Jumatano, 2 Machi 2016

Agizo la Kujihadhari na Manabii wa Uongo!



Yesu Kristo alifundisha katika mafundisho yake umuhimu wa kujihadhari na Manabii wa uongo Mathayo 7;15 kwa kukosa kuwa na ufahamu katika neno la Mungu tunaweza kujikuta tunachukuliwa na uongo wa shetani kwa kuikimbia kweli na kwenda mbali kabisa na neno la Mungu hata hivyo namna ya kuwatambua manabii wa uongo ni jambo linaloweza kukuchanganya kama hutakuwa na ufahamu kuhusu Neno la Mungu ni kwa msingi huo sasa leo tutachukua Muda  kujifunza neno la Mungu linasema nini uhusu manabii wa uongo ili tupate kujihadahri sawasawa na neno la Mungu.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-


Muhubiri huyu hapaswi kugusa chini wakati wa mahubiri hushinda juu ya migongo ya washirika

§  Maana ya neno Nabii
§  Jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo.

Maana ya neno Nabii.
Neno nabii lmejitokeza zaidi ya mara mia 300 katika agano la kale na mara 100 katika agano jipya katika agano la kale neno hili lilitumika kama Navi au Nabi ambalo maana yake mtu mwenye uwezo wa kupokea neno la Mungu na kulifikisha kwa watu, walifanya kazi ya kuzungumza mambo ya Mungu kwa wakati ulioko, uliopita na ujao, kwa ufupi leo tunaweza kusema kuwa manabii ni wanenaji kwa niaba ya Mungu au  watumishi wa Mungu wanaohubiri yale yaliyo haki na yale ambayo sio haki mbele za Mungu hao ndio manabii wa kweli Waefeso 4;11 nabii wa kweli kwa kawaida anakuwa na sifa kuu mbili A. atafundisha maneno ya kweli ya Mungu bila kuchuja kwa namna yoyote ile bila kujali cheo au sifa ya mtu na atafundisha njia ya Mungu kwa Usahii bila upendeleo Yohana 3;34, Mathayo 22;16, Wagalatia 2;4-6.B. Maisha yake yataonyesha matunda ya Kristo na ya Roho Mtakatifu maana Mungu anayemwakilisha ni Mtakatifu kwa hivyo maisha yake yataendana na yale anayoyafundisha  kila siku Matendo 1;1 Warumi 2;21-25 Wagalatia 5;22-25 pale tunapoona sifa izi kuu na nyinginezo sawasawa na neno la Mungu  ndipo tunapoweza kujua kuwa huyu ni nabii wa kweli  tuliyoipokea.

Jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo.
Maandiko yanatupa mwanga wa kutosha kuweza kuwatambua manabii wa uongo kama anavyo tufundisha Bwana wetu Yesu Kristo. Katika Mathayo 7;15-20 anasema tutawatambua kwa MATUNDA yao matunda ya manabii wa uongo kwa mujibu wa maandiko nikama ifuatavyo;-
a.       Manabii wa uongo hufundisha UONGO na katika maandiko wanaitwa mikia, Kufundisha uongo ni kufundisha yale ambayo hayako kwenye Biblia au yale ambayo Biblia haikumaanisha badala yeke watafundisha hadithi zilizotungwa na wanadamu na katiba zao hata kama ziko kinyume na neno la Mungu linatuonya  kuwa mbali nao katika jina la Yesu, tujihadhari kabisa Isaya 9;15-16, 2Petro 2;1-4.
b.      Manabii wa uongo hukiri kwa vinywa vyao kuwa wanamjua Mungu lakini kwa Matendo yao wanamkana  ni wenye machukizo na uovu wote Tito 1;16 watakuwa ni watu ambao wanashika Biblia au vitabu vya kidini na kwenda huko na huko kuhubiri dini lakini ukiangalia maisha yao ni ya uasherati, Uzinzi, usengenyaji, uongo, ushirikina, fitina, faraka na uadui  haya ni baadhi ya matunda ya mwili Wagalatia 5;22
c.       Manabii wa uongo kamwe hawakiri kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ila wanasema ni mwanadamu tu sawa na wengine 1Yohana 4;1-4
d.      Manabii wa uongo hukataa neema ya wokovu iliyokuja kwa mkono wa Yesu Kristo na hufundisha na kuwaambia watu kuwa watafika mbinguni kwa matendo Fulani ya sheria, Nyakati za leo hatuko chini ya sheria ya Musa ili tuko chini ya sheria ya kifalme ya Yesu Kristo ambayo tunawezeshwa na Yesu mwenyewe Tito 2;11-12 Wagalatia 5;4 2;16 Yohana 1;16-17, 2Petro 2;1-2.
e.      Manabii wa uongo huwaambia watu amani tu hata kama yale waliyoyafanya yako kinyume na neno la Mungu, manabii hao kusudi lao au mungu wao hasa ni tumbo Yeremia 23;16-17 Warumi 16;17-18 wafilipi 3;18-19. Fedha ndio lengo lau kuu wanatajirika kupitia washirika masikini ambao labda wangehitaji msaada kutoka kwao.
f.        Manabii wa uongo watasifiwa na watu wote na kutakuwa hakuna upinzani wowote wa kunenwa vibaya au vinginevyo. Nabii wa kweli kunakuwa na mchanganyo wa utukufu na aibu na kunenwa mabaya  Luka 6;20-26 angalia sifa za nabii wa kweli 2Wakoritho 6;4-10,Yohana 7;20,8:48.
g.       Manabii wa uongo hawaongozi na neno la Mungu ila wanaongozwa na mapokeo ya kibinadamu tu ndoto na maono ya uongo Wakolosai 2; 18-19, Marko 7;6-7,13. n.k.
Ni muhimu basi kujihadhari na kutokuwakubali walete upuuzi wao au kuanza kubishana nao 2Timotheo 2; 14, 23-24, waefeso 5;4 Mungu atupe neema ya kutokukubali kupotea. Lazima watumishi wenye kudai kuwa wanaihubiri kweli waishi sawa na injili, tunafahamu kuwa yako matatizo ya kibinadamu na udhaifu wa kibinadamu lakini manabii wa uongo kwa makusudi kabisa lengo lao ni kujitajirisha wao wenyewe wengine kuwaona ni gharama kubwa sana kuliko kumuona Yesu, washirika wanateseka mpaka wakiponyoka katika kanisa lao wanajisikia Huru Mungu awasaidie watu wake walioteswa na kundi kubwa la manabii wenye kujikinai na kutabiri uongo

Maisha ya Maombi !



Neno La Msingi 1Wathesalonike 5;17 “Ombeni Bila kukoma” Pamoja na kuwa Mstari huu tunaoutafakari una maneno matatu tu Ombeni Bila kukoma  ni muhimu kufahamu kuwa una uzito mkubwa sana  unaoelezea namna maisha ya mkristo au mtu aliyeokoka  anavyopaswa kuwa  yaani maisha ya mkristo ni maisha ya kuomba bila kukoma au kuacha. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-

Kuacha kuomba ni kuacha Ukristo
§  Umuhimu wa maombi kwa Mkristo.
§  Kielelezo cha Bwana Yesu 

Umuhimu wa maombi kwa Mkristo.
Mkristo akiacha kuomba anakuwa ameacha kuishi maisha ya kikristo, Kuacha kuomba ni kuacha ukristo, wako watu wengine ambao wanajiona wa kiroho sana na kwa sababu hiyo hawaoni umuhimu wa kuomba tena Yesu Kristo alikuwa wa Kiroho kuliko mtu awaye yote  alikuwa ni mtume mkuu na kuhani mkuu Waebrania 3;1 alikuwa pia ni Nabii mkuu Luka 7;16 alikuwa mwinjilisti mkuu ambaye watu walikuwa wanakimbilia na kutafuta mahubiri yake hata pale ambapo alitaka kupumzika, na Katika maombezi yake hakuna mgonjwa aliyekuja kwa Yesu asipokee uzima Luka 8;40, Marko 6;30-34 Mathayo 9;35, alikuwa ni mchungaji mkuu Waebania 13;20, alikuwa mwalimu aliyetoka kwa Mungu Yohana 3;2 zaidi ya yote alikuwa mwana wa Mungu  na anaitwa Mungu mkuu Waebania 14;14 Tito 2;13,   Pamoja na kuwa wa kiroho na huduma kubwa kiasi hiki Yesu hakuacha kuomba  naye ametuachia kielelezo.

Kielelezo cha Bwana Yesu.
Bwana yesu alikuwa mwombaji aliishi maisha ya maombi na hakuacha kuomba kila siku Bwana yesu aliomba na kila wakati nafasi ilipopatikana naye ametuachia kielelezo Alfajiri na Mapema  alifanya maombi Marko 1;35, wakati mwingine mchana aliacha huduma za muhimu na kwenda kuomba  Luka 5;15-16, wakati mwingine alikesha usiku kucha  katika kumuomba Mungu Luka 6;12 alijitenga na wanafunzi wake  akapiga magoto akaomba Luka 22;41,aliomba na kulia sana machozi Wabrania 5;7 aliomba wakati Fulani mpaka hari (jasho) lake likawa kama matone ya Damu Luka 22;43-44, Yesu aliishi maisha ya maombi, kama tunataka kutenda kazi alizozitenda na zaidi  kama alivyosema yeye Yohana 4;12 ni muhimu kufahamu kuwa haiwezekani kuzitenda kazi hizo bila ya kuwa waombaji, hatuna budi kuomba  kama Yesu ili kuzifanya kazi hizo ni kumba kwa namna hii ndiko kunakomfanya mtukutumiwa na Mungu kwa kazi za ajabu Mungu hafurahuiwi na mtu awaye yote asiyeishimaisha ya maombi kutokuishi maisha ya maombi so tu ni sawa na kuacha ukristo lakini ni kiburi kwani twaonyesha kuwa tunajitegemea jambo ambalo linamuhuzunisha mno Mungu 2Wakoritho 1;8-9, Pasipo Yesu Kristo sisi hatuwezi kufanya jambo lolote hata kama ni dogo kiasi gani Yohana 15;5 tukiishi maisha ya maombi Mungu anapendezwa na ndiyo shara ya kuwa tunamtegemea Yeye, mara kadhaa tunaonywa kwamba endapo tutaacha kuomba tutajikuta tukiingia majarini lakini kama tukiomba Mungu atatuepusha na majarib hayo Marko 14;38-40, 

Ni muhimu kukumbuka wakati wote kuombeana sisi kwa sisi kila siku Yakobo 5;16 na kuwaombea watakatifu wote  ili wasipepetwe na Ibilisi kama ngano waefeso 6;18 Luka 22;31-32 na pia kuwaombea wenye dhambi ili kwamba Mungu awape wokovu Warumi 10;1 ni muhimu pia kumombea Mchungaji wetu ili apewe usemi na Mungu katika kuubiri na kufundisha na pia ili apete kutumiwa kipekee aanapotuombea 1Wathesalonike 5;25,Waefeso 6;18-19, Matendo 4:29-30.

Dhambi ya kuacha kuwaombea wengine!



1Samuel 12; 23 “Walakini mimi hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi” Ni maneno ya nabii aliyeheshimika sana katika Israel ambaye Mungu alipendezwa naye sana Samuel alikuwa na ufunuo ulio sahii machoni kwa Mungu kuwa kutokuwaombea Israel ni dhambi ambayo yeye hangelipenda aifanye aliwaombea Israel. Kwa Msingi huo tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-



 Kwa nabii Samuel kutokuwaombea wengine ni dhambi



§  Dhambi ya kuacha kuwaombea wengine
§  Faida za kuwaombea wengine.

Dhambi ya kuacha kuwaombea wengine.
Kutokuwaombea wengine ni dhambi, mbele za Mungu dhambi yoyote ile inaweza kutupelekea kupata hukumu isiyo njema Mafndisho mengi kuusu maombi hayajaundwa katika namna ya mfumo wa kujiombea wenyewe tu angalia mfano Mathayo 6; 9-13, ….Utupe leo riziki yetu, utusamehe makosa yetu…usitutie majaribuni…. Lugha inayotumika katika maombi sio lugha ya kibinafsi yaani unipe leo riziki yangu, unisamehe dhambi zangu…usinitie majaribuni… Ni muhimu kwa kila mtu aliyeokoka kuwa na ufahamu kuwa Mungu hapendezwi na ubinafsi katika maombi anataka tuombeane, hu ni mfano ulio wazi kuwa Yesu alituombea sisi  hata kabla ya kuzaliwa Yohana 17;15-20 Maombi mengi ya wakristo hayajibiwi kwa sababu wanaangalia yetu wenyewe Wafilipi 2;4. Samuel aligundua siri ya ajabu kuwa kuacha kuwaombea wengine ni dhambi ingawa yeye alikuwa kuhani, sisi nasi ni ukuhani mteule, taifa takatifu watu wa milki ya Mungu kwa msingi huo nasi tunaweza kuliitia jina la bwana kwaajili ya wengine.
Faida za kuwaombea wengine.
Tunapouwa na Muda wa kuwaombea wengine tunapata faida kubwa sana katika ulimwengu wa Roho, tunavikwa silaha zote za Mungu pale tunapokumbuka kuwaombea wengine kimwili na Kiroho ni muhimu kufahamu kuwa maombi ambayo ni tishio kwa shetani ni yale yanayolenga  kuujenga ufalme wa Mungu na mapenzi a Mungu ili yatimizwe ndani yetu na mengine yanapaswa kufuata baadaye Waefeso 6;11,18-20 tunapoomba kwa uzito mkubwa siku zote kwaajili ya washirika wenzetu Mungu atatubariki upeo na kutupa ushindi dhidi ya adui yetu shetani Wakolosai 4;2-3 , tunapoomba kwa uzito kwaajili ya Mchungaji wetu Mungu atatubariki upeo na kutupa thawabu warumi 15;30-31,1Wathesalonike 5;25, pia ni muhimu kuomba kwaajili ya Ndugu na jamaa na majirani katika maeneo yetu ili kwamba Mungu awaokoe na ufalme wa Mungu uongezeka kuna tahwabu kubwa Mbinguni Warumi 9;1-5.
Nykati za kanisa la kwanza  kanisa lilikuwa na nguvu kubwa na lilikuwa na mamlaka dhidi ya adui kwa sababu hawakuwa na ubinafsi na kwa sababu hiyi Mungu alifanya mambo ya kutisha na kushangaza Matendo 2;43-47, 5;12-16. Wenzetu nyakati za kanisa la kwanza waliushinda umimi walikubali kuangalia mambo ya wenzao waebrania 10; 32-36 inawezekana bado hatujaona mambo makubwa ya kutisha na kushangaza katika huduma zetu kwa sababu Mungu hakai katika ubinafsi ni muhimu kufahamu kuwa maombi yanayompendeza Mungu ni maombi yanayohusiana na kuwaombea wengine.

Makusudi Ya kuokolewa !



Neno la Msingi Kutoka 10;3. “…………Bwana Mungu wa Waebrania asema hivi……..……Wape watu wangu ruhusa waende zao ili wanitumikie”


 Mungu ametuokoa kwa kusudi la Kumtumikia

§  Makusudi ya kuokolewa.
§  Faida za kumtumikia Mungu.

Makusudi ya kuokolewa.
Ni muhimu kufahamu kuwa mambo yaliyowapata wana wa Israel walipokuwa Misri na kuokolewa kwao hatimaye kuingia kanaani ulikuwa ni mfano kwetu kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani hizi 1Wakoritho 10;11 moja ya kjambo kubwa tunallojifunza kutka kwao ni uweza wa Mungu wa kuokoa Pamoja na moyo Mgumu wa Farao, ni wazi kuwa sisi nasi tumeokolewa kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel Jukumu letu kubwa la kuokolewa kwetu kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel ni ili TUMTUMIKIE Bwana  kusudi hili lilitajwa na kurudiwa tena na tena katika maandiko kwa msisitizo mkubwa. Kutoka 4; 22-23, 7; 16, 8;1, 8;20, 9;1, 9;13, 10; 3, 10; 24-26.  Sisi nasi hatuna budi kufahamu kuwa makusudimakubwa ya kuokolewa kwetu ni ili tumtumikie Mungu kama mtu aliyeokolewa haoni furaha ya kumtumikia Mungu ni kwa kutokujua ulitendalo na Bwana hana furaha na mtu wa aina hiyo.Kwa kukosa kuelewa makusudi ya kuokolewa watu wengine hawachukulii uzito swala la kumtumkia Mungu ni wazi kuwa kutokumtumikia Mungu kuna tuweka katika hali ya kujitafutia madhara lakini kwa kumtumkia Mungu kunakuwa na faida nyingi sana 

Faida za kumtumikia Mungu
Yesu aliahidi kuwa mtu akimtumikia pale atakapokuweko na mtumishi wake atakuwepo Yohana 12; 26 kwa msingi huo ikiwa tunataka kumuona Mungu akiwa pamoja nasi, ni muhimukufahamu kuwa baada ya kuokolewa tunapaswa kumtumikia Munmgu na kukumbuka ya kuwa kuna thawabu kubwa kwa watu watakaomtumikia Mungu mtu anakuwa wa thamani zaidi nyumbani kwa Mungu kwa kadiri anavyotumika kama ilivyo kwa chombo kinachotumiwa Nyumbani Mungu hutubariki kwa Baraka mbalimbali ikiwa tutayatoa maishayetu kumtumikia Yeye

§  Kutoka 23;25-26  atabariki chakula maji na kutuondolea magonjwa
§  Isaya 65;13-14  Luka 9;2-3,22;35 Hatutapungukiwa na kitu wakati wengine wakipungukiwa

Unaweza kumtumikia Mungu kwa namna gani? kwa kualika watu wengine kuja Ibadani, kushuhudia wengine habari ya wokovu, kufuatilia watoto wachanga kiroho ili kuhakikisha kuwa tunawafundisha na kuwasaidia kukua, kumtumikia Mungu kwa kuimba kwaya na kuhudhuria ibada pia kuitikia wito wa kumtumikia Bwana katika ngazi ya kichungaji kwa msingi huo ni vema tunapokuwa tumetambua umuhimu wa wa kumtumikia Munu basi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaongeza bidii ya utumishi kwa bidii kwani amelaaniwa kila aifanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu Warumi 12;11,Yeremia 48;10 kwa kufanya hivyo Baraka nyingi zinatungoja.

Wala Msiache Kukusanyika !



Andkiko la Utangulizi Waebrania 10; 25, “Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia”tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vikuu viwili.



§  Kukusanyika Nyakati za Kanisa la kwanza
§  Umuhimu wa kukusanyika pamoja

Kukusanyika Nyakati za Kanisa la kwanza.
Yakati za kanisa la kwanza watu wote waliookoka siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu na kufanya ibada zao nyumba kwa nyumba Matendo 2;46 swala la ibada kwao lilikuwa DESTURI kama ilivyo kwa wanadamu ni kawaida kula na kunywa  nyakai za kanisa la kwanza walihudhuria kila ibada , ni muhimu kufahamu kuwa mtu anayesema kuwa ameokoka kisha akashindwa kuhudhuria ibaa lilkuwa jamo la kushangaza sana, kwa namna hii Neno la bwana lilizidi kuenea na kushinda katika ulimwengu wa nyakati zao Matendo 19;20. Hata hivyo hatimaye watu kadhaa wakaanza tabia ya kuacha kukusanyika  pamoja na wengine kaka ibada na jambo hili linanyonya sana kiwango cha kiroho ni kwa sababu hii Roho wa Mungu alimuongoza mwandisi wa kitabu cha waebrania  kuwaonya watu wasiache kukusanyika Waebrania 10;25, Agizo hili ni kwa kila mmoja wetu pia katika nyakati hzi za leo, Mtu awaye yote asiyehudhuria ibada nguvu zake za kiroho hunyonywa na hatimaye kudhoofika  na kaa kanisa litakuwa wau wake wana tabia hizo litadhoofika lote  ni muhimu kwa kila moja wetu kuwa naufahamu kuwa kutokuhudhuria ibada ni kukiuka Neno au agizo la Bwana.

Umuhimu wa kukusanyika pamoja.
Ziko fikra potofu kuwa unaweza kujisomea Biblia wewe mwenyewe nyumbani na kufanya ibada pamoja na familia yako au kujiombea mwenyewe pamoja na uzuri wa kufanya mambo hayo mwenyewe nimuhimu kufahamu kuwa tunapokusanyika kunakuwa na kiu za ziada zaidi Bwana alisema  wakusanyikapo wawili watau kwa jna langu mimi niko katikati yao Mathayo 18;20 wawili watati ina maana zaidi ya familia moja  watu wanapokusanika pamja Mungu huwepokwa namna ya kipekee sana Zaburi 82;1 Biblia inasema katika andiko hilo “Mungu husimama katika kusanyiko la Mungu katikai ya miungu anahukumu” Kiongozi wa familia anapokuwa na jambo maalumu la kuzungumza na familia ni lazima aikusanye familia yake  ndivo ilivyo kwa Mungu hupenda tukusanyike ndipo anene kipekee Zaburi 50;5,7,. Mwili wa kristo yaani kanisa lna viuno tofauti tofauti na kila kiungo ni cha muhimu 1Wakoritho 12; 26-27. Tunapokusanyika miguu yetu husimama sawa mbele za Bwana Zaburi 26; 12 Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa na moyo wa kupenda kuhudhuria Ibada katika maisha yaker na kuzidi amen.

Kumbuka pia kuwa Mungu ana tabia ya ujitukuza katika kusanyiko kubwa  Zaburi 35;18 mahali penye watu wengi Nguvu za Mungu hushuka  kipekeee na tunapoomba kwa pamoja Mungu husikia Matendo 4;4,31 visingizio vovyote vle vinavyotuzuia khudhuria ibada  hatuna budi kuvitupilia mbali, shuhuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga neno la Mungu na kutufanya tusizae matunda yanayompendeza Mungu Mathayo 13;22 hatuna budi kuhakikisha kuwa tunayatupilia mbali udhuru wa aina yoyote  unaotuzuia kuhudhuria ibada  wala tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi yaw engine Mungu akubariki sana.