OBADIA MTUMISHI WA MUNGU NABII WA HAKI
Mwandishi
wa kitabu cha Obadia.
A. MWANDISHI
NI NABII OBADIA MWENYEWE
-
Jina
lake maana yake ni mtumishi wa Mungu sawa na “Abdullah” la kiarabu
-
Ni
maarufu kama nabii wa haki
-
Kitabu
chake hakina nukuu yoyote kuhusu yeye kazi yake
na wito wake
-
Tunajua
kuwa alikuwa ni Nabii aliyetumwa huko Edomu kusini mashariki ya Yordani
-
Kitabu
chake ndio kifupi kuliko vyote katika agano la kale
-
Tareha
ya uandishi inakadiriwa kuwa mwaka wa 586 k.k.
- Obadia
haelezi ni lini alipata maono na
ingawaje ni kutokana na yale anayoelezea unaweza kuhisi kuwa huenda ni baada ya anguko la
Yerusalem
B. UPEKEE
WA KITABU CHA OBADIA
-
Ni
kitabu cha pekee katika ujumbe wake na urefu wake
-
Ni
kifupi kuliko vyote katika Agano la kale na kinabeba Tangazo na hukumu nzito
kuhusu dhambi
-
Ujumbe
wa Obadia kimsingi uliihusu Edomu wana wa Esau
ingawa aligusia na kurejezwa tena kwa Wayahudi ambako kutatimia kwa
ukamilifu atakapokuwa anarudi Kristo baada ya dhiki ile kuu
C. HISTORIA
YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA OBADIA
-
Mwanzo
25;21-34,27;32-33 Hesabu 20;14-21, 2samuel 8;11-14-14, 2Nyakati 20;1-24,21;8-16
-
Ili
kukifahamu kitabu cha Obadia Vizuri msomaji anapaswa kurudi nyuma na kuangalia
maisha ya Mapacha wa Isaka yaani Yakobo na Esau
-
Mashindano
yao yalianza tangu tumboni mwa mama yao na yaliendelea kwa karne nyingi katika
ya vizazi vyao Mwanzo 25;21-34 watoto wote walikuwa na wazazi wacha Mungu na
haki sawa ingawaje Esau alikuwa na shauku kwa mambo ya mwilini zaidi wakati
Yakobo alikuwa na shauku ya mambo ya kiroho licha ya kuwa mwenye dhambi alikuwa
na shauku katika Mungu na ahadi zake Waebrania 12;16 inasema Esau hakuwa mcha
Mungu
-
Mungu
aliona tabia zao hata kabla ya Kuzaliwa Mwanzo 25;23 Tabia tofauti na mitazamo
Tofauti iliwapelekea vijana hao katika muelekeo Tofauti kidini, kiuchumi, na
kimafanikio.
-
Upendeleo
ulionyeshwa na kila mzazi ulichangia katika kuelekea kwenye migogoro wao
-
Baraka
ambazo Isaka baba yao alikusudia kumpa Esau na zikaibiwa na Yakobo zilipelekea
Chuki kubwa ya Esau dhidi ya Nduguye, Esau aliapa kuwa atamuua Yakobo na hii
ilipelekea Yakobo kukimbia mpaka Padan- aram kwa mjomba wake Labani
-
Esau
alitunza kisasi hicho kwa miaka 20 hivi mpaka wakati Yakobo alipokuwa anarudi na Esau alituma kikosi cha
askari 400 kumuua Lakini kwa neema ya Mungu, Mungu aliingilia kati na wakapatana
-
Ingawa
Esau na kizazi chake chote hawakuweza kuushinda uchungu waliokuwa nao dhidi ya
Yakobo na kizazi chake
-
Miaka
300 baadaye kwa ajili ya uchungu na chuki Edomu haikuwaruhusu Israel kupita
katikati yao walipokuwa wakitoka Misri Hesabu 20;14-21.
-
Mwaka 1042
k.k yaani kama miaka 700 hivi baadaye Daudi alizipiga nchi jirani na kupanua
mipaka ya Israel na kuwafanya wana wa Esau yaani Edomu kulipa kodi yaani
kutimiza unabii kuwa Esau angemtumikia Yakobo.
-
Wakati
wa utawala wa Yehoramu Edomu waliasi 2Falme 8;20-22 na miaka 146 ilipita ndipo
Edomu wakiungana na Waamoni na Wamoabu waliivamia Yuda wakati wa utawala wa
Yehoshafati lakini Mungu alimpa Yuda ushindi.
-
Mwaka wa
586 k.k Edomu walifurahia ilipoanguka Yerusalem Zaburi 137;7 Ezekiel 35;15
-
Inaonekana
kuwa baada ya Waedomu kushirikiana na Wakaldayo waliruhusiwa kukaa kusini mwa
Israel baada ya wayahudi kuchukuliwa mateka huko Babeli
-
Walifanikiwa
sana, lakini Makabayo baadae aliwashinda na kuwalazimisha kushika sheria za
kiyahudi na baadaye wayunani na Warumi walipotawala waliliita eneo hilo Idumeya
-
Inasemekana
kwamba Mfalme Herode mkuu anatokea katika jamii hiyo na eneo hilo
-
Baada ya
mwaka wa 70 B.K Waedomu walimezwa na waarabu na wametoweka leo hawako kama
Taifa au kabila.
D. MISTARI
YA MUHIMU
-
Msatari
wa 3-4
-
15
-
17
-
21
E. MIGAWANYO
YA KITABU CHA OBADIA
-
Kuanguka
kwa Edomu Mstari wa 1-16
-
Kuhuishwa
kwa Israel Mstari wa 17-21
F. UCHAMBUZI
Hukumu
ya Mungu dhidi ya Edomu mstari wa 1-14.
-
Unabii
unahusu kuanguka kwa Edomu mstari wa
kwanza unaonyesha kuwa kile Mwandishi aliandika sio mawazo yake lakini Mungu
alikuwa amemfunulia “Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana” hii inaweza kuhusu Obadia kusikia kutoka kwa Mungu kabla ya
kuandika na huenda Yeremia na Ezekiel pia walipokea ujumbe kama huo.
-
Mjumbe
aliyetumwa inaweza kuwa Malaika au Roho wa Bwana aliyetumwa kuyachochea
mataifa kuinuka dhidi ya Edom
G. HALI YA
EDOMU
-
Walikuwa
na kiburi Mstari wa 2-4 walijiinua kwa sababu walikuwa na eneo lisiloweza
kuvamiwa na mafanikio ya kijeshi na kisiasa waliyokuwa nayo iliwapelekea
Kujiamini na kuacha kumtumaini Mungu Zaburi 127;1 Bwana asipoulinda mji
aulindaye akesha bure.
Mabaki
ya mji wa wa Petra ambao ulikuwa chini ya serikali ya Edomu kama ngome zake
zinavyoonekana leo Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya Mchungaji Innocent
Kamote.
-
Ingawa
mji wao ulikuwa jangwani lakini mataifa mengi yaliionea wivu Edomu kwani
walikuwa matajiri wa visima vya maji na
mabonde mazuri
-
Walikuwa
na madini ya chuma na shaba na njia kuu za kibiashara hata kwa njia ya bahari hivyo utajiri wao pia ulichangia kiburi
walichokuwa nacho Mstari wa 5,-6.
-
Edomu
waliifanya biashara na Syria, Ashuru, India, Misri, Arabuni na Afrika
-
Mstari
wa 5-6 unaonekana katika maono ya Obadia
kwamba wangepoteza utajiri wao moja ya mji wao mzuri ungetekwa na huu ni mji wa Petra kiyunani au Sela
kiibrania ambalo jina hilo maana yake ni mwamba,
-
Ilikuwa
ni ngome kabambe isiyoweza kuanguka, tajiri na yenye kuzungukwa na mawe kila
upande Linganisha Edom na ushauri unaotolewa katika 1Timotheo 6;1-19 hasa 17.
-
Kumbuka
maagizo ya Mungu kwa Israel walipokuwa wakitoka Misri katika Kumbukumbu 2;4-5
na 23;7 na kitendo cha Waedom Hesabu 20;14-21 lakini pamoja na hayo chuki yao
iliendelea Zaburi 137;7 na kulingana na
Ezekiel 35;1-11 Kitendo cha Edomu kilitokana na chuki na wivu wa
kale Galatia 6;7wenye uchungu.
-
Kumbuka!
Mungu atayahukumu au huukumu mataifa kulingana na jinsi
yanavyoshughulika na watu wengine na hususani watu wake aliowachagua Edomu
walihukumiwa kutokana na tendo lao la kuwa kinyume na wanaoteseka katika
Mathayo 25;31-46 Yesu alifundisha kuwa tuwasaidie wale wanaoteseka au wenye
uhitaji kama wakimbizi, wathirika, masikini na wenye vita sasa ukilinganisha
Matendo ya Edomu na Mathayo 5;43-45 na 1Yohana 3;15-18 tunajifunza kanuni za
kuwapenda maadui zetu na chuki zinatufanya kuwa wauaji mbele ya macho ya Mungu
kama hatia iliyowapata Edomu.
H. SIKU YA
BWANA MSTARI WA 15-17.
Kwa
ujumla hii inazungumzia swala la siku ya hukumu ya Mungu dhidi ya Maadui zake,
Pia hutumiwa na Manabii kuelezea matukio ya mwisho wa dunia ambayo hujumuisha
·
Kunyakuliwa
kwa kanisa
·
Dhiki
kuu
·
Vita vya
Armageddon
·
Kurudi
kwa Yesu mara ya pili katika utukufu
·
Kuokolewa
kwa Israel
·
Hukumu
ya mataifa
·
Utawala
wa Yesu Kristo wa miaka 1000 duniani
Kwa ajili ya Edomu siku ya Bwana
ilimaanisha siku ya hukumu ya Edomu kwa ajili ya uchungu dhidi ya Ndugu zao
-
Kiburi
kingine cha Edomu ilikuwa ni rafiki zao Mstari wa 7 Waarabu walikuwa ndio
rafiki wa karibu wa Waedomu na walijiunga
nao katika kuishambulia Yuda Zaburi 83;5-6 pia rafiki zao Waamini, Wamoabu, na
wengine waliifanya biashara nao hawa waliwageuka
-
Kiburi
cha kisiasa Mstari wa 8-9 Waliwategemea wenye Hekima, Viongozi wao wa kisiasa
washauri na majeshi wataalamu wa Vita wa mlima Seiri walijulikana sana kwa Hekima na maarifa ya
ulimwengu inasemekana watu Rafiki wa karibu wa Ayubu mwenye Hekima Elifazi
Mtemani alitokea Temani ambazo ni sehemu
za Edomu Linganisha msatari wa 9 na
Ayubu 2;11. Hekima ya kibinadamu inaweza kutumiwa kwa ajili ya Mungu na
kwa utukufu wake kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa salama Yakobo 1;5 Ingawaje
maarifa na Hekima pasipo Mungu haiwezi
kusaidia katika kuikwepa hukumu yake.
-
Kiburi
kilichotokana na nguvu za kijeshi mstari wa 9; na kuwa na makomandoo wa
kivita mashujaa watemani vilitilia hofu
mataifa mengine Yeremia 49;16 walijitumainia katika hali hiyo lakini
ilitabiriwa kuwa askari wake wangechinjwa na watu wangeachwa bila ya ulinzi
-
Sababu
kuu za Maangamizi ya Edomu ni Mstari wa 10-14.
Uasi
dhidi ya Ndugu zao
Kusimama
peke yao kujitenga kiburi cha Kujiamini
Kufurahia
maangamizi ya ndugu zao
Kuwadharau
ndugu zao na kuwasengenya siku ya taabu zao
Kufurahia
utajiri na mali za ndugu zao na Kuwashambuilia mateka waliosalia.