UTANGULIZI
Katika sehemu nyingi za ulimwengu leo, kanisa
la Mungu linakua kwa kasi, Matokeo yake kumekuwa na kundi kubwa la wakristo
wanaohitaji huduma ya kichungaji na uongozi wa kiroho. Maandiko yanawaita watu
hao kondoo ambao wanahitaji mchungaji wa kuwaongoza, kuwatunza, kuwahudumia,
kuwalisha, na kusimamia usalama wao. Kristo alitumia mfano huu wa kondoo na
mchungaji kuonyesha ni huduma gani watu wanaihitaji, Kwa bahati mbaya Pamoja na
kuwa na wachungaji wengi na maaskofu wengi na waangalizi bado kondoo wengi
hawajaweza kufikiwa kwa huduma ya kichungaji huduma hii inahitajika sana.
Wewe
mwenyewe umekuwa ni shahidi jinsi ambavyo umekutana na Kondoo wengi nje ya
kanisa lako au waliokimbilia katika kanisa lako wakitokea sehemu nyingine na
huenda labda kwa mchungaji au askofu maarufu sana au kanisa maarufu sana na ukashangaa
kuona kuwa alishindwa kupata huduma ya kichungaji, Hili likufumbue macho kuwa
kama ulihudumia wa mwengine huenda na kondoo ambao Bwana amekuita kuwachunga
wamewahi kutafuta huduma ya kichungaji kwa mtu mwingine wengine wakisikia hivyo
wanaumia unaumia nini ? Jambo unalotakiwa kulifanya ni kudumisha na kuboresha
huduma ya kichungaji Sikia huduma hii ni zaidi ya Kuhubiri kwa mbwembwe
kupandisha sauti na kushusha au kufanya miujiza! Watu wanahitaji kufikiwa kwa
karibu zaidi kamuulize Musa miujiza haikusaidia kupunguza manung’uniko
waliyokuwa nayo watu na wala pamoja na upako aliokuwa nao hakuweza kuwafikia
watu woote kihuduma hata hatimaye aliiona kazi hii kuwa ngumu “Musa akamwambia
Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako?kwa nini sikupata neema machoni
pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa woote juu yangi?.... .MIMI SIWEZI KUWACHUKUA WATU HAWA WOTE
PEKE YANGU, KWA KUWA NI MZIGO MZITO SANA WA KUNISHINDA… kama
ukinitenda hivi nakuomba uniulie mbali..” unaona! Usifikiri basi kazi hii ya kichungaji
na huduma hii ya kichungaji ni rahisi tu wengi imewashinda wengi wetu leo
tungekuwa wahubiri wazuri na wakubwa sana lakini
tuko hapa tuliko pia kama matokeo ya kushindwa
kulelewa au kulelewa vizuri katika huduma nzuri za kichungaji yaani tumekosa
malezi ya kichungaji. (Hesabu 11;11-12,14-15)
Lengo
na kusudi la somo hili si kuangalia wapi tumetoka na kutafuta kulaumu wengine
hapana ni kujifunza kutokana na makosa na kuamua kutilia maanani kusudi kuu la
somo hili ili kwamba tuweze kufanya vizuri zaidi ya kizazi kilichopita au
kitakachopita katika huduma hii ya kichungaji kwa msingi huu basi tunapopitia
somo hili na tuache kiburi tujinyenyenyekeze na kukubali kufundishika bila
kujali kuwa tumechunga kwa miaka mingapi na taratibu moyoni omba sala hii
“Bwana
yesu wewe ndiye mchungaji mwema mimi si mwema kukushinda wewe nisaidie najua
kuwa umeniita katika huduma hii ya kichungaji lakini mimi siwezi kuchunga
nataka wewe unifungue akili zangu na moyo wangu nipokee maelekezo nawe unipe
zaidi ya maelekezo ili niwe faida katika mwili wako na kukuzalia matunda yaliyo
bora nisamehe kwa woote niliowapoteza kwa kutokuwa na huduma bora ya kichungaji
nisaidie tangu sasa kujifunza kutoka kwako asante Bwana Yesu kwa kuwa tangu
sasa utanifanya kuwa mchungaji mwema kama ulivyo wewe amen”
Naam
baada ya sala hiyo moyoni naamini wote tutakuwa tayari kujifunza somo hili
huduma za kichungaji kwa moyo wa unyenyekevu fuatana basi na muandaaji wa somo
hili Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote ambaye Mungu amemuandaa kutupa dira ya
huduma ya kichungaji katika kozi hii Mungu na akubariki unapofuatana nami Amen.
Huduma ya kichungaji
ni huduma ya pekee na ya tofauti Biblia
inasema Naye ametoa wengine Waefeso 4;11 kwa msingi huu kazi ya kuwajenga watu
wa Mungu wakue hata wafikie kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo ni
kazi ambayo Mungu amewapa watu maalumu aliowaita kwa kusudi hilo kwa hivyo kazi
hii inahitaji wito, Bila wito maalum mtu hawezi kuifanya kazi hii, haijalishi
kuwa mtu amesoma jinsi gani au amepata mafunzo kiasi gani bila ya wito mtu hawezi kukamilisha kazi hii ya huduma,
Mungu anapomuita mtu humpa mtu huyo neema maalum ya kuweza kuikamilisha kazi
hiyo.
Kwa
msingi huo kila mtu anapofikiri kuhusu Huduma ya kichungaji anapaswa kufahamu
kuwa bila ya wito ni vigumu kutimiza kile ambacho Mungu anataka kifanyike kwa
kondoo zake wito ni neema maalumu inayomwezesha mtu aliyeokoka kutimiza kwa
kuwezeshwa na Roho Mtakatifu wajibu katika eneo ambalo Mungu anakusudia
alitimize. Ni maombi yangu kuwa utatambua kwa upya kile ambacho Mungu
amekujalia kwa kukuheshimu na kukupa wito huo maalum wa kuhudumia kondoo zake
na hivyo utaomba na kuendeleza kile ambacho Mungu amekikusudia kwako kwa jina
lake.
A: UFAHAMU
KUHUSU WITO.
Neno wito
maana yake ni kumuita mtu au kumuhitaji kwa ajili ya shughuli Fulani maalumu, ofisini
au kumuajiri au kumuamuru aje, au mkutane, au mkusanyike au kumpigia mtu mbiu
kwa shughuli maalum nk. Hizi ni maana chache tu za neno wito zinaweza kuwako
nyingi zaidi ya hizo Katika Biblia neno wito
lilitumika kama kuita kwa sauti Mwanzo 3;9,Yohana 10;3, au kuita kwa
amri Daniel 4;14 na Matendo 4;18.Yesu alitumia neno wito kama mwaliko Mathayo
9;13 kuita pia kulikuwa na maana ya kumpa mtu jina 1Samuel 1;2,Mathayo 1;21,Na
pia neno wito lilitumika kwa mtu aliyechaguliwa na Mungu kwa ajili ya huduma
maalumu Waebrania 5;4.Neno wito pia lilihusisha maana ya kujitoa, kutumika bila
kuwa na matumaini ya kupata faida, kujitoa katika kuhudumia wengine hii pia ni
maana ya wito ijulikanayo sana kwa nchi ya Tanzania.
AINA KUU TATU ZA WITO.
Kibiblia wito umegawanyika katika maeneo
makuu matatu hata ingawaje waalimu wengine hufundisha kuwa kuna aina kuu mbili
za wito. Aina hizi za wito hutegemeana kwa kuwa huwezi kuwa na aina ile ya tatu
ya wito bila kupitia hizi mbili za kwanza na huwezi kuwa na ule wa kwanza bila
kutimiza huu wa pili kwa hivyo aina hizi za wito hutegemeana sana.
AINA YA
KWANZA YA WITO NI WITO WA JUMLA KATIKA WOKOVU.
Wito
katika wokovu ni wa kwanza ni wito unaokuja na tangazo la kumtaka mtu aokoke, au
akubali mpango wa wokovu, ni wito unaoambatana na kumtaka mtu atubu dhambi zake
kwa kumaanisha kuziacha na kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wito huu
hutolewa kwa watu woote wala haubagui mtu maandiko yanasema ili kila aaminiye
awe na uzima wa milele Yohana 3;16 wito huu unacho hitaji ni mwitikio wa mtu, haubagui
mtu lakini watu hujibaguwa wenyewe kwa kuifanya mioyo yao kuwa migumu kupokea
wokovu.
AINA YA PILI
YA WITO NI WITO WA JUMLA KATIKA UTUMISHI.
Aina hii
ya wito ni wito unaokuja moja kwa moja baada ya kukubali wito wa kwanza kila
mkristo aliyeokoka ameitwa kumtumikia Mungu, Mungu alipowaokoa wana wa Israel
kutoka Misri alibainisha wazi kusudi la kuwaokoa kwake kuwa ni ili wapate
kumtumikia Mungu angalia Kutoka 8; 1, 20, 9; 1, 13, 10; 7, 12; 31 Mungu
anapokuwa ametuita kutoka dhambini makusudi yake makubwa ni ili tumtumikie
hivyo basi kila mkristo ana wajibu wa kumtumikia Mungu
- Woote
tumeitwa kuwa mashahidi wake Matendo 1;8
- Woote
tunajumuishwa katika Agizo kuu linalobeba kuwaambia watu habari njema na
kufundisha (Mathayo 28;19,Marko 16;15-16,Luka 24;47)
- Nyakati
za kanisa la kwanza wakristo woote waliifanya kazi ya Mungu na ishara
zilifuatana nao Marko 16; 17.
- Roho
Mtakatifu alitolewa kwa waamini wote ili wote wawe na Nguvu za kushuhudia
Matendo 1;8
- Wengi
walianzisha makanisa kokote walikotawanyika Matendo 8;1,4,11;19-22 hili
lina maanisha kila mkristo yu aweza kufanya huduma au ameitwa kufanya
huduma hizi
- Mungu
anataka kila mtu amtumikie na hivyo ametoa karama mbalimbali 1Koritho
12;7,11, na Biblia inaonyesha ya kuwa kila mtu amepewa karama Fulani ya
neema 1Petro 4;10
- Kristo
anahitaji kila mkristo kujituma kulingana na neema aliyopewa ni kama mtu
anapojenga Nyumba atahitaji mafundi waashi, Seremala, bomba wa Umeme Rangi
n.k mtu mmoja tu hawezi kufanya kazi hizi zote Peke yake Kanisa linahitaji
waalimu wa shule za jumapili, waalimu wa watoto, viongozi, mashemasi,wanaoshughulika
na vijana n.k na ndio maana Mungu ametoa karama za kutenda kazi au
masaidiano Warumi 12:1-8
AINA YA TATU
YA WITO NI WITO MAALUMU KATIKA UTUMISHI.
Aina hii
ya wito inakuja miongoni mwa wakristo walioitwa katika wito wa wokovu na
waliokuwemo katika wito wa utumishi lakini sasa wanatengwa maalumu wawe Karama
kwa Mwili wa Kristo yaani kanisa kuuwezesha kukua kumwelekea Kristo (Waefeso
4;7-16) watu walioitwa katika wito maalum wa utumishi kwa ufupi tunaweza kusema
kuwa wameitwa katika wito maalumu wa uongozi katika Kanisa hawa ni Mitume, Manabii,
Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu. Watu hawa hawajiiti wenyewe katika Eneo
hili kwa ufupi ni kuwa wameitikia tu mpango wa Mungu katika maisha yao 1Timotheo
1; 12, Matendo 9; 15-16. Hivyo pamoja nakuwa kila Mkristo anayo huduma
tunapaswa kutambua kuwa ziko huduma hizi ambazo Mungu ameziweka za kimaongozi
na Hii ndiyo Huduma ya Kichungaji tuliyoitiwa.
MUNGU HUITA
WATU NAMNA GANI?
Inapofikia hatua ya watu kujadili kuwa
umeitwa namna gani na kila mtumishi kutoa ushuhuda wake jinsi walivyoitwa hapo
ndipo wengine hingia mashaka wakidhani kuwa huenda labda hawajaitwa kwa vile
wanavyojilinganisha na wengine Biblia inasema mtu anayejilinganisha na mwingine
hana akili (2Wakoritho 10; 12) Kila mtu ni tofauti na mwingine kwa sababu Mungu amekusudia uwe vile ulivyo,
Mungu huita watu kwa njia mbalimbali na kwasababu
kila mtu ni wa pekee Mungu humuita kila
mtu kwa njia ya tofauti .
- Musa
aliitwa kutoka katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto na hakiteketei
Kutoka 3; kwa kusudi la kuwaokoa waisrael
- Isaya
aliona maono hekaluni na kusikia sauti ikimwambia nenda na uwaambie (Isaya
6;1-9
- Paulo
aliitwa kwa kupigwa nchini kwa mwanga mkali Matendo 9;1-20
- Elisha
kwa kutupiwa vazi na Eliya na kuambiwa amfuate 1Falme 19;19-20 kuwa mrithi
wa Eliya
- Yoshua
kwa kuwekewa mikono na Musa Hesabu 27:18 Kuwaingiza watu katika Inchi ya
kanaani
- Timotheo
kwa kuchaguliwa na Mchungaji wake Paulo na kuwekewa mikono Matendo
16;1-3 kwa kusudi la kuwa
Mwinjilisti na Mchungaji
- Samuel
na Samsoni kwa kutolewa na wazazai wao kuokoa Taifa na kuwa kuhani Waamuzi
13,1Samuel1;11
- Barnaba
kupitia huduma yake Matendo 9;26,13:1-2 Kuwa Mishionari, Mchungaji, Mwalimu
na mwinjilisti
- Prisilla
na Akila Kupitia huduma zao kuwa waalimu na wamishionari Matendo
18;18-26,Warumi 16;3
- Gideoni
kupitia malaika Waamuzi 6 ili kuwashinda maadui wa Israel, Mariam Malaika
ili awe mama wa Masihi Luka 1; 26-38.
- Kwa
namna yoyote ile ambayo umeitwa wito unakuja kwa kupitia Roho wa Mungu
1Koritho 2;14,Yohana 10;27 na mtu husikia kwa masikio ya kiroho wala si
kwa masikio ya asili, Mungu ndiye ambaye huita haijalishi ametumia njia
gani kwani mtu huwa hajichagui mwenyewe Yohana 15;16, Mungu huwaongoza
watu wake aliowaita hatua kwa hatua mpaka kufikia lengo alilolikusudia
atumike Yohana 10;27, Zaburi 37;23 Matendo 13;2 na 16;6-10 Yeye Mwenyewe
atakujaza hamu ya kuhubiri na kutaka kuwahudumia watu wake na kuwasimamia
utajikuta unamtafuta na atathibitisha kwa namna nyingi kuwa yuko pamoja
nawe atakupa vipawa ambavyo vina sauti yake na hutafurahia kufanya kazi
nyingine yoyote.
MADHARA YA
KUIFANYA KAZI YA MUNGU BILA WITO;
Kuingia katika
utumishi bila ya wito ni jambo la hatari sana 2Samuel 18; 19-33, Ezekiel 13; 36
na Walawi 10;1-2. Wako watu wengine leo huingia katika huduma kwa nia mbaya
aidha wanataka Heshima au kuwa viongozi wakubwa katika watu au kuingia kwa
sababu yoyote ile isiyompendeza Mungu
UMUHIMU WA
WITO KUAMBATANA NA UPAKO.
Kama mchungaji umeitwa katika huduma
kwa maana kuwa umetumwa na Yesu kama yeye alivyotumwa na Baba yake, Yohana 17;
18 ni muhimu basi wito wako uandamane na upako Matendo 10; 38, Luka 4; 18 Kwa
msingi huo basi kama Bwana amekutuma, Roho wa Mungu atakuwa juu yako bila ya
kujali kuwa umeitwa namna gani na atakupaka mafuta maalumu kwa kusudi la
kutimiza yale aliyoyakusudia.
Umuhimu wa
upako
Tendo la kupakwa mafuta lilikuwa la
muhimu sana kwa jamii ya nyakati za Biblia na tamaduni za wakati ule Ruthu 3;3,
Ruthu alijipaka mafuta ili ajiwakilishe kwa Boazi, hata hivyo wakati wa huzuni
watu hawakujipaka mafuta Daniel 10;3, Mafuta pia yaliweza kutumiwa kama tiba
Luka 10;34 na pia yalitumika wakati wa kumweka mtu wakfu (Kutoka 30;22-29 na
1Samuel 16;1 kutoka 29;29,30;26.kwa msingi huu wafalme, makuhani na manabii waliitwa
wapakwa mafuta kwa sababu waliwekwa wakfu kwa kutiwa mafuta Lawi 4;3,4;16,6;20
na Zaburi 133;2 wakati mwingine waamuzi pia walikuwa na upako ingawa si kwa
kuwekewa mafuta
Matokeo ya
upako
Upako unapokuwa juu ya mtu unampa
Mungu nafasi ya kukamilisha wajibu fulani ndani ya mtu ambao kwa nguvu zake za
kawaida asingeweza kuutimiza (Waamuzi 14;6,14;19,15;15-16,16;30 Mchungaji anapohudumu
katika nguvu hizi huonekana shujaa.
Siri ya
upako
Siri ya
kuwa na upako ni rahisi na ngumu, Yesu katika uanadamu wake alijiachia kwa Roho
Mtakatifu kwa asilimia mia moja Hivyo Yesu alipokea Roho Mtakatifu bila kipimo
(Yohana 3; 34) Hivyo basi kipimo cha upako wa mtu kinategemea jinsi gani
anajiachia kwa Roho Mtakatifu na katika utii wa mapenzi ya Mungu, Kadiri mitume
walivyojiachia kwa Roho Mtakatifu ndivyo na Roho alivyowatumia Luka 24; 49,
Matendo 2; 37. Huduma ya kichungaji itakuwa na matokeo makubwa sana kama upako
utakuwa juu yetu hivyo ni lazima tuuhitaji upako kwa gharama yoyote Zaburi 92;
10
Tahadhari.
Upako utafanya kazi juu ya mtu
kulingana na wito ambao Mungu ameukusudia kwa mtu Matendo 9;15-16 Yohana
21;18-19 Paulo na Petro walikuwa na upako kulingana na huduma walizokuwa
wameitiwa.Ni muhimu kujiachia kwa Mungu ili atuongoze kama atakavyo Matendo
19;15,10;6-8,16;9-12,18;9-11, Kama Mungu amekupaka anaweza kukutumia hata kama
unatabia mbaya lakini hii ni hatari kwako kwani unaweza usiingie mbinguni,
kumbuka pia kuwa upako ni gharama na hupatikana kwa maombi na si kwa
kuambukizwa kirahisi tu, usiigize upako wa mtu mwingine,tumia upako kwa nidhamu
kwani unaweza kufanya mambo makubwa sana lakini ni muhimu kuutumia kwa adabu, usiufungie
mipaka, usiulazimishe wewe hubiri na kukaa katika neno 2Timotheo 4;2.
B:
KUENDELEZA MAISHA YA KIROHO.
Baada ya kuwa Mtumishi amethibitisha
kuwa ameitwa katika wito huu wa utumishi
ulio maalumu hana budi kufahamu kuwa ana wajibu wa kuhakikisha anajiendeleza
Kiroho ni hatari kuwahudumia wengine kisha tukajisahau kudumisha uhusiano wetu
na Mungu na kosa hili limekuwa likifanywa na watumishi wengi wa Mungu na
hatimaye hujikuta wakifilisika kiroho na kuharibika Wimbo uliobora 1;5-6.
- Mtumishi
awaye yote ni lazima awe amekutana na Mungu yeye mwenyewe kibinafsi, Mungu
tunayejifunza habari zake ni Nafsi na hushughulika na mtu mmojammoja
Binafsi Hivyo ni lazima ukutane naye Binafsi na abadilishe maisha yako
kupitia wokovu. John Wesley Mwanzilishi wa Methodist alihubiri kwa muda
kabla ya kuokoka si vizuri kwa mtu kuwa katika huduma huku akiwa
hajakutana na Mungu Binafsi na kuzaliwa mara ya pili Kumbukumbu 18; 20.
- Kuzaliwa
mara ya pili pekee hakutoshi ni lazima mtumishi ahakikishe anakaa ndani ya
Kristo Yohana 15;1-4 Matunda hayawezi kuzaliwa kama tawi litakuwa nje ya
mzabibu, Aidha haiwezekani kabisa Mkristo mtumishi kufanya kazi hii bila
kujazwa na Roho Mtakatifu Matendo
2;38-39, Matendo 9;17.19;2 Efeso 5;18 ni jambo lisilofaa mtu kuwa mwalimu,
muhubiri au mtumishi huku hajajazwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mafundisho
yoote mazuri na kukaa miguuni pa Yesu bado Aliwasisitiza wanafunzi wake
kutokuhubiri kwanza mpaka wamevikwa uwezo huu utokao juu Roho Mtakatifu
Luka 24;47-49 aidha ni muhimu ikumbukwe kuwa kujazwa Roho Mtakatifu sio
sababu ya kukufanya kichwa kivimbe kwa kiburi kusudi ni kutupa neema na nyenzo
tunazozihitaji kwa ajili ya kazi Matendo 3;12 siku hizi hata watu wa dini
wanajazwa Roho hivyo upentekoste sio issue ya kujivunia
- Lazima
uendelee kujifunza Biblia na kujisomea, Mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa
kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu Mathayo 4; 4.Inasikitisha kuona
kuwa watumishi wengi wa Mungu husoma neno la Mungu kwa sababu tu
anajiandaa kwenda kufundisha wengine, hii sio halali lazima ulisome neno
la Mungu kwa malengo na sio hovyo hovyo tu eti kwa kua unataka kufundisha
hapana.
- Biblia lazima isomwe kwa kumaanisha ikiwa umeitwa
na hii ndio huduma yako na unaishi kwa ajili ya Biblia basi huna budi kuisoma
kwa kumaanisha Neno la Mungu kwako liwe swala la kufa na kupona Lazima
ujifunze ujitoe kulisoma kuliishi na kulitegemea. Neno la Mungu ni upanga
wa Roho ni silaha ya pekee katika kumshida shetani (Efeso 6;10-17,Ebrania
4;12) Sasa kama silaha hii utaipuuzia ni rahisi kushindwa vibaya vitani ndo
maana haishangazi kuona watumishi wakishindwa leo.
- Lazima ulisome kwa moyo wa kutamani kujifunza na
kwa kupondeka Zaburi 119;20 Moyo uliopondeka unaotamani kujifunza uliojaa
shauku ya kumjua Mungu ni moyo ulio mwepesi kujua mapenzi na makusudi ya
Mungu Filipi 3;8-11 Moyo wa aina hii utakusaidia kujifunza na kuona hata
zaidi ya mipaka ya Dhehebu lako na theolojia yako. Roho wa Mungu
atakufundisha zaidi ya uyajuayo. Ubishi wa kimadhehebu umewafunga
watumishi wengi wa Mungu kumuwekea mipaka ya theolojia yao
na misingi yao
ya imani bila kufahamu kuwa Mungu hawezi kuwekwa katika kikombe Jifunze
hata kwa wengine.
- Biblia isomwe kwa kusudi la kujijenga kiroho, Wahubiri
wengi ukimuona anasoma neno ujue ana semina au anapaswa kuhubiri siku
Fulani huu ni ufisadi huko ni
kuwaibia watu ndugu yangu soma kwa kusudi la kujijenga kiroho wewe
mwenyewe kusoma kunakomaanishwa hapa si kwa ajili ya kutengeneza jumbe
kwani kujitoa kwako katika kujisomea neno kutakusaidia wewe kutengeneza jumbe pia hatuhitaji
kutoatu tunahitaji pia kupokea
- Soma Biblia kwa Mpangilio maalum Biblia ina vitabu
66 unapaswa kuisoma kwa mpangilio maalumu hatuwezi kukupa yoote lakini ni lazima ulenge kuisoma yenyewe
kwanza licha ya kusoma vitabu vitakavyoihusu biblia kusoma kwako kusiwe
kwenye mlengo mmoja tu soma kwa mpangilio utakaogusa agano la kale na
jipya kwa namna mbalimbali si lazima iwe kitabu kwa kitabu tu.
- Lazima
ujitoe katika Kuomba. Wengi tumesikia ule usemi usemao unaposoma neno la
Mungu Mungu huzungumza na wewe na unapoomba wewe unazungumza na Mungu ni
lazima tuwe na Muda na Mungu wa kwetu Binafsi tunahitaji maombi yetu
Binafsi, maombi na familia zetu, maombi na viongozi wa kanisa, maombi na
waalimu wa shule za jumapili maombi na watu wenye mahitaji n.k Pamoja na
yoote hapo maombi yako Binafsi ya sirini ni ya muhimu kwa shughuli zako za
kiroho na maisha yako.
- Lazima
ujifunze Kutafakari. Kutafakari ni fani iliyopotea kwa wakristo wengi na
watumishi pia hii ni kwa sababu ya uzembe, au uvivu au kutokupangilia au
kutokujua umuhimu au kutokuwa na Muda wa kufanya hivyo na kutoa kipaumbele
kwa mambo mengine. Lazima tuitafakari sheria ya Mungu (Zaburi 63; 6, 77;
12,143;5) Kutafakari sio swala la ndoto za mchana ni kuchukua muda wa
kukaa kimya na kuzama ndani kufikiri kile ambacho bwana anafundisha katika
neno lake, jinsi rehema zake zilivyo na kutaka kujua mengi kumuhusu.
- Lazima
uhakikishe unazaa matunda ya Roho Galatia 5; 22-23. Matunda ya roho ni
muhimu sana kwa watumishi wa Mungu haya ndiyo yanayodhihirisha kuwa
umekomaa kiroho matunda haya ni Upendo, Furaha, Amani, uvumilivu, utuwema,
fadhili, Uaminifu, upole, na kiasi. Inawezekana yakawa yako mengi zaidi ya
hayo lakini haya yanabeba mwelekeo mzima wa jinsi Mungu anavyotaka tuwe, Kwa
bahati mbaya wengi tumeshuhudia watumishi wengi wa Mungu wakiwa na
upungufu wa Matunda haya ya kiroho wengi sio waaminifu, wala hawana
uvumilivu wamejaa kiburi, ugomvi na hukumu dhidi ya wengine kwa ufupi yale
matendo ya mwili ndio hujidhihirisha kwao zaidi kuliko haya ya roho haipaswi kuwa hivi
ndugu zangu lazima Kristo aumbike ndani yetu Galatia 4;19, Watu ambao
Kristo hajaumbika ndani yao utaona matendo ya mwili yakidhihirika au
yakiwa ndani yao, ziko chuki, kuonea wivu huduma za wengine, uadui
kugombana, choyo, uhasama, wizi wa sadaka za waamini, kutokulipa zaka kwa
uaminifu, kupendelea watu ukabila kugombea ukubwa, taama za aina
mbalimbali hasira kali, kukosa uvumilivu, kufurahia shida na taabu za
wengine, kukomoa, kutoa adhabu kali kuliko kawaida na bila rehema kukosa
uvumilivu, hakuna upendo, ulafi kukomoana, kuweko na makundimakundi
faraka. tamaa za zinaa na uangaliaji wa picha za ngono, na mambo kadha wa
kadhaa Hizi ni hali zinazoonekana wazi leo kwa watumishi, Huku wengi
wakiwa wameridhika na pale walipo wakiwa hawana tena juhudi ya
kujiendeleza Kiroho hivyo wengi wamedumaa huku wakiwataka washirika wakue
Kiroho na kuwa kama Kristo huku wenyewe biashara imetushinda hali kama
hizi zisipofanyiwa marekebisho Hatuwezi kuujenga Mwili wa Kristo leo
Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake.
C:
Umuhimu wa Kujiendeleza Kielimu
Kujiendeleza kielimu ni moja ya
sehemu muhimu katika maandalizi kwa ajili ya huduma, ninaweza kusema kuwa elimu
ni ya lazima katika kumtayarisha mtu kwa ajili ya huduma hii inamaanisha kujizoeza kwa maarifa,nah ii
inamaanisha kuwa lazima uende shule kila mtu anayetaka kumtumikia mungu lazima
awe na elimu ya kutosha au apate ujuzi mwingi kadiri iwezekanavyo watu
humdharau mtu asiye na elimu na humuheshimu mtu mwenye elimu “Elimu huleta
ubaguzi wa halali” elimu itakusaidia katika kuilewa Biblia na kuwasilisha
ujumbe unaoukusudia kwa lugha inayoweza kueleweka na kukubalika Biblia
inaonyesha kuwa Mungu aliwatumia sana watu waliokuwa na elimu Musa Matendo
7;22,Daniel Daniel 1;4,17-20 na Paulo mtume 1Koritho 1;26-29.2;1-4,Wakolosi
1;9. Hta hivyo wenye elimu hawapaswi kujivunia elimu zao na kuwa na kiburi 1
Koritho 8;1-2, 1; 26-31 hata hivyo maarifa yaliyowekwa wakfu kwa ajili ya Mungu
ni yenye faida kubwa kuliko ujinga.
§
Elimu ya kawaida pia ni ya muhimu kwa kazi ya
Huduma John Wesley aliwaambia wahudumu vijana aliokuwa akiwafundisha kuwa
wasome au waache huduma ukweli ni kuwa aliona umuhimu wa kuwa na elimu na
uhusiano wa kufanya vizuri katika mambo ya kiroho Mchungaji asiyesoma
anafananishwa na gari lisilo na mafuta hutafika mbali.
§
Soma kwa malengo ya kupanua ufahamu,Mchungaji
unapaswa kufahamu mambo mengi ,wsoma kwa lengo la kuwa na ujuzi wa mambo
meni,Soma kwa lengo la kuwa na ujuzi wa mambo yanayoendelea Information huwezi
kuishi kama kisiwa tu maalbino wanauawa wewe hujui hata ni kwa nini wanauawa
lazima upate taarifa kumbuka Elimu tunayoizungumzia hapa sio tu ya kukaa
darasani lakini pia ya kujifunza wewe binafsi
§
Mchungaji anapaswa asome nini? Kuna mambo mengi
na taarifa nyingi sana duniani ambazo huwezi kuzipitia zote kulingana na
muda hivyo kanuni inapaswa kuwa lazima
uchague Be selective,Unahitaji kusoma na kusikiliza taarifa za habari na mambo
yahusuyo ulimwengu na mambo ya muhimu,
Soma vitabu mbalimbali vinavyohusu
maisha ,Historia, Sayansi Jiografia nk. Sio lazima yale unayosoma ya we ya Kiroho
tu hapana lakini soma mambo yatakayokufanya uwe na ujuzi fulanifulani kuhusu
ulimwengu na shughulishughuli zinazoendelea
§
Mchungaji lazima uwe mtu unayefundishika msingi
wa yote tunayoyazungumza hapo juu ni kuwa na moyo wa kufundishika kuna vyanzo
vingi vinavyoweza kutusaidia kujifunza na unaweza kujifunza hata kutoka kwa
mwendawazimu wako watu wengine kila wanacho kiona wanakikosoa tu ukiwa tayari
kusikiliza hata kwa mwendawazimu unaweza kujifunza kitu Samsoni alitoa asali
katika mzoga wa simba (Waamuzi 14;8-9). Nyuki wana tabia ya kuingia kila mahali
kuokoteza hata chooni lakini baadaye hutengeneza kitu kitamu sana yaani asali
wako watu wengine hawapendi kujifunza kutoka kwa wengine na matokeo yake
hawafanikiwi katika huduma zao.
UMUHIMU
WA MCHUNGAJI KUWA NA MAKTABA
Mchungaji
kuwa na vitabu ni jambo la muhimu usitegemee mafunuo tu mafunuo ya kweli na
halisi huja pia kwa kujifunza kutoka kwa wengine Paulo mtume aliheshimu sana
vitabu ingawa alikuwa ameketi chini ya waalimu maarufu walioheshimika sana
wakati ule kama Gamaliel,Alikuwa na uzoefu katika huduma kwa miaka ipatayo 30
hivi na alikuwa na mafunuo makubwa hata kupelekwa katika mbingu ya tatu lakini
bado alithamini vitabu angalia 2Timotheo 4;13 zaidi ya yote anamsihi Timotheo
kuwa afanye bidii katika kusoma 1Timotheo 4;13 mwana falsafa mmoja alisema
huyuni Edward Gibson “ ni afadhali niwe
masikini lakini mwenye moyo wa kupenda kusoma vitabu kuliko kuwa mfalme asiye
na moyo huo” kwa bahati mbaya sisi watu weusi hatuna tabia ya kupenda
kujisomea hata wazungu wametugundua na wana usemi usemao ukitaka kumficha kitu
mwafrika kiweke kitabuni. Muhubiri mashuhuri aliyeleta uamsho mkubwa Marekani
Jonathan Edwards alikusanya maarifa yoote kuhusu Mungu ambayo yangeweza
kumsaidia kupata maarifa kumhusu na kwa kweli kadiri alivyosoma ndivyo
alivyoandika amekuwa mfano wa kuigwa wa wachungaji na wahubiri ambaye alikuwa
na huduma kubwa kwa ajili ya upenzi wake wavitabu na kujisomea na kuwa na
maktaba kubwa
MAKTABA YA
MCHUNGAJI;
Mchungaji lazima uwe na maktaba yenye vitabu vya aina mbalimbali hata
hivyo kuna vitabu ambavyo tunavipa kipaumbele kama
vitabu vya msingi amabvyo sitarajii vikosekane katika maktaba ya mchungaji
Yeyote
- Biblia.
Biblia ni lazima ipewe
kipaumbele cha kwanza kuwepo katika maktaba ya kichungaji hata hivyo
haitoshi kuwa na biblia ya aina moja tu
lazima uwe na biblia za tafasiri tofautitofauti tangu King James
Version ilipotafasiriwa mwaka 1611
hata leo kuna zaidi ya tafasiri 500 za kiingereza peke yake na ni
vigumu kuelezea ipi ni nzuri hivyo ni muhimu kwa mchungaji kuwa na Biblia
za matoleo tofauti tofauti hata ya wale wa imani potofu na pia Biblia
zenye mafunzo Studies Bibles kwa bahati mbaya Nyingi ni za kiingereza.
- Kamusi
za biblia na kamusi za kawaida (Dictionaries)
Ni muhimu kuwa nazo si utahitaji kujua maana ya baadhi ya maneno ya
kawaida katika Lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili na kadhalika pia
utahitaji kujua historia ya neno Fulani katika biblia na hata maana yaeke
Bila kamusi za biblia utafahamuje hayo pia inasikitisha kuwa mpaka sasa
hatuna kamusi za Biblia za Kiswahili zaidi ya zile za Don Fleming hii ni aibu kwa wasomi wa Tanzania
kushindwa hata kutafasiri zile za kiingereza katika Kiswahili zikasaidia
watu watu wako na shughuli kasha unajiita Msomi mimi Bwana ameniagiza kuandika
Commentary ya Kiswahili na shughuli ya kuitengeneza inaendelea.
- Itifaki
(Concordance) Hiki ni kitabu
kinachosaidia katika utafutaji wa andiko Fulani badala ya kuchukua Muda
mrefu kutafuta katika Biblia itifaki inasaidia kulipata andiko kwa wepesi
katika kiswahili iko moja tu na inasemekana iliandikwa na walutheri
wapentekoste mpaka leo tumelala. Za kiingereza ziko nyingi lakini iliyo
nuri zaidi ni NIV Exhaustive Concordance of the Bible na Strongs hizo ni
nzuri sana
- Vitabu
vya mchanganuo mbalimbali ya maandiko Commenteries
Hizi nazo ziko za aina kuu mbili kitabu kimoja cha mchanganuo wa maandiko
ambavyo mara nyingi ni nafuu lakini vinachanganua kifupi sana vingine
vinavyochanganua kirefu vinakuwa ni mlolongo wa vitabu amabavyo kwakweli
ni gharama kununua kimoja kimoja na kwa bahati mbaya katika Kiswahili
tunayo moja tu ya bwana Don Fleming wa kanisa la biblia ambayo
imetafasiriwa Commentaries nyingi ni za kiingereza inasikitisha kukosekana
kwa Kiswahili niombee kwani Bwana amenipa mzigo wa kuandika katika
kiwswahili hivyo Kumbuka Mchungaji Innocent kamote katika maombi yako ili
nifanye hivyo kwa utukufu wake.
- Vitabu
vingine ambavyo sio vya Msingi bali vinapewa kipaumbele cha pili ni pamoja
na vitabu vya kitheolojia, kuna vitabu vingi sana vya kitheolojia lakini
vingi ni vya kiingereza, Vitabu vinavytoa maelezo kuhusu Biblia yaani
Bible Introduction, vitabu vinavyohusu historia ya kanisa , Israel na
vinginevyo
- Vitabu
vingine ni kama maarifa ya mchungaji,
namna ya kuhubiri namna ya kutumia maandiko kwa halali, utunzi wa hutuba
za kibiblia na mwisho vitabu vinginevyo vya kawaida.
MCHUNGAJI NA
ELIMU YA CHUO CHA BIBLIA.
Kadiri
muda unavyokwenda ndivyo changamoto zinavyoongezeka zamani masomo ya wachungaji
yaligusia tu maswala ya Biblia na huduma za kikanisa aidha na theolojia kidogo
lakini kadiri siku zinavyokwenda umuhimu wa elimu nao umeongezeka yako makundi
ya vijana yanayohitaji uangalizi maalumu, maswala ya muziki,maswala
yanayohusiana na ushauri nasaha Counceling ambayo kwa kweli ni huduma kamili na
inahitaji taaluma,maswala ya miradi,Vyombo vya habari na television, magazeti,
redio maongozi ya kifedha usimamizi wa kitaaluma n.k haya yote yanahitaji
kusoma na sio mafunuo tu.
Hitaji la
Elimu ya kichungaji limekaziwa katika maandiko Paulo anapoweka wazi kuwa kazi
ya mchungaji na mwalimu ni kuwaandaa watu wa Mungu hata kazi ya huduma itendeke
na mwili wa Kristo ujengwe ni lazima sisi wenyewe tuwe tumeandaliwa kwa kazi
hiyo ya huduma na elimu ndiyo inayoweza kufanikisha jambo hilo
Inashangaza kuona jinsi watu wanavyoiponda elimu ya
vyuo vya biblia lakini wenyewe wanataka kufundisha makanisani mwao unawezaje
kufundisha huku wewe hujajifunza? 2Timotheo 2;2 ni msingi unaosisitiza umuhimu
wa kujifunza kwa asili Vyuo vya biblia vilianzishwa wakati wa Nabii Samuel
ambaye alikuwa na vyuo vya wana wa manabii 1Samuel 10;5-6, na baadaye tunaona
Eliya akiwa anaendesha shule hii ya wana wa manabii 2Wafalme 2;3-7 hivyo
manabii walikuwa na shule zao maalumu
zilizokuwa zikiwandaa kwa huduma za kinabii Itashangaza sana kuona watu wa leo
wakipinga swala zima la watu kwenda vyuo vya biblia yako mambo mengi ambayo
kadiri tutakavyojifunza utaona kuwa kunahitajika elimu au utaalamu katika hilo
mfano namna ya kutafasiri maandiko lakini kwa kufupisha nataka kusisistiza tu
umuhimu wa mchungaji kupitia vyuo vya Biblia na semina mbalimbali.
Huduma
ya kichungaji ni huduma ya wito lakini ina viwango ambavyo kwavyo Mungu
ameviweka akikusudia kuwa tunapaswa kuwa navyo 1Timotheo 3; 2-5. Basi imempasa
Askofu awe mtu asiyelaumika; Mume wa mke mmoja mwenye kiasi na Busara mtu wa
utaratibu, Mkaribishaji ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga
watubali awe mpole, si mtu wa kujadiliana wala asiwe mwenye kupenda fedha, mwenye
kuisimamia nyumba yake vema ajuaye kutiisha watoto wake katika ustahivu (Yaani
mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)
Wala asiwe mtu aliyeongoka hivi karibuni asije akajivuna akaangukia katika
hukumu ya ibilisi, Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu woote walio nje ili
asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. Mistari hiyo hapo juu inaweka
mpango wa kiwango ambacho Mungu anakikusudia kwetu kama watumishi kukifikia
katika Eneo hili tutaangalia mahusiano ya mchungaji na familia yake ikiwa ni pamoja
na ndoa na wajibu wa mama mchungaji hali kadhalika mchungaji kama Mume, baba nyumbani na mtunzaji wa familia
haya yana mchango mkubwa sana katika huduma ya kichungaji na maisha ya utumishi
kwa ujumla viwango alivyoweka Mungu vinahitaji neema yake kuvifikia na penginepo
Mungu ameviweka ili tuone mapungufu tuliyonayo ili tusiwe wenye kuhukumu
wengine na badala yake tutambue mapungufu yetu tukijijua kuwa na sisi tunao
wajibu wa kutimiza pamoja na kuwa tunalisimamia kanisa la Mungu.
A: UMUHIMU WA NDOA ILIYO BORA KATIKA
UTUMISHI
Kama kuna jambo lililo la muhimu sana katika
utumishi ni ndoa na hasa ndoa iliyo bora, mahusiano ya ndoa kati ya mume na mke
yanakwenda moja kwa moja katika muda wa wanandoa hao walipoanza mahusiano
yao walipo pendana na kuchaguana hili
linapendeza sana Hata hivyo uchaguzi wa mke kwa Mchungaji ni swala la muhimu
zaidi linalohitaji umakini zaidi kwa ufupi maongozi ya kimungu (Mithali
19;14,31;10-12) woote tunajua umuhimu wa ndoa na woote tunajua mpango wa Mungu
kuhusu ndoa (Mwanzo 2;18, Mathayo 19;4-6) hatuwezi kujenga hoja katika namna
watu wanavyopata wake zao kwa sabbabu ya tamaduni tofauti lakini Mungu
alikusudia mwana ndoa awe Msaidizi mwenye kufaa, awe mwenzi wako na muwe na
umoja hii ni muhimu kwa kuwa ndoa hutoa
uponyaji wa kisaikolojia na kimwili, Mchungaji yeyote anayeweza kuwa na ndoa
iliyo bora ana nafasi ya kuwa kuwa mchungaji bora, ndoa yako na watoto wako
wana mchango mkubwa katika huduma yako Lakini zaidi sana uhusiano wako wa
kindoa na mumeo au mkeo una uwezo wa
kustawisha huduma na kuwa mfano wa kuigwa katika kanisa au huduma ambayo Bwana
amekupa kusimamia kwa maana nyingine ndoa mbovu inaharibu huduma na inashusha
heshima inayoonyesha una uwezo wa kusimamia familia nyingine na ndoa nyingine
ambazo Mungu amekupa kuzisimamia
Uchungaji wetu unaanzia katika ndoa zetu na
familia zetu wako wahubiri wengine wana sura mbili sura aliyonayo nyumbani ni
tofauti na sura aliyonayo kanisani wana familia lazima wamuone mchungaji kama
baba wa kiroho zaidi ya jinsi kanisa litakavyomuona.
B; WAJIBU WA
MAMA MCHUNGAJI.
Mama mchungaji ana wajibu mkubwa sana
katika maisha na huduma ya mumewe kule kukubali kuolewa na mchungaji lazima
kuambatane na kukubali au kuheshimu kuwa mtu huyo ameitwa na Mungu kwa kufanya
hivyo hata yeye ataishi maisha ya Furaha na amani kwa kuruhusu mapenzi ya Mungu
katika maisha yao. Mama Mchungaji lazima awe na ujuzi binafsi kuhusu Mungu na
awe na hekima itakayo muongoza yeye na mumewe pamoja na kazi ya Mungu
Kuwa mama
mchungaji si kazi rahisi kama tunavyofikiri wengi wameua huduma nzuri tu za
waume zao na wengi wamekuwa si mfano mzuri wa kuigwa wakati mwingine
wamechukiwa na washirika kwa kuwa vile walivyowategemea wawe sivyo wenyewe
walivyo Mchungaji anaweza kumsaidia mkewe kwa kumruhusu kuhudhuria semina
mbalimbali, kumnunulia baadhi ya vitabu au kumtafutia mwanamke mtumishi
anayefanya vizuri na aliyekomaa kiroho anayeweza kumsaidia lakini lazima nao
wawe wenye moyo uliopondeka wako mama wachungaji ambao hawafundishiki ni lazima
wawe na ujuzi katika neno na mapambano kwa kweli wawe hodari katika vita vya
utumishi wajue kuwa adui atapenda kuwatumia wao kama mlango wa kusambaratisha
huduma za waume zao Biblia imejaa mifano ya wanawake walioruhusu kutumiwa na
adui au kuwa kinyume na imani za waume zao hapa nitakupa mifano minne tu
- Hawa
aliweza kutumika kama mlango wa kuingiza
dhambi ulimwenguni Mwanzo 3;6.
- Mke
wa Ayubu alitumiwa kuwa kinyume cha imani ya mumewe Ayubu Ayubu 2;9-10
- Mke
wa Lutu inaonekana alipendezwa na maisha ya Sodoma na tabia zile kiasi cha
kutothamini wokovu waliopewa na kuamuriwa
kutokuangalia nyuma Mwanzo 19;26
- Mke
wa Manoa alikuwa na imani kwa Mungu akamtia moyo mumewe aliyekuwa na hofu
kuwa Mungu angewaua na walibarikiwa kumpata mtoto Samson Waamuzi 13; 2, 23.
Kwa msingi
huu mke wa Mchungaji anaweza kuwa Baraka au kusababisha matatizo katika huduma
ya mumewe, Mwanamke na atimize kila lililowajibu wake katika ndoa ikiwa ni
pamoja na kumtosheleza mumewe katika Tendo la ndoa Mwanamke mpumbavu huibomoa
nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe Mithali 14;1 ni maombi yangu kuwa Mungu
atawasaidia mama wachungaji kufahamu wajibu wao na kuhakikisha wanatunza zawadi
zile ambazo Mungu amezitoa kwa kanisa lake watumishi yaani hawa aliowatenga kwa ajili ya kazi yake
katika kanisa.
WAJIBU WA
MAMA MCHUNGAJI NYUMBANI
Jukumu la
kwanza la mke wa mchungaji ni Nyumbani kwake, Mchungaji na familia yake hata
wasipopenda lakini jamii itajua tu kuwa ni wapi mchungaji anaishi na
wataiangalia nyumba yake kama kielelezo kwa msingi huo watu wanatarajia nyumba
ya mchungaji kuwa mfano wa kuigwa na familia yake pia inapaswa kuwa mfano wa
kuigwa, na kama jamii haijawahi kuona familia ya Kikristo basi kwa mchungaji
ndipo patakuwa mfano. Lazima nyumba hiyo iwe safi vitu vikae katika mpangilio, ukaribishaji
uwe lugha nzuri ya mama na kujiamini wako wengine wanapoona wageni ndio huanza
kuwauliza waume zao nini cha kufanya kwakuwaita pembeni mbele ya wageni hii sio
tabia nzuri mama lazima ajiamini na kujifunza kumtegemea Mungu tabia ya choyo
ni mbaya sana kwa wakristo lakini ni mbaya zaidi ikiwa kwa mama mchungaji
majukumu ya kikanisa na kijamii yapewe nafasi ya pili ya kwanza ni nyumbani kwa
mchungaji
WAJIBU WA MAMA MCHUNGAJI KANISANI.
Mama mchungaji
hapaswi kuwa na vyeo vingi sana kanisani kule kuwa mama mchungaji tu tayari ni
wajibu mkubwa wa kutosha vinginevyo hataweza kukamilisha majukumu yote
atakayopewa na itakuwa lawama anaweza kufanya hivyo pale huduma inapokuwa
changa lakini majukumu yapungue kadiri wanavyopatikana watu wa kushika nafasi
hizo
- Mama mchungaji anaweza kukubali kwa
hekima nafasi kadhaa kama kuhubiri na kufundisha n.k kwa kuonyesha mfano
kwa wanawake wengine namna wanavyopaswa kutumika maana wengine usipotumika
kabisa inakuwa kero mbona yeye hatuoni akifanya
- Mama mchungaji anaweza kusaidia
katika kazi za madhabahuni wakati wa maombezi na ushauri pia akumbuke kuwa
ana nafasi kubwa katika kufundisha wanawake mabinti na vijana, wajane au
hata shule za jumapili. n.k
- Mama mchungaji lazima awe mtii kwa
mumewe na mtetezi wa mumewe na mlinzi wa mumewe unapaswa kumsaidia katika
kujua namna ya kuhubiri vizuri kwani una nafasi ya kumkosoa mumeo kwa
upendo na kupokea watu wanasema nini hivyo hakikisha unafanya kwa
ustaarabu.
- Mama mchungaji hatakiwi kuwa mmbeya
na mchonganishi wala hatakiwi kuwa na wivu mchungaji ni kiongozi wa jamii
na watu watapenda kumsogelea hata wa jinsia tofauti hivyo homa ya wivu wa
mama mchungaji haitakiwi kuwa juu muamini mumeo,Vumilia magumu na mapito
pamoja na mumeo
WAJIBU WA
MAMA MCHUNGAJI KWA MUMEWE
Kazi ya
kichungaji ni kazi ngumu yenye migandamizo mingi mama mchungaji anapaswa kuwa
mwenye kumtia moyo mumewe wakati wa kukata tamaa
Mama
mchungaji asaidie kutunza siri za washirika ambazo washirika watakuwa
wakiwaeleza mambo ya ndani wanayokutana nayo bahati mbaya wako wanawake ambao
ili waonekane wanajua mambo hupenda kuelezea vitu vya ndani vya washirika hii
itaharibu watu kuwa wazi kwenu tunza siri anazokupa mumeo kwa faida ya kanisa
kama amekueleza. Kwa kuwa mke mwema mama mchungaji ataweza kusababisha faida
nyingi baadhi ni hizi zifuatazo;-
- Atasaidia
watu wengine wanaojiandaa kuoa
- Atasaidia
watu wanaokuja kupata ushauri wa matatizo ya ndoa na kuleta ufumbuzi wa
matatizo yao
- Atawafanya
watu waige mfano wa ndoa yake na kuizungumzia kama
mfano
- Mungu
atakutana na mahitaji yake kusudi aweze kuwa mchango mzuri kwa jamii ambayo
Mungu amewaita kuitumikia kwa kweli Mungu atakubarikia.
C: Wajibu wa mchungaji kama mume baba na mtunzaji
wa Familia
- Kama Mume
Huduma ya kichungaji kwa mtumishi tunaweza kusema
kwa kiasi fulani kuwa imefanikiwa pale Mchungaji anapofanikiwa pia kuwa Baba mzuri
na Mume mzuri, kama familia ya mchungaji imefanikiwa kuishi kwa viwango
vinavyokusudiwa utaaminika zaidi katika kazi hii ya utumishi. Mchungaji
anapaswa kuonyesha upendo wa dhati kwa familia yake ingawaje waafrika wakiona
unampenda sana mkeo watasema unajidai Lakini Biblia imeagiza hivyo utaonyeshaje
kuwa unampenda mkeo Biblia imetoa namna unavyoweza kuonyesha kujali na kumpenda
mkeo
- Ishi
nae kwa akili onyesha kumuheshimu na kumuhesabu kama zawadi ya Mungu kwa
ajili yako na kwa kufanya hivyo dua zenu au dua zako zitasikiwa 1Petro 3;7
ingawaje kila mwanamke anastahili kuheshimiwa kujaliwa na kupendwa sana
kwa mke wa mchungaji inatakiwa izidi.
- Uwe
mwaminifu kwake ndoa ni uhusiano wa watu wawili wanaofanya muungano wa mwili
mmoja mtu mke na mtu mume Mwanzo 2;24
kwa kuwa mchungaji ni mtu maarufu kwa cheo alicho nacho wanawake
wengi huvutiwa na wachungaji na watajaribu kuvuta hisia zako kwao, wanawake
wanamuona mchungaji kama mwanaume wa pekee sana kwao ambao wao hawana kwa
hivyo kule tu kuwa mchungaji kunayafanya maisha yako yawe hatarini
mchungaji atajilinda mwenyewe kwa kuruhusu watu wajue kuwa unampenda mkeo
ufa wowote utakaogunduliwa na jamii kati yenu unaweza kuwa mwanya wa
mapinduzi katika ndoa yako na utaharibu huduma Mungu aliyoweka ndani yako.
- Mlee
mkeo kiroho, Kuweni na muda wenu binafsi wa kujitoa pamoja kwa Bwana katika maombi au kujisomea neno
au ibada mambo haya ni muhimu kwa kila mshirika lakini ni muhimu sana kwa
kila mchungaji, Wachungaji wengi wanaweza kuwa na maombi binafsi asubuhi
na hata kujisomea neno huku wake zao wakiwa katika shughuli za kuandaa
chai, kuandaa watoto kwenda shule au kufanya usafi hili linatufanya
kutofautiana nao sana kiroho, kama unampenda mkeo lazima ujenge tabia ya
kuwa na maombi ya pamoja na kutomuacha mbali kiroho wewe ni muhudumu mkuu
wa mkeo kiroho pia
- Kama Baba
Watoto wanatolewa kama zawadi kwa wazazi lakini pia Mungu ametuamini kwa kutupa watoto
na hivyo tunawajibika kuwatolea hesabu, Kwa ujumla wao hawachagui kuzaliwa
katika ulimwengu huu lakini wanazaliwa na wanatupa jukumu na wajibu wa maisha
yao, na maadili na hata umilele wao kwa msingi huu basi kunachangamoto katika
swala zima la malezi na jinsi mnavyojitawala
- Kuwa
mwangalifu unavyochukuliana na mkeo Hili ni jambo la msingi sana watoto
wataanza kujifunza upendo na ukristo wa
kweli kulingana na namna unavyochukuliana na mkeo hili lisipoangaliwa vema litapandikiza
mbegu nzuri au isiyo nzuri kwa watoto hivyo ninyi wenyewe muwe kielelezo
Mchungaji uko wakati utashughulika na mkeo katika maswala ya kutiana
nidhamu sio ngumi lakini watoto wasijue kinachoendelea
- Mchungaji
ni kiongozi kuanzia nyumbani uko wakati ambapo itakubidi kutumia mamlaka
kutiisha nidhamu kwa watoto na kuwaonyesha moyo wa kichungaji inahitajika
neema ya Mungu kwani kushindwa kuwasimamia wanyumbani mwako ni kushindwa
kulisimamia kanisa tutake tusitake.
- Nidhamu
ni lazima nyumbani wakati mwingine itakupasa kuchapa kama
biblia isemavyo Mithali 13;24,19;18 na 23;13 huku ni kufundisha sawa na neno
Displina la kilatini ambalo
maana yake ni kufundisha Efeso 6;4
- Malezi
ya kiroho ni muhimu na kuwapa watoto elimu iliyo bora ni vizuri wakisoma
shule nzuri na uwasimamie katika swala zima la kiroho na elimu. Pia
tuhakikishe kuwa tunapatikana nyumbani na kuwa na muda na watoto baadhi ya
watoto wa wachungaji walihojiwa na hivi ndivyo walivyosema
Ø
Ninamuona baba kwa nadra sana na wakati mwingine ni vigumu kumuona
Ø
Babaangu anakuwa safarini kila wakati alisema
atabadilika lakini hajabadilika bado
Ø
Wazazi wangu wanaona huduma yao kuwa ni ya muhimu kuliko sisi na kwa kweli ndivyo wanavyosema
Ø Wanaamini huduma yao ni muhimu kuliko sisi
Ø Wanafikiri kuwa maisha yao ni ya kutumika
tu na kutokatoka
Ø
Hawana hata muda wa kukagua madaftari yetu
Hizo ni baadhi ya lawama zitokanazo na watoto wa wa
wachungaji kwa sababu ya tabia zetu nyumbani zinazoathiriwa na huduma.
- Kama mtunzaji wa Familia.
Pamoja na majukumu yote ya kichungaji waliyonayo
watumishi, bado mchungaji ana wajibu wa kuitunza familia yake, Familia ni ya
muhimu sana.
Wewe ni shahidi kuwa wako watumishi ambao wamelazimika kuacha huduma kwa sababu
tu ya kutafuta kuzitunza familia zao na wako pia ambao wanalazimika kubaki
katika huduma ambazo labda wangeziacha lakini kwa sababu ya maswala ya kifedha
hawataki kutoka vyovyote iwavyo Mchungaji anapaswa kuitunza familia yake.
Biblia
hailaumu kuwa Fedha ni mbaya lakini ile tabia ya kupenda fedha zaidi ndio ovu
1Timotheo 6; 10. Kupenda fedha kwa namna hiyo ni kuabudu miungu Kolosai 3; 5, na
Efeso 5;5 1Yohana 2;15, moja ya migogoro mikubwa kabisa katika nyumba nyingi ni
maswala ya kifedha, Malalamiko ya mama mchungaji kuhusu maswala ya Fedha
nyumbani yanaweza kupandikizia watoto tabia ya kuchukia huduma wakijua kuwa
inachangia katika hali ya ukata waliyonayo, wanafamilia woote akiwemo mama
wanapaswa kuridhika na kuishi maisha yaliyo sawa na kiwango cha mapato yao.
Familia ya mchungaji iishi kwa bajeti inayolingana na mapato yao na ni lazima
wawe na akiba au kutafuta namna ya kuwa na fedha za tahadhari badala ya kuishi
kwa mikopo jambo linalopelekea wengine kukimbia huduma kwa aibu na wingi wa
madeni, Wakati mwingine italazimu mama mchungaji afanye kazi zitakazoingiza
kipato au hata mchungaji wakati anapoanza huduma anaweza aweza kufanya kazi za
kumuingizia kipato ili kuitunza familia
UHUSIANO WA MCHUNGAJI NA JAMII
A; Uraia wa
aina mbili.
Ni ukweli
unaokubalika kuwa injili sio tu inabadilisha tabia na kumuokoa mtu bali pia
inabadilisha uhusiano wake yaani akiwa raia halali na mkazi wa ulimwengu
hatawaliwi tu na sheria za ulimwengu huu, lakini ana uraia mpya na anaishi sawa
na sheria za nchi mpya za utawala wa Bwana Yesu Kristo
Uhusiano na
Mungu
Mchungaji ni mtumwa katika uhusiano wake na Mungu Mathayo 24; 45. Mungu
ametuita ili tuwe wafanyakazi pamoja na Yeye 1Koritho 3;9,2Wakoritho
5;17,Galatia 6;15,Efeso 4;24 na kolosai 3;10 watumishi ni mawakili wa siri za Mungu
Efeso 3;8-9 mtumishi anapaswa kuendelea
kudumisha uhusiano wake na Mungu Yeye ametuamini na ametupa injili 1Koritho 2;4
watumishi ni makuhani kwa ajili ya watu wa Mungu 1Petro 2;9 na ni walinzi
Ezekiel 3;17;18.
Uhusiano na
Bwana Yesu.
Mchungaji anapaswa kuwa na uhusiano wa kudumu chini ya Yesu ambaye ni
Mchungaji mkuu 1Petro 5;2-4,Matendo 20;28. Kondoo ni mali ya Yesu hivyo ni
wajibu wa Mchungaji kuwalisha kuwatunza na kuhakikisha anazalisha Warumi
6;1-23, Kolosai 3;1-25. ni Lazima tufanye kazi hii kama Kristo atakavyo na
kuiga mfano wake tukitafuta kufanya
mapenzi yake siku zote za huduma.
Uhusiano na
kanisa lako
Mchungaji ni mwangalizi wa mioyo ya wakristo Waebrania 13;17 hatuna budi
kulipenda kanisa na kulilinda na mbwa mwitu na kuwasaidia woote wanaojikwaa na
kuanguka Ezekiel 34;4, hakikisha kuwa unahusika vema na maisha na matatizo ya
watu uliopewa kuwachunga fanyika msaada mkubwa kwao wafundishe, wahurumie,
furahia maendeleo yao walinde ishi nao kama ndugu, Baba, kaka n.k aidha mchungaji kanisani wewe ni kiongozi
waongoze watu uwe na utawala bora watu hawawezi kufanya mambo bila kuongozwa
mfano mwema ukiwa ni uongozi katika familia yako 1Timotheo 3;4-5 ongoza wewe
ukiwa ndiye mfano mwema Wafilipi 3;17, 1Timotheo1;16 Ishi vizuri na wazee wako
wa kanisa kwa upendo na urafiki.
B; Uhusiano
wako na madhehebu mengine
Katika hali isiyo ya kawaida udhehebu
ni jambo linalochukua mioyo ya wengi hata kufikia hatua ya wengine kujifikiri
kuwa huenda wao ndio bora zaidi kuliko wengine, Mapema sana katika huduma ya
maisha ya Kristo mtu mwengine asiyeambatana na wanafunzi wa Yesu lakini huenda
aliwahi kuhudhuria baadhi ya mikutano ya mafundisho ya Yesu alikuwa akifanyia
kazi kile alichofundisha na kutoa pepo kwa jina la Yesu na wanafunzi wa Yesu
walitaka mtu huyo azuiliwe Marko 9; 39-40. ni muhimu kufahamu kuwa yako
madhehebu na vikundi ambavyo vyaweza kuwa tofauti na ulivyo vizoea lakini wako
kazini na wanaifanya kazi ya Mungu vilevile.
Umuhimu wa kuheshimu utendaji katika mwili
wa Kristo
Moja ya baraka kubwa ya kuwa katika mwili
wa Kristo ni kutambua kuwa utendaji wa Mwili wa Kristo ni mpana sana zaidi ya
kanisa lako la mahali pamoja ni lazima ujue kuwa madhehebu na mashirika
mbalimbali yanayohubiri injili ni mwili wa Kristo ni viungo vinavyofanya kazi
mbalimbali katika mwili wa Kristo yaani kanisa (1Koritho 12;13) hivyo kuna
umuhimu wa kutambua kuwa wengine wako pamoja nasi badala ya kugombana nao na
kijifikiri kuwa ninyi ndo wenyewe au ndo bora kuliko wengine hii sio tabia ya
Kristo. Yeye alituombea tuwe na umoja (Yohana 17;11,21-23.).
Mambo ya kuzingatia
Pamoja na kuwa mwili wa Kristo ni mmoja
tunapaswa kuwa na tahadhari dhidi ya imani potofu hivyo tunashirikiana bila
kushiriki katika imani zilizo tofauti na tunavyoiamini Biblia kwa mfano
- Chunguza kama kuna mafundisho
yasiyoendana na biblia ili ujue wanaamini nini na wanapelekaje injili.
- Chunguza
namna wanavyotumia fedha au mapangilio wa mapato na matumizi ya fedha
- Angalia
mpango wao katika ushauri, maombi na namna wanavyofuatilia washirika au
wanavyowapata.
- Kama
humjui kiongozi wa kundi hilo jaribu
kutafuta taarifa kwa viongozi wako au wachungaji wengine siku zote watu
wazuri huweka wazi mipango yao
ya injili bila kificho
- Unapogundua
kuwa ziko tofauti na zinatokana na ufahamu tu kutoka katika maandiko au
tamaduni zisizo na athari kubwa sana katika ukristo usisite kuwaheshimu
wengine hatuhitaji sana kufanana katika kila kitu jambo la msingi si namna
mtu anavyoabudu bali nani tunamwabudu, Mchungaji aliyekomaa hilo jaliwezi
kumsumbua.
Kuibuka Kwa
Madhehebu Kama Uyoga
Kuibuka
kwa madhehebu ni jambo la kawaida ambalo watu watalishuhudia kaatika nyakati za
leo, Madhehebu ni vikundi vya kidini
vilivyoungana au vinavyojenga kundi moja lenye
uongozi,mapokeo,mafundisho,uzoefu na mikazo Fulani ingawa madhehebu hayo
hayawezi kudai kuwa wao ni kanisa pekee la kweli lakini wanaweza kufikiri kuwa wao pekee ndio
wanawasiliswha ile kweli vizuri madhehebu mingine yana misimamo mikali na
mengine misimamo ya wastani baadhi ya wakristo wanachukizwa na madhehebu titiri
lakini wengine wako tayari kuyafia madhehebu yao, Nini sababu ya kuweko kwa
utitiri huu wa madhehebu ziko sababu kadhaa
- Madhehebu
mengi yalitokea wakati mwingine kwa sababu ya Kulinda usafi wa
kimafundisho hii hutokana na pale inapoonekana kuwa uchafu unaruhusiwa
katika kanisa tofauti na msingi uliokusudiwa ndipo baadhi ya watu
wanaotaka kulinda usafi wa mafundisho hutoka na kuanzisha dhehebu jipya
hawa wako sawa na Yuda 1;3.
- Sababu
za kimaongozi haya ni madhehebu
yanayotokana na maongozi zaidi kuliko mafundisho Labda yuko kiongozi
anayependwa na baadhi ya watu na inaonekana baadhi hawamkubali katika
hitilafu Fulani wale wanaoonekana kuonewa huweza kuamua kutoka na kiongozi
wampendaye kwa hiyo hawa hawatofautiani kimafundisho bali mfumo wa
maongozi
- Uonevu
kutokana na shida za kimaonevu katika makanisa mengi wakati mwingine mtu
anaweza kutoka na kuanzisha huduma yake huyu naye anaweza kuwa na
mafundisho kama yaleyale ya awali.
Tunaweza kushirikiana na wote wenye sababu kama hizi mbili za chini kwa
vile utunzaji wa mafundisho wawezakuwa msingi wa kutoka kwao.
Unyenyekevu
katika Dhehebu lako
Hakuna
dhehebu linaloweza kudai kuwa ndilo pekee linaloshikilia kweli yote pekee na
kwamba ndilo dhehebu kamili lisilo na mapungufu kwa msingi huo basi unaweza
kujinyenyekeza katika dhehebu lako kwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo
- Mshukuru
Mungu aliyeruhusu uwepo hapo ulipo na kujifunza kumjua yeye kwa sehemu
- Shughulika
na programu zote zinazokusudiwa katika kanisa lako ikiwemo katiba.
- Jilinde
wewe mwenyewe na mafundisho yako wewe mwenyewe (1Timotheo 4;16) pia Linda wale ambao Mungu amekuweka uwachunge
kwani utatoa hesabu kwaajili ya hao.
C; Maswala
ya huduma
Watumishi wengi wa mungu husongwa na mambo
makuu mawili mahitaji ya shughuli za kukamilisha na muda wa kukamilisha
shughuli zilizoko mbele yao matokeo yake wanajikuta wanchoka huku wakiwa
hawajafanikisha wanayo yataka na inaonekana kama kwambo muda wao hautoshi.
Unahitaji
kupumzika
Watumishi
wengi wanakuwa wanasongwa na hatia hasa
pale wanapojikuta wanahudumia sana watu
na kazi za kanisa na haimaye hujikuta wameshindwa kutimiza maswala yao
binafsi na mahitaji ya familia yake hii ina maana kuwa wakati mwingine
wanajisikia hatia kusema hapana kwa kazi ya Mungu na watu na kuwa nahitaji muda
na familia yangu ,Neno hili wao huliona kuwa ni dhambi lakini kutokuwahudumia
wa nyumbani mwako ni dhambi zaid Mchungaji unahitaji kupumzika na ili kutatua
tatizo hili unahitaji ratiba isiyovunjika vunjika huko mbale tutajadili kuhusu
ratiba lakini ni muhimu kuwa na wakati na familia yako na unahitaji mapumziko
Unahitaji
kuwa mkarimu.
1Timotheo 3;2 huduma ya ukaribishaji wageni (ukarimu) na kuwahudumia
kimsingi linawahusu wachungaji bahati mbaya katika siku za leo wachungaji
wanafikiri kuwa wao ndio hupaswa kuhudumiwa badala ya kyhudumia watu Biblia
moja ya kiingereza inafafanua hivi “He must enjoy having guests in his home” inawezekana ikawa ngumu kwa sababu ya kipato
ulichonacho lakini si lazima iwe chakula cha gharama unaweza kuwakaribisha hata
kwa chai tu, na unapokuwa ni wakati unahitaji mapumziko ni lazima watu wajue
kuwa unapumzika ili wasifikiri unapatikana.
A; Maisha
binafsi ya kichungaji. Afya.
Tumeona kuwa watumishi wa Mungu
wanakosa hata muda wa kupumzika ni watu wenye shughuli nyingi sana ,wachungaji
ambao saa zote wako na shughuli nyingi kiasi hiki wanahitaji kuwa na Afya
nzuri kwani afya yako ya mwili inauhusiano na Afya yako ya kiakili na kiroho
kwa msingi huu kumbuka kuwa mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Koritho
6;15-20) kwa msingi huo lazima ukumbuke kuwa Mwili wako si wako mwenyewe na
mwili huu ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa msingi huo kama mchungaji hatakuwa na
Afya nzuri atawezaje kubeba mzigo huu wa kazi kubwa ya mungu iliyoko mbeleni
kwa msingi huo yako mambo ya msingi unayopaswa kuyazingatia ili uwe na afya
nzuri kumbuka kuwa “A pastor should be phyisicaly fit”
Mchungaji
lazima awe na Afya nzuri..
- Uwe
na muda wa kutosha kupumzika na kustarehe kila mchungaji ana kazi ngumu na
majukumu mazito kwa msingi huo unapaswa kuwa na muda wa mapumziko Yesu
alimaanisha kitu aliposema kuwa Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu
Marko 2;27 miili yetu imeumbwa katika namna ambayo inaweza kujijenga
yenyewe ikipumzishwa vya kutosha. Kama Mungu mwenyewe alionyesha mfano wa
kupumzika kwanini wewe usipumzike Kutoka 20;9-11. Yesu mwenyewe kwa
kufahamu umuhimu wa kupumzika wakati Fulani aliwaambia wanafunzi wake wawe
peke yao
ili wapate kupumzika ( Marko 6;31)
- Uwe
na safari pamoja na familia yako mbali na nyumbani mpate Muda wa mapumziko
huko mapumziko yaweza kuchukua hata
muda wa wiki moja au muwe na likizo wachungaji wengi hasa sisi wa Afrika
hatuna likizo tunafanya kazi milele hii sio sifa bali ni kwa ujinga wako
- Uwe
na tabia ya kula vizuri kula vizuri hakuitaji wewe uwe tajiri hiki ni chakula bora chenye makundi
yoote muhimu ya chakula yanayojenga mwili na si kula sana kunakotakiwa
bali kula kwa nidhamu wachungaji wengi huona kuwa kula ni kama kupoteza
muda hivi hivyo hujali kazi zaidi.
- Fanya
mazoezi mazoezi sio dhambi kunawatu huokoka kupita kiasi hata wandhani
kuwa kuchukua mazoezi ni dhambi hii sio sawa mchungaji chukua mazoezi
cheza mpira ,kimbia n.k
Maisha
binafsi ya kichungaji Kuvaa vizuri
Mchungaji lazima utoke vizuri uwe na tabia ya kuvaa vizuri na kwa usafi
smatness hili ni swala la msingi sana hakikisha kuwa unapiga mswaki
vizuri,pakaa mafuta mazuri chana vizuri pafyumu nzuri,jitibu maralia na minyoo
na funga kwa mpango maalum si kwa namna itakayoharibu afya
Maisha
binafsi ya kichungaji Tabia yako
Mchungaji hushughulika na watu karibu
muda woote na kwa kawaida kila jamii ina viwango vyake vya maadili tafadhali
ishi sawa na viwango hivyo vinavyokusudiwa tabia yako njema itawavutia watu na
kuleta ushuhuda mzuri katika jamii
B; MAISHA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII
Maisha binafsi ya kichungaji uhusiano wako
na wachungaji wengine.
Mchungaji unapaswa
kuwa na uhusiano mzuri pia na wachungaji wengine au wachungaji wenzako, wakati
mwingine Bwana ataruhusu mchungaji kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine
na hivyo kuruhusu mchungaji mwingine kuchukua nafasi yake, hili
linapotokea nyakati nyingine limekuwa
chanzo kikubwa cha kuweko mahusiano yasiyo mazuri, kanisa ni mali ya Yesu Kristo kwa msingi huo
unapolijenga lazima ulijenge katika msingi wa watu hao kuwa tayari kupokea watu
wengine
Wajibu wako kama unahama
- Mzungumzie vizuri mchungaji anayekuja
nyuma yako
- Kabidhi kanisa katika hali nzuri na
moyo mweupe
- Mshirikishe maono na mipango ya mbele
ya kanisa husika
- Tumia hekima na uangalifu unapoalikwa
katika kanisa lako la zamani
- Uwe makini unapotembelea au
kuwasiliana na washirika wako wa zamani ili kuzuia kutokueleweka.
Wajibu wako kama unahamia
- Tambua mchango mkubwa wa mchungaji
aliyekutangulia wako watu wengine huponda kabisa mambo yaliyofanywa na
wengine waliowatangulia kana kwamba hawajafanya kitu chochote kabisa
- Tambua kuwa kila mtu ameumbwa kwa
namna tofauti hivyo yule hawezi kuwa wewe wala wewe huwezi kuwa yule
kumbuka kuwa kwa muda watu watakulinganisha na mchungaji wao wa kwanza
usijali unachotakiwa ni kuongeza bidii katika maeneo yenye upungufu lakini
usiigize kwani kila mtu ameumbwa tofauti
- Fanya mabadiliko kwa hekima pale
inapobidi kufanya mabadiliko fulani hakikisha unatumia hekima na
kuwaelewesha watu kwanini unafanya hayo unayoyafanya usifikiri kuwa kwakuwa yale yalifanywa
na mtu mwengine basi ni mabaya
Uchungaji kama taaluma yako.
Uchungaji pia ni
taaluma ukiacha ya kuwa kuna wito, kama taaluma ni lazima ujue kuwa wewe ni
wakili wa Mungu unamwakilisha Mungu hivyo lazima uishi sawa na viwango ambavyo Mungu anavikusudia
ili kuwakilisha ufalme wake, Lazima uiheshimu kazi yako kama mtu mwenye taaluma
ya kazi hiyo kwa bahati mbaya hakuna mtu atakayekusimamia nini cha kufanya
katika kazi yako ya uchungaji hivyo ni wewe ndiye mwenye wajibu wa kujisimamia
lazima ujisimamie na kujiuliza je mambo haya yanakwenda sawasawa
- Jiulize je unakuwa na wakati wa
kujisomea? Wengine huzurula mjini tu
- Je unachukua muda wakutosha kujiandaa
kwa jumbe mbalimbali?
- Je nina ratiba maalumu ya
kujiendeleza mwenyewe kiroho?
- Je naweza kujifanyia tathimini
mwenyewe kuwa sio muaminifu katika kazi hii?
- Je naweza kujitathimini kwamba
ninajitahidi kuendeleza huduma ambayo Mungu amenipa? Lazima mchungaji
uonyeshe bidii katika maswala mbalimbali ya kihuduma ili ijulikane pia
kuwa kazi hii pia ni taaluma yako na umeisomea na unaithamini.ili
kujiwekea mipaka fanya pia mambo yafuatayo
- Uwe na
bidii katika kutimiza majukumu ya kazi zako.
- Fika kwa
wakati katika kila eneo unalopaswa kufanya hivyo
Mchungaji kama mwenyeji.
Kuna wakati ambapo
labda mtaalika mchungaji mgeni kwa kusudi la semina, mkutano au jambo lingine
lolote hii ni muhimu kwa kuwa kanisa halijengwi na mtu mmoja tu hivyo si vibaya
kualika wengine kwa ajili ya kujaziliza maeneo ambayo labda hujayafikia semina
zisitumike kama gea ya wewe kupumzika kwa uvivu wa kuandaa masomo na kufundisha
msingi wa kualika mgeni uwe ni baraka na mpango wa kufikia maeneo ambayo
wengine wamepakwa mafuta kuyafikia kama Mungu anavyokusudia japokuwa
unapomwalika mgeni ni muhimu kuzingatia yafuatayo
- Mwelekeze namna ya kufika mahali
ulipo na kanisa lilipo
- Mpe eneo analopaswa kufikia na endapo
atahitaji utulivu basi eneo hilo liwe hivyo
- Mpe muda wa yeye kujua kuwa atapaswa
kuoga,kujisomea na muda wa kula
- Mwelezee muda wako wa ibada namna
mnavyoendesha ibada zenu na kama kuna namna anavyotaka kuendesha ibada
iliyo tofauti
- Mweleze kuwa ibada inatakiwa iwe
ndefu kiasi gani wengine huimba mpaka wanasahau muda wa mahubiri au
kumbana muhubiri asiwe na mda wa kutosha
- Unapokuwa mgeni nawe ni muhimu
kuchukua tahadhari zenye kupunguza usumbufu viko vitu ambavyo kama
utaviacha vinaweza kuleta usumbufu kwa mfano Taulo,mswaki n.k. na pia jihadhari
na tabia ya kujichagulia vyakula na kupenda starehe au matazanio ya juu
kifedha
A; Mchungaji
na Mahubiri yake
Kuhubiri
ni moja ya majukumu ya msingi ya kichungaji na ni swala la lazima
linalokamilisha huduma ya kichungaji (1Koritho 9;16) watu huokolewa kupitia
mahubiri 1Koritho 1;21
Kuhubiri
maana yake ni nini kwa kilatini kuhubiri ni kutangaza hadharani lakini maandiko
yanapo zungumzia kuhubiri humaanisha nini? Neno kutangaza limetajwa mara 61, na
kutangaza habari njema limetajwa mara 50, na kufundisha limetajwa mara 90,
kuhubiri kwa kibiblia ni kuzungumza habari zisizo za kwako, kwa asili habari
zinazohubiriwa chanzo chake ni Mungu Biblia inaonya kuwa yeyote aliyesema kuwa
Mungu amesema huku hakutumwa Mungu hakuwaheshimu watu hao Yeremia 14;14. hivyo
mkazo katika Biblia unaohusu kuhubiri unahusu kile Mungu anachotaka kisemwe
ndio maana Neno ”Asema Bwana lilikuwa maarufu ” hii ilikuwa inaonyesha ni kwa
mamlaka gani mzungumzaji anazungumza si kwa sababu tu yeye ni mjumbe kwa hivyo
tunaweza kusema kuhubiri kunahusisha ujumbe kutoka kwa Mungu.
Mjumbe.
Ukweli
kuwa kuhubiri kunahusisha ujumbe kutoka kwa Mungu ina maana kuwa mnenaji ni
njia tu ya kupitisha ujumbe wa Mungu kwa watu wake vinginevyo ujumbe
ungefikaje? Mungu ndiye lilikuwa somo kuu na manabii walikuwa ni wajumbe tu na
hivyo si wao waliokuwa wakiupa ujumbe mamlaka bali Mungu hivyo watu walilipokea
neno la manabii kama neno la Mungu
1Thesalonike 2;13.
Kwa
msingi huo ujumbe unahusiaha sehemu kuu tatu Mungu mtoaji wa somo,Mjumbe
mpitishaji na watu wapokeaji wa somo husika
hivyo basi mahubiri huuhusisha maeneo makuu matatu na sio kujisemea tu.
Kwanini tuhubiri?
Warumi 10;13-15 ni andiko ambalo linajibu
wazi kwanini tuhubiri hii inaonyesha wazi kuwa mahubiri yana sababu tangu mwanadamu amefarakana na Mungu kwa
sababu ya dhambi anahitaji kupatanishwa na Mungu Injili ya Yesu Kristo ni habari njema kutoka kwa Mungu kuwa
mwanadamu anaweza kupatanishwa tena na Mungu kupitia kazi ya Kristo pale
msalabani na wakaokolewa (Rumi
1;16,10;14) Neno linapohubiriwa wenye dhambi husikia wanaamini wanaokolewa
wanamkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi na kuokolewa hivyo mahubiri ni njia ya
watu kuokolewa, Ni kuwawekea wazi kilichofichika,ni kuleta changamoto
inayohitaji mwitikio,ni kuleta Habari maalumu sana.
Namna ya kuupeleka ujumbe
Mungu anapokuwa amemuita mchungaji kama
mtoa ujumbe ni muhimu kufahamu kuwa mtu huyo sasa anakuwa kati ya Mungu na
wanadamu, Kwa msingi huo huwezi kusema unajiandaa bila kugusanishwa na pande
zote mbili na kwakuwa wewe umeitwa na
Mungu unahitaji kumwangalia Yeye kwanza kwa ajili ya maandalizi.
Maandalizi ya ujumla
§ Tunza hali endelevu ya Kiroho na maisha
yako kwa maana ya uhusiano wako na Yeye
§ Hakikisha kuwa unatunza jumbe zako au
shamba lako la jumbe hii inamaanisha mambo unayojisomea n.k unayoyasikia kutoka
katika jumbe za wengine ambayo baadaye yaweza kukufanya uweze kutengeneza jumbe
zinapo hitajika Endeleza tabia ya kujaza mambo yawezayo kukusaidia katika
kuapta jumbe.
Fanya maandalizi maalumu
Ujumbe kutoka kwa Mungu
Maandalizi maalumu
Tengeneza
Wasilisha
Kufanya maandalizi maalumu namna ya kupata
ujumbe wa kuhubiri lazima Mchungaji aulize au aombe kutoka kwa Bwana, Mungu
atatupa wazo kutoka katika neno lake kisha ingia katika maandalizi, fanya
matengenezo ya jumbe kisha tumia ujumbe katika mazingira husika tunasikitika
kuwa hatutaki kuingia ndani sana katika swala zima la somo la kutunga hutuba
ambalo hushughulika na swala hilo hapa tunagusia kwa ufupi tu ili kukumbusha au
kukupa mwanga.
- Maaandalizi maalumu huanza na
kupatikana kwa ujumbe.
- Maandalizi maalumu hufuatiwa na
kutafasiri biblia kwa usahihi hili hujumuisha
- Historia
ya andiko
- Lugha
iliyotumika
- Ushahidi
kutoka katika maandiko mengine
- Maana ya
kitheolojia ya andiko.
- Baada ya hayo angalia uhalisi wa
maisha ya watu husika
- Tafuta taarifa zaidi katika shamba
lako la jumbe au maktaba yako
- Pangilia ujumbe wako kama kanuni za
hotuba zinavyotaka.
Namna ya kuwasilisha ujumbe
- Kusudi na kile kinachobebwa katika
ujumbe kinawakilisha na kuamua ujumbe upelekwe vipi na hayo yatatambulisha
kuwa Mungu anataka nini yaani kama ni ujumbe wa upendo sauti na muonekano
wako utaashiria upendo siku hiyo
- Angalia watu wako walivyo na kiwango chao cha ufahamu na kiroho
huku ukikumbuka kuwa wako wanaotaka kutambuliwa,wako waliovunjika moyo
wako wenye majaribu ya aina mbalimbalio hivyo peleka ujumbe wako kwa hekima
usiwaongezee watu matatizo bali utatue matatizo
- Tumia sauti yako kwa makini yaani
kulingana na kundi la watu usipaze sauti sana kama kuna watu 20 tu
matumizi yako ya sauti ni lazima yaendane sawa na kundi lilioko
- Hakikisha unavaa vizuri kwa namna ambayo
itasaidia watu kupokea kile unachokikusudia
- Unapotumia notes si vizuri kuzisoma
unaweza kufanya hivyo mwanzoni lakini haitafurahisha kuendelea kuzisoma,
kumbuka mwili wako nao uanzungumza.
- Usiogope swala la hofu ni la kawaida
na baada ya muda Roho wa Mungu atakusaidia
Hitaji la Jumbe tofauti tofauti
Watu wanahitaji jumbe tofauti tofauti kwa
hivyo ni muhimu ukawasilisha jumbe si katika namna ileile ya siku zote jaribu
kutumia jumbe tofautitofauti kuna aina nyingi sana za jumbe lakini zilizo kuu
zinazojulikana sana ni tatu tu Ujumbe wa somo topical ujumbe wa andiko textual
na ujumbe wa uchambuzi wa kifungu cha maandiko Expository.
Pangilia jumbe zako
Kama mchungaji anahubiri mara tatu kwa
wiki maana yake ni kuwa kwa mwaka utahubiri mara 156 hizi ni jumbe nyingi
sana na kama utahubiri kutoka katika
eneo moja tu kwa mfano jumbe 156 za maswala ya unabii tu litakuwa swala gumu
sana hivyo ni lazima uwe na mpangilio utakao ruhusu kutoa mlo kamili wa
kibiblia kwa watu wako huku ukizingatia mahitaji yao lakini itakupasa kuhubiri
kutoka katika nyanja mbalimbali za
kibiblia.ili kuwafikia watu katika namna
mbalimbali zingatia mambo yafuatayo
§ Angalia mahitaji ya watu wako
§ Tumia kalenda ya Kikristo
§ Tafuta namna ya kuwainua kiroho
§
Fundisha mafundisho ya biblia na watu maarufu
katika Biblia biographical Sermons
B: Mchungaji
na mafundisho yake
Mchungaji au muhubiri pia ni mwalimu ujumbe wa
mahubiri unapohubiriwa pia unakuwa na mafundisho,Kristo alifanya kazi zote
mbili alihubiri na kufundisha Mathayo 4;23 kuhubiri kunahusisha kushawishi, kuchochea,
kutaka kutangaza, wakati kufundisha kunalenga kumpa mtu maarifa kuelimisha
wataalaamu wanaamini kuwa kanisa linakuwa vizuri kiroho likiwa na mafundisho
hata hivyo ni muhimu kufahamu pia kuwa wakati mwingine katika kufundisha kuna
kuhubiri na katika kuhubiri kuna kufundisha vitu hivi huingiliana japo ni vitu
viwili tofauti na kufundisha kunalenga
§
Kuleta matunda ya ufahamu
§
Kupandikiza tabia iliyo nzuri
§
Kupandisha juu viwango vya kikristo na utumishi
alioitiwa kila mtu
Kufundisha kumeagizwa katika agizo kuu Mathayo
28;19-20 na kilichoagizwa kufundishwa ni neno la Mungu yoote niliyowaamuru, Kufundisha
kuliagizwa kwa mataifa yoote, Mchungaji fundisha kwa mamlaka Yesu alifundisha
kwa mamlaka Mathayo 4;24,5;1. Marko 1;22, Kufundisha ilikuwa ni sehemu muhimu
ya lazima ya maisha yake na huduma Marko 10;1, kufundisha ilikuwa ni sehemu ya
nyakati za kanisa la kwanza neno kufundisha
kwa kiyunani ni Didasko
kufundisha ambayo ilikuwa ni sifa ya mtu aliyetakiwa kuwa kiongozi katika kanisa
1Timotheo 3;2. Lazima uwe na mbinu mbalimbali za ufundishaji somo la principal
of teachings litashughulikia hilo, Fundisha ukiwa unachunguza nini kinaendelea,
Fundisha kwa kufunua kweli zilizofichika Exposition na wakati mwingine ni vema
ukitoa nakala za somo unalofundisha hii inasasidia kanisa kukua kwa haraka.
C: Mchungaji
na huduma ya kichungaji
Kazi ya mchungaji kwa lugha ya
kiyunani ni Poimen ambalo neno hili
kwa asili ni kulinda au kuchunga neno
hili kuchunga limetumika mara kumi na nane
katika Agano jipya tukielewa kazi zilizokuwa zikifanywa na wachungaji wa
mifugo wa kawaida kama kondoo, ng’ombe n.k. tutaweza kuifahamu vizuri sana kazi
ya kichgungaji
Mfano wa
Yesu Kristo kama mchungaji mwema
Karibu mara saba katika injili waandishi
wanatumia neno mchungaji kumhusu Yesu, na pia Kristo ametajwa kama mchungaji
mkuu Waebrania 13;20 na Petro 2;25 na ingawaje injili inavyomwelezea Yesu moja kwa moja kama mchungaji
Mwema ni Yohana 10;11-14 Yesu anatoa mtazamo mzima wa kuwa yeye ni mchungaji
mwema na hii ilikuwa ni kutimiza mtazamo mzima wa agano la kale kumhusu Yehova
kama Mchungaji mwema Zaburi 23;1.Yeye anaonyesha mtazamo tofauti na viongozi
wengine wachungaji ambao walikuwa waovu mioyoni mwao badala ya kuondoa uhai wa
kondoo mchungaji mwema anautoa uhai wake kwa ajili ya kondoo hii inaonyesha
jinsi kazi ya kichungaji inavyopaswa kuwa badala ya kufaidika Mchungaji anajali na kujihusisha na
kondoo kufikia viwango vya kujitoa uhai wake kwa maslahi ya kondoo hata ingawa
walimkataa lakini alikuja kwa ajili yao
aliwahurumia aliugua kwa ajili yao na hasa pale alipoona wametawanyika kama
kondoo wasio na mchungaji Luka 13;34, Mathayo 6;36. kuwahurumia katika lugha ya
asili ni kuugua kwa huzuni kubwa kiasi cha kufikia hatua ya kuumwa Luka 15;4-6 inaonyesha
zaidi jinsi mchungaji anavyoguswa hata na kondoo waliopotea ambapo mchungaji
huyo hujihusisha sio tu na kuchunga lakini pia na kutafuta waliopotea na sio
kutafuta tu hutafuta mpaka ampate ni watumishi wangapi leo wanafanya hiki
ambacho Biblia inasema?
Mfano wa Paulo Mtume kama mchungaji
Moja ya vifungu maarufu sana
vinavyoizungumzia vema kazi ya kichungaji ni
Matendo 20;18-31 hapa tunaona mfano wa huduma ya kichungaji miaka mitatu
Paulo mtume aliitumia pale Efeso kama mchungaji wa kondoo huku akitumika kama
mtumwa mst 19, hata alipokuwa akiondoka alitilia maanani usalama wa kondoo kama
mchungaji kiongozi wa kanisa akitamani uangalifu mkubwa wa kondoo kuendelezwa
mst 28.Daudi aliwachunga kondoo wa baba yake na kuwa tayari kugharimika kupambana
na dubu na simba mchungaji ana wajibu wa kuwalinda washirika kuhakikisha
wanaukulia wokovu, kuwalinda na mafundisho potofu na waalimu wa uongo, Mfano
huu wa Bwana Yesu na Paul unatufundisha
jukumu kubwa la kichungaji kwa hivyo mafano wa wachungaji katika maandiko
unaweka bayana swala zima la shughuli za
kichungaji kwamba kwa ujumla shughuli ya kichungaji ni kushughulika na mahitaji
ya watu kuchunga kujali na kulinda bila ya upendeleo kwa gharama yoyote
Shughuli ya kichungaji hujumuisha ;-
Kuhubiri
injili 1Koritho 1;21 Tito 1;3,Warumi
15;19,
Kufundisha Neno la Mungu 1Koritho 12; 28, Efeso
4; 8, 11.
Kusimamia Ibada kuhakikisha zinafanyika kwa
Heshima na utaratibu 1Koritho 14;23,32,Efeso 5;18
Kulitunza kanisa kuhakikisha linajaa amani na
upendo na umoja Yakobo 3;16 galatia 5;22.
Kuhakikisha wakristo wanakamilika Kiroho kufikia
utakatifu Efeso 4;13,Kolosai 1;28 Mchungaji ni lazima uhakikishe watu hawapotei
Yohana 17;12, hakikisha watu wanakua katika huduma na kutumia vipawa
walivyopewa, Kukuza wale watakaosaidia katika shule za jumapili na
maongozi na kupandikiza moyo wa kupenda
kuihubiri injili.
Mchungaji ni lazima ahakikishe kuwa anafanya
maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali, watu wana shida nyingi sana
wanahitaji kuponywa Mathayo 9;35, Marko 16;17-18, Isaya 53;5
Hakikisha unakuwa na maono kwa ajili ya kanisa
la Mungu Torati 2;3 kutoka 14;15 hakikisha unakua na hekima jinsi ya kutimiliza
maono Epuka kuwatwika watu mizigo ya michango isiyo ya lazima hakikisha watu
wanajitoa kwa hiyari kwa kadiri ya neema kama matokeo ya kujifunza na sio
kulazimishwa Mungu huwabariki wanaotoa kwa moyo
Hakikisha unakua mvumilivu na unajifunza
kumtegemea Mungu
Hakikisha kuwa unawatembelea washirika na wasio
washirika katika mtaa wako au eneo uliuoko,hii ni njia ya kuwafikia kihuduma
lakini hakikisha unakuwa na ratiba ya namna ya kufanya matembezi, gawa mji wako
katika sehemu mbalimbali
Hakikisha unakua na huduma ya ukarimu katika
nyumba yako kwa kukaribisha watu
Tembelea Hospitalini na magerezani lakini pia
unaweza kuwashirikisha wengine katika huduma hii.
MCHUNGAJI
NA HUDUMA YA USHAURI (COUNSELING)
Tunaweza
kusema kwa ukweli kuwa ushauri wa kichungaji ni huduma kamili kabisa ya
kichungaji wakati mwingine tunaweza kusema kuwa huduma ya kichungaji haiwezi
kuwa kamili bila ya kuweko kazi ya ushauri, Hata hivyo ushauri ni taaluma
kamili na tunashauri mchungaji kujisomea zaidi kuhusu somo la ushauri wa
kichungaji
Ushauri
kwa mtazamo wa Kikristo ni shughuli ya kukuza na kubadilisha mawazo wa
muathirika kupitia ofisi ya mchungaji ambaye ndiye mshauri ambaye atatumia
mbinu za kawaida na za kimungu kuhuisha kwa upya, kuponya, kukuza na kumfanya
mtu kutua mzigo alionao na kuwa na uwezo wa kukabiliana na hali yoyote ngumu au
iliyokuwa imeleta fadhaa uathirika hapo hau-husu tu maswala ya kimwili bali na
kiroho pia
Ziko
aina nyingi za ushauri kama ushauri wa moja kwa moja na ushauri usio wa moja
kwa moja ule wa moja kwa moja mchungaji na muathirika wataongea na kutafuta
suluhu ya tatizo kwa siku moja au hata kwa siku kadhaa ule usio wa moja kwa
moja Mchungaji huweza kutumia makundi katika kutatua tatizo la muhusika bila
kundi hilo kuelewa kuwa wanatatua tatizo huku ukijumuisha mbinu nyingine
zinazoweza kutumika.
Viwango vya
athari na maumivu wayapatayo watu LCU
Tukio
|
Kiwango
LCU
|
Tukio
|
Kiwango
LCU
|
Kufiwa & mpenzi
|
100%
|
MtotoShuleni
|
29%
|
Takaka
|
73%
|
Shida kisheria
|
29%
|
Watoto
wapweke
|
65%
|
Mke kuacha kazi
|
26%
|
Kufungwa
|
63%
|
Hali ya hewa tof
|
25%
|
Kufiwa na ndugu
|
63%
|
Kupitia tabia
|
24%
|
Kujiumiza
|
53%
|
Boss mkali
|
23%
|
Shughuli za ndoa
|
50%
|
Kubadili saa za k
|
20%
|
Kufokewa kazini
|
47%
|
Mabadiliko shule
|
20%
|
Ndoakupatanisha
|
45%
|
…”….kanisani
|
19%
|
Kujiuzulu
|
45%
|
…”…Kulala
|
19%
|
Afya mbaya
|
44%
|
…”…kula
|
15%
|
Mimba
|
40%
|
Likizo
|
15%
|
Ugumu ktk sex
|
39%
|
sikukuu
|
13%
|
Mtoto mpya
|
39%
|
|
|
Biashara mbaya
|
39%
|
|
|
kuchacha
|
38%
|
|
|
Kifo cha rafiki
|
37%
|
|
|
Kuhamishwa
|
36%
|
|
|
|
|
|
|
Mchungaji zingatia hayo hapo juu ni maumivu
yanayowapata watu na viwango vya maumivu kwa asilimia zake hii ikupe changamoto
namna ya kushughulika na watu wanaohitaji kuponywa majeraha hayo katika
Kuwashauri waathirika wako
_____________
Used by
Permisiion of Holmes, T.H & Rahe, R.H.The Social readjustment rating
Scale.Jounal of Psychosomatic Research II: 213-218, 1967.
Mchungaji
kama kuhani au Mchungaji na huduma ya maombezi
Karibu asilimia kubwa ya huduma ya
kichungaji hufanyika hadharani.ingawaje inaweza kufanyika kwa ubora na kuleta
matokeo yanayokusudiwa kama itafanyika sirini
(Mathayo 6; 6) .hii haimaanishi kuwa huduma hiyo ya maombezi ni lazima ifanywe
ndani tu lakini tunamaanisha swala la msingi inapofanyikia Luka 6;12. Mchungaji
lazima awe muombezi kwa ajili ya watu katika eneo alioko
Mchungaji
kama Kuhani
Makuhani katika agano la kale walikuwa
ni mawakili wa watu kwa Mungu na msemaji wa watu kwa Mungu na ilikuwa ni
kupitia kuhani watu wangeweza kuwa karibu na Mungu au kupatanishwa na Mungu,
Kupitia kifo cha Kristo kila mmoja leo anaweza kwenda moja kwa moja kwenye kiti
cha rehema cha Mungu bila ya kuhitaji kuhani wa kibinadamu tangu pazia la
hekalu lilipopasuka vipande viwili kutoka juu hata chini (Mathayo 27; 51)
waamini wote wanaweza kukifikia kiti cha rehema cha Mungu kwa kuwa sasa wao ni
makuhani na wafalme (Ufunuo 1;6,1Petro
2;5,10).pamoja na hayo Biblia bado inatuagiza kuombeana sisi kwa sisi Yakobo 5;
16 na kuchukuliana mizigo Galatia 6;2.
Kwa
msingi huo basi mchungaji ana nafasi ya kipekee katika kuwafanyia watu maombi
kwa kuwa anayajua mahitaji ya watu na yanawekwa wazi kwake kuliko kwa mtu
mwingine awayeyote ni Mchungaji anayebeba waliojeruhiwa na mara nyingi ndiye
anayebeba mzigo wa kanisa hususani pale linapoteseka Waebrania 4-5 imejaa
mifano mizuri ya kazi za kikuhani jambo linalotoa picha ya kiazi ya kichungaji
hivyo mchungaji kama kuhani anapaswa;-
§ Kuwa
mwepesi kujua mahitaji ya watu
§ Kuwa
na moyo wa huruma kwa ajili yao wanaorudi nyuma au kuanguka dhambini lazima
uwajulishe kuwa kuna neema na rehama
wakati wa uhitaji Waebrania 4;16, wakati mtu anapoanguka sio wakati wa
kuanza kumshutumu na kumlaumu na kutangaza madhabahuni kwani neno la Mungu
linatosha kwa kwa kuonya na kufundisha
2Timotheo 3;16-17 hivyo litumike kwa upendo katika kutatua tatizo kwa
huruma na rehema itakayo mwezesha muathirika kupokea msamaha
§ Onyesha
kuhusika na maisha ya kila mtu,Hakuna ukuhani bila watu wala huwezi kumtenga
kuhani na watu,Maandiko yanatuambia kuwa Yesu alijaribiwa katika mambo yote
bila kufanya dhambi ,Kujua mambo ambayo watu wanapitia kunaweza kukusaidia
wanapitia nini hivyo kuwafikia na kuwasaidia kwa kua unaelewa na unafahamu hivyo maombi
na yawe silaha yako katika namna ya kuwahudumia.
Mchungaji na
maswala ya kutia nidhamu
Moja ya
maswala magumu sana na yanayohitaji uangalifu mkubwa kwa mchungaji na viongozi
wake wa kanisa ni maswala ya kutia
nidhamu.Hakuna mtu anayependa kutiwa nidhamu au anayekubali nidhamu na kwakweli
wachungaji wengi hawapendi hata kuizungumzia nidhamu na kwa kweli biblia
inapozungumzia nidhamu ina maana pana zaidi ya adhabu ambayo watumishi wengi
hufikiria.
Nidhamu ni
nini?
Neno
nidhamu linajumuisha maeneo makuu mawili Kufundisha na kusahihisha, Kufundisha
ina maana ya kutoa mafunzo,kumkamilisha mtu, kitaaluma au kimaadili na
kusahihisha maana yake ni kudhibiti au kurudisha katika utaratibu, siku zote
kutia nidhamu au kusahihisha mtu lazima kuendane na kumpenda mtu yule unayempa
nidhamu kama afanyavyo baba wa kawaida wa kidunia kwa wanawe.
Kusudi la
kutia nidhamu
Lengo kuu la kutia nidhamu ni
kurejesha na sio adhabu au kukomoa.
(Waebrania 12; 10-11) Ni muhimu nidhamu itolewayo na kanisa iwe na lengo
la kurejesha na sio kukomoa, ni kuhakikisha mtu anarudi katka uhusiano mzuri na
Kristo na kanisa na sio kummbomoa mtu, ni kuhakikisha mtu anakuwa na tabia za
kikristo na anaendelea katika kiasi, Watumishi wengi wa Mungu wamepoteza wengi
katika eneo hili kwa kuwaharibu watu kabisa badala ya kuwaponya wametumia
nafasi ya mtu kukosea kama sehemu ya kukomoa watu na kuhukumu kuliko hata Mungu
alivyokusudia to hell! Hivi miili yetu inapougua si tunaitibu? Na hata kama kiungo kunachoumwa ni kimoja tunafanya hivyo kwa kuwa
mwili woote unaugua si ndio? Na hata kama
inahitaji operation kwa kweli mwili woote utaugua lakini kwa bahati mbaya wengi
tumewapoteza kwa sababu za kipuuzi tu.
Nidhamu
inayohitaji operation ni zile zinzoonyesha kuwa Mtu huyo analeta mafundisho potofu
Warumi 16;17;1Timotheo 6;3-5 au anaishi maisha ya uchafu Marko 7;20-22,1Koritho
5 na akitubu hurejezwa 2Koritho 2;5-11 na Mtu asiyetaka kutubu au mwenye kiburi
Mathayo 18;17.
Kanuni za
kumtia mtu nidhamu
- Nidhamu
lazima iendane na kanuni na sheria za kanisa husika wako wachungaji ambao
hutoa adhabu kinyume hata na katiba au hata maongozi ya kanisa husika
wakivunja hata katiba zao
- Usimuhukumu
mtu ndugu kaka au dada bila kumpa nafasi ya kujieleza na unapomtia nidhamu
lazima ajue asili ya kosa lake
na adhabu
anayoistahili Mathayo 18;15-17
- Adhabu
lazima iwe ya kibiblia ambayo mara
nyingi lengo lake
ni kumleta
muathirika katika toba na sio vinginevyo
- Inapokuwa
hadharani ni kwa ajili ya kuonyesha toba aliyo nayo mtu kwa kanisa na
kasha unamrejesha lakini wengine hufanya hivyo kwa kusudi la kudhalilisha
na kumuaibisha mtu
- Mtu
aliyetubu lazima arejeshwe kwa ukamilifu katika ushirika (Yohana 21;15-19)
Yesu hakumuuliza Petro ilikuwaje ukarudi nyuma bali alimuuliza swali
kuhusi upendo wake kwake na kujikabidhi kwake fahamu ya kuwa hesabu ya kila mshirika
utaitoa siku ile endapo utakuwa umempoteza kwa uzembe.
C: Mchungaji
na huduma maalum
Huduma maalumu ni ibada za kichungaji
za kidini ambazo huusihsa maswala ya ubatizo, Harusi, Mazishi na meza ya bwana,
pia ziko ibada za uanachama, ibada za kuweka wakfu majengo na kuweka wakfu
watoto n. Ibada hizi hutegemeana na kanisa husika namna na jinsi wanavyotakiwa
kuziendesha hapa tutagusia kwa ufupi tu lakini ni jukumu la kila mtumishi
kujifunza kuendesha ibada hizo kulingana na kanisa lake na tamaduni zao ingawa
mara nyingi sana ibada hizi hufanana.
Ibada ya
ndoa.
- Zingatia
matakwa yote ya serikali yahusuyo ndoa
- Hakikisha
kuwa wanandoa ni watu huru na sio waliolewa au kuoa mara ya kwanza na
wenzi wao wako hai
- Hakikisha
kuwa ni wazima wa afya na wamekubaliana na kuaminiana
- Endesha ibada sawa na kanuni za
kanisa lako
- Epuka kuwa na mahubiri marefu na
yenye kuchoisha siku ya ndoa uwe na mafundisho ya kutosha na wanandoa
kkabla ya siku ya harusi yao .
Ibada ya Mazishi.
- Uwe na uzoefu wa mila na desturi za
eneo husika
- Tunia kanuni za kanisa lako katika
mazishi,
- Fika mapema na kutoa pole kwa wafiwa
kisha kajiandae kwa ibada
- Fika kwa wakati hubiri kwa ufupi na
kuwakumbusha watu wajibu wao kwa Mungu
Ibada ya
ubatizo wa maji.
- Ibada
ya ubatizo wa maji ni tangazo la kumpokea Yesu ni ishara ya nje ya
ushahidi kuwa umeamua kuwa mkristo kwa hivyo ni muhimu kwa waamini wapya
kubatizwa haraka iwezekanavyo na ni sehemu ya agizo kuu Mathayo 28;19.
- Mafundisho
ni muhimu yakitolewa kwa wahusika au muhusika kama
ilivyokua kwa towashi wa kushi na mkuu wa gereza katika Matendo 8 na 16
- Hakikisha
watu wamejiandaa vizuri,mavazi yavaliwe vizuri na kuweko nguo za
kubatiziwa na kubadili,batiza wanaume kwanza kasha wanawake,hakikisha maji
ni safi na
ikiwezekana yawe yanayotembea
Ibada ya
ushirika wa meza ya bwana.
- Yesu
aliagiza ushirika wa meza ya bwana kufanyika kwa ukumbusho wake (Luka 22;
19). Tendo hili ni kuutangaza mauti ya Kristo hata ajapo 1Koritho 11;26
hakuna muda au wakati maalumu uliowekwa kibiblia kushiriki meza ya bwana
hivyo kila kanisa litafanya kulingana na nafasi yake na katiba zao
- Andaa
watu kuandaa meza ya bwana yaani mkate na vikombe hasa mashemasi na ni
lazima wajue kuwa kila inapotangazwa wana wajibu wa kufanya maandalizi
yanayo lingana.
- Fundisha
kuhusu mkate na juisi itumikayo vinawakilisha nini ili kuondoa dhana
potofu kuhusu meza ya Bwana.
- Andaa
ibada na wale watakaokusaidia katika kushirikisha Nyimbo za ibada hii
lazima zilenge kwenye kuendana na tukio husika,Lazima watu waongozwe
katika kujichunguza kwa upya na kwa ndani zaidi kuhusu uhusiano wao na
Mungu na kudhamiria kuwa na uhusiano imara zaidi au mpya zaidi
Ibada ya
kuweka wakfu watoto
- Fanya
maandalizi kwa ajili ya ibada hii watangazie wazazi wawe tayari kwa ibada
hii
- Elezea
maana na faida ya tendo hili kibiblia elezea tofauti yake na kwa nini
hatubatizi watoto wadogo
- Weka
wakfu ibada toa vyeti.
A; Maswala
ya kuyapa kipaumbele.
Tunaelekea
katika kujadili madaya mwisho kabisa katika somo letu zuri za huduma ya
kichungaji katika sehemu zote tumeona kuwa sehemu kuu za huduma ya kichungaji
inatawaliwa na kuhubiri, kufundisha, kutoa ushauri wa kichungaji na huduma
maalumu kwa ujumla huduma hizi zote tayari zinaweza kuwa mzigo wa kutosha kwa
mchungaji na kumfanya kuzidiwa na shughuli hizi huku akihitajiwa kutimiza mambo
yake na shughuli nyingine hivyo ni muhimu kwa mtumishi kujifunza namna ya
kuchukuliana na majukumu aliyo nayo na kujua ni namna gani atayapa kipaumbele
mchungaji anapofahamu majukumu yake ndipo anapoweza kujua kuwa ni kitu ngani
nakipe kipaumbele Yesu alisema hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake
unapokuwepo Mathayo 6;21, hii maana yake ni kuwa pale tunapotoa kipaumbele
ndipo panapoonyesha tumepapa umuhimu mkubwa! Kwa msingi huo wale walioitwa na
Mungu hutoa kipaumbele katika kile Mungu alichowaitia.
Usipojiwekea
majukumu utamaliza siku ukiwa hujatimiza kitu “Aim at nothing and that is
exactly what you will hit”Moja ya tatizo kubwa sana tulilonalo makanisani ni
wachungaji pamoja na watu wao kutokujua kwa nini wapo na kwa msingi huo
makanisa mengi yamepoteza mwelekeo huku watu wakiwa wenye shughuli nyingi sana
lakini bila kuwa na kusudi maalumu tunakwenda lakini hatujui wapi tuendako, Lazima
tujiulize kwa nini tuko duniani na kwa nini Mungu alistawisha kanisa hapa
duniani?. Na ninini jukumu la kanisa hapa duniani haya maswali tukijiuliza
yaweza kutupa kipaumbele cha kujua nini cha kufanya?
Majukumu aya kanisa tunaweza kuyagawa katika maeneo
makuu matatu yafuatayo;-
- Jukumu kwa Mungu.
i)
Kumuabudu Mungu katika roho na kweli Yohana 4;
24.
ii)
Kutunza uhusiano usiovunjika na Mungu 1Yohana 1;7 na Efeso 4;15-16
iii)
Kushiriki katika huduma ya kuwaombea wengine
Warumi 8;26
iv)
Kujiachia kwa Roho mtakatifu na kudhihirisha
karama zake na matunda ya roho 1Korithians 12; 7; 14. Na Galatia 5;22-25.
- Jukumu kwa waamini
i)
Kufanya kazi ya kutimiza Agizo kuu.1 korithians
3;9.
ii)
Kulitumia
neno la mungu kwa halali katika kanisa na kwa matumizi binafsi kolosai 3;16
iii)
Kutambua
majira ya kinabii na wakati tulionao 1Thyesalonike 5;2
iv)
Kuweka
uthamani kwa mambo ya milele 2korotho5;10-11.
- Jukumu kwa ilimwengu.
i)
Kuwahubiria injili kwani watu kimsingi
wanahitaji wokovu Yohana 3;3
ii)
Kutoa uthamanio kwa nafsi za wanadamu amabo Yesu
aliwafia 1Petro 1;18-19
iii)
Kutambua kuwa kuna hukumu ya milele na kuwa
watapotea tusipowajibika
iv)
Kuhitaji nguvu za Roho mtakatifu ili kuwafikia
na kuwaleta kwa Yesu Mdo 1;8.
Mchungaji na
majukumu yake
Majukumu katika mwili wa kristo ni mengi
hivyi hakikisha kuwa unaweka mizani sahihi katika kuyatimiza yoote si vizuri
kuelemea katika jukumu moja tu yako makanisa ambayo wao ni hodari kwa
uinjilisti tu na sehemu nyingine wamelala,pia mchungaji hakikisha kuwa unatoa
mlo kamili wa kiroho kwa washirika wako ili wakue kiroho Waebrania 5;11-14
Mchungaji tekeleza majukumu yako kwa malengo hakikisha kanisa linatimiza
wajibu wake wanaookolewa wafundishwe, wanaopotea wafuatiliwe, andaa viongozi na
kuhakikisha kuwa kila mmoja anawajibika kufikia lengo la kumtumikia Mungu
Tumia fedha vizuri na fanya tathimini ya
malengo yako huku ukitoa kipaumbele kwa kazi uliyoitiwa.
B. Umuhimu
wa matumizi mazuri ya Muda
Kutokana na majukumu ya kichungaji
tuliyo nayo mara nyingi utaona au tumeona Muda ukiwa kama haututoshi kwa kweli
kutimiza majukumu tuliyo nayo, kunaendana pia na jinsi tunavyoutumia muda mbona
wengine wanati miza majukumu yao pamoja na muda
kuonekana kama usiotosheleza? Kila wiki una
masaa 168,na kila siku masaa 24 kwa wastani unaweza kuyagawa masaa 24 katika
maeneo makuu matatu
1)
Masaa nane ya kazi
2)
Masaa nane ya kulala
3)
Masaa nane ya shughuli nyingine kama kula, mazoezi, kusafiri, kutembea na kutafuta
mahitaji mengine jihoji kuwa unayatumiaje masaa 24? Unawajibika kujipanga au
kupanga ratiba kwa ujumla utaona kuwa wachungaji wana muda wa kutosha sana lakini hawajui
kutumia muda ipasavyo na hivyo wengi hupoteza muda tu mtu mmoja alijaribu
kufanya utafiti na kugundua kuwa kwa wastani wachungaji hutumia kipindi chao
cha kuishi cha miaka 70 kwa mtindo huu ufuatao
- Miaka mitatu
ya elimu
- Miaka
nane ya mzaha
- Miaka
sita ya kula
- Miaka
mitano ya kusafiri
- Miaka
mine ya kuongea
- Miaka
kumi na nne ya kufanya kazi
- Miaka
mitatu kujisomea
- Miaka
ishirini na nne ya kulala
- Miaka
mitatu ya kupoteza muda
Unapofanya tathimini utagundua kuwa muda mwingi
unapotea bure bila jambo la maana kufanyika kwa msingi huo basi ni muhimu
kuhakikisha kuwa unatumia nyenzo ambazo zitaweza kurahisisha kazi kazi pia
unaweza kujaribu kupunguza na kugundua vitu vinavyopoteza muda kama vifuatavyo
- Punguza ndoto za
mchana yaani kuwaza mambo ambayo unataka kuyatimiza kama
kumaliza matatizo yako n.k
- Punguza kutokuwa na
malengo kujifanyia shughuli alimradi siku iende tu au shughuli za zimamoto
- Punguza mazungumzo
ya kijamii na utani yasiyo ya msingi sana
- Hakikisha kuwa
unakabidhi watu majukumu ambao wanauwezo wa kuyatimiza na kuwa
hayatakugharimi wewe kushughulikia kila kitu
- Kutokumalizia kazi
fulanifulani si vema kwa mchungaji jiepushe sana na kuhairisha kazi za
kufanya.
C; Umuhimu
wa kupanga ratiba
Ili
kuepuka usumbufu usio na msingi ni muhimu kwa mchungaji kuwa mtuzaji wa muda
kwa kujipangia ratiba uwe wakili mzuri wa muda 1Koritho 4;2
Uwe na malengo usijifanyie kazi hovyo hovyo
Ni muhimu kujipangia ratiba panga kuanzia na mambo
ya msingi na yanayofuatia chagua mambo ya msuingi kila iitwapo leo amabyo ni
muhimu kwako kuyatekeleza, jipangie malengo na muda wa kuyakamilisha malengo
yako, ruhusu wakati mwingine kuingiliwa kwa ratiba yako hayo ni mambo ya
kawaida, jifunze kusema hapana kuna mambo amabyo kama unaona haya kuyasemea
hapana yanaweza kukugharimu muda, panga muda kwa familia yako, jiwekee ratiba
itakayozingatia afya yako.
D ; Kuwaandaa washirika kwa kazi ya huduma
Mchungaji
jukumu lako kubwa ni kuwaandaa washirika
kwa ajili ya utumishi Training jambo hili linawasumbua wachungaji wengi sana
lazima utofautisha washirika wa mwaka huu na mwaka juzi kwa maana ya kuwa na
madarasa ya wokovu yanayolingana na ukuaji na uzoefu katika utumishi wakipitia
mafundisho ya maalumu ya kazi mbalimbali
Kumbuka kuwa kanisa sio
1)
Kituo cha mafuta ya gari hapo si mahali ambapo
watu wanakuja na mchungaji anawahudumia kasha wanakwenda zao ni lazima wafanye
kitu
2)
Kliniki mahali ambapo watu wanazaliwa
wanaangaliwa afya zao kasha wakikuwa wanaondoka
3)
Ukumbi wa sanaa watu wanakuja wanapata burudani
kasha wanaondoka zao msanii mkuu ni mchungaji
4)
Kiwanja cha michezo ambapo watu huja kutazama
michezo lakini wao si wachezaji kasha huenda zao
5)
Betrii inayochajiwa ambapo hutumika huko na
kasha huja kuchajiwa tena washirika ni lazima wazalishe lazima watumike kanisa
lolote ambalo limekufa washirika wake huwa hawana la ziada la kufanya zaidi ya
kuwa watazamaji leo washirika wengi hata kushuhudia hawawezi
6)
Ondoa dhana potofu kuwa ni mchungaji tu mwenye huduma au karama au
kufikiri kuwa ni wachache tu wenye huduma au karama au waliojaaliwa kutumika
7)
Wakumbushe wajibu wa kibiblia wa kuhudumu ambapo
biblia inaamini kuwa kila mtu ana karama Efeso 4;7 1Petro 4;10 na kuna tofauti
za huduma 1Koritho 12;4 Warumi 12;6,na kuwa kila karama inahitajika Efeso 4;16
na kuwa kila mshirika ana jukumu la kuitumia karama aliyonayo 2Timotheo
1;6.1Timotheo 4;14.
8)
Washiriksa wakumbushwe kuhubiri na kufundisha
kwa usahii, wafanye huduma na kupata uzoefu, watambue uwezo walionao, na wawe
mfano wa kuigwa
9)
Tumia njia mbalimbali za kufundisha washirika
zikiwemo semina, vitendo, kuwatambua, kuwatumia viongozi waliojifunza wape
majukumu, weka wazi majukumu yao chagua watu kwa ajili ya majukumu husika
Falsafa ya mwandishi wa somo;
“Uchungaji ni
jukumu lililo zito sana wenye akili hulikimbia,Wajinga hulikimbilia,Wapumbavu
huligombania Bali wanyenyekevu na wenye hekima
husema Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana nisiye na faida na iwe kwangu kama upendavyo”- Kamote.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima