UTANGULIZI
Karne tisa kabla ya kuzaliwa kwa Yesu
Kristo nchini Israel kulikuwa na ukengeufu mkubwa kwani watu wengi waliiacha
imani, waliacha kumcha Mungu na Mungu aliruhusu vita pamoja na mateso ya aina
mbalimbali, kwa ujumla ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Israel, Washami walikuwa
wameivamia Israel na kuizingira pande zote, na walikuwa wakitafuta kila iwezekanavyo kuangamiza kila
kilichosalia katika jeshi la Israel, habari hizi zilikuwa zikienea mji kwa mji
hofu ilitawala katika kila eneo watu
wakihofia kupoteza kila walicho nacho, Hatimaye siku moja ilisikiwa kuwa washami
wanauvamia mji wa Dothan, kwa msingi huo mapema alifajiri mtumishi wa nabii
Elisha aliamka kwenda kuthibitisha kama habari hizo ni kweli na aliona jeshi kubwa sana la washami wakiwa
wameuzingira mji pande zote kwa mshangao alipiga kelele Ole wangu Bwana wangu
tunaangamia tutafanya nini? Elisha alijibu kwa kumthibitishia mtumishi wake “Usiogope kwani walio upande wetu ni
wengi kuliko wao” Mpaka wakati huu mtumishi
alikuwa bado hajatia akilini kuwa bwana wake alikuwa anamaanisha nini Elisha
aliomba maombi mafupi ili kwamba bwana amfungue macho 2Wafalme 6;13-17 mara
moja mtumishi wa Elisha alifunguliwa macho yake
na aliona jeshi kubwa sana la kiroho (Malaika), hata ingawa jeshi la
washami lilipozwa na Israel walipata ushindi wa bila mapigano lakini tunapata
ufunuo mkubwa wa kuweko kwa kundi kubwa la malaika wanaowahudumia wale
wanaourithi wokovu.Ikiwa huduma hii kubwa ya malaika ilikuwa hivi wakati wa
Elisha ni muhimu kufahamu kuwa nyakati
za agano jipya sisi tuko chini ya agano lililo bora zaidi na roho hawa hutumwa
kwaajili ya kutuhudumia Biblia inasema hivi katika Waebrania 1;13-14 “ Je yuko
malaika aliyemwambia wakati wowote Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka
adui zako chini ya nyayo zako? Je hao
wote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Agano jipya
pia linatupa ufunuo Fulani kuhusu malaika na huduma zao aidha, Paulo mtume alikuwa akiwafundisha
wakristo kule Efeso kuwa na Ufahamu kuhusu maswala ya ulimwengu wa kiroho,
Waefeso 6;10-18, Ulimwengu wa kiroho una majeshi makubwa ya makundi ya malaika
, makundi haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, Malaika wateule yaani
wale walioonyesha utii kwa Mungu walipopata nafasi ya kutumia utashi wao na
kundi linguine ni la malaika walioasi hili ni kundi lenye asili ya moja ya tatu
1/3 kutoka katika kundi la malaika wateule lakini waliamua kwa utashi wao
kumfuata shetani na hivyo kuwa pamoja na shetani na kumtumikia yeye na kupewa majina mengi yanayofanana na
utendaji wao wa kazi majina waliyopewa ni Mashetani, majini, mapepo, roho
chafu, maruhani, na kadhalika, jina linalotumika katika Biblia kuhusu viumbe
hao ni Pepo wachafu, hili ndilo tutakalolitumia zaidi katika kitabu hiki au
somo hili. Ni jambo la furaha sana kujifunza kuhusu malaika.
Biblia inasema pia Atakuagizia
malaika zake wakulinde katika njia zako zote Zaburi 91;11 Kumbe wako viumbe
ambao wamewekwa na Mungu kwa shughuli
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa watu wa Mungu, wakati lile kundi la
pili si kundi jema wao wapo kwa ajili ya kudhuru, kushawishi kutenda uovu,
kukatisha tamaa na kuwapinga wanadamu wenye asili ya uumbaji wa Mungu kwa sura
na mfano wake wakitesa na kuua na kuharibu, haya sio mawazo ya kipuuzi kama
wanavyofikiri wana sayansi ambao
hawaamini katika mambo yasiyoweza kupimwa na kuthibitika kwa kuonekana kwa
macho, wazo kuhusu viumbe vya kiroho yaani malaika ni wazo la kweli na pia kuhusu uwepo wa pepo ni wazo la kweli
na so ushirikina kwani Neno la Mungu linatufundisha hivyo. Ni imani yangu kuwa
Mungu ata kusaidia kupitia Roho wake mtakatifu ili uweze kuelewa na kupata
ufahamu wa kutosha kuhusu malaika.
***********************************************************
Neno au jina malaika lina asili
ya kiyunani ambayo ina maana pana kadhaa
jina hilo kwa kiingereza ni Angel
ambalo limetokana na jina la kiyunani Angelos
(Angelos)ambalo
lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) ambalo pia maana yake
ni mjumbe wa Mungu lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa kumaanisha
maswala kadhaa yafuatayo;-
·
Neno hili angelos lilitumika pia kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa” na matumizi kama
hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika
Matendo 12;15 ambapo wanafunzi walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga
mlango hii ni kwa sababu kimsingi wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na
isingeliwezekana kutoka gerezani na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama
vile hii ni kwa sababu walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa
Yakobo pamoja na kuwa waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro
kuweza kuwa hai. Jambo lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa
kama malaika kwa msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia
ilimaanisha wazi kutumiwa kama neno malaika.
·
Neno malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe wa Mungu aliye mwanadamu” mfano
katika ufunuo 2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu
inakisiwa kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani wajumbe
ambao wanabeba gombo la chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa
ambayo Yohana alikuwa akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa
na ufunuo 1;11, ambapo agizo linaonyesha
kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo ukayapeleke kwa hayo makanisa
saba Efeso, na Simirna, na Pergamo na Thiatira, na Sard na Filadelfia
na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano wale waliopeleka magombo
hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa inamaanisha viongozi
wa kila kanisa ambao husimamia makanisa
na huwasomea watu maandiko kama ilivyokuwa wakati wa matumizi ya
masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza kazi ya kiongozi ilikuwa ni
kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo walikuwa ni watu wanaowajibika
kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo viongozi hao pia waliitwa malaika
yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha
viumbe wa kiroho wa Mungu ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa
yale na imani hii ina mzizi katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa
malaika wa kila eneo, na pia kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya
mbinguni hapa duniani.
·
Kwa msingi huo sasa tunapojifunza somo hili
Angelology inamaana ya angelos-logos
yaani Elimu kuhusu malaika au Ufahamu kuhusu malaika
·
Malaika ambao tunajifunza habari zao ni viumbe
wa kiroho wenye maadili na uwezo mkubwa
wa Ufahamu ambao hawana miili ya kibinadamu na wale wa aina hiyo lakini wakaasi
na kuitwa mashetani kwa msingi huo somo hili halitahusu aina nyingine za
malaika zile ambazo zimetwajwa hapo juu kama roho ya waliokufa, wanadamu,
wasomaji maandiko , wasimamizi wa kanisa au sinagogi au wachungaji ama kanisa
lenyewe ambalo humwakilisha Mungu duniani
·
Malaika pia wana majina kadhaa katika maandiko
kama vile Wana wa Mungu Ayubu 1;6,2;1,Watakatifu Zaburi 89;5,7. Roho Waebrania
1;14, Walinzi Daniel 4;13,17,23,Enzi, Falme , mamlaka na usultani Wakolosai
1;16 na nguvu Waefeso 1;21.
MALAIKA WALIUMBWA LINI?
Malaika kuna
uwezekano mkubwa kabisa kuwa waliumbwa kabla ya siku saba za uumbaji ‘Basi
mbingu zikakamilika na jeshi lake lote’ Mwanzo 2;1 ni muhimu kufahamu kuwa jeshi wakati mwingi
humaanisha viumbe vya kiroho au mbinguni, lakini mtu anaweza kubisha kutokana
na andiko hili Kutoka 20;11 ambao unasema Katika siku sita Mungu aliziumba
mbingu na nchi na vyote viujazavyo na siku ya saba akapumzika kwa hiyo mtu
anaweza kudai kuwa malaika nao waliumbwa ndani ya siku sita za uumbaji.
Ni muhimu kufahamu kuwa tunaweza kupata vidokezo mkuhusu kuumbwa kwa
malaika kabla ya ndani ya siku sita tunaposoma Mwanzo 1;1 Biblia inasema hapo
mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi na mara baada ya kulisoma hili ndipo
tunapata taarifa kuwa nao ulimwengu ulikuwa mkiwa tena, utupu…’ lakini wakati
huu hatuambiwi kitu kuhusu mbinguni Mwanzo 1;2 hivyo huenda ni wazi kuwa Mungu
alikuwa tayari amekwisha kushughulika na uumbaji kuhusu Mbingu na alikuwa tayari
amekwisha weka uataratibu unaokusudiwa Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja
na wana wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha
ni wakati gani wakati misingi ya dunia ilipowekwa Ayubu 38;6-7. Kama malaika walishangilia
wakati Mungu alipouumba ulimwengu ni wazi kuwa malaika waliumbwa mapema kabla
ya ulimwengu, lakini kwa ujumla wake Mungu hatupi uwazi sana kuhusu alivyoumba
malaika swala kama hili laweza kuwa siri Kumbukumbu 29;29. Hata hivyo tunapata
vidokezo kadhaa kuhusu malaika Kwa mafano shetani alitokea na kumjaribu Hawa
Mwazo 3;1 pia tunaambiwa kuwa kuna baadhi ya malaika waliasi 2Petro 2;4, Yuda 6,
lakini maandiko haya hayatupi uwazi kamili lini malaika waliumbwa na kufanya
maasi hayo, hususani pale Mungu anaposema tazama kila kitu kimekuwa chema
Mwanzo 1;31 lakini ni wazi kuwa waliumbwa kabla ya wanadamu au kabla ya
ulimwengu .
A.
Malaika
ni viumbe.
Tunaposema
kuwa malaika ni viumbe maana yake wameumbwa na Mungu kwa neno lake pasipo
chanzo chochote ni kwa nguvu za Mungu,
hatuambiwi kuwa waliumbwa wakati gani, lakini ni wazi kuwa waliumbwa kabla ya
wanadamu, wamekuweko muda mrefu sana na
baadhi yao walioasi wamekuwa chini ya shetani 2Petro 2;4 Yuda 6 kwa msingi huo tuna aina
mbili kuu za malaika wema na wabaya ,Kama viumbe malaika hawakubali kuabudiwa
Ufunuo 19;10,22;8-9 na mwanadamu kwa sehemu yake amekatazwa kuwaabudu malaika
Wakolosai 2;18.Paulo anaeleza kuwa Mungu aliumba vyote vinavyoonekana na
visivyoonekana hii ikimaanisha kuwa ni
pamoja na malaika Wakolosai 1;16, Ezara alisema Wewe Bwana peke yako umeumba
mbingu na nchi na mbingu za mbingu na jeshi lake lote, Malaika wana uwezo
mkubwa kiakili na hutumwa kuzungumza na wanadamu kama maandiko yasemavyo
Mathayo 28;5,Matendo 12;6-11, na huimba na kumsifu Mungu Ufunuo 4;11,5;11
B.
Malaika
ni viumbe vya kiroho.
Malaika ni
viumbe wa kiroho, sio kama wanadamu, hawafungwi na mipaka ya kibinadamu,au
asili ya kawaida, wanatokea na kupotea kama watakavyo, wanauwezo wa kusafiri
kwa kasi ya kushangaza bila kutumia njia za kawaida za asili, na ingawa ni roho
wana nguvu ya kuchukua miili ya kibinadamu ili kwamba waweze kuonekana katika
muonekano unaoleta maana kwa mwanadamu Mwanzo 19;1-3, Malaika hata hivyo ni
viumbe bvya kiroho ambao hutumwa kuwahudumia wale watakao urithi wokovu
Waebrania 1;14, kwa kuwa ni viumbe vya kiroho hatuwezi kuwaona kwa macho
isipokuwa Mungu anapotupa uweza maalumu kuweza kuwaona Hesabu 23;31, 2Wafalme
6;17, Luka 2;13, ni wenye kuongoza na kulinda na pia hujiunga pamoja nasi
katika kuabudu Waebrania 12;22, hawawezi kuonekana lakini katika wakati Fulani
hutumia huchukua miili ya kibinadamu ili kutokea Mathayo 28;5, Waebrania 13;2.
C.
Malaika
wana miili ya kudumu.
Malaika tayari wana miili ya
milele, au miili ya kudumu kwa msingi huo kifo hakiwawezi, Luka 20; 34-35 Yesu
aliwafafanulia masadukayo ambao walikuwa hawaamini katika ufufuo kwamba
watakatifu watakao fufuliwa watakuwa kama malaika wa Mungu kwa maana kuwa
hawataweza kufa tena
D.
Malaika
hawahesabiki.
Maandiko yanatufundisha wazi kuwa
idadi yao ni kubwa mno Maelfu elfu…na makumi elfu mara kumi elfu, Daniel
7;10,majeshi zaidi ya kumi na mbili ya malaika, Mathayo 26;53 Jeshi kubwa la
mbinguni, Luka 12;22Kundi kubwa la malaika, Waebrania 12;22, Muumba wao na
Bwana wao kwa hiyo anatajwa kama Bwana wa majeshi.
E.
Malaika
hawana viungo (Via) vya Uzazi.
Malaika siku zote wanaelezwa kama
wanaume lakini katika hali halisi hawana via vya uzazi na kwa sababu hiyo
hawana uwezo wa kuzaliana Luka 20; 34-35. Wala hawana uhusiano wa kama familia
za wanadamu na kwakuwa maandiko hayaweki wazi zaidi kuhusu via vya uzazi au
uwezo wa kuzaa na wanadamu ni muhimu kukaa kimya badala ya kujaribu kubuni
mambo yasiyokuwa ya uhakika.
F.
Malaika
na tabia za ainabinadamu.
Kwa kawaida malaika huwatokea
watu wakiwa na umbile la kibinadamu isipokuwa Maserafi tu kama tnavyoona katika
Kitabu cha Isaya 6;2, hawana tabia ya kujitokeza kama wanyama hata kidogo, wala
kitu wala moto au nyani ama aina ya mnyama awaye yote, Hakuna pia nukuu katika
maandiko inayoonyesha malaika wema wakimtokea mtu muovu Mathayo 24;37-39 siku
zote malaika wema huwatokea watu wema, Malaika wamewahi kumtokea Abrahamu, Musa,
Daudi, Daniel, Yesu, Petro, Paulo, Filipo na wengineo, na kila wakati malaika
wamejitokeza kama wanaume na sio wanawake au watoto na siku zote wanakuwa
wamevaa nguo na sio uchi. Kama Kristo alivyojifananisha na wanadamu kwa
kuchukua mwili wa kibinadamu Incarnation Malaika huutwaa mwili wa kibinadamu
kwa muda wanapotaka kujidhihirishwa kwa wanadamu na hujitokeza katika namna
ambayo unaweza kufikiri ni wanadamu,Abrahamu aliwahudumia malaika watatu na
kuwaandalia chakula cha jioni wakizunumza katika hali ya kawaida na mmoja akiwa
amebakia kuzungumza nae wawili walielekea Sodoma na kuwa na Muda na Lutu Mwanzo
18;2,19;1, kupitia tukio hili mwandishi wa kitabu cha waebrania anatuasa kuwa
makini kuwakarimu wageni Waebrania 13;2, Yoshua kabla ya kuinia kanaani kivita
Mtu mmoja alisimama akiwa na upanga na huyu alikuwa Malaika wa Bwana! Yoshua
5;3 Gidion halikadhalika hakujua kuwa mtu aliyekuwa akizungumza nae alikuwa
malaika mpaka alipokuwa amemhudumia kwa chakula na baadaye wote kuandaa sadaka
ya kuteketezwa kwaajili ya Bwana Waamuzi 6;21-22 na Malaika wa bwana mara
nyingi alijitokeza kama mtu akiwamo Manoa na Mkewe Waamuzi 13;21 ni katika
matkio machache malaika wa Bwana hujitokeza katika hali za kushangaza mfano ni
wazi kuwa alipomtokea mke wa manoa muonekano wake ulikuwa dhahiri kuwa ni kama
malaika wa Bwana! Na ilitisha Waamuzi 13;6, Wanawake walioamka asubuhi na
mapema waliwaona malaika kama wanaume wawili waliowatokea na kuwapa taarifa
Luka 24;4 jambo ambalo pia liliwatokea wanafunzi wote wakati Kristo alipopaa
kwenda mbinguni wanaume wawili walisimama wakiwa na mavazi meupe Matendo 1;10.
Ujuzi zaidi wa namna malaika
walivyo unaweza kupatikana katika kitabu cha Daniel ambapo Daniel anapambanua
muonekano wa malaika jinsi ulivyokuwa kwani alikuwa akiwaka uso wake kwa mwanga
mkali na miguu yake na mikono yake ikiwa kama shaba iliyosuguliwa sana Daniel
10;5-6 na wakati mwingine malaika ufafanuliwa kama wanadamu au wene mfano wa
wanadamu Ezekiel 40;3,Daniel 10;18 Zekaria 2;1 na katika mazingira yote haya
malaika walifanya wajibu wao kwa haraka na kueleweka baadaye kuwa malaika ,
matukio yanayoashiria malaika kutoea na kujulikana mapema sana ni kama wakati
alipomtokea Balaam Hesabu 22;31 na Daudi 2Samuel 24;17 na Zekaria hekaluni na
Mariam mamaye Yesu Luka 1;11 na 26.
UTARATIBU
WA MAMLAKA ZA MALAIKA.
Kwa kuwa utaratibu
ni sheria kwanza ya mbinguni inategemewa kwamba malaika wana mamlaka ambazo
zimepangiliwa katika madaraja maalumu kama inavyoonekana katika 1Petro 3; 22
Bliblia inasema “Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu amekwenda zake mbinguni
malaika na enzi na nguvu zikiishwa kutiishwa chni yake Kwa msingi huo tunapoona
mamlaka na nguvu maana yake tunajifunza kuhusu mamlaka mza malaika katika
madaraja hayo tutayachambua kama ifuatavyo
Malaika wa Bwana
Maandiko
kadhaa hususani katika agano la kale yanaeleza kwa undani kuhusu malaika wa bwana
katika namna ambayo inasadikika kuwa ni Mungu mwenyewe, anachukua namna ya
mwili wa kibinadamu na kujitokeza kwa Muda wakati mwingine neno malaika wa
Bwana hutajwa katika namna inayoashiria kuwa ni Mungu mwenyewe Lakinni hata
namna anavyozungumza huashiria kuwa ni Mungu mwenyewe mfano Mwanzo 16;10
“Hakika Nitauzidisha uzao wako” na kasha Hajiri alijibu kwa wazi kuwa Amemuona
Mungu aonaye Mwanzo 16;13. Jambo la jinsi hii tena linaonekana wakati Ibrahimu
alipokuwa anataka kumtoa Isaka sadaka ya kuteketezwa malaika wa Bwana alimtokea
na kusema Sasa najua ya kuwa unamcha
Mungu kwa kuwa hukunizuilia mwanao mwanao wa pekee Mwanzo 22;12, malaika huyu
wa Bwana alipomtokea Yakobo katika ndoto alisema Mimi ni Mungu wa baba zako
Mwanzo 31;11,13, Pia Malaika huyu wa Bwana alipomtokea Musa katika mwali wa
moto alisema Mimi ni Mungu wa Baba zako,
Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Kutoka 3;2,6 kwa m,sigi huo
kunaushahidi kuwa malaika huyu wa bwana hutokea katika hali inayoashiria kuwa
huenda alikuwa ni Mungu mwenyewe aliyekuwa akijitokeza katika mwili wa
kibinadamu kwa muda mfupi ili
kujiwakilisha kwa mwanadamu,Ingawa pia kuna uwezekano kuwa malaika huyu wa
Bwana akawa ni Bwana Yesu mwenyewe kabla ya kuja ulimwenguni katika mwili,
lakini tunaweza kuwatambua kwa utendaji wao ili kutofautisha Baba mwenyewe na
Kristo mwenyewe wakati wa agano la kale walipokuwa wakija katika matukio kama
malaika (Theophany) tutaona tofauti
zao wakati tutakapokuwa tukijifunza kuhusu malaika wa uso wake kipengele
kinachofuata. Lakini wakati mwingine malaika huyu wa Bwana hutajwa katika namna
tofauti na Mungu kwa mfano katika
2Samuel 24;16, Zaburi 34;7, Zekaria 1;11-13 na katika Luka 1;11 katika
mazingira kama haya ilimaanisha kuwa ni malaika aliyetumwa na Mungu.
Malaika wa uso wake.
Malaika huyu anaitwa malaika wa
uso wake, The angel of His Presence au uso wangu, kwa kawaida ni malaika
anayehusika na uwepo wa Mungu, malaika huyu naye hutajwa akiwa na sifa za Mungu
kamili lakini zaidi sana Malaika huyu Israel wanaaswa wasimtia kasirani kwani
hata wasamehe makosa yao kwa kuwa jina la Mungu limo ndani yake Kutoka 23;20-23.
Huyu ni malaika anayeshughulika na kazi za Maongozi, kwa kawaida wana theolojia
wengi wanaamini juu ya Mungu Baba kuja katika umbile la kibinadamu na
kuzungumza akiwa kama Mungu mwenyewe mfano alipozungumza na Ibarahimu soma
Mwanzo 18; 1-15, Ni wazi kuwa malaika huyu alikuwa Mungu Baba lakini malaika
huyu wa Uso wa Mungu yaani malaika wa uwepo wake au uso wake huyu ni tofauti
Isaya anamtaja vizuri kuwa ni Roho Mtakatifu Isaya 63;9 – 14 , Ni wazi kuwa
malaika huyu ni Roho Mtakatifu kwani ikiwa tunaamini kuwa Mungu baba, au wakati
mwingine Mungu mwana waliwahi kujihusisha na Mwanadamu katika ukombozi wakati
wa agano la kale na kama hivyo ndio ilikuwa tabia ya Mungu na tunaamini kuwa
Roho Mtakatifu ni Mungu mimi naamini kuwa katika somo kuhusu malaika kamwe
hatuwezi kumuacha Roho wa Mungu kwani ni wazi tabia zake kama zinavyotajwa
katika agano jipya ndivyo zinavyodhihirika katika agano la kale malaika huyu
hushughulika na maongozi na hutajwa kama uwepo wa Mungu au uso Kutoka 32;34,
33;14-15, kwa sababu malaika ni mjumbe na tunawezaje kuwatofautisha malaika
hawa kwa nia Rahisi tunaweza kumtambua
·
Mungu baba kwa shughuli za Mipango na majira
·
Mwana wa Mungu kwa shughuli za ukombozi na
wokovu au uponyaji
·
Roho Mtakatifu kwa kazi au shughuli za maongozi.
Kwa msingi huo ni wazi kuwa malaika aliyemtokea Ibrahimu na kufanya
agano naye na kumtakia Sara ahadi ya kuzaliwa Isaka alikuwa ni Mungu baba kwa
sababu alishughulika na majira Mwanzo 18;1-15. Na ni wazi kuwa Malaika
aliyemtokea Yoshua alipokua akiikabili Yeriko alikuwa ni Bwana Yesu Yoshua 5;
13-15. Na Ni wazi kabisa malaika huyu anayetajwa kama malaika wa uso wake ni
Roho Mtakatifu Kutoka 23;20-23, Na unapofuatilia sifa zinazo tajwa hapo na
kuchunguza tabia za Roho na mafundisho ya Kristo kuhusu Roho unapata picha kuwa
akikosewa kuna uwezekano wa kutokusamehewa makosa bila shaka inazungumziwa
dhambi ya kumkufuru Yeye na hapa ndipo inapotajwa na Mungu kuhusu malaika huyu.
Malaika mkuu.
Malaika mkuu Biblia inamtaja kwa jina lake wazi wazi kuwa ni Mikaeli unaweza
kuona hili katika Yuda 9., Ufunuo 12;7 Habari zake nyingine katika maandiko
zinatajwa katika 1Thesaloooniiike 4;16, Malaika Mikaeli pia hujitokeza kama
malaika mlinzi wa Taifa la Israel Daniel 12;1, katika namna nyingine malaika
Gabiel huonakana kuwa katika daraja linguine chini kidogo ya malaika mkuu
mikael kwa sababu husimama katika uwepo wa Mungu Luka 1;19 na kupitia yeye
ametumwa mara kadhaa kuleta habari muhimu sana kuhusiana na ufalme wa Mungu
Daniel 8;16, Daniel 9;21, Kutajwa kwa Mikaeli kama malaika mkuu kunaashiria
kuwa ana mamlaka juu ya malaika wote , hutwa moja ya wakuu katika Daniel 10;13
na ndiye pia mkuu wa majeshi ya malaika , ndiye aliyelipiga joka ambalo pamoja
na malaika zake jaka lilipigwa Ufunuo 12;7-8, Biblia inapotaja kuja kwa bwana
katika 1Wathesalonike4;16 huenda inamaanisha Mikael au huenda kuna malaika
wengine wakuu maandiko hayatuwekei wazi.
Makerubi
Cherub ni neno la Kiebrania ambalo wingi wake ni cherubim, Wanaonekana kuwa malaika wa ngazi ya juu
zaidi wanaonekana kuwa na Mungu sambamba katika jambo lolote ikiwamo ulinzi
katika maagizo ya Mungu mfano walitumiwa kulinda mti wa Bustani ya Eden baada
ya Adamu na Hawa kuasi Mwanzo 3;24 na pia katika maswala ya kusaudi la ukombozi
Kutoka 25;22., hutumiwa na Mungu pia kama magari ya safari Zaburi 18;10,
Ezekiel 10;1-22, wakati wa Sanduku la agano wawili waliwekwa kufunika kiti cha
enzi cha Mungu kiti cha rehema Mbawa zao zikiwa zimefunika kiti cha rehema na ni hapo Mungu alihaidi kuwa angekutana na
watu wake , na kusema na watu wake na
kukutana nao kwaajili ya rehema Kutoka 25;22,18-21., Makerubi ni aina za
malaika wanaohusiana na maswala ya kijeshi au vita na ulinzi
Maserafi
Ni aina nyingine ya kundi la malaika ambao pia wako
katika daraja la juu sana hakuna habari nyingi sana za kutosha kuwahusu lakini
tunawaona katika Isaya 6;1-7,wanatajwa katika sifa za tofauti na inaonekana
kuwa wana upendo mkubwa sana kwa Mungu upendo ambao huwaka kama moto kwani maanga ya
Maserafi ni wanaowaka Neno Seraph ni
lenye asili ya kiebrania ambalo wingi wake ni Seraphim, ni wenye kuabudu Mungu
kwa kiwango cha juu sana wanaonekana wakiitana wenyewe kwa wenyewe wakisema
Mtakatifu , Mtakatifu, Mtakatifu ndiye Bwana wa majeshi Mbingu na nchi zimejaa
uwake Isaya 6;3.
Malaika wa mataifa.
Daniel 10;13,20, Katika maandiko
haya tunajifunza kuwa kila taifa au kila kabila lina malaika wake ambao
hujihusisha na ulinzi dhidi ya taifa hilo, wakati jamii ya wayahudi walipokuwa
wakijiandaa kurudi Yerusalem na Daniel nabii alipokua anaomba na kufunga
kwaajili ya kurejeshwa baada ya wiki tatu Malaika alimtokea na kumpa sababu
kuwa ni kwanini alichelewa kuleta majibu
kumbe mkuuu wa anga la uajemi alikuwa amemzuia Daniel 9;1-2, na penngine
malaika huyu alikuwa akimzuia kwa makusudi ya kutokupoteza umaarufu kwaajili ya
uajemi,kutokana na kuondoka kwa wayahudi, malaika alikuja kusaidiwa na malaika
Mikael ambaye ni mlinzi mkuu wa taifa la Israel Daniel 10;21. Na muu wa anga wa
uyunani hakuwa ameng’ang’ania sana kama ilivyokuwa kwa mkuu wa anga wa uajemi
kuhusiana kuondoka kwa wayahudi kutoka utumwani Daniel 10; 10, kwa msingi huo
katika angano jipya neno lile wakuu wa anga huenda linamaansisha kundi hili la
malaika ambao huusika na mataifa na wakuu wa anga hutumika kwa pande zote mbili
kwa malaika waovu na kwa malaika wema Waefeso 3; 10; Wakolosai 2;15, Waefeso
6;12.
Viumbe wenye uhai.
Kitabu cha Ezekiel na ufunuo vinatuambia
kuwa kuna aina nyingine za Malaika ambao wana daraja Fulani miongoni mwa
malaika na wanatajwa kama viumbe vyenye
uhai ambaovyo viko karibu na kiti cha enzi cha Mungu Ezekiel 1;5-14, Ufunuo
4;6-8 huenda waliitwa vimbe vyenye uhai kwa sababu ya aina za maumbile yao vina
uso wenye sura nne kama simba, ng’ombe, mwanadamu na tai, huenda wana wakilisha
ukuu wa uumbaji wa Mungu katika maeneo mbalimbali wakiwemo wanyama wa angani,
mwituni, wa kufugwa na binadamu, hawa humuabudu Mungu wakati wote wakimsifu kuwa ni mtakatifu
,mtakatifu,mtakatifu ni bwana Mungu mwenye enzi, aliyekuweko, aliyeko na ajaye
Ufunuo 4;8.
Malaika wateule
Malaika kwa ujumla wake wako
katika makundi makuu mawili yaani malaika wateule na malaika waovu. Malaika
wateule hili ni lile kundi ambalo wakati wa matukio ya uasi kule mbinguni
waliendelea kuwa watii kwa Mungu na hivyo walipata thawabu ya kudumu ya kuwa
wateule, na wale walioungana na shetani katika kuasi wali walipata thawabu ya
kuwa mashetani na kuhukumiwa milele 1Timotheo 5;21, Mathayo 25;41.
Malaika wa kuharibu.
Malaika wa kuharibu pia huitwa
“Muharabu” destroyer au Malaika wa
mauti 1Koritho 10; 10 malaika huyu hushughulika maalumu na kusababisha maafa
pale watu wanapokuwa wameasi Hesabu 16; 41-49, ni wazi kuwa huyu ni mjumbe wa
Mungu kwa sababu maalumu za hukumu mara nyingi hutumia tauni katika kuangamiza
kama ilivyokuwa kwa mapigo ya tauni za aina mbalimbali katika mapigo yale kumi
kule Misri Kutoka 10; 12-13 niliaminilo ni hili ingawa Bwana anasema maana
nitapita.... Bwana anazungunza kuwa atapita na kuipiga Misri, je unafikiri
Bwana ndiye aliyekuwa anapita Hapana ni Malaika wake maalumu wa kushughulika na
hukumu alipita akiwa ametumwa na Bwana,Mara nyingi Mungu anaporuhusu hukumu
huhesabika moja kwa moja kuwa ni yeye anayehusika kuleta tauni au mapigo kwa
sababu yeye ndiye ameruhusu lakini ni muhimu kufahamu kuwa malaika wake hushika
Upanga na kuanza kupiga kwa Tauni ona mfano 1Nyakati 21: 14-22 Mstari wa
15 unaonyesha kuwa Bwana alituma malaika
wake na jina la malaika huyu ni Aharibuye (Auaye) malaika huyu hutenda kazi ya
kuua anapotumwa na mara nyingi mapigo yake huzimwa kwa sadaka aidha ya kuteketeza
au uvumba wa chetezo malaika huyu ndipo hasira yake hupoa, kwa namna Fulani
malaika huyu huweza kutumiwa kwa mauaji kama wa upande wa shetani wanavyomtumia
jinni makata.huenda mwandishi wa Zaburi ya 35 ambaye ni Daudi alikuwa akiomba
kwa Bwana malaika wa aina hii awashughulikie adui zake Zaburi 35;1-28 mstari wa
8 kuna neno “Uharibifu na umpate” ni wazi kuwa muomaji anaomba malaika huyu wa
kuharibu alete uharibifu dhidi ya adui, katika mazingira Fulani ni ruhusa
kuwatumia aku kumtumia malaika huyu wa kuharibu na kusababisha uharibifu dhidi
ya yale yaliyo kinyume nasi, kuna uwezekano mkubwa kuwa malaika huyu alitumiwa
na Eliya kushusha moto kutoka mbinguni na kuharibu vikosi viwili vya maakida
waliomuita bila nidhamu 2Wafalme 1;9-15 ni wazi kuwa hatimaye malaika huyo
alimsihi Eliya kukubali ombi la Akida wa tatu kwa sababu alikuja kwa
unyenyekevu.
SIFA
ZA MALAIKA
Malaika wana
Utii uliotimia.(Obedient)
Malaika ni watii hutii maagizo yao bila kusita na
ndio maana tunaomba mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni
Mathayo 6;10, Zaburi 103;20, Yuda 6, 1Petro 3;22 malaika hutii kile
walichoagizwa na sio vinginevyo kama kuna kitu ambacho hawakuagizwa hawakifanyi
hata kama ni malaika mkuu sawa na Yuda 6.
Malaika ni
waabudu (Reverent).
Kazi yao kubwa ni kuabudu , wanamuabudu m,ungu
wakati wote wanamuheshimu na kumsikia na kumtii wanamfanyia bwana ibada katika
kila tendo lake jema Nehemia 9;6,Wafilipi 2;9-11. Waebrania 1;6
Malaika ni
wenye hekima (Wise)
Nyakati za zamani za wafalme katika Israel mtu
alipokuwa na hekima na ujuzi wa kupambanua mema na mabaya aliitwa mwenye hekima
kama malaika 2samuel 14;17 ni wazi kuwa hekima ya malaika inazidi ile ya
wanadamu katika maisha haya, ingawaje malaika hawawezi kusoma mawazo yetu
1Wafalme 8;39 na ujuzi wao kuhusu neema ya Mungu kwetu kwao ni siri 1Petro 1;12.
Malaika ni
wapole na wanyenyekevu (Meek).
Kwa kawaida hawapeleki mashitaka ya mtu awaye yote
wala hawapigani na wale wanao wapinga husikiliza na kuyatii maagizo ya Bwana
wao tu 2Petro 2;11 Yuda 9.
Malaika ni
wenye nguvu (Mighty)
Malaika wana nguvu za kupita kawaida lakini sio
wenye nguvu zote nguvu zaoi zinazidi zile za kibinadamu Zaburi 103;20.
Malaika ni
watakatifu (holy)
Kwa kuwa wamewekwa wakfu kwaaajili ya Mungu na wako
kwaajili yake malaika wametakaswa ni watakatifu Ufunuo 14;10.
KAZI ZA MALAIKA:
Ni Mawakili wa Mungu (God’s Agents)
Malaika wanatajwa kama mawakili
wa Mungu humwakilisha Mungu katika kazi
ya hukumu Mwanzo 3;24, Hesabu 22;22-27, Mathayo 13;39, 41, 49, 16;27, 24;31, Marko
13;27, Mwanzo 19;1, 2Samuel 24;16, 2Wafalme 19;35, Matendo 10;4;13-17
Ni wajumbe wa Mungu (God’s Messengers)
Kwa ufupi malaika maana yake ni
mjumbe kwa msingi huo moja ya kazi kubwa ya malaika ni kupeleka ujumbe kutoka
kwa Mungu kuja kwa wanadamu , kupitia wao Mungu huwatuma kutangaza Luka 1;11-20
,Mathayo 1;20,21. Malaika pia hutumwa kuleta maonyo Mathayo 2;13,Waebrania
2;2,Hutumwa kutoa Maelekezo Mathayo
28;2-6, matendo 10;3, Daniel 4;13-17,Malaika hutumwa kutia moyo Matendo 27;23,Mwanzo 28;12, Aidha malaika pia
hutumwa kuleta mafunuo au ufunuo Matendo 7;53, Wagalatia 3;19,Waebrania 2;2,
Daniel 9;21-27 Ufunuo 1;1.
Ni watumishi wa Mungu (God’s Servants).
Je wao si roho wanaotumwa
kuwahudumia wale watakao urithi wokovu,Waebrania 1;14Malaika hutumwa kutia
nguvu Mathayo 4;11Luka 22;43,1falme 19;5 , hutumwa kulinda Mwanzo
16;7,24;7,Kutoka 23;20,Ufunuo 7;1, hutumwa kuwaokoa watu Hesabu 20;16Zaburi
34;7,91;11 Isaya 63;9,Daniel 6;22Mwanzo 48;16 Mathayo 26;53 huingilia kati
Zekaria 1;12 Ufunuo 8;3,4 Kuwahudumia watakatifu baada ya kufa Luka 16;22.
NAFASI
YA MALAIKA KATIKA KUSUDI LA MUNGU
1.
Malaika wanaonyesha ukuu wa upendo wa Mungu
na mpango wake kwetu.
Malaika pamoja
na wanadamu ndio viumbe wa pekee wenye akili na maadili katika viumbe ambavyo
Mungu ameviumba, kwa msingi huo tunaweza kufahamu kwa uapana na kina kuhusu
mpango wa Mungu na upendo wake kwetu hususani tunapojilinga sisi na Mungu.
Moja ya jambo la kwanza la msingi
tunalijifunza kati yetu na malaika ni kuwa malaika hawatajwi kuwa wameumbwa kwa
sura na mfano wa Mungu wakati wanadamu wanatajwa kuwa wameumbwa kwa mfano na
sura ya Mungu Mwanzo 1; 26-27,9;6 kuwa na sura na mfano wa Mungu maana yake ni
kuwa kama Mungu kwa hivyo si vibaya
tukihitimisha kuwa Wanadamu wana fanana na Mungu zaidi kuliko malaika.
Jambo kama hilo linathibitishwa na
ukweli kuwa iko siku Mungu atatupa mamlaka dhidi ya malaika na kuwa
tutawahukumu Je hamjui ya kuwa ninyi mtahukumu malaika? 1Wakoritho 6;3 ingawa kwa muda huu sisi ni
wadogo ukilinganisha na malaika Waebrania
2;7, wakati wokovu wetru utakapokamilika
tutakuwa juu ya malaika na tutawatawala
na kwa ujumla hata sasa malaika ni tayari wanatutumikia Waebrania 1;14.
Jambo lingine ni kuwa Mungu alimpa
binadamu uwezo wa kuzaa na Adamu akazaa watoto kwa sura na mfano wake Mwanzo 5;3 hii ni alama nyingine ya Ubara
ambayo Malaika hawana kwani wao hawana
uwezo wa kuzaliana na kuongezeka Mathayo 22;30, Luka 20;34-36
Malaika wanawakilisha ukuu wa na
upendo wake kwa wanadamu kwani ingawa wao ni wengi lakini mara walipofanyadhambi
na kuasi hakuna hata mmoja wao aliyeokolewa Petro anatuambia kuwa …Mungu
hakuwaachilia malaika waliokosa bali aliwatupa shimoni akawatia katika vifungo
vya milele walindwe hata ije hukumu” 2Petro 2;4 Yuda anawaita malaika wasioilinda
enzi yao wenyewe lakini wakayaacha makao yao ya asili imewekwa kuwa dalili wakiadhibiwa katika moto
wa milele Yuda 1;6.
Aidha tunaona kuwa Kristo Yesu
alipokuja duniani badala ya kutwaa asili ya Malaika alitwaa asili ya Binadamu
kwa uzao wa Ibrahimu Biblia inasema haya katika Waebrania 2;16 “Maana ni hakika
hatwai asili ya maklaika ila atwaa asili
ya mzao wa Ibarahimu” Kwa msingi huo ingawa Mungu aliumba makundi makuu mawili
ya viumbe wenye akili yaani malaika na
wanadamu na ingawa malaika ni bora zaidi ya aina binadamu Neema kubwa ya
mahusiano inaonekana kuwa pamoja na wanadamu Bwana asifiwe sana ni upendo
mkubwa na neema ya ajabu! Kwa nini ndani ya makundi haya mawili Malaika
hawakuasi wote baadhi tu waliasai lakini kwa upande wa wanadamu woote waliasi
Mungu angepaswa atuache woote na kututupia ,mbali katika hukumu ya milele na hakuna ambaye angelaumu ingeuwa ni haki tu
kufanyiwa hilo Lakini Mungu alikusudia kutuokoa sisi wanadamu na hata kama
angeokoa watano tu miongoni mwa wana wa aina binadamu pia ingelikuwa haki naangekuwa ameonyesha
rehema na neema na angekuwa sahii lakini Mungu amekusudia kutuokoa kwa wingi wa
mamilioni wasiohesabika na wote watakao kubali neema yake jamii hiyo anayoiokoa
ni kutoka katika kila jamii ya aina binadamu kabila na taifga Ufunuo 5;9 huu ni
upendo neema na rehema zisizoweza kufahamika
ni zaidi ya uwezo wetu wa kuelewa ni upendeleo usiostahili ukweli huu
unatufanya sisi tuwe na uwezo wa kuimba
wimbo ambao malaika hawangeweza
kuimba, huenda watausikia na kuufurahia wimbo wa kumsifu Mungu kwa neema yake
isiyoweza kupimika lakini kamwe hawawezi kuufanya kuwa wimbo wao.
2.
Malaika
wanatukumbusha kuwa ulimwengu wa roho ni halisi.
Nyakati za
maisha ya Kristo duniani dhehebu la masadukayo walikuwa wanaamini kuwa Hakuna
ufufuo,Hakuna malaika wala roho Matendo 23;8, hata katika nyakati zetu wako
watu wanaoamini kuwa maswala ya ulimwengu wa kiroho sio Halisi, wengine
hawaamini katika lolote wasiloliona, Lakini mafundisho ya kibiblia yanaonyesha
kuwa kuna malaika na biblia
inatukumbusha mara kwa mara kuhusu ulimwengu wa kiroho usioonekana na kuwa
ulimwengu huo ni halisi, hatuwezi kuuona ulimwengu huo kwa macho ya kawaida
lakini Mungu atakapotupa neema hiyo au kufungua macho yetu kama ilivyokuwa kwa
mtumishi wa nabii Elisha utaweza kuliona jeshi kubwa la malaika na magari yao
ya moto 2Wafalme 6;17. Waandishi wa zaburi pia wanatukumbusha kuhusu ulimwengu
wa kiroho na kuwasihi malaika waimbe sifa za Mungu Zaburi 148;2, mwandishi wa
kitabu cha Waebrania anatukumbusha kuwa
tutaingie Yerusalemu ya Mbinguni pamoja na jeshi kubwa la malaika Waebrania 12;22, walimwengu wa kawaida
wanaweza kudhani kuwa swala kuhusu malaika ni swala la kichawi lakini maandiko
yanatukumbusha kuwa ni halisi.
3.
Malaika
ni mfano kwetu.
Kwa namna iwayo
yote malaika ni mfano kwetu namna wanavyo tii na wanavyoabudu wanatupa sisi mfano wa kuiga, Yesu
alipofundisjha kuhusu kuomba alisema Yatendeke hapa duniani kama huko mbinguni
Mathayo 6;10, huko mbinguni mapenzi ya Mungu hutimizwa na malaika kwa
ukamilifu, kwa haraka , kwa furaha bila maswali
kwa msingi huo ni muhimu kuomba kuwa utii wetu na wa wengine uwe kama
ule wa malaika mbinguni, wao ni watumishi wa Mungu wanyenyekevu na waaminifu na
hufanya wajibu wao kwa furaha liwe
jukumu kubwa au dogo.
Malaika pia
wanatufundisha jinsi wanbavyoweza kuabudu
na kumtumikia Mungu wao kwa mfano maserafi kwa humuona Mungu kuwa ni
Mtakatifu wanatambua hivyo na humsifu kwa kurudia tena na tena Mtakatifu, mtakatifu matakatifu ni BVwana
Mungu wa majeshi nchi yote imejawa na utukufu wake Isaya 6;3, aidha Yohana aliona kundi kubwa la
malaika wakiwa wamekizunguka kiti cheke cha enzi maelfu kwa maelfu
wakimsifu mwana kondoo aliyechinjwa na kusema kuwa anastahili nguvu na utajiri na hekina na mamlaka na utukufu na abarikiwe Ufunuo 5;11-12 kama
malaika wanavyo msifu Mungu kwa furaha kila siku na kila wakati wakitambua kuwa ni mkuu na anastahili je inatupasaje sisi katika wakati huu tulio
nao?
4.
Malaika
hutimiza majukumu kadhaa ya Mungu.
Maandiko
yanawaona malaika kama watumishi wa
Mungu ambao hutimiza majukumu kadhaa ya
Munguna mipango yake hapa duniani, Wanatumika kuleta ujumbe wa Mungu kwa
wanadamu Luka 1;11-19, Matendo 8;26, 10;3-8,22, 27;23-24, wanabeba baadhi ya
majukumu ya kuleta hukumu na mapigo mfano kwa Israel 2Samuel 24;16-17, kuwapiga
viongozi wa Ashuru 2Nyakati 32;21, kupigwa kwa mfalme Herode kwa sababu ya
kutokumpa Mungu utukufu Matendo 12;23 na kumwaga hasira za Mungu duniani wakati wa dhiki kuu
Ufunuo 16;1 na wakati Kristo atakapokuja Duniani ayakuja na jeshi kubwa
linaloambatana na mfalme Mathayo 16;27, Luka 9;26 2Thesalonike 1;7, Malaika pia
huzunguka duniani kama wawakilishi wa Mungu
Zekaria 1;10-11, pia hufanya vita dhidi ya mapepo Daniel 10;13, Ufunuo 12;7-8 Yohana katika
maono yake aliona shetani akifungwa na malaika
miaka 1000 ufunuo 20;1-3 na Masihi
atakapokuwa akirudi Malaika watatangaza
ujio wake 1Thesalonike 4;16 Ufunuo 18;1-2,21,19;17-18.
5.
Malaika humtukuza Mungu.
Malaika hufanya
kazi nyingine ya kumtukuza Mungu moja kwa moja kupitia utumishi wao kwa msigi
huo katika uumbaji wa Mungu na viumbe wenye akili wanaomtukuza Mungu malaika
humtukuza Mungu kwa jinsi alivyo katika njia iliyo bora zaidi Zaburui 103; 20
Mhimidini Bwana enyi Malaika zake Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake Mkiisikiliza
sauti ya neno lake.Pia Zaburi 148;2 Maserafi huendelea kumsifu Mungu kwa
utakatifu wake Isaya 6;2-3 jambo ambalo pia hufanywa na viumbe wale wenye uhai
Ufunuo 4;8,
Malaika pia humtukuza Mungu kwa mpango wake
mkuu wa wokovu, tunawaonawalivyo mtukuza Mungu alipozaliwa Kristo huko
Bethelehemu Luka 2;14 Waebrania 1;6 Yesu alisema Pia kuna furaha kubwa mbele ya
Malaika wa Mungu mwenye dhambi mmoja atubupo Luka 15;10 hii yote inamaanisha
kuwa malaika hufurahia hufurahia kila wakati Mtu anapokuwa anaokolewaPaulo
mtume anaeleza kuwa Mungu alimtuma kuihubiri injili kwa Mataifa katika hekima
ili kwamba uweza wa Mungu upate kujulikana kwa Falme na mamlaka Katika
ulimwengu wa roho, Petro anatuambia kuwa mambo haya malaika wanatamani
kuyachungulia 1Petro 1;12 kwa ajili ya utukufu mkubwa na mpango mzima wa wokovu
unaotenda kazi ndani ya kila aaminiye,Malaika pia hushuhudia maisha ya waamini
wanapokuwa ibadani na humtukuza Mungu kwa ajili ya ibada zetu na utii wetu
1Koritho 11;10, Aidha Paulo alipokuwa akiagiza jambo la Muhimu kwa Timotheo kwa
ajili ya kusisitiza alisisitiza kuwa
nakuagiza mbele zake mungu na Yesu
Kristo na Malaika wateule 1Tomotheo
5;21,1Koritho 4;9 maana yake ni kuwa wakati timotheo atakapokuwa akitii maagizo
aliyopewa Malaika watashuhudia utii wake na watamtukuza Mungu na kama hato tii
malaika wataona na kusikitishwa.
UHUSIANO
WA WANADAMU NA MALAIKA
1.
NI
LAZIMA TUWE WAANGALIFU KUHUSU MALAIKA.
Maandiko
yanatuwekea wazi kuwa Mungu anataka tuwe makini na kuweko kwa malaika na
utendaji wao , hii haina maana kuwa kujifunza kuhusu malaika hakuna umuhimu
katika maisha yetu hapana lakini katika
mazingira Fulani tunapaswa kuwa makini
kuhusu kuweko kwao na huduma zao hata wanazozifanya leo
duniani,Tunapomwabudu Mungu sio tu kuwa tunaungwa moja kwa moja na watakatifu
ambao wamekwisha kufa katika bwana na roho zao zimekamilishwa kwake lakini pia
tunaungana na jeshi kubwa la amalaika wanaomwabudu Mungu ambao hawahesabiki
Waebrania 12;22-23, kwa msingi huo ingawa katika hali ya kawaida hatuwezi kusikia
au kuona namna Fulani ya ibada za kimbinguni
lakini kwa namna Fulani tunashuhudiwa na furaha na uwepo mkubwa wa Mungu
nah ii inatupa uhakika kuwa malaika wanaungana na si kila tusimamapo kuabudu
Lakini tunapaswa
kuwa makini kwani malaika wanaangalia kutii kwetu na kutokutii kwetu katika siku nzima, kama tunafikiri kuwa
dhambi zetu tunazofanya sirini ni siri na kuwa haiwezi kuhuzunisha wengi ni
muhimu kukumbuka kuwa malaika kwa maelfu yao wanashuhudia na kuhuzunishwa na
dhambi yetu hali kadhalika tunapokuwa tunamtii Mungu hata katika hali ya kuwa
wenyewe ni muhimu kufahamu kuwa kutii kwetu hata kama hakuonekani kwa wanadamu
Mungu aoneaye sirini anaona lakini pia maelfu ya majeshi ya malaika wanaangalia
kutii kwetu na jinsi tunavyotaabika peke
yetu katika kumtii Mungu na kujiepusha na kumkosea yeye na tunatiwa moyo kuwa
Malaika wanashuhudia jinsi tunavyoheshimu kazi kubwa ya ukombozi iliyofanywa na
kristo katika maisha yetu.
Akifundisha
jinsi utendaji wa malaika ulivyo mwandishi wa kitabu cha waebrania anasema kuwa
tusiache kuwa wakarimu kwa wageni kwani katika namna isiyo ya kawaida huchukua
miili ya kibinadamu na kutembelea kwa lengo la kuchunguza kwa kusudi la
kuthibitisha maswaka kadhaa Waebrania 13;2, Mwanzo 18;2-5,19;1-3 hili linatutia
moyo katika swala zima la kuendelea kuwahudumia wenye uhitaji hata wale
tusiowajua siku moja mbinguni tutakutana na malaika ambao yuliwahudumia bila
kujijua kuwa tunahudumia malaika
Wakati mwingine
tunapokuwa tumeokolewa na ajali mbaya ni muhimu kufahamu kuwa huenda Mungu
alimtuma malaika wake kutuokoa na tunapaswa kumshukuru Mungu, Malaika walifunga
vinywa vya simba ili wasimdhuru nabii Daniel, Daniel 6;22, waliwafungulia
mitume kutoka gerezani Matendo 5;19-20 na baadaye walimtoa Petro gerezani
Matendo 12;7-11, walimuhudumia Bwana Yesu huko jangwani wakati wa kumalizia majaribu Mathayo 4;11.
Ni muhimu
kukumbuka kuwa wakati gari linapotaka kutugonga na likatukosa ni lazima
tukumbuke kuwa sio tunapswa kuhisi kuwa Mungu ametuma malaika zake kutuokoa
lakini tunapswa kuwa na ufahamu kuwa aliahidi
kumtuma malaika wake kutulinda
katika njia zake zote Zaburi 91;11-12 kwa msingi huo kumshukuru Mungu
kwa kumtuma malaika wake kutulinda ni swala sahii.
2.
MAONYO
KUHUSU UHUSIANO WETU NA MALAIKA.
a. Uwe makini kupokea Mafundisho potofu kutoka
kwa malaika.
Biblia inatuonya kuhusu kupokea mafundisho potofu
yanayodaiwa kutoka kwa malaika Wagalatia 1;8 “Lakini ijapokuwa sisi au
malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi
injili iwayo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri
na alaaniwe”Paulo anatufundisha swala hili kwa sababu alijua kuwa kuna
uwezekano wa kudanganyika kwa sababu
alisema pia wala si ajabu kwani hata shetani mwenyewe hujigeuza awe kama
malaika wa Nuru 2 Wakoritho 11;14 hii ni
sawa na nabii wa uongo aliyemrubuni mtu wa Mungu katika Wafalme 13;18 huku maandiko yakiweka
wazi kuwa lakini alimdanganya, huu ni mfano wa mafundisho potofu huu ni mfano
wazi wa utendaji wa shetani katika kutaka kutukosesha ili tusiyatii maagizo na amri za Mungu
1Wafalme 13;9 hili ni onyo kwa wakristo wote kuwa makini na aina hizi za
mafunuo yaliyo kinyume na injili ya kweli mfano ni madhehebu ya Mormonism
wanaodai kuwa malaika NMoroni alizungumza na Joseph Smith na kumfunulia kuhusu
dini ya Mormonism ambayo mafunuo yake yakoi kinyuma na injili ya kweli
Mafundisho ya kweli na sahii yamefungwa katika neno la Mungu na ni Muhimu kwetu
kufahamu kuwa ufunuo wowote ambao utadaiwa kutoka nje ya neon la Mungu kana
kwamba mtu huyo ana laziada kuliko maandiko tunapaswa kuwa makini na mafundisho
ya aina hiyo.
b. Hatupaswi kuwaabudu, kuwaomba au kuwatafuta
malaika.
Kuabudu malaika Wakolosai 2;18 ni moja ya mafundisho
potofu yaliyokuwa yamelivamia kanisa la Kolosai na ingawaje malaika walimtokea
Yohana mtume na kumpa kitabu cha ufunuo Yohana alionywa asimwabudu malaika bali
amuabudu na kumsujudia Mungu Ufunuo 19;10, aidha hatupaswi kuwaomba
malaika bali tunapaswa kumuomba Mungu
yeye anauwezo wa kusilkia maombi yetu hata kama ni ya watu wengi yaya ni Mungu
anayejua yote pia Mungu ana nguvu zote
anajua yote Mungu mwana na Roho Mtakatifu pia wanaweza kuombwa lakini hili sio halkali kwa kiumbe kingine
zaidi ya hao tu, Paulo anaonye pia kuwa hakuna mpatanishi mwingine kati ya Mungu na wanadamu bali mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni
mmoja Kristo Yesu 1Timotheo 2;5, tunapowaomba malaika maana yake ni kuwa
tumawapa cheo kimoja sawa na Mungu na
hakuna mahali kokote katika maandiko ambapo mtu Fulani alimuomba malaika kwa
jambo lolote. Wala pia maandiko hayajatuagiza kuutafuta uso wa malaika wao
hujitokeza wenyewe kwa maagizo au neema ya Mungu tu endap[o wametumwa kutimiza
jukumu Fulani wajibu wetu mkubwa ni
kutembea na Mungu ambaye yeye ni Kamanda
wa majeshi ya malaika ingawaje si vibaya
kumkumbusha mungu sawa na ahadi yake kumtuma malaika ili kutulinda Zaburi 91;11 wakati wa mahitaji.
c. Je malaika hutokea watu leo?
Nyakati za kanisa la kwanza vipindi vya mwanzoni malaika
walikuwa wakijitokeza kufanya kazi, ni malaika aliyemwambia Filipo kuelekea kusini mwa njia ya kuelekea Gaza kwaajili ya wokovu
wa towashi wa kushi Matendo 8;26, Malaika alimwelekeza Kornelio kutuma mtu
kwenda Yafa kumuita Petro Matendo
10;3-6, walimsihi Petro kuamka na kutoka gerezani Matendo 12;6-11, alimuhakikishiaPaulo
kuwa hakuna mtu aliye katika meli yao atakayepoteaMatendo 27;23-24 mwandioshi
wa kitabu cha waebrania alioonya watu kuendelea kuwa wakarimu kwani wanaweza
kuwakarimu malaika hii maana yake ni kuwa kuna uwezekano hata sasa kwa mujibu
wa Biblia tunaweza kuwaona malaika lakini jambo la msingi la kuzingatia ni kuwa
hatuwezi kukubaliana na kupokea muongozo
mpya kutoka kwa malaika kuhusu injili jambo hili litakuwa sio la kawaida na kwa
vyovyote vile yatakuwa mafundisho potofu ya shetani 2Koritho 11;14 maandiko
yataendelea kuwa muongozo wetu dfaima malaika hawawezi kwa namna yoyote ile
kuleta ufunuo mpa ulio kinyume na injili Wagalatia 1;8.
UFAHAMU
KUHUSU SHETANI.
Baadhi ya watu hawaamini kuwa
kuna kiumbe cha aina hii kinachoitwa shetani, lakini unapoziangalia kazai za
uoavu zinazofanyika hapa duniani katika namna iliyo rahisi sana unaweza
kujiuliza ni nani aana simamia zoezi hili la uovu ulimwenguni? Biblia
inatuambia kuwa yuko na anaitwa shetani.
1.
Asili
ya shetani.
Isaya 14;12-15,
Ezekiel 28;12-19. Kuna wazo maarufu sana ambalo limo miongoni mwa watu ambao
hufikiri kuwa shetani ni wazo tu lililochukuliwa miongoni mwa wapagani na sio
la kibiblia, Lakini kwa mujibu wa maandiko Shetani kwa asili ndiye Lusifa
(Lucifer – ambalo maana yake ni mwenye kuwaka) alikuiwa mionbgoni mwa malaika
wenye utukufu mkubwa, lakini kwa majivuno alitamani kujiinua na kuwa kama Mungu
na akaangukia katika hukumu ya Mungu na kuwa shetani kama sehemu ya hukumu yake
1Timotheo 3;6.
Kwa mujibu wa
historia ya maandiko ya Isaya 14 na Ezekiel 28 watu hushangaa kwanini Wafalme
wa Babel na Tiro ndio wanatajwa kwanza kabla ya kutajwa kwa shetani? Moja ya
majibu juu ya hilo ni kuwa Manabii
wanaelezea kusudi la kuanguka kwa shetani kwa kusudi la kivitendo, Wafalme wa
Babeli na Tiro walikuwa ni wenye kukufuru wakitaka waabudiwe kama Mungu
mwenyezi Linaghanisha na Daniel 3;1-12; Ufunuo 13;15, Ezekiel 28;2 na Matendo
12;20-23, na kwa sababu hiyo mfano wao unakuwa ni somo la wazi wa tabia
aliyokuwa nayo lusifa , kwa kusudi la kuwaonya viongozi wao nabii anavuviwa
kunukuu tukio lililotokea huko nyuma sana
la malaika hao na huyj aliyeasi na kutaka kuwa kama Mungu, kwa msingi
huo kama Mungu aliweza kumuhukumu malaika wake aliyekufuru hatashindwa
kuwahukumu kiburi cha wafalme hawa wa Babeli na
Tiro wanaotaka kujiinua kiasi cha
kuchukua nafasi ya Mungu, mashambulizi ya aina hii na aina hii ya kiburi hutoka
kwa Yule muovu, ni katika namna kama hiyo kumbuka kuwa alitaka kuwaingizia
Tabia hii wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa Soma Mwanzo 3;5 na Isaya 14;14 na
hii ndio roho ya Ibilisi, wakati wote anatamani sana kuabudiwa angalia Mathayo 4;9 Kama Mungu wa dunia hii
2Koritho 4;4 ni tama ambayo itatimizwa kwa Muda wakati atakapokuja kusimamisha
utawala wake kupitia mpinga Kristo Ufunuo 13;4.
Kama adhabu ya
uovu wake shetani alitupwa nje pamoja na
jeshi lake walioungana naye katika tabia
ya uasi Mathayo 25;41, Ufunuo 12;7, Waefeso 2;2, Mathayo 12;24, alijaribu
kumpata eva kama njia ya kuingiza uasi lakini Mungu alikuwa na mpango wa
kuuleta ukombozi kwa njia yua mwanamke
Mwanzo 3;15
2.
Sifa
za Shetani.
Sifa za Shetani
ziko wazi kupitia majina yake aliyopewa
a. Anaitwa shetani.
Shetani maana yake ni adui, mpinzani, kazi yake siku
zote ni kuzuia makusudi upinzani huu unaonekana wazi katika majaribio yake ya kuharibu
kabisa mpango na makusudi ya Mungu alijaribu kuharibu mpango wa Mungu wa
kumleta masihi aliyetabiriwa katika Mwanzo 3; 15 na mapema sana aliweka nguvu
zake kupitia Kaini na kumuua habili 1Yohana 3; 12, Mungu alimpa Hawa mtoto
mwingine ambaye alikuwa kama mbegu
iliyochaguliwa kwaajili ya kumleta mwokozi ulimwenguni huyu ni Seth lakini sumu
ya nyoka huyu ilijaribu kuharibu uzao huo kwa kuuchanganya na uovu kiasi
ambacho ilimlazimu Mungu kuleta mafuriko ya gharika, lakini angalau kupitia
Nuhu mtu mwenye haki Mungu alianzisha
ukoo mpya wa ukombozi na hivyo shetani alishindwa katika mpango wake
kuzuia kusudi la Mungu.
Na kutokana na mwana wa Nuhu Shemu alikuja kutokea Abrahamu ambaye alikuwa ni
chaguo la watu wa Mungu ambaye kupitia yeye Mungu angeleta wokovu kwa Dunia, Na
kupitia asili shetani alijaribu sana kuweka uadui dhidi ya watu wa Mungu,
Ishimael alimpinga Isaka, Essau alijaribu kumuua Yakobo, Farao alijaribu
kuwakandamiza Israel, Hali kadhalika shetani anajaribu sana kuliangamiza
kanisa kwa njia kuu mbili kupitia mafundisho
potofu hii ni mashambulizi ya ndani (1Timotheo 4;1 na Mathayo 13;38-39) na
mashambulizi kutoka nje yaani mateso Ufunuo 2;10 na ule ukweli kuwa Israel ni
kanisa la nyakati za agano la kale , ile
hali ya kutengenezwa kwa sanamu ya dhahabu ni jaribio endelevu katika historia
nzima ya kujaribu kuwafanya watu kuabudu mungu mwingine, Na katika kitabu cha
Esta kuna mfano ulio hai dhidi ya kuwaharibu watu wa Mungu. Lakini wakati wote
watu wa Mungu wameendelea kuweko kwa sababu ya neema ya Mungu kila wakati Mungu
hujisazia mabaki na wakati mkamilifu ulipokuja Mkombozi alizaliwa Herode
alijaribu kutaka kumuangamiza mapema lakini Mungu alimchenga shetani na shetani
akachanganyikiwa, huko jangwani shetani alijaribu kumzuia masihi wa Mungu na
kumzuia katika mpango wake lakini alishindwa vibaya tena na kisha Kristo
aliendeliendelea kutenda mema akiwaponya wote walioonewa na shetani. Hata hivyo
mapambano haya dhidi ya shetani na kazi za Mungu yatafikia ukomo wake katika
kilele wakati Shetani atakapomuingia mpinga Kristo ambaye ataharibiwa wakati wa
kuja kwa Kristo.
b. Mshitaki
Shetani huitwa mshitaki wetu Ibilisi ni mmshitaki
dhidi ya Mungu na watu wake Mwanzo 3;2,4,5. Na Mwanadamu, Ufunuo 12; 10, Ayubu
1;9, Zekaria 3;1,2, Luka 22;31.
c. Muharibifu.
Shetani anaitwa muharibifu au muharabu kwa kiyunani ni
Apollyon na kwa kiebrania Abaddon Ufunuo 9;11 akiwa amejawa na chuki dshidi ya Muumba na kazi zake
anajiweka mwenyewe kama Mungu wa uharibifu.
d. Nyoka
Shetani huitwa Yule nyoka wa zamani Ufunuo 12;9 huenda
inatumika kukumbushia namna alivyojibadili
zamani akimtumia nyoka kama njia
ya kupitisha majaribu na kusababisha anguko la mwanadamu.
e. Mjaribu.
Mathayo 4;3
kujaribu maana yake kuonja au kuweka majaribuni wakati mwingine Mungu
hujaribu lakini kujaribu kwake ni kwaajili ya kutoa mtihani test kwaajili ya
kutupandisha daraja kwaajili ya wema
wake Mwanzo 22;1 wakati Mungu huwajaribu wanadamu kwaajili ya
mema yao zaidi Shetani huwajaribu watu kwa kusudi la kuwaangusha na
kuwaangamiza.
f.
Anaitwa
mfalme na Mungu wa dunia hii.
Yohana 12;31 2Wakoritho 4;4,Majina haya yanahusiana na
kazi anazozifanya dhidi ya jamii kama zilivyogawanywa na Mungu mwenyezi
ulimwenguni Ulimwengu huu uko chini ya uovu dhidi ya ibilisi 1Yohana
2;16,ulimwengu unaotajwa kimaandiko unahusu utaratibu wa kibinadamu ambao
unaongozwa na utatu wa Heshima, anasa na faida , sheatani anashikilia kila kitu
ulimwenguni anatawala njia za uchumi na anasa na faida akiwa na mamlaka
aliyoipora kutokana na mwanadamu kushindwa kutawala vyote kama Mungu alivyomuamuru,
ni katika anguko la mwanadamu shetani amekuwa mtawala wa ulimwengu huu akitumia
tamaa ya macho, kiburi cha uzima.
3.
Kazi
za Shetani.
a.
Kwa asili kazi za shetani ni kupingana
na mpango wa Mungu 1Thesalonike 2;18, hufanya kazi ya kupingana na injili
Mathayo 13;19 2Wakoritho 4;4, anafanya uvamizi,anapiga upofu, anadanganya
anaweka mitego, Luka 22;3,2,Wakoritho 4;4, Ufunuo 20;7,8 1Timotheo 3;7,
Anafanya mashambulizi Ayubu 1;12 anajaribuwatu wa Mungu,1Wathesalonike 3;5
Anasemekana ni mwenye hila na hupindua maandiko 4;4,5,
Anakiburi na majivuno 1Timotheo 3;6, Ni
mwenye nguvu Waefeso 2;2 ni
mchonganishi, Ayubu 2;4 ni mwerevu Mwanzo 3;1
ni mdanganyifu Efeso 6;11 ni mkatili na mkali 1Petro 5;8
b.
Hutenda kazi kam malaika wa Nuru, katika namna
isiyokuwa ya kawaida shetani hujifanya kama malaika wa nuru katika utendaji
wake wa kazi 2Wakoritho 11;14, inaonekana kuwa tangu mwanzo amekuwa
akijihudhurisha katika makundi ya wana
wa Mungu mfano ayubu 1.Kwa kusudi kama hilo huweza kujipenyeza katika kanisa la
Mungu na kupenyeza mafundisho yake 1Timotheo 4;1 au kwa lugha nyingine sinagogi
la shetani Ufunuo 2;9 na watumishi wake pia hujifanya kama malaika wa nuru
2Wakoritho 11;15 makusudi makubwa ya utendaji wake anapojiingiza katika makundi ya watu wa
Mungu ni kwaajili ya kuliharibu
kanisa kwani anajua kuwa akifanikiwa
kuwaharibu wale ambao ni chumvui ya ulimwengu na kuwateka watu kuwa watumishi
wake itakuwa rahisi kwakekupata mawindo
na kupanda roho ya kuasi kwa jamii ya
ulimwengu wote.
c.
Hutenda kazi kwa chuki kubwa sana unaweza
kujiuliza kwanini shetani hutaka watu wabakie kama magofu tu? hii ni kwa sababu
shetani anachukizwa sana na ile sura na mfano wa Mungu ambao mwanadamu aliumbwa
nayo na itakuwa ndani yetu, anachukizwa na ile hali ya kuwa wanadamu lakini
wakati huohuo tumefananishwa na wana wa Mungu, ana chukizwa na utukufu wa Mungu
tulio nao na mpango wa Mungu wa kumtukuza na haimaye kuwa na mwisho wenbye
furaha anachukizwa na furaha iliyo ndani yetu tunayopewa na Mungu ambayo
tutakuwa nayo milele, kwa ujumla anachukizwa nasi kwa sababu maelfu elfu kama
myahudi mmoja wa zamani alivyosema kuwa ni kwa wivu wa shetani kifo kilikuja
ulimwenguni na wale wamfuatao wako
upande wake.
d.
Sheatani ana mipaka, Pamoja na kuwa shetani
anatajwa kuwa mwenye nguvu lakini ni muhimu kufahamu kuwa hana nguvu zote, kwa
wale wamwaminio Kristo shetani amekwisha shindwa hana kitu kwetu Yohana 12;31
na ana nguvu kwao wale wasioamini na kwetu sisi tunaoamini hana nguvu na kama
tunampinga anaweza kutukimbia Yakobo
4;7, ana nguvu lakini nzinz mipaka
anaweza hata kuleta majjaribu au vishawishi Mathayo 4;1 anashambulia
Ayubu 1;16 anaweza kuua Ayubu 2;6, Waebrania 2;14 na anaweza kumgusa mwamini
kwa ruhusa ya Mungu tu.
e.
Shatani ana mwisho, tangu mwanzo Mungu alikuwa amekwisha kuhaidi
kuwa atashughulika na nguvu
zilizopelekea mwanadamu kushindwa Mwanzo 3;15 huyu ni uzao wa mwanamke ambao
utamponda shetani kichwa, shetani alikwisha kutupwa kutoka mbinguni tangu
zamani na wakati wa dhiki kuu atatyupwa hata nchi Ufunuo 12;9 na wakati wa
millennium atafungwa katika shimo kwa
miaka 1000 na baada ya miaka 1000 atatupwa katika ziwa liwakalo moto Ufunuo
20;10 wakati huu Neno la Mungu linatuthibitishia kuwa uovu utakuwa umefikia
ukingoni.
UFAHAMU
KUHUSU MALAIKA WALIOASI.
1.
Malaika
walioasi.
Malaika
waliumbwa wakiwa wakamilifu, wasio na doa wala waa kama ilivyokuwa kwa
mwanadamu, lakini Mungu aliwaumba wakiwa na utashi yaani uwezo wa kuamua, chini
ya uongozi wa shetani wengi wa malaika hao waliasi na kufukuzwa mbinguni Yohana
8; 44, 2Petro 2;4 Yuda 6 Dhambi kubwa waliyokuwa nayo na aliyokuwa nayo
kiongozi wao ni kiburi baadhi wamefikiri kuwa tukio hili la kuasi ni ufunuo
ujao wa wakati wa kuzaliwa kwa Kristo na
shetani kutaka Kuabududiwa Lakini Yesu alimshinda.
Baadhi ya kundi hili la malaika walioasi
wamewekwa katika kifungo 2Petro 2;4 na baadhi wamo ulimwenguni, angani na kila
mahali wakituzunguka 1Yohana 12;31,14;30.2Koritho 4;4, Ufunuo,12;4,7-9, kwa
kuwa walifanikiwa kumuingiza mwanadamu katika dhambin wamekuwa na nguvu kubwa
kuliko wanadamu 2Wakoritho 4;3-4, Waefeso 2;2,6;11-12, Lakini nguvu hizo
zimeharibiwa kwa wale waliookolewa na
wanaodumu kwa uaminifu katika Kristo kwa ajili ya ukombozi mkuu alioufanya
Kristo Ufunuo 5;9,7;13,14. Malaika hawa kwa bahati mbaya hawajapewa nafasi ya ukombozi
1Petro 1;12 Lakini moto wa milele umeandaliwa kwaajili yao kwaajili ya hukumu
Mathayo 25;41.
2.
Mapepo.
Maandiko hayaelezi
kwa asili mapepo chanzo chake ni nini, kwa sehemu kubwa inaonekana siri inayozunguka ulimwengu wa uovu, lakini
yanashuhudia kwa uwazi kuweko kwao na
vitendo vyao Mathayo 12;26,27, Katika injili tunawaona kama roho wabaya wasio
na mwili na huwavamia watu na kuwatesa hususani wale wanaoitwa kuwa wamepagawa
na pepo na inaonekana kuwa wakati mwingine pepo hao kwa wingi wao huweza kumkalia
mtu mmoja Marko 16;9,Luka 8;2 na athari
za kukaa kwa wingi ndani ya mtu ni pamoja na kuweko kwa kichaa, kupooza,na
magonjwa mengine, hususani yale
yanayohusiana na mfumo wa fahamu Mathayo 9;33,12;22, Marko 5;4,5 Mtu
anayemilikiwa au aliyepagawa na mapepo huwa wakati mwingine hawezi kujidhibiti
mwenyewe na roho hao wachafu huweza kutumia hata kinywa chake na kuzungumza, au
wanaweza kumfanya mtu kuwa bubu au asiyesikia
na huweza kuwaendesha wanaowavamia bila wao kupenda kama chombo chao na wakati mwingine kumpa
nguvu zao
UFAHAMU
ZAIDI KUHUSU PEPO.
Pepo kwa kiingereza ni Demon ambalo limetokana na neno la
kiyunani Daimon (Dainamon) ambalo
maana yake ni roho chafu zenye akili na uweza wa kufanya maajabu na kazi
nyinginezo mbalimbali
Mawazo ya kiyunani kuhusu Mapepo.
Kwa wayunani neno Daimon lilitumika na wazo kuhusu Mungu,
au nguvu za Mungu ambalo lilimaanisha pia nguvu zenye vurugu kuhusu Mungu au
mtu mwenye akili za kupita kawaida na mwenye uwezo wa kutabiri au kupiga ramli
au nafsi ya mwanadamu iliyoishi zamani na inayoweza kuunganisha watu na miungu,
hata hivyo pia neno hili lilitumiwa likihusihwa moja kwa moja na nguvu
zinazohusiana na kuleta magonjwa ambazo ziliaminika kuwa zinatawala mazingira
na maisha aidha pia mapepo walifikiriwa kuwa ni wazuri na wabaya na wengine
waliwafikiria kuwa ni mizimu, wengine walifikiria kuwa ni roho zinazomwangalia
mwanadamu na kumfuatilia tangu anapozaliwa na ambazo zinaweza kuwa rafiki au
adui, wengine waliwafikiria kuwa ni nguvu za kisasi zinazotoa adhabu kwa sababu
ya makosa Fulani, Baadhi ya wanafalsafa wa kiyunani kama Thales alisema kuwa
“kila kitu kimejaa miungu” wakati mwanafalsafa Pythagoreans Yeye alifundisha
kuwa anga lote limejawa na nafsi zinazoitwa Mapepo na mashujaa na ni nafsi
zisizo na mwili ambazo ziliaminiwa kuwa zimetumwa kushughulika na Afya na
magonjwa kwa wanyama na wanadamu ili kwamba wanadamu watafute utakaso na
kurejesha mahusiano na Mungu na kutenda mema, na kuishi kwa utaratibu
uliokusudiwa, Mwanafalsafa Heraclitus aliamini kuwa kila mtu ana pepo
linalomkalia na kumuongoza au kumdhibiti, na mwanafalsafa Empedocles alichangia
kuwa pepo ni roho wenye kutia shaka wasioweza kuelezeka vema wenye kushughulika
na uovu na kuna uwezekanao wakawa ni wanadamu waliogeuka kuwa kitu kingine baada
ya kufa kwao, Mwanafalsafa maarufu Socrates yeye alisema hapendelei kuzungumzia
swala lolote linalohusiana na mawazo yenye kuhusu uungu au vile visivyoweza
kuthibitika ingawaje aliheshimu kuwa huenda maswala hayo yako kutokana na
uzoefu anaokutanao mtu mmojamoja kupokea maoni ya kimungu na ishara mbalimbali,
Mwana falsafa Plato yeye alisema kuwa Pepo ni nafsi za watu waliokufa ambao
hutumika kufanya kazi tofautitofauti ikiwa ni pamoja na kutafasiri maswala
kadhaa kuhusu Mungu na wanadamu akiunga mkono hoja ya mwanafalsafa Heraclitus
yeye Plato aliamini kuwa kuwa muongozo
wa kweli wa mwanadamu uko katika akili zake ambazo ndio nafsi ambayo ni zawadi
kutoka kwa Mungu. Mwanafalsafa Aristotle hakuwa na wazo kubwa sana kuhusu
mapepo ingawa kwa kiasi Fulani aliamini kuwa kila mwanadamu ana mapepo ambayo
huambatana naye siku zote za maisha yake.Mwanafalsafa Stoics ni kundi
lililokuwa likiamini kuwa kila kitu kina Mungu Pantheism pia waliamini katika
maswala kuhusu nguvu za giza ambazo kwa uwezo wa kipepo mwanadamu anaweza
kuonyesha kuvumilia, kuonyesha hisia, maumivu na furaha na kadhalika waliamini
kuwa pepo wako katika hali ka hizo wakifurahia kuwepo kwao milele na kuwa wako
katika maeneo yote karibu na mwezi, wakati kundi la wanafalsafa wa Epicurus wao
walikwenda nje kabisa wakiamini kuwa hakuna mapepo na kuwa kama wako hawana uwezo
wa kuwasiliana na aina binadamu kwa njia yoyote.
Mawazo ya kikaldayo (Mesopotamia) kuhusu pepo.
Tangu mwanzo watu wa ukaldfayo au
Mesopotamia walikuwa ni wachawi kupindukia hii huenda ni kwa sababu ya kuishi
katika mazingira yaliyozingukwa na mfumo huo wa maisha uliochangiwa na dini
zao, kama ilivyo huko Misri mpango wao wa kimaendeleo ulikuwa ukichangiwa na
kuwako kwa mto Nile huko Mesopotamia nako waliishi wakipambana na mfumo kama huo
wa kuzungukwa na mto Tigris na Frati jamii ya kusumerian ilitoa tafasiri ya
maswala kadhaa kutokana na dini za asili za kimesopotamia na kujenga mawazo na kanuni huku wakiwa na
ufahamu wa juu kuwa mwanadamu ndie kiumbe wa juu zaidi kuliko uungu na hivyo
walikuwa na vihadithi vingi kuhusu ulimwengu wa chini yaani kuliko na miungu
kuwa kuna Anunnaki na miungu wengine waovu saba walioitwa Assakki au mapepo
ambao pia walikuwa wakishikilia nyadhifa za maeneo yao, ilifahamika wazi kuwa
kazi ya Pepo ni pamoja na kupigia ramli,kusababisha magonjwa hususani pepo
wanapoingia kichwani na katika maeneo ya kichwa na sehemu za ndani na ili
kufanikisha maswala hayo ilikuwa ni lazima kazi za kichawi zifanyike
zikihusisha uvaaji wa vifaa Fulani kama shanga na mapambo ya thamani na
yanayofanana na hayo,Pia walikuwa na imani kwamba ili kujilinda kutoka katika
mashambulizi ya magonjwa yatokanayo na nguvu za kichawi ambayo hupitia katika
mdomo pua na masikio miungu kama Ea ambaye ni miungu ya maji waliombwa ili
kusaidia aina hizo za uvamizi, Miungu hiyo ambayo ilikuwa na makuhani maalumu
pia ilikuwa na kazi za kutafasiri ndoto na kuondoa mapepo, mungu huyu Ea pia
aliitwa Madruk!, aidha mtu alipokufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya
kuzikwa utafiti ungeganyika kuweza kubaini sababu za kifo hicho kama ni mizimu
au mengineyo Mizimu hiyo ilijulikana kwa jina la Etimmu na makuhani wake
maalumu waliitwa Eship, Wakaldayo pia waliwapa pepo majina kulingana na
utendaji wa kazi wa mapepo hayo kwa mfano wako pepo walioitwa Rabisu au The
Croucher pepo huyu aliaminika kuwa na
uwezo wa kulala chini akijificha na kuvizia maadui ili kuwadhuru na
kuwashughulikia au kuwaua kwa msingi huo tendo kama lile la kaini kumuua Habili
alipoambiwa dhambi iko inakuotea kwa wakaldayo dhambi hiyo ni Pepo Rabisu
aliyemuingia Kaini ili kuvizia Habili na kumuua Mwanzo 4;7
Huenda ni katika sababu kama hizo Pepo
walipewa majina katika jamii ya kisumerian, watu wa Babeli walitoa nguvu kubwa
sana katika kuamini juu ya kuwepo kwa mapepo na kuamini nguvu za kichawi
waliamini pia kuwa ili mtu amtoe Pepo ilikuwa ni lazima awe ni kuhani anayejua
jina la Pepo huyo na tabia zake ndipo amtoe Marko 5; 9, Luka 8; 30 aidha katika
mazingira Fulani aina Fulani za magonjwa na matukio husababaishwa na mapepo.
Mawazo ya kimisri kuhusu pepo.
Kama ilivyo kwa tamaduni za
mataifa mengine hapo juu wamisri nao zamani sana waliamini kuweko kwa mapepo
wengi sana, na waliamini na kuzitegemea nguvu za mapepo hayo katika kila jambo,
wao waliwahusisha miungu yao na mapepo bila kuwatofautisha, waliamini kuwa ndio
waliohusika na kila aina za matukio yakiwemo mafuriko, dhuruba, kama ilivyo kwa
wakaldayo wamisri waliamini pia kuwa kila aina ya magonjwa ilisababishwa na
mapepo hao kuja na kumuibia mtu hali yake ya kawaida na kumuachia maumivu homa
na hata kifo na hivyo ili kujilinda nao ilikuwa lazima mtu kuvaa hirizi na vitu
vingine vya ulinzi, waliaminiwa pia kuwa pepo wanamiliki anga, pia wamisri
waliogopa sana mapepo yaliyokuwa na uwezo wa kuvaa mwili wa aliyekufa na kuja
kama mizimu ili kulipiza kisasi kwa binadamu wenye matendo maovu hivyo
waliogopewa sana na kupewa majina kama walipizi,wauaji,makata,na majina
mengineyo, waliamini pia kuwa pepo hao pia huja kuwa miungu, hata hivyo katika
Misri hwakuwa na imani kuwa kuna mapepo wanaoweza kuwavamia watoto au mapepo
waliokuwa na uwezo wa kunywa damu ya mtu kama ilivyo sehemu za Babeli.
Mawazo kuhusu pepo katika agano la kale na Vitabu vya apokrifa.
Katika jamii za kale za kiebrania
hakukuwa na hali kamili inayoeleweka kuhusu Pepo badala yake kuna majina
yaliyotumika kuwahusu kama mungu yalitumika pia kumaanisha pepo, Mungu aliitwa
Lohim na mtu mwenye kuvuviwa na aina Fulani ya nguvu za Mungu aliitwa mtu wa
lohim yaani mtu wa Mungu, au muonaji, kwa hiyo jina lohim lilitumika kumaanisha
nguvu Fulani inayojitengeneza na kusababisha ushindi au aina Fulani ya ushindi
kupitia mieleka mfano wa lugha hizi unaonekana katika Mwanzo 30;8, kwa hiyo
aina hiyo ya nguvu inapomjia mtu na kumuwezesha kutabiri ilifikiriwa kuwa ni nguvu ya Mungu au upepo
Ruah lohim mfano wa maswala kama hayo ni kama swala la Balaam Hesabu 24;2 au
kile kilichomtokea Sauli 1Samuel 10;11,19;20-23 na matumizi ya lohim
yakihusishwa na pepo pia yanaonekana katika
2Samuel 16;15-16,23
Yako matukio ambayo waebrania walifikiri
moja kwa moja kuwa yanatokana na Mungu, hata kama matukio hayo yalisababishwa
na shetani katika hali ya kawaida ilionekana ni kama Mungu ndiye anayeruhusu
shetani au mapepo kushughulika na mtu huyo mfano tukio kama la Saul 1Samuel
19;9-10, hali kadhalika hali mbaya iliyompata Ayubu ilifikiriwa kuwa inatoka
kwa Mungu Ayubu 2;7 kwamba maovu yaliyompata yalitoka kwa Mapepo au shetani
yakliruhusiwa na Mungu, Kwa msingi huo agano la kale lina maswala ya kufikirika
tu kuhusu elimu au ujuzi wa utendaji wa mapepo na shetani kwa ujumla “It is
some illusions” kwa msingi huo waebrania walikuwa na ujuzi kuhusu mapepo na
utendaji wa kichawi kutoka kwa mataifa mageni yaliyokuwa yakiwazunguka tu Kumkukumbu
32;16;17, Biblia ya Septuagint ilitumia neno miungu migeni ambayo kwa kawaida
ilikuwa ikihusisha au ikizungumzia mapepo au mashetani Zaburi 106;37 pia iliitwa, miumgu ya kipagani
na kwa namna Fulani Biblia inawataja hao kuwa majini katika Mambo ya Walawi 17;7,2Nyakati 11;15 pia waliitwa
jeshi la mbinguni Matendo 7;42-43.
Mawazo kuhusu pepo katika vitabu vya Apokrifa
Mafundisho kuhusu malaika kama
yanavyoonekama katika Apokrifa yana utata kama ilivyo katika khadithi za
kiislamu kuhusu Mapepo a majini mfano tunaona katika Kitabu cha 1Enoko15;9-16
kwamba malaika wenye tama walijaribu kutatua tatizo la kuweko kwa dhambi kwa
kuwaoa wanawake wa kibinadamu duniani. Kwa
ujumla mafundisho kuhusu viumbe hao wa kiroho katika apokrifa ni kama
maluweluwe “illusions” ingawa wengine inaonekana kuwa walinukuu historia kadhaa
za kweli ya kibiblia kuhusu msaada wa malaika kwa mfano 1Makabayo 7;41 tunaona
Yuda makabayo akiomba malaka kuwasaidia katika vita kama alivyofanya wakati wa
Hezekia na pia 2Makabayo 11;6, 15;22-23 inaonekana wazi kuwa Yuda Makabayo mara
kwa mara aliomba Munu kusaidia kmtuma malaika wake kwaajli ya msaada wa
kivita na Mungu aliwapa ushindi,wakati
kitabu cha kiapokrifa cha hekima ya Suleimani hakina nukuu yoyote kuhusu
malaika au pepo zaidi ya kunukuu kila kinachofanana na ufafanuzi wakitabu cha
kutoka Hekima ya Suleimani 18;15. Vitabu vingine vya apokrifa vina hadithi
ambazo zimetiwa chumvi sana kuhusu malaika na mapepo baadhi wanaamini katika
malaika wema na wabaya lakini katika hali iliyotiwa chumvi mmno na wengine
wanaaamini kazi zao mfamo kitabu cha Tobia, agano la mababa 12, ufunuo wa
Baruku, 2Edras na kitabu cha jubilee. Mwandishi anaonekana kuzungumzia
akihisisha matukio ya asili na maswala ya kiroho kama ilivyo katika kitabu cha
Ayubu. Ayubu 2;2,10;5 wakati kitabu cha agano na mababa 12 kinazungumzia kuweko kwa tabia mbaya kwa wanadamu kama
matokeo ya kazi za kipepo wakiwemo pepo saba wa udanganyifu, roho hizo ndio
zinazowaongoza wanadamu katika kufanya dhambi na kwa ujumla ilikuwa ikifikiriwa
kuwa utendaji huo unafanyika chini ya uongozi wa Beliariau Shetani kama
inavyogusiwa katika Zaburi ya 18;4-5.
Vitabu vya ufunuo vya kiapokrifa
vingi vinamaoni kuwa Mungu alimpindua shetani na nguvu ya wema ikaanza kutawala
kabla ua ulimwengu kuumbwa Asher 1;9,6;2 Jarubu la Daniel 1;6 Jaribu la Yuda
13;3,14;2 kwa ujumla kuna mawazo mengi ya kipagani katika apokrifa kuwahusu
Pepo au malaika kwa ujumla wayahudi wenye msimamo mkali walikuwa wanachangamoto
za kutaka kuonyesha uwezo wa Mungu na ili kuueleza vema kwa wanadamu wengi
walimfikiri shetani kuwa pepo mkuu aliyejaribu kumpotosha mwanadamu Hekima ya
Suleimani 2;4 na Enoko 3;31 waandishi hao walimpa jina shetani kama Diabolos
yaani asi wakimuonyesha sawa na nyoka aliyemdanganya Hawa katika Bustani ya
aden, aidha wengine walikuwa na mashaka kuwa viumbe hao mashetani walimuasi
Mungu pale walipojaribu kuwaingilia wake za Binadamu Mwanzo 6;1-4 na Ezekiel
28;13-17 inasemekana mazwazo uya aina hii yanadhaniwa kupandikizika na watu
walioamini kuwa kila kitu ni kiovu hivyo kwa tendo la amalaika kuwaingilia
Binadamu walitenda uovu “Dualism” imani inayoamini kuwa kila kitu ni kiovu
ukiwem mwili.
Katika vitabu vyenye asili ya
kiapokrifa habari za kusisimua zaidi kuhusu malaika tunaipata katika kitabu cha
Tobia au tobiti pia tunaona habari ya
utendaji wa kijini (Pepo) na kutajwa kwa malaika Rafael ambaye anajitambulisha
kuwa mmoja wa malaika saba walio watakatifu na wanaopeleka sala za watakatifu
na kuingia katika utukufu wa Mungu Kitabu cha Tobia 12;15-21. Kwa ufupi katika
kitabu cha tobiti tunaona jina la
msichana aliyekuwa akiitwa Sara ambaye kila alipokua anakaribia kuolewa Mumewe
aliuawa na jinni usiku wa siku ya harusi
na ilitokea hivyo mara saba Jini
lililokuwa likihusika na kazi hiyo liliitwa Asmodeo jinni la kiume kwa sababu
ya misiba hiyo Tobiti na Sara waliamu kumuomba Mungu ili wafe kwa kukata tama lakini Mungu
aliwahurumia na kugeuza huzuni yao kuwa furaha
akamtuma malaika Rafael amsindikize mwanadamu Tobia kwa Raguel baba wa sara , huo wakaozwa na kifo hakikutokea tena, Hizi ni habari za
kusisimua kuhusu malaika na majini katika utendaji wao kama tuonavyo katika
kitabu hki cha Tobiti chenye asili ya kiapokifa kwa ufupi kinaonyesha kazi za
majini na kazi za Malaika katika jukumu lilelile la kuwahudumia wanaomcha
Mungu.
Mwandishi na mchoraji maarufu
Francesco Botticini alichora habari kutoka kwenye vitabu vya apokrifa
akionyesha malaika watatu wakimsindikiza Tobia Malaika aliyemshika mkono tobia
ndiye malaika Rafael Picha hii
ilichorwa mwaka 1470 na ilihifadhiwa huko Uffiz Gallery huko Flolrence Italy.
(Tobiti 12;1-21)
Mtazamo wa waislamu
na Quran kuhusu Mashetani, Majini na Malaika
Waislamu wanaamini
kuwa kuna viumbe walioumbwa na Mungu ambao hawaonekani kwa macho ya kibinadamu
viumbe hawa wamegawanyika katika makundi makuu matatu.
- Shetani
Shetani ambae
hutambulika pia kama ibilisi “iblis” ameitwa hivyo kwa sababu alilaaniwa na
Allah kwa kukataa kumtii allah
alipomuamuru kumsujudia Adamu mara baada ya kuwa amemuumba (Surat al-baqara 2;28-38 na al aaraf 7;10 na al khaf 18:50) kutokana na laana hiyo
alipewa muda na Allah ili awapoteze watu kwa kuwakalia pande zoote na alipewa
ruhusa baada ya kujiombea kufanya hivyo(al-aaraf
7;16-17)Allah alitoa nafasi ya kuingia motoni kwa yeyote atakayemfuata
shetani,Hivyo kwa waislamu shetani ni adui mkubwa na hulaaniwa kila mwislamu
anapotaka kufanya jambo lolote hujikinga na muovu huyu kwa dua hii “ aaudhubiiIlah mina shaytwaani rajiim” yaani
najikinga kwa allah na shetani apigwae mawe,ameitwa apigwae mawe kwa kuwa
Ibrahimu na mwanawe Ismael walimpiga mawe Punde alipotaka kuwadanganya wasiitii
amri ya Allah ya kutaka kumtoa Ismail dhabihu,Mashetani ni kundi kubwa sana na
baba yao majini ni shetani.Vitabu maarufu vya kiislamu vinathibitisha soma (Itqaan fiy’uluwmi al-juzuu 4 uk 374,hadith
5,553).
·
Majini
Kumbuka shetani alikuwa miongoni mwa
majini(al-kahf 18;50) hivyo shetani
ni jinni na jinni ni shetani,quran inafundisha kuwa viumbe hawa waliumbwa kwa
ndimi za moto(al-Hijir 15;26-27,ar
–Rahman 55:14-15) woote wanaofanana na shetani woote wamezaliwa na shetani
woote kazi zao zinafanana,Hivyo majini yana nafasi kubwa sana katika uislamu
kujaribu kuwatenga majini na mashetani
ni kiini macho tu kwani majini yalisilimu (surat 72;1-14) ingawa kuna kundi lingine halikuslimu, Hata hivyo
Allah aliwatumia woote katika kazi mbalimbali
mfano kumsaidia Sulemani katika kazi zake mbalimbali za ujenzi, kumletea
johari na vito vya thamani toka baharini,kumjengea nk.Soma (Surat al anbiyaa 21;81-82)Allah alikuwa
mlinzi yaani msimamizi, Allah pia huwatumia majini kufarikisha watu aliwatumia
huko Babeli na kufundisha watu uchawi hawa mashetani huitwa Haruta na Maruta soma (al-Baqara 2;102)
aidha katika namna ya kushangaza Allah alimletea kila nabii maadui aliowatuma
mwenyewe yaani majini na Mashetani (surat
al anam 6;112 na al-Hajj 22;52).Baadhi ya Madhehebu kama ahmadiyya
walipogundua kuwa majini ni mashetani na mashetani ni majini walianza kukataa
dhana hii na shehk Farsiy anawakanusha vikali katika ufafanuzi chini,Waislamu
wanatambua kuwa majini ni ndugu zao na ndio maana moja ya mashart ya swala
katika kumalizia kikao cha mwisho kiitwacho (atahiyat) lazima kwa kila Muislamu asalimie pande zoote mbili
yaani kwa kugeukia kushoto na kulia,kushoto ni kusalimia muislamu mwenzako na
kulia ni kusalimia kundi kubwa la majini ambao hujumuika na waislamu katika
swala (arshad-alMuslim) hii ni
lazima hata kama mwislamu atakuwa pekeyake wakati wa swala kwani majini
hujumuika nae.Aidha muhamad anasema kila muislamu anapozaliwa anapata ulinzi
toka kwa majini na mashetani (soma
al-muslim,Miskat), Majini yana ufahamu mkubwa sana wa quran na uislamu,
yameslimu Muhamad alipokwenda kwa majini na kuanza kuwauliza mambo ya uislamu
majini yalijibu vizuri kuliko wanadamu soma (surat al ahqaf 46;29-30) soma pia ufafanuzi wa aya hiyo chini
katika quran ya Farsiy.Kwa ujumla hutakutana na jinni ambalo lina jina la
kikristo majini yoote yana majina ya kiislamu anaeleza Desmon Mkumbo moja ya
wataalamu wa huduma ya biblia ni jibu Tanzania.Majini pia huhubiri Uislamu kwa nguvu na huhusika kusilimisha watu ukiwa
na ugonjwa au pepo limekupagaa ukipelekwa kwa sheikh au maalim akusomee duwa
utapewa masharti ya kubadili dini,jina, kusilimu au kuswali haya ni maagizo ya
majini Mwenye masikio na asikie!.
·
Malaika (malaikat)
Hili ni kundi la tatu katika imani ya
kiislamu kuhusu viumbe wasioonekana kumbuka waislamu huamini malaika na
inasemekana kuwa Allah aliwaumba viumbe hao kwa nuru,Idadi yao haijulikani,kazi
yao ni kumsifu Allah wako malaika wa muhimu watano nao ni jibril huyu ndiye
malaika mkuu Allah humtuma kuwasiliana na manabii wake Quran humuita Roho
mtakatifu (surat an nahl 16:102). Ni
Roho wa mafunuo na Nguvu Laylatul-Qadr (surat
al qadr 97;1-4)Mikail huyu yuko chini ya jibril (al baqara 2;98),Israfiil
ni malaika anayeaminika sana,anasifika sana hatajwi katika quran lakini
anaaminika kuwa ndiye atakaye puliza parapanda siku ya mwisho, Izrail pia hatajwi katika quran lakini
anaaminika kuwa ndiye mtoa roho za watu (al
anam 6:61),Hamalat al arsh hawa wako nane inaaminiwa kuwa watabeba kiti cha
Allah siku ya hukumu (al- haqqah 69;17), Waislamu huamini pia wako malaika wengine watano ambao
hujulikana kwa kazi zao hao ni hafadhan hulinda binadamu kutoka katika mikosi
na balaa kwa mujibu wa Muhamad katika hadithi zake anadai wako kumi.Katibun
hawa huandika habari za mtu wako wawili mmoja huandika habari za matendo mabaya
na mmoja mema, wa mabaya hukaa kushoto wa mema hukaa kulia kila mtu anao wawili
(az-zukhuf 43;80 na qaf 50;17-18),Malik
ni mlinzi wa moto wa Jehanam(az-zukhuf
43;77),Ridhiwan hulinda pepo (paradiso),Munkar
na Nakir hawa ni wakali sana huuliza
maswali kaburini mtu anaezikwa huulizwa maswali juu ya uislam, hivyo muislamu
anapozikwa Masheikh humfundisha namna ya kujibu maswali hayo mtu aliyezikwa ili
kumuepusha na adhabu ya malaika hao.
Mtazamo wa mapepo katika agano Jipya:
Wakati waandishi wengi wa nyakati
za agano la kale hawakuwa na mvuto wowote kuandika habari kuhusu mapepo
waandishi wengi wa Agano jipya walizungumzia sana swala la mapepo huenda ni kwa
sababu labda Yesu alikuwa na huduma ya kutoa pepo kwa sababu hiyo katika agano jipya kuna nukuu
nyingi sana kuhusu pepo ambao kimsingi walifikiriwa kuwa ni viumbe vya kiroho
ambavyo ni adui wa Mungu na wanadamu na mkuu wao alifikiriwa kuwa ni Belizebuli
Marko 3;22 ingawaje pia kuna nukuu chache sana
kuwahusu Pepo pia walifikiriwa kuwa ni miungu migeni Matendo 17;18,
Waliitwa pia mashetani 1 Koritho 10;20,Ufunuo 9;20 kwa kiyunani neno mashetani
linasomeka “Dainamonia” ambayo
ilimaanisha miungu ya kipagani na sio “Demons”
yaani mapepo na hii ilitokana na kutolewa sadaka kwa miungu, kwa mafundisho ya
Kristo kuhusu uwezekano wa kutokuwatumikia mabwana wawili Mathayo 6;24, Luka
16;13 kuweko kwa huduma za kiinjili za utoaji mapepo katika agano jipya ni wazi kuwa inaashiria uwezo wa Kristo wa
kuwa kinyume na Mapepo na Nguvu za giza na Biblia agano jipya linaonyesha wazi
kuwa kutoa pepo sio kazi rahisi ni vita Mathayo 17;19, Marko 9;28 na ni
uthibitisho ulio wazi kuwa Yesu Kristo ana nguvu kubwa kiasi gani na ni uthibitisho
ulio wazi kuwa Pepo wanatambua wazi kuwa
asili ya Kristo ni Mungu Luka 11;15, Yohana 7;20,10;20 na hii inathibitisha
wazi kuwa ule usemi wa Yesu kuwa ufalme hauwezi kusimama ukifitinika kwa nafsi
yake kwani utaanguka Luka 11;17-18 kwa msingi huo Kristo aliweka wazi kuwa
anatoa Pepo kwa Chanda cha Mungu kwa hiyo kutoa pepo ni sehemu ya kuusimamisha
ufalme wa Mungu na kubomoa ule wa Shetani Mathayo 12;28 Yesu pia alishirikisha
karama hii ya utioaji wa mapepo kwa wanafunzi wake Luka 9;1 na 10;17 ni wazi
kuwa walirudisha Ripoti kuwa Pepo wana watiii kwa jina la Yesu.
Katika agano jipya maneno mawili
pia yalitumika “Ponera” la kiyunani
kumaanisha Pepo na “akatharta”
ikimaanisha roho chafu ingawaje katika mazingira dulani roho chafu na pepo
hutumika kwa kubadilishana Luka 8; 27-29
ni katika Luka 11;24 kwa Kiswahili neno pepo mchafu hutumika zaidi Marko 1;23,7;25,
Kwa msingi huo ni wazi kuwa pepo ni jeshi la shetani a,bal liko kinyume na
Mungu na wanadamu na kuwafukuza na kuwatoa kwa jina la Yesu ni fundisho lililo
wazi kuwa ufalme wa Mungu uko kazini na ni wazi kuwa Yesu ana nguvu dhidi ya
kazi za shetani na kuwa Yesu ni Mungu.
MAPEPO NA ASILI YA UOVU:
Kwa asili Biblia agano jipya
inatufunulia wazi na kutufundisha wazi kuwa kuna uhusiano wa Karibu kati ya
uovu au mambo mabaya au magonjwa na mapepo ingawa tunaweza kusema kuwa si yote
lakini katika mazingira kadhaa aliyokutana nayo Yesu katika huduma yake na
katika swala zima la ufukuzaji wa Pepo ni wazi kuwa uko uhusiano huo Mathayo
4;1-11 Marko 1;12-13 na Luka 4;1-13 mjaribu aliyetaka Kristo atende uovu
alikuwa ni shetani, pia tunaona asli ya uovu sehemu nyingine ni waz kuwa
muhusika wa aina hiyo ya uovu ni shetani na majeshi ake yaani pepo Marko 5;9,
Luka 8;30 ni wai kuwa Kristo alitaka kuonyesha ni kazi gani mbaya wazifanyazo
mashetani na wanapowaingia binadamu husababbisha maovu makuu mmno na zaidi ya
yote ni wazi kuwa nguvu zao hazina kitu dhidi ya utendaji wa Mungu Mathayo
7;22.
Pepo kutoka kwa jina la Yesu swala hili
lilimaanisha kuwa kuna nguvu katika jina la Mungu au ni wazi kuwa Kristo
alikuwa anabeba nguvu ya uungu tangu zamani waandishi walionyesha uhusiano
ulioko wenye nguvu katika jina la Mngu Zaburi 20;7, 118;12 ni wazi kuwa tangu
zamani Mungu aliwapa watu wake ushindi kupitia jina lake maadui wa watu wa
Mungu waliweza kukatiliwa mbali, na kwa sababu weng walifahamu uwea unaotenda
kazi ndani ya Yesu Kristo walishawishika kulitumia jina lake kwa ajili ya
kufukuza Pepo Matendo 19;13
Jina Muharabu (Muharibu)
“destroyer one” anayetajwa katika 1Koritho 10;10 huwa haimaanishi kuwa ni
shetani au pepo lakini ni wazi kuwa ni malaika wa Bwana aliyepita jioni ile
kuwahukumu Wamisri alihusika katika kuhukumu waovu au waasi 2Samuel 24;16, pia yuko malaika ambaye ni mfalme aliitwa pia malaika wa kuzimu kwa kiebrania
Abadoni na kwa kiyunani Apolioni Ufunuo 9;11 huyu naye inaonekana kuwa ni
shetani.
Makala na
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
+255718990796
+255784394550
Maoni 8 :
Mafundisho mazuri
asante sana Charles Bieda Mungu akubariki kwa kufaidika na Mafundisho hayo
Mafundisho yako ni mazuri, Asante Kuna vitu vingi nimejifunza.
Isipokuwa waislamu wanapotoa salamu baada ya sala, ni wanamsalimia Malaika wa ulinzi aliyeko kushoto na aliyeko kulia. Sio kweli kuwa kulia wanasalimia muislam mwezao na kushoto wanalima majini. Waislamu wanaamini Kuna Malaika wa ulinzi aliyeko kulia ambae kazi yake ni kuandika mema yake, na yule Malaika wa kushoto kazi yake ni kuandika maovu yake. Inaweza fanana na Malaika aliyetajwa zaburi ya 91:11 ambae anakuwa na sisi kila mahali.
Otherwise nimependa mafundisho yako
Asante kwa mafundisho.mazuri, nimejifunza sana
Good!
Mafundisho mazuri sana ubarikiwe
Mafundishi mazuri
Haya mafundisho yameshiba barikiwa sana mtumishi wa Mungu.
Chapisha Maoni