Neno La Msingi 1Wathesalonike
5;17 “Ombeni Bila kukoma” Pamoja na kuwa Mstari huu tunaoutafakari una maneno
matatu tu Ombeni Bila kukoma ni muhimu
kufahamu kuwa una uzito mkubwa sana unaoelezea
namna maisha ya mkristo au mtu aliyeokoka
anavyopaswa kuwa yaani maisha ya mkristo
ni maisha ya kuomba bila kukoma au kuacha. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele viwili vifuatavyo;-
Kuacha kuomba ni kuacha Ukristo
§ Umuhimu
wa maombi kwa Mkristo.
§ Kielelezo
cha Bwana Yesu
Umuhimu wa maombi kwa Mkristo.
Mkristo akiacha kuomba anakuwa
ameacha kuishi maisha ya kikristo, Kuacha kuomba ni kuacha ukristo, wako watu
wengine ambao wanajiona wa kiroho sana na kwa sababu hiyo hawaoni umuhimu wa
kuomba tena Yesu Kristo alikuwa wa Kiroho kuliko mtu awaye yote alikuwa ni mtume mkuu na kuhani mkuu
Waebrania 3;1 alikuwa pia ni Nabii mkuu Luka 7;16 alikuwa mwinjilisti mkuu
ambaye watu walikuwa wanakimbilia na kutafuta mahubiri yake hata pale ambapo
alitaka kupumzika, na Katika maombezi yake hakuna mgonjwa aliyekuja kwa Yesu asipokee
uzima Luka 8;40, Marko 6;30-34 Mathayo 9;35, alikuwa ni mchungaji mkuu Waebania
13;20, alikuwa mwalimu aliyetoka kwa Mungu Yohana 3;2 zaidi ya yote alikuwa
mwana wa Mungu na anaitwa Mungu mkuu
Waebania 14;14 Tito 2;13, Pamoja na
kuwa wa kiroho na huduma kubwa kiasi hiki Yesu hakuacha kuomba naye ametuachia kielelezo.
Kielelezo cha Bwana Yesu.
Bwana yesu alikuwa mwombaji
aliishi maisha ya maombi na hakuacha kuomba kila siku Bwana yesu aliomba na
kila wakati nafasi ilipopatikana naye ametuachia kielelezo Alfajiri na
Mapema alifanya maombi Marko 1;35, wakati
mwingine mchana aliacha huduma za muhimu na kwenda kuomba Luka 5;15-16, wakati mwingine alikesha usiku
kucha katika kumuomba Mungu Luka 6;12
alijitenga na wanafunzi wake akapiga
magoto akaomba Luka 22;41,aliomba na kulia sana machozi Wabrania 5;7 aliomba
wakati Fulani mpaka hari (jasho) lake likawa kama matone ya Damu Luka 22;43-44,
Yesu aliishi maisha ya maombi, kama tunataka kutenda kazi alizozitenda na
zaidi kama alivyosema yeye Yohana 4;12
ni muhimu kufahamu kuwa haiwezekani kuzitenda kazi hizo bila ya kuwa waombaji,
hatuna budi kuomba kama Yesu ili
kuzifanya kazi hizo ni kumba kwa namna hii ndiko kunakomfanya mtukutumiwa na
Mungu kwa kazi za ajabu Mungu hafurahuiwi na mtu awaye yote asiyeishimaisha ya
maombi kutokuishi maisha ya maombi so tu ni sawa na kuacha ukristo lakini ni
kiburi kwani twaonyesha kuwa tunajitegemea jambo ambalo linamuhuzunisha mno
Mungu 2Wakoritho 1;8-9, Pasipo Yesu Kristo sisi hatuwezi kufanya jambo lolote
hata kama ni dogo kiasi gani Yohana 15;5 tukiishi maisha ya maombi Mungu
anapendezwa na ndiyo shara ya kuwa tunamtegemea Yeye, mara kadhaa tunaonywa
kwamba endapo tutaacha kuomba tutajikuta tukiingia majarini lakini kama
tukiomba Mungu atatuepusha na majarib hayo Marko 14;38-40,
Ni muhimu kukumbuka wakati wote
kuombeana sisi kwa sisi kila siku Yakobo 5;16 na kuwaombea watakatifu wote ili wasipepetwe na Ibilisi kama ngano waefeso
6;18 Luka 22;31-32 na pia kuwaombea wenye dhambi ili kwamba Mungu awape wokovu
Warumi 10;1 ni muhimu pia kumombea Mchungaji wetu ili apewe usemi na Mungu
katika kuubiri na kufundisha na pia ili apete kutumiwa kipekee aanapotuombea
1Wathesalonike 5;25,Waefeso 6;18-19, Matendo 4:29-30.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni