“Do not let The sun go
down”
Waefeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu
wenu bado haujawatoka;”
Utangulizi.
Maisha ya
mwanadamu ni mafupi sana na yamejawa na taabu na changamoto za aina
mbalimbali na yanapita upesi sana Zaburi
90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa
tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita
upesi tukatokomea mara.” Biblia inaonyesha kuwa siku za mwanadamu kuishi
ni chache na zinapita haraka lakini pia zimejaa taabu unaweza pia kuona katika Ayubu
14:1-2 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake
za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha
hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe”
Kutokana
na hali hiyo Maandiko yanatutaka kila mmoja wetu kujifunza jinsi ya kuishi kwa
furaha na kuacha kufadhaika kabisa Wafilipi 4:4-7. “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole
wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote;
bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo
yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
Ni jinsi
gani tunaweza kuishi maisha ya furaha na amani, jinsi gani tunaweza kuwa mbali
na masumbufu ya ulimwengu huu maisha ni mafupi sawa lakini kama mtutaishi kwa
huzuni na kukosa amani yatakuwa mabaya zaidi, ni lazima tukubali kujifunza
kuishi kwa furaha na amani na kutokuweka Uchungu moyoni Biblia inapotuamuru kufurahi
na kuachilia mamnbo kwa haraka kabla ya kwenda kulala au kabla jua halijachwa
inajua kuwa uwezo huo uko katika maamuzi yetu, tunaweza kuamua kuwa wenye
furaha na tunaweza kuamua kuwa wenye huzuni ni vema kuamua kuwa wenye furaha
muda wote na kutokuogopa.
Mfano
Profesa
mmoja wa saikolojia alikuwa akitembea mbele ya jukwaa akiwafundishwa watu jinsi
ya kuwa mbali na stresses na migandamizo ya maisha, ukumbi ulikuwa umejaa
wanafunzi wengi sana , aliposimama aliagiza glasi ya maji ya kunywa ambayo ilikuwa
na maji nusu, pia aliagiza nyingne iliyokuwa imejaa na akazishika mikononi
mwake , wanafunzi wote walikodoa macho wakimuangalia kwa mshangao
Profesa
aliuliza swali je hizi glasi nilizoshika zina uzito kiasi gani, wanafunzi
waliinua sauti zao na kujibu huyu hivi na huyi hivi huku wakitaja uzito wa aina
mbalimbali
Kisha
profesa yule alijibuna kuwaambia kwa mtazamo wangu kwa hakika kabisa uzito wa
glasi hizi hauna maana yoyote “Haujalishi” lakini jambo kubwa la maana ni muda
ninaotumia kuzishika glasi hizi, endapo nitazishika kwa muda mfupi mikono yangu
haitaumia, lakini kama nitazishika kwa muda mrefu sana mikono yangu itaumia na
hatimaye nitachoka na mwisho nitalazimika kuzivunja glasi hizi, kwa sababu hiyo
uzito wa glasi hapa hauna maana lakini muda ninaoutumia kuzishika ndio
utakaonifanya nione uzito wa glasi hizi
Wanafunzi
walishangaa sana na walikubaliana na mafundisho yake , ndipo alipowaambia
unapokuwa na migandamizo na unapoendelea kuwa na hofu katika maisha yako ndivyo
unavyoendelea kujiumiza moyo wako, unapofikiri chanhgamoto unazazipitia kwa
muda kisha ukaziondoa moyoni hakuna kitakachotokea lakini ukifikiri kwa undani
sana utashindwa kuendelea na hatimaye madhara yatatokea
Ni
kwaajili ya swala kama hili Biblia inatukumbusha kuondoa uchungu mioyni mwetu
kabla jua halijachwa, Mungu hapendi tutale na uchungu na hofu, haijalishi nini
kinatutokea mchana, ikifikia jioni yatupe yote yaliyokuwa yanakusumbua ,
usiyabebe usiku nkucha na kuamka nayo,
kama utaamka nayo basi kumbuka ni wakati wa kuweka Glassi chini
Biblia pia
inatushauri Kuomba na kumsihi Mungu atupe amani naye atatupa kamwe tusigope!
Kuna Baraka kubwa sana katika kuwasamehe wengine na kuondoa kila kitu mioyoni
mwetu Mathayo 6:14-15 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu
hatawasamehe makosa yenu”.
Na Rev.
Innocent Kamote.
Mkuu wa
wajenzi Mwenye Hekima!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni