1Samuel 12; 23 “Walakini mimi
hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi” Ni maneno ya nabii
aliyeheshimika sana katika Israel ambaye Mungu alipendezwa naye sana Samuel
alikuwa na ufunuo ulio sahii machoni kwa Mungu kuwa kutokuwaombea Israel ni
dhambi ambayo yeye hangelipenda aifanye aliwaombea Israel. Kwa Msingi huo
tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-
Kwa nabii Samuel kutokuwaombea wengine ni dhambi
§ Dhambi
ya kuacha kuwaombea wengine
§ Faida
za kuwaombea wengine.
Dhambi ya kuacha kuwaombea wengine.
Kutokuwaombea wengine ni dhambi,
mbele za Mungu dhambi yoyote ile inaweza kutupelekea kupata hukumu isiyo njema
Mafndisho mengi kuusu maombi hayajaundwa katika namna ya mfumo wa kujiombea
wenyewe tu angalia mfano Mathayo 6; 9-13, ….Utupe leo riziki yetu, utusamehe
makosa yetu…usitutie majaribuni…. Lugha inayotumika katika maombi sio lugha ya
kibinafsi yaani unipe leo riziki yangu, unisamehe dhambi zangu…usinitie
majaribuni… Ni muhimu kwa kila mtu aliyeokoka kuwa na ufahamu kuwa Mungu
hapendezwi na ubinafsi katika maombi anataka tuombeane, hu ni mfano ulio wazi
kuwa Yesu alituombea sisi hata kabla ya
kuzaliwa Yohana 17;15-20 Maombi mengi ya wakristo hayajibiwi kwa sababu
wanaangalia yetu wenyewe Wafilipi 2;4. Samuel aligundua siri ya ajabu kuwa
kuacha kuwaombea wengine ni dhambi ingawa yeye alikuwa kuhani, sisi nasi ni
ukuhani mteule, taifa takatifu watu wa milki ya Mungu kwa msingi huo nasi
tunaweza kuliitia jina la bwana kwaajili ya wengine.
Faida za kuwaombea wengine.
Tunapouwa na Muda wa kuwaombea
wengine tunapata faida kubwa sana katika ulimwengu wa Roho, tunavikwa silaha
zote za Mungu pale tunapokumbuka kuwaombea wengine kimwili na Kiroho ni muhimu
kufahamu kuwa maombi ambayo ni tishio kwa shetani ni yale yanayolenga kuujenga ufalme wa Mungu na mapenzi a Mungu
ili yatimizwe ndani yetu na mengine yanapaswa kufuata baadaye Waefeso
6;11,18-20 tunapoomba kwa uzito mkubwa siku zote kwaajili ya washirika wenzetu
Mungu atatubariki upeo na kutupa ushindi dhidi ya adui yetu shetani Wakolosai
4;2-3 , tunapoomba kwa uzito kwaajili ya Mchungaji wetu Mungu atatubariki upeo
na kutupa thawabu warumi 15;30-31,1Wathesalonike 5;25, pia ni muhimu kuomba
kwaajili ya Ndugu na jamaa na majirani katika maeneo yetu ili kwamba Mungu
awaokoe na ufalme wa Mungu uongezeka kuna tahwabu kubwa Mbinguni Warumi 9;1-5.
Nykati za kanisa la kwanza kanisa lilikuwa na nguvu kubwa na lilikuwa na
mamlaka dhidi ya adui kwa sababu hawakuwa na ubinafsi na kwa sababu hiyi Mungu
alifanya mambo ya kutisha na kushangaza Matendo 2;43-47, 5;12-16. Wenzetu
nyakati za kanisa la kwanza waliushinda umimi walikubali kuangalia mambo ya
wenzao waebrania 10; 32-36 inawezekana bado hatujaona mambo makubwa ya kutisha
na kushangaza katika huduma zetu kwa sababu Mungu hakai katika ubinafsi ni
muhimu kufahamu kuwa maombi yanayompendeza Mungu ni maombi yanayohusiana na
kuwaombea wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni