Andkiko la Utangulizi Waebrania
10; 25, “Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine bali
tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa
inakaribia”tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vikuu viwili.
§
Kukusanyika Nyakati za Kanisa la kwanza
§
Umuhimu wa kukusanyika pamoja
Kukusanyika Nyakati za Kanisa la kwanza.
Yakati za kanisa la kwanza watu
wote waliookoka siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu na kufanya
ibada zao nyumba kwa nyumba Matendo 2;46 swala la ibada kwao lilikuwa DESTURI
kama ilivyo kwa wanadamu ni kawaida kula na kunywa nyakai za kanisa la kwanza walihudhuria kila
ibada , ni muhimu kufahamu kuwa mtu anayesema kuwa ameokoka kisha akashindwa
kuhudhuria ibaa lilkuwa jamo la kushangaza sana, kwa namna hii Neno la bwana
lilizidi kuenea na kushinda katika ulimwengu wa nyakati zao Matendo 19;20. Hata
hivyo hatimaye watu kadhaa wakaanza tabia ya kuacha kukusanyika pamoja na wengine kaka ibada na jambo hili
linanyonya sana kiwango cha kiroho ni kwa sababu hii Roho wa Mungu alimuongoza
mwandisi wa kitabu cha waebrania
kuwaonya watu wasiache kukusanyika Waebrania 10;25, Agizo hili ni kwa
kila mmoja wetu pia katika nyakati hzi za leo, Mtu awaye yote asiyehudhuria
ibada nguvu zake za kiroho hunyonywa na hatimaye kudhoofika na kaa kanisa litakuwa wau wake wana tabia
hizo litadhoofika lote ni muhimu kwa
kila moja wetu kuwa naufahamu kuwa kutokuhudhuria ibada ni kukiuka Neno au
agizo la Bwana.
Umuhimu wa kukusanyika pamoja.
Ziko fikra potofu kuwa unaweza
kujisomea Biblia wewe mwenyewe nyumbani na kufanya ibada pamoja na familia yako
au kujiombea mwenyewe pamoja na uzuri wa kufanya mambo hayo mwenyewe nimuhimu
kufahamu kuwa tunapokusanyika kunakuwa na kiu za ziada zaidi Bwana alisema wakusanyikapo wawili watau kwa jna langu mimi
niko katikati yao Mathayo 18;20 wawili watati ina maana zaidi ya familia
moja watu wanapokusanika pamja Mungu
huwepokwa namna ya kipekee sana Zaburi 82;1 Biblia inasema katika andiko hilo
“Mungu husimama katika kusanyiko la Mungu katikai ya miungu anahukumu” Kiongozi
wa familia anapokuwa na jambo maalumu la kuzungumza na familia ni lazima
aikusanye familia yake ndivo ilivyo kwa
Mungu hupenda tukusanyike ndipo anene kipekee Zaburi 50;5,7,. Mwili wa kristo
yaani kanisa lna viuno tofauti tofauti na kila kiungo ni cha muhimu 1Wakoritho
12; 26-27. Tunapokusanyika miguu yetu husimama sawa mbele za Bwana Zaburi 26;
12 Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa na moyo wa kupenda kuhudhuria Ibada
katika maisha yaker na kuzidi amen.
Kumbuka pia kuwa Mungu ana tabia
ya ujitukuza katika kusanyiko kubwa
Zaburi 35;18 mahali penye watu wengi Nguvu za Mungu hushuka kipekeee na tunapoomba kwa pamoja Mungu
husikia Matendo 4;4,31 visingizio vovyote vle vinavyotuzuia khudhuria
ibada hatuna budi kuvitupilia mbali,
shuhuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga neno la Mungu na kutufanya
tusizae matunda yanayompendeza Mungu Mathayo 13;22 hatuna budi kuhakikisha kuwa
tunayatupilia mbali udhuru wa aina yoyote
unaotuzuia kuhudhuria ibada wala
tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi yaw engine Mungu akubariki sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni