Mambo
yanakwenda shaghala baghala kinaweza kuwa kilio cha watu wengi waliookoka
katika nyakati tulizonazo, kila kitu katika maisha kinachoachwa chenyewe bila
kushughulikiwa kinasambaratika kama ni katika maswala ya kisayansi tungweweza
kusema kuwa mambo ynajiendea kiasili bila utaratibu
Hivi ndivyo inavyokuwa katika ulimwengu wa
kiroho kadhalika mambo yasipokuwa na usimamizi madhubuti hatimaye
yanaparaganyika, karama isipochochewa inakufa 2Timotheo 1;6 Paulo alimuandikia
Timotheo kusudi kwamba aichochee karama iliyo ndani yake, Maisha ya kiroho
wakati wote yatahitaji kuendenda kwa
roho ili kuweza kuyatunza Wagalatia 5;25, Ni muhimu kukumbuka kuwa tunayaanza
maisha yetu ya kiroho kwa kuzaliwa mara a pili baada ya kuzaliwa kiroho
kutokana na Roho wa Mungu, na baada ya kuzaliwa huko kunakotokana na Roho wa
Mungu tunahitajika kujazwa na Roho Mtakatifu mara moja na ujazo huo unafungua mlango wa kukutana na
aina nyingne za Baraka za Mungu.
Kila mtu anayekuwa amepitia hatua hiyo
analazimika sasa kutokuridhika na kiwango hicho na kubweteka kwa sababu tu eti
amebatizwa katika Roho hatua hiyo sio mwisho hata kidogo kwa ujumla ndio mwanzo
wa safari ya kiroho, na wala mtu asifanye makosa kusema kwakuwa sasa amejazwa
kwa Roho anaweza kustarehe na kujishughulisha na maswala mengine zaidi, ni
muhimu kuzingatia kuwa maisha ya kuendelea kuwa na ufahamu zaidi na kutembea na
Roho Mtakatifu yanapaswa kuunzwa na kuendelezwa
zaidi katika kijitabu hiki tunataka kujadili jinsi ambavyo mtu
aliyejazwa kwa Roho Mtakatifu anavyoweza
kuendelea kutembea na Roho Matakatifu
na katika kuiyatimiza hayo tutajadili maswala makuu mawili yaani Umuhimu
wa kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu na muongozo wa namna ya kuendeleza
maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu na kwa kufanya hayo maisha ya kiroho
hayataweza kuparaganyika kiasi cha kutokupata kibali mbele za mfalme na
kutokukataliwa wakati wa kuja kwake au kuwamfano wa wale wanawali wapumbavu
watato ambao Bwana Harusi alipokuja alikuta taa zao hazina mafuta Bwana ampe
neema kila mmoja wetu anayepitia kijitabu hiki kutokupoteza Nguvu za Roho
Mtakatifu na kuyaona mambo akiparaganyika katika jina la Yesu Kristo Amen!
SOMO LA KWANZA: UMUHIMU WA
KUTUNZA HALI YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.
Mara baada ya mwamini
kumpokea Roho Mtakatifu swala la kuhusu kutunza na kuendeleza ujazo wa Roho
Mtakatifu huwa halitiliwi mkazo wala halina maundisho na itakuwa ni uzembe wa
hali ya juu kudhani kuwa hakuna la ziada la kufanya kwani hali ya ujazo wa Roho
Inapaswa kutunzwa siku zote za maisha yako.
§ Uzoefu wa ujazo ni lazima utunzwe.
Haijalishi mtu ana
upako kiasi gani au alifurika kiasi gani wakati wa kujazwa Roho Mtakatifu ana
weza akawa amejazwa kwa nguvu kubwa sana lakini kama mwamini huyo hatunzi kile
alchokipokea katika maisha yake kupitia maisha ya maombi, kushuhudia,na kuishi
maisha matakatifu ukweli ni kuwa mtu huyo atapoa haraka sana na haribiko
litafuata ni muhimu kufahamu kuwa Ujazo wa Roho Mtakatifu unamleta mwamini
katika uhusiano na Roho ambao unapaswa kudumishwa kwa kiutunza na kuuendeleza kila wakati.
§ Wajibu wa kila Mwamini.
Kila mwamini katika
Kristo anapaswa kukubali kwamba anawajibika katika kutunza maisha yake ya
Kiroho, Ingawa Mchungaji na washirika wengine jamaa na marafiki katika Bwana
wanaweza kukutia moyo na kukuchochea katika swala zima la kuendelea kuwa na
uhusiano mzuri na Mungu ni muhimu kufahamu kuwa jukumu la mwisho ni lako
mwenyewe kwa msingi huo ni lazima ujifunze kujitia nguvu mwenyewe katika Bwana
1Samuel 30;6.
Kushindwa kulisimamia
hilo matokeo yake yatakuwa ni kurudi nyuma na kupoteza nguvu, na kwa bahati
mbaya mtu anaweza hata kupoteza wokovu na ni kwa kusudi hilo Paulo alimuhimiza
Timotheo kichochea Karama iliyokuwa
ndani yake 2Timotheo 1;6 kama jinsi tanuru la moto linavyohitaji kuchochewa
kupitia kuni ndivyo na maisha yetu ya kiroho yanavyopaswa kuchochewa na kama
tukilala usingizi moto huo na utazimia
kwa msing huo ni muhimu kwetu kuhakikisha kuwa tunawajibika
kikamilifu katika kutunza maisha yetu ya
kiroho.
SOMO LA PILI: MUONGOZO WA KUTUNZA HALI YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.
Moto unahitaji
kuchochewa ili uweze kuendelea kuwaka na
mafita yanahitaji kuongezwa ili
kuongezea mwanga kuwaka zaidi katika namna kama hiyo ni muhimu kuendelea kuwa
na wakati wa kujisimamaia na kujichunguza na kuyalinda maisha yetu ya
kiroho kwa kujiangalia kila wakati ili
kutunza hali ya ujazo wa Roho Mtakatifu, Paulo mtume aliwafundisha wakoritho
kuwa na tabia ya kujihoji wenyewe ili
kujiona kuwa uko kaika kiwango gani cha kiimani 2Wakoritho 13;5 kila mwamini
anao wajibu na anapaswa kukubali wajibu wa kujisimamia kiroho na kama mkristo
akiharibika kiroho chake hana mwingine wa kumlaumu isipokuwa ajilaumu yeye
mwenyewe
Mtu anaweza kujiuliza
Kama ninawajibika kujisimamia kiroho changu mwenyewe je ninapaswa kufanya nini?
Na ni hatua gani ninaweza kuchukua katika kuhakikisha kuwa ninadumu katka
kutembea na Roho katika maisha yangu? Yako maswala ya msingi nane ambayo
tutayaangalia kama mbinu za kuhakikisha kuwa unajisimamia kiroho na unatuza
maisha yenye kujawa na Roho wa Mungu.
§ Tafuta kujazwa upya kila wakati.
Kama mkristo anataka
kubakia akiwa amejaa Roho Mtakatifu ni lazima atafute kujazwa na Roho Mtakatifu
kila wakati kama ilivyoainishwa kuwa kila mwamini ni lazima abatizwe katika
Roho Mtakatifu mara tu anapokuwa ameokoka Matendo 1;4-5, 8:14-17 ubatizo huo wa
Roho Makatifu ni neema ya ajabu katika maisha yetu. Ingawa mwamini anapaswa
kutambua kuwa kubatizwa katika Roho Mtakatifu sio mwisho wa kuendelea kujaa
tena na tena na kila mwamini ni lazima atafute kujazwa tena na tena siku zote
za maisha yake
Tunaweza kuona
ushahidi katika maandko kwamba wanafunzi wa bwana walijaa Roho Mtakatifu siku
ya Pentekoste katika Matendo 2;4 lakini huo haukuwa mwisho kwani wakati Fulani
tena walijazwa tena Matendo 4;8,31, Paulo alijaa Roho Mtakatifu kwa mara ya
kwanza huko Dameski Matendo 9;17-18 lakini alijazwa tena huko Kipro Matendo
13;9 Wanafunzi huko Efeso walikuwa wamejazwa Roho walipoammini na Paulo
alipoweka mikono juu yao Matendo 19;6
lakini alipowaandikia Waefeso aliwasihi wajae Roho Waefeso 5;18, Kila mwamini
anapaswa kujazwa kwa Roho Mtakatifu lakini anapaswa kujazwa upya kila
wakati katika maisha yake ya Ukristo.
Unaposoma kwa makini
jinsi na namna Paulo anavyowaasa waefeso kujazwa na Roho katika Waefeso 5;18
pia utaweza kugundua kuwa kanuni ya kukazia kujazwa na Roho inakaziwa kama
kanuni ya kanuni ya nguvu za kiroho na tena neno hilo katika Biblia ya kiyunani
mjezwe Roho liko katika wakati uliopo na unaoendelea , hii ikiwa na maana basi
mjazwe Roho ni tendo endelevu kwa lugha rahisi tungeweza kusema muwe mnajazwa
Roho. Dr Stanley Horton alichangia hivi kuhusu andiko hilo la Waefeso 5;18
“Tunapaswa kutunza kuendelea kujazwa
Roho Mtakatifu” na hii ndio maana halisi ya adniko hilo katika kiyunani kwa
hivyo sio swala la kujazwa mara moja tu hapana! Ni swala endelevu kama kitabu
cha matendo ya mitume kinavyoweza kuonyesha.
Mkristo aliyejaa Roho
anapaswa kujua kwamba anapaswa kuendelea kutunza hali ya kuendelea kujazwa Roho
kila siku ya maisha yake , Yesu alipokuwa akizungumza kuhusu ujazo wa Roho
Mtakatifu alisema hivi Nami nawaambia Ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi
mtaona bisheni nayi mtafunguliwa” Luka
11;9 baadaye alisisistiza hili katika mstari 13
“basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je Baba aliye mbinunihatazidi sana kuwapa
Roho Mtakatifu hao wamuombao” unaweza kuona Dr. Horton Mtaalamu na mwalimu wa maswala ya Roho
Mtakatifu Duniani anasema hivi swala la
kuomba kutafuta na kubisha ni swala
endelevu na sio la mara moja kwa msingi
huo nikama Yesu anasema endeleeni kuomba, endeleeni kutafuta na endeleeni
kugonga kwa maana kila anayeendelea kufanya hayo atapokea, Ili kuendelea kujaa
Roho Mkristo anapaswa kuendelea kutafuta kujaa Roho kwa hiyo swala la kupokea
au kujaa Roho ni swala endelevu.
§ Omba bila kukoma.
Moja ya maswala a
msingi ambayo yanaweza kumuweka mwamini kaika hali ya kujaa Roho ni kuomba kuomba bila kukoma ni maombi endelevu
1Thesalonike 5;17 maombi ni muhimu sana kwakla mkristo ni kama kujitia nidhamu
kwa msingi huo mkristo anapaswa kuishi maisha hayo ya kujitia nidhamu na
kujitia nidhamu ni kutembea katika Roho,Paulo anawaambia wathesalonike kuendelea kuomba kila wakati na kushukuru
katika mazingira ya aina yoyote na kwamba wasimzimishe Roho angalia mstari ule
wa 17-19 kumbuka na angalia kwa makini hapa ni kama Paulo anasema kama Mwamini
akiendelea kuomba hatafanya makosa ya kumzimisha Roho mstari wa 19 kwa msing
huo msiatari hii inapaswa kutafasiriwa kivitendo tusiache kuomba, Paulo
aliwafundisha waefeso kwamba mwamini ana vita vya kiroho Waefeso 6;10-18 na
alikamilisha maelekezo yake kwa kuwataka waombe katika Roho mstari wa 18 somo liko wazio hapa kwamba ili kuyatunza
maisha yetu kiroho na kuwa tayari kwa
vita ya kiroho tunapaswa kuomba katika Roho katika mazingira yote maana yake ni kuwa kila siku tunapaswa pia
kuomba kujazwa kwa upya na Roho na kuhitaji muongozo wake katika maisha yetu,
au maombi yetu kila siku yanapaswa kuwa ni pamoja na kuomba kwa kunena kwa
lugha kila siku na Paulo alisema maombi ya jinsi hii humjenga yaya anenaye kwa lugha
1Koritho 14;4 na ndo maana akasema
napenda kila mmoja anene kwa lugha au aombe kwa kunena kwa lugha mstari 5 na kasha namshukuru Mungu kwama
nanena au naomba kwa lugha kuliko wote matsri 18 na tunapoomba kwa lugha
tunadumisha nguvu nza roho ndani yetu kwa kuwasiliana na Mungu.
§ Kuwa mtu wa kujituma katika kuabudu.
Njia nyingine ya
mkristo kutunza uwepo wa Roho Mtakatifu
ni kujituma katika kuabudu, kuabudu kunabeba umuhimu mkubwa sana wa
maisha ya kiroho hususani katika maisha ya mtu aliyejazwa Roho ni kwa njia
ya kuabudu roho tunaketishwa katika ulimwengu
wa roho na Yesu kristo Waefeso 2;6 aina hii ya kuabudu kwa roho ndiyo inayotupa
nyakati za kuburudishwa Matendo 3;19. Ili kuyalinda maisha yetu na kuyadumisha
kiroho ni lazima tutafute nafasi ya kujituma katika kuabudu nafasi hii
tunaitumia kama nafasi pekee ya aina kubwa ya kujitoa kiroho na kuimarisha
maisha yetu binafsi kiroho nguvu kubwa ya kiroho itakuja kupitia kujituma
katika kuabudu binafsi Isaya 40;31, lakini wakati huo huo ni muhimu kukumbuka
kujiunga na waamini wengine katika matukio ya kuabudu Biblia inakazia kwamba
wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine Waebrania 10;
25.
Kila nafasi
inapopatikana ya kuabudu ni muhimu kujituma na kujiingiza na kujimwaga katika
kuabudu kwa moyo wetu wote Zaburi 100;4 Daudi aliomba eenafsi yangu Umuhimidi
Bwana na vyote vlivyo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu 103;1
Paulo anazungumzia moja ya njia kuu za kuendelea kuyatunza maisha yetu ya
kiroho kuwa ni pamoja na kujaa Roho Waefeso 5;18 anasisitiza mjazwe Roho na kisha
katika mistari inayofuata anaeleza ni namna gani tunaweza kujazwa Roho Mstari
wa 19-20 kwa zaburi, kwa tenzi na kuimba
nyimbo za rohoni mtu anapoabudu kutoka moyoni kwa kudhamiria katika kuabudu na
kumwaga moyo wake kwa Bwana anajiweka katika hali ya kuendelea kujaa Roho
Mtakatifu.Paulo pia anaweka wazi kwamba
kuabudu ni moja ya nia yenye nguvu sana ya kutunza uwepo wa Roho
Mtakatifu katika maisha mtu anapoabudu roho yake inafanywa upya, imani yake
inajengeka na nafsi yake inaburudishwa
na zaidi ya yote anatiwa nguvu kwa makusudi ya vita vya kiroho.
§ Tafakari neno la Mungu.
Kila siku tunapaswa kulitafakari neno la Mungu
kama tunataka kuendelea kutunza uwepo wa Roho mtakatifu katika maisha yetu Yesu
alisema Roho hutia uzima na mwili si
kitu Maneno haya niliyowaambia ni Roho na uzima Yohana 6;36 Kile Kristo
anachokisema kuhusu maneno yake
kinayahusu maandiko yaani neno la Mungu neno la Mungu ni roho tena ni
uzima, tunapoisoma biblia na kuitafakari
Roho wa Mungu anazungumza nasi na kutuhuisha katika maisha mapya na kama tunataka kudumisha maisha yetu kiroho
tunapaswa kuendelea kuyatoa maisha yetu kila siku katika kujisomea na
kulitafakari neno la Mungu neno la Mungu ni chakula cha kiroho kwa mtu wetu wa
ndani na ni kupitia kulisoma neno la Mungu ndipo roho zetu zinapokea maisha
mapya na kutiwa nguvu Zaburi 119:92-93. Ni muimu kufahamu kuwa haitoshi tu
kujisomea Biblia na kasha kutokufanya lolote kuhusu, lakini inatupa sa kulitii
na kuitumia ile kweli yake katika maisha yetu Yakobo alisema tusiwe wasikiaji
tu bali tuwe watendaji wa neno Yakobo 1;22 Yesu alisema kila ayasikiaye maneno
yangu asiatende atafananishwa na mtu mpumbaqvu aliyejenga nyumba yake kwenye
mchanga Mathayo 7;26 majaribu yajapo na
kuipiga nyumba ile anguko lake litakuwa baya na haita weza kusimama , maisha
yetu ya kiroho yanatunzwa sio tu kwa kusoma neno la Mungu lakini kwa kulitii
katika yale linayoagiza.
§ Tembea kwa imani.
Mbinu nyingine ya
kutunza maisha yetu ya kiroho ni kutembea kwa imani, kwa maana nyingine
kutembea kwa Roho ni kutembea kwa imani na maswala haya yanakwenda sambamba
Paulo anaunganisha swala la kutembea kwa imani na kutembea kw Roho alipoandika
hivi “sisi kwa njia ya Roho kwa imani tunasubiri katika matumaini ya haki
Wagalatia 5;5, ni kwa imani watu humpokea Roho Wagalatia 3;2,14 na kwaimani
vilevile anatunzwa Wagalatia 3;3. Ndio kwa imani vile vile tunapata karama za
Roho na miujiza hali kadhalika mstari wa 5 kwa msisitizo huo wa Paulo ni wazi kuwa
upatikanaji wa Roho Mtakatifu na utendwaji wa miujiza vinapatikana kwa imani na
kwa sababu hiyo tunaenenda kwa imani wala si kwa kuona 1Koritho 5:5-7 kwa
msingi huo yeye anayetamani kuishi katika Roho anapaswa kuishi kwa imani na sio
kwa kuona
§ Ishi maisha ya kujitoa.
Kuna jambo la sita
ambalo mtu anapaswa kulifanya ili kuendelea kuwa rohoni na hili ni kwamba
lazima ujifunze maisha ya kujitoa hii ikimaaniska kijikabidhi kwa Roho
Mtakatifu na mapenzi yake nah ii
inajumuisha kuanzia na mtazamo, tabia , uwazi na kutamani kuishi siku zote
akiwa na utayari wa kumtii Roho Mtakatifu na sauti yake, Yesu aliishi maisha ya
kujitoa alishuhudia kujihusu hakutenda jambo lolote kwa nafsi yake na kwa jinsi
hiiyo baba alimpenda Yohana 5;19-20 Yesu alijitoa moja kwa moja katika
kuyafanya mapenzi ya Mungu. Hii ilijumuisha pia swala zima la kujikabidhi kufa
msalabani. Yohana 8;28-29.
Katika mazingira kama haya mitume pia waliishi maisha ya kujitoa na
kumtii Roho Mtakatifu lolote walilolifanya kama ni kuomba au Luka 24;53, Matendo 1;14,
3;1, 4;31 Kuabudu Matendo 11;15, 13;1-4 kushuhudia 1;8, 4;8, 31 kuhudumu 6;8,
16;6-10 au hata kuendesha mikutano a kanisa 15;28 walifanya yote chini ya
uongozi wa mamlaka ya Roho Mtakatifu,
kama tunataka kutembea tukiwa na uwepo wa Roho Mtakatifu wakati wote ni laizma tujifunze kumtii Roho Mtakatifu na
kujifunza kutenda mapenzi ya Mungu na makusudi yake.
§
Uwe makini katika maswala ya kiroho.
Jambo linguine la muhimu kwa kuishi maisha
yaliyojaa Roho ni kuwa makini kiroho “spiritualsensitivity” yaani uwezo wa kuwa
na hisia kali dhidim ya maswala ya kiroho au kuwa makini katika kutaka kujua
Roho mtakatifu anataka ufanye nini? Na kasha kufanya hali hiyo ya uamkini wa
kiroho ni ya muhimu kwa kila mtu anayetaka kweli kumfuata Roho wa Mungu lazima
uwe makini kuisikiliza sauti yake na uwe
mwenye kutekeleza kwa haraka kile anachokisema na kuwa mtu wa toba ikibidi.
Mara ntyingi tunapowasha redio zetu huwa tunasikiliza kuwa ni radio gani
tunaitune ili kwamba tuweze kupata usikivu mzuri wa kile tunachokiaka hali
kadhalika katka ulimwenu wa Roho ni
lazima tujifunze kuweka masikio yetu kwa Roho wa Mungu Biblia inasema leo kama mtaisikia sauti yake
msiifanye mioyo yenu kuwa migumu waebrania 3;8,15,4:7, moja ya namna ya
kuifanya mioyo yetu kuwa migumu ni kutokuisikiliza vema sauti ya Roho wa Mungu
hii ni sawa ni kile alichokisema Paulo msitweze unabii 1Thesalonike 5;19-20
msimzimishe Roho, kwa kuifanya mioyo yetu uwa migumu tunaweza kuuzima moto wa
Mungu katika maisha yetu kwa msingi huo kamwe tusikubali fanya jambo lakijinga
kisi hiki.kwa kuwa kinyume na Roho.
§
Tembea kwa utii.
Kutembea kwa utii na maisha
matakatifu ni swala lingine la kutunza uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha
yetu, tumajifunza kuwa tnaweza kumzimisha Roho na kisha maisha yetu ya kiroho
yakawa mashakani na kashatukaishi maisha yasiyofaa kitu katika Waefeso 4;29-31 Paulo aliorodhesha baadhi ya dhambi ambazo
zinamzimisha Roho Mtakatifu kuwa ni pamoja na
§
Mazungumzo
mabaya/Marafki wabaya
- § Uchungu,
- § Hasira/Ghadhabu,
- § Kelele na matukano
- § Kila namna ya ubaya
- § Kutokusamehe
- § Kutaka kulipiza kisasi
Matukio a jinsi hiyo yasio ya
kitakatifu na tabia za aina hiyo zinamuhuzunisha Roho Mtakatifu na kumzimisha
kutembea kwa wepesi katika maisha yetu na kama tukimuhuzunisha hatimaye
anaondoka
Kwa maana nyingine tunapomtiii na
kuisikiliza su\auti yake uwepo wake unakuwa mkubwa katika maisha yetu na wakati
huo huo tunajifunza kumfuata vema Waebrania 5;14 na Roho wa Mungu ataachilia
vipawa vyake na karama zake na roho ya kuomba na tukitii kwa haraka tunakuwa na nguvu zaidi katika roho zetu.
Hitimisho.
Mambo yameparaganyika ili kuyajenga
maisha yetu ya kiroho au kama hayako sawa sawa kama hatujali, kama tutakjali na
kuyafanyia kazi yaliyomo humu hakika yake utakuwa na uhusiano mzuri na Roho wa
Mungu na ukiendelea kuyatunza maisha yako kuwa katika hali ya buujik na Roho wa
Mungu tutapiga hjatua kwa namna yoyote na kamwe hatutakuwa kama tulivyo Bwana
ampe neema kla mmoja wetu kutunza uhusiano wake na Mungu na kuzidi kaika jina
la Yesu amen!
Rev. Innocent Mkombozi Kamote
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550
Maoni 13 :
MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA MTUMISHI NIMEJIFUNZA MENGI SANA LEO
MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA MTUMISHI NIMEJIFUNZA MENGI SANA LEO
Nimebarikiwa sana mtumishi wa MUNGU aliye juu
Kwa kwel umezungumza na mm MUNGU aendelee kukutumia kwa viwango vya juu zaid
Ameni nimebarikiwa sana
Barikiwa,kwa kazi njema ya ufalme wa MUNGU.
Amina
SoMo Hili ni tamu sana
Somo zuri sana Mungu anitie nguvu niliweke rohoni
Amen saana mtumishi nimepata vitu vya kunisaidia pia vya kuwasaidia na wengine Barikiwa na Yeah kristo
Jina langu ni Mt. Edma mgaya nipo daresalam
Mungu akubariki mtumishi nimebarikiwa sana na mafundisho Yako,Mungu anisaidie niyaweke moyoni na niyafanyie kazi
BWANA YESU AKUBARIKI BABA MIMI MWANAO MCH JOSEPH GENGE MUHEZA
Chapisha Maoni