisha uweza na utendaji wa Mungu, yako mambo kadhaa katika maisha
yetu hayawezi kufanikiwa kama mkono wa Mungu hautakuwa juu yako ama kuwa pamoja
nawe, Katika maandiko tunamuona Naomi akilia akiamini kuwa alipatwa na mikasa
mbalimbali mibaya kwa sababu Bwana ameondoa mkono wake juu yake
(Ruthu 1:11-13) “Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee;
kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu,
hata wawe waume zenu? Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni
mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume
hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima?
Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko
kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu”.
kwa msingi huo Nyakati za Biblia watu wengi
waliofanikiwa walifahamu kuwa mkono wa Bwana uko pamoja nao, Hakuwezi kuwa na
mafanikio ya aina yoyote kama Mkono wa Bwana ukitupungukia, lakini uko ushindi
mkubwa sana kama Mungu akiunyoosha mkono wake kutenda jambo.
Uweza wa mkono wa Bwana
·
Mkono wa Mungu ukinyoosha kila kilicho kigumu
kinashughulikiwa Kutoka 3:19-20
Biblia inasema hivi “19. Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa
mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu. Nami
nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya
kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.”
·
Mkono wa Bwana ukinyooshwa hakuna jambo gumu la
kumshinda Hesabu 11:4-15, 18-23, 31-32.
“4. Kisha
mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao
wakalia tena, wakasema, N'nani atakayetupa nyama tule? 5. Twakumbuka samaki
tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu,
na vitunguu saumu; 6. lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote;
hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. 7. Na hiyo mana ilikuwa mfano
wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola. 8.
Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au
kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa nyunguni, na kuandaa mikate; na tamu
yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya. 9. Umande ulipoyaangukia marago wakati
wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao. 10. Basi Musa akawasikia watu wakilia
katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana
zikawaka sana; Musa naye akakasirika. 11. Musa akamwambia Bwana, Mbona
umenitenda uovu mimi mtumishi wako? Kwa nini sikupata neema machoni pako, hata
ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? 12. Je! Ni mimi niliyewatungisha
mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya,
wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye,
uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? 13. Nipate wapi nyama ya kuwapa watu
hawa wote? Kwani wanililia, wakisema Tupe nyama, tupate kula. 14. Mimi siwezi
kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa
kunishinda. 15. Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba
nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu.”
“18. Kisha
uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama;
kwa maana mmelia masikioni mwa Bwana, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule?
Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama,
nanyi mtakula. 19. Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala
siku kumi, wala siku ishirini; 20. lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata
hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa
sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka
Misri kwa maana gani? 21. Musa akasema, Watu hawa ambao mimi ni kati yao, ni
watu sita mia elfu waendao kwa miguu; nawe umesema, Nitawapa nyama, ili wale
muda wa mwezi mzima. 22. Je! Makundi ya kondoo na ng'ombe yatachinjwa kwa ajili
yao, ili kuwatosha? Au samaki wote wa baharini watakusanywa pamoja kwa ajili
yao, ili kuwatosha? 23. Bwana akamwambia Musa, Je! Mkono wa Bwana umepungua
urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.”
“31. Kisha
upepo ukavuma kutoka kwa Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao
ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande
huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao
wakafikilia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi. 32. Watu wakaondoka
mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao
kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi;
nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote.”
Dhiraa mbili (2 Cubic )ni sawa na Futi Tatu kwenda juu au
mita moja, na mwendo wa siku nzima ni sawa na KM.
Siri ya Mkono wa Bwana
·
Isaya anauliza Ni nani aliyesadiki Habari
tuliyoileta na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Kisha isaya anaeleza habari za
Yesu Kristo na mateso yake ambayo yameleta ukombozi mkuu kwa wanadamu
·
Ni wazi kuwa Biblia inapozungumzia juu ya mkono
wa Bwana inaeleza siri iliyo wazi kuwa Yesu ndio mkono wa Bwana ni wazi kuwa
ukiiamini injili, Habari njema na kuiamini kazi iliyofanyika msalabani kwamba
ni kwaajili yetu, na kuwa Yesu ametunukiwa jina kuu kuliko yote nay a kuwa
tukiliitia jina lake tunaokolewa
·
Hakuna jambo litakalokuwa Gumu kwetu, hakuna
jambo linaloshindikana Mkono wa Bwana utafunuliwa kwako tu, mweke Yesu mbele,
kubali kazi zake usimkatae Yesu utauona uwezo wake, Musa alilia alikata tamaa
wanataka Nyama, nitoe wapi nyama Kama nimepata fadhili machoni pako inatosha
Heri nife, inawezekana umefikia pointi ngumu sana katika maisha yako, kwamba
sasa Mungu uko wapi, kwanini haya yanatokea, heri uniuwe kabala ya aibu hii,
yatosha baba lakini nakuthibitishia leo kuwa Mkoo wa Bwana haujapunguka urefu
wake
·
Yeye alisema niite nami nitakuitika na
kukuonyesha Mambo makubwa na Magumu usiyoyajua
Kizuizi kwa Mkono wa Bwana
·
Isaya
59:1-2 1. “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka,
hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2. lakini
maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso
wake msiuone, hata hataki kusikia”.
Biblia inaonyesha wazi kuwa ni dhambi tu ndio
inaweza kumfanya Mungu aionyeshe mkono wake na ni maovu tu ndio yanayoweze
kumfanya asisikie sasa dawa ya hili ni rahisi, lazima tukubali kutubu na Yesu
anatusubiri na tukiungama yeye ni mwaminifu na atatusamehe kabisa 1Yohana 1:9 “Tukiziungama
dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na
kutusafisha na udhalimu wote.”
Na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.