Shule Maalumu ya Uongozi somo namba moja
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
Somo; Wito wa kuwaongoza Kondoo.
Leo Tunaanza kujifunza mfululizo wa masomo yahusuyo
shule ya uongozi kwa kujifunza somo hili la msingi “Wito wa kuwaongoza kondoo”Tutajifunza
Somo hili kwa kuligawa katika vipengele vitano vifuatavyo;-
·
Watu
waliookoka huitwa Kondoo
·
Mungu
ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo
·
Wachungaji
wanadamu
·
Jinsi
isivyowezekana Mchungaji kuongoza kondoo peke yake
·
Wito
wa kuwaongoza kondoo.
* Watu
waliookoka Huitwa Kondoo.
Watu waliookoka huitwa kondoo (zaburi 79;13;100;3;Yohana10;27-28) Kwanini wanaitwa kondoo,Kondoo ni
wanyama wasioweza kufanya lolote bila kuongozwa au kupewa msaada wa Kiroho,wao
hutembea wakitazama chini na kuiangalia miguu ya kiongozi wao yaani Mchungaji
wao Kondoo wanahitaji Malisho na kunyweshwa maji (Mwanzo 29;7,Yohana 10;2-4).Kondoo
watatulia mahali Fulani wakingoja Maelekezo ya Kiongozi wao tofauti na Mbuzi au
wanyama wengine na kutafuta Malisho
wenyewe nk.Siyo hilo tu kondoo ni rahisi sana kuvamiwa na wanyama wengine
wakali na kuuawa bila kujitetea kwa lolote
hawana mbio kama wengine wala viungo vya kujitetea kama pembe kali
nk.hivyo maisha ya kondoo yanahitaji
sana Mchungaji au kiongozi Kadiri mchungaji
wao alivyo shujaa ndivyo wanavyo faidika, mchungaji akiwa mtu mbaya nao
pia Hudhurika (1Samuel 17;34-35, Yohana
10;11-12)Hivyo maisha ya watu waliookoka yanatutegemea sana sisi viongozi
Tukiwa wema kondoo wataishi maisha Mazuri ya kupendeza(Yeremia 50;6;Ezekiel 34;5-6)
Kilio cha kondoo wakati woote ni kupata kiongozi wa kuwaongoza wao hulia
wakati wote wakisema ni nani atakayeniongoza hata Edom(zaburi108;10)Bila kiongozi
watu waliookoka wanaweza kufanya yaliyo mema machoni pao wenyewe na
kumhuzunisha Mungu. (waamuzi 21;25).
* Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa Kondoo.
Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo
ambao pia ndio kanisa ni kondoo zake kanisa ni mali yake (Waebrania 13;20;1Petro 5;4;Zaburi 23;1-3).Mungu kama mchungaji mkuu
wa kondoo,Yeye ndie Kiongozi mkuu wa kondoo wake na maongozi yoote ya Kondoo
hutokana na neno lake(Kutoka
13;17;Yohana8;47;Zaburi 119;9)hata hivyo ingawa Mungu ndiye Mchungaji mkuu
wa kondoo katika mpango wake wa Uongozi ameweka wachungaji wanadamu ambao
hufanya kazi pamoja na Mungu(1Koritho
3;9).
*
Wachungaji wanadamu.
Katika
mpango wake Mungu anawaongoza kondoo wake kwa kuwatumia wachungaji wanadamu(zaburi 78;70-72;2Samuel 5;1-2, Zaburi 77;20
Kutoka 15;22 Hesabu 27;15-21 Yohana
21;15-17).Mungu huwatumia wachungaji wanadamu hawa kufanya kazi ya
kuwaongoza kondoo kwa maelekezo ya neno lake(Kutoka 32;34)Hata hivyo uongozi wa wachungaji hao wanadamu wanadamu hufikia mpaka wanapokuwa na
kundi kubwa la kondoo nao huitaji wanadamu hawa wengine wengi wa kutenda kazi
pamoja nao
* Jinsi isivyowezekana Mchungaji kuongoza
kondoo Peke yake.
Kadiri
kanisa linavyoongezeka kunakuwa na kundi kubwa la kondoo wanahohitaji
uongozi.kiongozi mmoja hata angekuwa na
uwezo Mkubwa namna gani huelemewa na kushindwa kukidhi mahitaji ya uongozi wa
kondoo wengi, matokeo yake kondoo wengi hujisikia upweke kwa kukosa msaada wa
uongozi na matokeo yake hutawanyika na kuliacha kanisa hilo na kutafuta mahali
Pengine wanapoweza kupata uongozi wa maisha yao lakini wengine kwa kukosa
uongozi hurudi nyuma na kuacha wokovu(Waamuzi 18;1,30-31). Kiongozi Musa alipokuwa amewaacha kondoo bila kiongozi
,pale alipopanda mlimani Sinai kupokea amri kumi za Mungu huku nyuma kondoo walipoona hawana kiongozi maana kiongozi wao amekawia
kurudi walirudi nyuma na kuacha wokovu na kufanya machukizo makubwa mbele za Mungu.(Kutoka 32;1-8,15-24).Ufumbuzi wa Tatizo la watu waliookoka kurudi nyuma na kuacha
wokovu ni kuwa na viongozi wengi
wanaomsaidia Mchungaji.Kadiri tunavyokusudia kanisa letu kuwa na watu wengi
zaidi ndivyo inavyotupasa kuwa na viongozi wengi zaidi wa kumsaidia Mchungaji
kuliongoza kanisa,Viongozi hawa watakuwa wanashughulikia matatizo madogomadogo
ya kondoo na kuyapatia ufumbuzi na yale makubwa tu ndiyo yatakuwa yanapelekwa
kwa Mchungaji, Bila kufuata mpango huu Kanisa litadumaa na haliwezi kuongezeka
kiimani na kiidadi, Hata kama watu wengi watakuwa wanakata shauri,hawataendelea
katika zizi la kondoo kwa kukosa uongozi.Musa na watu wake waliukubali na
kuufuata mpango huu wa Mungu na matokeo yake walifanikiwa (Kutoka 18;13-26) Bwana amusaidie kila mmoja wetu ili tusiwe
kwazo la kukua na kuongezeka kwa kanisa.
*Wito wa Kuwaongoza kondoo.
Kilio
cha watu wa Mungu humfikia Mungu (Kutoka
2;23;Mwanzo 18;20-21,Yakobo 5;4)
Kondoo wa Mungu wanaohitaji uongozi
wanapolia wakisema nina atakayetupeleka
hata mji wenye Boma?ni nani atakaye tuongoza hata edomu (Zaburi 108;10).Kilio hiki humfikia Mungu,Kondoo hawa wana wasi wasi
wa kulala Porini na kuwa katika hali ya kushambuliwa na mbwa mwitu au simba
wanataka kiongozi atakaye wapeleka kwenye mji wenye Boma (yaani zizi la
kondoo).Kondoo hawa pia wanalia wakihitaji mtu wa kuwaongoza hata wafike Edomu nchi yenye
malisho mengi na maji mengi(Hesabu
20;14-19).Ndivyo kondoo wa Mungu wanavyolia pia,wanahitaji viongozi
watakaohakikisha wokovu wao unadumu na hawawezwi na shetani samba aungurumaye
na tena wanahitaji viongozi wa
kuwahakikishia wanapata malisho na kuangaliwa na kutunzwa ili wafurahie raha ya
Wokovu. Kilio hiki cha kondoo kikimfikia Mungu ,Mungu nae anatoa wito kwa watu
wake akitaka wajitoe kuwaongoza Kondoo yaani kiongozi wa kanisa,Mungu anauliza
Hapana hata mmoja wa Kumshika mkono? Miongoni mwa wana wote aliowalea(Isaya 51;18) Kwa sababu hiyo mungu anauliza
ni nani atakaye kwenda kwa ajili yetu?-Isaya 6;8 Isaya alisema Mimi hapa, sisi
nasi hatupaswi kumuachia mchungaji pekee kuifanya kazi hii peke yake na hivyo
tunapaswa kushirikiana nae katika kulitunza Kundi.
Shule
maalumu ya uongozi somo la Pili
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
Somo;
Faida ya kuwa kiongozi wa kanisa.
Wanafunzi wa Yesu waliitikia wito wa Mungu
na wakawa tayari kuwaongoza kondoo,na wakawa tayari kuacha vyoote walivyokuwa
navyo ili kutekeleza wito huo Hata hivyo waliuliza Tutapata nini Basi (Mathayo 19;27).Kila mmoja wetu
angependa kuwa kiongozi wa kaniasa kama angefahamu faida za kuwa kiongozi wa
kanisa kwa sababu hii somo letu la pili katika mfululizo wa masomo ya shule ya
uongozi ni Faida za kuwa kiongozi wa kanisa,tutajifunza somo hili kwa
kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-
*Gharama za kuwa kiongozi
wa kanisa
*Kukwepa uongozi wa kanisa
*Faida za kuwa kiongozi wa
kanisa
*Gharama za kuwa kiongozi wa kanisa
1.Gharama za kuchukua udhia,Mizigo na mateso
ya kondoo.
Kuwa
kiongozi wa kanisa ni tofauti kabisa na
kuwa kiongozi wa mataifa yaani kuwa
kiongozi wa serikali au shirika la umma au kampuni Fulani,mtu anapokuwa kiongozi
katika shirika,au kampuni Fulani au serikalini uongozi huo kwa kawaida huambatana
na maslahi Fulani heshima na marupurupu au maslahi makubwa na kupata raha au
kustarehe zaidi,Uongozi wa kanisa ni tofauti kabisa,huu ni uongozi wa kitumishi
ni kuwatumikia kondoo wa mungu kwa kuchukua udhia na mizigo yao na kukubali
mateso ya aina yoyote ile nyakati za biblia mtu aliyekuwa kiongozi alikuwa
akikabiliwa na kuuawa wakati wowote (1Timotheo
3;1…) Lengo la uongozi huu ni kurahisisha matatizo ya kondoo wa bwana ili
waweze kuingia mbinguni.hivyo hatupaswi kutumaini maslahi yoyote hapa duniani
isipokuwa kutazamia malipo yetu mbinguni,Yesu kristo alikuwa ni kiongozi
atumikaye ,kiongozi wa kanisa naye anapaswa kutumika bila kutegemea faida za
kidunia kama ilivyo kwa viongozi wa kawaida wa duniani (luka 22;24-27).Kuwa kiongozi wa kanisa ni kukubali kubeba mizigo ya
watu na kuwafanya wapumzike (Mathayo
11;28) kubeba mizigo ni kubeba huzuni zao,na masumbufu ya aina yoyote ile
ili waone raha katika safari yao ya kwenda mbinguni (Kutoka 18;21-22) ni kuwa kama mama au baba anaye beba mizigo na
udhia wa watoto wanaohitaji malezi ni kama mtumwa anayebeba mzigo wa bwana wake
ili yeye atembee kwa raha,kazi ya maongozi ya kiroho si kazi nyepesi ni nzito
ina lawama huwezi kuwapendeza woote na hawawezi kuridhika na lolote
utakalowafanyia, watakuteta, watasema kuwa huwajali, watakulalamikia na
kukulaumu, watakupiga mawe na wakati mwingine watakukataa na itakupasa
kuendelea kuwatumikia bila kujali haya yaliwapata wengi wa viongozi waliokuwa
viongozi wakubwa akiwemo Musa (Hesabu
11;11-15;kumbukumbu 1;9-18).
Kiongozi katika kanisa hapaswi kuwaza juu
ya malipo ya kazi anayoifanya ni
viongozi wachache sana wa kanisa ndiyo watapaswa kutunzwa na kanisa kwa mapato
ya kanisa hawa ni wale tu wanaokuwa wameacha shughuli nyingine ili wapate muda
wa kulihudumia neno kama ilivyokuwa pia wakati wa kanisa la kwanza (Matendo
6;2-4). Ingawaje hata Paulo na barnaba
kwa kipindi Fulani ilibidi wafanye kazi
ili kupata mahitaji yao na ya wale waliokuwa wakiwaongoza (Matendo 20;33-35;!Thesalonike 2;9) mtume pauilo alifanya hivi ili
kupata mahitaji ya wale aliokuwa akiwaongoza hivyo viongozi woote ambao
wanamsaidia mchungaji inawalazimu kufanya kazi kama zile za kaisari ili kupata
mahitaji yao na kukulisaidia kanisa aidha ni muhimu kukumbuka kuwa Paulo
alifanya vile ili kutoa kielelezo kwa Wathesalonike ambao walikuwa hawataki
kufanya kazi (2thersalonike 3;6-9).
2 Gharama za kujikana
nafsi zaidi kwa ajili ya kondoo.
Viwango vya mungu kwa kiongozi wa kanisa ni
vya juu zaidi kuliko vile vya kondoo wa kawaida,yako mambo ambayo yatakuwa
halali kwa kondoo wa kawaida kuyafanya lakini yasiwe halali kwa kiongozi wa
kanisa kuyafanya, Kwa mfano nyakati za agano la kale ilikuwa ni halali kwa watu
wa kawaida kunyoa nywele zao,Kurarua mavazi yao na kuomboleza walipopatwa na
misiba (2samuel 1;11-12,ayubu 1;18-20).
Hata hivyo kuhani au kiongozi wa kanisa
wa nyakati hizo yeye hakuruhusiwa
kufanya hivyo au kufanya mambo mengine kadhaa wa kadhaa ambayo wengine
walikuwa wameruhusiwa kuyafanya (Walawi
21;10-15) Hata wanawe Haruni; Nadabu na Abihu walipokufa Haruni kiongozi wa
kiroho hakuruhusiwa, kuomboleza,kuwazikana kunyoa nywele zake (Walawi 10;1-7) Kwa msingi huu kiongozi
wa kiroho kwakweli anapaswa kujikana nafsi yake
kwa ajili ya wengine (Yohana
10;11;Marko 8;35)Wakati mwingine itakugharimu kuwa wa mwisho kuondoka
kanisani wakati viongozi wengine wako majumbani (Mathayo 14;22-23)Wakati mwingine inaweza kukugharimu kutokwenda
likizo endapo kufanya hivyo kunaonekana kutaathiri utendaji wa kazi ya Mungu.
Kukwepa
uongozi wa kanisa
Baada
ya kuwa tumefahamu mzigo huu mkubwa wa
kuwa kiongozi wa kanisa watu wengine waliookoka ,hutafuta visingizio mbalimbali
vya kukwepa uongozi wa kanisa na kuona bora wawe kondoo wa kawaida katika
kanisa (Kutoka 4;10;13;Yeremia 1;4-6)
Hawa watakuwa ni watu wasiofahamu faida za milele zinazoambatana na kuwa kiongozi
wa kanisa,hii ni sawa na mtoto anayetoroka shuleni kwa madai eti kuwa masomo ni
magumu,mwanafunzi wa jinsi hii atakuwa hajui faida zinazoambatana na
kusoma,mkulima anayekubali taabu ya
kilimo huwa wa kwanza kufurahia apatapo chakula tele,wale wanaokwepa mzigo wa
kilimo hupata shida baadaye .(2Timotheo2;6;Mithali 28;19).
Faida za kuwa kiongozi
wa kanisa
Isaya
alipomwambia na Mungu “MimI hapa nitume
mimi” nakuanza kufanya kazi ya Mungu
kama kiongozi wa Kiroho,hatimaye alifikiri kuwa anajitaabisha bure na kutumia
nguvu zake bure bila ya faida,lakini baadae akakumbuka faida au thawabu zinazoambatana na kuwa kiongozi wa kiroho hivyo aliendelea
kumtumikia mungu mpaka mwisho alipouawa
kwa kukatwa misumeno (Isaya 49;4,Ebrania
11;37).sisi nasi ni muhimu kufahamu kuwa kuna faida za kuwa kiongozi wa
kiroho katika kanisa na hili litatutia moyo kumtumikia Mungu kwa gharama yoyote
Faida hizi ziko katika makundi makuu mawili
1. Faida za Duniani.
Ziko ahadi nyingi za Mungu alizozitoa kwa
kiongozi wa kiroho yeyote anayemtumikia Mungu ni wajibu wetu kumkumbusha Mungu
wakati woote wa utumishi wetu (Isaya
43;26);-
- Kuheshimiwa na Mungu(Yohana,12;26) Mungu anapokuheshimu hukupa kipaumbele
- Kuna kula na kushiba (Kumbukumbu 11;13-15;Isaya 65;13).
- Atabariki chakula chako na maji yako, atakuponya, hapatakuwa na aliyetasa wala mwenye kuharibu mimba na hesabu ya siku zako ataitimiza (Kutoka 23; 25-26).
- Mungu atakuponya katika hatari yoyote kubwa itakayokuja au inayokukabili (Daniel 6;16,20-22)
- Mungu atakuwa pamoja nawe katika kazi yote ya utumishi mpaka kazi yake itakapomalizika (1Nyakati 28;20).
2. Faida za Milele
- Kung’aa kama nyota milele na milele (Daniel 12;3)
- Atakuwa na daraja njema (1Timotheo 3;1,12-13 na Ufunuo 21;14)na katika utawala wa Kristo miaka elfu duniani watapewa utawala (Luka 19;15-19).
- Kuna taji ya utukufu isiyokauka (1Petro 5;1-4)
- Kuna taji isiyoharibika(1 Koritho 9;23-25)
- Atakuwa miongoni mwa wale waliobarikiwa (Mathayo 25;34-40)
- Atalipwa mshahara mkubwa mbinguni na kujaa furaha tele (Yohana 4;35-36).
Shule maalumu ya uongozi somo la Tatu
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
Somo;
Kuigwa kwa kiongozi wa Kanisa
Hakuna furaha kubwa kwa baba yetu wa
Mbinguni anayoipata kuliko anayoipata
anapowaona watoto wake wanaitikia wito wa kuwaongoza kondoo wake.kuitikia wito
wa kuwaongoza kondoo ni moja ya hatua zinazodhihirisha kukua kwa mtu aliyeokoka.katika
hali ya asili Mzazi asingependa kumuona mtoto wake anabaki mchanga tu siku zote
na hakui, Furaha ya mzazi hutimia anapoona moja ya watoto wake akiwaongoza
wadogo zake na kusaidia kufanya majukumu ya mzazi katika hali kama hiyo Mungu
hufurahi anapoona mtu aliyeokoka anakua na kuifikia hatua ya kuwaongoza wengine
Lakini ni muhimu kuufahamu mapema kuwa wale ambao tumekubali kuwaongoza huwa
wanaiga sana Tabia zetu hivyo ni muhimu kujifunza somo hili “kuigwa kwa
kiongozi wa kanisa” tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu;-
Jinsi
kondoo wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa.
Wajibu
wa kiongozi wa kanisa kuwa kielelezo
Kiongozi
wa kanisa ni mwakilishi wa Mchungaji
Jinsi kondoo
wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa.
Watoto
wa kike huwaangalia kwa makini mama zao wanapopika chakula katika hali ambayo
wakati mwingine ni vigumu hata mama kujua kinachoendelea na hatimaye utaona nao
wanatafuta vyombo vya kitoto vinavyofanana na kuanza kuwaiga jinsi ya kupika
kumbe watoto ndivyo walivyo ni kwa msingi huu watoto wakiroho huwaiga wale
wanaowaongoza au waliowatangulia katika wokovu kwa jambo lolote lile liwe jema
au baya. Kuna usemi mmoja unaosema “ukitaka kufahamu tabia ya kiongozi
waangalie wale anaowaongoza” Kiongozi kamwe hapaswi kuwaambia watu fuateni
yale ninayosema na si yale ninayotenda kiongozi huyo hajui analolisema, Kuigwa
kwa kiongozi katika Matendo yao ni kanuni iliyoandikwa mioyoni mwa watu na haiwezi kuepukika Biblia ina mifano mingi ya jinsi watu
wanaooongozwa wanavyowaiga wale waliowaongoza angalia mifano hiyo katika 1Falme 22;51-53, 2Nyakati 22;1-4, Yeremia
9;14, Amosi 2;4, 2 Nyakati 17;3-4,26;3-4, 2Tomotheo 1;5.Biblia inaonyesha
kuwa Simeon Petro aliandaliwa mapema kuwa kiongozi wa kanisa Luka 22;31-32,Matendo 1;15,2;14. Simeon
Petro wakati mmoja kama kiongozi wa kanisa aliamua kuacha majukumu yake ya
kiutumishi na kuamua kwenda kuvua samaki wanafunzi wengine walipomuona waliamua
kujiunga na kiongozi wao kuvua samaki Yohana
21;7.Yesu alipowakuta wao Baharini Petro alifahamu kuwa ameonyesha mfano
mbaya hususani kwa wanafunzi wale wengine akajuta na kujitupa baharini Yohana 21;7 sisi na si kama Viongozi
tunawajibu mkubwa wa kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kufahamu kuwa kuishi
maisha ambayo si kielelezo ni sawa na kuisaidia kazi ya shetani, Viongozi
wataigwa na wale wanaokuja nyuma yao kwa kila kitu kama tunawahi ibada, ni
waombaji, tuna bidii,tunatii neno la Mungu na kulitetemekea tunatii wachungaji
n.k watu wanaoongozwa humtazama kiongozi wao kwa kila jambo hata kama ni baya
kama uvivu, ulegevu, uzembe n.k kwa msingi huo ni muhimu kuwa makini tunapokuwa
tumeingia katika ngazio ya maongozi.
Petro alimwangaluia sana kiongozi wake
Yesu jinsi alivyokuwa anafanya maombi ya kufufuka wafu naye akaiga vilevile
kabla ya kufanya maombi ya kufufuka wafu
kumbuka kuwa Yesu aliwatoa watu nje
na Petro akaiga vilevile Linganisha Marko
5;39-42 na Matendo 9;39-41 sisi
nasi tukiwa kama Viongozi wa kanisa tunaangaliwa katika kila jambo. Waebrania 13;7 Nyakati za kanisa la
kwanza waliwaiga Viongozi wao katika kila jambo walichofanya Viongozi ni
kuwasihi wauchunguze mwisho wa mwenendo wa Viongozi wao.
Wajibu wa kiongozi wa
kanisa kuwa kielelezo
Mpaka hapo tumeona jinsi kiongozi wa
kanisa anavyoweza kujenga ufalme wa Mungu au kuubomoa,kiongozi wa kanisa
akafanya vema atawafanya wanaomuongoza nao kufanya vema ni kwa sababu hii ndio
maana Mungu huwaheshimu sana Viongozi wa kanisa na ndio maana anataka Viongozi
wa kanisa wawe vielelezo Neno la Mungu linatoa wito na wajibu kwa Viongozi wa
kanisa kuwa vielelezo 1Timotheo4;12,16
Tito 2;7;1Petro 5;2-4.Viongozi
Nyakati za kanisa la kwanza walijitahidi sana kuwa vielelezo na ndio maana
ufalme wa Mungu ulijengeka kwa kasi sana na kwa namna ya kipekee katika wakati
wao 1Koritho 11;1, 4;16,Wafilipi
3;17,4;9,1Thesalonike 2;10,2Thesalonike 3;7,9, Mungu hana upendeleo Neema
ya Mungu iko kwa kila kiongozi
kutusaidia kuwa kielelezo kwa ajili ya kujenga ufalme wake Bwana ampe
neema kila mmoja wetu kuwa kielelezo katika jina la Yesu Kristo.
Kiongozi wa kanisa ni
mwakilishi wa Mchungaji.
Ni
muhimu kuufahamu kuwa mtu anapoteuliwa kuwa kiongozi katika sehemu yoyote iwe
kanisa au cell au makanisa ya nyumbani au vijana au kina mama au maombi au
kikundi chochote yeye ni ana kuwa ni
mwakilishi wa Mchungaji katika eneo husika ina maana ya kuwa kiongozi huyo
huongoza eneo lake hilo kwa niaba ya Mchungaji hivyo unafanya kile ambacho
Mchungaji angekifanya katika sehemu hiyo
Luka 10;1, hivyo anayemsikiliza
kiongozi anamsikiliza Mchungaji anayekataa hamkatai Mchungaji tu bali na yeye
aliyewatuma Luka 10;16,Kwa msingi
huo ingawa Viongozi hawa hawaitwi wachungaji Lakini ni wachungaji wa maeneo yao
waliyopewa kuyasimamia hivyo kila unapofanya jambo jiulize kuwa hiki
ninachikifanya je Mchungaji angekifanya? Kwa msingi huo wewe kama kiongozi ni
muhimu kukumbuka kuwa uko karibu na watu kusaidia huduma ya kichungaji na hivyo
maisha yako kama kielelezo yatasaidia kujenga au kubomoa ufalme wa Mungu na
kanisa lake kwa nia moja kabisa tukatae kutumiwa na ibilisi kuliharibu kanisa
la Mungu na chini ya neema ya Mungu tuseme kama Paulo mtume “MNIFUATE MIMI, KAMA
MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO”
Shule
maalumu ya uongozi somo la Nne
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
Somo; Sifa za kiongozi wa
kanisa
Somo
letu la nne katika Mfululizo wa Masomo ya shule hii maalumu ya Viongozi ni somo
sifa za kiongozi wa kanisa tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele
vikuu viwili vifuatavyo;-
Sifa
za kiongozi wa kanisa
Kiwango
cha kuanzia tunapoitwa kuwa Viongozi wa kanisa.
Sifa za kiongozi wa
kanisa
Neno la Mungu linaeleza waziwazi sifa za
kuwa kiongozi wa kanisa na tutakapokuwa tunaichambua sifa moja baada ya
nyingine itakuwa ni rahisi kwa kila mmoja wetu kujipima na kuangalia pale
palipopungua kisha kumuomba Mungu neema ya kuzifikia sifa hizi za maongozi
katika kanisa kama apendavyo Mungu.
- Awe Mwanafunzi wa Yesu;-
Neno la Mungu linaelekeza kuwa
Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu ambaye ameokoka hivi karibuni 1Timotheo 3; 6 Baada ya mtu kuokolewa
anapaswa Kwanza kujifunza Neno la Mungu na kulitendea kazi hata kufikia ngazi
ya kuwa Mwanafunzi wa Yesu. Mwanafunzi wa Yesu ni mtu aliyeokoka ambaye
analitendea kazi Neno la Mungu bila ubishi au kulijadili na kukaa katika neno
Yohana 8;31 wao wanakuwa watii si kwa neno tu Lakini wanaelewa pia faida za
utii kwa Viongozi wake utii uhuu unafananishwa na ule wa kijeshi Wafilipi 2;5-8 askari hujifunza kutii
amri za Viongozi wao hata kama amri hiyo itamsababishia kifo Mwanafunzi wa Yesu
hali kadhalika ni askari wa Yesu 2Timotheo 2;3,Filemoni
1;2 , hivyo Mwanafunzi wa Yesu ni mtu aliyeokoka ambaye analitii neno la
Mungu na Viongozi wake wa kiroho kama askari kwani watumishi wa Mungu ni
wajumbe wa Bwana wa majeshi Malaki
2;7,Filemoni1;21 Yesu Kristo aliwatuma wale thenashara kwenda kwa niaba
yake baada ya kufikia kiwango cha utii
kama wa askari wa kijeshi Mathayo 11;1
Makanisa mengi hayafanikiwi kwa sababu watu hawajafunzwa kuwa kama askari hivyo
kunakila aina za uasi na majadiliano kuhusu maagizo yanayotoka kwa Viongozi
wao, Mtu aliyeokoka hivi karibuni ataona ni ngumu kuyatii maagizo ya kiongozi
wake kama askari hivyo hafai kuwa kiongozi akiambiwakama Anania “Simama Enenda”
atafanya hivyo mara moja Matendo 16;1-3.
- Awe mume wa mke mmoja au Mke wa mume mmoja;-
1Timotheo
3; 2, 12 Mwanamume
yeyote ambaye ana mke zaidi ya mmoja au mwanamke aliyeolewa na mume mwingine
wakati mumewa kwanza bado yuko hai watu wa jinsi hiyo huwa hawapewi uongozi
kibiblia Kristo ni mmoja na ni kichwa cha kanisa mwili ni mmoja vivyo hivyo mume
mmoja kichwa na mke mmoja mwili.
- Awe anayaamini mafundisho yote.
2Koritho 4;15 Kiongozi wa kanisa
anapaswa kuwa ni mtu anayeshika na kuyaamini mafundisho ya imani yetu kama
vilevile anavyofundishwa Tito 1;9, 2Wathesalonike 2;15 ni muhimu kwa kiongozi
wa kanisa kuwa anayeamini mafundisho yoote ya kanisa lake na sio sehemu tu
fulanifulani Mafundisho hayo ni pamoja na Wokovu, ujazo wa Roho Mtakatifu,
Ubatizo wa maji mengi, mafundisho ya toba na Malipizi, unyenyekevu na utii, kujitenga
na dunia, uponyaji na miujiza kiongozi anapokuwa anapinga baadhi ya mafundisho
kama hayo ya muhimu basi huyu ni
kiongozi wa watu waliomkamata Yesu kama Yuda Matendo 1;15-17,.
- Awe anaisimamia Nyumba yake vema.
Kama kiongozi wa kanisa ni Mwanamume
basi kama kichwa anapaswa kuwa na msimamo mkali na thabiti utakaomfanya mkewe
na watoto kufuata maagizo yake kama mwili unavyotekeleza maagizo yote ya kichwa
kutoka katika ubongo aidha lazima awatiishe watoto wake katika ustahivu woote
yaani watoto wake wawe katika hali ya kumtii na kumuheshimu mtu asiyejua
kuisimamia nyumba yake mwenyewe moja je atawezaje kulisimamia kanisa lenye
nyumba nyingi? 1Timotheo 3;4-5,12.Kama watoto wa kiongozi ni wakaidi jeuri na
wasiotaka kutii ni lazima ithibitike kuwa amechukua hatua kali na thabiti
katika kuwazuia kufanya wanayoyafanya na sio kuzungumzia nao kwa kuwadekeza
1Samuel 2;12, 22-25, 3;12-14. Mtu ambaye atawaona watoto wake hawafuati njia za
Bwana kisha akawachekea tu bila kuchukua hatua kadhaa huyo hafai kuwa kiongozi
wa kanisa
- Awe analifahamu neno la Mungu na kujua kulifundisha kwa uhakika akionyesha tabia na Matendo yanayolingana na neno analolifuindisha.
Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa na
bidii katika kulisoma neno la Mungu kulisikia Kupitia ibada na njia za kaseti,
tv, Vitabu n.k na kujifunza ili alifahamu kwa uthabiti na kumudu kulifundisha
1Timotheo 1;7;3, 2, 4;13 Tabia na Matendo yanayoendana na neno analolifuindisha
hayana budi kuwa yenye kuonekana katika maisha yake Kutoka 18;21, 1Timotheo
3;1-12, Tito 1;5-8
- Awe na moyo wa msamaria.
Kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mtu
aliye tayari kuchukua mizigo ya waaminio na awe tayari kufanya hivyo kwa wakati
unao faa na usio faa Luka 10; 30-35, 2Timotheo 4;2.
- Awe Mtu asiye na upendeleo.
Mtu awaye yote anayekuwa kiongozi wa
kanisa hapaswi kuwa mtu wa upendeleo kwa namna yoyote ile wako Viongozi ambao
hufanya upendeleo kwa watu wa kabila lake tu au kwa wasomi na matajiri kwa
ajili ya mafungu au kuipokea uso wa mwanadamu mtu wa namna hii hafai kuwa
kiongozi wa kanisa Kumbukumbu 1;17, Yakobo 2;1-9.
- Awe mtu wa kweli na mwenye kuchukia mapato ya udhalimu
Shetani ni baba wa uongo, kiongozi
wa kanisa anamwakilisha Yesu ambaye ni kweli hivyo anapaswa kuwa mkweli wakati
woote Mtu mwongo hafai kuwa kiongozi wa kanisa, aidha kiongozi wa kanisa
anapaswa kuwa mtu anayechukia mapato ya udhalimu Kutoka 18;21. Aidha anapaswa
kuwa mbali na mizaha na tabia zozote za kuchukiza Mithali 26;18-19; 19;29.
- Awe mtu ambaye uasherati au uzinzi haitajwi kwake
Uasherati au zinaa ni mwiko kutajwa
kwa mtu yeyote anayedai kuwa ameokoka na ni zaidi sana kwa kiongozi wa kanisa
Waefeso 5;3 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa Mithali 6;32 Kumbukumbu
1;13.
- Awe mtu aliyejaa imani, anayeishi maisha matakatifu na aliyejaa Roho Mtakatifu na Hekima Matendo 6;3-6
Aidha kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mtu
mwenye Hekima anayeishi maisha matakatifu na aliyevikwa uwezo utokao juu yaani
Roho Mtakatifu Luka 24;49 Anapaswa kuwa mstari wa mbele katika imani akiamini
kwamba kwa Mungu yote yawezekana.
Kiwango cha kuanzia
tunapoitwa kuwa Viongozi wa kanisa.
Baada ya kujifunza sifa hizi ni rahisi kwa
kila mtu mmoja mmoja kujihisi kuwa huenda Hastahili na ana upungufu katika eneo
Fulani. Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hatuiti katika uongozi tukiwa wakamilifu
mia kwa mia Mungu hakuwaita kina Petro wakiwa kama watu maalumu wala Yakobo na
Yohana hawakuwa wakamilifu kulikuwa na mapungufu kadhaa wa kadhaa katika maisha
yao Hivyo si ajabu kwetu kujikuta tukiwa na mapungufu Fulani na ndio maana
Mungu hutufundisha hatua kwa hatua hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha
utimilifu wa Kristo Waefeso 4;11-13 jambo la msingi kwetu ni kumuomba Mungu
atujazilize katika kile ambacho kimepungua katika maisha yetu na kufanya sehemu
yetu ya kuipokea kwa imani na kulifanyia kazi neno Yakobo 1;5-7.
Shule
maalumu ya uongozi somo la Tano
Mchungaji
Innocent Kamote.
******************************************************
Somo ;
Wito wa kumtumikia Mungu
Somo tunalojifunza sasa katika Mfululizo
wa Masomo maalumu ya shule ya uongozi ni Wito wa kumtumikia Mungu hili ni moja
ya Masomo muhimu sana na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitano
vifuatavyo;-
Mafundisho
ya msingi kuhusu wito wa kumtumikia Mungu
Aina
tatu za wito wa kumtumikia Mungu
Njia
Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
Aina
ya watu wanaoitwa na Mungu
Neema
ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu
Mafundisho ya msingi
kuhusui wito wa kumtumikia Mungu
Wako
watu wengine katika kanisa la Mungu ambao kwa kukosa Ufahamu husema hawawezi
kukubali kumtumikia Mungu au kukubali nafasi yoyote ya uongozi katika kanisa
kwa madai kuwa eti mpaka wasikie Sauti halisi ya Mungu ikiwaita katika utumishi
huo, huku ni kukosa Hekima na sio sahihi Wito wa kumtumikia Mungu sio lazima
uambatane na kuisikia sauti halisi ya Mungu Elisha hakusikia sauti ya Mungu
alipoitwa ni Eliya alipita karibu naye na kumtupia vazi 1Falme 19;19-21 pamoja
na hayo Mungu alikuwa pamoja naye na alimtumia kwa upako maradufu kuliko Eliya,
Yoshua hakusikia pia sauti ya Mungu bali
alitwaliwa na Musa na kuwekewa mikono Hesabu 27;22-23 pamoja na hayo Yoshua
alikuwa mtumishi wa Mungu wa kipekee, upande mwingine pia wako watu ambao
hujipachika majina makubwa kama Mwinjilisti, Mwalimu, Mchungaji n.k bila ya
kuwa na wito maalumu wa kuwafanya wawe na nafasi hizo watu wa jinsi hii hufanya
makosa na wanapojaribu kufanya kazi hizo kamwe hawawezi kupata matokeo mazuri
mfano wa kibiblia ni kwa AHIMAASI mwana wa Sadoki na mkushi mmoja Ahimaasi alikuwa na moto wa kijipachika cheo
cha kuwa mchukuwa habari na kufikiria kuwa ni swala la kuwa na ubingwa wa kupiga
mbio na ni kweli alikuwa wa kwanza kufika kwa mfalme Lakini alipofika na kuulizwa habari
alibabaika tu na hakuwa na ujumbe maalumu kama ilivyokuwa kwa mkushi aliyekuwa
na wito maalumu wa mchukua habari 2Samuel 18;19-33. Awaye yote anayetaka
kumtumikia Mungu ni muhimu kuwa na wito.
Aina tatu za wito wa
kumtumikia Mungu
Ziko
aina kuu tatu za wito kuelekea katika kumtumikia Mungu
1.
Wito wa jumla katika wokovu- huu ni wito ambao mtu huitwa kutoka dhambini na
kusamehewa dhambi ili apate kumuabudu Mungu
na ili kuurithi uzima wa milele hata hivyo wito huu huambatana na wito
wa jumla wa kumtumikia Mungu yaani Mungu anapokuwa amekuokoa anataka pia
umtumikie
2.
Wito wa jumla wa kumtumikia Mungu- Mtu hawezi kuingia katika wito wa jumla wa
kumtumikia Mungu kabla hajaokoka, Lakini punde mtu huyo anapokuwa ameokolewa
anakuwa ameitwa katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu na wito wa kuyaishi
maisha matakatifu Waefeso 4; 1,1Petro 1; 15-16 kila mtu aliyeokoka amepewa wito
wa kuenenda ulimwenguni mwote na kuihubiri injili kwa kila kiumbe Mathayo
28;19-20 Marko 16;15 wito huu ni kwa jinsia zote, Nyakati za kanisa la kwanza
watu woote waliitikia wito huu pale walipotawa nyika na kwenda huko na huko
wakiwaacha mitume pale Yerusalem Matendo 8;1,4. Hivyo kila mtu aliyeokoka bila
hata ya kungojea sauti ameitwa katika wito huu wa kumtumuikia Mungu
3.Wito
maalumu wa kumtumikia Mungu- wito huu hutolewa na Mungu kwa Mtu maalumu ili kufanya utumishi Fulani wa kimaongozi
katika kanisa wakati mwingine wito huu
utaambatana na karama maalumu zitakazomwezesha mtu huyo kulitimiza Jukumu
alilopewa kwa ufanisi .Yusufu alipewa wito maalumu wa kuhifadhi roho za watu na
maisha yao wasife kwa njaa na alipewa karama maalumu za kutafasiri ndoto Mwanzo
45;5-8 wito huu ulioambatana na karama hizo maalumu ulimuwezesha kuwa waziri mkuu katika inchi ya
Misri, Esta 4;15-16 alikuwa na wito maalumu wa kuliokoa taifa la kiyahudi
lisiangamizwe na aliwezeshwa kuwa tayari kuangamia au kukutana na magumu ya aina yoyote ile
hivyo ili mtu awe Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu lazima wito
wake uambatane na neema maalumu itakayomwezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi wa
kipekee, aidha wito maalumu pia huambatana na mtu kuwa mwaminifu katika
kutekeleza wito wa jumla wa utumishi kabla ya kuingia katika wito maalumu wa
kumtumikia Mungu Matendo 13;1-3 Barnaba na Sauli walikuwa waaminifu sana katika
wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hawajaitwa katika wito maalumu wa
kumtumikia Mungu baada ya kupewa wito maalumu huduma zao zilibadilika kabisa.
Njia Tofauti za
kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
- Kujipachika mwenyewe uongozi
Hii ni sawa na ule mfano wa Ahimaasi
mwana wa Sadoki 2Samuel 18;19-33 na tuliona kuwa matokeo yake haya kuwa mazuri,
Uzia alijipachika kufanya ukuhani na matokeo yake alipatwa na ukoma na kufa
2Nyakati 26;16-23 kora na wenzake hawakuwa tayari kuwa chini yza Musa yeye na
wenzake wakataka na ukuhani matokeo yake walipoteza hata nafasi ile waliyokuwa
nayo wakafa kifomcha aibu Hesabu 16;1-35 ni hatari kubwa mtu kijipachika
uongozi katika kanisa.
- Kuchaguliwa na wanadamu bila kufuata uongozi wa Roho mtakatifu.
Kiongozi wa kiroho kamwe hachaguliwi
kwa kupigiwa kura au baada ya kufanya kampeni nyingi kama za kisiasa,tunaweza
tukampigia kura mwanadamu Fulani na ikawa Bwana hakumchagua huyo Baada ya
Mathiya kupigiwa kura na kushindwa kwa kura katika Matendo 1;23-26 hatuoni jina lake likitajwa tena katika Biblia najua
kuwa Vitabu vya kihistoria vinaeleza kazi alizozifanya Lakini hatuoni tendo la upigaji kura
likirudiwa tena katika agano jipya Mungu ndiye anayechagua Viongozi katika
1samuel 16;6-7 Samuel alimchagua Eliabu Lakini Bwana hakuwa amemchagua huyo, Ni
marufuku kuchagua kiongozi wa kanisa kwa kumpigia kura swala hili limeleta
migogoro mingi katika makanisa Kiongozi wa juu wa kiroho ndiye anayechagua Viongozi walio chini yake kwa kuongozwa na Roho wa Mungu Luka 6;12-16
Matendo 15;40-41;14;23;Toto 1;4-5 au Mungu kusema Kupitia Roho Mtakatifu
Matendo 13;1-3.
- Kuchaguliwa na Mungu Mwenyewe.
Mungu anaweza kuchagua mwenyewe
Viongozi mbalimbali wa kanisa Yeremia 1;15 Hata hivyo Mungu anapochagua
mwenyewe huduma ya mtu huyo itakuwa dhahiri katika kanisa na kutakuwa na
udhihirisho wa wazi wazi unaothibitisha
kuwa huduma ya mtu huyo imetoka kwa Mungu.
- Kuchaguliwa na Mungu Kupitia watumishi wake.
Yoshua alichaguliwa na Mungu Kupitia
mtumishi wake Musa Hesabu 27;16-18.elisha alichaguliwa na Mungu Kupitia Eliya
1Falme 19;15-16 Paulo mtume alimchagua Silla
kwa uongozi wa Mungu Matendo 15;40 halikadhalika Viongozi wengi wa
Nyakati za kanisa la kwanza walichaguliwa na watumishi wa Mungu kwa uongozi wa
Mungu Matendo 14;23,Tito 1;4-5 kwa msingi huu basi Mchungaji akimchagua mtu
kuwa kiongozi wa kanisa la nyumbani sehemu au zone au kuongoza idara nyingine
yoyote hufanya hivyo kwa uongozi wa Mungu na hivyo mtu huyo aliyechaguliwa
hakujitwalia mwenyewe heshima hiyo Waebrania 5;4 na anakuwa ameitwa na Mungu.
Aina ya watu wanaoitwa
na Mungu
Mungu katika Hekima yake huwaita watu
wengi wasio na Hekima ya mwilini au wasio na nguvu wasio na cheo au
wanaoonekana kuwa wapumbavu na dhaifu wanyonge na wanaodharauliwa ili adhama na
sifa kuu ya uwezo wa iwe ya Mungu mwenyewe na sio ya mtu yule dhaifu 1Koritho
1;26-29, 2Koritho 4;7 hivyo hatupaswi kujiona kuwa hatufai Kuchaguliwa . Musa
alikuwa na kigugumizi, Yeremia alikuwa mtoto n.k sisi nasi tunaweza kujiona
kuwa tuna mapungufu Fulani wakati Mungu anapotuita kwenye utumishi hayo
yasikukatishe tamaa kwani yeye ndiye atakaye tuwezesha si kwa nguvu wala kwa
uwezo bali kwa Roho wangu asema Bwana wa majeshi Zekaria 4;6 Warumi 9;16.
Neema ya kuwekewa
mikono katika Mpango wa Mungu.
Tunapochaguliwa kuwa Viongozi wa kanisa na
kuwekewa mikono na yule aliyetuchagua kuwa Viongozi kwa uongozi wa Mungu Sehemu
ya heshima yake na uwezo wake aliopewa hutushukia Hesabu 27;18-23. Yoshua baada
ya kuwekewa mikono na Musa alibadilishwa
kabisa na watu wakamuheshimu Kumbukumbu 34;9.Kuwekewa mikono namna hiyo
huchochea karama zilizofichika ndani yetu na kizifanya zijitokeze 2timotheo 1;6
Kwa msingi huo Mchungaji anapotuwekea mikono ili tuwe Viongozi wa Makanisa na
idara na sehemu nyinginezo sehemu ya uwezo aliopewa huja kwetu na kutusaidia
kikamilifu
Shule
maalumu ya uongozi somo la sita
Mchungaji
Innocent Kamote.
******************************************************
Somo; Jinsi ya kuliongoza kanisa
Tunaendelea
kujifunza Mfululizo huu wa Masomo maalumu yahusuyo uongozi na sasa tunajifunza
somo hili Jinsi ya kuliongoza kanisa la Mungu tutajifunza somo hili pia kwa
kuzingatia vipengele viwili
Hatari
ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa
Jinsi
ya kuliongoza kanisa.
Hatari ya kuwa na
Viongozi vipofu katika kanisa
Ni hatari kubwa kama tutakuwa na Viongozi
vipofu katika kanisa. kipofu alimuongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni
wote wawili Luka 6;39 kwa kukosa akili au Ufahamu wa jinsi ya kuliongoza kanisa
sisi nasi tunaweza Kuhesabiwa miongoni mwa vipofu Mathayo 15;14-16 ilitupate
Ufahamu wa kutosha kuhusu kuliongoza kanisa tutachukua muda mwingi katika somo
hili kujifunza mambo kadhaa wakadhaa yahusuyo jinsi ya kuliongoza kanisa.
Jinsi ya kuliongoza
Kanisa.
Yako mambo kadhaa ambayo ni muhimu
kuyaangalia na kuyazingatia kwa makini ili tupate mafanikio yanayokusudiwa
katika kuliongoza kanisa
- Kujiamini.
Mungu anapokuwa ametuchagua
kuliongoza kanisa tunaweza kujikuta kuwa tuna umri mdogo kuliko wale
tunaowaongoza, hii sio ajabu Musa alikuwa mdogo kuliko kaka yake Haruni Lakini
ni Mungu aliyemchagua Musa aliye mdogo kumuongoza kaka yake Kutoka 7;7 sio hilo
tu Mungu aliwachagua Viongozi waliokuwa na umri mdogo mno na Biblia inaonyesha kuwa wengi kati ya hao
waliongoza vizuri na kwa mafanikio makubwa
Mfano ni Yoashi aliyeongoza akiwa na miaka saba 2Nyakati 24;1-2 Yosia
alinza kuwa kiongozi akiwa na umri wa miaka nane 2 Nyakati 34;1-2 Uzia alikuwa
na umri wa miaka 16 2Nyakati 26;3-4 Yothamu na Hezekia woote walikuwa na umri
wa miaka 25, 2Nyakati 27;1-2,29;1-2. Timotheo naye alikuwa kijana mdogo tu kama
Yeremia alipoanza kuongoza 1Timotheo 4;11-12,Yeremia 1;4-7 tunaweza kuwa sio tu
na umri mdogo Lakini pia Elimu ndogo kuliko wale tunaowaongoza hii pia sio
ajabu Viongozi wakubwa wa kanisa, Petro na Yohana walikuwa ni watu ambao walikuwa hawana Elimu
wala maarifa Matendo 4;13 lakini
waliifanya kazi ya Mungu kwa ujasiri na kuliongoza kanisa. Hatupaswi kamwe
kujidharau wala kubabaika kutokana na
vigezo hivyo vya kibinadamu tunapaswa Kujiamini na Mungu atawatiisha chini yako
wazee na wasomi nao watakusikiliza
kumbuka kuwa si sisi tuliojichagua wenyewe na kuwa ni Mungu ndiye
aliyetuchagua hivyo yu aweza kutupa uwezo wa kuongoza na kulisimamia kanisa
lake Yohana 15;16,Zekaria 4;6;Wafilipi 4;13 kwa sababu hiyo yeye aliye dhaifu
na aseme mimi ni Hodari maana uhodari wetu uko katika Bwana aliye tuwezesha maana amesema atakuwa pamoja
nasikatika utumishi wetu woote Yoel 3;10, 1Nyakati 28;20, Mathayo 28;19-20.
- Kuwa na utii uliotimia kwa Viongozi wetu wa juu.
Uasi wa namna yoyote kwa kiongozi wetu wa juu unamfanya Roho Mtakatifu
atuache, wakati wowote ni muhimu kwa Viongozi wa kanisa kuhakikisha kuwa
wanawatii Viongozi wao wa juu na wajuu wanawatii wale wa juu, utii huu ni kama
ule utii wa jeshini ni utii usio na
ubishi wala majadiliano hata kama moyoni
unadhani kuwa agizo hilo lina dosari, mradi sio agizo la kufanya dhambi ni muhimu kulitii kwanza tukijiona kuwa tuna kitu chochote cha ziada
kuliko kiongozi wetu wa juu na kuacha
kumtii basi Roho Mtakatifu anatuacha Barnaba alipoacha kumtii kiongozi wake
Paulo na kushindana naye kuanzia hapo Roho wa Mungu aliacha kutupa historia
yake akiwa na Marko Bali Roho anatupa ripoti ya Paulo na wale aliofuatana nao
katika utumishi yaani Silla na Timotheo Matendo 15;36-41,16;1-3 kama Viongozi
wa kanisa tunataka kuona Roho wa Mungu akiwa pamoja nasi na kututumia katika
viwango vya kupita kawaida basi siri ni utii uliotimia 2Koritho 10;4-6.na
tatizo la Viongozi wengi katika makanisa ya kiroho shida yao kuu ni kukosa utii
na hasa utii uliotimia, Viongozi wengi watataka kufanya kazi kwa kusukumwa
sukumwa tu na kwa msingi huo utendaji wa Mungu na karama za Roho Mtakatifu
hufifia Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mtii na kuzidi katika Yesu.
- Kuwaongoza watu kwa kutumia maombi
Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa mtu muombaji siku zote akiwaombea wale
anaowaongoza kwa kuwataja majina na
kuwaombea juu ya udhaifu walio nao, tukiwa tunapenda kufoka tu bila maombi ya
kutosha pamoja na kufoka kwetu sana
tutaona mambo hayatendi kama inavyokusudiwa Yeremia 31;9 kuomba ni kumhudumia
bwana inatupasa kumhudumia bwana zaidi kabla ya kuwahudumia watu tunao waongoza
ili tuone mafanikio maombi ni kama mafuta yanayolainisha msuguano au ugumu wa
mioyo ya watu tunaowaongoza bila maombi ya kutosha kanisa letu haliwezi kukua
kiidadi na pia wale tunaowaongoza hawawezi kukua kiroho na watadumaa kadiri mtu anavyopewa majukumu makubwa ndivyo
anavyopaswa kuomba zaidi maombi husaidia kunyonya kiburi cha kibinadamu
tukipenda kuwahudumia watu bila maombi ya kutosha ni rahisi kujidhuru kiroho sisi wenyewe
- Kuacha kuongoza pale tunapokuwa vipofu.
Katika sheria za usalama
barabarani dereva anashauriwa kusimamia
ikiwa haoni vizuri mbele kutokana na ukungu au moshi n.k vilevile dereva
anashauriwa kuegesha gari pembeni na
kulala ikiwa anaona usingizi Dereva
akipuuzia ushauri huo ni rahisi kupoteza maisha
vivyo hivyo kama Viongozi wa kanisa hatupaswi kumshauri mtu kitu ambacho
hatuna uhakika nacho tukiwashauri watu makosa tutapata adhabu iliyo kubwa
zaidi Yakobo 3;1,Mathayo 18;6-7 lolote
lile tusilokuwa na uhakika nalo ni vema kuulizwa kwa uongozi wa juu zaidi kisha
kutoa majibu yapasayo hivyo ni muhimu
kuacha kufanya jambo lolote tusilolifahamu vema.
- Kuongoza kwa neno la Mungu
Tukiona lolote kwa wale tunaowaongoza lisilofaa inatupasa kutumia neno
la Mungu kulirekebisha kwa upendo na sio
Maneno matupu ya kibinadamu Neno la Mungu lina uwezo mkubwa wa kumbadilisha mtu
wala sio adhabu zetu au Maneno yetu ya kuumiza mwanadamu huwezwa na Mungu tu
Maneno ya kibinadamu husukumia tatizo kuzidi Mithali 6;21-23; 2timotheo
3;16-17,4;2.
- Kutokubali kuvunjika moyo.
Adui Ibilisi humwandama kiongozi wa kanisa na kutumia kila aina ya mbinu
ili kumvunja moyo, iwe ni kwa matatizo ya kikazi, kifamilia au kibiashara,
kusengenywa, kunenewa vibaya kwa kila aina ya Maneno, n.k na wakati mwingine atatuonyesha hali za
kutokufanikiwa kwa njia mbalimbali hata kukuonyesha jinsi kanisa lako
lisivyokua na atakushauri ni afadhali
uache yamekushinda kamwe hatupaswi kusikiliza ujinga huo na
kukubali kuvunjika moyo kwa lolote hata kama tuna watu waili au mmoja katika
kanisa Endelea kuwalisha kwa uaminifu na tudumu katika kazi ya bwana kwa
uaminifu kwani kuna majira ya kupenda na kuvuna Matendo 21;9-14 Zaburi 126;5-6
Muhubiri 3;1-2 marufuku kukata tamaa tusikubali kuvunjika moyo kwa namna
yoyote.
- Kuongoza kwa Hekima.
Ni vigumu kuongoza kanisa la Mungu
huku hatuna Hekima Hekima inatusaidia kujua kuwa tuseme nini, tujibu nini au
tufanye nini na kwa wakati gani Hekima
ya Mungu ndio ufumbuzi wa tatizo hilo na hufumbua kwa amani Hekima humfanya mtu
ajue neno la kuzungumzia wakati Fulani na sio kuropoka tu na kusababisha
matatizo zaidi Mithali 25;11-12 kwa Hekima tunaweza kuwapa watu Elimu ya Mungu
Mithali 16;21 hekima hutupa kujua jinsi ya kuwashughulikia wazee Tofauti na
vijana n.k 1Timotheo 5;1 kwa sababu hii Suleimani alipofanywa kuwa mfalme jambo la kwanza lilikuwa ni kuomba Hekima
sisi na si ni muhimu kumuomba mungu atupe Hekima kila siku katika shughuli zetu za maongozi
2Nyakati 1;7-10,Yakobo 1;5.
- Kufanya kazi ya Mungu kwa bidii.
Hatuwezi kuwa na mafanikio makubwa katika kazi yoyote ya Bwana kama sisi
wenyewe ni watu wavivu au walegevu inahitajika bidii kubwa ili kufanikiwa
Yeremia 48;10 Warumi 12;11 hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa na vipindi vya
mapumziko na kukumbuka kula chakula vizuri ili tusimpe ibilisi nafasi Marko
6;31-33.
- Kumbuka kuwaita moyo wale tunaowaongoza.
Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu wa kuchokonoa mabaya tu ya kondoo
wake na kutaja mapungufu yao tu inatubidi pia kutafuta yale yaliyo meme hata
madogo na kuyainua hayo na kuwaita moyo na kuwapongeza kwa kawaida pongezi
humtia mtu moyo wa kufanya vizuri zaidi na husaidia kuondoa makosa makubwa ya
mtu na kufanya bidii zaidi 2samuel 11;22-25,Kumbukumbu 3;28.
- Kutangulia mbele ya Kondoo
Mchungaji hutangulia mbele ya kondoo wake kuongoza , hii maana yake ni
kuongoza kwa mfano huku ndio kuongoza kunakoleta mafanikio makubwa kiongozi
anayechelewa kufika mahali pa ibada na kuonyesha udhaifu Fulani Fulani huyo sio kiongozi anayewatangulia kondoo
Yohana 10;4 Waamuzi 5;2 Marko 10;22-25 Kumbukumbu 3;28.
- Kuwa na utayari wa kuwapa wengine majukumu
Kiongozi aliye botra hafanyi kazi yeye mwenyewe bali huwa tayari kuwapa
wengine majukumuhususani wale anaowaongoza na wakati mwingine hata wale
wachanga Kutoka 18;13-17.
- Kuheshimu mipaka ya madaraka uliyo nayo.
Mithali 22;28 ni muhimu kutakuwa na kimbelembele kwa mambo yasiyohusiana
na madaraka uliyo nayo fanaya kazi ndani ya mipaka yako mfano kama wewe sio
msomaji wa kanisa usipendelee kuzungumzia lolote kuhusu kanisa acha wenye
mamlaka kuu zaidi wazungumzie.
Shule maalumu ya uongozi somo la saba
Mchungaji
Innocent Kamote.
******************************************************
Somo;
Majukumu ya kiongozi wa kanisa
Kufahamu
majukumu ya kazi za kiongozi katika kanisa ni mojawapo ya Jukumu muhimu kwa
kiongozi wa kanisa, Mara nyingi imetokea Viongozi wengi wa makanisa ya kiroho
hawajui majukumu yao na hii inachangia kwa kiasi Fulani kutokuyafikia malengo. Tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia mambo mawili yafuatayo
Viongozi
wa kanisa ni wachungaji.
Majukumu
ya kichungaji ya kiongozi wa kanisa
Viongozi wa kanisa ni
wachungaji.
Viongozi wa makanisa ya nyumbani au cells na
Viongozi wengine woote na wasaidizi wao woote ni wachungaji wa kondoo wa Mungu,
Hawa ni wachungaji wanaotenda kazi chini ya Mchungaji hata ingawa hawaitwi kwa
jina hili, lakini majukumu yao wanayoyafanya ni ya kichungaji, katika mpango wa
Mungu kila mtu ana husika katika utendaji kama makuhani wa Mungu Ufunuo 1;5-6,
1Petro 2;5,9 kama ikiwa kila mtu aliyeokoka Maandiko yanamuita kuhani ni zaidi
sana mtu anapokuwa kiongozi katika kanisa Viongozi katika kanisa ni wachungaji
wanaotenda kazi chini ya Mchungaji na kumsaidia katika huduma za kichungaji
Majukumu ya kichungaji
ya kiongozi wa kanisa.
Viongozi wa kanisa kama ilivyo kwa
Mchungaji wana wajibika kufanya kazi ya uiunjilisti uchungaji na ualimu katika
eneo lao walilopewa na Mungu leo tutachukua Muda kujifunza majukumu mbalimbali ya kiongozi wa yanayohusiana na uinjilisti na ualimu na
uongozi kwa ujumla wake
- Kuwafahamu Kondoo kwa sura na majina Yohana 10; 2-3.
Ni wajibu wa kiongozi katika kanisa
kuwafahamu kondoo wake kwa majina na sura, kadiri kanisa linavyokua na
kuongezeka lazima kanisa liwe na mfumo unaoruhusu watu kujulikana kama kuwa na
makanisa ya nyumbani ambapo kiongozi anapaswa kuwatambua kwa sura na majina ,watu
hupenda kutambulika na hujisikia salama pale
anapokuwa anatambukiwa Kanisani hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwatambua
watu wake, na kutokana na kuwafahamu kwa majina na sura inakuwa rahisi kuwaombea kwa kuwataja majina
yao Viongozi wanapaswa kuwafahamu wale Viongozi wengine walio chini yao pia tunapaswa kujua mahudhurio yao katika
ibada zote za mafundisho siku ya bwana na kadhalika
- Kuhubiri na kufanya uinjilisti Marko 1;38-39;Matendo 20;27.
Kiongozi yeyote wa kanisa kwa ngazi
yoyote ni lazima awe muhubiri na
anawajibika kuwahamasisha watu walio chini yake kuwa na furaha ya kuona watu
wakiokolewa na kuongezeka katika kanisa
tuhakikishe kuwa tunawahubiri watu na wageni wanaokuja katika kanisa
letu na kuwaaalika katika ibada mbalimbali za kanisa ,aidha kama ni kuiongozi
wa cell au kanisa la nyumbani hakikisha kuwa unalihubiri eneo lote
linalokuzunguka na kuhamasisha watu kuhudhuria ibada zote aidha tunapofahamu kuwa Fulani na Fulani
hawakuhudhuria ibada ni muhimu kuwatembelea na kujua ni kwanini
hakuhudhuria na kutoa msaada unao
hitajika kwa pia kufanya ufuatiliaji kwa
washirika wachanga kiroho na kuwalisha kwa neno na mafundisho,kiongozi anapaswa
kukumbuka kuwa mfano au kielelezo kwa watu aliopewa kuwaongoza.
- Kufundisha au kulilisha kanisa. Matendo 20;28.
Lisha kondoo zangu huu ni wito kwa kila kiongozi wa kanisa kwa msingi
huo ni wajibu wa kiongozi wa kanisa la nyumbani n.k kujiandaa na kujitayarisha
mapema kwa habari ya somo atakalolifundisha
kila siku ya ibada za makanisa ya nyumbani au katika vipindi vya ibada
za idara n.k. Masomo yanayopaswa kufundishwa ni yale yaliyo maalumu kwa ajili
hiyo au yale yanayofundishwa Kanisani ni hatia kuleta mafundisho mageni 2Yohana
1;9-11,Tito 1;9 kufundisha kwetu hakuna budi kuwe na malengo ya kuondoa au
kurekebisha matatizo yaliyopo katika
sehemu zetu za maongozi tabia kama masengenyo, kuchelewa ibada au kutohudhuria
n.k kumbuyjka kuwa inahitaji maombi na maandalizi ya kutosha kabla ya kufundisha somo au siyo kondoo
watajkuwa hawashibi na matokeo yake
hawatavutiwa kuendelea kuja katika
katika kipindi husika.
- Kuwatunza kondoo.
Ni wajibu wa kiongozi kufanya kazi
ya msamaria katika kutunza kondoo wake Luka 10;30-37 ni lazima kuwatafuta
waliopetea na kujua kuwa ni kwanini hawaji katika ibada,lazima tumuombe Mungu
atupe karama na vipawa ili kuwahudumia
watu wake kuomba kwa ajili ya uponyaji kwa ajili ya wote wenye shida za magonjwa
na kuwafungua waliovunjika moyo kwa kuwapa neno la Mungu la kuwaita moyo
Ezekiel 34;1-2,4-6.
- Kuwatembelea washirika na kujua hali zao za kimwili na kiroho.
Yeremia 23;1-2 matendo 15;36.
Kiongozi yeyote wa kanisa anatakiwa kuifahamu kila nyumbay a mshirika
wake na kuwatembelea mara kwa mara na
waqkati mwingine kwa kushtukiza ili ajue hali ya kimwili na kiroho ya washirika,
bila matembezi ya jinsi hii ni rahisi
kumkuta kondoo amejerihiwa iwapo kuna
taarifa ya tabia mbaya ya mshirika awaye yoote
zifanyiwe uchunguzi wa kina na wa haki kisha zitafutwe njia za kumsaidia
kiroho endapo liko juu ya uwezo wako likabidhio kwa Mchungaji kumbuka katika
kuwatembelea washirika pia ni muhimu kuweka kipaumbele kwa wale walio wachanga
,wageni na wenye kuugua au waliopatwa na misiba na matatizo mbalimbali haita
kuwa busara sana kwa mshirika aliyekomaa kiriho kuwa na madai ya kutembelewa na
badala yake wao nao washirikiane na Viongozi katika kuifanya kazi ya
kuwatenbelea washirika na kuwaita moyo.
- Kutoa ushauri kwa kondoo. Mithali 20;18;12;15.
Mengi tunayoletewa na kondoo kutaka
ushauri mara nyingi ni yale yaliyo mepesi kuyatolea ushauri hata hivyo Mengine
huwa magumu na mtu unapoletewa tu ni rahisi kuona moyoni kuwa hili limenizidi
kimo katika mazingira kama hayo hilo
lipeleke kwa kiongozi wako wa juu na katika kanuni za kutoa ushauri ni vizuri
uwe mwepesi wa kusikia kuliko kusema Yakobo 1;19 Roho wa Mungu hudondosha
ushauri kwetu tunapokuwa watu wa kusikia au katika hali hii ya utulivu, na wakati huo huo zingatia kuwa ni Kinyume na
mapenzi ya Mungu kutoa siri za matatizo ya mtu aliyekuomba umpe ushauri Mithali
25;2,9.
- Kumlinda Mchungaji 1 Samuel 26;16
Viongozi katika kanisa ni wawakilishi wa Mchungaji na wana wajibu wa
kumlinda Mchungaji na kuhakikisha kuwa kila roho ya uasi inayoinuka kinyume na Mchungaji
inashughulikiwa ipaswavyo na kuitolea taarifa lazima kiongozi wa kanisa awe na
moyo wa kiuchungaji Isaya 40;11,1Thesalonike 2;7 Bila moyo huu utendaji wetu wa
kazi utaingia dosari.lolote linalopungua katika karama hii ya kumtumikia Mungu
tumuombe Mungu atupe karama hizo za kutuwezesha kuifanya kazi yake aidha sivibaya kuwatumia wale ambao Mungu
amewapa karama hizo kutusaidia katika
kuwahudumia wale tunao waongoza.
Shule maalumu ya uongozi somo la nane.
Mchungaji
Innocent Kamote.
******************************************************
Somo:Umuhimu
wa kuwa na maono
Tunaingia
katika somo muhimu sana katika Mfululizo wa Masomo haya ya shule maalumu ya
uongozi na kama livyo kwa Masomo mengine somo hili umuhimu wa kuwa na maono kwa
Viongozi ni somo la muhimu na tutajifunza somo hli kwa kuzingatia
vipengele vitano vifuatavyo.
Umuhimu
wa kuwa na maono
Maana
ya maono.
Makusudi
ya Kuchaguliwa kuwa kiongozi katika kanisa
Faida
za kuwa wengi katika kanisa
Umuhimu
wa kuwa na maono kivitendo.
Umuhimu wa kuwa na
maono.
Katika Mithali 29;18 maneno pasipo maono
watu huacha kujizuia katika Biblia ya
kiingereza ya KJV (King James Version) yanasomeka “Where there is no vision
,the people Perish” tungesema kwa usahii kwamba pasipo maono watu huangamia au huacha kujizuia kuangamia.Watu
wanapokosa la kufanya kuhusiana na mapenzi ya Mungu hawana budi kuangamia kutokana na
kutokuyafanya mapenzi ya Mungu. Kiongozi wa kanisa akiwa ni mtu asiye na maono
yoyote watu anaowaongoza hawataacha
kujizuia kufanya yasiyo mpendeza mungu na wanaweza tu kuyafanya yanayo mpendeza
mungu kwa kufanya mapenzi yake ikiwa
kiongozi ana maono.
Maana ya maono
Neno
maono linalozungumzwa katika Mithali 29;18 maana yake ni “mawazo ya jinsi ya
kutekeleza mipango na makusudi ya Mungu “kiongozi mwenye maono maana yake nui
mtu aliyejaa mawazo ya mipango mbalimbali inayoweza kufanya makusudi ya Mungu
yakatimilika ni muhuimu kwa kila kiongozi kuwa na maono hayo.
Makusuidi ya
Kuchaguliwa kuwa Kiongozi katika kanisa
Mungu
anamchagua kiongozi katika kanisa kwa makusudi ya kulifanya kanisa liweze kukua
kuzaa matunda na kuongezeka Yohana 15;16 mungu anapendezwa na tawi linalozaa
matunda hivyo ni wajibu wa kiongozi katika idara au kanisa la nyumbani au eneo
lolote la maongozi ya kikanisa kuhakikisha kuwa anayafanya hayo mapenzi ya
Mungu na kuufanya ufalme mzima wa mungu kukua na kuongezeka endapo tunashindwa
kufanya hivyo tawi hilo litakatwa Yohana 15;2
mungu anafurahi wakati woote anapoona kuwa kiongozi katika kanisa
anasababisha kanisa kukua kiroho na kiidadi na kanisa kuwa kubwa hata kufikia
kiasi cha kugawanywa ikiwezekana Viongozi wa jinsi hii ndio wanao mtukuza mungu Yohana 15;8 ni muhimu
kwa kiongozi kuhakikisha kuwa nafanya jitihada mbadala ili mti huo
aliokabidhiwa uzae matunda Luka 13; 6-9 mungu huonyesha furaha kuu kwa mtunzaji
wa shamba la mzabibu ambaye shamba lake linazaa na kuongezeka Yohana 15;16
kiongozi wa jinsi hiii maombi yake huwa
na matokeo makubwa sana na mungu hujibu hujibu maobi ya kiongozi hyo kwa
ufanisi Yohana 15;16 Hivi ndivyo ilivyo ulimwenguni kote leo Viongozi ambao
makanisa yao yanaongezeka na kukua kwa kasi kubwa maombi yao huwa na nguvu
kubwa ya kuleta majibu kutoka kwa Mungu Viongozi Nyakatiza kanisa la kwanza
maombi yao yalikuwa na matokeo makubwa sana kwa sababu tu makanisa yao yalikuwa
kwa kasi sana bwana atupe neema ya kuwa
na maono na mipango ya kanisa kubwa katika Kristo.
Faida za kuwa wengi
katika kanisa
Kiongozi yeyote wa kanisa nanpaswa kuwa na
mawazo ya kukua na kuongezeka kwa kanisa lake usiku na mchana Ndiyo maana
utaweza kuona kuwa Nyakati za kanisa la kwanza
walizingatia wakati woote kuhesabu idadi ya watu katika kanisa ili waone
kama wanaongezeka ? Matendo 2;41,4;4,5;14,6;1,7, 9;31,11; 24,16;5. Kwa ujumla
hesabu yao iliongezeka kila siku huu
ndio mukhtasari wa Nyakati za kanisa la kwanza walivyokuwa wakitenda kila siku
kila kiongozi wa kanisa anao wajibu wa kuhakikisha kuwa anawapandikizia moyo
washirika woote kuwa na mzigo wa kuliona kanisa linaongezeka bila kufikia kiwango cha kuridhika na idai
yeyote ni lazima tulisisitize hili tena na tena
hata lizame katika mioyo yao pia
ni muhimu kuwaelezea watu umuhimu wa kuwa wengi kwamba sio tu kunamfurahisha
Mungu na kumtukuza na kutekeleza agizo
la mungu 1koritho 10;31,Lakini kukua kwa kanisa pia ni kwa faida yetu, Kanisa
linapokuwa kubwa tunaweza kushirikiana na watu wengi katika matukio kama
Misiba,harusi,furaha za kujifungua mtoto
n.k kunakuwa na watu wengi sana na wa namna mbalimbali wa kushirikiana
nasi na kutupa msaada sio hilo tu tuankuwa
na watu wengi wa kutuombea kwani kanisa ni lazima watu wawe wanaombeana wao kwa
wao
Umuhimu wa kuwa na
maono kivitendo.
Ni muhimu kwa kila kiongozi wa kanisa
kujua kuwa ni mapenzi ya Mungu na ni ahadi ya Mungu kutuongeza kiroho na
kiidadi katika makanisa Yetu Mwanzo 28; 3, 35; 11, Kutoka 1;7, Kumbukumbu
12;20, Zaburi115;14, Zekaria 10;7-8 ni muhimu kufahamu kuwa kiongozi wa kanisa
ana nafasi kubwa ya kufanya kanisa lake likuwe na kuongezeka lakini ili kanisa
likue na kuongezeka kiongozi katika ikanisa hana budi kufanya mbao ya msingi
yafuatayo
- Kuhamasisha anao waongoza
Kwa kawaida watu tunaowaongoza huwa
wanangoja tuwambie nini cha kufanya kwa kuwahamasisha ndipo wapambe moto,kwani
tukikaa kimya nao hufanya hivyo ni wajibu wetu kufungua zizi la kondoo na
kuwaacha watoke nje tukilifunga tu nao
wataendelea kukaa humo Yohana 10;4 Mungu hutupa kondoo ili tuwatumie na sio
kuwafurahia kuona wanakaa humo ni muhimu kuwatumia kondoo kuongoza idadi ya
kanisa hivyo kukua na kuongezeka kwa
kanisa ni muhimu kuwa wimbo wa kanisa letu mpaka kieleweke
- Kuhakikisha watu wanawaalika wageni.Zekaria 3;10.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa watu au wageni wanaalikwa kwa wingi katika
kuhudhuria ibada zetu, watu wenye uwezo mkubwa wa kuwaalika wageni sio wale
walio na muda mrefu katika wokovu hii hufanya kazi kwa kiwango kizuri kwa wale
waliookoka hivi karibuni yaani wachanga wao ni rahisi kuwaalika marafiki zake,
wa zamani kabla hawajamkimbia kwa sababu ya wokovu mtu aliyeokoka karibuni
maisha yake hayatofautiani sana na wasiookoka
na hivyo ni rahisi kwao kuwa wenye kupatana kwa urahisi hivyo ni muhmu kuwahamasisha wale wachanga
kufanya kazi ya kuwaalika wengine na
kuacha kupiga kelele hizi kwa wale wa zamani tuwafahamishe kuwa wanapowaleta
wageni watatoa taarifa kwa Viongozi ili wapenyeze ujumbe wa wokovu kwa wageni
hao na kuwaleta kwa Yesu
- Kushuhudia Yohana 4;28-30,39;Marko 16;15. Wale waliookoka zamani tuwahamasishe zaidi katika maswala ya kushuhudia hata kama hawajapitia katika shule maalumu ya uinjilisti tuwafundishe namna wanavyoweza kushuhudia au kuambatana nao katika shughuli ya ushuhudiaji.
- Kuwafuatilia watoto wachanga Waebrania 5;13,1Petro 2;2. Tusi wangojee watu kufikia hatua ya kupitia shukle ya uinjilisti ili wajifunze ufuatiliaji ni lazima tuwafundishe sisi wenyewe na kuwakomaza katika kuifanya kazi nzima ya ufuatiliaji tukafanya hivi kwa upendo tutaweza kuona matokeo mazuri bila haja ya kukemea na kukaripia hasa kama ni watoto wachanga
- Kuhakikisha kuwa wanapata neno la Mungu Mathayo 4;4 Neno la Mungu ni muhimu na lina uzito mkubwa hasa katika ibada za kanisa kuu hivyo tuwasisistize watu kuja ibadani na kulisikiliza neno la mungu wakati mwingine ghata kama ni kwa njia ya kaseti.
- Kufanya maombi kwa ajili ya kukua kwa eneo lako au kanisa lako. Kukua kwa kanisa hakuwezi kutokea bila kuwako kwa maombi ni muhimu kuwa na maombi ya aina mbalimbali kama ya kufunga au kufanya maombi ya mapatano na kuwa na maombi maalumu pia kwa ajili ya ukuaji wa kanisa Zaburi 2;8.
- Hakikisha ya kuwa unawajali kondoo.
Imani hutenda kazi kwa upendo
Wagalatia 5;6 Ni muhimu kutilia mkazo
kwa uzito mno kuhusika na wagonjwa na wenye shida ,misiba wasio na nauli za
kuja ibadani wanaojifungua n.k ng’ombe anayetunzwa vizuri mara nyingi hutoqa
maziwa mengi na mbwa mkali ni tule anayejaliwa na kutunzwa tukipunguza matedno
ya ukarimu na upendo tunashusha chini kiwango cha ukuaji wa kanisa letu na
kutoa mwanya wa kwenda mahali wanakoona kuwa wanajaliwa zaidi tukipungua katika
eneo hili nqa kuwataka watu watende kazi tu tutaona upungufu mkubwa upendo ndio
ufunguo mkubwa wa kukua kwa kanisa
- Washrikishe watu malengo
Eleza juu ya mahudhurio toa ripoti
za aina mbalimbali ikiwemo maswala ya fedha na matumizi waeleze juu ya ongezeko
la kanisa waeleze furaha ya Mungu ya kuona wakiongezeka kama ni kanisa la nyumbani likifika idadi ya
watu 250 ni muhimu luikigawanywa na kuendelea kuwa na matawi mengi zaidi ya
nmakanisa ya nyumbani au cells hii
itakuwa nifuraha kubwa kwa Mungu Ezekiel 19;10;Marko 4;30-32,.
- Panga mipango mwingine ya kuongezeka kwa kanisa lako.
Kiongozi mzuri ni yule mwenye
ubunifu mkubwa hata zaidi ya ule tulio jifunza katika mbinu za kijeshi kiongozi
wa kijeshi anatakiwa kuwa Hodari yaani Mashal huyu ni mtu mwenye uwezo wa kuwa
na mbinu ambazo ni zaidi ya zile alizijifunza
hizi unakutana nazo huku huko katika uwanja wa vita jaribu na usiogope kukosea mtu anayeogopa
kukosea hawezi kuwa kiongozi mzuri Petro alikuwa mwenye kujkosea sana na Yesu
alimfanya kuwa kiongozi wa kanisa ukikosea utarekebishwa na utaendelea Mbele,
Mungu akubariki sana
Shule maalumu ya uongozi somo la Tisa.
Mchungaji
Innocent Kamote.
******************************************************
Somo: Maelekezo
kwa kiongozi wa kanisa la nyumbani
Somo tunalojifunza sasa ni
miongoni mwa Masomo ya mwisho kabisa katika awamu hii ya kwanza ya Masomo
maalum ya shule ya uongozi somo hili ni muhimu endapo kanisa husika litakuwa na
mfumo huu wa makanisa ya nyumbani au cells na tutajifunza somo hili kwa
kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-
Jinsi
ya kufanya ili kondoo watupende, kututii na kutuheshimu.
Jinsi
ya kuongoza ibada ya makanisa ya nyumbani
Umuhimu
wa kutoa ripoti za makanisa ya nyumbani
Tahadhari
kabla ya hatari.
Jinsi ya kufanya ili
kondoo watupende, kututii na kutuheshimu.
Wengi wetu hususani Viongozi tunapenda
kuona watu wanatupenda kututii na kutuheshimu, lakini hatujui ni jinsi gani
tunaweza kuona hayo yakitimia kwa ukamilifu watumishi wengi wa Mungu na
Viongozi wengi wa kanisa wanapenda kuona kondoo walio chini yao wakiwapenda na
wakiwapenda kuwatii na kuwaheshimu lakini siri kubwa ya kupendwa na Kuheshimiwa
kwanza ni kujitoa kivitendo kuwapenda na kuwahudumia kwa upendo wa kweli na sio
wa Maneno tu au ulimi 1Yohana 3;18 uhusiano wa kondoo na kiongozi wao unafanana
na uhusiano wa mke(anyeongozwa) na mumewe (kiongozi)Mume ana wajibu wa kumpenda
mkewe kama nafsi yake mwenyewe ili ategemee Kuheshimiwa na kuipokea utii kutoka kwa mkewe Waefeso 5;24-25,28,33. Vivyo
hivyo siri ya kiongozi kupendwa na wale anaowaongoza na wakamtii na kumuheshimu
ni kuwapenda kondoo walio chini ya uangalizi wake Yohana 11;5,19;26,20;2 21;
7,13;34,15;12. Yesu Kristo aliwapenda kondoo wake kivitendo alishughulika na
matatizo yao na kuonyesha kuwajali na
kuwa karibu nao katika matatizo makubwa
na madogo kwa mfano Petro alipouguliwa na mkwewe kiongozi wake wa kanisa Yesu alihusika
mara moja na tatizo hilo Marko 1;30-31 alihusika pia na matatizo ya kondoo wake
Mariamu na Martha walipokuwa wamefiwa na
ndugu yao Lazaro Yohana 11;1-44 Yesu kama kiongozi na kielelezo aliugua nafsini
mwake na kulia machozi alipowaona kondoo
zake katika matatizo,hii ndio ilikuwa siri kubwa ya kondoo zake kumpenda kumtii
na kumuheshimu,hatuwezi kamwe kuipokea heshima na utii toka kwa kondoo hawa
kama tunawapiga nyundo na kuwasema kuwa wana kiburi tunawalaumu na kuwasema
kuwa ni kiburi au jeuri n.k kumbe tatizo letu tumeshindwa kuwaonyesha kuwa
tunawapenda kwa vitendo unapokwepa kuyafanya hayo usitarajie watu
watakuogopa na kukupenda na kukuheshimu never! Kupendwa na washirika kunahitaji
jitihada na juhudi nyingi kutoka kwa kiongozi 1Petro 1;22,4;8 ni lazima
tuonyeshe bidii na kufanya juhudi kutoka moyoni
kuonyesha kuwa tunawajali na kuhusika nao katika jambo lolote ambalo
linawapata iwe la furaha au la huzuni hata kama kondoo ankwenda au kurudi
kutoka likizo unaweza kupanga namna ya kumpokea au kumsindikiza kwa kuhusika
sisi wenyewe au kutuma wawakilishi
tukafanya hayo na kuzidi lazima kondoo watatupenda kutuheshimu na
kututii na hapo ndipo tutakapoiona kazi yetu na kifurahia sana kinume cha hapo
tutakuwa na kondoo jeuri na wakaidi na watatuletea shida kubwa sana.
Jinsi ya kuongoza
ibada ya makanisa ya nyumbani
Ibada za kanisa la nyumbani inaweza
kufanyika kila jumamosi au siku ifaayo kulingana na mazingira husika na twaweza kifanya kuanzia saa 9 kamili mpaka
saa 11 jioni ibada iaongoza na kiongozi wa kanisa la nyumbani au msaidizi
wake au kiongozi mwingine ufuatao unaweza kuwa utaratibu unaofaa katika
kuliongoza kanisa la nyumbani kiibada
Kipindi
|
Muda
|
dakika
|
Maombi
ya kufungua ibada
|
9;00 - 9;03
|
Dakika
3 tu
|
Kukaribisha
wageni kwa ma
|
9;03 - 9;05
|
Dakika
2 tu
|
Pambio
na kuabudu
|
9;05 - 9;10
|
Dakika
5 tu
|
Shuhuda
|
9;10 - 9;20
|
Dakika
10 tu
|
Neno
la Mungu
|
9;20 - 10;00
|
Dakika
40-45 tu.
|
Maombi
kwa ajili ya kanisa
|
10;00 -10;15
|
Dakika
15 tu
|
Kuombea
wenye uhitaji
|
10;15-10;35
|
Dakika
20 tu
|
Matangazo
kuhusu ibada
|
10;35-10;45
|
Dakika
10 tu
|
Kuombeana
|
10;45 - 10; 55
|
Dakika
10 tu
|
Maombi
ya kufunga
|
10;55 - 11;00
|
Dakika
5 tu
|
Ibada
za makanisa ya nyumbani hazipaswi kuwa ndefu zaidi ya muda uluiokusudiwa acha
watu warudi nyumbani mapema kweupe nuruni na sio usiku gizani
Umuhimu
wa kutoa ripoti za makanisa ya nyumbani
Ni muhimu kwa kiongozi wa kanisa la nyumbani
kutoa ripoti kwa Viongozi husika katika kanisa
kila wiki au kulingana na utaratibu mtakaojiwekea katika kanisa , hili
ni la muhimu kwani litamsaidia mchungaji kuwa na Ufahamu kuhusu kanisa na
kushughulikia matatizo husika ni dhambi kutokutoa ripoti ni sawa na kujenga
ufalme wako mwenyewe Marko 6;30;
Tahadhari kabla ya
hatari
1.
Ni
muhimu kufahamu kuwa unapokuwa kiongozi wa kanisa kwamba shetani atakutafuta
kwa viwango vikubwa ili yamkini akurudishe nyuma hakuna furaha kubwa sana kwa
shetani na ufalme wake kama anapofanikiwa kumrudisha nyuma kiongozi wa kanisa kwake huo ni ushindi mkubwa sana kuliko ule
wa kuangusha mshirika wa kawaida kiongozi akianguka maadui wa injili hufurahia
sana na shetani hufurahi kwani linachangia kuwafanya walio wachanga wengi
kuanguka pamioja na kiongozi wao yaani inachangia sana wachanga kuacha wokovu
hii huwafurahisha maadui wa wokovu wafilisti
2Samuel 1;17-20;12;7-14 siku zote unapoukata mti mkubwa unapoanguka
unaangukia na miti mwingine midogo na kuiua na hili linakuwa ni sababu ya
kuwakosesha watu wa Mungu walio wadogo, Mathayo 18;6-7 Bwana ampe neema kila moja
wetu amabye ni kiongozi wa kanisa kuendelea kuitegemea neema ili tatizo litakalotufanya turudi duniani Mathayo
26;31-35,56,69-75.Mathayo 26;21-22.
2.
Mbinu
nyingine ya shetani kuvunja heshima ya kiongozui ni kuleta mafarakano
mafarakano hayo huweza kuletwa na washirika wetu wakitumiwa na shetani,kila
kiongozi anapaswa kuwa upande wa kiongozi wake au mwenzake wanapokuwa mbele ya
kondoo,maswala ya Viongozi kwa Viongozi shughulikieni wenyewe pembeni 1timotheo
5;17,19,21, 1 Samuel 9;26-27. Viongozi ni muhimu kuchukuana faraghani na
kuambizana mambo yenu usipoheshimu mafuta mungu ni rahisi kukuacha mafuta ni
lazima yaheshimiwe wako watu wanawafanyia watumishi wenzao mambo ya kuwaaibisha
mbele za washirika huko ni kudharau upako na utavuna kudharauliwa hata na wewe
mwenyewe kwa washirika Viongozi lazima washikamane kama askari tukiifanya kazi
ya Mungu kwa pamoja
3.
Ni
muhimu kuiongozi kujilinda na kiburi majivuna humaliza kabisa huduma nzuri ya
kiongozi awayeyote na kutuingiza hukumuni Mithali 11;2,16;18 Yeremia 50;31-32
1Timotheo 3;6 Kiburi ni hali inayoinuka ndani ya mtu na kujiona yeye ni yeye
kama ni kiroho mtu huweza kujifikiri kuwa Yuko juu kuliko watu wote Hapo tayari
kichwa kimekuwa puto na kupasuka ni rahisi,watu wenye kiburi wamejiharibia
huduma au wameharibu huduma za watu wengine Kiburi! Hali ya kujiona Bora kuliko
wengine, kuhukumu wengine kuhitaji kuheshimiwa na kuabudiwa kama miungu wadogo
hii nishida kubwa Mtu akiwa na kiburi Mungu humuacha polepole hii ndio dhambi
iliyomfanya shetani akatupwa toka Mbinguni juu na kushushwa chini kuzimu Bwana
atupe neema kila mmoja wetu kuwa wanyenyekevu katika jina la Yesu amen.
Shule maalumu ya uongozi somo la
Kumi.
Mchungaji Innocent
Kamote.
******************************************************
Somo
;Wajibu wa msaidizi
Somo hili ni somo muhimu katika
Mfululizo wa Masomo maalumu ya uongozi wa kanisa,kukosa Ufahamu katika somo
hili kutalifanya kanisa kuwa bduni na dhaifu na kuwa katika nafasi ya
kushambuliwa na iblilisi na kutekeleza mipango yake iliyo kinyume na mapenzi ya
Mungu ufalme wa Mungu hauwezi kustawi kama ikiwa Viongozi wa kanisa watakosa
maarifa yatokanayo na kujifunza somo hili kwa msingi huhuu itakuwa sio rahisi kwa
kanisa kukua na kuongezeka na kuwa kanisa la maelfu ,malaki au mamilioni ya watu,kuwa na mafanikio makubwa
katika kanisa kutategemeana na jinsi gani Viongozi watalitendea kazi somo hili
Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuipokea maarifa yatokanayo na somo hili
katika jina la Yesu Amen.Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vingele sita
vifuatavyo;-
Umuhimu
wa kuwepo kwa wasaidizi wa kiongozi mkuu
Viongozi
wa kanisa kama wasaidiszi wa kiongozi mkuu
Sifa
za msaidizi
Wajibu
wa msaidizi
Madhara
ya msaidizi anayewasaidia waovu badala ya kumsaidia kiongozi mkuu
Mbinu
kubwa anayoitumia shetani kuharibu huduma ya kiongozi mkuu na jinsi ya
kuikabili.
Umuhimu wa kuwepo kwa
wasaidizi wa kiongozi mkuu
Hapo mwanzoni Mungu alimuumba Adamu
Mwanamume wa kwanza kuishi duiniani na kumkusudia kutawala peke yake .Hata
hivyo muda usio mrefu baada ya kuumbwa kwa Adamu Bwana Mungu alisema si vema
huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi Mwanzo 2;18. Kumbe mume anahitaji
msaidizi Ni muhimu kufahamu kuwa katika mambo mengi ya kifamilia yana fanana
sana na kanisa Waefeso 5;22-32 Kwa msingi huo si vema kiongozi mkuukatika
kanisa kufanya kazi peke yake hivyo ni muhimu kuwa na msaidizi.
Viongozi wa kanisa
kama wasaidizi wa kiongozi mkuu.
Maelekezo ya Mungu kupitia kwa mkwewe Musa
yalikuwa kama hayo Si vema Musa kiongozi
mkuu kuwa peke yake bila wasaidizi, kutokana na maelekezo hayo Musa alikuwa na
wasaidizi waliokuwa Viongozi wa Maelfu na mamia na wa hamsini na wa makumi,hawa
walimsaidia musa kuchukua mzigo wa kuwaongoza wana wa Israel au kanisa la
jangwani kutoka 18;13-26,Matendo 7;37-38. Hivyo ni muhimukuwa na mgawanyo wa
wasaidizi ili kuifanikisha kazi ya Mungu Mfumo huu umefanya kazi nzuri katika
kanisa la Full Gospel of Yoido Seoul Korea kwa Dr David Yonng choi na Full
gospel Bible Fellowship Tanzania kwa askofu Zachary Kakobe na Yaoundé Cameroun
.
Sifa za Msaidizi
Kila
kiongozi msaidizi wa kiongozi anapaswa kuwa na sifa zifuatazo na kupaswa
kuhakikisha anakua nazo katika maisha yake ni sifa za muhimu na za kibiblia;-
- Kufanana na kiongozi wake mkuu.
Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye (Mwanzo 2;18) Yeyote asiyefanana
na kiongozi wake mkuu hawezi kuwa msaidizi anayefaa Mwanzo 2;19-20, Kufanana na
kiongozi wako mkuu ni kuwa na nia moja naye kama ilivyokuwa kwa Timotheo kwa
kiongozi wake Paulo Wafilipi 2l;19-20 kuwa na nia moja ni pamoja na kuwa na
maono mamoja na kiongozi wako, yaani yale anayoyaona, anayoyataka yawe, yote
hayana budi kuonekana vilevile kwa msaidizi mipango na maono ya kiongozi mkuu
hayana budi kuwa ya msaidizi pia.
- Msaidizi ana paswa kuwa mwili mmoja na kiongozi wake Mwanzo 2;18-24 lazima uhakikishe kuwa unakuwa upande wakiongozi wako mkuu kwa gharama yoyote ile 2samuel 5;1-4 Nyakati 12;1,17-18 hivi ndivyo masaidizi anavyopaswa kuwa tumika pamoja naye katika mswala ya injili katika utii kwake kama mwana na baba yake Wafilipi 2;19-22 Msaidizi anayefaa hatakuwa mfuasi wa Bwana Yesu tu bali na wa kiongozi wake 1Thesalonike 1;6 msaidizi anayefaa ni yule anayekuwa tayari kuwa mfuasi wa Kristo na wa kiongozi wake mkuu.
Wajibu wa msaidizi
Jukumu kubwa la msaidizi kwa ujumla wake
ni kusaidia na sio kuwa kinyume na kiongozi wake utamsaidia kiongozi wako mkuu
kushinda maadui zake kutekeleza majukumu yote pamoja naye mipango na maazimio
yakewasaidizi wanapojitoa hivi kuwasaidia Viongozi wao siku zote ndipo kanisa
linapoweza kuwa Jeshi kubwa kama jeshi la Mungu, Kutoka 2;16-17, Yoshua 10;6,
2Nyakati 26;1, 15 2Samuel 21;15-17 1Nyakati 12;1, 14-18, 22.
Madhara ya msaidizi
anayewasaidia waovu badala ya kumsaidia kiongozi mkuu
Msaidizi anapoamua kuwa upande ulio
kinyume na mipango ya kiongozi wake mkuu mtu huyo anakuwa anawasaidia waasi na
waovu na kufanya hivi ni kutafuta adhabu ya Mungu 2Nyakati 19;2 Hatuna budi
kuwa waangalifu tunapokuwa Viongozi Maneno ya washirika na hata wasio washirika
yatatushawishi tusiwe upande wa kiongozi wetu mkuu na hivyio kuweko na usaliti
na kumsaidia shetani kazi yake jambo hili linaharibu sana kazi ya Mungu ni
vizuri kuwa upande wa Nabii na utapokea thawabu ya Nabii Mathayo 10;40-41.
Mbinu kubwa
anayoitumia shetani kuharibu huduma ya kiongozi mkuu na jinsi ya kuikabili
Tangu Mwanzo shetani amekuwa akiwatumia
wasaidizi kuharibu huduma za Viongozi wao wakuu,alimtumia hawa kumsaidia
shetani badala ya Adamu,pale alipompa tunda mumewe ale na hivyo kuharibu huduma
ya adamu Mwanzo 3;4-6,Shetani alimtumia Sipora mkewe Musa msaidizi na hivyo
ilibidi Musa aambatane na Haruni badala ya Sipora Kutoka 4;18-29 Shetani
alimtumia mkewe Ayubu msaidizi kujaribu kuiua huduma na maisha ya Ayubu Ayubu
2;9 alimtumia Yuda mmoja wa Viongozi wasaidizi wa Yesu kumsaliti Yesu,na hii
ndio maana Yesu alimuita Yuda Shetani Yohana 6;70 kwa sababu aliifanya kzi ya
Shetani Hata leo shetani huwatumia
Viongozi wa kanisa katika kuharibu mipango ya mungu kwa kanisa Ni muhimu
kuwa waangalifu kuhakikisha wakati woote tunakuwa upande wa Viongozi wetu na
kuwalinda na kuwatia moyo na kufanya kazi pamoja nao Sehemu nyingi duniani ziko
shuhuda za kutosha zinazoonyesha jinsi Viongozi wasaidizi walivyotumika
kuharibu kanisa la mungu tuwe makini kwani Viongozi katika kanisa ni Nguzo
Tunapo tetereka jingo yaani kanisa linakuwa katika wakati mgumu sana Wagalatia
2;9 Bwana atupe neema Tunapochaguliwa kuwa wasaidizi kutokukubali kutumiwa na
Shetani katika Jina la Yesu amen.
Shukurani maalumu
Masomo haya Mwandishi alijifunza alipokuwa mshirika wa kanisa la Full
Gospel Bible Fellowship Mwenge Dar-es-Salaam kwa msingi huo ni muhimu kwako
kuwa na Ufahamu kuwa kanisa hilo ni sehemu ya mwili wa Kristo kama ilivyo kwa
makanisa mengine , mimi bnimejifunza Mambo mengi sana nilipokuwa mshirika
katika kanisa Hilo chini ya Mchungaji wangu Zachary Kakobe hivyo nachukua
nafasi hii kutambua mchango wake kwangu na kwa kanisa la Tanzania ni Muhimu
kulizingatia hili na kukubali kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu Endapo utakuwa
unapiga vita huduma ya kanisa hilo basi hata mafundisho haya yanaweza yasitende
kazi utakapoyatumia katika kanisa lako sisi tu viungo katika Kristo Nyakati
hizi hatuwezi kuendelea kung’ang’ania udhehebu bali tunapofahamu kuwa mahali
Fulani inahitajika kweli au pana mambo mazuri ya kujifunza basi ni muhimu
kujifunza kutoka kwa watu hao. Hivyo nachukua nafasi hii kuitambua huduma ya
Zachary Kakobe na kitabu hiki ni wakfu kwa ajili yake Mungu ambariki na
namtakia huduma njema amen
Rev. Innocent Mkombozi Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni