UTANGULIZI
Homiletics ni somo linalohusu jinsi ya kuandaa na
kupeleka ujumbe wa kibiblia kwa kufundisha au kuhubiri.
Tunajifunza somo hili kwa kusudi la kuwa wanenaji
hodari na wazuri wa Neno la Mungu, Kuna njia kuu mbili tu za kuupeleka na
kuuwasilisha ujumbe wa neno la Mungu ambao ni kuhubiri na kufundisha, kwa kawaida hizi ni sehemu mbili za sehemu moja ya huduma, Huduma ya mitume na
Yesu Kristo ilijumuisha Kuhubiri na Kufundisha
ona Mathayo 4;23, Marko 1;21,27,28, Luka 4;44 na Matendo 18;4-5,11,18;19,19;8.
Kuna waalimu wengi ambao hawahubiri ingawa wachungaji wote wana huduma ya
Kuhubiri na kufundisha. Katika somo hili
tunajifunza jinsi ya kuwa wahubiri na wanenaji wazuri mbele za watu. Somo hili
litamsaidia muhubiri kuwa na uwezo wa kuandaa vema mahubiri yake na
kuyawasilisha lakini pia linakuandaa kuwa mnenaji hodari kila wakati
unaposimama mbele za watu au kuzungumza nao kupitia vyombo vya habari na
kadhalika.
Somo kuhusu utungaji wa hutuba na namna ya
kuwakilisha hutuba homiletics ni moja ya masomo ya muhimu sana katika jamii na
katika Nyanja ya kibiblia ni kupitia
hutuba ndipo mtu anapoweza kujifunua na kujieleza yeye ni nini na anataka nini, malengo yake ni nini, na
kufanya tathimini ya nini kimefanyika na nini kinapaswa kufanyika, kwa msingi
huo hutuba ina nafasi kubwa katika maisha yetu, watu wengi wametamka mambo
ambayo hawangepaswa kuyatamka na kujikuta wakijilaani baadaye aidha
waliyoyatamka yalikuwa ni matakwa yao binafsi na wakati mwingine hayana ukweli
halisi na kushindwa kujieleza hili ni
moja ya matatizo yanayopelekea kuweko kwa kwa watu mbalimbali na kushindwa kujieleza
kumekuwa na mchango mkubwa sana wa magonjwa ya kiakili na wengine wanajikuta
wakijitukana na kujilaumu kuwa wao ni wazembe, wabaya, hawafai, wao sio wema na
haitakuja itokee wao kuwa wema kwa sababu ya majuto ya namna tu walivyoshindwa
kujieleza na kupata aibu mbele ya hadahara aina hizi za maelezo hazitusaidii
kuwa watu wanaostahili.Badala yake tunahitaji kuwa na bidii katika kujifunza
kwani hakuna aliyezaliwa akiwa anajua kujieleza kwa msingi huo basi
Ni muhimu kujitambua wenyewe kwanza na kwa
kujifahamu kuwa sisi ni watu wa namna gani na kisha baada ya kujitambua ndipo
tuifanye kazi ya kujieleza vema na kuwakilisha mambo kwa uhakika, katika namna
chanya na yenye ushawishi na hapo ndipo tunapoweza kuwa watu wenye uwezo wa
kujieleza katika hutuba zetu yaani kutambua madhaifu yetu kwanza kisha
kujifunza kuyadhibiti kisha kuingia katika ulingo wa kuwa wanenaji hodari na
watoa hutuba wenye kujiamini na kujua kujieleza.
Lakini hutuba ni nini? Ni usemi
kwa ufupi tunaweza kueleza kwa namna hiyo “it
is just a speech” ni kuzungumza ni kutoa maelezo ni kujieleza kwa uhakika “Speaking to actuate” kuzungumza
kunakochochea vitendo huu ndio msingi mkuu wa hutuba za Kikristo, Kuhutubu ni
huduma kama ilivyo huduma ya uandishi ni huduma iliyoenea ulimwenguni kote
kuliko huduma ya uandishi imebeinika kuwa wale wanaoandika wakati mwingine
hutakiwa kuzungumza ingawa si kila anayezungumza hutakiwa kuandika kwa hivyo kuhutubia ni huduma kamili
kabisa na ili kuishawishi jamii kupitia
usemaji yaani hutuba inahitajika mbinu za kitaalamu na kujitoa katika
kushughulika na maswala hayo ya kihutuba somo hili linashughulikia swala lote
hilo la hutuba za kibiblia na hata zile zisizo za kibiblia ni matumaini yangu kuwa utabarikiwa unapopitia
somo hili na Mungu wa amani akubariki na kukupa moyo wa kujifunza katika jina
la Yesu amen!.
SURA
YA KWANZA: MUHUBIRI NA UJUMBE WAKE
Sifa za Kibiblia za
Muhubiri
Kabla ya kuanza shughuli ya kuhubiri na
kufundisha Neno la Mungu muhubiri anapaswa kuhakikisha kuwa anakuwa na sifa
zinazohitajika za kibiblia, kuhubiri Biblia ni tofauti na hutuba nyingine za
kisiasa au za kijamii, kazi hii ya
kuhubiri Biblia ni kazi ya Mungu na hivyo awaye yote anayeifanya ni lazima awe
ameungwa na Mungu kwa maana nyingine hapa tunazungumzia wito wa kiutumishi kila mkristo anaweza kuhubiri na kufundisha Neno
la Mungu kwa sababu Yesu aliagiza wakristo kufanya hivyo hilo ni jema lakini
hata hivyo wako ambao Mungu amewaweka wakfu kwa ajili ya kuifanya kazi hii hawa
ni wale walioitwa. Lakini penginepo
mtu yu aweza kuuliza swali wito ni nini? Ni msukumo unaowekwa na Mungu kupitia
Roho wake Mtakatifu kumuwezesha mtu aliyeokoka kusikia msukumo wa kufanya kazi
ya ya Mungu na kukubali kuwa na wajibu wa kuwahubiri na kuwafundisha watu Neno
la Mungu akisaidiwa na neema ya Mungu. Kuna aina kuu tatu za wito katika
ukristo;-
Wito wa Jumla katika wokovu.
Wito huu ni wa
jumla katika wokovu wito huu hutokea pale Mungu anapokuwa amemuokoa mtu kwa
neema yake anapokuwa amemuamini Yesu Kristo na kumkiri akijutia dhambi zake na
kupokea neema inayomuwezesha kukataa dhambi Tito 1;11 wito huu unaambatana na
pumziko la kutolewa katika nira ya sheria Mathayo 11;28, ni wito unaohusu
kuondoka gizani na kuja katika nuru kwa ajili ya maandalizi ya kuingia katika
uzima wa milele 1Petro 2;9,1Timotheo 6;12 wito huu pia hujumuisha swala la
kuishi maisha matakatifu 1Petro 15-16, wito huu kwa kiingereza ni “General call to the Salvation”. Wito
huu ndio msingi wa aina nyingine za wito.
Wito wa jumla wa kumtumikia Mungu.
Wito huu unajumuisha pamoja na
wito uliotangulia kuwa kila mtu aliyeitwa katika wokovu pia ameitwa kwa ajili
ya kumtumikia Mungu, na Mungu anamtaka kila mtu aliyeokolewa amtumikie wito huu ni wito wa jumla katika utumishi “General call to the service” wito huu
unaanza mara tu baada ya kuokolewa Kutoka 7;16,8;1,20,9;1,13 agizo la kuhubiri
na kufundisha ni la wakristo wote waliookolewa Mathayo 28;19-20 Matendo 8;1-4
na tunapata ushahidi kuwa nyakati za kanisa la kwanza washirika pia walihusika
katika kuhubiri injili na hata kuanzisha baadhi ya makanisa wakimtumikia Mungu.
Wito maalumu wa Utumishi na maongozi.
Baada ya aina hizo za wito ambazo
hutangulia ndipo sa wito huu maalumu wa maongozi huja huu ni wito maalumu kwa
ajili ya utumishi “Special call to the
service”ni wito ambao unaweza kugawanyika katika makundi makuu matano ya
karama za kihuduma wito huu kibiblia unaanza kwa kutenga au kuweka wakfu kwa
maneno haya “Mungu ameweka wengine “1Koritho 12;28 hawa ni mitume, manabii, wainjilisti,
wachungaji na waalimu Waefeso 4;11 Hawa hawakujiweka wenyewe bali wamewekwa na
Mungu na wamekubali kujinyenyekeza katika mpango wa Kristo kwa maisha yao yote
waebrania 5;4. Kazi yao ikiwa ni kuwaandaa watu kwa makusudi ya kazi ya huduma
itendeke na kuwakamilisha watu hata kufikia katika cheo cha kimo cha utimilifu
wa Kristo katika tabiana mwenendo.
Jinsi Mungu anavyoita watu.
Nyakati za zamani katika vyuo vya
Biblia kulikuwa na tabia ya kusikia shuhuda mbalimbali jinsi Mungu alivyowaita
watumishi wake kuingia katika huduma na
unaposikiliza shuhuda hizo nyingine zinatisha kwani wengine wameitwa kwa
kuisikia kabia sauti ya Mungu ikiwataka kufanya huduma hii na wengine walikuwa
na shuhuda nyingine za kawaida unaposikia shuhuda hizi unaweza kufikiri kuwa
labda aliyeitwa kwa kuisikia sauti ya Mungu kabisa ni maalumu sana kuliko
wengine, au Yule ambaye Yesu amemtokea na kumuita n.k,Hapa jambo la msingi ni
kujifunza kwamba Mungu huita watu kwa njia nyingi na kwa namna mbalimbali kwa msingi huo ni
upumbavu kujilinganisha na wengine kama maandiko yasemavyo 2Wakoritho 10;12
kila mwanadamu ni tofauti na mwingine
kwa sababu Mungu alikusudia iwe hivyo.
Na kwa kuwa kila mtu ni wa
tofauti Mungu pia huita watu kwa njia tofauti na kila wito ni halisi na hakuna
mtu anayeweza kudai kuwa ana wito sahii sana kuliko wa wengine kama ilivyo kwa
wokovu.
·
Musa aliitwa kupitia Maono kijiti kilichokuwa kinawaka Moto lakini
hakliteketei Kutoka 3;1-10
·
Isaya alikua hekaluni akaona maono na kuitwa
Isaya 6;1-9
·
Yeremia kupitia maono lakini tangu tumboni Mungu
alikusuduia kumtumia Yeremia 1;1-19
·
Sauli aliitwa baada ya kupigwa mweleka alipokua
akienda Dameski Matendo 9;1-20
·
Marko aliitwa kuwa masaidizi wa kwanza katika
safari za kimisheni za Paulo na Barnaba Matendo 12;25 baadaye alikataliwa na
Paulo kwa sababu alikuwa dhaifu kihuduma hata hivyo Barnaba aliendelea
kumlea na baadaye akafaa kwa huduma Matendo
13;13,15,37-38 na hata Paulo mtume alimihitaji sana baada ya kuona anafaa kwa
huduma tena ndiye aliyeandika injili ya Marko. 2Timotheo 4;11. (Yoshua alikuwa
mtumwa wa Musa Mungu akamuita kuwa kiongozi)
·
Elisha aliitwa kwa kutupiwa vazi na Eliya nakuamua
kumfuata 2Wafalme 2;12-15.
Mungu anaita
watu kwa njia mbalimbali na kwa namna nyingi inategemea tu mkao wako wa kiroho
kisikia jinsi Mungu anavoita Roho wa Mungu yuko kila wakati yeye ndiye Bwana wa
mavuno na huita watu kwa njia mbalimbali soma 1Koritho 2;14 Mambo ya kiroho yanajulikana kwa jinsi ya
Rohoni ni wale walio kondoo wa Yesu wanaoweza kuisikia sauti yake Yohana
10;27 vyovyote iwavyo hakuna mwenye
uwezo wa kudai au kuhukumu kuwa mwengine hakuitwa ni kazi ya Mungu kuita sio ya
mtu.
Mungu aliyachagua mambo mapumbavu.
1Wakoritho
1;26-29 “Maana ndugu zangu angalieni
mwito wenu ya kwamba si wengi wenye
hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheowalioitwa, bali
Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima, tena
alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu tena Mungu
alivichagua vitu vinyonge vya dunia na
vilivyodarauliwa naam vitu ambavyo
haviko avibatilishe vile vilivyoko mwenye mwili awaye yote asije akajisifumbele
za Mungu” unaona Mungu katika hekima
yake hachagui watu maalumu sana katika utumishi wake si kuwa Haiti kabisa wenye
hekima lakini biblia inasema si wengi.. wakati mwingine Mungu aliwaita watu
ambao kama ungeliwaona kwa macho yako wewe usingelikubali kuwaita na ndio maana
tunaona kuwa hata Musa alipoitwa alijifahamu kuwa ana kigugumizi, Yeremia
alijiona ni mtoto, Isaya alijiona kuwa ana midomo michafu hakuna aliyekua
anafaa hata mmoja Mungu hatuchagui kwa
sababu tunafaa anachagua mtu mwenye uwezo wa kuibeba neema yake watu ambao kwao Mungu atatukuzwa kupitia
wao.Hata hivyo madhaifu hayo sio tiketi ya kukubali kukaa katika hayo bali ni
kwaajili ya kuibeba neema ya Mungu.
MASWALA SITA YA LAZIMA ANAYOPASWA KUWA NAYO
MUHUBIRI.
a. Muhubiri anapaswa kuwa mtu asiyelaumika
1Timotheo 3;2
Hii ni sentensi ya ujumla
inayofuatiwa na sifa zipatazo tisa ambazo muhubiri anapaswa kuwa nazo katika njia
kuu mbili
·
Asiyelaumika katika macho yake mwenyewe maana
yeke ni nini? Dhambi inatufanya tuwe waoga
juu yetu wenyewe huwezi kuhubiri jambo Fulani kwa ujasiri kama jambo
hilo wewe mwenyewe umeshindwa kulifanyia kazi kwa mfano kma hutoi zaka huwezi
kuhubiri kwa ujasiri kuhusu utoaji wa zaka
unaweza kujikaza kwa unafiki tu, hivyo kama muhubiri mwenyewe huna maadili
ni ngumu kuhubiri maadili labda uwe farisayo ndipo uweze kuhubiri utakatifu kwa
wengine kuishi juu ya kiwango
kunakuwezesha kuwa muhubiri mwenye viwango, jasiri na unayejiamini.
·
Asiyelaumika katika macho ya wengine maana yake
ni nini? Biblia inasema katika Waebrania 12;13 “Mkaifanyie miguu yenu njia za
kunyooka ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe bali afadhali kiponywe” Muhubiri
anapokuwa mwenye kulaumika maana yake ni kuwa wale dhaifu ambao wana
mfuata wanakoseshwa na kuanguka wataangalia mfano wa muhubiri na kuigiza tabia
zakeau kuiacha imani kwa msingi huo muhubiri ni mfano wa maswala mema au
maswala mabaya, Biblia inaonyesha kuwa
tuwe kielelezo katika usemi mwenendo imani na usafi 1Timotheo 4;12. Hii maana
yake ni kuwa si kwamba muhubiri ataepuka kabisa kulaumiwa lakini lawama mbaya
ni zile za kweli lawama hizi zinafananiswa na kujitia matope wewe mwenyewe
lakini lawama ambazo hazina ukweli zinafananishwa na gari linalopita na
kukumwagia matope.
Gari linalopita linaweza kukumwagia matope lakini baadhi ya watu
hujipaka matope wao wenyewe. Mchungaji hapaswi kuwa na lawama za kweli lakini
mchungaji hawezi kukwepa lawama za kusingiziwa, lawama hizi ni kama gari
inayopita na kukumwagia matope, lawama ambazo hazina ukweli haziwezi kuwa na
nguvu katika maisha yako.
b. Muhubiri anapaswa kuwa Mume wa mke mmoja 1Tomotheo 3;2
Biblia
inaposema awe mume wa mke mmoja katika Biblia ya kiyunani tafasiri yake inaweza
kusomeka hivi kwa kiingereza “Be a One –
woma man” yaani awe mwanaume wa mwanamke mmoja huii maana yake sio lazima uoe na kuweka
ndani lakini uwe mwaminifu kwa mkeo ndio tafasiri halali hapo watu wanategemea kiongozi kuwa mtu mwenye maadili
ndani ya ndoa yake pia ili kukubalika katika jamii
Mwanasisa
Gary Hart alipendwa na wengi huko Marekani wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka
1984 alikuwa ni mwenye mvuto, mwenye elimu nzuri na maarufu sana na alikuwa mnenejia hodari sana mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi na watu
wengi walijua kuwa atakuwa raisi, baada ya muda ikagundulika kuwa hakuwa
mwaminifu kwa mkewe na mara vyombo vya habari vikatangaza ndugu huyo alipoteza ujasiri na aliachana na kampeni za kisiasa kumbe hata
watu wa kawaida nje ya kanisa wanahitaji mtu mwaminifu ni zaidi sana katika
kanisa la Mungu. Mungu nyu aweza kusamehe dhambi yoyote inapofanyika na mtu
akatubu lakini utakuwa umejichafulia kimaadili Mithali 6;32-33
c. Muhubiri anapaswa kuwa Mwenye kiasi na
Busara, mtu wa utaratibu 1Tomotheo 3;2
Kuwa
na kiasi maana yake kuweza kujizuia kuhakikisha kuwa unakuwa sawia katika
maeneo yote Usiiishi zaidi ya kiwango cha kawaida katika jamii yako, uwe na
kiasi katika mazingira yote yanayokuzunguka, ishi vizuri na watu , usigombane
au kupandisha hasira kupita kawaida wala
usipuuzie majukumu yako kuwa mtru unayeheshimika kwa matendo mema , hakikisha
kuwa unazitawala tama zako kama mpanda farasi anapomtawala farasi kwa kutumia
lijamu.
d. Muhubiri anapaswa kuwa mkarimu 1Timotheo
3;2
Mtu
mkarimu huwa pia ni mkaribishaji anakuwa mkarimu kwa watu na kuwahudumia hata
kwa vinywaji waliookoka na wasiookoka watu wewngi wanaweza kuokolewa kupitia
tabia zako za ukarimu
e. Muhubiri ni lazima ajue kufundisha
1Timotheo 3;2
Kuhubiri
na kufundisha ni sehemu kuu mbili za huduma ya muhubiri, muhubiri pia ni
mwalimu. Lakini huwezi kufundisha kitu ambacho hujajifunza kwa msingi huo
muhubiri wakati wote anapaswa kuwa mwanafunzi wa Biblia na kwa maana nyingine
hana mahafali, kufundisha kunahitaji zaidi ya maarifa ili uwe mwalimu mzuiri
unapaswa pia kuwa mtu mzuri 2Tomotheo 2;24-25 “Tena haimpasi mtumwa wa bwana
kuwa mgomvi , bali kuwa mwanana kwa watu wote awezaye kufundisha mvumilivu,
akiwaonya watu kwa upole wao washindanao naye ili kama ikiwezekana Mungu awape
kutubu na kuijua kweli”
Kuweza kufundisha ni moja ya majukumu muhimu
kwa mwalimu awaye tymwenye uwezo wa kufundisha anapaswa kuwa mnyenyekevu na
mwanana mwema na kama utajiona kuwa bado humfananii Kristo hilo lisikupe shida
endelea kumuomba Mungu na mwalimu mwema huendelea kuwa mwema Mathayo 5;12.
f.
Muhubiri
ni lazima ajue kuisimamia nyumba yake 1Timotheo 3;4
Kiongozi
wa kiroho anapaswa kuwa mwenye kuisimamaia nyumba yake vema na kutiisha watoto
wake katika usatahivu, Eli ni moja ya mifano ya kiongozi wa kiroho aliyepoteza
sifa kutokana na kukosekana kwa maadili
kwa watoto wake mwenyewe na kushindwa kuwasimamia 1Samuel 2-3, nyumba yake haikuwa mfano mzuri
wa kiroho, Baadhi ya wahubiri wamejaribu kuwalazimisha wake zao au watoto wao
mambo Fulani na matokeo yake wanavuna uasi na sio mahusiano mazuri , Mwanaume
anatakiwa ajifunze kumpenda mkewe kama nafsi yake na kama Kristo alivyolipenda kanisa Waefeso 5;25 hapo ndipo uwezekano wa kuishi
kwa amani naye unapotokea, wala watoto hutakiwi kuwalipukia kwa hasira lakini
inakupasa kuiwafundisha na kuwatika
katika nidhamu na kuwaelekeza katika
njia za Bwana Efeso 6;4 siku zote watoto
huwa na mwitikio mwema kwa baba anayeshughulika nao vema na kila unapopanda mbegu njema katika familia
yako unazivuna
Uwezo mkubwa wa kiongozi wa kiroho
aliyekomaa ni namna gani anahusiana na familia yake mtu anaposhindwa kuisimia nyumba yake vema
atafanya kosa kama hilo wakati akishughulika na kanisa na Yule anayefanikiwa
kushughulika vema na familia yake hali kadhalika hufanikiwa kwa kiwango kama
hicho katika kuliongoza kanisa Paulo
alishughulika na waamini kama ambavyo baba anavyo shughulika na familia yake
1Thesalonike 2;11 ukiwa mwaminifu katika mambo madogo anaweza kuwa mwaminifu
katika mambo makubwa pia Luka 16;10.
MASWALA MANNE AMBAYO MUHUBIRI HAPASWI KUWA.
a. Muhubiri hapaswi kuwa mtumwa wa ulevi
1Timotheo 3;3
Kwa
ujumla haipaswi kwa muhubiri kuonekana anakunywa pombe au hata kukaribia baa
ulevi ni kama nyoka mwenye sumu kali kwa msingi huo muhubiri anapaswa kuwa
mbali nayo Mithali 23;29-32 Biblia inakataza kulewa kwa mvinyo na badala yake
inasisitiza swala la kujaa Roho Waefeso 5;18.
b. Muhubiri hapaswi kuwa mgomvi wala mtu wa
kujadiliana 1Timotheo 3;3
Siku
zote hasira za mwanadamu haitendi haki ya Mungu Yakobo 1;20 “lakini hekima
ishukayo kutoka juu ni ya amani, ya upole , tayari kusikiliza maneno ya watu
imejaa rehema na matunda mema haina fitina, haina unafiki” Yakobo 3;17 ni
muhimu kila mmoja kuomba ili kwamba Mungu atuumbie tabia ya upole na kuwa na
maneno mem.
c. Muhubiri hapaswi kuwa mpenda fedha 1Timotheo 3;3
Kuna
hoja kadhaa kuhusu fedha baadhi wanahoji kuwa kukosekana kwa fedha ndio chanzo
cha kila aina ya uovu lakini hii sio kweli kwani hata watu wenye fedha pia ni
wenye dhambi, wala mtu haongezeki katika utakatifu kama anavyoongezeka katika
fedha, wala fedha hazitufanyi tuwe wa Mungu au kiroho, Tatizo sio ukosefu wa fedha
wala kuwa na fedha tatizo ni asili ya dhambi aliyonayo kila mwanadamu, kila
mmoja anahitaji fedha ni za muhimu situ
kuwa tunahitaji fedha lakini tunastahili kuwa nazo kila mtenda kazi anastahili ujira wake
1Tomotheo 5;18,1Koritho 9;9-11 lakini tunaaswa katika maandiko kuutafuta kwanza
ufalme wa Mungu na hakli yake na mengine yote tutazidishiwa Mathayo 6;33
Abrahamu alikataa fedha alizopewa na mfalme wa sodoma aliona ni muhimu kutunza
utakatifu wake na uhusiano wake na Mungu Mwanzo 14;23, dhambi kubwa ni kupedna
fedha zaidi kuliko kumpenda Mungu Mathayo 6;24.
d. Muhubiri
hapaswi kuwa aliyeongoka hivi karibuni 1Tomotheo 3;6
Dhambi
mbaya kuliko zote ni kiburi ni kwaajili
hii ndio maana shetani alihukumiwa na kutupwa
Mithali 16;18, shetani alijivuna kwaajili ya nafasi aliyo nayo kama
Malaika mkuu na hivyo alijivuna na kutaka kuwa juu ya Mungu Isaya 14;12-14 Yesu
alimuona akianguka kutoka mbinguni Luka 10;18, si vema mkristo mchanga kuwekwa
ju ya mamlaka ya kimaongozi katika kanisa anaweza kuanguka kutokana na kujivuna au kiburi kwa msingi huo lazima
kionngozi wa kanisa awe niu mtu aliye na Muda mrefu wa kutosha katika wokovu
ili kwamba mizizi iende chini kwa kiasi cha kutosha kabla ya kuhimili upepo wa
umaarufu
UMUHIMU WA KUJITAMBUA:
Kujitambua udhaifu wako;
Inapozungumziwa
swala la kujitambua inazungumziwa kujitambua nguvu zako na udahaifu wako na ni muhimu sana kujitambua udhaifu wako ili
kwamaba ujue ni maeneo gani yanahitaji kuyaendeleza na kutumia mbinu zitakazokusaidia katika
kujitia nguvu mara nyingi madhaifu ya
kawaida katika kuhutubia yako katika mazingira makuu matatu.
· Kuwa na misamiati michache
· Kutamka vibaya maneno na kushindwa kueleweka
· Kushindwa kujenga vizuri sentensi
Kwa kawaida
matatizo ya jinsi hii yanajitokeza kwa wingi pale mtu anapotumia lugha ngeni
lakini hata katika lugha hizi tilizozizoea kuna uwezekana wa matatizo ya aina
hiyo kujitokeza kwa msingi huo ili muhubiri aweze kujiendeleza katika kuwa meneji hodari anapaswa kuhakikisha yafuatayo moja endeleza ujuzi
kuhusu misamiati ili kwamba uwe na ujuzi wa maana ya maneno mengi sana ya
kutosha na anza kuitumia misamiati hiyo,
Pili Endeleza uwezo wako wa kutamka maneno kwa kuzungumza na watu wenye ujuzi
mzuri wa lugha na hususani wataalamu na
waalimu pia uwe na tabia ya kusikiliza sana vyombo vya habari, mwisho jenga
namna ya kuunda sentensi zako vema
hususani katika maeneo ambayo unashindwa kuayatamka vema .
Jaribu kujichunguza mwenyewe.
Socrates Mwana
falsafa wa kiyunani wa zamani sana
alisema lazima ujitambue wewe mwenyewe yaani ili kuufanyia kazi ushauri huu mzuri
muhubiri anapaswa kujifanyia uchunguzi
wa kila unachokizungumza jifanyie uchunguzi mwenyewe jinsi unavyoona mambo na
unavyowerza kuyaelezea katika kujijadili
wenyewe tutapata ukweli kujihusu hisia zetu
na jinsi tunavyojifahamu na hapo
ndipo tunapoweza kuweka malengo ambayo tunaweza kuyafikia kwa kujibadili sisi
wenyewe na ndipo tunaweza kuamua namna
tunavyoweza kuendeeleza kujitoa katika hali ya udhifu kuelekea kwemnye
kufanikiwa kuliko kukubwa kwa mfano ukimwambia mtu kuwa siwezi atakuifikiri
kuwa huwezi lakini ukimwambia mtu unaweza naye ataanza kukufikiri kama mtu
unayeweza kwa msingi huo tufikie uwezo
wa kutamka kamainavyotupasa kutamka.
Jifunze maswala yahusuyo namna ya
kuhutubia.
Ili mtu aweze
kuongeza uwezo wake katika kujieleza
anapaswa kujifunza na kuendeleza
uwezo wake wa kujieleza katika jamii, watu wengi sana wana tatizo la kushindwa kujieleza vizuri mbele za watu hususani tunapokutana na watu au kutakiwa
kukabiliana na kundi la watu na kujieleza, kumbuka kuwa kile tunachokisema na
namna tunavyosema ndivyo
vitakavyotuamulia kukubalika kwa wengine kwa wakristo kuna uwezekano usitakiwe
kusimama mbele za watu na kuzungumza na hadhara lakini kwa kuwa tuna ujumbe
muhimu wa injili tunatakiwa kuwa tayari kwani kwaajili ya ujumbe tulio nao
tutajikuta tunatakiwa kuupeleka kwa wengine hili linapaswa kututia moyo katika
swala la kujifunza kwa bidii kuwa
wazungumzaji wazuri kwa kususdi la kuieneza injili.
Jifunze kuwa Jasiri au kujiamini.
Kama unataka jamii
iamini kile unachokisema unapaswa kujiamini wewe mwenyewe, ujasiri au kujiamini
sio jambo tunalprithi linahitaji kujifunza na eneo la kujifunza ni katika
maisha yetu ya kila siku tunapoingiliana na watu, Fikiri vema kabla
hujazungumza, hakikisha kuwa uko sahii kasha zungumza kwa kujiamini na wakati mwingine fanya zoezi la kuzungumza
mahali pa siri kabla ya kuzungumza na hadhara, Unapokuwa mbele ya hadhira sio
wakati wa kuamua nini cha kukisema na namna ya kusema kwa sababu wakati huo
unahusika na usemaji nah ii itakupa
ujasiri na hadhira itahisi ujasiri wako.
Kujua kile kinachotarajiwa pia humpa
mnenaji ujasiri
Muhubiri
anapaswa kujua kuwa ni aina gani ya watu atazungumza nao, ukumbi gani atautumia
kuzungumza na mahali atakapozungumzia na aina ya vyombo utakavyotumia kama ni
vyombo au bila vyombo kujua maswala kadhaa ya mahali unapokwenda kuzungumza
kutakupa ujasiri wakati wa kuzungumza.
Kuhusiana na wapi unakwenda kuzungumza
§
Pata habari za kutosha kuhusu ukumbu au chumba
unachokwenda kuzungumza
§
Simu ya mtu ambaye anahusika na eneo unalokwenda
kuzungumza na maelekezo kuhusu
§
Muda unaotakiwa kutumika kutoka ulipo mpaka
katika eneo unakotakiwa kuzungumza
Kuhusiana na jamii ya watu unaokwenda
kuzungumza nao
§
Historia ya jamii hiyo na jinsi walivyo
§
Mambo wanayopendelea na mshikamano walio nao
§
Idadi ya watu unaokwenda kuzungumza nao.
Kuhusiana na vyombo wanavyokwenda kuvitumia
§
Aina ya vyombo
§
Aina ya vyombo vya dharula
§
Aina ya
vipaza sauti kama ni vya waya au visivyo na waya
§
Ujuzi kama hutuba itakuwa inarekodiwa au
haitarekodiwa
Si kila wakati
utakuwa na ujuzi wa maswala haya yote na kadiri unavyokuwa na ujuzi kuhusu
maswala hayo ndivyo na ujasiri wa namna ya kuzungumza unavyoongezeka, fahamu
pia wale utakaokuitana nao na wale utakaotambulishwa kwao, Haklikisha kuwa
umavaa vizuri kwa aajili ya matukio husika
na jiandae vema kwaajili ya ujumbe utakaoupeleka.
Wahubiri wengi
sana wanaogopa kusimama katika mimbari kwa msingi huo basi ni muhimu kuchukua
mazoezi ya kutosha kuhusu kuhutubu na maandalizi ya kutosha juu ya ujumbe
unaohusika haya yatakusaidia kupunguza
hofu ya mimbari hata kama ni mara yako ya kwanza au ndo unaanza kazi ya
kusimama mbele ya hadhara, lakini pia unaweza kufanya kazi ya kujiendeleza kiakili
kuhusu namna ya kundaa hali kiakili ya
kuweza kupunguza hofu ya kusimama mbele ya hadhara
1.
Umeaalikwa au kukaribishwa kuhudumu kwa sababu
una kitu cha ziada ambacho watu wanataka kukisikia kutoka kwako
2.
Ujumbe wako
ni wa muhimu sana na ni zaidi ya
namna unavyopaswa kuzungumza kwa sababu ya umuhimu huo hamu ya mtiririko wa
kuukamilisha na kuufikisha kwa watu ndio lengo lako kuu
3.
Fahamu kuwa ni kawaida kwa kila mtu kuwa na hofu
mwanzoni unapoanza kuhutubu
4.
Hofu imezungumziwa sana kiasi cha kutiwa chumvi
hivyo ipuuzie
5.
Unapo kuwa na uzoefu wa kuzungumza na kujiandaa
kwa umakini sana na kuwa na ujuzi na somo lako utashangaa jinsi kazi ya
kusimama katika mimbari inakuwa rahisi siku hadi siku
Jionyeshe kuwa una uwezo wa kufanya mambo
vema
Unapokuwa
unazungumza na watu kwa kawaida wakati huo huo ndio unajifunua utu wako kwao,
kwa mfano endapo mnenaji anawaangalia wasikilizaji wake moja kwa moja ina wasaidia wasikilizaji wake kuwa mnenaji anazungumza kweli au ni mkweli na unaposhindwa kuwaangalia
usoni wanahisi kama unawadanganya kuwatazama wasikilizaji ni muhimu kwaajili ya
sababu kubwa tatu
·
Kwanza wasikilizaji wanaona ya kuwa
unajihushisha nao.
·
Pili macho yanazungumza kama jinsi ambavyo sauti
inazungumza na viungo vingine
·
Macho
yanakusaidia kutambua muitikio wa wasikilizaji wako na kuona kama wanaguswa au
wanahisi kupotezewa muda , wamechanganyikiwa au wamekasirika au wanakubaliana nawe
Mnenaji wakati
wote anapaswa kuhakikisha kuwa anakuwa yeye ili kuepuka kuonekana ni kama
muigizaji, wakati huo huo ni muhimu kwa mnenaji kuhakikisha kuwa ana orodhesha kwa
mpangilio kile anachotaka kuwasilisha kwa jamii au wasikilizaji na wakati
mwingine ili kile unachotaka kukisema kiweze kueleweka vema inakupasa kuweka
mada yako katika mtindo wa maswali na majibu au unaweza kuielimisha jamii yako
kwa mpangilio wa kutafuta kutatua tatizo lilioko kwa mfano
-
Zungumzia tatizo unalotaka kulitatua katika
mfumo wa swali
-
Onyesha kweli kuhusu tatizo lenyewe
-
Onyesha njia za kutatua tatizo hilo
- Tumia njia zinzoonekana kuwa suluhisho la tatizo
- Fanya tathimini ili kuona kama njia iliyotumika
kutatua tatizo inaweza kufaa kutumika tena ka tatizo kama hilo
Njia nyingine
ya kujifanyia tathimini ni kuruhusu mijadala kutoka kwa jamii
Lakini kabla
ya kufanya hilo ni muhimu kujiuliza mswali kadhaa yafuatayo
-
Je mchango kutoka kwa wasikilizaji unaweza
kusaidia kusahihisha makosa?
-
Je mchango kutoka kwa wasikilizaji utaweka mambo
sawia au utakuchanganya zaidi?
-
Je mchango kutoka kwa wasikilizaji utaleta
vichekesho, vituko aui utaumiza?
-
Na kwa ufupi je mchango wao uatakuwa ni wenye
kujenga au kubomoa?
Endapo
utaridhika na matokeo yanayoweza kusababishwa na wachangiaji kutoka nje yaani
katika jamii basi sasa unaweza kuunda
kundi hilo la kujadili na yafuatayao
yanaweza kufanywa na kiongozi wa mjadala
-
Anzisha mjadala
-
Waweke wahusika katika kujua mada husika
-
Chagua kweli kadhaa na kuzibainisha kuhusiana na mada
-
Mpe kila
mwanachama nafasi ya kushiriki mazungumzo
-
Saidia kutatua matatizo na kuepusha migogoro
-
Hitimisha kwa mukhtasari maendeleo ya kundi
Kwa kufanya
mambo hayo hapo juu utakuwa umesaidia kukuza uwezo wa kufanya mambo na
kujieleza mbele ya watu na wakati huo huo kuwa na uwezo wa kufanya mabo mengi
kwa ubora.
Kuza uwezo wako wa kushawishi.
Wanenaji
hodari na wakubwa duniani ni wale ambao
wamejifunza kuwa na uwezo wa kujieleza
kama walivyo kwa kumaanisaha na kujieleza kwa bidii na wengine walikuwa na
uwezo kupitia unenaji wao kushawishi hata mambo ya kimataifa
-
Mnenaji mmoja aliyeitwa Savonarola alitoa ujumbe wa kimapinduzi uliowafanya raia
walioasi waovu katika karne ya 15 kubadilika na kuwa raia wema
-
Mnenaji Churchill alizungumza kwa hutuba yenye
kuchochea kumwaga damu, kutoka jasho na kulia machozi kwaajili ya taifa lake wakati wa vita vya
pili vya dunia
-
Wanenaji hawa baadhi ya misemo yao imekuwa ni
misemo ya kimapinduzi kwa miaka mingi hata leo kwa sababu ya unenaji wao wenye
kuvutia , kutia moyo na kutoa hoja za
nguvu
-
Mnenaji aliye hodari kumbe anaweza kabisa kutoa
hoja ambazo zinaweza kuishawishi jamii
na taifa na kusababisha mageuzi lakini
unenaji dhaifu unadhoofisha ushawishi wa mnenaji
Hakikisha kuwa unatoka vizuri kulingana na
mazingira
Unapokuwa
umevaa vema na unatoka kuhutubia watu unakuwa na mvuto sana kwa watu kutaka
kusikia kile unachokiwakilisha hii ikiwa
ni pamoja na namna unavyojieleza kwa msingi huo lazima muhubiri ujali nam,na
unavyo vaa kama utavaa vibaya hata kama
una ujumbr mahususi si rahisi watu kuweza kuukubali au kupokelewa vema ,
unapovaa vibaya unakaa vibaya kirahisirahisi unadhgaraulika na hivyo kuufanya
ujumbe wako pia usionekane wa maana utafiti unakubali kuwa wanenaji wanaovaa
vizuri wana nafasi kubwa ya kusikilizwa
kuliko wasiojali wametoka vipi.
Pichani
anaonekana mnenaji mwenye madai ya kuwa na ujumbe Yesu anakupenda na kukujali sana lakini namna
alivyotokea inasikitisha na kutatisha tamaa kiasi cha kuwafanya wapokeaji kuwa
na mashaka kama Mungu anawapenda.
AMRI
KUMI ZA MUHUBIRI WA BIBLIA
Utangulizi
Abrahamu
Lincon alikuwa ni Raisi wa Marekani
ambaye alijipatia sifa kadhaa
ikiwa ni pamoja na kuwaachia huru watumwa wakati mmoja alisema “Ninavutiwa na
muhubiri ambaye ni kama nyuki anayeuawa” kinachomvutia Lincon haikuwa kutembea
madhabahuni au kuruka ruka lakini
muhubiri ambaye anahisia za ndani kwa kile anachokihubiri yaani “Passion”
Mama mmoja kikongwe alimwambia muhubiri
mmoja mara baada ya kumaliza kuhubiri kwamba mchungaji nimehisi maumivu ya roho
yak oleo asubuhi, ulimwengu unaambatana na muhubiri ambaye anahisia kali dhidi
ya kile anachokihubiri , kwa maana hivyo Mchungaji au muhubiri anapaswa
kuhubiri ujumbe ambao yeye mwenyewe unamgusa sana , vinginevyo ujumbe huo hautakuwa na ushawishi kwa mtu
yeyote Mtu mmoja Adam Clarke alisema “Jifundishe mwenyewe kufa klisha jiombee
mwenyewe kufufuka” hili ni jambo la msingi sana Muhubiri ni lazima ahisi kile
anachokihubiri ili kiweze kushawishi.
Amri kumi za Muhubiri.
1. Onyesha ujasiri
Biblia
inasema usiogope uwe na moyo mkuu Yoshua 1;9
Kila mtu anapatwa na tatizo la hofu hususani linapokuja swala la
kusimama mbele za watuSauli alikuwa hivyo kabala ya kuwa mfalme, inaonekana pia
Timotheo alikuwa hivyo 2Timotheo 1;7, lakini kwa kuwa Mungu amekuchagua kuwa
mnenaji na kwa kuwa una kitu kwaajili ya watu usiogope kinene Matendo 13;15.
2. Uwe safi na uvae vizuri.
Watu
watahukumu aina ya ujumbe ulionao na jinsi ulivyo kama unatokea Porini au
unahubiri porini basi si neno baya ukivaa kama Yohana mbatizaji, lakini kama
unataka watu wapokee ujumbe wako vema unahitaji kuvaa vizuri si lazima mavazi
yawe ya thamani sana , lakini yawe mavazi safi nay awe yamepigwa pasi
3. Uwe na mikao mizuri
Ni
muhimu kuhakikisha kuwa unakaa vizuri na unasimama vizuri hasa unapokuwa
madhabahuni usikae kama mtu anayepunga upepo au mtu anaye jidai ukiwa umeweka
mkono mfukoni na kusimama mbele ya madhabahu, hakikisha unasimama vema mabega
yanakaa sawasawa na tumia miguu yote miwili wakati unasimama madhabahuni
usifanye kama jamaa huyu katika kielelezo chini
Usihubiri
huku ukiwa umesimama kwa mguu mmoja kama mtu aliyeegamia mti Tumia kwa kivuli
au aliyepanda daladala na kukosa siti.mikao ya aina hii huweza kueleweka vibaya
na wasikilizaji wako, aidha si vema kuweka mikono mfukoni swala hilo linaweza
kuonekana kama unajidai hususani hapa Afrika.
4. Iheshimu madhabahu
Usikohoe
kwa kubanja, au kutoasauti za kukoroma , kupnga kamasi au kuchokoa Pua, au
kitendo chochote kigeni kinaweza kuondoa usikivu kwa utendaji wako
madahabahuni, unaweza kufanya hayo unapokuwa umeketi au inapokutokea fanya kwa neema na kuomba
radhi kwani kumbuka watu wanakuangalia aidha kumbuka kuwa mpole madhabahuni
usipande madhgabahuni kwa kiburi.
5. Tumia sautuiyako vizuri
Sauti ni kama
vyombo vya muziki inaweza kuwa laini na inaweza kuwa na kelele, inapendeza
kuzungumza kwa saiuti kubwa kama kuna watu 20,000 lakini kama una watu 20 tumia
sauti ya kawaida, Spergion alisema “sauti kubwa yenye kelele haina nguvu kwani hugeuza majheshi ya maneno
kuwa maneno ya kikundi yasiyo na maana” maana yake ni kuwa wakati mwingine
maneno yenye maana katika ukurasa hupigiwa mstari ili kuonyesha umaana wake
lakini kama maneno ya ukurasa mzima umepigiwa mstari maneno hayo hayana maana
tena. Sivema kuanza na sauti kubwa na kuendelea nayo Muhubiri 10;10 kama chuma hakinoi itakusa kutumia nguvu
kubwa zaidi., si kila wakati sauti kubwa ni sauti ya Mungu 1falme 19;11-13 kwa
hiyo hata kama unahubiri polepole lakini kama maneno yako yana nguvu na upako
yatasaidia kufikisha ujumbe.
6.
Tamka
maneno yako vizuri
Maneno yako
ndiyo ya muhimu na ya maana sana na ndiyo yanayotakiwa kusikiwa na watu hivyo
ni muhimu yakitamkwa kwa ufasaha na vema zaidi Mathayo 5;2 Akafunua kinywa
chake akawafundisha, usizungumze na
kusikika kama Nyuki, zungumza maneno yako wazi tamka vema na acha nafasi kila unapokuwa umezunghumza
neno uziyaunganishe kama charahani na wakti huo huo epuka kutumia maneno ya kujazia “Gape filler” yaani maneno yenye
kutafuta kujazia nafasi unapokuwa umekosa cha kusema maneno haya ni kama vile Bwana asifiwe,
haleluya n.k na ni muhimu maneno hayo
yakatumika mahali husika panapo mtukuza Mungu sio “Yuda akaenda akajinyonga
Bwana asifiwe”!
7. Tumia vema vihisisho muafaka
Ni muhimun
kuhubiri bila ya kutumia vihisishi kuliko kuvitumia mahali ambapo sio muafaka,
kwa mfano baadhi ya wahubiri huonyeha mikono lakini haiendani na kile
anachokihubiri maana yake kama unaonyesha mbinguni juu basi mikono yako
ionyeshe ju na sio vinginevyo kumbuka mwili unawasiliana.
8.
Zungumza
kwa kutumia mikono.
Pampja na
matumizi sahii ya mikono sio vema kutokuitumia mikono na kuamua kusimama kama
askari, tumia mikono yako unapozungumza katika maeneo ya kuuliza msawali,
kuheshabu, kuhaidi, kubariki, kuhairisha, kukaribisha, kukubali, kuonyesha furaha
au huzuni n.k. sehemu nyingine za mwili zinasaidia kuonyesha muhubiri anahubiri
nini lakini mikono ni zaidi.
9.
Kumbuka
kuwa watu wanaangalia uso wako.
Watu wataupokea ujumbe wako vema kama uatakuwa una uso laini wa kuliko uso mgumu, watu wengi hawapokei ujumbe kwa muhubiri mwenye uso wa jiwe, uso wa aina hiyo unachosha sana uso wa aina hii unatewngeneza hali ya kupingwa wakati wote, unaweza kusema maneno magumu bila kuwa na uso mgumu kwa msingi huo uwe mcheshi na uonekane mwenye kukubalika zaidi kuliko kuwa mgumu.
Watu wataupokea ujumbe wako vema kama uatakuwa una uso laini wa kuliko uso mgumu, watu wengi hawapokei ujumbe kwa muhubiri mwenye uso wa jiwe, uso wa aina hiyo unachosha sana uso wa aina hii unatewngeneza hali ya kupingwa wakati wote, unaweza kusema maneno magumu bila kuwa na uso mgumu kwa msingi huo uwe mcheshi na uonekane mwenye kukubalika zaidi kuliko kuwa mgumu.
10. Waangalie watu unaowahubiri.
Wako wahubiri
wengine hawaangalii watu wanapohubiri utawaona aidha wanaangalia chini au juu
tu , au wanazungumza na mahubiri yao yaliyoandikwa kwenye karatasi au
kuiangalia Biblia tu kwa ujumla hili sio
jambo jema hakikisha unawaangalia watu
wako kwani macho yaweza kufanya m,akosa mengi wakati wa kuhubiri
Hakikisha kuwa
unafanya bidii kuzingatia kanuni hizi kumi za muhubiri na hakikisha kuwa
unawafurtahisha watu na ndipo, itakuwa vigumu watu makosa kwani wnafgurahishwa
nawe hata kama una udhaifu kimwili basi hakikisha kuwa unanguvu katika ujumbe
wako 2Koritho 10;10.
SURA YA PILI: MUHUBIRI NA
VYANZO VYA MAHUBIRI
Utangulizi
Kila muhubiri
anajua kuwa anapaswa kuhubiri lakini swala la kuchangua au nini cha kuhubiri
huwa ni jambo gumu sana kwa wahubiri wengi, lakini inatupasa kulihubiri neno
2Timotheo 4;2 lakini ni sehemu gani ya kuhubiri
hapo ndipo inakuwa shughuli
Kila mchungaji mwenye uzoefu anajua kuwa
inapofika siku ya jumamosi na huku bado hujapata ujumbe au hujui nini cha
kuhubiri presha inakuwa juu sana na shughuli ya kuchagua nini cha kuhubiri
linakuwa swala gumu sana hasa ikiwa
hujui ni nini utakisema jumapili, katika baadhi ya madhehebu huwa wanaaandaa mahubiri ya kila juma pili na hivyo inakuwa rahisi kwa
wachungaji wa madhehebu hayo kuwa na Muda wa kupumzika na kulala vizuri usiku wa jumamosi, Swala hilo
lina faida Fulani kwani muhubiri anakuwa na amani na inamsaidia namna ya
kupangilia ujumbe wake
Lakini kwa
namna nyingine Mchungaji anapaswa kuwa wazi kwa Roho wa Mungu, katika somo hili
pia nitakusaidia kupata kanuni kadhaa za kukusaidia kupata ujumbe na masomo
mazuri kwaajili ya mahubiri yako
Masomo na mada
Ni muhimu kufahaku kuwa hutuba nyingi
zinzzohutubiwa na watu hususani za kibiblia
zinagusa maeneo muhimu kama nane
tu, ambayo ni watu na vitu, maeneo na
matukio, michakato na mawazo, matatizo na mipangoau suluyhisho
·
Kuhusu
watu na vitu
Katika
biblia tumebarikiwa kuwa na hadthi za watu mbalimbali kama Ibrahimu, Isaka na
Yakobo au Yusufu, manabii kama Yeremia, Isaya na Daniel na nyingi ya hizi
hadithi ziko katika Agano la kale na kwa kuzingatia kuwa kuna nukuu za kila
aina ya hadithi katika Agano jipya pia na unapotumia itifaki ya Biblia utaweza
kuona hadithi nyingi sana kupitia majina ya watu na maandiko yao wengi wa watu
hao wana mabo mazuri na mabaya ambayo tunaweza kujifunza
§
Ibrahimu mfano katika Waebrania 11;8
§
Isaka mfano katika Wagalatia 4;28
§
Yusufu mfano katika Waebrania 11;22
§
Isaya mfano katika Marko 7;6-7
§
Yeremia mfano katika Mathayo 16;13-14
§
Daniel mfano katika mathayo 24;15
Kwa hiyo kumbe kupitia watu tunaweza kupata
jumbe mbalimbali za kutufunza mambo kadhaa katika Biblia na pia tunazo habari za kina Stefano, Petro,
Paulo Yesu na wengineo wengi ambao tuinaweza kujifunza vitu kutoka kwao,
wengine walikuwa na maadui kama Eliya na Yezebel, wengine walikuwa mashujaa na
walikuwa na madhaifu yao n.k haya yote ni ya muhimu kwaajili ya kutufunza sisi,
wengi wa waliotajwa katika bilia walikuwa ni watu halisi na habari zilikuwa
halisi ispokuwa katika baadhi ya mifano vingine vilitungwa kwa kusudi la kuleta
somo Fulani hii hasa ni katika mifano , hadithi nyingine sio nzuri lakini ziko
kwaajili ya kutufunza sisi kufanya vizuri na sio kurudia makosa yale,
Vitu
pia vina sehemu kubwa katika kutufundisha
wanayama , ni vitu, Pepo ni vitu kwa mfano Yesu alitumia mfano wa maua
ya mashambani Mathayo 6;28 kuweza kuwasilisha somo lake kuhusu kujali kwa
Mungu.
·
Maeneo na
matukio
Wakati
mwingine kuna matukio yanayotajwa pamoja na maeneo au maeneo na matukio ya
maeneo husika mara nyingi hutajwa pamoja katika maandiko haya nayo hutusaidia
kupata vitu vya kutufundisha na vya kuhubiri mfano Yeriko na swala la ukuta
Yoshua 6, Babel na swala la mnara Mwanzo 11;1-9, mlima wa faragha na Badiliko
la Yesu Mathayo 17;1-8, anguko la mwanadamu na Bustani ya Edeni, Kana na
muujiza wa maji kuwa Divai haya yote hutusaidia katika kupata jumbe za
kuihubiri yaani maeneo na matukio
·
Michakato
na mawazo
Michakato
ni hatua zilizopitiwa au zilizofanyika kuonyesha jambo Fulani lilivyoweza kuja
kutokea kuna aina hoiyo ya habai nyingi sana katika Biblia mfano Imani chanzo
chake ni kusikia Warumi 10;9 na Matendo 2;38 , aidha kuna wazo la upendo wa
Mungu, kuwekwa huru, maadili n,k na
maandiko yako kama Yohana 3;16, Ufunuo 6;10,16;5 zinazungumza kuhusu Mungu.
·
Tatizo na
mipango
Kwa
sababu watu wote hupatwa na matatizo mara nyingi basi ni muhimu kufahamu kuwa
wakati mwingi jumbe zetu zitakuwa na malengo ya kuondoa matatizo yanayowakumba
watu baadhi ya matatizo hayo ni kama
Dhambi, Magonjwa, vita matatizo ukimbizi, uchafuzi wa mazingira, umasikini,
rushwa, kukoseka na kwa haki, dhuluma na
matatizo mengineyo chungu nzima
Sasa
kama unahitaji kutatua matatizo hayo inakupasaa kuwa na mipango nah ii
itakulazimu kupanga jumbe katika mtindo unaohusika na kushughulika na tatizo
moja baada ya jingine
KANUNI
KUMI ZA KUKUSAIDIA KUPATA JUMBE
Unapaswa
kujitoa kila siku Daily devotions
·
Kila siku unapojitoa katika kuisoma Biblia na
kuomba Roho wa Mungu anakuwa na kitun
cha kusema nawe hiki ni mbegu ya kuweza kukupatia au kustawisha
ujumbe na unapokuwa na Muda wa
kutafakari ujumbe huo unakua na kama mchungaji unakuwa na shughuli kuliko
kawaida ni ngumu kwako kupokea jumbe kutoka kwa Roho wa Mungu hivyo uinapaswa
kubadili mwenendo
Unapaswa
kuisoma Biblia yako kila siku
·
Kumbuka kuisoma Biblia yako mara kwa mara na
unaweza kuisoma kwa mpangilio maalumu usiisome hovyohovyo, soma kifungu mara
nyingi katika njia tofauti toafauti ,
soma kwa kujiuliza maswali ili upate kuilewa
mfano mwandishi ni nani, walengwa ni akina nani, neno kuu ni lipi, tatizo
kuu ni lipi na majibu ya tatizo hilo ni yapi yalitolewa kisha ombea kile ambacho umekisoma kisha
jitahidi kuelewa kile ulichokisoma
Unapaswa kuwasoma watu wako
·
Baadhi ya jumbe zinapatikana kwa kuwasoma watu
wako, wahubiri wanapaswa kuwasoma watu wao kama vile wanavyoisoma Biblia ni makosa kujua watu waliishije nyakati za
kanisa la kwanza kisha tukashindwa kuwatambua watu ambao tunaishi nao hakuna
mtu anaweza kuwa mkweli kwa Biblia kama atashindwa kuyatumia kwa watu husika tulio nao leo.
Neno la Mungu lili tolewa kwa wanadamu na
sio wanadamu kwa neno Mahubiri yote
mazuri ni yale yanayohusu tatizo la mwanadamu na kutoa suluhisho la Kiungu
kutokana na neno la Mungu katika Biblia unapowasoma watu wako utyajua kuwa ni
jumbe gani zinapaswa kuhubiriwa, jumbe hizo ni lazima zitokane na neno la
Mungu ingawa uvuvio kuihusu ni ni cha kuhubiri unatokana na unavyowaona
watu, huitaji kusikia sauti kama radi ili kujua kuwa Mungu anataka nini kama unaona liko hitaji kwa watu huitaji
kutafuta jambo lingine.
Epuka kuhubiri jumbe zenye utata
·
Ujumbe
wowote ambao hauko wazi kimaandiko ni muhimu kujitahidi kuepuka kuhubiri jumbe
hizo baadhi ya jumbe zenye utata wa kitheolojia katika Biblia ni pasmoja na
Ø
Ubatizo wa wafu 1Koritho 15;29
Ø
Tofauti kati ya ufalme wa Mungu na ufalme wa
mbinguni ingawa tunajua kua ni jambo moja
Ø
Malaika walioasi wasioilinda Enzi yao 2Petro 2;4
Ø
Malaika Mikaeli kugombania mwili wa Musa Yuda
1;9
Ø
Yesu kuhubiri Roho zilizokuwa kifungoni 1Petro
3;19
Jumbe hizi ni jumbe ambazo zina
utata unaweza kuchangia wazo Fulani kuhusu lakini uzizifanye kuwa ni ujumbne wa
somo
·
Ujumbe
wowote ambao hauwezi kufanya kazi katika nyakati zetu au katika jamii yetu mfano wa jumbe hizo ni
kama
Ø
Salimianeni kwa busu takatifu
Ø
Kuvunja chombo cha dongo kilicho najisi Walawi
15;12
·
Ujumbe
wowote ambao hautafasiri maandiko kwa halali.
Ø
Watu wanaotumia
vibaya Mithali 6;2 kukiri mambo mazuri tu Possitive Confession si kila
wakati mafundisho hayo ni sahii
Ø
Biblia wakati mwingine inatutaka tuungame makosa
yetu Yakobo 5;16, udhaifu wetu 2Koritho 12;9-10. Lkukosa kwetu hekima Yakobo
1;5 na kuugua kwetu Yakobo 5;14
Ø
Andiko linguine litumikalo vibaya ni pamoja na
Yohana 11;26 Yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa andiko hili Yesu
alikuwa akizungumzia Maisha ya kiroho Yesu alionyesha wazi kuwa tutakufa Yohana
16;1-3, 21;1
Chagua viini vikuu
Si vibaya kwa mchungaji kuhubiri jumbne za aina mbalimbali kwa msingi
huo unaweza kuwa na masomo mengi na ya aina mbalimbali kulingana na aidha
kuhubiri kuhusu misingi ya imani ya kipentekoste au imani ya kanisa mfano
tunaamini katika maswala yafuatayo na kila swala ni somo au mafundisho unaweza
kufundisha kuhusu mambo kadhaa yafuatayo
·
Maandiko yamevuviwa
·
Mungu mmoja wa kweli
·
Uungu wa Yesu Kristo
·
Anguko la mwanadamu katika dhambi
·
Wokovu wa mwanadamu
·
Maagizo makuu ya kanisa
·
Ubatizo wa Roho Mtakatifu
·
Ushahidi kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu
·
Mafundisho kuhusu Utakaso
·
Mafundisho kuhusu kanisa na wajibu wa kanisa
·
Mafundishoi kuhusu Huduma
·
Mafundisho kuhusu Tumaini lenye Baraka
·
Mafundisho kuhusu utawala wa miaka 1000 ya
Kristo Duniani
·
Mafundisho kuhusu hukumu ya mwisho
·
Mafundisho kuhusu mbingu mpya na inchi mpya
Unaweza pia kuhubiri kuhusu, majaribu, maombi, msamaha, uwakili wema, kutembea
kwa imani, namna ya kushinda hali ya kukata tamaa, tamaa, kuupenda ulimwengu, kuwa
makini, matendo mema, Ndoa na nyumba na mengineyo mengi.
Hubiri kutoka katika Agano la kale pia
Baadhi ya wahubiri na wachungaji
hawalitendei haki agano la kale katika kuhubiri kwao, tunapaswa kuhubiri
pia kutoka katika agano la kale lakini
hatupaswi kuhubiri kana kwamba tuko chini ya sheria za agano la kale wanaweza
kuhubiri kutoka katika agano la kale mfano Kumbukumbu 28;7 wakati Biblia
inasema katika Mathayo 10;23, si kila wakati adui atatukimbia kuna wakati inatupasa
sisi kukimbia kwa maana hiyo muhubiri anapaswa kuwa na ujuzi wa kutosha katika
somo linalohusu jinsi ya kutafasiri na kutumia kwa ahalali maandiko
Hermeneutics, Wako wahubiri wengine wana lipuuzia kabisa agano la kale
hawalihubiri kabisa, Agano jipya lina nukuu 1100 kutoka katika agano la kale,
waamini wanapaswa kujifunza mambo mengi kutoka katika agano la kale wanapaswa
kujua kuhusu
·
Habari ya uumbaji
·
Vivulikuhusu Kristo (Typology)
·
Masomo mbalimbali kuhusu watu wa agano la kale
·
Mambo makuu katika Zaburi
·
Hekima mbalimbali kutoka kwenye Mithali
·
Maswala ya manabii na unabii
·
Kanuni kadhaa za maisha kama amri kumi.
Endapo mchungaji au muhubiri atayazingatia hayo ataweza kuwa na masomo
mazuri na mahubiri mazuri na hatakosa kitu cha kusema na kuhubiri kwa watu wake
maandalizi ya mapema kuhusu jumbe kama hizi zitamfanya mtumishi wa Mungu kuwa
na ujasiri wa kutosha anapokuwa anatoa hutuba
Kanuni nne za mwishoni zinauhusiano na mipango wakatiwa wa utoaji wa
hutuba
Hakikisha kuwa unatoa mlo kamili.
Ni muhimu kufahamu kuwa wako watu ambao
hujifanya kuwa wanaongozwa na Roho lakini wakati huo huo wanapingana na maswala
ya kupangilia jumbe, wanasahahu kuwa Roho wa Mungu naye anauwezo wa kuwasaidia
katika kupanga namna watakavyo hubiri jumbe zao, kuto kuwa na mipango katika
namna ya kuhubiri au jumbe za kuhubiri kunakuweka katika hali ya kujaribiwa
kuhubiri jumbe zilezile na hapo ndipo inapokuwa sawa na kuwalisha watu wa
chakula cha aina ileile inaweza kutushangaza kuwa inakuwaje mtu anayeongozwa na
Roho Mtakatifu akashindwa kuongozwa kupangilia jumbe Roho wa Mungu aliweza
kumpa Isaya jumbe kuhusu kuzaliwa kwa masihi miaka 750 kabla, Kanisani na chuo
cha Biblia ni wapi pa kiroho zaidi? Kwa
kunena kiwazimu chuo cha Biblia ni pa kiroho zaidi, kwa sababu ndipo mahali
panapoandaa wale wanaokuja kuchunga makanisa lakini katika vyuo vya Biblia
Masomo hupangwa mapema kabla, na kama waalimu watashindwa kufanya maandalizi
mapema basi kuna uwezekano wa kushindwa kufundisha masomo muhimu, kwa hiyo
mipango ni muhimu, pamoja na kufunga na kuomba na Roho wa Mungu atatupaka mafuta
tukipanga tunapanga na Roho Mtakatifu
Uwe na mipango kwaajili ya sikukuu
Kila
sikukuu inaweza kumsaidia muhubiri kuwa na somo kwa mfano kila sikukuu ya
krismasi tunahubiri kuhusu kuzaliwa kwa masihi, pasaka tunahubiri kuhusu
kufufuka kwa Yesu Kristo na kila sikukuu kama za uhuru na nyinginezo tunaweza
kuwa na ujumbe maalumu wa sikukuu hiyo, kumbuka kuwa ni kiroho kupanga kuwa na mipango kwaajili ya Mungu ni kwa
muhimu sana Luka 12;13-21 watu wa jinga ni wale walio na mipango ya maisha bila
Mungu, Yesu alihubiri au kufundisha maswala mengine kwa sababu alijua wanafunzi
wake wanawaza nini Mathayo 20;20-28
Pangilia jumbe zako katika mtiririko
unaofaa.
Ni muhimu kuwa na mpangilio wa jumbe ambao una
wiana unaweza kuwa na masomo kuhusu karama za kiroho 1Koritho 12 – 14.
Kumbuka kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu
Ni muhimu
kupangilia jumbe zetu mapema lakini ni muhimu kupanga na Roho wa Mungu au tunapokuwa tumepanga tuwe watu laini ambao
tunaruhusu Roho wa Mungu kuingilia kati kile tulichokipanga soma Matendo 16;9-18;28 mipango ni mizuri
kama tutaruhusu Roho wa Mungu kupanga pamoja nasi
AINA ZA MAHUBIRI (HOTUBA).
Ni muhimu kufahamu
kwamba kuna malengo kila wakati mtu anapokusudia kuhubiri na kutoa hutuba iwe
ya kawaida au ya Kibiblia, Kila aina ya mahubiri au hutuba ina makusudi, katika
makusudi ya mawasiliano wasomi wamegawanya makusudi ya mahubiri au hutubia
katika maeneo makuu Manne na ambayo ni Kufurahisha, kuelimisha au kujulisha,
kushawishi na kuchochea, kila moja ina makusudi yake kama nitakavyo yaainisha
wakati wa kuichambua moja baada ya nyingine
1. Kufurahisha (to entertain).
Kufurahisha
ni moja ya makusudi ya msingi ya hotuba aina hizi za hutuba hutolewa nyakati
za chakula cha jioni, kwenye sherehe
kama harusi au wakati watu wana hisia za kuchoka au wakiwa wamenuna au kwa makusudi mengine madogo madogo bali wakati
mwingine pasipo kuwa na sababu Hotuba hizi si nzuri sana katika msimamo wa
Kikristo kwa sababu kila kitu katikia ukristo kimemaanishwa na hatuna muda wa
mzaha kwa msingi huo aina hizi za hutuba
zinapotolewa katika mtazamo wa Kikristo
zinapaswa kulenga wakati huo huo jambo muhimu la kweli la kiroho na pia
wakati wakristo wana pokuwa katika koinonia za kifamilia za kanisa au wakati wa
mapimziko na kadhalika
2. Kuelimisha au kujulisha (to inform).
Aina
hizi za hutuba wakati mwingine huitwa hutuba za kufunua mambo au jambo
Expository speech kwa sababu inajengwa katika mfumo wa kutoa wazo kama
unapofundisha darasani, au mijadala au muhubiri anapoelimisha kuhusu jambo
Fulani, aina hizi pia hutolewa na kamati mbalimbali kwaajili ya kutoa taarifa
Fulani ambayo imefanyiwa uchunguzi na kamati na wajibu wa kushughulikia utakuwa
ni wa jamii husika,Ni muhimu kufahamu kuwa pia unapomtambulisha mtu aina hiyo
ya hutuba inaweza kuangukia katika kundi hili au unapomuelekeza mtu au
kuzungumzia maswala ya utalii kwa lengo la kutangaza, na pia unapochanganua
vifungu Fulani katika maandiko yaani Biblia na kuvifanya kueleweka kwa
wahusika aina hizo za hutuba ni za
kuelimisha au kujulisha.
3. Kushawishi (to Parsuade).
Ni
hutuba zenye mlengo wa kushawishi katika hutuba kama hizi unatakiwa kutumia
hoja ya nguvu logic na kuinua hisia za
watu, hutuba kama hizi hutumiwa zaidi na wainjilisti au wanasiasa wanapokuwa
katika kampeni lakini hata wachungaji huzitumia aina hizi za hutuba wanapokuwa wanawaita watu kuokoka, au
kuchochea utoaji kwaajili ya jengo au jambo fulani kusudi hasa ni kuhitaji
mwitikio wa mkutano kukubaliana na
muhubiri aina hizi za hutuba pia hutumiwa na wafanya biashara au wakati wa kampeni ili kushawishi wapiga
kura au katika mtindo wa maandalizi
kwaajili ya kuwa kiongozi baadaye, inaweza kutumika katika kushawishi uwekezaji
na maswala mengineyo lakini kumbuka kusudi letu hapa ni hutuba za kibiblia.
4. Kuchochea (to actuate)
Aina hizi za
hutuba hazina malengo ya kuushawishi mkutano kuona kuwa jambo hili ni zuri au
baya hapa unachojaribu kukifanya ni
kuwafanya wafanye katika mtazamo wa kikristo aina hii ya hutuba inataka mtu
ajikabidhi ajitoe afanye mfano Mathayo 4;19 Nifuateni nami nitawafanya ninyi
kuwa wavuvi wa watu, hili ni jambo la kimaisha ni la kudumu ni la kila siku kwa
hivyo wanafunzi walipoambiwa hivyo walitakiwa kuacha kila kitu na kutekeleza
kile alichokisema na kukitenda kristo
aina hizi za hutuba kwa wakristo ni njema na zenye matokeo mazuri, kwa
jamii ya kawaida aina hizi za hutuba
zina makusudi ya aidha kuwafanya watu waache au kupigana vita (mfano
uwezo wa kumpiga tunao nguvu za kumpiga tunazo sababu za kumpiga tunazo
tunataka dunia ituelewe hivyo) na mara nyingi hufanyika maamuzi ya muda mfupi
wakati ya kikristo ni ya maisha yote.
Hotuba za kimatukio (Speech for Ocasions)
Hizi ni hutuba zinazo husiana na matukio
mbalimbali mfano Kukaribisha (Courtesy), na za kukubali makaribisho, hutuba za
utambulisho introduction, hutuba za kutambua mchango wa mtu au kumuaga Tribute
na kadhalika kwa kawaida hotuba za aina hii huwa ni fupi na sio ngumu sana ingawaje ni za muhimu kwa watumishi kujifunza
na kuwa na Ufahamu wa aina hizo za hutuba .
Hotuba za kukaribisha (Courtesy)
Kwa
kawaida aina hii ya hutuba inapaswa kuwa yenye uzuri na yenye kumfanya mgeni kukubalika kwa watu
wanaomsikiliza inaweza kuwa mgeni wa kikristo au hata asiye mkristo lakini hilo
halimfanyi mkristo kuwa sio mkaribishaji mzuri na kama umechaguliwa kwaajili ya
kutoa aina hiyo ya hutuba ni muhimu kwa
mtoaji wa aina hiyo ya hutuba kujiuliza maswali yafuatayo kwaajili ya
maandalizi
·
Kwa nini nitatoa hutuba hii?
·
Kwa kina nani ninatoa hutuba hii?
·
Je ninajua sifa gani kuhusu mtu
nitakayemtambulisha au mtu ninayemzungumzia?
·
Je nitawakilisha vipi umuhimu wa wa tukio hili la kihutuba
·
Hakikisha kuwa unatumia lugha nzuri badala ya
kutoa maoni yako kuhusu mtu huyo na wakati huo huo hakikisha kuwa unapata
usikivu wa kutosha kutoka kwa watu, watosheleze watu kuhusu utambulisho wako, wape
picha ya kile wanachotarajia kukipata si lazima hatua hizi zizingatiwe kila
wakati utakapotoa hutuba ya aina hii.
AINA
ZA JUMBE ZA KIBIBLIA
Kuna aina
nyingi sana za jumbe za kibiblia za kuhubiri kwa ujumla kuna aina kuu kama Nane
za ujumbe ingawa tatu tu za jumbehizo hufundishwa sana katika vyuo vya Biblia. Hebu kwanza tuziangalie jumbe zote kisha
tutazungumzia zile ambazo hutumiwa sana katika vyuo vingi vya Biblia na
kukaziwa sana
Aina za jumbe
·
Ujumbe unaotokana na andiko Textual Sermon
·
Ujumbe wa somo au mada Topical Sermon
·
Ujumbe unaotokana na alama kivuli kuhusu Kristo
na mengineyo typical Sermon
·
Jumbe za vifungu zinazofunua kweli za kibiblia
Expository Sermon
·
Jumbe kuhusu maisha ya watu Biographical Sermon
·
Jumbe za kuchimba na kuchanganua somo kwa undani
Analytical Sermon
·
Jumbe za kuoanisha mambo au kulinganisha
Analytical Sermon
·
Ujumbe wa kuchambua mstari kwa mstari, sura kwa
sura na kitabu kwa kitabu Runing commentary Sermon.
Jumbe kuu
ambazo huubiriwa sana hutumika sana na kusisitizwa sana katika vuyuo vya Biblia
ziko Tatu kati ya hizo ni
1.
Ujumbe wa somo au mada Topical Sermon
2.
Ujumbe unaotokana na andiko Textual Sermon
3.
Jumbe za vifungu zinazofunua kweli za kibiblia
Expository Sermon
Ujumbe wa somo au mada topical sermon
Huu ni ujumbe
unaotokana na somo au wazo au kichwa ambacho aidha muhubiri anaamua au Roho wa
Mungu anampa wazo na baadaye unalipanga
wazo hilo katika migawanyo yake Bila kutegemea mistari au kifungu cha kibiblia,
somo lenyewe au wazo lenyewe ndio huwa kiini cha somo husika ujumbe wa somo
hauitaji mstari kutoka katika Biblia kama kiini cha kuanzia bali unahitaji wazo
la jumla la kibiblia na ambalo litaungwa
mkono na maandiko mbalimbali ya kibiblia
jumbe hizi hubeba kiini kimoja ambacho huwa kama mada mtu anapokuwa anataka kuuzungumzia kwa msingi huo basi ujumbe wa somo au mada
unaweza kujengwa kwa mawazo mabalimbali na kisha yakawa na umbile toka katika
maandiko mbalimbali ya Biblia mawazo hayo ni kama
-
Maana ya maombi
-
Nguvu ya maombi
-
Umuhimu wa kuomba
-
Matokeo ya maombi
-
Jinsi ya kuomba
-
Mifano ya watu waombaji
-
Maombi ya kufunga na kuomba
Kwa hiyo hapo
somo kuu ni maombi lakini hata hivyo kila mgawanyo unaweza kuwa somo au unaweza
kuwa somo au mada na ikazungumziwa kwa muda mrefu wa kutosha kwa hiyo wazo ni
maombi lakini ndani yake unapata mambo mengi kuhusu maombi na yako maandiko
mengi pia ya kutumia katika kufundisha juu ya maombi
Tatizo kuu la
ujumbe wa somo ni kuwa ni rahisi kuisingizia Biblia kusema kile ambacho haija
kisema au kutumia maandiko mahali ambapo si halali kwa andiko hilo kutumika na
kwa sababu hiyo kukiuka kanuni za kutafasiri maandikokwa halali hata hivyo ni
nzuri kwa watu wenye mapenzi mema, aina hii ya ujumbe hufananishwa na mbuzi
ambaye hana kamba anakuwa huru kula kokote anakotaka kula.
Mfano wa
ujumbe wa somo
SOMO:
JINSI YA KUOMBA
Mstari wa Msingi Luka 11;1 “Ikawa
alipokuwa mahali Fulani akiomba , alipokwisha mmoja katika wanafunzi wake
alimwambia Bwana tufundishe sisi kusali kama vile Yohana alivyowafundisha
wanafunzi wake”
Mara tu baada ya mtu kuokoka na kufanyika mtoto wa Mungu Yohana 1;12 inakuja shauku na hamu kubwa ya mtu huyo kutaka kuwasiliana na Mungu
aliye baba yake wa Mbinguni. Mawasiliano
hayo yanafanyika kwa njia ya maombi, Yesu kristo kiongozi mkuu wa wokovu wetu
waebrania 2;10 alikuwa mwombaji mkuu, Alfajiri na mapema sana alikuwa anakwenda
mahali pasipokuwa na watu akawa anaomba
Marko 1;35 Jioni pia alikuwa akifanya maombi Marko 6;46-47 wakati mwingine pia
alikuwa akifanya maombi usiku kucha Luka
6;12 Yesu alichukua muda mrefu wa kuomba
mpaka akalia sana na machozi Waebrania 5;7 , hakukubali kutingwa sana na
shughuli na kukosa muda wa kuomba, wakati mwingine hata katikati ya kilele cha
shughuli zake alikuwa akijiepusha na kwenda mahali pasipokuwa na watu na kuomba
Luka 5;15-16 wakati mwingine aliomba mpaka hari yake au jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka katika inchi Luka 22;44 Mara
nyingi aliwaambia wanafunzi wake waombe ili wasiingie majaribuni halafu yeye akajitenga mbali kidogo nao na
kuendelea kuomba , wanafunzi wake walipojaribu kuomba waliishiwa na maneno hata
ikawa kwao vigumu kuomba hata kidogo Luka 22;39-41 Mathayo 26;40-41 na ndipo
wanafunzi wake walipoona ni vema kumuomba awafundishe jinsi ya kuomba ni
makusudi ya somo hili sasa kujifunza jinsi ya kuomba , Yesu kristo alikuwa muombaji
na alikuwa ni kielelezo chetu Mtu awaye yote aliyeokoka hawezi kufika mbali
katika wokovu wake kama akiwa sio
muombaji tutajifunza somo hili jinsi ya kuomba kwa kuzingatia vipengele vitano
vifuatavyo
·
Mikao inayofaa kwa ajili ya maombi
·
Swala la kuomba kwa sauti kubwa
·
Swala la kuomba kwa kufumba macho au kufumbua
macho
·
Umuhimu wa kuomba kwa jina la Yesu.
·
Matumizi ya sala ya Bwana katika Maombi
Mikao inayofaa kwa ajili ya maombi.
Wako watu wengi sana wanaofikiri
kuwa wakati wote mtu anapotaka kumuomba Mungu ni lazima awe amepiga magoti, hii
sio sahii kwani tunaweza kumuomba Mungu katika mikao tofauti tofauti katika namna nyingine pia kutegemea na
nafasi, Kupiga magoti ni jambo linalimfurahisha Mungu sana wakati wa kuomba Isaya 45;23. Lakini hata
hivyo kuna njia nyingi za kibiblia za jinsi ya kuomba zifuatazo ni baadhi ya
njia zilizomo kwenye Biblia
a. Kupiga
magoti – Tunaona mifano katika Luka 22;41Yesu, Katika Daniel 6;10 Daniel,
katika Zaburi 95;6 Daudi, katika Matendo ya mitume 7;60Stefano, katika Matendo
9;40Petro na katika matendo 20;36,21;5
Paulo mtume na watu wengine.
b. Kupiga
magoti na kukunjua mikono kuelekea mbinguni – Mfalme Sulemani katika 1Wafalme
8;54, 2Nyakati 6;13, na pia Ezra kuhani katika Ezra 9;5.
c. Kuinamisha
kichwa Mwanzo 24;26,Kutoka 4;31, 12;27
na 34;8
d. Kuanguka
kifulifuli uso kugusa Ardhi - Tunaona mfano wa Yesu Mathayo 26; 39. Yehoshafati
2Nyakati 20;18 Eliya 1wafalme 18;42,Yoshua katika Yoshua 5;14,Musa na Haruni katika Hesabu 20;6
e. Kusimama
– Marko 11;25,Luka 18;11
f.
Kusimama na kukunjua mikono kuelekea mbinguni –
1Wafalme 8;22
Hizo zote hapo juu ni njia zinazo
faa kwaajili ya kumuomba Mungu ni mazingira tu ndiyo yatakayoamua njia gani
itumike, kwa mfano huwezi kupiga magoti ukiwa stendi ya mabasi au katika kanisa
lisilo na sakafu Lakini kama mazingira ni mazuri na yanaruhusu kupiga magoti
kufanya hivyo sio tatizo Daniel 6;10, wala sio busara kugusa uso chini mpaka
utoke sugu ili watu wajue kuwa wewe ni muombaji maombi ya jinsi hii ni ya
kinafiki Mathayo 6;1-5, Biblia inatufundisha kuwa mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu 1Koritho 14;40 kwa
msingi huo inatupasa kuchagua ni wapi na
ipinjia ipi inafaa na kuitumia kwa mfano
ukiwa una usingizi ukapiga magoti ili kuomba ni rahisi kulala usingizi hapo
njia sahii ni kusimama na kutembea huku unaomba itakusaidia kutokulala unaona.
Swala la kuomba kwa sauti kubwa
Kumekuwako na utata wa
kitheolojia kuhusu kuomba kwa sauti kubwa ikifikiriwa kuwa kufanya hivyo ni
kupayuka payuka kunakotajwa katika Mathayo 6;7-8 lakini tafasiri hiyo sio
halali katika Biblia ya kiingereza King James Version ambayo ni tafasiri iliyo
karibu na lugha za asili zilizoleta Biblia kwetu kiibrania na kiyunani Mathayo
6;7 husomeka hivi “But when ye pray use not vain repetitions as the heathen do”
kwa msingi huo kupayuka payuka ni kurudia rudia maneno yale yale kama kasuku
hii ilifanywa na mataifa kwa sababu hawajui kuomba hawana maneno mengi ya kutosha kujieleza
mbele za Mungu. Hivyo kuomba kwa kupaza sauti sio kupayuka Biblia imejaa mifano
ya watu wengi ambao waliomba kwa kupaza sauti na hata kulia sana machozi kama
alivyofanya Bwana Yesu Biblia inatoa ushauri wa kufanya hivyo
Waamuzi 2;4,21;21Samuel 30;3-4
Mithali 2;3-6 zaburi 77;1 Matendo 4;24
kuomba kimya kimya au kwa kupaza sauti kote ni sawa mbele za Mungu nako
pia kunategemea na mzingira, kwa mfano sio busara kufanya hivyo kwenye nyumba
ya kupanga au mahakamani ukiwa kizimbani
au wakati mumeo anayepinga wokovu akiwa chumbani anakusikia ukimuombea Niokoe
na Mume huyu mkaidi anayepinga wokovu n.k. maswala kama hayo ungeweza kuyaomba
kimyakimya Mathayo 7;6.
Swala la kuomba kwa kufumba macho au kufumbua macho.
Swala la kufumba macho au
kufumbua ni swala linalohusiana na maswala ya kisaikolojia kwa Mungu hakuna sharti Yeye huweza
kuwasiliana na mwanadamu hata akiwa amelala usingizi kwa njia ya ndoto, na hii
haina maana kuwa ukifumbua macho ndo kuna kitu utakiona wakati mwingine mtu anaweza kuona maono akiwa
amefumbua macho na macho hutumika
kuyaona maono hayo lakini roho zetu
huitwa zimezimia kwani tunakuwa hatuko katika hali ya kawaida Matendo 10;9-12 wakati mwingine kufumbua
macho kunaweza kusababisha kuingiza picha au mambo ambayo yatatutoa katika
kuzingatia mwelekeo wetu kwa Mungu kwahiyo hili nalo ni swala la kisaikolojia
na kimazingira kwa mfano kama unaendesha gari unaweza kuomba lakini sio kwa
kufunika macho
Umuhimu wa kuomba kwa jina la Yesu.
Kuomba kibiblia ni kuomba kupitia
jina la Yesu hili ni jambo la muhimu namna yoyote ya kutumia vitu
vilivyochongwa au kutengenezwa kwa shaba, mbao, dhahabu , fedha n.k na kuvisimamisha kati yetu na Mungu na kuviangalia wakati wa kuomba na kuvitaja ,
kuvitumia, kuviangalia au kuvitafakari
na kufikiri kuwa vitafanikisha sala zetu hiyo ni ibada ya sanamu ambayo
ni machukizo makubwa mbele za Mungu
Kutoka 20;4-5,1Yohana 5;21,1Wakoritho 10;14 Isaya 31;7, Sanamu yoyote au lozari
na vitu vyote vya jinsi hiyo siyo sehemu ya maelekezo ya jinsi ya kuomba katika
Biblia , Mungu ni Roho nao wamwabuduo au kumuomba wanapaswa kumuabudu katika
roho na kweli na siyo kwa kutumia kitu chochote kinachoonekana Yohana 4;23-24,
aidha ni muhimu kufahamu kuwa kuwaomba wafu pia ni chukizo kubwa mbele za Mungu
Kumbukumbu 18;9-12, kuwaomba watakatifu ambao wamekwisha kufa kama Petro,
Yohana, Paulo, Bikira Maria, Yusufu .n.k watuombee sio sahii kibiblia kila
mmoja anapaswa kuomba mwenyewe na kuzungumza na Mungu kwa jina la Yesu na
ukifanya hivyo anakusikia na kupokea dua zako,
Kila mtoto wa Mungu ana haki sawa
kabisa na mwenziwe anapoomba kila
aombaye hupokea Yohana 16;24, Luka 11;9-11 Biblia inaonyesha kuwa ni wawili tu
wanaotuombea hao ni Yesu Kristo na Roho
Matakatifu nao hufanya hivyo bila sisi kuwaomba watuombee 1Yohana 2;1 Warumi
8;26-27 Tukifanya jinsi neno la Mungu linavyotuongoza na kulitii ndipo tutakapofanikiwa
katika njia zetu Zaburi 119;9, aidha ni muhimu kufahamu kuwa kuwaombea wafu pia
siyo sahii Biblia inasema katika Waebrania
9;27 kuwa mtu amewekewa kufa mara moja tu na baada ya kifo ni hukumu,
tunaweza kuomba kwa ajili ya wale walio hai ili waokolewe kabla hawajafa lakini
inapotokea mtu amekufa hakuna kinachoweza kubadilika 1Yohana 5;14-16
Maombi yetu ili yaweze kuwa na
mafanikio inatupasa kumuomba Mungu baba kwa kupitia jina la Yesu Yohana 16;23,
sio maelekezo ya Biblia kumuomba Mungu kupitia Mariam kwa mawazo potofu eti ukipitia kwa mama wa
Mungu ndio utajibiwa kwa sababu kina
mama wana huruma ni muhimu kufahamu Kua
Maria kamwe sio mama wa Mungu Mungu hana mama wala Baba hana mwanzo wa siku zake
wala mwisho wa siku zake hali kadhalika
kwa Yesu Kristo hivyo hivyo Waebrania 7;3 Yesu hakuanzia maisha yake tumboni
mwa Mariamu yeye alikuwepo hata kabla ya
Ibrahimu hajazaliwa Yohana 8;58, Yesu ndiye aliyeufanya ulimwengu Waebrania 1;2
katika Yesu kila kitu kiliumbwa
Wakolosai 1;13-17 Yeye ndiye aliyemuumba Musa Waebrania 3;1-4 na pia
ndiye aliyemuumba Maria na watu wote,
aliyeumbwa hawezi kuwa mama wa aliyemuumba Biblia inaonyesha kuwa Maria
mwenyewe alihusika katika kumuomba Mungu
pamoja na wanafunzi wa Yesu Matendo 1;4,12-14 Bikira Maria kamwe hawezi
kujiita mama wa Mungu kinyume chake alijiita mjakazi wa Bwana yaani mtumwa wa kike wa Bwana Biblia inasema
katika Luka 1;38 “Mariam akasema Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana”
Matumizi ya sala ya Bwana katika Maombi
Mathayo 6;9-13 Yesu Kristo
alipowafundisha wanafunzi wake kuomba aliwaelekeza kuomba kwa misingi inayojulikana
kama sala ya Bwana, kimsingi hakuwa anamaanisha waitamke kama ilivyo na
kuimaliza kama kasuku kama watu wengi wanavyofikiri , Biblia inaposema katika
Mathayo 6;9 “Basi ninyi salini hivi baba yetu uliye mbinguni……” Tafasiri ya
kiingereza ya King James Version inasema “After this manner therefore pray Ye”
tafasiri ya kiingereza ya LIVING BIBLE inasema Pray alon these lines” Katika
Luka 11;2 kwa msingi huo kinachozungumzwa hapa ni kuwa sala ya bwana ni mafundisho
ya msingi ya kutumia katika maombi, kilichozungumzwa ni kuomba kupitia misingi
hii kila tunapotaka kuomba Luka 9;54 Mathayo 20;20-22 Kutamka sala ya bwana
kama ilivyo ingeweza kuchukua dakika mbili tu na isingelikuwa suluhisho la
kufundisha maombi ambao wao walikuwa wakitaka kujifunza kuomba kwa muda mwingi
wa kutosha kama alivyokuwa akiomba Bwana
Yesu vinginevyo Yesu hangeshangazwa na
wanafunzi wake kulala usingizi ikiwa sala Yenyewe ingeweza kuchukua dakika
chache. Mafundisho mengi aliyokuwa akiyatoa Bwana Yesu Mara nyingi yalikuwa
yakihitaji ufafanuzi Mathayo 13;36, na pia mafundisho ambayo wanafunzi waliweza
kuyaelewa leo yanahitaji ufafanuzi
Mathayo 13;51 Mengine ambayo yalikuwa magumu kueleweka kwa wanafunzi kwa
mfano habari za kuteseka kufa na kufufuka sio tatizo kubwa kueleweka leo Marko
9;30-32, Luka 24;44-45 na ndio maana kanisa linahitaji waalimu ambao wanaweza
kufunuliwa na Roho wa Mungu Neno lake
ili kulilisha kanisa 1Wakoritho 2;10.
JINSI YA KUOMBA KWA KUTUMIA SALA YA BWANA.
Baba yetu uliye mbinguni.Mathayo 6;9.
Tunapokuja kumuomba Mungu
inatupasa kufahamu kuwa Yeye ni baba yetu, kama unaweza kuwasiliana na baba
yako wa duniani anayejishughulisha
na na mahitaji yetu na kuyajali ni muhimu kufahamu kuwa Hatupaswi kumuomba
Mungu tukidhani kuwa yuko mbali ni lazima tuweke mawazo yetu kuwa Mungu ni baba
yetu na kuwa yuko karibu mno tunapomuomba Zaburi 145;18,Zaburi 119;151 103;13
Fahamu kuwa ni baba mwenye upendo mwenye uwezo anayejishughulisha sana na mambo yetu 1Petro 5;6-7 hatupaswi kufikiri kuwa yeye hatujali Zaburi
37;28 Isaya 49;14-16,1Wakoritho 10;10. Aidha uhusiano wetu na Mungu lazima uwe
wa baba na mwana maana yake kama hujazaliwa mara ya Pili huwezi kuwa na
uhusiano wa aina hiyo.
Misingi Saba ya kufuata katika maombi yetu Kama alivyotufundisha Yesu
Kristo
1.
Jina
lako litukuzwe Mathayo 6;9.
Maombi yetu
yanapaswa kuanza kwa kumtukuza Mungu na kumsifu si busara kuanza kumimina shida
tulizo nazo mtukuze Mungu kwa uweza wake
na uumbaji mfano Zaburi 104;5-28, mtukuze kwa wingi wa Rehema na huruma zake
Zaburi 103;8 na pia unaweza kumtukuza kwa matendo yake makuu aliyokutendea
Zaburi 106
2. Ufalme wako uje Mathayo 6;9 Baada ya
kuokolewa ujue kuwa umetolewa katika ufalme wa giza au utawala wa shetani hivyo inakupasa kuwakumbuka wengine omba watu
waokolewe katika taifa lako, ombea wale wasio na mafundisho na kuombea kazi ya
Mungu ikiwa ni pamoja na Bwana wa mavuno kupeleka watenda kazi katika kazi yake
Waebrania 12;14 Mathayo 9;37-38.1Wakoritho 10;24,Wafilipi 2;4 Warumi 15;1
3. Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama
huko mbinguni Mathayo 6;10 mapenzi ya Mungu kutimizwa ni watu kuishi sawa na Neno lake tumuombe
Mungu kwaajili ya serikali na wanaotawala duniani 1Timotheo 2;1-4,Mithali 21;1
ombea lolote lililo kinyume na mapenzi
ya Mungu lililotawala duniani mambo kama
rushwa, vita, njaa uonevu, kuzuia Neno la Mungu, kuenea kwa uislamu n.k
4. Utupe leo riziki Yetu Mathayo 6;11 Ni mapenzi ya Mungu baba
yetu kuwa kila mtoto wake apate riziki yake kila siku kuna riziki za aina nyingi Afya Marko 7;25-27, Yeremia 30;17, 33;6
Chakula nguo nazo ni aina za riziki
Zaburi 37;25,1Timotheo 6;8 zaburi 34;10 pia unaweza kuomba kwaajili ya mahitaji
ya wengine na mahitaji mengine
5. Utusamehe Deni zetu kama sisi nasi
tunavyowasamehe wadeni wetu Mathayo 6;12 Deni zinazozungumzwa hapa ni makosa au
dhambi Luka 11;4 katika maombi Mungu anatutazamia tuangalie
mahali tulipomtenda dhambi kwa kuwaza kusema na kutenda kwani dhambi ni kizuizi cha maombi lakini wakati huohuo tunapaswa kuwasamehe
wengine au kupatana na watu tuliokosana nao Luka 17;4 kwani kama
hatujasamehe dhambi zetu pia zinakuwa
ngumu kusameheka Mathayo 6;14-15.
6. Na usitutie majaribuni lakini utuokoe na
Yule mwovu kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele Mathayo
6;13, ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hamjaribu mtu Yakobo 1;13-14 lakini shetani
hatuwazii mema watu wa Mungu na ndiye ambaye anazunguka huko na huko akitafuta
mtu ammeze 1Petro 5;8 Kwa kuwa Mungu ni
mwenye nguvu zote inatupasa kumuomba atuokoe na mipango ya shetani Luka 10;18-19Mathayo 18;18,Daniel 10;11-13
Kemea mipango yote ya shetani juu ya watu wote na kanisa pia kazi ya Mungu na namna yoyote ya kuwazuia watu wasilielekee
Neno la Mungu.
7. Amina Mathayo 6;13 Neno hili amina
maana yake ni na iwe hivyo, baada ya maombi amini kuwa imekuwa sawasawa na kuomba
kwako Marko 11;24 Hivyo mshukuru Mungu kwa imani kwamba umepokea uliyoyaomba
1Thesalonike 5;18 Endelea kuwa mtu wa maombi Yeremia 33;3 penda pia kuwa mwenye
kushiriki siku za maombi kanisani ambako uatajifunza kutoka kwa watu wenye
uzoefu mkubwa wa kuomba na kupata changamoto. Mithali 27;17.
Ujumbe unaotokana na andiko Textual Sermon
Huu ni aina ya
ujumbe ambao unatokana na maandiko yaani mistari kadhaa katika Biblia ambayo
kitaalamu haipaswi kuzidi aya tatu, kichwa na migawanyo ya aina hii ya ujumbe
hutokana na andiko hilo aina hii ya ujumbe ni nzuri na pia maandiko mengine sio
mengi sana huweza kutumika katika kujenga au kuongeza nyama kwa aina hii ya
ujumbe Aina hii ya ujumbe hufananishwa na Mbuzi mwenye kamba ndefu anakula kwa
uhuru lakini sio mkubwa kama wa mbuzi wa ujumbe wa somo.
Mfano wa
ujumbe wa andiko
Andiko Ezra
7;10
Ujumbe Moyo wa
mtumishi wa Mungu
Somo makusudi
ya moyo wa Ezra
1.
Alikusudia kulijua neno la Mungu, kila mtumishi
wa Mungu anapaswa kuwa na moyo wa kujifunza kama ilivyokuwa kwa Ezra, huwezi
kuwapa watu vitu, huwezi kuwa mwalimu mzuri huwezi kuelimisha watu au
kufundisha somo lako kwa ujasiri kama hujajifunza kwanza Ezra alikuwa ni mafno
wa kuigwa
2.
Alikusudia kutii yaani kulitendea kazi neno la
Mungu, Matendo 1;1, 1Koritho 11;1 Ni vigumu kuwaambia watu kufanya jambo ambalo
wewe hulifanyi ili uweze kufanikiwa
katika kuhudumu kwako ni lazima wewe mwenyewe kwanza uwe kilelelezo cha kutosha
watu husoma zaidi matendo kuliko maneno Ezra aliamua kutenda kwanza Yesu
alisema utoe boriti kwanza kabla ya kuondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako
3.
Alikusudia kuwafundisha watu wa Mungu, Kristo
ametuagiza kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wake na kuwafundisha kuyatii
yote aliyo tuamuru, lakini kabla ya kuwaagiza wanafunzi wake kuifanya kazi hiyo
yeye mwenyewe alikaa nao na kuwafundisha wao kwanza na ndio maana Ezra
alijifunza kwanza kabla ya kuanza kuwafundisha wengine.
Sisi
nasi inatupasa kuiga mfano wa Ezra katika maisha yetu ya kila siku Mungu
akubariki
Aina za jumbe
za andiko zinahitaji kusoma kile kifungu
ili ukielewe kwanza , Ufahamu historia ya wakati ule na kuangalia nini kinahitajika leo ndipo
ufanye Exegesis na kutoa maana
iliyofichwa katika lugha za wakati ule uvilete katika matumizi ya wakati
huu na kutumia hatua hizi pia
zinahitajika kwa ujumbe wa Expository.
Jumbe za vifungu zinazofunua kweli za
kibiblia Expository Sermon
Jumbe za aina
hii mara nyingi huruhusu Biblia kujieleza yenyewe na ndio ujumbe wenye kufanikiwa kwa juu kabisa
kuhubiri kusudi la Mungu kwa wasikilizaji ni ujumbe ambao unachambua kifungu
cha maandiko kwa kutafuta maana iliyokusudiwa na mwandishi kisha na kisha
kuutumia kwa wakati ulioko katia ujumbe huu ni rahisi kwa muhubiri kushughulika
hasa na kusudi la Mungu ujumbe huu mara
nyingi ni tofauti na textual yaani ujumbe wa andiko huu unagusa kifungu
kizima na kuanza kuzamisha kwa kuifunua
kweli hivyo hufananishwa na Mbuzi mwenye kamba fupi lakini hula kwa kuzama
chini zaidi aina hizi za jumbe ndizo zenye uwezo mkubwa kabisa wa kulifanya
kanisa kukua na kuwa na ujuzi wa matumizi ya kweli kuhusu neno la Mungu kwa
hiyo inasisitizwa kutumiwa zaidi makanisani na kokote.
Mfano wa
ujumbe wa kifungu cha maandiko ni
SOMO;
UMUHIMU WA KUTUNZA UWEPO WA MUNGU
Mstari wa somo; 1Samuel 4; 12-22.
UTANGULIZI;
Katika mistari hii tuliyoisoma
tunagundua habari zakusikitisha sana katika Historia ya Israel ambazo
hazijawahi kutokea na huenda tukio hili linakumbukwa sana katika matukio
yanayopaswa kukumbukwa, Israel walipigwa vibaya katika vita na wafilisti, waliona njia pekee ya kuleta ushindi katika
maisha yao ni kulileta sanduku la agano la Mungu katika uwanja wa vita na watu
walishangilia sana maana chombo hiki muhimu na kitakatifu sana kilikuwa
kinawakilisha Uwepo wa Mungu Asiyeonekana chombo hiki pia kilikuwa ndio moyo wa
Ibada zao katika hema na Hekalu, Sanduku
la agano liliwakilisha uwepo wa Mungu ambaye ana historia ya kuleta ushindi
dhidi ya maadui wa Israel hivyo hata inchi jirani ziliogopa sana maadui
waliogopa waliposikia chombo hiki kinaletwa katika uwanjawa vita, kwani walijua
yaliyotendeka kuanzia Misri na sehemu
zote ambazo Israel walipitia na kwa kweli kote ilikuwa ni ushindi katika kisa
hiki kuna mambo muhimu ya msingi ya kujifunza kama ifuatavyo;-
·
Umuhimu wa kuutunza uwepo wa Mungu
·
Hasara za kuupoteza uwepo wa Mungu.
·
Kumlilia Mungu kwa ajili ya uwepo wake.
Umuhimu wa uwepo wa Mungu Mstari wa 18a-,19
Ujuzi wa mke wa Finehasi kuhusu uwepo wa
Mungu unaonekana ulikuwa juu kuliko watu woote haiyamkini kuwa mwanamke huyu
alikuwa mcha Mungu hata pamoja na kuwa mumewe alikuwa muovu, Yeye alifahamu
kuwa sanduku kuchukuliwa mikononi mwa wenye dhambi hakuikuwa kitu cha kawaida
katika Israel wote tunajua kuwa Eli alikufa ghafla aliposikia sanduku
limetwaliwa, Mwanamke huyu naye aliingia katika hali ya kufa na kuzaa kwa
uchungu ghafla kwa kusikia sanduku limetwaliwa
ikatika adhabu ambazo ni kubwa kuliko zote ni kutengwa na uwepo wa
Mungu Mwanzo 4;9-14, Kaini alijua kuwa uwepo wa Mungu ni ulinzi mkubwa
sana na kuwa kama mtu atatengwa mbali na uwepo wa Mungu kifo ni halali yake,
Daudi alijiombea alipokuwa anatubu dhambi zake katika Zaburi ya 51;11, alitambua jinsi uwepo wa Mungu ulivyokuwa wa
Muhimu katika maisha yake,Musa alimwambia mungu yakuwa uwepo wako au uso wako
usipokwenda pamoja nasi usitutoe kutoka mahali hapa ( Kutoka 33;1-4,14-15. ) uwepo wa Mungu pia uliitwa utukufu wa Mungu
mwanadamu anapopungukiwa na utukufu wa Mungu.
Hasara za kuupoteza uwepo wa Mungu mstari wa
20-21.
Ujuzi wa mke wa Finehasi
kuhusu sanduku la agano kwa baadhi ya wanawake wa Israel ulikuwa Tofauti wao
walitafuta kumfariji kuwa jipe moyo mkuu
Usiogope maana umezaa motto mwanamume, wao walijua kuwa wanaweza kumtia moyo
kwani hata kama mkwewe amekufa,mumewe amekufa Lakini alitakiwa ajipe moyo kwani
yuko mtoto mwanamume huenda alikuwa mtoto wake wa kwanza na huenda angeendeleza
kazi ya ukuhani kwani babu yake na baba yake walikuwa wamekufa hivyo alikuwa
mtoto wa muhimu sana Lakini mkewe
finehasi aliona kuwa motto huyo hakuzaliwa kwa wakati unaofaa kwani utukufu
ulikuwa haupo umeondoka hapa tunajifunza hasira za kupoteza uwepo wa Mungu
Hata kama tutasoma sana, kuwa katika dhehebu kubwa sana kuliko yote
duniani au la kwanza kutoka kwa mitume
au tukawa madaktari auy tukaimba sana kama ndege au tukawa makuhani au mapadre
au maaskofu wa dini kubwa sana Lakini kama dini hiyo imepoteza uwepo wa Mungu
ni ikabodi haiwezi kuiwa na faida yoyote,ndoa zetu,watoto wetu na chochote kile
kama uwepo wa Mungu hauko havina maana ni hasira kubwa Daudi alifahamu kuwa kwa nabii samweli kuna
uwepo aliamua kukimbilia huko akawa salama adui wakikutafuta wakijua kuwa umejificha
katika uwepo wa Mungu utakuwa salama
Kumlilia Mungu kwa ajili ya uwepo
wake.mstari wa 20-22
Jambo la kushangaza na ambalo halikuwa jema
kwa mke wa Finehasi pamoja na kujua kuwa
tatizo ni utukufu umeondoka badala ya kumlilia Mungu na kutubu ili uwepo wa
Mungu urudi aliamua kufa tu na alikufa kweli wako watu ambao wanajua kuwa
kanisa linapita katika hali ya kupoteza uwepo wa Mungu duniani Lakini badala ya
kumlilia Mungu ili uwepo urudi nao wanaamua kufa badala ya kumlimlia Mungu na
kutubu, wanakubali kuendana na hali halisi ya matukio shetani hata aacha
kupigana nasi hata kama tuna uwepo wa Mungu au hauko na hata kama anaujuzi kuwa
Mungu ana nguvu haachi kushindana nasi hivyo nasi tusiache kumpiga vita kwa
gharama yoyote
UMUHIMU WA
KUTUMIA NYENZO KWAAJILI YA MAANDALIZI YA UJUMBE
Kwa kawaida
kila muhubiri anapaswa kuwa na nyenzo muhimu ambazo zitakusaidia katika kuandaa
maomo ya kibiblia na kwa kawaida uandaaji huendana na utendaji kuhusu kanuni za
kutafasiri maandiko hivyo katika kujiandaa pia muhubiri anatafasiri maandiko
hivyo kazi hizi huenda pamoja nyenzo hizo ni kama ifuatavyo;-
A. ROHO
MTAKATIFU;
1. Ni nyenzo ya kwanza na ya Muhimu
sana mtu awaye yote anayetaka kuwa mtafasiri mzuri wa Maandiko ni lazima
akubali kujazwa Roho Mtakatifu kumbuka kuwa yeye ndiye aliyevuvia watu kuliandika
neno na ni mwalimu anaweza kutukumbusha na kutufundisha kile ambacho Mungu
amekikusudia kwetu hivyo lazima mtafasiri wa maandiko awe amejazwa Roho ikiwa
wale waliokuwa mashemasi nyakati za kanisa la kwanza walizingatiwa kuwa wenye
Roho je si zaidi sana wanaojitia katia kazi ya kuyatangaza Maandiko ona mfano
wa Stefano Matendo 6;8-55 kwanini ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu?
2. Ni Mtafasiri mzuri
(a) Ndiye Mwandishi wa Biblia 1Kor. 2:10-16, Yoh 14:26, 16:13
(b) Anajua kile Ambacho Mungu anakijua
B. HAKIKISHA KUWA UNA BIBLIA ZA MATOLEO
TOFAUTI
1. Biblia ya Kiswahili na za aina mbalimbali
za matoleo ya kiswahili cha kisasa
2.
English Bible matoleo tofauti
3.Zile zilizoandikwa katika Lugha Tofauti
Tofauti (Greek, Hebrew, Latin, Aramaic, etc.)
C. UWE NA UJUZI KUHUSU AINA ZA MATOLEO YA BIBLIA
Kwa kawaida kuna matoleo makuu ya aina tatu
za kibiblia zile zilizotafasiri neno kwa neno Literal translations, Zile zilizotafasiri kutokana na maana
iliyokusudiwa,Dynamic Equivalent na
zile tafasiri huru za lugha za kisasaau matoleo kwa watu maalum Free translation.
Literal translations Dynamic Equivalence translations Free translations
KJV RSV,
Weymoth, NIV JB TEV, MOFFAT, PHILIPS, LB
NASB NAB NEB
NEB GNB
Neno kwa neno Maana kwa maana Tafasiri huru
B.
UWE NA BIBLIA ZENYE MAFUNZO NDANI YAKE
; REFERENCE OR ANNOTATED
·
Uwe na Biblia zenye mafunzo Studies Bible
Zinatoa maana ya baadhi ya aya:
(i)
Mfano mzuri ni Full life study Bible (NIV)Biblia
ya mafunzo ya uzima tele
(ii)
Life Application Bible (LB)
(iii)
Dake Bible
(iv)
Scafield Bible, etc.
C.
COMMENTARIES:
(Zenye uchambuzi wa mstari kwa mstari).
Baadhi ya Commentaries nzuri
ni Pamoja na
1. Adam Clarke’s Commentary
2. The New International Commentary
3. The Evangelical Bible Commentary
4. Mathew Henry Commentary.
F. CONCORDANCES ITIFAKI
o
Itifaki
yenye maneno yafananayo
o
Itifaki
za maana ya meneno mfano Malazi yawe
safi -Ndoa
o
Mlinganio
wa maneno yanayopatikana katika sehemu nyingine za Biblia.
o
Mfano
Upendo upi? – Agape? Phileo? Storge? Eros?
o
Mahali
lilipo neno Fulani
§
Mfano
wa itifaki nzuri ni pamoja na ;-
1. Young’s Analytical Concordance
2. Strong’s Exhaustive Concordance etc.
3. Niv Exhaustive Concodance.
·
Kumbuka nyingine zina Kamusi za kiibrania na
Kiyunani Lexicons (=Dictionaries ).
Muhubiri asiyetumia nyenzo hutumia muda mrefu kuandaa
ujumbe sawa na mtu anayejaribu kukata mti bila ya upanga kama jamaa huyu
anayekata mti kwa kutumia nyundo itamgharimu kutumia muda mwingi na mrefu sana kuliko anayetumia msumeno wa mashine Chainsaw
B.
VITABU
VINAVYOHUSU TAMADUNI ZA KIBIBLIA & MASWALA YA UCHIMBAJI WA MAMBO YA KALE
·
Hii
itakusaidia kuufahamu na kuwa na ujuzi kuhusu mambo ya kale kama na maneno
yaliyotumiwa kama Busu takatifu, Tundu la sindano na mambo mengineyo.
C.
KAMUSI ZA BIBLIA NA ZA LUGHA ZA KAWAIDA &
ENCYCLOPAEDIAS:
Zinafafanua maana ya maneno Mbalimbali kwa
ajili ya maswala ya kibiblia na maswala ya kawaida
1. Kamusi
za kawaida ni pamoja na zile za Kiingereza na kiswahili
(a) English Language Dictionary
(b) Swahili Language Dictionary etc.
(Kamusi)
2. Kamusi
za Biblia ni pamoja na zilizo maarufu kama zifuatazo nyingi ni za kiingereza
(a) Unger’s Bible Dictionary
(b) Pictorial Bible Dictionary
(c) Westminster Bible Dictionary
(d) Greek
Lexicon & Hebrew Lexicon
3. Kamusi za kitheolojia (Theological
Dictionary).
Kwa ajili ya kujifunza Mambo
mbalimbali ya kitheolojia Mfano ni
1.
Baker’s Dictionary of Theology
4. Encyclopedias,
Mfano;
- International Standard Bible Encyclopedia
D.
MAFAFANUZI YA KIBIBLIA (BIBLE HANDBOOKS :)
·
Kwa ajili ya ufafanuzi wa Maswala mbalimbali,
Vifungu, Maandiko, Tamaduni, Matukio ya kihistoria, Ugunduzi wa maswala ya kale (archaeology), na
kadhalika
Mfano
1. Halley’s Bible Hand Book
2. Unger’s Bible Hand Book
I. MASOMO MBALIMBALI AU JUMBE MBALIMBALI
(TOPICAL BIBLE).
·
Vitabu vinavyo weka mpangilio wa ufafanuzi wa
masomo mbalimbali vikiwa na maandiko yoote husika sawa book arranged according to different topics
with all the texts related to each topic.
Mfano Nave’s topical Bible
J.
ATLASI ZA KIBIBLIA NA MSWALA YA KIHISTORIA (BIBLE ATLASS) & HISTORY
Kwa ajili ya kutambua sehemu Mbalimbali na
umbali kwa kilomita za mraba n.k na vipimo kama homeri, yadi, mwendo wa sabato,
Ridhaa n.k
e.g.
1. Baker’s Bible Atlas
2. The Oxford Bible Atlas
MPANGILIO
WA HUTUBA AU MAHUBIRI
Makusudi ya Mpangilio
Karibu kila
kitu ambacho tunakifahamu tumejifunza, kila mmoja kuna eneo Fulani hajui kwa msingi huo si ajabu wanafunzi au
washirika wakawa hawajui umuhimu wa mpangilio wa hutuba zao za kibiblia, kusudi
kubwa la kupangilia ni ni kuweka mambo yaweze kwenda sawa kila moja ana kabati
la nguo au wengi wa watu wana makabati ya nguo au hata masanduku, nguo
zilizopangiliwa vema katika kabati ni rahisi sana kuziona na kuchagua ile
unayoitaka kuliko nguo ambazo zimemwagwa tu katika kona ya nguo ndivyo ilivyo
kwa jumbe zisizopangiliwa
Katika
kupangilia unaweza kupangilia kwa kutumia herufi kubwa au ndogo na pia unaweza
kutumia namba za kirumi, upangiliaji wa masomo unasaidia ujumbe kuweza
kueleweka kulingana na mpangilio wake na mfuatano wa mawazo na ujenzi wa hoja
unakuwa ni wenye mvuto kuliko ujumbe ambao hauja pangiliwa katika somo hili
inashauriwa angalau ujumbe uonyeshe maeneo kama matano hivi kwa mfano huu
utakaoonyeshwa chini mara baada ya maelezo kuhusu mpangilio wa ujumbe
Umuhimu wa kichwa cha ujumbe.
Kila aina ya
ujumbe unaohubiriwa ni lazima uwe na kichwa, kazi kubwa ya kichwa cha ujumbe ni
kumtaarifu msikilizaji kuwa ujumbe wako unahusu nini? Kichwa cha ujumbe ni kama
kibao kinachotoa maelekezo kuwa tunakwenda wapi, lazima kichwa cha ujumbe kiwe
na mvuto na kiwe kifupi na kiwe kinajenga mazingira ya watu kutaka kusikiliza kuwa
ndani ya ujumbe kuna nini, kwa ufupi kichwa kinatakiwa kuwa ni mukhtasari wa
kile ambacho muhubiri anakwenda kukihubiri na kinatakiwa kuwa katika hali
nyepesi na iliyowazi hata ikitokea kuwa Muhubiri anakufa ghafla wasikilizaji
watajua kuwa marehemu alitaka kuzungumzia nini, wako wahubiri wanaweka kichwa
chenye utata sana au kutokuwa na kichwa cha ujumbe kabisa kiasi cha watu
kushindwa kuelewa nini kinazungumzwa na wapi wanaenda
Utangulizi
Lengo kubwa la
utangulizi ni kupata usikivu wa watu ni kama vile mchungaji amekwenda madhabahuni
na mfuko na ndani ya mfuko huo kuna sauti za wanyama mbalimbali kila mtu atakodoa
macho ili kutaka kujua ni nini kimo
ndani yake hii ni kama kusudi la
utangulizi, lakini sio tu kupata usikivu lakini pia kupata hamu na shauku ya
kutaka au kupenda kile kinachofuata, utangulizi unatakiwa kurudisha akili zao
katika somo na kuwaondoa watu katika
hali ya kulipinga neno na kukubali mabadiliko kumbuka kuwa tunahubiri ili
kubadilisha maisha ya watu katika maeneo kadhaa mfano
·
Tunawahubiri wenye dhambi ili waokolewe na
kumuamini Kristo
·
Tuanawahubiri wakristo ili wawe kama Kristo
·
Tunahubiri ili kubadili mitazamo na tabia mbaya
na mafundisho mabaya
·
Tunahubiri kuondoa watu kutoka katika
migandamizo, hali za kutokusamehe, kukata tamaa na kuondoka katika hali za
uchungu.
Kwa msingi huo
utangulizi unaweza kuanza kwa kichekesho, kuuliza swali, kufanya igizo Fulani au
kuimba, shuhuda au mfano ili kuwafanya watu wafungue mioyo yao na kupokea
ujumbe.
Tatizo linaloshughulikiwa
Ujumbe wa
kibiblia unapaswa kujengwa katika misingi ya kuondoa tatizo kulingana na
uhitaji wa watu ulioko au kulingana na mawazo ya watu lazima uwe hodari katika
kupangilia kwako jumbe ni lazima uwe makini katika kuyachota mawazo ya watu
wafanye watu kuwa na kiu ili wanywe maji wenyewe, huwezi kumlazimisha ngombe
kunywa maji hata kama unaweza kumpeleka mtoni, lazima ujue kuwa watu wanahitaji
nini kisha utoekitu ambacho watu wale
wanakihitaji, kwa mfano kama watu wanaogopa basi hofu inasababisha watu kuweka
hela benk, kuweka walinzi kutembea wakiwa na hofu na kadhalika kwa hiyo
unaonyesha tatizo la hofu katika jamii kisha kipengele cha suluhisho unatatua
tatizo.
Picha
zifuatazo zitakusaidia kuona umuhimu wa kufanya kile ambacho watu wanakitarajia
na usilazimishe yale unayotaka wewe yawe.Wafanye watu kutamani mahubiri yako na
kuwa na hamu na shauku ya kuyasikiliza kila siku kama wafanyavyo watu
wanaoandaa vipindi vya tamthilia huandaa katika namana ambayo wateja wao
hutamani kipindi kifike ili wakiangalie wahubiri nao wanapaswa kuwa werevu
kuliko watu wa michezo ya kuigiza watu watamani wenyewe neno la Mungu na
kuhudhuria mahubiri yako bila kuwalazimisha
Suluhisho.
Katika kutoa
suluhu Muhubiri anatoa suluhu ya matatizo husika kwa kuonyesha ni namna gani
watu wanaweza kupata suluhu na ni njia gani wanaweza kuzitumia au vitendo gani
wanapaswa kufanya, kwahiyo kama wana hofu unaweza kuwaelekeza kuiondoa kupitia
maombi au kuwa na mawazo sahii na kutokuogopa ua kumshukuru Mungu na kadhalika
na unaweza kutoa mifano
Matokeo
Hapa muhubiri anaonyesha matokeo ya ujumbe
wake endapo utafanyiwa kazi kwa mfano kwa swala la hofu Unaweza kuonyesha jinsi
ambavyo utakuwa huru kutoka katika hofu na hautaogopa tena na kuwa utatembea kifua mbele
Mwaliko
Muhubiri
anachokifanya hapa ni kuwafanya wasikilizaji wake kukutana na Mungu kivitendo
na kuwaombea ili wapokee neema ya kutoka katika tatizo walilo nalo Hapa
muhubiri anaweza kuomba na wale wenye hofu ya kupita kawaida na kuwafungua kwa maombezi ili waweze kuwa
huru kutoka katika hofu.
Mpangilio wa
ujumbe sasa unaweza kuonekana katika mtazamo huu
Kichwa cha ujumbe.
Hatua ya kwanza. I. Utangulizi
Hatua ya pili. II. Tatizo unaloshughulikia
A. Kweli kuu
1.
Mfano kuhusu kweli kuu
2.
Mfano kuhusu kweli kuu
B. Kweli kuu ya pili
1.
Mfano kuhusu kweli kuu ya pili
2.
Mfano kuhusu kweli kuu ya pili
Hatua ya Tatu. III. Suluhisho la tatizo
A. Kweli kuu ya kwanza
1.
Mfano wa kweli kuu
2.
Mfano wa kweli kuu
B. Kweli kuu ua Pili
1.
Mfano kuhusu kweli kuu ya pili
2.
Mfano kuhusu kweli kuu ya pili
Hatua ya nne. IV. Matokeo
Hatua ya tano. V.
Mwaliko wa madhabahuni au kuomba na kuhitimisha .
KITU
CHA ZIADA KWA HUTUBA ZA KIBIBLIA (UPAKO)
Hotuba za watu wa Mungu ni
tofauti na hutuba za wana siasa wa kawaida ni muhimu kufahamu kuwa kama
muhubiri wa maneno ya Mungu atakosa upako mahubiri yake hayatakuwa tofauti na yale
ya wana siasa, unapokosa upako unakuwa sawa tu na Samsoni asiyekuwa na nguvu
kwa msingi huo ili hotuba zetu ziweze kuwa na kitu cha ziada upako ni wa muhimu
nani lazima muhubiri autafute uso wa Mungu
na kuwa na mahubiri yenye nguvu na uweza wa kugusa na kubadilisha maisha
ya watu
Ufahamu kuhusu upako
-
Upako sio uweza wa kibinadamu 1koritho 2;1-1-5,4;19-20
-
Upako haumfanyi mtu kuepuka kazi ngumu Matendo
8;26-30
-
Upako sio mbadala wa kutokwenda chuo cha Biblia
kuwa na upako hakumaanishi kuwa wahubiri hawapaswi kuhudhuria katika mafunzo ya
chuo cha Biblia 2Timotheo 2;2,Matendo 19;9-10 Badala yake upako wa Roho Mtakatifu
unatupeleka kwenda chuo cha Biblia
-
Upako sio badala ya mwalimu 1Yohana 2;27, waefeso 4;11
-
Upako sio mwaliko wa kujitegemea, Paulo
alipoitwa bado Roho wa Mungu alimuongoza kujitia chini ya viongozi
waliomtangulia na kupata maelekezo ili kwamba kazi yake na maono yake yasiwe
Bure Wagalatia 2;1-2 Kazi ya Mungu haiwezi kukamilika bila kushirikiana
Chanzo kikubwa cha imani ya “Jesus Only” ni muhubiri Willium Branham
ambaye alikuwa na upako wa kupita kawaida
akitumiwa kwa nguvu na ishara na miujiza
katika kazi ya uinjilisti lakini kwa bahati mbaya hakuwa na ushirika na
mwili wa Kristo yeye aliamini kuwa yeye
ndiye kiongozi pekee mwenye mamlaka ya
mwisho aliyeangaziwa kweli na hivyo alikataa
wazo au fundisho kuhusu utatu wa Mungu
ambao kanisa limeamini kwa karibu na zaidi miaka 2000 na akasema
anayepingana naye amekosa na matokeo
yake ilienea imani hii potofu ya Jesus Only warumi 12;3 kamwe upako haukufanyi
wewe kuwa Bora kuliko wengine
-
Upako ni Neema ya Mungu inayompa mtu nguvu za
kutumika kwa msaada wa Roho wa Mungu
-
Upako ni uweza wa Mungu katika maisha ya huduma
na katika kuifanya kazi yake
-
Upako unatofautiana kwa viwango kati ya muhubiri
na muhubiri kwa utii,1Koritho 12;4-11
-
Kuwa na upako sio alama ya kukomaa kiroho bali
matunda ya roho Wagalatia 5;24
-
Upako ni lazima uendane na mwenendo au tabia
njema sawa na viwango vya kibiblia
Upako na ujumbe
Ili jumbe zetu ziweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa ni lazima ziwe na
upako, upako huongezeka kwa kadiri ya namna na jinsi tunavyojitoa kwa Mungu
·
Osward Chambers alijitoa kuutafuta uso wa Mungu
na kuomba na kusoma neno la Mungu na alituma wamishionari 400 Duniani
·
John Wesley alikuwa akiomba masaa mawili kila
siku asubuhi alitumiwa kuleta uamsho mkubwa sana uingereza
·
Martin Luther aliomba masaa mnne kila siku
asubuhi na kusoma neno
·
Muhubiri David Yongg Cho hakutani na watu kwanza
mpaka akutane na Mungu kwa saa tatu
Muhubiri anashauriwa kuwa na tabia ya kukaa miguuni
kwa Mungu na kujifunza kumuabudu yeye
kwa kadiri ya neema unayopewa na hapo
utajifuza kumfahamu Yesu vema Luka 10;40-42, ni vema kutegemea upako zaidi
kuliko kupeleka jumbe zetu zikiwa kavu
Yohana 16;37,Matendo 2;37,24;25, muhubiri mshuhuri katika historia za kanisa
Charles Finney 1825 alikuwa ni mtu mwenye upako wa kupita kawaida aliitwa na
shemeji yake katika kiwanda cha pamba na
alipoingia alikutana na binti mmoja aliyekuwa akidhihaki mara nyingi na
kuzungumza mabaya juu yake
alipomuangalia binti alianza kulia na mara kila mtu alianza kulia na kiwanda kizima kila aliyemwangalia alikuwa
akilia na hatimaye waliomba na kuokolewa Upako ni zaidi ya uwezo wa kibinadamu
Zekaria 4;6 unaleta matokeo yaliyokusudiwa.
UMUHIMU
WA KUTUMIA MIFANO WAKATI WA KUHUBIRI
Mifano inaleta mwanga kwa watu
kuweza kuelewa ujumbe wako vema kwa wepesi na kwa ubora zaidi kwa msingi huo
inahsuriwa kuwa wahubiri watumie mifano katika jumbe zao, mifano ni njia ya
Mungu ya kuwasiliana na mwanadamu, Mungu ndiye mwandishi wa biblia kupitia Roho
wake na katika biblia kuna mamia ya
mifano ambayo Mungu aliitumia ili kuwafundisha
watu wake kitu kama alivyo mtuma nabii Hosea ili kuwasilisha ujumbe wake kwa
Israel na tabia yao ya kuabudu miungu kwa msingi huo tunaona kuna umuhimu kwa
wahubiri kuwa na ujuzi wa matumizi ya mifano katika mahubiri yao
Yesu Kristo alitumia mifano,
inasemekana kuwa asilimia 52 ya injili ya luka ina mifano angeweza kuwasiliana
apendavyo lakini alitumia mifano kwa sababu ina faida nyingi sana kama
nitakavyoziorodhesha hapo chini, kila mara alizungumza kweli Fulani na kisha
alitoa mifano, mfano katika Luka 12;13, 15, 22-33, kuhusu toba Luka 13;1-10,
gharama za kumfuata 14;27, 28-30, 31-33, mwana mpotevu Luka 15, shilingi
iliyopotea na kondoo.Mifano mingine aliyoitumia Yesu ni pamoja na mbwa mwitu,
Mbweha, Ngamia, tai, njiwa, shomoro yaani mbayuwayu, jua , mwezi, Anga, dunia,
mkulima, milima , bahari, upepo, udongo, mbegu, miti, miamba , samaki,
yai, mikate, divai, mvua , radi na mifano
mingine mingi yoote aliitumia katika kuwasilisha kweli Fulani za kiroho.
Mifano inaweza kuwa
Hadithi
Miujiza
Uponyaji
Mgongano wa mawazo
Kuoanisha nyimbo
Mashairi mfano Matendo 17;28
Vitendawili
Mifano
Matukio mfano Luka 13;14
Kufananisha
Maigizo
Grafu au takwimu
Matumizi ya picha
Kwa nini ni muhimu kutumia
mifano?
-
Inaweka wazi
-
Inavutia
-
Inavuvia
-
Inarahisisha
-
Inasisimua
-
Ianakazia kweli
-
Inarudia kweli kwa undani zaidi
-
Inasababisha watu kukumbuka
-
Inagusa mioyo
-
Inashawishi watu kusikiliza
-
Inaburudisha
-
Inasisimua
-
Inasimama kama daraja
-
Ina shughulika na tatizo moja kwa moja
Ujumbe usio na mifano unafananishwa na barabara ambayo imenyooka moja
kwa moja na haina hata kona hata hivyo wahubiri wengi sana hawana mifano ya
kutosha na hivyo hukosa mifano kwa madai kuwa aidha muda ni mfupi au wanaona
mifano ni kama jambo la kitoto, ai wengine huiona ni vigumu kueleza au haipatikani
kwa urahisi, lakini inashauriwa kuwa na kitabu au faili la kutunzia mifano na
unaweza kuiandaa katika mtindo wa herufi A-Z utaitunza kila unapoisikia
Muhubiri mmoja alitumia mfano wa kijana na mbwa aliyekufa, kufundishwa
habari ya msamaha, kijana alimpenda sana mbwa wake na siku aliyofariki mbwa
huyo kijana alimuomba baba yake mbwa huyo azikwe lakini mkia uachwe nje, kila
mara kijana alipomkumbuka mbwa wake alikwenda na kuuvuta mkia mwisho ikawa kila
wakati kuna harufu mbaya baba yake alimshauri kijana Yule kufukia kabisa, nasi
katika kusamehe hatupaswi kukumbushiana machungu yaliyopita msamaha lazima
uendane na swala la kuachilia kila kitu kabisa, Kumbe mifano inasaidia somo
kuwa wazi na kueleweka vema itumie kila iwezekanavyo.
Kanuni za kutumia mifano.
·
Hakikisha kuwa unakuwa mkweli unapotumia mifano
·
Usitumie mfano wa mtu mwingine kana kwamba tukio
hilo limekutokea wewe
·
Usieleze katika mifano vitu visivyoweza
kuaminika, asipunguze waka kuongeza chumvi
·
Uwe mwangalifu usitoe siri ya mtu wala usitoe mifano inayoendana na tukio
halisi lililofanyika kanisani, wala usitaje jina la mtu katika mifano tata
·
Jiandae usitumie mifano kama njia ya kupotezea
muda wala usitumie muda mrefu kwa mifano
·
Usianze mfano kwa kusema huu ni mfano
·
Kuwa mbunifu kuhusu mifano, toa mifano ya
kimatukio
·
Hakikisha kuwa ndani ya mifano kuna somo moja
kuu linalosisitizwa.
SURA YA TATU: MUHUBIRI NA
JAMII YAKE
Ujuzi kuhusu mawasiliano yasiyo
na sauti
Kama itakuwa umewahi kumsikiliza muhubiri ambaye amesimama tu katika
mahubiri yake bila kutikisa hata mkono bila shaka utakuwa hukuridhishwa na aina
ya muhubiri wa jinsi hii na inakuwa vigumu pia kumsikia anasema nini? Mwenendo
wa mwili una sehemu kubwa sana wakati wa kuhubiri unachangia kwa kiasi kikubwa kuleta usikivu kwa jamii yako mwenendo huo wa
mwili wako ndio unaitwa mawasiliano yasiyo na sauti Nonverbal communication
mawasiliano yasiyo na sauti huwakilishwa
na maeneo makubwa manne
·
Muonekano wa uso wako
·
Matumizi ya mikono
·
Macho yako kama unawatazama watu au vinginevyo
·
Na muonekano wa hali ya hisia zako za ndani kwa
nje
Muonekano wa uso wako
Muonekano wa uso wako unaweza
kuonyesha dhahiri nini kinaendelea sawa
kabisa na jinsi unavyoweza kuzungumza wanasaikolojia wanaamini kuwa karibu nusu
ya au zaidi ya athari za ujumbe wa
mtu kwa jamii yake unapokelewa kutoka
usoni, uso ndio unaofunua ushawishi wa Mnenaji na kusaidia kukubalika kwa wazo
lake hata kama mtu ameficha hisia zake ni rahisi kuziona hisia hizo usoni
Furaha na huzuni, Maumivu au uchungu, kushangaza au kuvutia, kuona
huruma na kuguswa, upendo au chuki, kupenda au kutokupenda haya yote huweza kusomeka
kupitia mawasiliano haya.
Matumizi ya mikono
Hapa tiunazungumzia sio tu swala la matumizi ya mikono bali pia mabega,
kichwa na mwili mzima kwa ujumla vyote vinatakiwa kuonyesha kuwa uko katika
kuwasiliana, wakati mwingine mwenendo wa mwili una tusaidia kusema hata kabla
ya maneno na hivyo kukamilisha swala la mawasiliano.
Macho yako kama unawatazama
watu au vinginevyo
Kama ilivyo kwa alama nyingine za mwili macho nayo ni ya muhimu sana
katika mawasiliano unapaswa kuwaangalia wasikilizaji wako kwa sababu unapaswa
pia kujua kinachoendelea na pia kitendo cha kuwaangalia moja kwa moja
kinamaanisha kuwa mzungumzaji anazungumza na jamii yake jambo hili linasaidia
katika maswala ya mawasiliano.
Maswala mengine yanayosaidia katika mawasiliano ni pamoja na
vijichekesho au hata kuwa karibu na wasikilizaji wako
MAWASILIANO KATIKA MTINDO WA
SAUTI
Sauti ni kama muziki inaweza kuwa laini au kubwa
wakati wa kuwasiliana ni lazima uhakikishe kuwa unaitumia sauti yako
vema swala la utoaji wa sauti ni swala
gumu sana kwa sababu utoaji wa sauti
unategemeana na utendaji wa kazi wa
viungo vingi sana , ili sauti iweze kutoka kuna viungo vinavyohusika katika
utoaji wa sauti, Pua, taya, ulimi, meno, bomba la hewa, koo, mapafu na
dayaframu
Sauti iliyo nzuri inaanza na upumuaji ulio mzuri pia kwa msingi huo muhubiri unaweza kuwa na
mazoezi ya kusaidia upumuaji wako ili wakati mwingine sauti iweze kutoka vizuri
nunaweza kulala sakafuni na kuwekla kitu kizoto kati ya mapafu na tumbo kasha
ukaanza kupumua taratibu na kuanza kutoa sauti za matamshi kama ha kasha ho , pia unaweza kuchukua mazoezi kwaajili ya
kuitoa sauti yako ili iweze kusikika
vuta pumzi ndani sana mkisha anza
kuiacxhia polepole na kutamka maneno yanayotakiwa kutamka kama ya kimaandiko
jitahidi usitumia pua katika kuzungumza wala usiikoromeshe sauti yako
MASWALA YA USIKIVU
Kwa kawaida Muhubiri anapaswa kusikilizana na jamii yake wao wakusikie
na wewe uwasikie hili linakuja hasa pale mzungumzaji atakapokuwa akijihusisha
na maswala ya mijadala kama wasikilizaji hawakupati vizuri mara nyingi
kunauwezekano wa wana jamii kutoa aina Fulani ya sauti hivyo hapo muhubiri
unapaswa kuwa makini.
Wakati wa kusikiliza unapaswa
kuzingatia
·
Uchaguzi – yaa ni kua na hali ya kuamua wapi
usikilize kwani kuna sauti nyingi lakini wapi tunatoa usikivu ndipo panapoweza
kutufanya tusikie
·
Kusudia - Mfano mtu anakuliza umesikia lazima
ujiulize kusikia nini? Kila ambacho unakiulizia umesikia nini ndicho kilae
ambacho mtu anakuwa amekikusudia kwa
hiyo katika kusikiliza uwe unakusudi
·
Uwe na ustadi
o
Lazimna uweze kutafuta wazo kuu katika kusikia
kwako
o
Lazima ukumbuke uchambuzi wa ndani sana wa kile kilichozungumzwa
o
Lazima ujue kwanini hoja au mada au
kinachozungumzwa kinawakilishwa kwa njia hiyo
o
Lazima ujue maana ya maneno ambayo mzungumzaji
anayatumia
o
Ujue kuhusianisha wazo la mneneji na kile
anachokiwasilisha
o
Lazima uchambue au kufanya hukumu kuhusu mawazo
ya mneneji
o
Lazima ujue kusudi kuu la mzungumzaji na kile
anachokitarajia
·
Uwe makini
Hakuna mtu anayesikiliza wakati wote kile
kinachozungumzwa na mneneji kukosa umakini ndio moja ya maadui wa kubwa wa kujifunza
inasemekana mara nyingi ni nusu tu ya watu wanaweza kuelewa mnenaji
anazunghumza nini na wengine wanapata juu juu tu na watoto wanakuwa kama viziwi
kabisa hata ingawaje wanasikia unaweza kujifanyia utafiti kwa kuweka kaseti na
kuwaomba watu wasikilize kasha waulize wameelewa nini? Kunahitajika umakini
katika kusikiliza
MIJADALA
Mahubiri yanaweza kuwasilishwa pia kwa
njia ya mijadala hususani wakati wa kuweko studio kwa njia ya redio au
television na hata kanisani pia njia hii inaweza kutumika kuna aina nyingi za
mijadala
Mijadala yenye kuhusisha watu
wengi Panel
Hawa wanaweza kukaa katika
mzunguko wa kuweza kutazamana au kuitazama jamii kwanmi jamii inahitaji kuona
nyuso zenu lugha itakayotumika ni ya kuelimisha na yenye kuzingatia kuwa hapa
mmnajadili sio mahubiri
Mijadala inayohusisha
kuwasilisha kitu katika kikao symposium
Mijadala hii kila mmoja anakuwa
ameandaliwa kuwasilisha jambo
Fulani na kila mmoja atakuwa amepewa
muda maalumu wa kuwasilisha mada kama ni somo litakuwa limegawanywa katika
vipengele kadhaa na kila mmnenaji anakuwa na kipengele chake cha kuwasilisha
Makusudi ya mjadala
o
Kubadilishana mawazo
o
Kuchukua uamuzi
o
Kutafuta
suluhu
o
Kutoa elimu
Mijadala ni lazima iandaliwe
vizuri, kila mmoja anapaswa kuonyesha ushirikiano na kunapaswa kuwako mwenye
kiti wa mijadala anayejua kuendesha vizuri majadiliano hii inafanyika hivi kwa
sababu makanisa yanabarikiwa na ni rahisi leo kuwa na vyombo vya habari kama tv
na radio na kadhalika
SURA YA NNE: MUHUBIRI NA
MASWALA YA VYOMBO VYA HABARI NA TAMADUNI TOFAUTI
Ujuzi kuhusu namna ya
kuwasiliana katika Redio na Television
1. Haya ni mawasiliano kwa njia ya vyombo vya
habari “Media communication” Mahubiri kwa njia ya Redio na televisheni au
mahubiri yaliyochapiswa huingia katika eneo la mawasiliano kwa njia ya habari
mtindo huu wa mawasilianoi unaweza kuvuka tamaduni tofauti na kufika mbali
A. Vyanzo na Mchakato
1. Mchakato – tendo
la redio au televisheni kupekleka ujumbe linaweza kuwa
i.
Tendo la mtu Fulani pakee
ii.
Tendo la matumizi ya mtandao
Mtandao wa kituo husika unakusudia au
unaungana na vituop vingine kutuma ujumbe kwa wakati muafaka na kwa msingi huo
watenda kazi wa Kikristo wanapata nafasi ya kluwahubiri maelfu kupitia vyombo
vya habari
Vyanzo – Kuna vyanzo vingi sana vya kueneza
habari na program za vyombo vya habari kama televisheni na redio kama
unakusudia kuwa na matumizi ya vyombo hivi vya habari unaweza pia kuwa na
vyanzo kama
Wahubiri mbalimbali wanaorusha vipindi
Waigizaji wanaoweza kufurahisha watu ili
kuwavutia
Watenda kazi wa kiristo wanaoshughulikia
maswala ya kurusha vipindi n.k.
Unapozungumza
katika Redio au Televisheni
Hakikisha umeandaa ujumbe wako vilivyo kwa
makusudi ya kukutana na mahitaji ya jumla ya wasikilizaji wako
Watu wana matatizo mengi na hivyo vipindi vyako
view na uwezo wa kugusa mahitaji ya watu husika
Radio yako au televishenio yako inatakiwa iwe na
mvuto wa kuwafanya wasikilizaji kupenda kusikiliza au kutazama
Kumbuka kama hawatafurahia wanachokisikia
watazima au kubadilisha chaneli
Maswala ya Fedha kwaajili ya vyombo vya
habari
·
Uhakikishaji wa kupata fedha kwaajili ya vyombo
vya habari kama Redio na Televisheni hufanyika katika namna nyingingi sana
o
Kwa kukusanya watu ambao watakuwa taryari
kugharimia urushwaji wa vipindi
o
Kwa kuwatangazia wale wote wanaopenda kudhamini
vipindi kwa makusudi ya kibiashara
o
Matangazo ya kibiashara na kadhalika
Program.
o
Hakikisha kuwa wanafaidika na kutangaza kwao
kupitia tv yako au redio yako endapo inaweza kufika mbali kwa masafa yake
o
Hakikisha kuwa vipindi vyako vinakuwa na ubora
mkubwa unaokusudiwa ili kuwavuta watu wengi sana kusikiliza ili wafanya
biashara waweze kuvutwa kutangaza katika redio yako
o
Uwe na program nzuri za muziki za kuvutia zenye
ujumbe mzuri ili kuvuta usikivu
o
Kumbuka kuwa wasikilizaji pia watakuwa
wakiongezeka kutokana na umahiri wa vipindi vyako.
Nguvu na Sheria
·
Redio na televisheni vina uwezo mkubwa sana wa
kutawala mawazo ya watu kila tuachokiona na kukisikia kinavuvia akili zetu na
upande mwingine wa kusikia na kuona ni
kunyonya kile tulichosikia na kuona na
kuyatumia
·
Maswala ya program za Kikristo katika vyombo vya
habari yanatakiwa kuwa ya kweli nay a kivitendo ili kuvutia akili za watu
·
Uwe makini na kila aina ya ujumbe au
kinachorushwa katika televisheni yako au redio
·
Jumbe na kila kinachorushwa kina nguvu sana ya
kuchochea wema ama uovu kwa jamii husika
·
Ili kulinda ni vema kuamua muda wa kitu gani
kinarushwa na saa ngapi nani anaweza kusikia na nani hawezi kusaikia kitu kibaya kinaweza kusababisha wasikilizaji
wako kuzima redio /televbisheni yako na kwenda kwengine
·
Televisheni na redio zina nguvu sana hata kwa
watu wasiojua kusoma au kuandika
·
Maswaloa ya kuzungumzia dini hayana maana sana
kwa jamii kwani watu wakati wote hutafuta majibu ya maswali ya matatizo yao na
sio vinginevyo.
Ujumbe wa Mawasiliano.
A. Mawasiliano
na wasikilizaji
i.
Ujumbe wa mawasiliano katika redio na
televisheni unaweza kuwa wenye kuonekana au usio wa kuonekana kwa watu wote
wawili yaani wasikilizaji na mtangazaji, unap[okuwa unatangazia kutoka studio watazamahji
au wasikilizaji wanaweza wakawa hawakuoni kwa maana ya Redio
ii.
Kama ni vipindi vinavyochukuliwa kanisani ni
rahisi kuwana wasikilizaji wako au wao wakakuona
iii.
Lazima uwe makini katika kuhakikisha kuwa unajua
namna ya kuiwasiliana na jamii hiyo ya watu hasa kama unatunmia redio wale
wasiokuona unaweza kufanya mawasiliano nao kama mtu uonaye na kuwa fanya
wwajisikie kama uko pamoja nao kwa upande wa televisheni yako mab ambayo
yanaweza kusaidia wasikilizaji kujiona kama wako na wewe moja kwa moja kuliko
redioni
Mambo mengine ya msingi ya kuzingatia.
Maandalizi mazuri ya vipindi ni muhimu
yakafanyika kabla ya kipindi kuruishwa
Hakikisha kuwa una wataalamu au mafundi wakio
hodari
Unapozungumza na watu moja kwa moja katika
televisheni itazame kamera ili watazamaji waone kuwa sasa unazungumza nao
Uwe na kamera nzuri na vipaza sauti vilivyo na
ubora kama una rekodi hakikisha kuwa unatumia vyombo safi.
Kwa habari ya Lugha
Tumia lugha nyepesi tu
Pangilia hotuba yako kwa mawazo yanayokubaliana
ijulikane unatoka wapi kwenda wapi
Hakikisha kuwa unatamka wazi meneno yako
Tumia lugha ambayo inatumika na wasikilizaji
wako na isiyo ya matusi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni