Zaburi ya 124;1-8.
Biblia
inasema Hivi “
1.
Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, 2. Kama si Bwana
aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. 3. Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu
4. Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 5. Papo
hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. 6. Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa
kuwa mawindo kwa meno yao. 7. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa
wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. 8.
Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi”.
Zaburi ni mojawapo ya vitabu vya kipekee
sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu
viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote
katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano,
inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko
vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika
zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa
hisia za watu, utafiti wa kiroho unaonyesha kuwa wengi wenye kuzisoma kuzipenda
na kuzikariri maisha yao huwa na mafanikio makubwa sana asante Bwana Mungu
wangu Mungu wa baba zangu kwa kitabu hiki kizuri Zaburi
·
Zaburi
ziliandikwa kwa sababu mbalimbali za kihisia kama vile watu walipokuwa na
furaha, huzuni, nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kama shwari katika tenzi za rohoni aliimba wimbo huo kwa
sababu ya ajali mbaya iliyokumba familia yake nay eye peke yake alipona na
kutunga wimbo huo, kwa hiyo hata zaburi ziliandikwa kutokana na mapito
mbalimbali waliyoyapitia wanadamu, kuna sababu nyingi zilizopelekea zaburi
kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1. Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili
mfano zaburi ya 1
2. Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingu
huanza kwa kusema mshukuruni Bwana
3. Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4. Zaburi za kifalme au za kimasihi
5. Zaburi za kihistoria au za kukumbuka
matukio maalumu
6. Zaburi za kusifu au Halel Psalms ambazo
huanza na neno Haleluya
7. Zaburi za maombolezo
8. Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani
Mfano zaburi ya 351-8
Zaburi
ya 124 ni zaburi ya kihistoria ni ya kukumbuka matukio na ni zaburi inayokisiwa
kuwa imeimbwa na mfalme Daudi au mtu wa karibu na Daudi Kwani zaburi
zimeandikwa na watu wengi akiwemo Musa, Sulemani wana wa Kora n.k na Daudi
anazo zaburi kama 73 hivi na nyingine ni zaburi yatima yaani haijulikani nani
aliandika, Zaburi hii ya 124 inakisiwa ndiyo iliyonukuliwa na Paulo katika
Warumi 8;31 “Mungu akiwa upande wetu ni nani atakayekuwa juu yetu?” Inaonekana
mwandishi wa zaburi hii alikuwa akitafakari kwa niaba yake na kwaniaba ya Taifa
la Israel jinsi hasira za adui shetani
zilivyokuwa juu yao jinsi alivyokusudia kuiangamiza Israel kwa moto, maji
mitego na mbinu mbalimbali, jinsi alivyokusudia kutumaliza lakini hatimaye anaanza na hitimisho kuwa kama Bwana
asingelikuwa pamoja nasi Tungeliangamia huku Israel wakiwa mashahidi ya wema wa
Bwana na utetezi wa Mungu Hivyo kama si bwana Israel na aseme sasa Israel ni
taifa linalotetewa na Mungu hata leo ni mara kadhaa wamepitia misukosuko ambayo isingelikuwa rahisi
kuiepuka kwa hali ya kawaida
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
![*](file:///C:\Users\User\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
Sisi nasi tunapotafakari maswala ambayo
adui ameyakusudia kwetu na kuona ushindi wa ajabu ni muhimu kufahamu kuwa kama
si Mungu kuwa upande wetu tungelifutiliwa mbali kweli Kama si Bwana Israel na
aseme sasa!
Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni