“Je Unajua kuwa watumishi wengi sasa wanaogopa kufanya maombezi ya kuombea watu ujazo wa Roho Mtakatifu? Wasaidie ili wapate ujasiri wa kuwaombea watu wangu ili wapokee Roho Mtakatifu hii ni zawadi ya hali ya juu niliyowaahidia watu wangu lakini inakuwa kama Historia unadhani ni kwa nini? Kamote! Ahaa ni kwa sababu wengi wanajifikiri kuwa kuna watu maalumu sana wanaopaswa kufanya maombezi haya tafadhali nikumbushie watu wangu”
Yalikuwa maneno ya kuhuzunisha ya Roho wa
Mungu wakati ananisukuma kuandika kijitabu hiki kwa hivyo kiko mikononi mwako
kwa kusudi la Mungu na kwa mapenzi kamili ya Mungu, unataka nani aje kanisani
kwako au nani asaidie wakristo wengine kupokea Roho Mtakatifu? Kwa nini somo
hili linakwepwa siku za leo? Watenda kazi wengi hawajajua namna ya kuombea
wengine kumpokea Roho Mtakatifu kwa sababu hiyo nawaandikia ninyi watenda kazi ili
kwamba mfunguliwe macho na kuona umuhimu wa kuifanya huduma hii ambayo ni
mapenzi ya Mungu kabisa.
Wenzetu
nyakati za kanisa la kwanza Tangu walipotambua umuhimu wa waamini kujazwa Roho
Mtakatifu walitilia maanani sana swala zima la kufanya maombezi ili watu
wampokee Roho Mtakatifu mara tu walipoamini angalia kwa mfano Matendo 8;14-17
Biblia inasema “Na
mitume waliokuwako Yerusalem waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la
Mungu wakawapeleka Petro na Yohana ambao waliposhuka wakawaombea wampokee Roho
Mtakatifu kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao ila wamebatizwa tu kwa
jina lake Bwana Yesu Ndipo wakaweka mikono juu yao nao wakampokea Roho
Mtakatifu”
Swala la maombezi ya aina hii lilikuwa
ni swala la kawaida kwa wenzetu walikuwa na ujasiri katika huduma hii ya
maombezi kwaajili ya ujazo wa Roho Mtakatifu hawakusita!, kushuka kwa mitume
hapa kuna maana zaidi ya kumuunga mkono Filipo na kuonyesha kushirikiana naye
katika huduma hii swala hili halina maana ya kutuambia kuwa ni watu maalumu tu
wenye mamlaka ya kuombea wengine kumpokea Roho tunachoweza kusema ni kuwa
mitume waliona umuhimu mkubwa sana kwa watu kupokea Roho walikuwa na shauku
kile walichokipokea na wengine wakipokee.
Kwa muhktasari tunaweza kusema kuwa Roho
Mtakatifu ni Suluhisho la matatizo yoote katika kanisa au kiboko cha matatizo
yoote na hii ndio maana Nyakati za kanisa la kwanza alipewa kipaumbele
kinachostahiki Luka 24;49 Matendo1;8. Nyakati za kanisa la kwanza swala la Roho
Mtakatifu lilipewa kipaumbele kama swala la sala ya toba Matendo 8;14 na 19;1-7
Je mlimpokea Roho takatifu hapo mlipoamini? Lilikuwa moja ya maswali ya muhimu
sana alilouliza Paulo mtume katika kutaka kuthibitisha kuwa washirika wake
wanakuwa imara katika maswala ya kiroho je wakati wa leo tunatoa nafasi kwa
kiasi gani kwa Roho Mtakatifu kupokelewa katika kanisa Bwana anahuzunika sana
anapoona tumeacha sio tu kuombea lakini hata kufundisha kuhusu Roho Mtakatifu
limekuwa swala adimu sana.
Wengi
wanaogopa wanafikiri kuwa wanaweza kuita watu kupokea Roho Mtakatifu kisha
kusitokee lolote Huku ni kukosa Imani na kusababbisha matatizo katika kanisa la
Mungu kama kuna upungufu wa aina yoyote leo katika kanisa basi tunapaswa kurudi
kwenye msingi na kujiuliza kwa ni nini wenzetu walimpa kipaumbele hii ni kwa
sababu walijua kuwa; Roho Mtakatifu ni suluhisho kwa tatizo la Kimaongozi Ni
suluhisho la uadui Ni suluhisho la uonevu, suluhisho la upinzani wa kidini Ni
suluhisho dhidi ya nguvu za giza uchawi, Ni suluhisho dhidi ya mateso na uonevu
wa Ibilisi Ni suluhisho kwa woga kukata tamaa na kukabiliana na changamoto za
ulimwengu huu, Nisuluhisho la hekima tunapokuwa katika hali ya kutokujua nini
cha kufanya, Ni suluhisho la kutokuweko kwa Karama za Rohoni kwa msingi huo
somo hili msikilizaji wangu linakusudia ili uwe Baraka katika maisha yako ya
huduma na utumishi naaminikuwa ni kwa ufupi lakini Baraka zake zitakuwa kubwa
sana utahisi uwepo wa Mungu tangu unapoanza kufuatilia habari hizi za Roho Mtakatifu
na namna ya kuwasaidia watu kupokea Ubarikiwe na Bwana Ndimi mjoli mwenzenu
shambani mwa Bwana Mchungaji Innocent Kamote.
SURA
YA KWANZA: MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA.
Kabla ya kujadili kuhusu hatua za
kumuongoza mtu anayetaka kubatizwa katika Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza ni
muhimu kwetu kuzingatia maswala muhimu yafuatayo. Kwanza ni nani anaweza
kujazwa na Roho Mtakatifu, Pili ni nani anaweza kuomba na wengine kumpokea Roho
Mtakatifu na Tatu Mambo yanayoambatana na kumpokea Roho Mtakatifu.
Kwanza Ni nani anaweza kujazwa Na Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu ni ahadi ya Mungu
Baba na inaweza kupokewa na mtu yeyote aliyezaliwa mara ya pili yaani
aliyeokoka, hili ni jambo la msingi. Kwa msingi huo kupokea Roho Mtakatifu sio
swala la wakristo waliofikia ngazi Fulani ya kiroho au waliookoka muda mrefu a
kufikia ukomavu Fulani wa kiroho wala sio kwa daraja la watu Fulani muhimu
katika dhehebu Fulani ni ahadi ya Mungu kwa wakristo wote wamjiao Bwana kwa
kila kizazi Matendo ya Mitume 2;17-18,38-39.
Pili Ni nani anaweza kuomba Na wengine kumpokea Roho Mtakatifu
Kumbuka kuwa swala la
kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu pia sio la watu Fulani maalumu hili ni
la kila mtu ambaye amekwisha jazwa nguvu na kumpokea Roho Mtakatifu na sharti
la kutaka kuwaombea wengine ujazo wa Roho Mtakatifu ni kutamani kuona wengine
wakipokea ahadi hii yenye Baraka na kufurahia kuona wengine wakibarikiwa na
kutumiwa na Mungu Matendo 8;14-17.
Mambo yanayoambatana na kumpokea Roho Mtakatifu.
Ni muhimu kwa kila
mtenda kazi kuwa na ufahamu kwamba kuna maswala matano muhimu yanayohusika kama
ishara ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu maswala hayo ni shauku au hamu, Imani,
maombi, utii, na kujiachilia katika neema ya Mungu.
1. Shauku au Hamu.
Biblia inakazia umuhimu wa kuwa na kiu au shaku au hamu Biblia
inasema “Heri
wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa” Mathayo 5;6, mtu mwenye njaa na kiu humtafuta
Mungu kwa Bidii na kila unapomtafuta Mungu kwa bidii hupatikana Yeremia 29;13,”Nanyi mtanitafuta na
kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu
wote”
Tafuteni nanyi mtaona Luka 11:9 Mtu awaye yote mwenye kiu na hamu na shauku na
kuvumilia katika kutamani kuendelea kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu atapewa,
kwa hiyo kiu na hamu au shauku ni ya Muhimu sana.
2. Imani.
Imani ni nguzo ya msingi na muhimu katika kupokea nguvu za Roho
Mtakatifu au kiu chochote kutoka kwa Mungu, Paulo anawakumbusha wakristo wa
Galatia kuwa walimpokea Roho Mtakatifu kwa imani na sio kwa kutokana na matendo
ya sheria ni kwa kuamini Wagalatia 3;2 Yesu alisema yeyote Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji
yaliyo hai (yaani Roho Mtakatifu) atatiririka ndani yake Yohana 7;38 kwa msingi
huo ni wajibu wa kila mtu anayetaka kuwaombea wengine ujazo wa Roho Mtakatifu
kuwapandisha wapokeaji wake imani
3. Maombi.
Roho Mtakatifu hutolewa kama jibu la maombi yanayoambatana na
imani, Yesu alisema ombeni nanyi mtapewa Luka 11;9, sehemu nyingine alifundisha
akisema kila muombalo aminini ya kuwa limekuwa lenu Marko 11;24-25, Kumbuka
kuwa wakati Yesu alipokuwa anaomba ndipo Roho alipompaka mafuta Luka 3;21-22,
ni jambo kama hilo liliwatokea wanafunzi siku ya Pentekoste walikuwa
wamejifungia wakiomba Matendo 1;14, Kabla Paulo mtume hajajazwa Roho alikuwa na
Muda wa kuomba Matendo 9;11 kwa msingi huo kila mtu anayetaka kujazwa na nguvu
za Roho Mtakatifu anapaswa kuomba kwa bidii na kwa sauti kubwa.
4. Utii.
Moyo wa utii ni wa muhimu sana katika kumpokea Roho Mtakatifu,
Petro alisema Mungu anampa Roho Mtakatifu kwa wote wamtiio Matendo 5; 32,
alikuwa akizungumza kuhusu wale watakaomtii Mungu na kuiamini injili yake
Mstari 29-32 na kusudi la msingi la kumpokea Roho Mtakatifu pia ni kwaajili ya
kushuhudia Matendo 1;8 na Mungu Yuko tayari kumpa nguvu kila mtu ambaye yuko
tayari kwaajili ya kazi yake na kutii agizo kuu.
5. Kujiachilia katika neema ya Mungu.
Kujiachilia kwa Mungu au kujinyenyekeza ni moja ya hatua nyingine muhimu
katika kumpokea Roho Mtakatifu, Kama ilivyo kwa mtu anayebatizwa katika maji
anapaswa kujinyenyekeza kwa Mchungaji anyembatiza, Kujazwa kwa Roho Mtakatifu
nako kwahitajiwa kwa mtu kujiachilia katika neema ya Mungu ni lazima ukubali
kufuata maelekezo ya Bwana huku ni kujiachia Mwili nafsi na roho Warumi 6:13,
12:1 ni kwa kupitia kujitoa na kujinyenyekeza katika neema yake ndipo Roho wa
Mungu anachukua nafasi na hatimaye kukuwezesha kuzungumza kwa lugha.
HATUA
ZA NAMNA YA KUMUOMBEA MTU ILI AMPOKEE ROHO MTAKATIFU
Hapa naweza kupendekeza hatua
tatu za kichungaji za kuweza kumuombea mtu akampokea Roho Mtakatifu aina hizi
za maombi ni pamoja na mahojiano, kuingia katika maombezi, na Muongozo kabla ya
maombi
1.
Hatua
za mahojiano.
Endapo utatumia
njia hii ya majojiano latika kutaka kumuombea mtu ujazo wa Roho Mtakatifu
unapaswa kuzingatia maswala muhimu manne kwanza ikiwa ni pamoja na kustawisha
uhusiano mwema na muhitaji yaani kutafuta kujenga mahusiano naye kisha
utatakiwa kumshawishi na kuikuza imani ya muhitaji na tatu unatakiwa kuelewa au
kugundua hali halisi ya muhitaji kuwa ana kiu kiasi gani na mwisho utamfundisha
muhitaji kipi anatakiwa akifanye ili apokee Roho Mtakatifu.
§
Kustawisha uhusiano hili ni kusudi la kwanza kabisa
katika kifikia hatua ya kumpokea Roho unapaswa kuwa umemfahamu vema na kama
yeye hakufahamu ni vema na yeye akakufahamu unaweza kuzungumza jambo ambalo
litamfanya yeye kujisikia vema na salama, kisha mpe nafasi ya kujieleza kila
anachokihitaji msikilize vema kila anachokieleza na wakati wote tumia jina lake
kila unapowasiliana naye.
§
Chochea na kukuza imani yeke ni muhimu sana
kjaribu kuinua imani ya muhitaji na kuichochea unaweza kumueleza jinsi
unavyofurahishwa na jinsi alivyoitikia swala la kuja kumpokea Roho Mtakatifu,
umefanya uamuzi ulio sahii sana unaweza pia kumuhakikishia kuwa hii itakuwa
siku ya kihistoria katika maisha yake na kuwa Mungu ana kitu maalumu sana
kwaajili yake na inawezekana kuwa
muhitaji anaweza asiwe na ujuzi kuhusu hilo lakini kwa ujumla linamuandaa
katika kufungua moyo wake kumpokea Roho Mtakatifu.
§
Gundua hali halisi ya muhitaji moja ya mambo
muhimu ya kutafuta wakati huu ni kujua kwanini muhitaji amekuja mbele na
kugundua uthamani na uelewa wake na kuwa yuko kiwango gani cha kiroho unaweza
kumuhoji swali kama je unahisi umekuja kujazwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu?
Usihisi Bali tambua ya kuwa amekuja kujazwa anaweza kuwa amekuja kwa sababu
nyingine kwa hiyo unaweza kujenga imani yeke kuwa kupokea hili kunaweza kuwa
suluhu pia la mahitaji yake mengine. Mengi ya maelekezo haya pia huweza
kutolewa kwa njia ya mahubiri au wakati wa huduma ya madhabahuni.unaweza pia
kumuuliza kama aliwahi kujazwa kabla na kama aliwahi kujazwa kabla anaweza
kukushirikisha ilivyokuwa japo kwa mukhtasari na kama hakuwa amejazwa atahitaji
kujazwa anahitaji maelekezo zaidi. Unaweza pia kumuuliza kama alishawahi
kumuona mtu aliyejazwa kwa Roho Mtakatifu anaweza kuwa na wazo sahii ya kile
anachokitegemea na kama sivyo anahitaji ufafanuzi zaidi endapo utakuwa umemaliza
kumuuliza maswali haya na kumsikiliza vema na kujibu maswali yake vemandipo
itakapokuwa rahisi kwako kumpeleka katika hatua nyingine.
§
Mafundisho wakati huu sasa mtenda kazi wa Bwana
utatakiwa kufanya maswala ya msingi mawili moja likiwa ni kuchochea imani ya
muhitaji katika moyo wake na kumleta sasa katika uelewa halisi wa nini
anatakiwa kukifanya na nini kitatokea
wakati tendo la kujazwa Roho linapotokea kuichochea imani ya muhitaji ni pamoja
na kumuhakikishia kuwa hii ni ahadi ya Mungu na kuwa Mungu yuko tayari na kuwa
kama amezaliwa mara ya pili Mungu atamjaza kwa Roho wake mkumbushe swala la
kuomba Luka 11;9-10 na kuwa anapaswa kuamini na kutegemea kuwa atapokea na
atanena kwa lugha nyingine kama matokeo ya kuwa Roho anamuwezesha.Mkumbushe
kujiandaa na kuwa anapaswa kutambua kuwa kujazwa Roho sio swala gumu na kuwa ni
jambo la kawaida kwa wakristo na kuwa hatapokea roho nyingine bali Roho halisi wa
Mungu Ukimuomba Munu baba mkate hawezi kukupa jiwe na kuwa kujazwa Roho ni
rahisi tu ni kama kupuliziwa pumzi Yohana 20;22. Mkumbushe pia kuwa Roho huyo
hayuko mbali kwani alishakaa ndani yake tangu siku aliyookoka kisha muhitaji
anapaswa kujua kuwa nini kitatokea hivyo mwambie kuwa tutaomba pamoja kisha
nitakuongoza katika maombi yatakayokusaidia kubatizwa katika Roho Mtakatifu
tunachotakiwa ni kumuomba Mungu aje na kutubatiza kwa Roho wake Mtakatifu na
Mungu ni lazima atatusikia kwa sababu tunaomba sawa na mapenzi yake 1Yohana
5;14 na wakati huu ni muhimu sana kuwa na usikivu mkubwa kwa Roho Mtakatifu na
utahisi ujio wake. Na kisha baada ya hilo itakupasa kuchukua hatua ya imani ya
kumpokea Roho na kisha nitakuombea na utapokea Marko 11;24 na mara utakapopokea
utasema kwa lugha mpya linapotokea hilo usiogope endelea kujiachilia katika
neema yake. Muulize kama ana swali lolote na kama hakuna ingieni katika maombi.
2.
Hatua
ya Maombezi.
Katika hatua ya
maombezi utapaswa kuzingatia maswala muhimu mawili utamuongoza muhitaji kuingia
katika maombi ya kumuomba Mungu amjaze kwa Roho Mtakatifu na pia utainua imani
yake kwa kumuongoza kumpokea Roho Mtakatifu.
§
Muongoze muhitaji katika kuomba kama
unavyomuongoza mtu kumpokea Yesu sasa unaweza kumuongoza muhitaji katika
kumuomba Roho Mtakatifu Bwana mwema nimekuja mbele zako sasa na mbele za Roho
wako sasa sina ninalohitaji katika maisha yangu sasa zaidi ya ahadi yako
nategemea utanihurumia utanipa kibali na utanijaza kwa Roho wako niwezeshe
nijaze kwa Roho wako mwambie Bwana nijaze kwa Roho wako jiachilie kwake paaza
sauti omba tarajia uwepo wake sasa.
§
Muongoze muhitaji katika hatua ya imani anaweza
kuinua mokono yake juu na kuomba kwa imani
nawe waombee wapokee Roho sasa na unapoiona imani yao iko juu amuru
wapokee sasa atahisi uwepo wa Mungu kwa ndani sana na ataanza kunena kwa lugha bila kutumia
akili kunena huko hakutakuwa kwa kulazimisha kunakuja tu kama matokeo ya Roho
wa Mungu kuja ju yake na inapotokea watie moyo kuwa wasiogope bali waendelee
kujiachia katika uwepo wa Mungu mwili nafsi na roho na anaponena kwa lugha tia
moyo ili waendelee waache kwa muda waendelee kunena kwa lugha ni raha iliyoje
kwani wakti huu sasa unajua kuwa Mungu amemuhudumia muhitaji.
3.
Muongozo
kabla ya maombi.
Ni muhimu sana
kufanya au kutoa ushauri kabla ya maombi kwa muhitaji kama amekwisha kujazwa na
Roho Mtakatifu utampa aina ya ushauri na kama hajajazwa pia atahitaji aina moja
ya ushauri
§
Kama amepokea Ujazo wa Roho Mtakatifu na kunena
kwa lugha ushauri ufuatao utamfaa sana Mweleze kuwa kumpokea Roho hakujaishia
hapo kwani jukumu kubwa la kumpokea Roho Mtakatifu ni kwa kusudil a kumtumikia kwa
hivyo huu sio mwisho bali ndio mwanzo Mungu sasa ataanza kukutumia kwa nguu
sana unaposhuhudia unapoomba na kuombea wengine kwa msingi huo una wajibu wa
kushuhudia wengine na kuendelea kuomba katika Roho haya yatakupa nguvu
kubwa kila siku katika maisha yako pia
usisahau kuendelea kujisomea Neno la Mungu.
§
Kama muhitaji ahajapokea unapashwa kumpa ushauri huu kwamba usikate
tamaa kwa sababu hukumpokea Roho wakati huu kumbuka kuwa ahadi ya Yesu Kristo
ni dhahiri na ni kwa kila mtu aliyempokea Luka 11;10 kwa hivyo endelea komba na
kutafuta na utapokea kama Mungu apendavyo hata ukiwa popote Luka 11;9
SURA
YA TATU: MAMBO YA MSINGI YA KUYAZINGATIA
Tunapokwenda kumalizia kijitabu hiki naona ni muhimu
nikikukumbusha kwa ufupi maswala matatu ya kuyazingatia unapomuongoza mtu
kumpokea Roho Mtakatifu
1. Ni muhimu kuwa na ujuzi wa kile Biblia
inachokisema kuhusu somo hili
Ni muhimu
kufahamu kuwa kama mtu anapenda kusaidia wengine kwa kusudi la kumpokea Roho
Mtakatifu anapaswa kufahamu na kutafuta kujua kwa undani kuhusu somo la Roho
Mtakatifu na hivyo atapaswa kusoma neno la Mungu hususani kitabu cha Matendo ya
mitume ili kuona somo hili kivitendo na pia anaweza kusoma Vitabu vingine
vizuri vinavyozungumzia kwa undani kuhusu Roho Mtakatifu kwa kadiri mtu anavyomjua
Roho Mtakatifu na kazi zake na utendaji
wake katika maisha ya waamini na umuhimu
wake ndivyo anavyokuwa msaada mkubwa na Baraka katika swala hili.
2.
Usikubali
uvivu wa kiroho ukuharibie wajibu wako
Kama unasaidia
watu kumpokea Roho Mtakatifu ni lazima uhakikishe kuwa unaacha uvivu wa Kiroho
kwa sababu sio kazi rahisi kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu na ndio
maana wengine wanaona aibu kufundisha somo hili na kutokujishuhulisha kuwafanya
wengine wapokee Roho Mtakatifu na kama una tabia hii unapaswa kutubu, tubia
uvivu wa Kiroho ulionao na jitoe kwa ukamilifu katika huduma na Mungu
atakutumia
3.
Laizima
ufikie ngazi ya kujihusisha sana.
Mwisho msomaji
wangu ni muhimukufahamu kuwa kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu
kunaambatana na kufikia ngazi ya kujihusisha
sana na kutaka wengine wajazwe hili ni swala linalohitaji kujituma na
kumaanisha na kuhurumia na kutia moyo wengine kupokea Roho wa Mungu uwe na
Bidii katika kuomba na hapo utakuwa na mafanikio, sasa tunafikia mwisho wa somo letu la jinsi ya
kumuongoza mtu kupokea Roho Mtakatifu Ni matumaini yangu kuwa sasa utajiweka
wakfu katika kazi hii muhimu kama nini na hii ndio kiu kubwa tuliyonayo
kuwasaidia watu wajazwe na kuishi katika uwepo na nguvu za Roho wake siku zote
za maisha yao Mungu akubariki ni matumaini yangu somo hili litakuwa Baraka na
kuwa utalitendea kazi na kulifanya halisi katika maisha yako ya huduma na kuwa
tangu sasa utakuwa ukiwafanyia watu maombezi ya kumpokea Roho Mtakatifu bila
woga ubarikiwe na Bwana Neema yake iwe juu yako Amen!.
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
ikamote@facebook.com
0718990796
0784394550
Maoni 14 :
mtumishi BWANA Yesu apewe sifa , tafadhari ninaomba unitumie somo hili kuhusu roho mtakatifu katika e mail yangu eddowk2010@yahoo.com
Ubarikiwe.
Edward.
Bwana yesu asifiwe nimepata ujumbe mzuri nimebarikiwa na mimi natamani nijazwe na roho mtakatifu na nipate macho ya rohoni
amina
selinapius840@gmail.com
Namba zako hazipatikani
Asifiwe Yesu Mtumishi wa Mungu..Mwenyezi-Mungu akubariki sana na azidi kukutia nguvu za kueneza ujumbe wake..
Bwana wetu yesu kristo asifiwe ubalikiwe sana mtumishi kwa somo zuri ninaomba unitumie hili somo pia Nina swali apo me nataka kujazwa Bila kuombewa au kuwekewa mikono je inawezekana au
Naombaa kutumiwa masomo ya Roho mtakatifu kupitia email yangu
MUNGU AKUBARIKI
Nahitaji zaidi masomo ya roho mtakatifu saidilaurent8@gmail.com contact of Sim 0742377340
Naitwa Laurent saidilaurent8@gmail.com nahtj masomo ya roho mtakatifu
Nimesoma na kuelewa kile Mungu alikupa kuongea na Watumishi wake. Ubarikiwe sana kwa kazi hii ya Uandishi
Nimebarikiwa
Ujumbe maridhawa
Ubarikiwee zaidi na zaidi minister....Yesu azidi kukuinua viwango na viwango kwenye huduma
Ubarkiwe umenikuza kiroho
Chapisha Maoni