Matendo 2:46-47 “Na siku
zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba,
na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na
kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa
wakiokolewa.”
Lakewood Church ni Kanisa linaloongozwa na Mchungaji
Joel Osteen, jijini Houston Texas Nchini Marekani ni kanisa kubwa lenye washirika wapatao
45,000, Kanisa hili lina uwezo wa kuketisha watu 16,800 kwa wakati wa ibada
moja na wana ibada nne za kiingereza na ibada mbili za Kihispania kwa wiki, hii
ni moja ya mfano wa Kanisa kubwa
Utangulizi:
Somo hili
linazungumzia kuhusu ukuaji wa Kanisa, kitu chochote chenye uhai kinakuwa,
Kanisa lililo hai linakuwa na kuongezeka, kwa kawaida kanisa linakuwa, kiroho,
kiidadi na kijiografia, yaani watu wake wanakua kiroho wanakomaa, wanakuwa na
uzoefu wa kutosha katika kuukulia wokovu, lakini pia wanaongezeka kwa idadi ya
watu waoookolewa kila siku, lakini pia linatawanyika kuyafikia maeneo mengine
ambayo hayajafikiwa Matendo 8:4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko
wakilihubiri neno.” Ili kanisa liweze kukua katika mazingira hayo
makubwa matatu, kuna mbinu za ukuaji wa kanisa, mbinu hizo ndizo ambazo
tunakwenda kuzizungumzia kwa undani, kwa kina na mapana namarefu katika somo
hili Muhimu:-
Katika somo hili
yako maswala mbalimbali kadhaa ambayo tutakenda kujifunza kwa undani kwa
kuzingatia maswala kadaa wa kadhaa:-
Maana ya Mbinu za ukuaji wa kanisa (the Strategy For
church Growth)
Mithali 24:5-6 “Mtu mwenye
hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya
akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.” Biblia ya kiingereza ya MSG inasomeaka hivi
Proverbs 24:5-6 “It’s better to be wise than
strong; intelligence outranks muscle any day. Strategic planning is the key to
warfare to win; you need a lot of good counsel.” Neno Mbinu au Strategy linamaanisha ni kampeni za kijeshi, au Mbinu
inayotumiwa na wewe au adui yako ili upoate au apate ushindi
·
Neno mbinu au Stategy Linatokana na neno la kiasili
la kiyunani Strategos Strategy ambalo maana yake ni
kuongoza Jeshi kwa hivyo kimsingi linatokana na maswala ya uongozi wa kijeshi (General)
lakini linaweza kutumiika pia katika kampeni za mambo mengine na mikakati ya
aina yoyote
·
Yesu alisema Nitalijenga kanisa
langu juu ya mwamba wala malango ya kuzimu hayataliweza ni tamko la mikakati ya
kijeshi kwani shetani amejaribu kuliharibu kanisa, kulidhoofisha na
kulisambaratisha na kulitoa katika malengo yake makuu na kulifanya lisiendelee
lakini wewe kama kiongozi wa kiroho katika eneo lako unapaswa uwe na mbinu na
mikakati ya kuhakikisha kuwa kazi hii inaendelea na ushindi dhidi ya upinzani
wa adui unapatikana na kazi inaendelea Mathayo
16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya
mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
·
Uongozi hapa unajumuisha kuwasaidia watu kufuata vema mpango mkakati
na kushinda vikwazo na kufikia malengo yaliyokusudiwa katika staili ya kijeshi
hii ndio mbinu, Kwa hiyo Mtumishi wa Mungu wa Kanisa la mahali pamoja ni mkuu
wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Kanisa ambaye anapaswa kuwa na fikra au
mikakati ya kuhakikisha kanisa linakuwa na kusonga mbele kwa gharama ya dhamu
ya Yesu kristo iliyomwagika pale msalabani
Neno kukua kwa kanisa lina maanisha kuwa kanisa ni
·
Kanisa ni zaidi ya dhehebu au
shirika, ni kitu chenye uhai, na kitu chochote chenya uhai, kinakua, kinasegea,
kinaweza kwenda mbele au kurudi nyuma, kusimama au kukaa au kutembea lakini la
msingi Zaidi kadiri siku zinavyokwenda linapaswa kukua.
·
Ni kama mwili ulio hai wenye
uwezo wa kukua na kujizalisha wenyewe, hii ina maana ya kuwa kila kanisa la
mahali pamoja lina uwezo wa kukua na kujizalisha lenyewe na kupanda makanisa mengine
hivyo kama kanisa lina uhai basi ni muhimu kanisa likaelewa jambo hili la
msingi Yesu mwenyewe alitoa msingi wa ukuaji wa kanisa wenye nguvu ambapo
kanisa linapaswa kukua kiroho, kiidadi na kijiografia.
·
Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine
kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine
kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi
ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote
tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu
mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe
tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa
elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”
·
Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu,
wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa
moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha
kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”
·
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu,
akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
·
Maandiko yote hapo juu
yanazungumzia ukuaji wa Kanisa kiroho, kiidadi na kijiografia na hii ina maana ya kuwa kanisa linaweza kupandwa
mahali kokote na katika jamii yoyote na
likaongezeka kutoka katika jamii hiyo na lika sambaa kuelekea katika jamii nyingine na kuweza kufika hata sehemu nyingine
ulimwenguni au mwisho wa nchi, huku watu wakibadilishwa katika tabia na
mwenendo ili wamfananie Kristo, huu ndio msingi wa kimungu kwa hivyo mtu awaye
yote asiogope kupanda kanisa au kuanzisha kanisa huu ndio ulikuwa mkakati wa Yesu Kristo
kuhusu kanisa lake na ahadi yake ni kuwa
pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari.
Kwanini tunasoma Mbinu za ukuaji wa kanisa?
·
Somo hili litatusaidia jinsi ya
kushughulikia na maswala ya kiroho,tamaduni na nguvu ya jamii husika katika
upandaji au ukuaji wa kanisa na litakufundisha
asili na ukuaji wa kanisa
·
Litasaidia kukuonyesha wewe na
jamii ya watu unaowahudumia umuhimu na ulazima wa agizo kuu katika Mathayo 28:18-20 “Yesu
akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru
ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” hii itakusaidia kuweza kuwa mfuatiliaji wa
karibu wa kujua kuwa kanisa linakua au la kwa kutumia grafu au utafiti wa
kawaida wa Ugunduzi kuhusu ukuaji wa kanisa,litakufundisha namna ya kuanzisha
na kuendeleza kanisa.
·
Somo litakupa mifano mbalimbali
ya ukuaji wa makanisa katika maeneo mbalimbali Duniani na kukuonyesha faida na
uzuri au utamu wa kukua kwa kanisa pia katika eneo lako utajifunza tamaduni na
muundo wa jamii unayoihudumia na
kuchagua njia inayofaa kwa ajili ya kujenga kanisa lenye nguvu litakalojieneza
na kujiendesha na kijitegemea lenyewe indigenous church.
·
Kujifunza jinsi na namna ya
kupanga mikakati ya kushambulia kwa injili miji na pamoja na kufikia kila jamii
kwa injili, kupanda makanisa na kufanya kazi na watu na makundi yao katika
namna mbalimbali, kutumia mbinu za kifundi kugundua ni maeneo gani yanapokea
injili kwa haraka na kuchukua hatua za
haraka kupanda kanisa hapo, pia kupanga mipango au kuweka malengo ya baadaye
katika eneo unalo lihudumia au uatakalolihudumia
·
Kuwa na uelewa kuwa nguvu ya
ukuaji wa kanisa inategemeana na uhusiano wetu na Roho Mtakatifu kwako na kwa
watu unaowahudumia ili kuweza kuubeba
agizo lile kuu na kanuni hizi zinazotolewa zinaweza kufanya kazi katika eneo
lolote iwe mijini, kijijini kwa kanisa kubwa au kanisa lililo dogo.
Mbinu za ukuaji wa Kanisa:-
FANYA KAZI SAWA NA KANUNI ZA
KIBIBLIA ZA UKUAJI WA KANISA
Mtu awaye yote
ambaye anataka kanisa lake liweze kukua au anataka kupanda kanisa ni muhimu
kwanza akafanya kazi au akakubaliana na kanuni za ukuaji wa kanisa zinazotolewa
na Biblia hii ndio kanuni ya msingi ya upandaji na ukuaji wa kanisa katika sura
hii tunashughulikia msingi huu wa Kibiblia na kitheolojia wa ukuaji wa kanisa
katika msingi huu basi tutajifunza kwa kuzingatia maeneo manne
·
Lazima ujue kuwa unajenga
kanisa lenye msingi wa Agano jipya
·
Lazima ukubali kuwa mwaminifu
katika majukumu ya Shughuli hii
·
Lazima uweke au utoe kipaumbele
kwa kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele
·
Lazima ujue kufanya kazi na
Mungu katika Uamsho
LAZIMA UJUE KUWA UNAJENGA KANISA LENYE MSINGI WA AGANO
JIPYA
Biblia ni neno
la Mungu na ndio msingi mkuu wa kwanza unaotuongoza katika mbinu yoyote ya
ukuaji na upandaji wa kanisa, Biblia inafunua kuwa ni aina gani ya kanisa Mungu
anataka na ni namna gani anataka kanisa likue
kwa msingi huo mbinu yoyote mbadala ya ukuaji au upandaji wa kanisa ni lazima
itokane na misingi inayopatikana katika Biblia, Unapopanda kanisa kinyume na
msingi ule unaowekwa na Biblia tunaouona katika agano jipya Basi ukuaji wa
kanisa hilo utaingia matatani kama tunataka makanisa yetu yakuwe basi lazima
tujenge msingi wa kanisa linalokuwa kwa mujibu wa makanisa ya agano jipya
kumbuka kuwa mjenzi mkuu wa kanisa ni Yesu Kristo na ndiye aliyetualika sisi nasi
kujenga pamoja naye Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”kwa
msingi huo ili kanisa liweze kukua linatakiwa kuzingatia maswala ya msingi
makuu matatu yafuatayo
a.
Lazima ujenge kanisa kwa msingi
wa kibiblia
b.
Lazima ujenge kanisa ambalo
Yesu Kristo ndiye kiini kikuu
c.
Lazima ujenge kanisa ambalo
Roho Mtakatifu anapewa kipaumbele.
Lazima ujenge kanisa kwa msingi wa kibiblia
Ni muhimu kabla
ya kuangalia kanisa kwa msingi wa kibiblia tuchukue Muda kujifunza neno kanisa
kwanza lina maana gani:-
1.
Neno kanisa kwa kiingereza
Church limetokana na neno la kiyunani Kuriake
yaani mali ya Bwana
2.
Neno linalotumika katika agano
jipya kuhusu kanisa ni neno la kiyunani Ekklesia ekklesia
ambalo maana yake ni kusanyiko ambalo neno lake la msingi ni Ekkleo yaani “walioitwa watoke miongoni mwa”
3.
Kwa msingi huo Yesu alipokuwa
anazungumzia habari za kujenga kanisa hakuwa anamaanisha kuwa atajenga Hekalu
zuri juu ya mawe, alikuwa akizungumzia watu ambao angewaita watoke miongoni mwa
udunia na kuwa awakusanye pamoja wawe wake kwa Makusudi yake ya milele
4.
Hata hivyo Biblia inapotumia
neno kanisa hususani agano jipya ambalo hutueleza jinsi kanisa lilivyoanza na
kukua na kuenea tunaweza kusema neno kanisa pia lina maana kuu nne zifuatazo
·
Ni kanisa la mahali pamoja (the
Local church) Warumi 16:4-5 “Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile
amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike.
Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.”
Kwa hiyo hapa kanisa yaani ni kundi la watu waliookoka
wanaokusanyika pamoja kila wakati kwa Makusudi ya kuabudu katika miji
mbalimbali, au kijiji, au nchi sehemu Fulani fulani
·
Ni wakristo (The society of
People) ni jamii ya watu Matendo 11:20-26
“Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na
Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri
habari njema za Bwana Yesu. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi
wakaamini, wakamwelekea Bwana. Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa
kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.
Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote
waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho
Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana. Kisha akatoka
akaenda Tarso kumtafuta Sauli; hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia.
Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha
watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.” Kanisa
ni jamii ya watu wanaofundishwa ili waishi maisha yanayofanana na Kristo, na
ndio kusudi hasa na maana ya jina wakristo
·
Mkutano au jamii ya watu
walioko mahali Fulani wote wakiwa na Imani moja Mwili wa Kristo (The body of
Jesus) Waefeso 1:22-23 “akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe
kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake,
ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote akavitia vitu vyote chini
ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
·
Ni kila mwamini wa kweli katika
Kristo waliopita, walioko na watakaokuja walio duniani au mbinguni kokote ambao
majina yao yameandikwa mbinguni ni kanisa Waebrania
12:23. “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa
kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu
wenye haki waliokamilika,”
5.
Maana nyingine za kanisa ni
pamoja na
·
Jengo mahali au nyumba ambapo wakristo hukutana kwa ajili
ya kufanya ibada
·
Dhehebu, huu ni ushirika wowote
wa Kikristo wenye mafundisho fulani sahii na namna fulani ya ibada za Kikristo
na namna zinavyoendeshwa
Kwa msingi huo
kuhitimisha maana ya kanisa tunaweza kusema kuwa kanisa ni kundi la watu
wanapokutana pamoja kuabudu, kujifunza, na kuhudumiana na wanaomkubali Yesu
kuwa Bwana na mwokozi wakifuata mafundisho yake na kumtumikia.
Kanisa lenye msingi wa kibiblia
·
Nyakati za kanisa la kwanza
walitambua na kulikubali neno la Mungu kuwa limevuviwa na kuwa kanisa
limetokana na Neno la Mungu, Kwa Msingi huo kanisa lazima litokane na
kuhubiriwa kwa neno la Mungu na wale wanaolisikia kuliamini Matendo 4:4 “Lakini
wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa
kama elfu tano.”
·
Waliamini katika ahadi za
kibiblia na mafundisho ya mitume
·
Walikubali kuongozwa na neno la
Mungu na kuwa ndio mamlaka ya mwisho lenye kuongoza kimaadili na kiimani
·
Walikuwa na imani yenye nguvu
iliyojengwa katika msingi wa neno la Mungu
·
Walikataa kila aina ya fundisho
lisilikubaliana na neno la Mungu au lenye msingi wa mila na tamaduni za
kimapokeo
·
Walikubali kuteseka na
walipotawanyika walieneza injili, walikubali kufa kwa ajili ya imani na
walihubiri kotekote
·
Mafundisho yao yalikuwa yenye
msingi wa kibiblia sawa na Mafundisho ya Bwana wetu Yesu
Kwa msingi huo mtu awaye yote akipanda kanisa kulingana na msingi wa
neno la Mungu kanisa hilo litakua na kuendelea mbele na kamwe halite tikiswa,
kwa sababu litakuwa sawa na kanisa alilolikusudia Kristo, watu wanalisikia
neno, wanaliamini, wanalitii, wanaungana na mitume, wanajifunza, wanabatizwa,
wanakuwa kiroho, wanakuwa waombaji, wanakuwa na misimamo, wanaichukia Dunia,
wanaishi maisha yanayomuakisi Kristo, wanafundisho la mitume, wanaamini katika
nguvu ya ujazo wa Roho Mtakatifu, wanamsikiliza, anawaongoza, wanafunga,
wanatoa, wanatoa pepo, wana dalili zote za kanisa tunalolisoma katika kitabu
cha matendo ya Mitume
Kanisa lenye msingi wa
kibiblia
Lilizaliwa kutimiza andiko |
Matendo 2;1-21 |
Imani yeke katika Kristo
ilitokana na maandiko |
Matendo 17;2-4, 18;28 |
Mafundisho yalitokana na
maandiko |
Matendo 17;11-12 |
Washirika walifundishwa neno |
Warumi 15;4,Matendo 18;11 |
Matumaini na kujitia moyo sawa
na maandiko |
Warumi 15;4 |
Maadili sawa na maandiko |
1Koritho 10;5-11,1Timotheo 3;15-16 |
Mafundisho ni Neno la Mungu |
Matendo 6;2-4,18;11 |
Imani na nguvu yao ni neno la
Mungu |
Efeso 6;13-17 |
Kukua kwake kulitegemea Neno la
Mungu |
2Petro 2;2 |
Kutawanyika kwao kulitegemea
Neno la Mungu |
Matendo 6;7,8;4,12;24.13;49 |
Lazima ujenge kanisa ambalo Yesu Kristo ndiye kiini
kikuu
Kanisa lolote
lile haliwezi kukua kama Kristo sio kiini kikuu cha kanisa hilo, Lazima tujenge
kanisa lenye uhusiano na Kristo aliye mizabibu wa kweli Yohana 15;1-8 na sisi
tu matawi ndani yake na ya kuwa hatuwezi kufanya neno lolote pasipo yeye hii
ndio kanuni ya nyakati za kanisa la
kwanza walizingatia swala zima la kumpa Kristo kipaumbele Yohana 15:1-8 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli,
na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila
tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu
ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani
yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa
ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi
ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo
mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje
kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.Ninyi
mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote
nanyi mtatendewa.Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa
wanafunzi wangu.”
·
Kanisa lilikuwa kwa sababu
lilikuwa na uhusiano mzuri na Kristo, watu walibaki ndani ya Kristo.
·
Kristo alihesabiwa kuwa kichwa
na kanisa ni mwili wake walimtii walitumia mamlaka yake na jina lake waliamini kuwa yeye ndiye anayetoa maelekezo
anayelitunza na kulilisha kanisa
Wakolosai 1:9-19 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia,
hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi
yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu
kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi
katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya
utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu
katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza
katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani,
msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa
viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu
vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na
visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu
vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu
vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa;
naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi
katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;”
Waefeso 1:16-19 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo
mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni
vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia
yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote
hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni
mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;”
1Wakoritho 12:26-27 “Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na
kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi
mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.”
·
Kristo alihesabiwa kama Mume na
kanisa kama bibi harusi kwa hivyo Yesu
alilipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake analisafisha na kulitunza na kanisa kama bibi harusi
linajitoa kwa Kristo linampenda na kumtii linajitunza katika usafi na uzuri 2Koritho 11;2-3,Warumi 7;2-4,Efeso
5;23-30,Ufunuo 19;7-8,21;2
·
Kristo anahesabiwa kama Mjenzi
au jiwe kuu la Pembeni ndiye mjenzi mkuu na mbunifu wa swala zima la kanisa na
kanisa ni Jengo la Mungu kwa msingi huu walifuata mpango wake walikuwa na umoja
kwa ajili yake walijifanya kuwa nyumba halisi ya Mungu, Kwa msingi huo basi
kanisa linalohitaji kukua ni lazima lijenge msingi wake katika kumuweka Kristo
kama kiini kikuu cha maswala yote ya kikanisa.
Lazima ujenge kanisa ambalo Roho Mtakatifu anapewa
kipaumbele
Kabla ya
kuondoka kwake kwenda mbinguni Yesu aliwaambia wanafunzi wake waziwazi kwamba
wanapaswa kusubiri nguvu za Roho Mtakatifu kabla ya kuanza kujaribu chochote
katika agizo kuu Luka 24:44-49 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia
nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote
niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo
akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba
Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa
kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya
Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”
Matendo 1;1-8 “Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi.” kwa msingi huo Matendo yote ya kanisa tunayo
yasoma katika kitabu cha Matendo ya mitume ni matokeo ya Nguvu hizo au agizo
katika Matendo 1;8 Roho Mtakatifu ndiye anayetoa nguvu ya huduma na kusababisha
kanisa kubeba kazi ya Mungu kwa ufasaha kwa msingi huo kanisa likizingatia hili
na washirika wakiwa ni waliojaa Roho Mtakatifu na Viongozi litafanikiwa katika
kila walifanyalo na walitendalo kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu .
Kwanini Roho Mtakatifu apewe kipaumbele katika
Shughuli za upandaji na ukuaji wa kanisa?
·
Kwa ajili ya kushuhudia na kueneza
injili Matendo 1;8
·
Kwa ajili ya kumtukuza Mungu na
kuelezea kazi zake Matendo 2;1-11
·
Kwa ajili ya kuhubiri na
kufundisha Matendo 2;14-47
·
Kwa ajili ya kutumia nafasi
kuhudumu na kushuhudia Matendo 3;1-26
·
Kwa ajili ya ujasiri wakati wa
upinzani Matendo 4;5-20
·
Kwa ajili ya kutiwanguvu upya
kueneza neno Matendo4;23-31
·
Kwa ajili ya kuelewa na
kutambua unafiki Matendo 5;14-16
·
Kwa ajili ya uponyaji na
mijadala Matendo 5;28-29
·
Kwa ajili ya furaha wakati wa
majaribu Matendo 5;40-42
·
Kwa ajili ya kumhudumia watu kwa
haki Matendo 6;1-7
·
Kwa ajili ya uaminifu hata kufa
Matendo 7;1-60
·
Kwa ajili ya kuhubiri kila
mahali Matendo 8;1-13
·
Kwa ajili ya kupambana na nguvu
za upinzani Matendo 8;9-13,Matendo
13;6-11.
·
Kwa ajili ya kusaidia wengine
kuipokea Roho Mtakatifu Matendo 9;14-17
·
Kwa ajili ya kazi maalumu
alizotuitia Matendo 9;10-20
·
Kwa ajili ya kuvuka mipaka ya
kitamaduni Matendo 10;1-48
·
Kwa ajili ya kuwapelekea injili
watu wasio wa utamaduni wetu Matendo11;1-26
·
Kwa ajili ya kufikia mahitaji
ya wale wenye kuhitaji Matendo11;27-30
·
Kwa ajili ya kutuokoa kimuujiza
wakati wa hatari Matendo12;1-17
·
Kwa ajili ya uongozi wake
katika safari za umisheni Matendo
13;1-52
Lazima uweke
msingi sio wa kumpa kipaumbele Roho Mtakatifu tu bali nafasi ya kuliongoza
kanisa katika Nyanja zote, Nyakati za Kanisa la kwanza walifanikiwa sana
kuupindua ulimwengu wa nyakati zao kwa sababu walimpa kipaumbele Roho
Mtakatifu, Kumpokea Roho Mtakatifu lilikuwa ni swala nyeti kwa wakristo na
mitume waliwauliza wakristo kama wamempokea Roho Mtakatifu sawa na kama
walivyouliza watu wasiookoka je mmeokoka? Je mlipomkea Roho Mtakatifu pale mlipoamini?
Kwa nini walifanya hivi kwa sababu Roho
Mtakatifu alikuwa wa Muhimu sana katika maisha ya muamini na ukuaji wa kanisa
na huduma zake.
Matendo 19:1-6 “Ikawa,
Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika
Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea
Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho
Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema,
Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba,
akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia
haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono
yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na
kutabiri.”
LAZIMA UKUBALI KUWA MWAMINIFU KATIKA MAJUKUMU YA
SHUGHULI HII
Ukuaji na
upandaji wa kanisa ni somo gumu kueleweka kivitendo kutokana na mfumo wa kanisa
na njia mbalimbali za ukuaji wake hii maana yake ni kuwa Shughuli hii inahitaji
uaminifu kwa majukumu yoyote ambayo Mungu anakupa hata kama wakati mwingine
mambo yaweza kuwa kinyume na matarajio hata kinyume na yale tunayokuwa
tumemuomba Mungu kuyafanya pamoja nasi
Utata katika ukuaji wa makanisa
1.
Yesu alisema nitalijenga kanisa
langu juu ya Mwamba na malengo ya kuzimu hayataliweza Mathayo 16;18 kwa msingi
huo jambo la muhimu ni kutimiza kusudi lake na kwa kweli kanisa linakua kwa
kasi ulimwenguni
·
Kanisa la Presbyterian huko
Korea ya kusini lilikuwa kwa kasi na kuongezeka mara mbili katika miaka ya 1950
hata leo
·
Huko Ethiopia waongofu wapatao
120,000 walibatizwa
·
Watu 80,000 wa nyanda za juu
walimfuata Yesu huko Formosa
Huu ni ushahidi ulio wazi kuwa kanisa
linakua lakini wakati mwingine ni vigumu kujua kuwa kanisa linakua kwa sababu
kadhaa zifuatazo
·
Mlipuko wa ukuaji au kuongezeka
kwa idadi ya watu na hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu wasiofikiwa
·
Kiburi cha udhehebu na matatizo
ya kugawanyika kwa makanisa
· Matukio yanayozuia ukuaji wa
kasi wa kanisa kama vita, upinzani wa injili, ukimbizi n.k.
· Kukosekana kwa taarifa za
ukuaji wa makanisa duniani, kutokutunzwa kwa Kumbukumbu za ukuaji wa kanisa na
kushindwa kutoa kipaumbele kwa maswala ya kuwafikia wale wasiofikiwa na injili
·
Kuwafikia wasiofikiwa na injili
leo limekuwa si swala la muhimu katika makanisa, Makanisa yanayotuma
wamishionari na Fedha za kusaidia kazi za umisheni wako gizani hawajui
yanayoendelea huko, Matukio yanayozuia ukuaji wa kanisa hayabadilishwi na
hubakia hivyo hivyo
Je Kanisa linaweza kukua kwa kasi kwa njia gani?
1.
Weka msingi wa ukuaji wa kanisa
mapema wakati watu wanapoanza kuokoka
a.
Ukuaji wa kanisa ni jambo
ambalo linatakiwa kupandwa mapema ndani ya watu wanaookolewa katika kanisa lako
njia hii ilitumiwa na kanisa la Yoido
Full Gospel Church (Assemblies of God) huko Seoul, Korea na kupata
mafanikio makubwa sana
Ø Mwaka 1973 Washirika walifikia 20,000 na kabala ya mwaka 1979 kanisa
lilifikia idadi ya washirika 100,000.
Ø Mwaka 1994 kanisa lilikuwa na washirika 700,000 watu wazima, Na sasa
kanisa hilo lina watu washirika wapatao milioni mbili 2,000,000
2.
Zingatia umuhimu wa kuwa na
makanisa ya nyumbani
Ø Moja ya njia nyingine iliyotumika Korea ni kutawanya makanisa ya nyumbani,
Mungu alimuongoza Mchungaji David Yonggicho na kumpa uwezo wa kukabidhi
madaraka au kugawa majukumu kwa washirika kuhudumiana katika makanisa ya
nyumbani
Ø Washirika walikubali majukumu hayo na kuanza kufungua makanisa ya
nyumbani ya kujifunza Biblia na maombi
Ø Majirani walianza kukubali wokovu na matokeo yake idadi ya kanisa
iliongezeka na mwishoni mwa mwaka 1979
kulikuwa na makanisa ya nyumbani yapatayo 7,000 waliokuwa wakikutana kila wiki
kwa ajili ya kuabudu pamoja wakijifunza maandiko na kuomba na kuabudu
Ø Ilipofika Mwaka 1994 kulikuwa na makanisa ya nyumbani yapatayo 21,800
3.
Zingatia umuhimu wa kuligawa
kanisa linapokuwa limeongezeka
Ø Mpango huu ndio mpango wa ukuaji wa kanisa unaouma lakini unasaidia
sana katika ukuaji wa kanisa au ni mojawapo ya njia ya ukuaji wa kanisa kwani
wakati mwingine inashauriwa kutumika kwa njia hii maadamu tu Mchungaji asiwe na
roho ya ubinafsi
Ø Njia hii inaweza kuleta uchungu na kuzuia ukuaji wa kanisa wengi wameiacha imani kutokana na tabia
zisizo za Kikristo na kukosekana kwa upendo
kunakotokana na mafarakano
Ø Wakati mwingine kundi moja linapoondoka lile linalobaki huona wanazidiwa katika kukabiliana ana majukumu yaliyokuwa mbele yao mgawanyo huu unaweza kusababisha kutokuweko kwa umoja katika kanisa katika mwili wa Kristo vyovyote iwavyo Historia ya kanisa inaonyesha ya kuwa Mungu huitumia njia hii wakati mwingine ili kusababisha ukuaji wa kanisa, Baadhi ya madhehebu pia yamezaliwa kutokana na kuchangiwa na tabia za kutokupokelewa vema katika makanisa yao ya awali
Moja ya njia za ukuaji wa kanisa wakati mwingine ni kugawanyika.
Mambo ya kufanya njia hii inapotokea
Kanisa linapogawanyika hata kama ni kwa mafarakano au kwa Ridhaa ya
Mchungaji wa kanisa mama ni muhimu kufahamu kuwa unawajibika kufanya mambo ya
msingi yafuatayo
·
Kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu
Kanisa kukua hata kama njia inaweza kuwa sio sahii lakini wakati mwingine Mungu
kwake ni sahii
·
Omba kwamba Bwana awabariki
wale walioondoka na kuwa Mungu awatumie kuwa Baraka na kufanya kazi ya injili
na kuieneza katika eneo lao
·
Waonyeshe upendo wale
walioondoka na shirikiana nao kwa njia yoyote iwezekanayo ambayo haiko kinyume
na Biblia
·
Hakikisha kuwa unalifanyia kazi
swala la kusamehe na kutokuwaona wapendwa katika Bwana kuwa maadui zako na
elewa kuwa ni njia ya lazima katika kuzalisha ukuaji wa kanisa
4.
Zingatia umuhimu wa kanisa mama
kuzaa kanisa jipya
Maswala ya kuzaa makanisa mengine ni lazima yawekewe msingi katika
makanisa mama au wachungaji husika, mara nyingi kunakuwa na visingizio vingi
lakini kama tupo kwa ajili ya Mungu mpango huu ni wa lazima
Ø Unaweza kupunguza idadi ya washirika wanaotokea upande fulani au
familia zinazotokea upande fulani kisha kisha ukazaa kanisa jipya
Ø Au unaweza kuweka mpango wa aina nyingine kutoka kanisa mama kuzaa
kanisa
Ø Au unaweza kuweka mpango wa kufundisha watenda kazi au kuandaa
watumishi ndani ya kanisa lako kisha ukawatuma katika eneo jipya na kuzaa makanisa
kanisa lililo hai huzaa na kuongezeka lenyewe
5.
Kumbuka kuwa njia kubwa ya
mafanikio ni ile ya makanisa ya nyumbani
Ø Njia hii ndio njia nzuri zaidi kwani watenda kazi walioandaliwa
kumhudumia makanisa ya Nyumbani makanisa hayo yanapokuwa katika mitaa yao
baadaye yanaweza kugawanywa na kuwa makanisa kamili hii imefanikiwa kule Korea
6.
Njia nyingine za upandaji au
ukuaji wa makanisa ni pamoja na
Ø Kushuhudia nyumba kwa nyumba katika maeneo ya kanisa
Ø Kulenga kuyafikia maeneo yaliyo mbali na kanisa, kuwafikia walioko
magerezani,kufanya mikutano ya injili, kugawa tracts na kuwazuia Biblia kwa bei
nafuu
Ø Kuongezeka kwa kuzaliana
Ø Kuwatumia washirika wanaohamishwa katika maeneo yasiyofikiwa
kuanzisha makanisa
Ø Kujaribu kuwarejesha wale waliorudi nyuma
Ø Kutumia vyombo vya habari, kama televisheni, radio na magazetu
pamoja na huduma za jamii
Ø Kuanzisha vyuo vya Biblia kwa wale wanaopenda kujifunza Biblia kwa
mitindo hii kanisa litaweza kukua
Kanisa kukua ni swala la uaminifu kwa Mungu
Uaminifu kwa
Mungu katika kuhakikisha kuwa kanisa lake linakuwa hujumuisha swala zima la
1.
Kuhubiri injili lakini kuhubiri
injili bila kufanya wanafunzi au kufanya ufuatiliaji ni tabia isiyo ya uaminifu
kwa kanisa, kama kanisa halijajipanga kuhakikisha wanaookolewa wanasimama ni
bora kutokufanya mikutano
2.
Kuhubiri injili kisha
kutokufanya ufuatiliaji wa kiuanafunzi kwa waongofu wapya ni kutimiza au kuwa
mwaminifu kwa sehemu tu ya lile agizo kuu
3.
Ni kushindwa kuliko wazi kwa
kutafuta waliopotea ambao wameweza kuitikia vema ujumbe wa injili
4.
Ni kushindwa kuona umuhimu wa
nini kifanyike baada ya kushuhudia au Kuhubiriwa kwa injili na watu kuokolewa
hili ndilo tatizo la makanisa mengi leo
5.
Kanisa la kwanza hawakuwa
hodari katika kuhubiri pekee bali katika kuhakikisha wale waliohubiriwa wanakaa
katika Imani ona Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba,
Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno
la Bwana, wa hali gani.”
Kuna njia Tano muhimu za kuonyesha uaminifu wetu kwa
Mungu sambamba na ukuaji wa makanisa
1.
Kutoa zaka na matoleo mengineyo kwa uaminifu kama utii
kwa neno la Mungu ili Fedha itumike kwa Makusudi ya injili
2.
Kumtangaza Kristo kama mwokozi,
kila mahali na kila wakati
3.
Kuweka mikakati na kuwafikia
waliopotea kwa njia na namna mbalimbali
4.
Kuhakikisha kuwa waongofu hao
wapya wanafuatiliwa na kulishwa neno la Mungu
5.
Kueneza kanisa lililojaa Neno
na nguvu za Roho Mtakatifu
6.
Kutunza Kumbukumbu ya watu
wanaookolewa na idadi yao
7.
Kuhakikisha walioamini wanakuwa
wanafunzi kwa kupanga madarasa ya kibiblia
Uaminifu kwa Mungu ni swala gumu na wala sio swala
rahisi kama tunavyofikiri
Historia
inaonyesha kuwa ukuaji wa kanisa unatofautiana katika kila eneo kutokana na
hali zinazochangiwa na eneo husika au na watu husika na ziko sababu mbalimbali
zinazochangia hali kuwa rahisi au kuwa ngumu sababu hizi zinaweza kuwa ni
kanisa lenyewe husika au jamii au siasa au uchumi au hali ya tamaduni na
maswala mengineyo yanaweza kuchangia katika ukuaji au kutokukua kwa kanisa na wakati mwingine sababu zinaweza kuwa za
kipekee sana kiasi cha kuweza kusababisha hali iliyotumika mahali fulani
isifanye kazi katika mazingira mengine
Uamsho huko Philippines.
Nchini Ufilipino
(Philippines) kumewahi Kuweko na Uamsho mkubwa sana kwa sababu ya Mafundisho
kushuhudia na makanisa mengi yalipandwa na kustawi lakini ni hali gani
zilichangia Filipino Kuweko na Uamsho huu
a.
Wakati wa vita vya pili vya
dunia wafilipino wengi waliamua kuishi milimani mbali sana
b.
Mchungaji mmoja aliyeitwa Dia
na mkewe waliamua kukataa kushirikiana na maadui na kwenda kuhubiri huko ndani
milimani na Mungu aliwaongoza kuifikia miji mitatu midogo, huko walipata
washirika ingawa Mchungaji wao alikuwa dikteta Kanisa lilikuwa licha ya Historia
hiyo ya kukatisha tamaa, kuzunguka nakutawaliwa na maadui mazingira ambayo
sehemu nyingine huweza kufanya kanisa lisikue, kuzungukwa kwa hatari kwa
Mchungaji Dia na nchi ya milima kulimfanya kutopuuzia kuyafikia makundi ambayo
Mungu alitaka aweze kuyafikia na kuleta Uamsho
c.
Mambo yaliyochangia kukua kwa
kanisa huko Ufilipino ni pamoja na mialiko,uwezo wa kuwafuata watu ndani sana, Mafundisho
na mahubiri mazuri Uamsho wa wakristo, ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba, ufuatiliaji
na kustawisha makanisa yaliyozaliwa hali hii ilipelekea kuwako kwa Uamsho
mkubwa nchini Filipino
Maeneo mapya ya kinjili
India
·
Mpaka mnamo nusu ya Karne ya 19
na mwanzoni mwa karne ya 20 Tatizo kuu
nchini India lilikuwa ni ubaguzi wa wenyewe ka wenyewe ujulikanao kama Caste system mpaka nyakati za hivi
karibuni bado jamii ya kihindu wanafuata ubaguzi huu wa kijamii kwa sheria
iitwayo Manu jamii ya kihindu imegawanyika katika makundi manne ya jamii
·
1 Brahmins hii ni jamii ya makuhani na wasomi
·
2 Kshatriya hii ni jamii ya
mashujaa wanajeshi
·
3 vaishyas hii ni jamii ya wasanii,wafanya biashara na wakulima
·
4 Sudras hii ni jamii ya vibarua na walala hoi
·
5. Outcastes hii ni jamii ya watu wenye hali ngumu nay a chini sana na
wanaodhaniwa kuwa waliolaaniwa
Brahimas Kshatriyas Vaishyas shudras outcastes
Jamii ya madaraja ya ubaguzi ya kihindu Kama
yanavyoonekana katika michoro Picha na maelezo kwa hisani ya Library ya Mwalimu
wa somo Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote
·
Katika madaraja hayo manne ya watu huko India kuna madaraja
ambayo yanaingilika na kuna madaraja
ambayo hayaingiliki kwa maswala ya kuwapelekea injili au hata mawasiliano ya
kawaida
·
Mahatma Gandhi wakati fulani aliwahi kufunga siku 21 na
kuhatarisha maisha yake ili kuwapandisha watu hao daraja na alifanya kila jitihada kuwainua na walijulikana kama Harijan ambalo ni jina
maalumu kuwa watu wa Mungu hili ni jina walilopewa na Mahatma Gandhi
·
Jamii hii ya watu wa daraja la chini ni rahisi kuipokea injili
huko india ukilinganisha na madaraja mengine
Zambia
·
Zambia injili iliingizwa kwa kupandikizwa shule wamishionari wengi
waliopanda makanisa kusini mwa jangwa la sahara walitumia shule na hivyo
ilisaidia watoto wa wapagani waliokuja kusoma kuingiziwa injili na kuikubali
·
Kwa msingi huo njia ya kuingiza injili katika eneo fulani
inategemea kuwa mazingira hayo yakoje na Mungu anakupa namna gani ya kupenda
kanisa au kupeleka injili kulingana na eneo husika
Iceland
·
Injili ilipandwa kupitia kuongoka kwa familia nzima nzima mpaka
mwaka wa 1000 baada ya Kristo kisiwa chote kilikuwa kimeukubali ukristo
Amerika ya
kusini Latin America
·
Injili iliwafikia kupitia Vyombo vya habari Redio, Television na
magazeti yalitumika kuwafikishia ujumbe wa injili vilitumika aidha kwa ajili ya kutangazia
semina za kuandaa Viongozi, kampeni za maombi, watenda kazi na mikutano mikubwa
ya injili iliyokuwa na nguvu za Roho na uponyaji vilizifanya nchi za Brazil na
America ya kusini na kati kufikiwa kwa injili
·
Waliompokea Kristo walifanyiwa ufuatiliaji, walipewa Biblia na
madarasa ya waongofu wapya yalianzishwa, makanisa ya nyumbani na shule za
Biblia kwa njia ya Posta
Kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa
ukuaji wa kanisa unatofautiana kati ya udongo na udongo au kati ya sehemu na
sehemu na nivigumu wakati mwingine kutumia kanuni iliyotumika sehemu fulani
ikafanya kazi sehemu nyingine na kama tulivyoona maeneo mengine Fedha
inahitajika sana katika kuwafikishia injili
LAZIMA UWEKE AU UTOE KIPAUMBELE KWA KILE AMBACHO MUNGU
ANAKIPA KIPAUMBELE
Jambo kubwa la
msingi kabla ya kuangalia kanuni zozote za ukuaji wa kanisa ni kukubali kutoa
kipaumbele kwa kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele yaani kusudi lake la
kuwafikia watu wote duniani ni la Muhimu sana ukiisha kuwa na moto ambao Mungu
anao ndipo sasa yeye atakupa njia na msaada wa kukujulisha wapi uweke nguvu kubwa,
wapi utoe Muda wa kutosha, wapi utapata Fedha kwa ajili ya kutimiza huduma aliyokuitia
ni kitu gani ambacho Mungu anakipa kipaumbele?
·
Ni mpango mzima wa Mungu kwa
wanadamu
·
Kila kinachofanywa sawa na
maagizo ya Yesu ni mpango wa Mungu na Mungu amekipa kipaumbele mfano, Kutoa chakula kwa wenye njaa,
kuonyesha upendo na kuipeleka injili kwa kila jamii au kushughulikia na yatima
na wajane n.k.
·
Kubwa zaidi ni kuipeleka injili
na kutimiza agizo kuu kusudi kuu la Mungu ni kutafuta waliopotea ni
kuwarudishia watu uhusiano wake na Mungu Yohana
20:21 “Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu;
kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.” 2Wakoritho 5:18 “Lakini
vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo,
naye alitupa huduma ya upatanisho;”
·
Kanisa ndilo lenye wajibu huu
na kila mwamini anao wajibu huu pamoja na kutimiza Mathayo 5:16 “Vivyo hivyo nuru yenu na
iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu
aliye mbinguni.”
Kusudi la Mungu ni kutafuta kile kilichopotea
1.
Luka 15 ina mafundisho
yanayohusu Jinsi Mungu anavyotoa kipaumbele katika kutafuta kile kilichopotea
kuna mifano kadhaa inayotolewa katika sura hii kama vile
·
Mchungaji kutafuta mwana kondoo
aliyepotea
·
Mwanamke kutafuta shilingi
iliyopotea
·
Baba kumpokea mwana mpotevu
·
Mifano yote hiyo inaishia na
kuonyesha furaha na ushindi wa kukipata kile klilichokuwa kimepotea
·
Mungu ni lazima atafute kile
kilicho chake kilichopotea ni haki yake kwa sababu ni uumbaji wake kwa msingi huo kusudi la Mungu ni kuokoa na
kuhakikisha wale waliopotea wanarudi kwake na sio kupotelea huko
·
Kutafuta ni muhimu na kwa
sababu hiyo kusudi kuu la Mungu au kile ambacho Mungu anakipa kipaumbele ni
kuhakikisha kuwa waliopotea wanakuja nyumbani.
·
Kusudi la Mungu na huruma zake
limefunuliwa katika Luka 15 aidha tunaona katika sehemu nyingine pia za Biblia
zikiunga mkono kusudi hili la Mungu kwa mfano
Maombi ya Bwana Yesu kwa
wanafunzi wake Mathayo 9;37-38
Agizo la Bwana Yesu kwa
wanafunzi wake Mathayo 28;19-20
Mifano hiyo ya Bwana yesu
kuhusu vilivyopotea Luka 15
Kusudi Yesu alilolitoa kwa
ajili ya kuja kwake Luka 19;10
Msukumo wa Mungu kumtoa mwana
wake wa pekee Yohana 3;16
Kazi ya mitume katika kutimiza
agizo kuu Matendo 2;37-38
Ujumbe kwetu kama mabalozi wa
Kristo 2Koritho 5;18-20
·
Kwa msingi huu basi Mungu anataka
kila kanisa la mahali pamoja kuweka kipaumbele katika maswala ambayo yeye
ameyapa kipaumbele na tukafanya hivyo makanisa yatakua na kuwafikia wengi
waliopotea duniani.
2.
Fuata maelekezo ya Mungu katika huduma
a.
Biblia inatoa maelekezo ya
namna ya kutimiliza huduma tulizo nazo katika kuwafikia wasio fikiwa kwa msingi
huo kila muumini katika kanisa ni lazima atumie nafasi uwezo na kipato alicho
nacho katika kuhakikisha kuwa wanavitumia vile Mungu alivyowapa katika kazi
yake.
Kila mshirika atiwe moyo
kutumia kile alichopewa na Mungu kwa faida ya ufalme wa Mungu
Kumbuka ule mfano wa talanta Mathayo 25:14-30 unatupa ujumbe gani
Unatoa onyo kwa wale wasiotumia
kile walicho nacho hata kama ni kidogo
Kanisa litakuwa na kuongezeka
kama kila mshirika atatumia kwa makini au kufuata kwa makini maelekezo ya
Mungu na kutumia njia na uwezo aliopewa
na Mungu kwa namna yoyote ile kuwafikia wengine
Kwa msingi huo kila mmoja
anahitaji maelekezo Binafsi ya Mungu ili kushiriki au ashiriki namna gani
katika kulitimiza Jukumu lililoko mbele yetu
b.
Wajibu wetu Kibiblia sasa ni
lazima kuweka kipaumbele katika mambo yale ambayo Mungu anayapa kipaumbele
tukikumbuka kuwa watu Bilioni tatu hivi duniani hawajafikiwa wala kuisoma
Biblia hata ile ya agano jipya Jukumu hili si la watu fulani ni Jukumu la kila
mtu kwa hiyo watu wafanye nini sasa ili
kutimiza majukumu yao?
Kila mtu anawajibu wa
Kushuhudia watu nyumba kwa nyumba au mtu kwa mtu
Kuwezesha vipindi katika vyombo vya habari
Kufanya mikutano ya mitaani
Kutembelea wagonjwa
mahospitalini na magereza
Huduma kwa wanafunzi mashuleni
na vyuoni
Na kuwafikia wasiofikiwa kwa
kubuni mbinu ambazo zitaleta matunda
Kuonyesha upendo kivitendo.
Kufanya kazi hii na Roho
Mtakatifu.
LAZIMA UJUE KUFANYA KAZI NA MUNGU KATIKA UAMSHO
Uamsho ni nini?
Hakuna malezo ya
kutosheleza katika msemo mmoja juu ya Uamsho lakini kuna semi nyingi zinazoweza
kutumika kuelezea Uamsho
1.
Ni nguvu kubwa ya kiinjilisti
iliyoamka inayowaleta watu katika mguso wa Roho wa Mungu
2.
Ni kazi ya Roho Mtakatifu ya
kupandikiza maisha mapya na nguvu za Ukristo na kanisa
3.
Ni Kuamka kwa hali ya kujirudia
ndani ya waamini ili kuwafikia wasio fikiwa au wenye dhambi
4.
Ni Ufufuo au hali ya kurudisha
uhai tena , ni kuamsha hali za kulipuka kwa utendaji mkuu wa kimungu katika
kanisa
5.
Ni nguvu kubwa ya kupanda
makanisa na kuhakikisha yanasitawi kila mahali ambako injili haijafika
6.
Ni kiu ya kuona maelfu kwa
maelfu wanakuja kwa Yesu, makanisa yanaongezeka kiroho, kiidadi na kijografia
7.
Kiu ya watu kujazwa Roho
Mtakatifu, kuwepo kwa Karama na utendaji mkubwa wa Roho Mtakatifu, kiu kubwa ya
maombi na kufunga bila watu kusukubwa, kiu ya kujifunza na kusoma neno la
Mungu, kiu ya kuhudhuria ibada na kuwa tayari kujifunza na kuyatendea kazi yale
watu waliyojifunza
Mambo sita yanayo saidia kuleta Uamsho
1.
Kusudia kuwa na uhitaji wa
Uamsho
Lazima kama unahitaji Uamsho katika kanisa lako basi kiwe ni kitu
kilicho maanishwa kabisa hii ni kwa sababu kuna wakati mwingine hutokea
washirika wengine hawahitaji Uamsho kwa sababu kadhaa zifuatazo
Wako washirika wanaogopa Uamsho
Wanahofia kuwa kutatokea
mitikisiko mikubwa na maswala mengine
yatafumuka
Wanahofia kutokea kwa
migawanyiko kwani baadhi watakuwa wanakiu ya kumtafuta Mungu kwa undani sana na
wengine hawata mtafuta Mungu
Hivyo ni lazima kama unataka
Uamsho ukusudie kweli kweli na washirika pia, washirika wakongwe wasiwavunje moyo
wachanga na badala yake wawaonyeshe upendo na kuwatia moyo ili wakue
2.
Kubaliana na Hali za
Kipentekoste
Kumbuka kuwa ile hali ya
wakati wa pentekoste itashuka katika kanisa
Mabadiliko ya waamini binsfi na
kundi lazima yatokee
3.
Kubaliana na Mfumuko wa maombi
Watu wataungana kwa pamoja
katika kuomba sawa na Matendo 4:24-31
Ujasiri wa kushuhudia na
kuhubiri Matendo 28:30-31
Kuokoka kwa wenye dhambi Matendo 9:3-5
Huduma za uponyaji na miujiza Matedno 19:11-12
Mapepo kufumuka na kutolewa Matendo 19:11-12
Kusamehe maadui na kuwaombea
maadui Matendo 7:54-60
Kutokea kwa mateso na majaribu
makali na watu kukubali hata kufa Matendo
20:9-12
Matukio ya kupita kawaida
wakati wa ibada na wakati wa kuabudu Matendo 19:11
4.
Soma kwa undani kitabu cha
Matendo ya mitume
Wengi wa watu waliofanikiwa kupata
Uamsho wanashuhudia kuwa walipata nguvu hiyo kutokana na usomaji wa kitabu cha
Matendo ya mitume na kutamani kuyaona waliyoyasoma
Uamsho mara nyingi huwajia watu
wanaouhitaji na kuuomba kwa bidii na hivyo lazima kuukaribisha na kusoma kitabu
cha Matendo ya mitume ni maandalizi ya Uamsho na namna ya kuukaribisha Uamsho kwa kawaida unaturejesha katika kile
kilichofanyika katika nyakati za kanisa la kwanza na hivyo tunahitaji kujua nini
kilitokea ili kujiandaa
Soma historia za uamsho kwa
mfano uamsho wa (Azusa Street Rivival) ambapo umasho mkubwa ulitokea kati ya Tarehe
9 mwezi April mwaka 1906 na kuendelea mpaka 1915, ambapo uamsho huu ulianza na
Muhubiri Mmarekani mweusi William Seymour ambaye alialikwa huko Los Angels ambaye
alikuwa akisisitiza sana kuhusu mjadala uliokuweko kuhusu Ujazo wa Roho
Mtakatifu ambapo alipokuwa anahubiri watu kadhaa walijazwa Roho Mtakatifu na
kuanza kunena kwa Lugha, wakipiga kelele huku wakimtukuza Mungu jambo
lililoshitua watu na kusababisha watu kuja kushangaa na huko wagonjwa
waliponywa na watu wakajazwa Roho na ndio ukawa Mwanzo wa uamsho wa
kipentekoste ulioenea kote duniani hata leo
5.
Omba kwa ajili ya Uamsho
Hakuna mahali ambapo Uamsho
ulitokea Bila maombi ya bidii kila mahali katika historia za Uamsho watu
walianza kuomba sana kwa bidii wakati mwingine kwa kuendelea kwa majuma na
miezi bila kukoma
Huko Korea mwaka 1907 waamini
walianza kuomba kila saa 11 alfajiri na
jambo hilo lilichangia katika kukua kwa kanisa (Maombi ya Alfajiri)
Amerika Mwaka 1858 watu
walihudhuria maombi kwa viwango vikubwa sana
mpaka ikashindikana namna ya kupata mahali pa kuwaweka miguu, muungano
wa madhehebu katika maombi ulichangia sana katika kukua kwa kanisa
Huko Scotland 1859 walianzisha
maombi ya jioni kila siku jioni kwa muda
wa mwaka mzima na Uamsho mkubwa ulitokea
Swala la kuomba na Uamsho
linaonekana kwa wale 120 walioamua kusubiri kwa maombi kusubiri nguvu
waliyoahidiwa na Kristo
Uamsho uliotuletea makanisa ya
Kipentekoste ya karne hii ya 20 ulianza na maombi kulikuwa na vikundi vya
waombaji kutoka makanisa mbalimbali kama Lutheren, Methodist, Presbyterian,
catholics na washirika wa makanisa mengine
Ni muhimu kuimba, kuhubiri na
kufundisha kuhusu Uamsho pangeni Muda manaokubaliana kikanisa kwa ajili ya
maombi ya Uamsho
Mahubiri kuhusu Uamsho
yatawahamasisha kuwa na hamu na shauku kwa ajili ya Mungu na kupandisha imani
na kutaka Uamsho huo
Mwisho fanyia kazi yale yote
unayoayaombea kwani Imani bila Matendo imekufa Yakobo 2;20.
Ombea watu ujazo wa Roho
Mtakatifu, hubiri, panda makanisa, ombeni, anza kiri Uamsho.
Vikwazo Vikuu vya Uamsho katika makanisa
Mambo yanayosaidia kukua kwa kanisa |
Vikwazo vinavyozuia kukua kwa kanisa |
Mazingira 1.
Watu wanaopokea Injili
kirahisi 2.
Mazingira ya watu wakarimu na
wakaribishaji 3.
Watu wanaoingilika |
Mazingira 1.
Watu wasiopokea injili kwa
urahisi 2.
Mazingira ya wasio wakarimu na wakaribishaji 3.
Watu wasioingilika wagumu
kuwafikia |
Watu wa Ndani ya Kanisa 1.
Watu wanaobadilishwa na
Kristo, waliokomaa 2.
Kuishi kwa furaha na Amani,
Mchungaji na watu wake 3.
Wakristo wepesi washuhudiaji 4.
Mchungaji na washirika
waliojaa Roho Mtakatifu 5.
Mvuto wenye nguvu katika
maisha 6.
Maono, Imani na maombi 7.
Imani katika Neno la
Mungu |
Watu wa Ndani ya Kanisa 1.
Watu ambao ni , vuguvugu, na
waliodumaa 2.
Watu wasio na Amani, wenye
mafarakano, na migongano 3.
Watu wasiojua wajibu wao kazi
ya injili ameachiwa Mchungaji tu 4.
Wachungaji na washirika
waliopoa wasio na Roho Mtakatifu 5.
Maisha yasiyo na ushuhuda 6.
Hakuna maono, Imani wala
maombi 7.
Hakuna Imani katika neno la
Mungu |
Programu za ndani ya
Kanisa 1.
Ibada zenye mpangilio na mvuto mzuri 2.
Roho wa Mungu kupewa nafasi
3.
Kanisa linye lengo la kufikia wengine 4.
Mafunzo kwa washirika wote
5.
Kanisa linalojali mshirika mmojammoja 6.
Wote wanashiriki huduma kikamilifu 7.
Watenda kazi wazuri
wanafungua kazi |
Program za ndani ya
Kanisa 1.
Ibada zisizo na mpangilio unaoeleweka 2.
Ibada zisizo na mwelekeo 3.
Kanisa lenye kujiangalia lenyewe pale pale lilipo 4.
Mafunzo kwa baadhi ya washirika tu 5.
Kanisa ambalo Mshirika anapotelea humo hajaliwi 6.
Huduma inaachiwa wale wanaolipwa tu 7.
Watenda kazi wazuri wanapewa uongozi |
Njia zinazotumiwa na Kanisa husika 1.
Kuhubiri na kuifundisha
Biblia 2.
Watoto wa washirika wanaokoka 3.
Wanayafikia maeneo
yasiyofikiwa 4.
Mikutabo ya injili mara kwa
mara 5.
Kutembelaa na kushuhudia 6.
Kutumia vyombo vya habari 7.
Mafunzo ya Biblia kwa njia
mbalimbali 8.
Maombezi, miujiza na uponyaji 9.
Washirika wanaojitoa kwa 100% 10.
Wenye mipango ya
kuongezeka |
Njia zinazotumiwa na Kanisa husika 1.
Mafundisho na mahubiri duni 2.
Watoto wa washirika
wanasahaulika 3.
Wanahubiriana ndani tu 4.
Ibada za kawaida tu
zinaendelea 5.
Hakuna kutembelea wala
kushuhudia 6.
Hakuna matumizi ya vyombo vya
habari 7.
Hakuna mafunzo ya Biblia kwa
njia nyionginezo 8.
Hakuna, maombezi miujiza wala
uponyaji 9.
Washirika hawajitoi kwa dhati
ni unafiki tu 10.
Hakuna mipango ya namna ya
kuongezeka |
UPANDAJI WA MAKANISA NI MOJA YA NJIA YA KUKUA KWA KANISA.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ukuaji
wa kanisa umegawanyika katika makundi makuu
matatu yaani Kiroho, Kiidadi na kijiografia kukua kiroho ni hali ya
kutoka katika uchanga kuelekea katika hali ya kukomaa, kiidadi ni kuongezeka
kwa idadi ya watu wanaookolewa katika kanisa la mahali Pamoja, na kijiografia
ni kutwawanyika kutoka mahali pamoja na kupeleka injili na amakanisa katika
maeneo mengine
·
Waefeso 4:11-14 “Naye alitoa wengine
kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine
kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi
ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote
tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu
mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe
tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa
elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”
·
Matendo 2:46-47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu,
wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa
moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha
kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”
·
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu,
akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
·
Matendo 8:4 “Lakini wale waliotawanyika
wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.”
KUKUA KIROHO
Kukua Kiroho ndio msingi wa kukua kwa
namna nyinginezo zinazobakia, njia ya
ukuaji wa kiroho ambayo Bwana Yesu ametuachia ni pamoja na Roho Mtakatifu na
watumishi wenye wito maalumu ambao wanaoitwa na Bwana kwa kusudi la
kulikamilisha kanisa Matendo 1;8,Efeso 4;1-16 kwa msingi huo Kujumuika na
wengine pia ni njia ya kukua Kiroho. Washirika wasokua kiroho ni tatizo kubwa
sana katika kusababisha uamsho utokee, lazima kila mmoja aiskubali kudumaa
akubali kukua kiroho kufikia hatua ambayo Mungu ameikusudia,
Waebrania
5:11-14 “Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika
habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa
maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji
kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa
mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa
hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni
cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na
mabaya.”
KUKUA KIIDADI
Kukua kiidadi ni moja ya njia ya
kuonyesha uhai wa kanisa hata hivyo yako mambo yawezayo kuchangia ukuaji wa
kanisa hasa unapoangalia hali halisi ya ukuaji wakati wa Kanisa la kwanza
Kanisa lilikuwa kwa namna ya kupita kawaida lakini moja au baadhi ya mambo
yaliyochangia ukuaji ni pamoja na Miujiza na Ushirika Biblia inatoa mwanga
unaochangia katika ukuaji wa kanisa kuwa ni pamoja na Kuhubiriwa kwa injili,
kumruhusu Bwana afanye kazi pamoja nao na kuthibitishwa kwa neno kupitia Ishara
na miujiza Marko 16:20, “Kisha
wanafunzi Wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi
pamoja nao na kulithibitisha neno Lake kwa ishara zilizofuatana nalo.” Mambo mengine yaliyochangia katika ukuaji wa kanisa yako wazi
katika kitabu cha matendo ya mitume kiidadi.
MATENDO |
TUKIO AU MATUKIO |
MATOKEO |
2:1-41 |
Pentecoste, Kujazwa Roho, Kunena
kwa lugha, Mahubiri. |
a |
2:42-47 |
Mafundisho, Ushirika, maombi,
Miujiza, Umoja, Kuabudu, Kuwapendeza
watu wote |
b |
4:4 |
Kuponywa kwa mtu aliyepooza na
mahubiri |
c |
5:12-16 |
miujiza, *kumbuka inawavuta wengi
wasioamini na ni chambo chambo |
d |
5:42-6:1-7 |
Mafundisho na kushuhudia Hekaluni
na nyumba kwa nyumba. |
e |
9:31 |
Wakati wa amani, Kuishi kwa ajili
ya Kristo na kutiwa moyo kwa Roho Mtakatifu |
f |
14:1 |
Kuhubiri kwa ujasiri katika
masinagogi |
g |
16:4-5 |
Kukataa mafundisho ya sheria,kutembelea
makanisa na kutoa msaada Kiroho |
h |
17:10-12 |
Kuhubiri huko Beroya na
kuyachunguza maandiko |
i |
19:8-20 |
Kuhubiri na kufundisha na miujiza
ya kila siku |
j |
Kwa hiyo utaweza kuona kuwa kanisa la
kwanza lilianza na idadi ya watu 120 na likakua na kuongezeka toka siku ya
Pentekoste kwa kufikia 3000 na baadaye 5000 na baadaye watu waliendelea
kuongezeka kiasi ambacho Mwandishi wa kitabu cha matendo yaani Luka anaeleza kuwa idadi ya watu wanaume kwa
wanawake wakaongezeka kwa Bwana Matendo
5;14 inasema “Lakini walioamini wengi wakaongezeka kwa
Bwana, idadi kubwa ya wanaume na wanawake” Kwa msingi huo kuongezeka kiidadi
ni mpango wa Mungu na tunapaswa kuuwaza na kuufanyia kazi aidha ni muhimu
kuweka Rekodi ya idadi ya watu kanisa la kwanza walijuaje kuwa kanisa
linaongezeka hii iko wazi kuwa walikuwa wakiwahesabu kila wakati chukua idadi
ya washirika wanaohudhuria. Kwa msingi huo katika kanisa atakuwepo mtunza
takwimu mwenye kuangalia kama idadi ya washirika inakuwa au kupungua na kutunza
kumbukumbu hizo.
KUKUA
KIJIOGRAFIA
Huku ni kukua kutoka eneo moja
kuelekea eneo lingine Ni muhimu kufahamu kuwa kanisa la kwanza pia walikuwa
kijiografia ingawa kutawanyika kwao mwanzoni ilikuwa kwa ajili ya mateso lakini
waamini waliotawanyika walikuwa kama mbegu zilizokufa na kuzaa matunda, aidha
agizo kuu pia liko kijiografia Matendo
28; 18-28 Marko 16; 15 Matendo 1; 8 Kwa hiyo Yesu alikuwa na mpango wa
kijiografia wa kuifikisha injili ulimwenguni kuanzia Yesrusalem, Uyahudi, Samaria,
na hata mwisho wa nchi
Umuhimu wa
kukua kijiografia
Kukua
kijiografia ndio kiini cha somo hili kwa ufupi ndio kupanda makanisa, kupanda
makanisa ni njia nzuri ya Kufanya uinjilisti iliyo bora zaidi kuliko zote
Mchungaji ukiona kanisa lililo komaa lina kusumbua unaweza kulikabidhi kwa
wachungaji wengine na ukaamua kupanda kanisa jipya utajisikia Raha ya ajabu
sana na utafurahia aina hii ya uinjilisti kuna usemi usemao “NI RAHISI KUWA NA MTOTO KULIKO KUFUFUA MFU”
hapa simaanishi kuwa kanisa lililo kwisha anzishwa ni mfu hapana lakini
hapa nazungumzia kushughulikia na kanisa lililo na udumavu wa kiroho ni kazi
ngumu kuliko kuanzisha kanisa jipya
Kwa nini ni muhimu kupanda makanisa
1.
Kupanda kanisa ni mpango wa
Mungu wa Kibiblia na ni mpango wa Mungu sawa na Matendo 1;8
2.
Kupanda kanisa ni njia ya
kuzalisha Viongozi wapya wa kanisa
3.
Kupanda makanisa ni njia ya
kuleta Uamsho kwa makanisa ya zamani mara nyingi tunajua kuwa makanisa
yaliyotangulia huwa na tabia ya kujisahau na hivyo linapoanzishwa kanisa jipya
tayari hofu huwapata wale waliotangulia na hivyo Mungu hufurahia sana huko
mbinguni kwani ni changamoto kwa kazi na ufalme wa Mungu unajengeka
4.
Kupanda kanisa ni kuzuri kwani
kunakusaidia kulifikia eneo jipya ambalo halijafikiwa na injili Paulo mtume
alisema hamu yake na shauku ni kuipeleka injili kule ambako Kristo hajasikika Warumi 15:20 “kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili,
nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya
msingi wa mtu mwingine;”
5.
Kupanda makanisa kunaimarisha
Dhehebu lako si kwamba kupanda kanisa kwa kweli kwa undani kunaimarisha mwili
wa Kristo tu lakini dhehebu lako unalofanya kazi pamoja nalo linaimarika kwa
kueneza injili na kufikia maeneo yasiyo fikiwa.
Maadui wakuu wa upandaji wa makanisa
a.
Wakristo wa mwilini
Tunapozungumzia wakristo wa mwilini tunazungumzia jamii ya watu
ambao aidha walimwamini Yesu na kuipokea badiliko la kiroho na kuwa na uwezo wa
kushinda dhambi lakini baadaye wakapoa na wakabaki na jina tu kuwa ni wakristo
lakini wamekufa
Ufunuo 3;1“Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye na zile Roho saba za
Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai,
lakini umekufa.” Pia ni jamii ya wakristo
wanaoishi maisha vuguvugu
Ufunuo 4;14-16 “Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu
na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kwamba
wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. Hivyo kwa kuwa
u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani
Mwangu.”
Hawa ni wakristo wa majina tu na sio wakristo halisi pia wanaweza
kuwa wakristo waliozaliwa katika dini za Kikristo na hivyo wanaishi maisha ya
kawaida sana hawa wanakuwa kizuizi katika kupanda makanisa kwa vipi?
Hawawezi kuubeba injili na
kuwapelekea wale ambao bado hawajafikiwa na injili Warumi 10;14-15 “Basi wamwiteje
yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo
mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama
nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”
Kanisa linakuwa na Jeshi dhaifu
wakati Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu yaani watu wenye wivu wa
kimapinduzi kwa ajili ya Mungu Mathayo
11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa
ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”
Kanisa linakuwa na watu
wasioweza kuzaa matunda kwani wako nje ya mizabibu Yohana 15;5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami
ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo
lote.”
Kanisa linaweza kuwa na
watumishi wasio na wito au kuwapa uongozi watu wasio wakristo, ndoa
zisizoeleweka, na kuweza kupata makanisa mbali sana na watu kukosa sehemu za kuabudu
Wakristo wanaogombana wenyewe
kwa wenyewe 1Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na
watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na
watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa
kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi
ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si
watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? ”
b.
Chanzo cha wakristo wa mwilini Kuweko
·
Kukosekana kwa maombi
·
Kuanza kuchukuliana na dunia
·
Ubinafsi katika kutoa
·
Kuhubiri dini zaidi kuliko
injili
·
Kushindwa kuwafikia wanafunzi
kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vya Biblia
·
Kukosa Viongozi wazuri wa
kiroho
·
Wakristo wasio na matunda ya
Roho Mtakatifu, wamedumaa, wanamafarakano, washabiki wa wahubiri, hawatambui
uwepo wa kara tofauti tofauti.
c.
Uongozi Mbaya
Ni muhimu kufahamu kuwa
aina za Viongozi tunaowaandaa inaweza kuleta mafanikio makubwa au kutofanikiwa
kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa kanisa na upandaji wa makanisa,Yesu
alichukua Muda wa kutosha kuandaa Viongozi, mwanzoni hakulenga tu kujikusanyia
maelfu ya watu lakini alikaa na wachache ili kuwapandikizia kusudi la Baba
yake na kisha kupitia wao kanisa
lilikuwa na kuongezeka Viongozi hufananishwa na Nguzo Wagalatia 2:6-9. “Lakini wale wenye sifa ya
kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa
mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; bali, kinyume cha
hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro
ya waliotahiriwa; (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa
ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); tena walipokwisha kuijua ile
neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo,
walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa
Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;” utafiti unaonyesha kuwa moja ya matatizo
makubwa ya kutokukua kwa makanisa mengi ni Viongozi, viongozi wasio na utii,
viongozi wanaotaka kusikilizwa wao, viongozi ambao hawana maono, hawashirikiani
na Mchungaji, wanaompiga vita mchungaji na kuwacha kuangalia ni nini mapenzi ya
Mungu kwa watu wake na kanisa lake na wajibu wa kanisa duniani,
d.
Kukosa majibu ya matatizo
ya watu na mahitaji yao
Kanisa linalokua ni lile
ambalo matatizo ya watu hupata ufumbuzi,kama kanisa haliwezi kukutana na
mahitaji ya watu basi halitimizi wito wake kwa ukamilifu chunguza duniani
ukaone Popote duniani mahali kanisa limekua ni pale ambapo watu hupokea majibu
ya mahitaji yao hii ndio huchangia wakati mwingine kuwa hata imani potofu zenye
majibu ya matatizo ya watu watu hujikusanya huko ni muhimu kuwa na kanisa
ambalo Mwenye dhambi anapokea Msamaha, wenye kiu wanakunywa, wenye njaa ya roho
wanajazwa, wenye magonjwa wanapona, walioteswa na ibilisi wanafunguliwa asiye
na matumaini anapokea matumaini watu wanatiwa moyo na wanautazamia uzima wa
milele.
e.
Kukosekana kwa maombi
endelevu
Maombi endelevu
yanapokuweko katika kanisa ni lazima kanisa litakua na kufunikwa na furaha ya
kimungu watu wanapokusanyika kwa ajili ya Mungu na kuomba Mungu huwa katikati
yao na Mungu humwaga Roho ya furaha kwa kujibu maombi na kushughulikia na
mahitaji ya watu na watu wanapotoka na furaha
watu huvutiwa kuwako mahali penye furaha, shetani hakimbii watu
wanapohubiri au wanaposhiriki meza ya bwana yeye hukimbia watu wanapoomba
maombi yana nguvu kubwa ya kulifanya kanisa kusimamia na kukua na kuongezeka
f.
Kushindwa kuwaachilia watu wa kawaida kwenda
kuanzisha kazi mpya
Kama watumishi Viongozi wa
makanisa wanataka makanisa yao yakuwe ni lazima wakubali kuwaachia watu wa
kawaida kutoka na kuanzisha kazi mpya lakini ni muhimu pia kanisa likiwaandaa
kwa kazi hizo kama kanisa halina muundo unaoruhusu watu kumtumikia Mungu basi
hata kama kuna watu wenye kiu ya kufanya hivyo hawawezi kufanya hivyo
wachungaji wanao wajibu wa kuwafundisha na kuwatia moyo watu wa kawaida na
kuwatuma katika huduma hata kama wakati mwingine watu hao ni muhimu katika
kanisa mama unapoacha ubinafsi na kujaribu kulifanyia kazi hili kanisa litakua
kwanini kanisa lisikue kwa mtu wa aina hii.
g.
Kukosekana kwa maono
Makanisa mengi yasiyokuwa ni
yale yenye Viongozi wabinafsi na wasio na maono ya kiulimwengu wao hujitazama
wenyewe tu jambo hili linaweza kupelekea watu kujichokea kanisa lazima liwe na
maono ya kupeleka injili kila mahali kusikofikiwa, lazima liwaombee watu hao na
kuwawezesha kanisa linapofanya haya haliwezi kuzeeka bali linakuwa kijana,zuri
na lenye nguvu kinyume cha hapo linakomaa na mazoea huchukua nafasi na kunakua
hakuna jipya
h.
Kukosa kiongozi mwenye
uwezo mkubwa wa kimaongozi
Mchungaji anatakiwa kuwa mtu mwenye
maono makubwa imani na uwezo mkubwa wa kuongoza akiwa amejaa maombi, asiyekata
tamaa, mwenye uwezo wa kupokea maono toka kwa Mungu na kuongoza watu, Kama
katika kanisa lako hakuna mtu anaweza kufanya lolote mpaka kwa ruhusa ya
Mchungaji fahamu kabisa kanisa hilo haliwezi kukua lakini lazima Kuweko na
umoja yanapokuja maono kama ni kwa Mchungaji Viongozi wakiyaunga mkono kwa
kauli moja kunakuwa na nguvu kubwa na
kazi itafanikiwa, Kama uongozi wa Mchungaji ni dhaifu kanisa lote linakuwa
dhaifu Mchungaji akiwa na uwezo mkubwa wa kuubeba maono basi washirika
watayapokea kwa nguvu na kumuunga mkono na kumtia moyo,makanisa mengi hayakui
kwa sababu tu hayana Viongozi wenye uwezo wa kubeba Jukumu kubwa la kimaongozi
SIFA ZA MTU MWENYE KUANZISHA KANISA
Kanisa
linaweza kuanzishwa na mtu Yeyote
Kanisa linaweza kuanzishwa na mtu wa
aina yoyote anaweza kuwa Mmisheni, Mwinjilisti, Mchungaji, mtume au nabii au
mtu yeyote wa kawaida ambaye katika mpango wa Mungu amepata nafasi ya kufanya
hivyo lengo likiwa ni kumpanda Kristo katika jamii ya watu wasiomfahamu na
kuanzisha ushirika wa mahali pamoja kwa msingi huo kupenda kanisa hakuhitaji
mtu fulani maalumu sana au mwenye sifa ambazo ni za hali ya juu sana Nyakati za
kanisa la kwanza makanisa mengine mengi yalianzishwa na watu wa kawaida tu Matendo 8;4 “Lakini
wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno” kwa msingi huo hatupaswi kuogopa kuanzisha
makanisa unahitaji imani tu je unafikiri
mtu anayepaswa kuanzisha kanisa anatakiwa kuwa wa namna gani?
·
Hakuna sifa maalumu za mtu anayepaswa kuanzisha kanisa Mungu hutumia
watu wa kawaida tu
·
Mtu anaye anzisha kanisa anapaswa tu kuwa mtu anayekubalika na
watu wale anaotaka kuwafikia katika jamii na Elimu yao
·
Awe ni mtu mwenye haiba ya kuingiliana na watu wapya na kuwavutia
kwa muda mfupi tu na kuweza kuzungumza na watu wa kila aina na kila ngazi, Mtu
anayejificha, na kujitenga na watu na kutokusikia raha kuhusu watu hasa wageni
hawezi kufanikiwa katika kuifanya kazi hii
·
Awe ni mtu anayejali sana
watu na kuwajibika kwa ndani sana kuhusu matatizo yao ya binafsi watu na jamii
·
Lazima awe mtu wa Mungu yaani aliyeokolewa ingawa si lazima awe na
ujuzi sana au aliyeenda chuo.
·
Lazima awe anasukumwa na upendo wa ndani sana wa kimungu kwa ajili
ya watu wanaopotea sawa na Mchungaji
anayetafuta kondoo aliyepotea Luka
15;3-7
·
Awe mtu wa maombi Wakolosai
1;9-11,2;1-3,Efeso 3;14-19 1Wathesalonike 1;2-3 Mathayo 9;39 Yesu alisema
Ombeni ili Bwana wa mavuno atume watenda kazi katika shamba lake
·
Anatakiwa kuwa mtu wa maono na mbunifu huku akiwa na mvumilivu na
mtu asiyeweza kukata tamaa akiwa mtu wa imani kwamba anachokifanya ni mpango wa
Mungu na kuwa Mungu amemtuma kuifanya kazi hii.
Jinsi ya
kuanzisha kanisa
Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna njia maalumu
ya kuanzisha kanisa uongozi wote wa namna ya kuanzisha kanisa unaachwa kwa Roho
Mtakatifu, njia iliyotumika eneo fulani inaweza isifanya kazi katika eneo
lingine kwa msingi huo tunaweza kujifunza tu kutoka katika uzoefu wa namna watu
wengine walivyotumiwa na Mungu katika kuanza makanisa na mafanikio waliyoyapata
kutokana na njia walizozitumia wakawapata watu waliookolewa na makanisa
yakakua, tunajua kuwa kuna shuhuda nyingi sana kuwa kuanzisha kanisa ni kazi
ngumu lakini kumbuka kuwa Roho wa Mungu ndiye anayefanya kazi na mtu anaye
anzisha kanisa njia hizi hutumika katika kuanzishwa kwa makanisa.
·
Kuanzishwa kanisa kupitia Mikutano ya injili na baadaye kuwa na
mpango wa namna ya kuwatunza wale waliookolewa na kuwalisha Neno, Kumbuka kuwa
kuhubiri pakee hakutoshi ni lazima kuhubiri injili kuambatane na Kuweko kwa
mipango ya malezi ya watu wanaookolewa
·
Kuanzishwa kupitia ushuhudiaji wa mtu kwa mtu hii ni njia yenye matokeo makubwa sana kuliko
hata mkutano wa injili katika maeneo mengine na imeleta matokeo mazuri na
mahusiano mazuri yanayoweza kufungua njia ya kufanya ufuatiliaji kwa waongofu
wapya
·
Kanisa mama kugawa watu na kuanzisha tawi lingine kwa amani hii
nayo ni njia inayoweza kutumika katika kuanzisha kanisa jipya na kuyafikia
maeneo yasiyofikiwa inawezekana tu kwa wachungaji wasiojali maslahi yao
Binafsi.
·
Kuna njia nyingine yoyote inayoweza kufaa katika uanzishaji wa
kanisa basi inaweza kutumiwa katika kuanzisha kanisa
Mambo ya
kuzingatia wakati wa kupanda kanisa
1.
Hakikisha unafanya
uchunguzi wa eneo unalotaka kuanzisha kanisa (Survey).
Kufanya
survey ni jambo la msingi sana na la kibiblia kabisa wote tunakumbuka kuwa
wakati Mungu alipokuwa anataka kuwarithisha wana wa israel nchi ya kanaani
alimwamuru Musa kuwatuma watu 12 wapelelezi ili kuipeleleza nchi maana yake ni
kufanya uchunguzi kuwa nchi ile ni ya namna gani
Hesabu 13; 1-21. “BWANA akamwambia Musa, Watume baadhi ya watu
wakaipeleleze nchi ya Kanaani,ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila
kabila la baba zao tuma mmoja wa viongozi wao.’’ Hivyo kwa agizo la BWANA Musa
akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. Haya
ndiyo majinayao: Kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri, kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori,
kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Isakari, Igali
mwana wa Yosefu, kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni, kutoka kabila
la Benyamini, Palti mwana wa Rafu, kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa
Sodi, kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi, kutoka
kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali, kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana
wa Mikaeli, kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi, kutoka kabila la
Gadi, Geueli mwana wa Maki. Haya ndiyo majina ya watu ambao Musa aliwatuma
kuipeleleza nchi. Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina la Yoshua.”
Musa
alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, ‘‘Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya
vilima. Mwuone nchi ni ya namna gani na kama watu waishio humo wana nguvu au
dhaifu, iwapo ni wachache au wengi. Kwamba wanaishi katika nchi ya namna gani?
Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au
ngome? Ardhi ikoje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la?
Jitahidini kadri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.’’ (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.) Hivyo wakapanda
na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo Hamathi”.
·
Peleleza mfumo wa jamii yao
jinsi ulivyo
·
Chunguza vikwazo vya kiroho
vilivyoko katika eneo husika
·
Chunguza sheria zao na mila na
tamaduni zao
·
Mahusiano ya kifamilia katika
jamii
·
Dini na madhehebu yaliyoko
hapo
· Viwango vyao vya maadili aina ya watu, uchumi wao Lugha zao,tamaduni zao
2.
Hakikisha unaanza na eneo ambalo linapokea injili kwa urahisi
(Receptive Areas)
Jambo la
msingi katika kupenda makanisa baada ya kuwa umefanya Survey chunguza ni wapi
mavuno yako tayari kisha anzia huko ndege kubwa huanguka na kuvunjika
kunapokuwa na wing uzito au ukungu unaomfanya Pilot asione vizuri na wakati
mwingine ndege inaweza kupata ugumu wa kutua na kugonga milima kwa sababu ya kutokuona vizuri hii ni kwa sababu ya kushindwa kuona vizuri,
hali kama hii huweza kutokea wakati wa kupenda kanisa Mungu anapokutuima katika eneo fulani atakuongoza kule ambako kuna upenyo wa watu
kuipokea injili wakati mwingine atakuongoza kwa Roho wake na wakati mwingine atakuongoza kupitia
kutazama vema Matendo 10;1-23 Yohana 4;30-35 kwa msingi huo ni muhimu kugundua
maeneo ambayo injili inapokelwa kwa uarahisi na kuyafikia kwanza ili utaligundua kwa upokeaji wao wa injili na
mwitiko mkubwa wanaoonyesha kwa ujumbe wa injili
3.
Hakikisha kuwa unayafikia makundi yote
Mpango wa
Mungu ni kuwafikia watu wote kwani kwa
Mungu watu wote ni sawa ,Yeye hushughulika na watu wote na mahitaji yao na
matatizo yao kwa viwango vyovyote walivyo navyo awe masikini au tajiri,msomi au
mjinga kwea msingi huo Mungu hana upendeleo
kwa hiyo zingatia kuyafikia makundi yote kosa moja lifanywalo na watumishi
wengi sana ni kulenga kundi fulani na kuacha kundi jingine huu sio mpango wa
Mungu fikia Masikini, wafanya biashara, matajiri, wanasiasa,Viongozi, vibarua
,wasio na kazi usipendelee kundi fulani kwa ajili ya mafungu Ubaguzi ni dhambi
Yakobo 2;1-9
4.
Panda kanisa linalojitegemea (the Indigenous churches)
Moja ya
matatizo yanayoyapata makanisa mengi na kuathiri ukuaji wa makanisa hayo ni
kutegemea msaada hii ni sumu mbaya sana mchungaji au mpandaji wa kanisa lazima
ahakikishe kuwa kwa kadiri inavyowezekana anapanda kanisa linalojitegemea na
kujiendesha na kujiongoza na
kujieneza na kujitafasiria Maandiko sawa
na mazingira yake kanisa la namna hii lipande kila mahali ambako injili
hupokelewa kirahisi, sio dhambi kutegemezwa kwa sababu ni mpango wa Mungu pia
lakini msingi mzuri ni kutokutegemea watu bali kumtegemea Mungu jambo la namna
hii litakusaidia katika kuhakikisha unakuwa na kanisa lenye ufahamu wa kutosha
na linaloweza kuwa na faida kubwa katika ufalme wa Mungu kwa kazi za baadaye
Ufunguo wa kanisa linalotaka kukua lazima uwe Kanisa
linalojitegemea Self suppoting church, kanisa linalojiongoza Self governing,
Kanisa linalojieneza self propagating linalojaa roho na kujitafasiria Maandiko
kulingana na mazingira yake.
5. Hakikisha kuwa unaweka
msingi mzito wa muhimu kwa kanisa jipya
Mtu anayeanzisha kanisa anapaswa kuahakikisha kuwa
anajenga msingi imara kwa kanisa analolianzisha
msingi huo ni mafundisho mazuri na sahii kwa, Mwanzilishi wa kanisa ni
kama mjenzi na kwa msingi huo anapashwa kujenga msingi imara katika kanisa
analolianzisha kwa faida ya umaliziaji wa baadaye na ili kanisa liweze kuwa na msingi wa kukua
lazima lifundishwe majukumu ya kila mkristo na Baraka za kutimiza majukumu hayo
na waelekeze kazi na wajibu wa kanisa kwa Mungu kwa kanisa lenyewe na kwa jamii
inayolizunguka kanisa yaani kuabudu, ushirika na kuwafgikia wasiofikiwa.
6. Hakikisha kuwa unapanda
kanisa lenye nidhamu
Kanisa linalopandwa lazima liwe kanisa linaloweka
msingi wa nidhamu mbele na pia kutowaaacha wale walioanguka katika neema ya
Mungu bila kuwarejesha katika ushirika na utumishi, Mungu anachukizwa na wachungaji
wasiojali kondoo Soma Ezekieli 34,
Wagalatia 6;1-2 Mithali 24;16, Mika 7;8 1Thesalonike 5;14 Isaya 35;3 na
Waebrania 12;13 Lengo likiwa kurekebisha, kurudisha kutunza ushuhuda na
kuwaonya wengine Mungu atakupa Hekima ya kushughulikia na matatizo hayo kwa
njia mbalimbali. Aidha tujihadhari kutenga watu kwa jazba na chuki, hakikisha
unamsaidia mtu mpaka kwenye kilele cha ubora wa ugfuatiliaji usikubali kupoteza
mtu kirahisi, Yesu hakupoteza hata mmoja aliwalinda wote wale ambao amepewa na
Mungu, Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako
ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa
upotevu, ili andiko litimie.”
Na. Rev
Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima