Zaburi 16:1-9 “Mungu, unihifadhi mimi, Kwa
maana nakukimbilia Wewe. Nimemwambia
Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako. Watakatifu waliopo
duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. Huzuni zao zitaongezeka
Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja
majina yao midomoni mwangu. Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe
changu; Wewe unaishika kura yangu. Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam,
nimepata urithi mzuri.Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu
umenifundisha usiku. Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni
kwangu, sitaondoshwa. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu
unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.”
Utangulizi:
Daudi alikuwa mtu wa mapambano
alipokuwa Duniani, alipambana vita vingi sana kwaajili yake, watu wake na
kwaajili ya ufalme wa Mungu, kwa msingi huo katika kuabudu kwake kwa njia ya
zaburi mara nyingi sana analugha tamu zinazoweza kujenga imani na ujasiri
katika maisha yetu, na kutufanya tusiogope lolote linalotukabili katika maisha
yetu, Lakini sio hivyo tu, kuna kujengeka kwa uhusiano wetu wa karibu na Mungu
unapofuatilia zaburi za Daudi ambaye anaonyesha mara kadhaa sababu za ushindi
wake na siri ya ushindi wake kuwa ulitokana na namna na jinsi alivyojenga
uhusiano wake wa karibu na Mungu. Katika zaburi hii tunasoma :-
Zaburi 16:1-9 “Mungu, unihifadhi mimi, Kwa
maana nakukimbilia Wewe. Nimemwambia
Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako. Watakatifu waliopo
duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. Huzuni zao zitaongezeka
Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja
majina yao midomoni mwangu. Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe
changu; Wewe unaishika kura yangu. Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam,
nimepata urithi mzuri.Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu
umenifundisha usiku. Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni
kwangu, sitaondoshwa. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu
unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.” Kuna
maswala kadhaa ya kujifunza ambayo Daudi anayataja lakini mazuri zaidi au yale
ambayo nimevutiwa nayo leo ni ule mstari wa nane unaosema Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa
yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. Katika mstari huu kuna mambo
mawili ya msingi ya kujifunza na ambayo yalikuwa siri kubwa sana ya ujasiri na
ushindi wa Daudi katika maisha yake yote. Mambi hayo tukiwa nayo nasi vilevile
kama Daudi tutakuwa na ushindi mkubwa sana katika maisha yetu, tutajifunza somo
hili Kwa
kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. Kwa kuzingatioa vipengele
vitatu viofuatavyo:-
1.
Kumuweka
Bwana mbele Daima.
2.
Kwa
kuwa yuko kuumeni kwangu.
3.
Sitaondoshwa.
Kumweka Bwana mbele Daima
Lugha inayotumika hapo Kumuweka
Bwana mbele Daima ina maana ya kumpa Mungu kipaumbele au kumtegemea Mungu na
kutambua uwepo wake kwenye kila jambo, kwamba Mungu yuko pamoja naye iwe usiku
au mchana, kumfikiri yeye wakati wote, kumtafakari na kumkiri mbele ya watu, ni
kuutambua uwepo wake kila mahali na kila wakati na katika hali zote, kumhisi
kuwa yuko pamoja naye, kutambua tu mara zote kuwa macho yake yako pamoja naye,
ni kufikiri wazi kuwa wakati wote niko katika uwepo wa Mungu na wakati wote
yeye ananiangalia kutokana na umuhimu ya jambo hili ganao
jipya pia limeuridia mstari wetu wa msingi katika namna nyingine ;- Matendo 2:25 “Maana
Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko
upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.” Mwandishi wa zaburi
hii haoni kitu kingine kwanza haoni msaada mwingine kokote, yeye msaada wake na
kipaumbele chake ni Mungu kwanza, wakati wote na siku zote anamtanguliza Mungu,
ni sawa na kusema au kutii amri ya Mungu inayotaka tusiwe na miungu mingine ila
yeye peke yake ona Kutoka 20:3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Siri ya
ushindi katika maisha ya Daudi ni kuwa kabla ya kufikiri kutafuta msaada kwa
mwingine yeye msaada wake ni Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi Mungu aliye hai,
wakati watu wengine katika vita wanategemea wingi wa majeshi yao, wanategemea
akili zao, wanategemea silaha zao nzito, mbinu na mikakati ya ajabu ya
kibinadamu mwandishi wa zaburi yeye anataja jina la Bwana Zaburi 20:7-8 “Hawa wanataja magari na hawa
farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na
kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.” Siri ya ushindi wetu ni
kumuweka Mungu mbele, zinapokuja changamoto za aina yoyote Mungu anataka kwanza
ufikiri kuhusu yeye, uone yeye kuwa ndio msaada umtegemee yeye na kumwangalia
yeye lakini ukitegemea mengine wewe uko chini ya laana Yeremia 17:5-8 “Bwana asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona
yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi
isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni
tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi
yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa
bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa
matunda.” kwa msingi huo maandiko yanatutaka tumuweke Mungu mbele na
kumfanya yeye kuwa wa kwanza katika kila
jambo, agano jipya linasema tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na
mengine yote mtazidishiwa, asili ya ushindi wetuni kumuweka Mungu mbele! Na ndio
ilikuwa siri kuu ya Daudi.
Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu!
Nyakati za utawala wa kifalme
zamani mtu kukuweka mkono wake wa kuume ilikuwa na maana ya Heshima au ukuu, ni
nafasi ya kuheshimika na ya juu kabisa kukaa upande wa kuume wa mfalme au
katika meza moja naye, na kula chakula pamoja naye 2Samuel 9:1-8 “Kisha Daudi akasema, Je!
Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya
Yonathani? Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi
wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema
Mimi, mtumwa wako ndiye. Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba
ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani
anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. Mfalme akamwambia, Yuko wapi?
Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli,
katika Lo-debari. Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya
Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. Basi Mefiboshethi, mwana wa
Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu.
Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! Daudi
akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya
Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako;
nawe utakula chakula mezani pangu daima. Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni
nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? ” lakini vilevile kijeshi mtu aliyekaa mkono
wa kuume maana yake alihesabika kama mlinzi, mtu aliye karibu sana, aliye
tayari kuokoa au kulinda au kuzuia uzipatwe na madhara ni askari mwenzako
mjamaa, kwa kiingereza your colleague au COMRADE Zaburi 109:30-31 “Nitamshukuru Bwana kwa kinywa changu, Naam, nitamsifu
katikati ya mkutano. Maana atasimama mkono wa kuume wa mhitaji Amwokoe na
wanaoihukumu nafsi yake” ona pia Zaburi 110:5 “Bwana
yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake.” Kwa
msingi huo ili tuweze kuona maisha ya ushindi katika kila eneo la maisha yetu
lazima tuwe na hisia kuwa tuna mpiganaji aliye karibu mkono wetu wa kuume
kutulinda na kutusaidia, ni rafiki wa karibu wa mtazamo mmoja sawa na sisi yeye
atatoa msaada kwa hiyo Mwandishi wa
zaburi alikuwa anamwangalia Mungu kuwa yuko mkono wake wa kuume na kwa vyovyote
vile hatasinzia atahakikisha anatutetea katika kila jambo linalotukabili
atatulinda na mabaya yote Zaburi 121:1-8
“Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada
wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala
hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana
ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa
usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda
utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.”
Sitaondoshwa!
Daudi anaonyesha sasa hiyimisho
kwamba ikiwa umemuweka Mungu mbele daima na ukamuweka mkono wako wa kuume
kinachofuata sasa ni kuwa hutaiondoshwa, maana yake ni kuwa hakuna cha
kukutikisha, hakuna cha kukusumbua, unakuwa na ujasiri ulio wazi, utasimama
milelel, utaimarika. utakuwa salama, hutaogopa, utalindwa dhidi ya maadui,
watatawanyika wanaokutafura nafsi yako, wataanguka na kurudishwa nyuma utadumu Zaburi 10:6 “Asema
moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.” Hakuna kutetemeshwa utasimama imara Zaburi 46:5 “Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia
asubuhi na mapema.” Wakati wote mtu anayemtegemea Mungu hatatikiswa
na lolote, hata kama yatatokea magumu kiasi gani, fitina kiasi gani, majungu
kiasi gani, vitisho kiasi gani, uzushi kiasi gani, vita kiasi gani, masengenyo
kiasi gani, njaa, kiasi gani aibu kiasi gani, mitego kiasi gani, chuki kiasi
gani, panga panghua kiasi gani, nia ovu kiasi gani, kuchafuliwa kiasi gani,
mashambulizi ya kiwango chochote kile, Hakuna kitakachozeza kukuondosha, Mungu
akiwa pamoja nawe na akiwa ndio Comrade wako anayeketi mkono wako wa kuume, uko
pamoja naye umempa heshima yake nataka nikuambie ya kuwa hatakuazha kamwe ,
hatasinzia atahakikisha kuwa unasimama, sasa inategemea wewe umemuweka Mungu
wapi, maisha yako yatakuwa na mashaka sana kama Mungu sio kipaumbele chako,
utayumbishwa hukona huko kwa sababu umeweka tegemeo lako kwa wanadamu,
umewafanya wanadamu kuwa kinga yako, Muweke Mungu mbele, tengeneza uhusiano
wako na yeye, mfanye bwana kuwa rafiki yako, muweke mkono wako wa kuume na
hutatikiswa
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni