Jumapili, 27 Desemba 2020

Familia takatifu !

Andiko la Msingi: Luka 2:41-49 “41. Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; 43. na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. 44. Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; 45. na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46. Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 48. Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.49. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa mara baada ya sikukuu ya krismas Kanisa huwa linasheherekea siku ya familia takatifu, Tayari Yesu Kristo amezaliwa na tayari imekuwa familia kamili, Yenye baba, Mama na mtoto, hii sasa ni familia ya watu wanaomcha Mungu, Familia ndio asili ya kila kitu, hakuwezi kuwa na taifa pasipo familia, hakuwezi kuwa na kabila pasipo familia, hatuwezi kuwa na viongozi wazuri wasiotoka katika familia, hatuwezi kuwa na watetea haki, waamuzi, wanamapinduzi,  manabii, na wachungaji ambao kwa namna moja ama nyingine hawajatokana na familia, hivyo familia ndio taasisi ya kwanza kabisa kabla ya kuweko kwa taasisi nyingine, Kwa msingi huo basi ili tuweze kuwa na kila jambo zuri, lazima jambo hilo lianzie katika familia, Leo tutachukua muda kujifunza namna familia ya Yesu, ambayo ilimjumuisha Mariamu, mama yake na Yusufu Baba yake mlezi na kijana mtoto Yesu. Hii ilikuwa ni familia ambayo imeleta Baraka kubwa sana duniani na hivyo kuna mambo ya kujifunza

1.       Hakuna familia isiyokuwa na Changamoto.

Ni muhimu kufahamu kuwa kila familia inapitia changamoto zake, Familia ya Yesu ilipitia changamoto za aina mbalimbali, Lakini kutokana na kumtanguliza Mungu, Mungu aliwatoa katika changamoto hizo:-

 

a.       Walipitia katika umasikini uliokithiri ;-

 

Kabla ya Yesu kuzaliwa ni wazi kabisa kuwa Yusufu na Mariamu hawakuwa na uchumi mzuri, walikuwa na ukata, usafiri waliotumia ulikuwa usafiri wa punda,  sadaka walizokuwa wakitoa Hekaluni ilikuwa ni njiwa wawili ambayo ni sadaka ya chini mno iliyotolewa na watu waliokuwa masikini, Hata hivyo umasikini huu haukuwa sababu ya manung’uniko kwao, wala sababu ya kuiba, au kutapeli, au kukopa na kutokurudisha, au kuomba omba, waliweza kuvumilia na kuendelea kumtegemea Mungu huku wakifanya kazi kwa bidii, Maisha yao yalibadilika baadaye baada ya sadaka ya Mamajusi waliotoa dhahabu, uvumba na manemane hivyo ndio viliweza kuibadili hali ya familia hii iliyomtegemea Mungu, Wakristo lazima tujifunze kuwa wavumilivu na kuusubiri wakati wa Mungu wa kutufanikisha bila kupitia short cut kwani Mungu ana majira na nyakati za kutubariki, Familia hii ilivumilia magumu na changamoto walizozipitia mpaka Mamajusi walipotoa zawadi zilizowatajirisha sana ona

Mathayo 2:10-12 “10. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. 12. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”


Tunaimba kwamba mjini mwaka mfalme Daudi palikuwa zizi nyoge... Yesu alizaliwa katika hali ya unyonge lakini maisha ya uvumilivu na subira ilibadilisha maisha ya familia yake na wakawa sasa wana uwezo wa kwenda Misri na kuishi huko kwa muda wakijikimu maisha yao, Lazima kila familia iwe na uvumilivu, usijilinganisha na watu wengine mtegemee Mungu, na Mungu atawabariki

 

b.      Walimsikiliza Mungu (Walitii mapenzi ya Mungu):-

 

 

Familia takatifu lazima iwe na uwezo wa kumsikiliza Mungu, Kumsikiliza Mungu ni kulisikiliza neno lake, kusikiliza watumishi wake na kuhudhuria ibada, Familia hii iliweza kudumu kwa sababu ilikuwa familia ya wazazi ambao wote walikuwa na uwezo wa kumsikiliza Mungu, kuliko kusikiliza maneno ya watu wa mtaani, Yusufu alipoona Mariamu ana Mimba biblia inasema aliamua kumuacha kwa siri! Unaona lakini mapema sana Malaika wa Bwana alimuonya Yusufu asimuache mariamu mkewe, ona katika

Mathayo 1:19-21 “19. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

Unaona Kama Yusufu angekuwa ni mwenye kusikiliza maneno ya watu wa mitaani ndoa yake ingevunjika mapema na familia hii isingekuwa Baraka kwa dunia, Familia takatifu ni lazima iwe familia inayosikiliza maneno ya Mungu na kufuata uongozi wa Mungu, ni kwa kujua unyenyekevu na usikivu wa Yusufu, Mungu alisema na Yusufu tena kupitia malaika wake ili kukimbilia Misri na kuyalinda au kuyatunza maisha ya Yesu asiuawe na Herode ona 

Mathayo 2:13-14 “13. Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;

Unaona ni maisha ya usikivu wa Yusufu ulioweza kumfanya Mariamu na mtoto Yesu kuwa salama kule misri na kuepuka kifo kutoka kwa Herode, Leo hii familia nyingi zinaharibika na watoto wanaenea mitaani wakipoteza muelekeo, au hata wakikosa kusoma kwa sababu ya wazazi waliokosa usikivu kwa Mungu na kwa wazazi, vijana wengi wanaishi vile wanavyojisikia na kujibu kile wanachojisikia na hata wazazi wamekosa kuwa mfano bora kwa kuigwa na watoto wao kwa sababu ya kutikumcha Mungu, Yusufu, na Mariam na Yesu walikuwa ni familia ya mfano katika kumcha Mungu.

 

c.       Walimuabudu Mungu;’-

 

Mstari wa msingi tuliousoma unasema “Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka,” Unajua maana yake nini hawakukosa ibada kuu katika hekalu lililokuwako Yerusalem, wazee wake maana yake wazazi wake kila mwaka walikwenda Hekaluni kusali na hawakuenda wenyewe walikwenda na vijana wao akiwemo Yesu, wao wenyewe walimuabudu Mungu lakini waliwafundisha watoto wao kumuabudu Mungu na kumpenda jambo hili lilijenga uhusiano mkubwa wa Yesu na Mungu baba wa Mbinguni, kiasi ambacho licha ya Yesu kuwaheshimu wazazi wake alimuona Mungu baba wa Mbinguni kuwa baba yake

Luka 2:48-49 “48. Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 49. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?

tuwafunze watoto wetu wajue kuwa japo sisi ni wazazi wao lakini wanaye baba wa Mbinguni wamsikilize, wamtiii wampende wamuabudu familia takatifu lazima wajijenge tabia ya kuabudu. Kuimba, kuomba, kusoma neno la Mungu na kuhudhuria makusanyiko ya ibada na kujifunza na kudumisha uhusiano na Mungu ni jukumu la kila familia kuhimizana na kutiana moyo, kumuheshimu Mungu.

 

d.      Walipeleka watoto shule

 

Katika desturi za kiyahudi kijana aliyefikisha miaka 12 alikuwa tayari amefunzwa kuijua Torati na kufanya kazi za kujitegemea, wengine walijivunza uvuvi, wengine ukulima, wengine ujenzi na wengine kushoma mahema kama Paulo mtume, Yesu alikuwa na ujuzi wa torati na alikuwa amejifunza ujenzi “Carpenter” hii iliwajengea watoto uwezo wa kujiamini na kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha Hivyo Yesu alijengewa kupenda kujifunza na alikuwa msikivu kwa walimu wake na alikuwa mdadisi aliuliza maswali ona

“Luka 2:45-47 45. na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46. Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.”

Familia takatifu na iliyo njema inapaswa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata Elimu nzuri, na wanakuwa na uwezo wa kujitegemea wanaweza kufanya kazi mbalimbali, na wanakuwa na ujuzi wa maadili na sheria za ukoo na familia zao, leo hii tunaona kuna mmomonyoko mkubwa wa uadilifu lakini ni kwa sababu tatizo kubwa limeanzia katika ngazi ya familia, wazazi wanapaswa kuwa kitu kimoja na kuhakikisha kuwa wote kwa pamoja wanawajengea watoto uwezo wa kijitegemea ili watoto hao wasigeuke kuwa mzigo kwetu endapo hatutawaandaa vema Yesu alijengewa uwezo mkubwa sana na hatimaye akawa Mwalimu mwema alikuwa na wanafunzi 12 maalumu na wanafunzi wengine wengi, aliuitwa RABBI yaani Mwalimu, uwezo wake mkubwa wa kufundisha ulitokana na uwezo wake mkubwa wa kujifunza, kawaulize walimu hakuna Mwalimu mzuri ambaye sio mwanafunzi mzuri, Lazima tuwajengee uwezo wa kielimu watoto wetu

 

e.      Waliwalea watoto wao katika uadilifu

 

Tunasoma hivi katika Luka 2:52 “Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Swali jepesi la kujiuliza je watoto wetu leo na familia zetu leo zinampendeza Mungu na wanadamu? Tunaambiwa Yesu alizidi kukua akiwa na hekima lakini vilevile akimpendeza Mungu na wanadamu, Je tunampendeza Mungu na wanadamu, hii haiwezi kutokea kama hatutakuwa chuo cha maadili kwa vijana wetu, ni muhimu kuwafunza watoto wetu, na kuwalea katika uadilifu, tikifanya hivi tutakuwa na watoto wenye muelekeo thabiti katika taifa letu, leo hii tujnashuhudia mmomonyoko mkubwa waa maadili lakini sababu kubwa ni kuanzia ngazi ya familia kutokujali uadilifu na mwenendo mwema kwa watoto wetu.

 

f.        Walijali Ndugu jamaa na kule walikozaliwa/kulelewa

 

“Human being is a social being” Mungu hakutuuumba tuishi kama kisiwa, aluiposema si vema mtu huyu awe peke yake alimaanisha wanadamu tunahitajiana wakati mwingine ili uweze kujengeka unapaswa kuwa na muda wa kusikiliza wengine na hapo ndipo tunapoweza kujengwa na kukua au kutiana moyo, Mariam alipopata ujauzito wa ajabu malaika alimueleza kuwa jamaa yako  Elizabeth pia ana mimba ya mtoto wa kiume, kusudi kubwa ilikuwa ili Mariamu aweze kutiwa moyo kustahimili kile kilichomtokea hivyo Mariamu alimtembela Elizabeth ona

Luka 1:36-44 “36. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; 37. kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 38. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake. 39. Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, 40. akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. 41. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; 42. akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. 43. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? 44. Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.


Unaoma Mariamu anamtembelea Elizabeth anajifunza mambo mablimbali kutoka kwa mwanamke mzee mwenye uzoefu wa kutembea na Mungu, na hivyo anajifunza mambo mbalimbali Mariamu kutoka kwa watu wa rika linguine je leo hii wanawake watu wazima huwafunza wanawake vijana ? je watu hutembeleana nyakati  za leo? Je watu hutembelea kule walikozaliwa au kulelelwa familia zenye upendo hutembeleana Yesu pia alitembelea Nazareth kule alikolelewa na kuwafundisha mambo makubwa ya Mungu ona

Luka 4:16-21 “16. Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.17. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18. Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19. Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.


Yesu alienda Nazareth kule alikolelewa, Ni muhimu kukumbuka na nyumbani, watu wengi sana wanapofanikiwa hawakumbuki nyumbani, watu wengi wa Tanga waliosoma zamani walitawanyika huko na huko na kusaidia watu wengine na kuwaelimisha lakini waliisahau Tanga,  wabunge wengi  hukumbuka nyumbani wajkati wa kupiga kura, Yesu pamoja na umaarufu wake wote na alikuwa Mungu hakuweza kusahau kule alikolelewa, tunawashangaa wachaga tu wanapoenda nyumbani msimu wa sikukuu, hebu na sisi tujifunze na kukumbuka kuenda kule tulikolelelwa na kukulia na kuwa Baraka kwao pia

Tuwe tayari kujitoa kwa wengine

Kusudi kubwa la Yesu kuzaliwa ni ili awaokoe watu wake na dhambi zao Yusufu alielezwa hili mapema ona

Mathayo 1:20-21 “20. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.”


Yusufu alielezwa mapema kuwa Yesu ni mwokozi, familia ina wajibu wa kulea vijana na kukuza viongozi ambao watakuwa faida si kwaajili yao tu bali kwaajili ya ulimwengu mzima Mariamu pia alijulishwa kuwa mtoto wake sio wake pekee bali amewekwa kwaajili ya wenginona

Luka 2:34-35 “34. Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. 35. Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.

  
Ilikuwa wazi kuwa Mungu aliwaamini Mariamu na Yusufu kuwa walezi wa kiongozi mkubwa ambaye atakuwa Baraka kubwa kwa ulimwengu ni mwokozi wa ulimwengu, kama familia hatuna budi kuwatunza wanafamilia wote na kuwasaidia kutimiza ndoto zao ili makusudi yote ya Mungu yapate kutimizwa ndani mwao, nani ajuaye kuwa mtoto uliyembeba ni Raisi ajaye, ni Mwalimu ajayem, ni daktari ajaye, Mungu ana makusudi na kila aliyezaliwa na hakunanayezaliwa kwa bahati mbaya hivyo tuendelee kuwa na ustawi katima familia zetu ili Mungu ajiinulie watumishi wake kutioka katika familia zetu watakaokuwa Baraka kwa wengine

Yohana 13:17 “Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda!”

Bwana Mungu awabariki na kuwafadhili tunapoadhimisha siku ya familia takatifu katika jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu amina

Na. Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!

0718990796

Ijumaa, 25 Desemba 2020

Mfalme wa Amani!


 Isaya 9:6-7 “ Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.“      


Utangulizi:

Leo ni sikukuu ya Christmas wakristo kote nchini wanaungana na waktristo wote duniani katika kuadhimisha siku hii maalumu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Masihi, na mwokozi wa ulimwengu, Yesu Kristo kulikotokea huko Bethelehemu Israel zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Katika siku hii muhimu ni muhimu kwetu tukajikumbusha mambo kadhaa kumuhusu Yesu Kristo.

Andiko letu la Msingi  Isaya 9:6-7 “ Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.“

Kimsingi yalikuwa ni maneno ya nabii Isaya aliyetabiri kuzaliwa kwa mwokozi wa ulimwengu miaka  zaidi ya 700 kabla ya kuzaliwa kwa  Yesu, Isaya anamuona masihi kama kiongozi mkubwa sana na mwenye uwezo mkubwa wa kutatua matatizo na changamoto mbalimbali walizonazo wanadamu, Nyakati za Biblia wafalme ndio ambao walikuwa wanatakiwa kutatua changamoto zozote zilizowakumba watu wao na walipaswa kuwatatulia matatizo yao na kutioa ufumbuzi ona mfano

2Wafalme 6:24-30 “Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha. Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni? Mfalme akamwambia, Una nini? Akajibu, Mwanamke huyu aliniambia, Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu tutamla kesho. Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake. Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake.

unaweza kuona kwa hiyo kuwa mfalme halikuwa jambo rahisi, ilikuwa ni lazima uwe na uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu, hata leo viongozi wakubwa wanapotembelea maeneo mbali mbali huzomewa risala na kuelezwa changamoto kubwa mbalimbali zinazowakabili wananchi na wanatakiwa kuzitatua, hapo moja ya wafalme alishindwa kutatua changamoto na kuamua kufunga na kuomba kwa kuvaa magunia maana yake tatizo lilikuwa kubwa sana

Mungu alizungumza na manabii kuwa atakuja kiongozi mkubwa sana atakayetatua changamoto mbali mbali za watu wake sio katika Israel tu bali dunia nzima huyu ndiye masihi, tunapoadhimisha kuzaliwa kwake leo tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu ametupa kiongozi mwenye uwezo wa kutatua changamoto za aina mbalimbali ulimwenguni na kwa wanadamu wote na huyu si mwingine ni Yesu Kristo.

Isaya anamuelezea kiongozi huyu kuwa ni mwenye uwezo na mamlaka kubwa  na kuwa atatua changamoto nyingi zinazowakabili wanadamu na moja ya changamoto kubwa inayowakabili  wanadamu ni kukosekana kwa amani na utulivu mioyoni mwao na ndio maana Yesu anaitwa Mfalme wa Amani, kwanini mfalme wa amani

Ni muhimu kufahamu kuwa tunapozungumzia amani hii inayozingumziwa katika maandiko;-

Tunazungumziia ustawi, utulivu starehe amani na mafanikio makubwa ya mwanadamu ambayo asili yake ni Mungu, Amani hii ilikuwepo katika bustani ya Eden kabla ya anguko la mwanadamu, lakini baada ya anguko la mwanadamu amani hii ilitoweka Neno linalotumiska kuielezea amani hii katika lugha ya kiebrania ni SHALOM, neno shalom maana yake ni amani na ustawi na mafanikio ya kiunghu katika Nyanja zote, Waaarabu wanatumia neno SALAM,  kwa kiaramu linatumika neno SALEMI, ni maneno yanayofanana sana katika lugha ya kiebrania, kiarabu na Kiswahili, kwa Kiswahili tunalo neno SALAMA  ni hali ya amani, ni hali ya kuwa mbakli na masumbufu, ni hali ya kuwa na utulivu, Daudi alipigana sana vita katika maisha yake yote mpaka Mungu akamuita mtu wa Damu, Lakini mwanaye Suleimani hakukuwa na vita wakati wake, SULEMANI, SOLOMON maana yake ni utulivu na ustawi,  Yerusalem maana yake ni mji wa amani, Dar es Salaam maana yake ni bandari ya amani, jina la mji wa mzizima Dare s Salaam lilitolewa na sultan Baraghash aliyekuwa anatawala Zanzibar na pwani na alitoa jina hilo kwa mji wa mzuizima kwa sababu aliamini badari hii ni mahali salama mno na patulivu

Isaya anazungumzia kuwa masihi anazaliwa duniani kwa kusudi na malengo ya kuleta utulivu kwa wanadamu, utulivu huu ni ustawi wa mwanadamu katika Nyanja zote  na ndio maana siku Yesu alipozaliwa malaika waliimba wimbo huu  kuonyesha kuwa kiongozi mkubwa mwokozi wa ulimwengu atakayetatua matatizo na kuleta majibu na ufumbuzi wote wa mwanadamu amezaliwa na atatoa amani kwa watu wote atakaowakubali

Luka 2:8-18 “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;  maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.  Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.”

Kila mtu anayemwamini Yesu anapewa amani hii moyoni mwake ni amani ambayo hata upatwe na changamoto ya aina gani wewe unakuwa na imani kuwa nitatoka nitatoboa kwa sababu ninaye mfalme ambaye ana uwezo wa ajabu mno anayetoa amani tofauti na jinsi ulimwengu utoavyo  amani anayotupa Kristo ni amani ya pekee nay a tofauti sana ona Yesu anatuachia mani hii Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. “              

Hatupaswi kufadhaika wala kuogopa kwa sababu Yesu ametuachia mani, na yeye ndiye mfalme wa amani, tunapoadhimisha kuzaliwa kwake leo, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaruhusu amani yake itawale katika mioyo yetu na kila mahali hatupaswi kufadhaika kwa jambo lolote tunapokuwa na fadhaa, udhaifu, magonjwa, changamoto na lolote lile ambalo linatuondolea amani yetu, tunaweza kumueleza Yesu Kristo mfalme wa amani yetu na akaweza kabisa kutatua na kushughulikia yala yanayotukanili na kutupa amani ya kweli, Nikutakie sikukuu njema ya Christmas

 

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Kupimwa kwa kazi ya kila mtu !

1Wakoritho 3:10-15 “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto” 

 

 


 


 

Utangulizi:

 

 

Ni muhimu kufahamu kuwa katika ulimwengu tulionao Mungu alimleta kila mtu Duniani kwa kusudi la kutimiza wajibu Fulani katika maisha yake,  kwa sababu hiyo  siku ya hukumu kila mmoja atatoa hesabu ya kazi au kusudi alilolifanya hakutakuwa na kisingizio kuwa hili linanipata kwa sababu ya Fulani, wote tutatioa hesabu mbele za Mungu na kila mtu atabeba mzigo wake kulingana na kazi au namna alivyotimiza  wajibu na kusudi lake duniani ona.;- 

 

Wagalatia 6:4-5 “Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. 

 

Tutajifunza so mo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

 

·         Umuhimu wa kutimiza kusudi la Mungu!

·         Mifano ya watu waliotimiza kusudi la Mungu kwa uaminifu!.

·         Faida za kutimiza kusudi la Mungu!

 

Umuhimu wa kutimiza kusudi la Mungu!

 

Kwa msingi huo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anajua ni kwa nini yuko Duniani na amekuja kufanya nini duniani, kisha pambana kwa kila namna uwezavyo kuhakikisha kuwa unafikia lengo na kusudi kubwa la Mungu jkukuleta duniani, Katika maandiko Daudi anatajwa kama mtu aliyeweza kutimiza kusudi au shauri lote la Mungu, hakuondoka duniania akiwa amebakiza kazi fulani alihakikisha kuwa anaitimiza yote yaliyomo katika moyo wa Mungu na hata alitaka kuzidisha!

 

Matendo 13:36 “Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.

 

Shauri l Mungu maana yake ni Kusudi lote la Mungu, kila mmoja anao wajibu wa kutimiza kusudi lote la Mungu, kuhakikisha kuwa unamaliza vema unahitimisha kazi yako vema, unatenda vema kusudi la Mungu, kama ni kuhubiri ni lazima tuhakikishe kuwa tunahubiri kusudi lote la Mungu, kama ni kuchunga tunachunga kwa kusudi lote la Mungu kama ni kufundisha tunafundisha kama Mungu anavyokusudia, kama ni kusoma tunasoma kama Mungu alivyokusudia, kama ni kuhubiri injili unahubiri kama Mungu alivyokusudia na kama ni kuongoza unaongoza kama Mungu alivyokusudia, Paulo Mtume alipohubiri injili aliweka wazi kuwa aliwahubiria watu kile ambacho Mungu alikusudia na hivyo  alihubiri kusudi lote la Mungu!

 

 Matendo 20:25-27 “Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.”

 

Mifano ya watu waliotimiza kusudi la Mungu kwa uaminifu!.

 

Wako watu mbalimbali katika maandiko ambao wanatajwa kuwa walitimiza makusudi ya Mungu kwa uaminifu na walitioa hesabu na kujifanyia tathimini;-

 

1.       Yesu mwenyewe alijifanyia tathimini na kutoa Ripoti kuwa amemaliza kusudi lote la Mungu, ukiacha kuwa siku ya kusulubiwa kwake alisema IMEKWISHA yaani alitimiza makusudi yote ya Mungu lakini vilevile alitoa hesabu ya kile ambacho baba alikuwa amemuagiza kukitimiza na kwa uhakikika kabisa alikuwa ameyatimiza hivyo kama asemavyo mwenyewe katika  injili ona ;-Yohana 17:1-13 “Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.  Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.  Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.”

 

2.       Paulo Mtume alihakikisha kuwa ametimiza kusudi lote la Mungu na kwa ujasiri kabisa alimuekleza Timotheo kuwa anasubiri taji yaani thawabu kubwa kwa sababu alikamilisha kile alichokusudiwa na Mungu kwa uaminifu mkubwa kwa mapambano na kwa mwendo mrefu na aliukamilisha  ona 2Timotheo 4;6-8 “Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;  baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”

 

3.       Musa alikuwa mwaminifu katika kazi yote nya Mungu, maana yake alikamilisha jukumu lake duniani, Musa alilitumikia kusudi la Mungu mpaka akasahau kifo, ilibidi Mungu amkubushe kwamba apande kwake mlimani akafe kwa sababu alikuwa mwaminifu mpaka sekunde ya mwisho Waebrania 3:5 “Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;

 

4.       Yoshua alikuwa kiongozi mkubwa jemadari na shujaa alitimiza makusudi ya Mungu hadi  mwisho na kuhakikisha kuwa anaonyesha msimamo wake hata kwa wana wa Israek kuwa yeye na nyumba yake wameamua kwa dhati kuwa watamtumikia Mungu aliye hai ona Yoshua 24:14-18 “Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana. Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine;  kwa maana Bwana, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao. Bwana ndiye aliyewafukuza watu wa mataifa yote watoke mbele yetu, naam, Waamori waliokaa katika nchi hii; basi, kwa sababu hiyo sisi nasi tutamtumikia Bwana, maana yeye ndiye Mungu wetu.”               

 

5.       Nabii Samuel aliishi maisha ya haki, hakudhuklumu mtu na mbele ya watu wote alijipambanua kuwa hakuwa na tatizo na Mtu he was a man of integrity   alihitmisha akiwa na ujasiri kuwa hakuwahi kumuonea mtu wala kumdhulumu mtu na kuwa alihitimisha akiwa na mikono safi je wewe unahitimisha vipi katika utumishi wako, je watu watakumbuka namna ulivyowaliza? Na kuwaonea na kuwatendea mabaya? Samuel alimaliza vema ona  katika 1Samuel 12:3-5 “Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za Bwana, na mbele ya masihi wake,nalitwaa ng`ombe wa nani? au nalitwaa punda wa nani? au ni nani niliye mdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi. Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote. Akawaambia, Bwana ni shahidi juu yenu, na masihi

 

6.       Henoko alikuwa mwaminifu alitembea na Mungu, mwandishi wa kitabu cha mwanzo anamfanyia tathimini Henoko na kumuonyesha kuwa mtu wa tofauti, yeye licha ya kuzaa kama wengine licha ya kuishi maisha marefu alitembea na Mungu kiasi Mungu aliamua kumfanya kuwa malaika

 

Mwanzo 5:8-14 “ Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa. Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa. Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa. Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.  Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.”

 

Hao walikuwa ni baadhi ya watu muhimu katika biblia ambao walijifanyia tathimini katika maisha yao na kutimiza makusudi ya Mungu vema, kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake vema, tukikumbuka na kuelewa ya kuwa tutatoa hesabu mbele za Mungu, katia Nyanja yoyote ambayo Mungu amekuita unapaswa kuhakikisha kuwa unafanya vema, Florence Nightingale mwanzilishi wa uuguzi duniani alisimama vema katika kusudi lake mpaka leo anakumbukwa kwa kazi yake katika siku ya wauguzi duniani,  ni vema kila mmoja akafanya vema, mainjinia wasipunje, viwango vya barabara za lami hata kwa chepe moja la kokoto, Mizani za wafanya biashara ziwe za haki, madaktari na wafanye kwa uadilifu, Walimu wafundishe kwa bidii na wanafunzi wasome kwa bidii ni wakati wa kila mmoja kutimiza wajibu wake vema ili mbele za Mungu anwanadamu tuonekane kuwa na haki na kuepuka hukumu wakati kazi zetu zitakapopimwa!

 

Faida za kutimiza kusudi la Mungu!

 

Mungu ataipima kazi ya kila mmoja wetu kama lisemavyo neon la msingi, kila mmoja anapaswa kujifanyia tathimini kama anafanya kwa ubora kile ambacho Mungu amekusudia ndani yake, katika hukumu za Mungu ziko hukumu za aina nne Mungu aatakazowahukumu wanadamu

 

1.       Present judgment – hukumu iliyoko sasa kama mtu hajampokea Yesu hajamuamini huyo kwa sasa tunapozungumza ujumbe huu amekwisha kuhukumiwa angalia Yohana 3:16-18 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.  Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.” Ili kuepuka hukumu hii basi mwanadamu anapaswa kumuamini Yesu

 

2.       Hukumu ya adhabu Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Hukumu hii ni hukumu ya aibu hukumu ya adhabu kwa kiyunani inaitwa KRI MA Mungu atafunua siri zote za uovu za wale wasiomuamini Mungu na wale waliotenda vibaya ona Muhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” Mungu atafupisha maisha au hata kazi za mtu asiyetenda vema hakikisha kuwa unatenda vema

 

3.       Hukumu isiyo ya adhabu Warumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Hii ni hukumu ya watakatifu, pamoja na neema ya kuingia mbinguni Mungu atamlipa kila mmoja sawa na kazi njema aliyoitenda kazi hizo zitajaribiwa kwa moto  kama ni ya majani, miti na nyasi itateketea na haitaleta heshima kwetu, lakini pamoja na kumuamini Yesu tunapaswa kutenda vema hukumu hii kwa kiyunani inaitwa KRINO ni hukumu isiyo ya adhabu kwa wale walio katika Kristo lakini kazi ya kila mmoja itapimwa, Yesu ataketi katika kiti cha Enzi kiitwacho Bema na kutoa thawabu kwa kazi zetu1Wakoritho 3:10-15 “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto  

 

4.       Mungu anajua, un predictable judgment hii ni hukumu isiyotabirika   Warumi 14:4 ” Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.“Yeye ni Bwana ana maamuzi yake kama unavyokwenda kwa hakimu anaweza kuamua lolote kama apendavyo mwenyewe hakuna mtu anayejua rehema za Mungu, haiyamkini bwana anaweza kutyangaza rehema kwa mtu, yeyote au hata kwa watu wote kwani utamwambia nini yeye si ndio Mungu? Ndio anaweza kuamua lolote utamfanya nini aliamua utamuuliza nini, Tufanye kazi zetu kwa bidii kwani maandiko yamesema iko thawabu kubwa sana waongoze wengi katika kutenda haki nawe utafaidika!

 

Daniel 12;3  Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.

 

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

0718990796

Upendo mwingi!

Yoahan 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”



Utangulizi:

Moja ya maagizo ya mwisho kabisa ya Yesu Kristo kwa wanafunzi wake kabla ya kuteswa, kufa na kufufuka ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wake wanakuwa na upendo, wote tunafahamu kuhusu kupenda, lakini Yesu hakutaka tu tuwe tunapenda lakini alitaka wawe na upendo mwingi sana, unaweza kujiuliza upendo mwingi ni upendo wa namna gani? Biblia nyingine za Kiswahili zinatumia neno upendo mkuu, biblia ya kiingereza inatumia neno “The Great love” ambalo ka Kiswahili ni Upendo mwingi au upendo mkuu! Kwanini Yesu anazungumzia upendo mwingi kwani kuna upendo kidogo au mchache ndio kuna upendo kamili “Perfect Love au “sacrificial love” na upendo mwingine wenye upungufu!

Katika Lugha ya kiyunani neno upendo linaelezewa vizuri, sana kwa kuzingatia maeneo manne

1.       Phileo – Huu ni upendo au uhusiano wa kirafiki, unampenda mtu kwa sababu ni rafiki yako mahusiano yenu ni ya kirafiki, upendo huu una mipaka, kwa sababu unaweza kufa unaweza kuharibika ndio maana unaweza kuona watu wanafarakana na wanaweza hata kusalitiana na urafiki ukageuka kuwa uadui mkubwa

2.       Storge – Huu ni Upendo au uhusiano wa kindugu, unampenda mtu kwa sababu ni ndugu yako, mna uhusiano wa damu, uhusiano wa kubaiolojia ni babam ni mama, ni mama mdogo ni baba mdogo, ni binamu, ni shangazi, ni babu, ni bibi na kadhalika upendo huu pia una mipaka na unaweza kuharibika na ndugu wakageuka kuwa maadui wakubwa sana

3.       Eros – Huu ni upendo au uhusiano wa kimapenzi, ni upendo wa asili ya kibinadamu ambao mvutio wake unatokana na mapenzi, so unaweza kumpenda mtu kwa sababu ana usio mzuri, hana malolo, Yakobo alimpenda Raheli kuliko Leah kwa sababu Lea alikuwa na macho dhaifu alikuwa na malolo, unaweza kumpenda mtu kwa sababu ana makalio makubwa, mazito, hips za kutikisa dunia, ana chuchu zilizosimama, saa sita ni mkwaju wa nguvu umbo namba nane, potable au ana mzigo mzito wa kitikisa dunia na kadhalika huu ni upedno wenye hisia za kimapenzi

4.       Agape – Upendo huu sasa ndio unaoitwa upendo mwingi, ni upendo wenye kujitoa sacrificial love , upendo huu ni mgumu kuwa nao, ni watu wachahce sana wanaweza kuwa na upendo kama huu, Yesu aliuita upendo huu kuwa ni upendo mkuu, ni upendo mwingi, unahusisha kupenda mpaka kuyatia maisha yako kwaajili yaw engine Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele upendo huu mtu akiwa nao ndio tunasema amekomaa kiroho, ni upendo ambao una sifa za kipekee 1Wakoritho 15:1-13Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”

 

Ukomavu wetu wa juu sana Kiroho utajulikana pale tunapokuwa tayari kuyatoa maisha yetu kwaajili ya wengine 

 

Yuda - Mwanzo 44:1-34,·  Alikuwa mwenye upendo mwingi sana alikuwa tayari kufa kwaajili ya kuitunza familia yake na baba yake na kwaajili ya ndugu zake

Daudi - 2Samuel 18:31-33·   alikuwa na upendo mwingi kiasi ambacho alilia kwaajili ya Absalom mwanaye japokuwa yeye alikuwa amekusudia kumuua baba yake

 

Yesu Kristo Yohana 15:13:- “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake· kwa ajili ya rafiki zake”.

 

1. Daktari mmoja wa Uingereza aitwaye Will Pooley alikuwa ni moja ya madaktari waliokuwa mstari wa mbele Nchini “Sierra Leone” huko walikuwa na wenzake wengi wakipambana na wagonjwa wa EBOLA na virusi vyake katika harakati hizo Madaktari wengi sana na Manesi wengi sana wakiwemo wa Afrika Magharibi waliambukizwa virusi vya ebola wakati walipokuwa wakiwauguza wagonjwa na wengi wao walikufa Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90. Shirika la afya duniani, WHO katikatovuti yake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan. Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho, kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa. Maambukizi hupatikana kwa kila aina ya majimaji yanayotoka katika mwili wa binadamu ni ugonjwa hatari na unaoua kwa haraka na hauna tiba Will Pooley alipoupata ugonjwa huu alirejeshwa katika ndege maalumu na kuanza kutibiwa chini ya uangalizi maalumu huko uingereza Jambo la kushangaza ni kuwa baada ya kupona kwa bahati tu Will Pooley alitangaza nia yake ya kurudi tena Sierra Leone kusaidiana na wenzake kupambana na ugonjwa huo. Mtu huyu aliwashangaza wengi sana na kuwaogopedha wengi sana akiwa amepona kwa asilimia 100%alisema atarudi Africa kusaidia zaidi maana alizaliwa kwaajili ya hayo, jambo hili lilimfanya aandikwe kama shujaa na mwanadamu mwenye uwezo wa kujitoa kwa kiwango cha juu.

 

2. Maximilian Kolbe alikuwa ni Padre aliyetokea Poland aliuawa kama mfungwa tarehe 14 August 14,1941, Jeshi la wa NAZI waligundua kuwa baadhi ya wafungwa wamejaribu kutoroka na hivyo waliamua kuwaua wafungwa kadhaa, walijaribu kuwaua kwa njia mbalimbali, na hivyo walichagua wafungwa 10 ili wauawe na kifo chao kiliamuriwa kuwa kifo cha njaa, wafungwa waliamuriwa kujitoa mmoja mmoja yeye mwenyewe na mfungwa wa kwanza kuchaguliwa alijulikana kama Franciszek Gajowinczek mfungwa huyu alipochaguliwa alilia kwa huzuni kubwa akimtaja mkewe, watoto wake na familia yake na kusikitika kuwa hatowaona tena kutokana na swala hili Maximillian alisimama na kusogea mbele na kuomba afe yeye kwa niaba ya Franciszek ombi lake lilikubaliwa, wafungwa waliwekwa kizuizini kwa muda wa siku kadhaa bila kula wengine walikunywa mikojo yao ili waweze kuishi, Maximillian alikaa kwa wiki mbili bila kufa huku wengine wote wakiwa wamekufa, walimchoma sindano ya kufa hakufa na hivyo waliamua kukata kichwa Pope John Paul II alimtangaza kuwa Mtakatifu kutokana na moyo wake

 

3. Mifano hii inatusaidia kujua kile ambacho Bwana wetu Yesu amekifanya Pale alipojibu kuwa kwaajili ya haya Nalizaliwa alikuwa akimkumbusha Pilato kuwa yeye amekuja kuwafia wanadamu, amekuja kuwaonyesha upendo wa Mungu jinsi ulivyo Isaya 53:1-5 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumatatu, 23 Novemba 2020

Mzeituni umeao katika nyumba ya Mungu!

Zaburi 52:8 “Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu katika hekima yake alipouumba ulimwengu, aliiuumba ili uwe zawadi kubwa kwa wanadamu,  na aliweka miti na mimea kwaajili ya uhai na utatuzi wa matatizo ya kiafya kwa wanadamu, kwa msingi huo basi utaweza kuona kuwa, Miti ina uhusiano mkubwa wa uhai maisha na hata nafsi ya mwanadamu Lakini miti pia ina uhusiano wa kiroho na maisha ya mwanadamu. Mungu aliitoa miti na mimea kama zawadi kwa wanadamu kwaajili ya kunufaisha maisha yao ona Mwanzo 1:29 “Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

Katika miti au miche ambayo ilitolewa kama zawadi kwa wanadamu moja ya mti wa ajabu sana wenye nguvu za mwilini na rohoni ni mti wa Mzeituni, mti huu ni malimbuko ya amani ya dunia ni ni mti wa kwanza kutajwa mara baada ya gharika wakati wa nabii Nuhu, ukiacha mti wa mtini ambao ulitajwa mapema sana mara baada ya anguko la mwanadamu ona Mwanzo 8:6-12 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani. Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.

Mungu aliweka uwezo wa ajabu katika mti huu, na miongoni mwa miti inayofanya kazi ya kuleta heshima kwa Mungu na wanadamu Mzeituni ni mojawapo ni mti  wa kwanza katika miti hiyo  maarufu ya kibiblia angalia Waamuzi 9:8-12 “Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu. Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu. Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu.

Sifa za mti wa Mzeituni!

Moja ya sifa ya mti wa Mzeituni ni kuwa ni mti wenye uwezo mkubwa sana wa kustahimili ukame, lakini ni mti usioweza kufa, ni mti wenye uwezo wa kufufuka, mizizi yake ina uwezo mkubwa sana wa kwenda chini na kujiunganisha na maji, kwa sababu hiyo sio rahisi kuuua mzeituni, ukitaka kuuua lazima uchomoe mizizi yake na kuitenganisha na maji huko ardhini, hapo ndipo utaweza kuua, unaweza kuifyekelea mbali lakini baada ya muda fulani unachipua tena!

Mti huu ulitumika nyakati za Agano la kale kusimika watu waliokusudiwa kuwa watumishi wa Mungu katika Nyanja mbalimbali, kama Wafalme, Makuhani na manabii, ili mtu aweze kumtumikia Mungu katika nafasi hizo alipakwa mafuta ya mzeituni kwa maelekezo ya Mungu na maisha ya mtu huyo yalibadilika sana, Makanisa makubwa ya zamani kama Anglican na Kanisa Katoliki huyatumia mafuta ya mzeituni katika ibada za kipaimara na wakati wa kusimika viongozi wa kanisa wakiwemo makuhani wa madhehebu hayo, hii ni kwa sababu wanakumbuka huduma za kikuhani za kupoaka mafuta zilizokuwa zikifanywa na makuhani au manabii nyakati za agano la kale mifano ifuatayo itakusaidia kuelewa uhusiano wa kiroho ulioko kati ya mwanadamu na upako wa mafuta ya mzeituni unaokaribisha nguvu za Mungu Roho Mtakatifu! Ona  

1Samuel 10:1-7 “Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu? Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE. Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.

1Samuel 16:1-13Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako. Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu.  Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na ROHO YA BWANA IKAMJILIA DAUDI KWA NGUVU tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.”           

Katika Agano jipya ishara ya kupakwa mafuta inaweza kuwa mafuta halisi ya mzeituni au kuwekewa mikono na mtumishi wa Mungu aliyepakwa mafuta aliyewekwa wakfu, sio lazima yawe mafuta kama yale yaliyokaa katika pembe lakini Mchungaji aliyepakwa mafuta anaweza kukuwekea mikono na kutamka kusudi la kukuwekea mikono na ikawa sawa kabisa na kupakwa mafuta, lakini hata akikupaka mafuta halisi ya zeituni, bado uweza utakuwa uleule wa kuwekea mikono au kupakwa mafuta, Ndio maana Yesu hakuwekewa mikono lakini alipakwa mafuta na Mungu mwenyewe mara baada ya kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mtu anapowekwa wakfu kwa kupakwa mafuta anakuwa mtu mwenye uweza wa kiungu ndani yake na kumfanya kuwa mtu wa tofauti! Ona tangazao la Yesu la kuwa mpakwa mafuta;-

Luka 4:18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”

Mungu anaporuhusu katika kanuni zake uwekewe mikono au upakwe mafuta unakuwa na uweza wa kiwokovu ndani yako na mungu anakupoa neema inayokuwezesha kuwatetea wengina na kutimiza majukumu yako ambayo Mungu anakuwa ameyakusudia

Mzeituni umeao katika nyumba ya Mungu!

Zaburi 52:1-9

Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.

Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila

Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.  

Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka;

Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake.

 Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.

Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu.

Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.

Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

 

Katika msitari wetu wa Msingi Mwandishi anaonyesha ya kuwa yuko mtu wa hila, mtu mwenye kiburi mwenye uwezo wa kupoteza watu, muovu  inaonekana mtu huyu ana madhara ni hodari na mwenye nguvu, anawaandama wanadamu anapigana nao ana hila bila shaka ni wazi kabisa mtu huyu ni Ibilisi anasimama kushindana na makusudi ya Mungu ndani ya kila mmoja wetu anataka kutuahribia anataka kutuumiza anataka kuweka jeraha katika mioyo yetu, anataka tushindwe, anazuia mafanikio yetu, anapoingana na makusudi ya mungu ndani yetu na ndani ya mwandishi wa zaburi hii ambaye ni Daudi.  Mwandishi anamkumbusha  mtu huyo (Shetani) kuwa Yuko Mungu mwenye nguvu kushinda yeye, anauwezo wa Kumuharibu milele, anauwezo wa kumfutilia mbali, na ana uwezo wa kumng’oa na Daudi anatabiri kuwa wenye haki watamcheka!  Watashangaa kwanini mtu huyu wa kiburi hakumfanya Mungu kuwa nguvu yake? Kwa nini alitumainia mali zake na kujifanya hodari kumbe hana nguvu! Daudi anaeleza kuwa mtu anayemtegemea Mungu anayeutumainia  wema wa Mungu anayetambua kuwa Mungu ni mwema siku zote yaani hata wakati wa nyakati ngumu au ndani ya jambo gumu bado Mungu ni mwema tu! Hao ni sawa na Mzeituni uliopandwa katika nyumba ya Mungu,  yaani wale wanaomtegemea Mungu na kuzitumainia nguvu zake  watamea katika nyumba ya Mungu yaani katika uwepo wa Mungu watastawi watahuishwa, kwa sababu wanategemea fadhili za Mungu wanalitizamia jina lile jema yaani jina la Yesu, hawa hawatatikiswa wala hawataogopa, wakikatwa wanachipua tena! huwezi kuwazibia wameunganishwa mizizi yao na chemichemi ya uzima na chanzo cha uhai ambaye ni Mungu!,  watu walioungwa na chemichemu ya uzima wanautazamia wema wa Mungu siku zote Zaburi 52:1, hao hawawezi kutikiswa hawaogopi wana jina wanalolitumainia wanakaa katika uwepo wa Mungu wanazitumainia fadhili za Mungu milele na milele hawa ni watu wasiowezekana

Ndugu  tunalo tumaini lisiloweza kutikiswa sisi ni kama Mzeituni unaomea katika nyumba ya Mungu. Kila anayemtegemea Mungu na anayezitegemea fadhili zake hapaswi kuogopa, hatupaswi kufadhaika maana sisi kama ilivvyo kwa daudi ni mzeituni unaomea katika Nyumba ya Mungu, Mizeituni huwa haifi, mizeituni huwa inadumu milele, mizizi yake imeungwa na chemic hemi za chini sana za maji, ili tutoweke ni mpaka wachomoe mizizi inayotuunganisha na fadhili za Mungu, Usiogope!

 

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima

0718990796