Warumi 8:38 -39. “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala
uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo,
wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala
yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa
Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Utangulizi:
Nick Vujicic ni moja ya walemavu ambaye alizaliwa akiwa hana miguu
wala mikono na wataalamu wa kitabibu walishindwa kuelewa sababu kuu ya ulemavu
wake na hata namna ya kumtibu, lakini kwa sasa amejipatia umaarufu mkubwa sana
duniani kutokana na bidii kubwa aliyo nayo na mafanikio makubwa sana katika
maisha akiwa hana viungo hivyo muhimu yeye mwenyewe anasema Namnukuu “I was born without arms or legs and given no
medical reason for this condition. Faced with countless challenges and
obstacles, God has given me the strength to surmount what others might call
impossible.” “Nalizaliwa pasi na mikono wala miguu na sikupewa
sababu za kitabibu za kuzaliwa hivyo, Nimekumbana na changamoto nyingi na
vikwazo, Mungu amenitia nguvu kupambana na hali ngumu ambazo wengine
walizishindwa” Ni mwanzilishi wa shirika liitwalo Life without Limbs na Mwinjilisi mkubwa sana Duniani na pia ni
Motivational speaker ambaye aliweza
kupitia vikwazo na magumu na kuvishinda kwa nguvu na tumaini lililo katika
Kristo Yesu.
Siri kubwa ya mafanikio ya
Mlemavu huyu Duniani ni “Mungu alimtia
Nguvu” Kumbe kwa Mungu hakuna lisilowezekana, tunaishi katika misuguano na
kujikuta tumezingirwa na mipaka pande zote dunia ikikulazimisha kusalimu amri
na kuishia hapo ulipoishia au hapo ulipokatia tamaa kwa sababu hujatambua chanzo cha nguvu zako, kwa hiyo dunia na mazingira
na vikwazo vimekukwamisha hapo ulipo umeambiwa haiwezekani, haitowezekana,
huwezi lolote, hustahili kitu hutoweza, ndugu zako walishindwa, Mfupa
uliomshinda fisi wewe mbwa utauweza wapi.
Siri ya mafanikio.
Siri ya mafanikio ya watu kama
kina Nick Vujicic na wengineo ambao tunawasoma katika maandiko
ni NGUVU ZA MUNGU nyuma ya maisha
yao, Maandiko ni ufunuo wa Nguvu za Mungu, unaposoma na kuona shuhuda za watu
kama kina Yusufu kutoka gerezani na kuwa mtu mwenye mamlaka kubwa duniani ni
Matokeo ya Nguvu za Mungu, Unaposoma habari za kusisimua za kina Daniel na
Hekima kubwa walizokuwa nazo na uwezo mkubwa katika kupambanua mambo ni kuwa
siri kubwa ni Nguvu za Mungu, Roho wa Mungu alikuwa juu yake, hii ndio siri
iliyowafanya waonekane kuwa ni wa kipekee.
Kila mtu Duniani Mungu alimuumba
kwa kusudi, na moja ya kusudi la kuumbwa kwako ni ili ufanikiwe na kuwa Baraka
kubwa kwa wengine pia, Lakini ni nguvu ya Mungu kiasi gani unayohitaji ndiyo
itakayoamua hatima ya maisha yako, wengi tunaishi maisha yenye mipaka Lakini
Mungu hakukusudia iwe hiyo! Hata kidogo, Mungu ametupa Nyenzo ya kutusaidia
kufikia kiwango kikubwa na cha juu cha mafanikio Nguvu hizo ni Roho Mtakatifu.
·
Mwanzo
41:38-40 “Farao
akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani
yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana
mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa
neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko
wewe.”
·
Daniel
5:10-12 “Basi
malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba
ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako
zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike. Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye
roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru
na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako,
naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na
Wakaldayo, na wanajimu; kwa kuwa roho
njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na
kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo,
ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha
tafsiri.”
·
1Wakoritho
2:4-5 “Na
neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi
akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya
wanadamu, bali katika nguvu za Mungu”.
Paulo hakuhubiri Falsafa,
hakutumia ushawishi wa kiakili lakini alifanikiwa sana katika injili kuliko wote
kwa sababu alikuwa na Nguvu za Mungu
Kuishi bila
Nguvu za Mungu ni kujiweka katika hatari kubwa sana, lakini ili tuweze kuwa
washindi ni lazima tuishi katika uwepo na nguvu za Mungu, Mungu alituleta
Duniani kama watu maalumu, alitukomboa ili tuwe Makuhani na Wafalme na watawala
wa Dunia Ufunuo 5:10 “ukawafanya kuwa
ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Mwanadamu
ni kiumbe cha thamani sana, Mungu amewadhimisha wanadamu kuliko malaika lakini
ili tuweze kuwa na mafanikio Duniani na kuitawala kama wafalme na makuhani
hatuna budi kujiungamanisha na Nguvu za Mungu, Mungu hafurahii kutuona tukiishi
kwa mipaka kwa ujumla hatukuumbwa ili tuje kuteseka na kufungiwa duniani bali
Mungu alikusudia tuitawale dunia na kila kilichomo Haya yanawezekana tu kama
tutajiachilia katika nguvu za Mungu na Roho wake hakuna jambo
litakaloshindikana kwetu Zekaria 4:6-7.
“Akajibu
akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa
uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. Nani
wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye
atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema,
neema, ilikalie.” Unaweza
kuona sasa kama tunasumbuka katika Dunia hii, tumejawa hofu, tumejawa kukata
tamaa, tumepoteza ujasiri, tunalia, tunaugua, tunaonewa kuna kitu hakiko sawa
ni kwamba hatujatambua kuwa sisi ni akina nani na Mungu ametuandalia Nini? Yesu
alianza kupata umaarufu mkubwa mara moja tu alipokaliwa na Roho wa Mungu na kumruhusu
aongoze maisha yake
Luka 4:1 “Na Yesu, hali
amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku
arobaini nyikani” 14 “Yesu akarudi kwa
nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.”
Yesu anarejea akiwa amejaa nguvu za Mungu, na tangu tukio hili utaweza kuona umaarufu
wake ulienea katika nchi zote za kandokando ya Israel, Wanafunzi wa Yesu
walikuwa waoga walijifungia chumbani kwa siku kadhaa lakini alipokuja Roho
Mtakatifu mambo yalibadilika waliupindua ulimwengu, Bila Roho Mtakatifu, bila
neema na bila nguvu za Mungu tutaendelea kuwa wanyonge na kuishi katika kiwango
cha chini cha maisha bila mafanikio na maisha yenye mipaka mingi.
Katika Warumi 8:38-39 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba,
wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala
yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga
na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Paulo Mtume
anazungumza kwa ujasiri unaotokana na uzoefu wake akikazia kwa msisitizo mkubwa
sana wa imani ya kitume kuwa yeye sasa kutokana na Mambo ambayo Mungu
amemfunulia, kutokana na jinsi Mungu alivyoufunua upendo wake kwetu, yeye
pamoja na wengine wote wenye kuamini Hakuna kitu kinaweza kututenga na upendo
wa Kristo, Hili halitokani tu na ufunuo mkubwa alioupata bali kazi kubwa ambayo
Mungu amewatendea wanadamu, kwa kutuchagua, kwa kutufanya kuwa wana wake,
ametambua kuna usalama Mkubwa katika Kristo na kuwa ni vigumu sana jambo
lingine lolote kupingana na kusudi la Mungu, hivyo yote yanayoogopewa na
wanadamu hayawezi kuwa mpaka wa kututenganisha na Mungu
·
Kifo
hakina ubavu – Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya
nguvu yake
·
Maisha
hayana ubavu– Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya
nguvu yake
·
Mamlaka
hazina ubavu– Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya
nguvu yake
·
Serikali
hazina ubavu– Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya
nguvu yake
·
Malaika
au mashetani – Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu
ya nguvu yake
·
Mamlaka
na falme– Haiwezi kuwa tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya
nguvu yake
·
Mambo yaliyopo
yaani sasa na yajayo– Haiwezi kuwa
tishio la kuharibu kusudi la Mungu kwa sababu ya nguvu yake
Kama Nick
ameweza kufanikiwa na hakuzaliwa akiwa na mikono wala miguu, bali kwa nguvu za
Mungu ameweza kuwa mtu maarufu Duniani na kufanikiwa katika kuwatia moyo wengine
wote, wanaofikiri kuwa wao si kitu, wanaofikiri kuwa hawawezi, Maandiko
yanatutaka tuinue macho yetu na kumuangalia Mungu Nguvu zake zinatosha
kutupeleka katika level nyingine na kutufanya tufanye mambo yasiyokuwa ya
kawaida, Hakuna sababu ya kukata tamaa, tuitafute Nguvu ya Mungu, tuutafute
upako na kufanya kazi zetu kwa bidii hakuna kitakachoweza kusimama na kuzuia
kusudio la Mungu katika maisha yako, usikubali kukatishwa tamaa, usikubali hata
kujikatisha tamaa, usikubali maneno yaliyonenwa juu yako, wao sio Mungu yuko
Mungu mwenye uweza usio na mipaka hakuna wa kukuwekea mpaka Mungu amekupa uhuru
wa kuyafurahi maisha katika nguvu zake, kaa katika hizo na utafurahia sana.
Ziko sababu za kuishi maisha yasiyo na mipaka kutokana na upendo mkubwa sana wa
Mungu wetu na mambo ambayo ametukarimia.
1.
Hakuna
hukumu ya adhabu Rumi 8:1
2.
Roho
wa aliyemfufua Kristo anaishi ndani yetu 11
3.
Roho
anatuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa 26
4.
Mungu
yuko upande wetu 31
5.
Aliweza
kumtoa Yesu kwaajili yetu 32
6.
Hakuna
wa kuwashitaki wateule 33
7.
Sisi
ni washindi na zaidi ya kushinda 37
Nakuombea Mungu
akuvike Nguvu zake ili usiishi katika mipaka uliyowekewa au kujiwekea Bali ujae
nguvu za Mungu na uweza wake
Na. Mkuuwa wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote.