Neno la Msingi Kutoka 10;3.
“…………Bwana Mungu wa Waebrania asema hivi……..……Wape watu wangu ruhusa waende zao
ili wanitumikie”
Mungu ametuokoa kwa kusudi la Kumtumikia
§ Makusudi
ya kuokolewa.
§ Faida
za kumtumikia Mungu.
Makusudi ya kuokolewa.
Ni muhimu kufahamu kuwa mambo
yaliyowapata wana wa Israel walipokuwa Misri na kuokolewa kwao hatimaye kuingia
kanaani ulikuwa ni mfano kwetu kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani
hizi 1Wakoritho 10;11 moja ya kjambo kubwa tunallojifunza kutka kwao ni uweza
wa Mungu wa kuokoa Pamoja na moyo Mgumu wa Farao, ni wazi kuwa sisi nasi
tumeokolewa kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel Jukumu letu kubwa la kuokolewa
kwetu kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel ni ili TUMTUMIKIE Bwana kusudi hili lilitajwa na kurudiwa tena na
tena katika maandiko kwa msisitizo mkubwa. Kutoka 4; 22-23, 7; 16, 8;1, 8;20,
9;1, 9;13, 10; 3, 10; 24-26. Sisi nasi
hatuna budi kufahamu kuwa makusudimakubwa ya kuokolewa kwetu ni ili tumtumikie
Mungu kama mtu aliyeokolewa haoni furaha ya kumtumikia Mungu ni kwa kutokujua
ulitendalo na Bwana hana furaha na mtu wa aina hiyo.Kwa kukosa kuelewa makusudi
ya kuokolewa watu wengine hawachukulii uzito swala la kumtumkia Mungu ni wazi kuwa
kutokumtumikia Mungu kuna tuweka katika hali ya kujitafutia madhara lakini kwa
kumtumkia Mungu kunakuwa na faida nyingi sana
Faida za kumtumikia Mungu
Yesu aliahidi kuwa mtu
akimtumikia pale atakapokuweko na mtumishi wake atakuwepo Yohana 12; 26 kwa msingi
huo ikiwa tunataka kumuona Mungu akiwa pamoja nasi, ni muhimukufahamu kuwa
baada ya kuokolewa tunapaswa kumtumikia Munmgu na kukumbuka ya kuwa kuna
thawabu kubwa kwa watu watakaomtumikia Mungu mtu anakuwa wa thamani zaidi
nyumbani kwa Mungu kwa kadiri anavyotumika kama ilivyo kwa chombo kinachotumiwa
Nyumbani Mungu hutubariki kwa Baraka mbalimbali ikiwa tutayatoa maishayetu
kumtumikia Yeye
§
Kutoka 23;25-26
atabariki chakula maji na kutuondolea magonjwa
§
Isaya 65;13-14 Luka 9;2-3,22;35 Hatutapungukiwa na kitu
wakati wengine wakipungukiwa
Unaweza kumtumikia Mungu kwa
namna gani? kwa kualika watu wengine kuja Ibadani, kushuhudia wengine habari ya
wokovu, kufuatilia watoto wachanga kiroho ili kuhakikisha kuwa tunawafundisha
na kuwasaidia kukua, kumtumikia Mungu kwa kuimba kwaya na kuhudhuria ibada pia
kuitikia wito wa kumtumikia Bwana katika ngazi ya kichungaji kwa msingi huo ni
vema tunapokuwa tumetambua umuhimu wa wa kumtumikia Munu basi hatuna budi
kuhakikisha kuwa tunaongeza bidii ya utumishi kwa bidii kwani amelaaniwa kila
aifanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu Warumi 12;11,Yeremia 48;10 kwa kufanya
hivyo Baraka nyingi zinatungoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni