Wafilipi 2:3-4
“Msitende neno
lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na
amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake
mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”
Musa Mtumishi wa Mungu mara kwa mara aliwaombea israel na kuwatanguliza wao kuliko yeye
Yakobo
na Yohana walikuwa marafiki wa karibu sana, walikuwa majirani, walisoma pamoja kisha
walikwenda chuoni pamoja na pia walipata kazi sehemu moja.
Siku
moja waliamua kusafiri kwa meli kwenda katika visiwa vigeni, walianza safari
yao na kuzunguka na meli na wakatokomea mbali sana, kwa bahati mbaya safari yao
ilikumbwa na dhoruba kubwa sana kiasi ambacho meli waliyokuwa wakiitumia
ilivunjika vunjika na baadhi ya abiria walikuwa, lakini hata hivyo Yakobo na
Yohana walifanikiwa kuogelea kwa muda mrefu na kufikia moja wapo ya kisiwa
kilichokuwa karibu.
Kisiwa
hiki kilikuwa kama nyika tu hakukuwa na miti ya maana na Yakobo na Yohana
waligundua kuwa hakuna uwezekano wa kuishi pale bila msaada wa Mungu, Hivyo
waliamua kuomba Mungu aingilie kati, lakini waliambiana tuone ni maombi ya nani
yatakuwa yenye nguvu? Yakobo aliamua kwena upane wa mashariki ya kisiwa na
Yohana aliamua kwenda upande wa Magharibi wa kisiwa kila mmoja alidhamiaria
kwenda kumuomba Mungu huko ili msaada utokee
Yakobo
aliomba kwanza Mungu ampe chakula ili aweze kuishi, na mara akaona sahani ya
chakula na matunda na mboga za majani na samaki, akaanza kula,
Baada
ya siku mbili aliomba apate mwanamke mzuri sana ili awe mke wake kwa vile
alihisi upweke wa hali nya juu kule kisiwani, baada ya masaa machache kulikuwa
na Meli iliyopata ajali karibu na kisiwa kile kwa mbali na ni mwanamke mmoja tu
aliyeweza kupona katika ajali ile kwa kuogolea mpaka kisiwani na Yakobo
alimpokea kama mke wake, sasa ikawa kila anachokiomba Yakobo anakipata.
Hatimaye
kama mwezi mmoja ulipita tangu ajali ile ya meli itokee, Yakobo aliomba kutokee
meli itakayomrudisha nyumbani yeye na mkewe, na kwa hakika ikatokea meli na
kumchukua yeye na mkewe kurudi nyumbani.
Lakini
walipokuwa wanakaribia kuingia katika lango
la meli, Yakobo alisikia sauti ikimwambia “Je unaondoka mwenyewe? Bila
mtu muhimu katika maisha yako?” Yakobo alishangaa na kujibu hebu niambie
unamaanisha nini ? mtu muhimu katika maisha yangu ni mke wangu na niko naye
hapa!
Sauti
ikamwambie mimi ndiye uliyekuwa ukiniomba na ndiye niliyekuwa nikijibu Maombi
yako, ndiye niliyekupa chakula na kuyatunza maisha yako na hata huyo mke wako
mimi ndiye niliyekupa, Yakobo alipiga magoti na kumwambia Mungu asante kwa
fadhili zako zote.
Kisha
Yakobo akamkumbuka Yohana ambaye alikuwa amekwisha sahau habari zake, na
akajisikia vibaya
Mungu
akamwambia sikuwa najibu maombi yako kwa sababu ya wema wako, nilikuwa wakati
wote nasikiliza maombi ya Yohana na kuyatimiza, Yohana wakati wote alikuwa
akiomba ombi moja tu Mungu wangu tafadhali mkumbuke rafiki yangu Yakobo
mtimizie kila anachokihitaji hayo ndio yalikuwa maombi ya Yohana wakati wote.
Yakobo
alilia sana na alikimbia magharibi ya kisiwa kwaajili ya kumtafuta rafiki yake,
alitambua kuwa alikuwa mbinafsi hakufikiri kuhusu wengine alijifikiria mwenyewe
tu na kufurahia baraka zile, hata hivyo alipofika magharibi ya kisiwa hakumuona
Yohana na Yakobo alimuuliza Mungu sasa yuko wapi Yohana Mungu akamwambia
Nilimchukua na yuko name, Mtu mwenye moyo wa dhahabu kama Yohana anapaswa kukaa
na mimi, lakini nitayatimiza maombi yake kama nilivyomuahidi.
Yakobo
alijisikia vibaya sana na ndipo alipogundua kuwa rafiki yake ndiye aliyekuwa na
maombi yenye nguvu kuliko yake, kwa sababu maombi yake, hayakuwa na hata chembe
ya ubinafsi kama yak wake.
Maombi
yenye nguvu ni maombi ambayo ndani yake hakuna chembe ya ubinafsi. Watu wakubwa
katika maandiko hawajiombei wenyewe wanaombea wengine, Manabii waliokuwa rafiki
wakubwa wa Mungu ni wale walioombea watu na sio kujiombea wenyewe, Mungu ampe
neema kila mmoja wetu kuacha ubinafsi.
Kumbukumbu 9:18-20
“Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na
mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa
yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa
kumkasirisha. Kwa kuwa
niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia Bwana kutaka kuwaangamiza. Lakini
Bwana alinisikiza wakati huo nao. Bwana akamkasirikia sana Haruni akataka
kumwangamiza; nikamwombea Haruni naye wakati huo.”
1Samuel 7: 5-9
“Samweli akasema, Wakusanyeni Israeli wote Mispa, nami
nitawaombea ninyi kwa Bwana. Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na
kuyamimina mbele za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia Bwana
dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. Hata Wafilisti
waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa
Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli
waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. Wana wa Israeli wakamwambia Samweli,
Usiache kumlilia Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya
Wafilisti. Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea Bwana sadaka
ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia Bwana kwa ajili ya Israeli; Bwana
akamwitikia.”
Mafanikio
yako wakati wote kumbuka kuwa kuna watu wanaoomba kwaajili yako na wala sio kwa
sababu ya wema wako na Tunapoomba kwaajilin yaw engine Mungu hujishughulisha na
mahitaji yetu pia.
Na
Rev. Innocent Kamote
Mkuu
wa wajenzi mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni