Wakristo wengi hawaelewi uhusiano
ulioko kati ya Kanisa na Taifa la Israel Ni muhimu kufgahamu kuwa hatuwezi kuepuka
nlabda kwa shingo ngumu kuwa kwa namna yoyote ile uhusiano ulioko kati ya
kanisa yaani wakristo na wana wa Israel kuwa tuna uhusiano katika ilimwengu wa
Roho ingawa tunaweza tusiwe na uhusiano wa kitaifa au kibalozi lakini katika Mungu
Israel wanaungwa mojakwa moja na Kanisa Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vitatu vifuatavyo;-
- · Israel imewekwa wakfu
- · Kwa nini niipende Israel
- · Uhusiano wa Kanisa na Isarel
Israel imewekwa wakfu.
Neno wakfu au kuwekwa wakfu maana
yake ni kutenga kitu au watu au kutakasa kitu au mtu ili atumike kwa utukufu wa
Mungu na si vinginevyo au kulaani kisitumike kwa namna nyingine isipokuwa Mungu
tu na kwa sababu hiyoi kitu au mtu anapokuwa amewekwa wakfu anafanyika kuwa
mali ya Mungu Kutoka 13;2, 29;1
Katika maana hiyo basi ni muhimu kufahamu
kuwa Israel ni Taifa au kabila na jamaa ambayo imewekwa wakfu, imeteuliwa na kutengwa
kwa kusudi maalumu hivyo wao ni mali ya Mungu Kumbukumbu
14;2,4;20,Zaburi 135;4. Israel ni Taifa la Mungu na Yerusalem ni mji wake mtakatifu na kamwe Mungu hawezi
kuwasahahu mji hu na inchi hii na watu wake Zaburi 137;5-6, Mungu wa Israel
ndiye Mungu tunayemuabudu wokovu tulio
nao umetoka kwa wayahudi, Masihi tunayemwadhimisha alikuwa myahudi na ametoka
kwa wayahudi, hata mifumo ya ibada zetu tumerithi kwa wayahudi na Biblia tuliyo
nayo kwa sehemu kubwa imeandikwa na wayahudi na manabii wote tunaowaamini ni wa
jamii ya kiytahudi kwa msingi huo kanisa
linapaswa kuwa na uzalendo wa kisayuni kwa wana wa Israel na kuonyesha
kuwapewnda na kuwajali na kuwa wanatuhusu, Leo hii vyomboi vya habari na jamii ya watu wengine wa kisiasa na
ulimwengu wa Kiislamu wamekuwa na mtazamo duni na hafifu dhidi ya Israel na hivyo kuichukia na wakati mwingine kuilaani
katika vitendo kadhaa jambo hili linapaswa kuchukuliwa kwa umakini na watu
wanayoyajua maandiko Hili ni taifa masihi na ni taifa la Mungu ardhi hii aliyopewa Ibrahimu alipewa na Mungu
kwa hiyo kila mkristo anapaswa kuielewa siri hii na kuipenda Israel
Kwanini niipende Israel
1.
Kuipenda
Israel ni kumpenda Mungu
Amri iliyo kuu kuliko zote ni kumpenda Bwana Mungu
Kumbukumbu 6;5, kama tunampenda Mungu kwa dhati , bila hska pia tutapenda kile
anachokipenda na kuchukia anacho
kichukia , Maandiko yanaonyesha kuwa Mungu anaipedna Israel na mji wake
Yerusalem Zaburi 87;1-2 Labda mtu atasema sisi wenyeji wetu uko mbinguni na
kama Abrahamu tunautazamia mji wenye misingi ambao mwenye kuubuni na kuujenga
ni Mungu Waebrania 11;10, Wafilipi
3;20,Wagalatia 4;26 dhana hiyo ni kweli kabisa
kila mkristo anajua kuwa kuna mji Yerusalemu ya mbinguni na Yesu alisema
Yerusalemu huu wa sasa hatuwezi kukwea na kwenda kuabudu Yohana 4;21-24 Lakini
Maneno ya Bwana yesu yanshitua zaidi unaposoma katika Mathayo 5;34-35 kluwa usiape
kwa Yerusalem nmaana ndio mji wa mfalme mkuu (Yaani Mungu) na Yesu alisema kuwa
mji huu utakanyagwa na mataifa kwa wakati tu Luka 21;24 uko wakati ambapo
Heshima na utukufu wa Mungu utarudi na Mungu mwenyewe ataiatawala Dunia nzima kuanzia hapa Israel Zekaria 14;4,9.
Pichani ni jiji la Yerusalem
ambalo wayahudi wameapa hautagawanywa milele ,Upande wa kushoto ni Msikiti (The Dome of Rock) ukiwa umejengwa
mahali ambapo palikuwa ni Hekalu la Wayahudi, hapo ni mahali makini wayahudi
hawajapagusa bado,Waislamu huamini ndipo alipopaa Muhamad kwenda mbinguni
(Uongo mtupu),na ni kibla ya kwanza kabla ya Makka.Ukouwezekano kwa wayahudi
wenye msimamo mkali wa kidini kulijenga tena hekalu hilo mahali hapa
(Picha kwa hisani ya maktaba ya Mwandishi wa somo Innocent Samuel Kamote.)
2.
Kuipenda
Israel ni ufunguo wa mafanikio
Mungu amekuwa
mwema kwa Israel kwa karibu miaka 1720 hivi Waisrael hawakuweko katika inchi
yao mpaka mwaka wa 1948 waliporudi ambapo mji wao mkuu kwa wati huo ulikuwa ni
Tel-aviv-Jafa ambao una bandari na wakati huo Yerusalemu haukuwa mikononi mwao
Leo mji huu uko mikononi mwao Mungu ameanza kuirehemu Israel sawa na Zaburi ya
102;13-14 katika wakati huu ambapo Israel inazungukwa na mataifa adui wasio
watakia mema hata kidogo ni muhimu kuipenda Israel na kuwaombea amani kwani kwa kufanya hivi tunaruhusu Baraka
biunafsi na za taifa letu kwa ujumla Zaburi 122;1-9
3.
Kwa
sababu kanisa ni tawi na Israel ni shina yaani (asili).
Mkristo awaye
tyote na mchungaji au kikundichochote cha faragha wanapaswa kutambua kuwa
Israel ndio shina la wokovu wetu au ni
sawa na tawi lililopandikizwa katika shina ambalo ka asili ni Israel Warumi
11;11-21 Mungu anatuionya kanisa kuwa
sisi ni tawi tu lililopandikizwa na Israel ndio shina halisi, kutokutii kwao na
kumkatraa maishi kumeleta wokovu mkubwa kwa amataifa mengine kluweza kufurahia
neema hii ya wokovu na baraka zitakuwa kubwa zaidi kama wakitii, kwa msingi huo
kutokuipenda Israel ni kuchukia asili huku sisi tukiwa ni tawi tu
lililopandikizwa Yesu alionyesha dhahiri kuwa wokovu wetu asili yake unatoka
kwa wayahudi Yohana 4;22 Biblia yote
kuanzia Mwanzo mpaka Malaki ambayo tunaiita Agano la kale ni kitabu cha Mungu kwetu lakini kwa asili ni
Biblia ya waebrania yaani wayahudi kwa msingi huo huwezi kamwe kumteganisha
Mkristo na Myahudi adui wa wayahudi lazimam pia anakuwa ni adui wa wakristo
anayetaka kuifuta Israel Bila shaka pia atataka kuufutilia mbali ukristo kwa
msingi hio kila mkristo anawajibika kuikumbuka Israel
4.
Kuilaani
Israel ni kujilaani na kuibariki Israel ni kujibariki
Tangu mwanzo
Mungu alipomuita Ibrahimu ambaye ndiye baba wa Taifa hili alimtamkia Baraka zitakazoambatana
na wale watakaombariki lakini pia Mungu aliweka laana kwa wale watakaomlaani
Ibrahimu Mwanzo 12;1-3,26;1-6,28;10-15 Baraka hizio na matamko haya yanawahusu
Israel hata leo kwa msingi huo kila mtu anapaswa kufahamu kuwa Mungu yuko nyuma
ya maswala yote ya Israel tangu wakati wa Ibarahimu na uzao wake wale watakaomnenea mema watabarikiwa na wale
wanaomnenea vibaya watalaaniwa. Tafuta ukaone katika historia wale wote
waliowahi kuitishia Israel waliishia wapi na Historia itakuambia kuilaani
Israel ni kujiweka katika hatari
Uhusiano wa Kanisa na Israel.
somo limeandaliwa na
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima