Ujumbe: Mwanadamu ni nini hata
Umkumbuke?
(“What is Man that You Are Mindful of Him?”).
Ni muhimu kwetu kwa kila mmoja wetu kujiuliza, kuwa
katika akili zetu ni nani tunampa kipaumbele kikuu kila siku? Tunaweza kuhisi kuwa
wengi wa wale tunaowapa kipaumbele kwanza wanaweza kuwa ni wana familia zetu,
wapenzi na marafiki na labda Mungu!
Au kama kuna mtu mwingine
uneyeweza kumpa kipaumbele zaidi anaweza kuwa mtu unayemchukia, adui yako anayekusumbua
na kukunyima raha, Kwa kawaida tunapenda kufikiri vile vyenye umuhimu katika
maisha yetu na vile visivyona umuhimu au mguso tunaweza kuvipuuzia na kuvitupa
kando. Ni uwazi ulioje kuwa kuweko kwa
Mungu kumekuwa ni kama dhana inayofikiriwa kuwa ni ya kusadikika tu, wengi wetu
kwa ndani sana tunaweza kufikiri kuwa Mungu hayuko na hajishughulishi na
chochote kuhusu wanadamu na hususani tunapopitia nyakati ngumu tunafikiri kama
Mungu yupo kweli angelitazama hili bila kushughulika nalo?
Wagiriki wengi walikuwa hawaamini
katika Mungu na hivyo walikuwa na miungu mingi dhana kuhusu Mungu haikuwa
halisi katika maisha yao na hivyo waliabudu miungu mingi ili kutafuta msaada na
kutafuta kuwezeshwa na miungu hiyo baadhi ya miungu yao ni kama hii
1.
Aphrodite alikuwa Mungu wa Mapenzi
2.
Apollo alikuwa Mungu wa Music na
Uponyaji
3.
Ares alikuwa Mungu wa Vita
4.
Athena alikuwa Mungu mke bikira na
mungu wa Hekima
5.
Hermes alikuwa Mungu wa Ujumbe
Pamoja na miungu kadhaa wa kadhaa
Biblia inatufundisha kwamba Mungu tunayemuabudu yeye ni wa
tofauti kabisa ni Mungu anayemjali mwanadamu na kujishughulisha naye bila
kujali hali yake, kwamba ni msomi au mjinga ni masikini aua tajiri, mweusi au
mweupe ni wahali ya juu au ya chini, ni mwanamke au mwanamume, ni mtakatifu au
ni mwenye dhambi, Mungu anapendezwa na Mwanadamu sana, Watakatifu
waliotutangulia waliona upendo huu wa Mungu kwa ndani sana akijishughulisha na
wanadamu kwa namna ya kupita kawaida Katika tafakari zake mfalme Daudi
alifikiri hivi? Na kujiuliza maswala haya hasa baada ya kugundua namna Mungu
anavyomjali Mwanadamu
Waebrania 2: 5-8 “Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao
tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema, 6. Mwanadamu
ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie? 7. Umemfanya
mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu
ya kazi za mikono yako; 8. Umeweka vitu
vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake
hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote
kutiwa chini yake.”
Katika
Mistari hiyo hapo juu kuna maswala Matatu Muhimu ambayo Mungu anamfanyia
mwanadamu kuonyesha namna alivyomthamini “Hata umkumbuke” “Hata Umwangalie”
“Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako” haya yanadhihirisha uthamani na upendo
mkuu wa Mungu wetu kwetu.
1.
Mungu humkumbuka Mwanadamu “Mindful of Him”.
Biblia inaushahidi mwingi
unaodhihirisha kuwa sisi ni wa thamani machoni pa Mungu na kuwa Mungu
anatuwazia sisi kama kipaumbele chake hata kama sisi hatumjali na kumuheshimu yeye alituumba kwa mfano wake alitupenda mno Zaburi 8:3 Isaya 43:4. Biblia
inathibitisha kuwa Mungu hajatuacha wala hatatusahau, anatuhurumia na kuwa
ametuchora katika vitanga vya mikono yake Isaya
49:15-16 Kama ilivyongumu kwa Mama kumsahau mtoto wake anyonyaye ndivyo
ilivyo na kwa Mungu wetu.Ndugu yangu Mungu hajakusahau Mungu hajakutupa Umejaa
katika wazo la Mungu.
2.
Mungu humwangalia Mwanadamu “Care of Him”
Licha ya Mungu kujawa na binadamu
katika akili zake ni muhimu pia kufahamu kuwa Mungu anakuangalia!, anajali Mungu
anapokuangalia anajisikia kukufanyia mambo makubwa sana anaguswa na maumivu
yako na huzuni ulizonazo na anajali Luka
7:11-16 Hataweza kukuachia hata umezwe na huzuni na jaribu kuliko uwezo
wako ataingilia kati na kuleta faraja Kama alivyo mfanyia mjane huyu katika
Luka na watu wakakiri kuwa Mungu amewaangalia watu wake tunaye Mungu ambaye
huangalia.
3.
Umemtawaza
juu ya kazi zako “ You put everything under his feet”
Mungu
ameweka kila kitu chini ya miguu yetu, ametupa kutawala, ametiisha hata malaika
hutuhudumia mwanadamu ametukuzwa na Mungu kwa kiwango kikubwa cha kifalme Luke
10:18-19 Mungu ametiisha kila kitu chini yetu hatupaswi kuogopa, tunapaswa
kuelewa jinsi Mungu anavyotujali, anavyotukumbuka na anavyotuangalia na uwezo aliotupa, Mungu anapendezwa na
wanadamu kuliko hata malaika, waoa wanatajwa kama roho wanaotumwa kuwahudumia
wale watakaourithi wokovu Waebrania 1:13-14. Kama ikiwa Mungu anatujali
kwa kiwango hiki………
Swali la
Kumalizia ni kuwa wewe je unampa Mungu kipaumbele? Umamuheshimu, Unamuogopa au
unamvunjia Heshima?
Mwandishi wa zaburi alikaa chini
akatafakari na kugundua kuwa mwanadamu ni sehemu ndogo sana ya uumbaji wa Mungu, ndogo mmno lakini
akajiuliza swala kwa vipi Muumba anatoa nafasi kubwa kwa wanadamu? Daudi
mwandishi wa zaburi hii alikuwa anaona kwa Mbali jinsi Kristo atakavyoacha enzi
na utukufu na vyote na kuja kumkomboa mwanadamu kwa Damu yake ya Thamani jambo
linalotudhihirishia Uthamani mkubwa sana alio nao mwanadamu, swali
Mwanadamu ni nani hata umkumbuke?
Kamwe hatuwezi kutambua uthamani wetu kama Mungu sio Kipaumbele cha Maisha yetu
Kadiri tunavyojifunza kuhusu Mungu ndivyo tunatambua uthamani wetu na kusudi la
kuweko kwetu duniani.
Yeye aligharimika mno kwaajili
yetu Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu” Biblia
ya kiyunani ingesomeka hivi Katika namna isiyoweza kuelezeka Mungu aliipenda
Dunia iliyojawa na uasi na udhalimu na desturi zenye kila aina ya machukizo
“Cosmos” hata akamtoa mwanae wa Pekee, Maisha yetu yamegharimu Damu ya Yesu
“Wewe sio matokeo ya vile watu
wanavyosema wewe ni matokeo ya vile Mungu anavyosema”
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.