Yoshua 22: 9-10.
“Basi
wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wakarudi,
wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende
nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na
amri ya Bwana kwa mkono wa Musa. Nao walipofika pande za Yordani, zilizo katika
nchi ya Kanaani, hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na nusu ya kabila ya
Manase, wakajenga madhabahu huko karibu na Yordani, iliyoonekana kuwa ni
madhabahu kubwa.”
Utangulizi.
Mara baada ya kuingia katika nchi
ya kanaani wakati wa Yoshua Wana wa Israel yaani walioishi ng’ambo ya Yordan
ambao ni kabila la Wareuben, Gadi na Nusu ya Manase, walimjengea Bwana
Madhabahu kubwa sana ambayo ilileta utata na kutaka kusababisha vita ya wenyewe
kwa wenyewe, Mungu alipompa Musa sheria alieleza wazi kuwa watu wasijenge
madhabahu isipokuwa ile iliyoamriwa.
Kumbukumbu 12:1-14 “Hizi ndizo amri na hukumu mtakazotunza kuzifanya katika nchi
aliyokupa Bwana, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya
nchi. Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa
mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti
wenye majani mabichi; nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na
maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao
zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo. Wala msimfanyie hivyo
Bwana, Mungu wenu. Lakini mahali atakapochagua Bwana, Mungu wenu, katika kabila
zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo,
nawe wende huko; pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na
zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka
zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;
na huko mtakula mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote
mtakayotia mikono yenu, ninyi na wa nyumbani mwenu, aliyokubarikia Bwana, Mungu
wako. Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama
aonavyo vema machoni pake; kwani hamjafikilia bado katika raha na urithi akupao
Bwana, Mungu wako. Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi
anayowarithisha Bwana, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande
zote, mkakaa salama; wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua
Bwana, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu
ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na
sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa
Bwana. Nanyi mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na
binti zenu, na watumishi wenu wanawaume na wanawake, na Mlawi aliyemo malangoni
mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu. Ujihadhari usitoe sadaka zako za
kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; bali katika mahali atakapopachagua
Bwana katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa,
ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo.”
Kutokana na mtazamo huo wana wa
Israel walitambua kuwa ndugu zao wamekiuka agizo la Mungu, kwa kujenga
madhabahu iliyoleta utata na hivyo walipaswa kupigwa na kufutiliwa mbali , wazo
la kuwapiga na kuwafutilia mbali lilikuwa
sawa na agizo la Torati.
Kumbukumbu 13:12-16 “Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo
Bwana, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa, Kumetoka katikati yako mabaradhuli
kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu
miungu mingine msiyoijua; ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii;
nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano
wa haya yafanyika katikati yako; hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa
makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na
wanyama walio humo, kwa makali ya upanga. Na nyara zake zote uzikusanyie
katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe
sadaka kamili ya kuteketezwa kwa Bwana, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele;
usijengwe tena.”
Israel na uongozi wa Magharibi
ulikuwa umezingatia maagizo haya ya Mungu, wao walikuwa wametafasiri kuwa ndugu
zao wamekusudia kuabudu miungu mingine na kuwa wamekiuka agizo la Mungu kupitia
torati ya Musa, lakini jambo lililokuwa jema zaidi ni kwamba walitaka kufanya
uchunguzi ili kujiridhisha kabla ya kuingia vitani, Kabila la Warubeni na Gadi
na Manase, walifafanua matumizi ya madhabahu hiyo kuwa ulikuwa ni ukumbusho kwa
Bwana Mungu wao, wao walikuwa wametenganishwa na mto kijiografia , Lakini
walitaka kuonyesha muungano wao wa kiroho, Madhabahu yao ilikuwa ni Ishara ya
umoja na sio uasi, wao walikuwa na nia ya kutunza maisha ya kiroho ya watoto
wao Yoshua 22:12-29 “Basi, wana wa Israeli waliposikia
habari hiyo, mkutano wote wa wana wa Israeli wakakutanika pamoja huko Shilo,
ili waende kupigana nao. Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana
wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, hata nchi ya
Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani; na pamoja naye wakuu
kumi, mkuu mmoja wa nyumba ya mababa kwa ajili ya kila kabila ya Israeli; nao
kila mmoja alikuwa ni kichwa cha nyumba ya mababa katika maelfu ya
Israeli. Nao wakawafikilia hao wana wa
Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, katika nchi ya
Gileadi, na wakasema nao, wakinena, Mkutano wote wa Bwana wanena, Ni kosa gani
hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha
kumwandama Bwana, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya Bwana?
Je! Ule uovu wa Peori haututoshi, ambao hamjajitakasa nafsi zenu katika huo
hata hivi leo, ijapokuwa ilikuja tauni juu ya mkutano wa Bwana, hata ikawa
hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumwandama Bwana? Kisha itakuwa, kwa kuwa
ninyi mwamwasi Bwana hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa
Israeli. Basi kwamba hiyo nchi ya milki yenu si tohara, ndipo ninyi vukeni na
kuingia nchi ya milki yake Bwana, ambayo maskani ya Bwana inakaa ndani yake,
nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi Bwana, wala msituasi sisi, kwa
kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wetu. Je! Huyo
Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira
ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake
katika uovu wake? Ndipo hapo wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya
kabila ya Manase, wakajibu, na kuwaambia hao waliokuwa ni vichwa vya maelfu ya
Israeli, wakasema, Mungu, Mungu Bwana,
naam, Mungu, Mungu Bwana, yeye yuajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika
uasi, au kama ni katika kosa juu ya Bwana, (usituokoe hivi leo); sisi
kujijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumwandama Bwana; au kama ni
kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni
kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye Bwana mwenyewe na alitake jambo hili;
au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hadhari sana, tena makusudi, huku
tukisema, Katika siku zijazo wana wenu yamkini wakanena na wana wetu, na
kusema, Ninyi mna nini na Bwana, yeye Mungu wa Israeli? Kwa kuwa yeye Bwana
ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati ya sisi na ninyi, enyi wana wa
Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika Bwana; basi hivyo wana wenu
wangewakomesha wana wetu wasimche Bwana. Kwa ajili ya hayo tulisema, Na tufanye
tayari ili kujijengea madhabahu, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala
kwa sadaka yo yote; bali itakuwa ni ushahidi kati ya sisi na ninyi, tena kati
ya vizazi vyetu baada yetu, ili kwamba tufanye huo utumishi wa Bwana mbele yake
kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu
za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika zamani zijazo,
Ninyi hamna fungu katika Bwana. Kwa hiyo tulisema, Itakuwa, hapo
watakapotuambia neno kama hilo, au kuwaambia watu wa vizazi vyetu katika zamani
zijazo neno kama hilo, ndipo sisi tutawaambia, Angalieni huu mfano wa madhabahu
ya Bwana, walioufanya baba zetu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wala
kwa ajili ya dhabihu; lakini ni ushahidi kati ya sisi na ninyi. Mungu na
atuzuie msimwasi Bwana, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, hata
mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au
dhabihu, mbali na ile madhabahu ya Bwana, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya
maskani yake”.
Walipogundua hilo,Kuhani mkuu
Finehasi na makuhani na wazee waliwaambia Reuben na Gadi na Manase walipata amani Yoshua 22:30-34 “Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, maana, ni hao
waliokuwa vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo
walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na
wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhia sana. Naye Finehasi, mwana wa
Eleazari, kuhani, akawaambia wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa
Manase, akasema, Siku hii ya leo twajua ya kwamba Bwana yu kati yetu, kwa
sababu hamkukosa katika jambo hili mbele ya Bwana; sasa ninyi mmewaokoa wana wa
Israeli na mkono wa Bwana. Kisha Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, na hao
wakuu, wakarudi na kuwaacha wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakatoka katika
nchi ya Gileadi, na kuingia nchi ya Kanaani; wakawarudia wana wa Israeli, wakawapa
habari. Wana wa Israeli nao wakaliridhia jambo hilo; nao wana wa Israeli
wakamhimidi Mungu, wala hawakusema tena habari ya kuwaendea juu yao kupigana
nao, wala kuiharibu nchi waliyoikaa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi. Basi hao
wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakaiita madhabahu hiyo Edi; wakasema, Kwa
kuwa ni ushahidi kati yetu ya kwamba yeye Bwana ndiye Mungu”.
Mgogoro ulimalizika, tukio hili
linatufunza kuwa Hatupaswi kuhukumu kwa haraka na kufikia katika hatima ya
jambo kabla kwanza ya kusikiliza, Nikodemo alimtetea Yesu kwamba sheria yetu
haimuhukumu mtu kwanza kabla ya kumsikiliza na kuangalia kile anachokifanya
Yohana 7:51, “Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya
kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?” Mithali
18:13. “Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na
aibu kwake.”
Mara nyingi tumewahukumu watu
kutokana na mitazamo iliyoko ndani yetu tu na hatujawapa Muda wa kuwasikiliza,
hatuwezi kufikia suluhu ya jambo lolote kwa kudhani kuwa mawaazo yetu ni sahihi
tu wakati wote, ni lazima tuwasikilize na wengine
Wakati wote unapofanya mambo
makubwa na ya kushangaza, lazima watakuweko watu watakaotafasiri tofauti lolote
ulifanyalo, Hakikisha unaweka alama kubwa katika maisha yako, unaacha wasifu mkubwa
katika maisha yako, unapata maxi kubwa katika masomo yako, unafanya makubwa
katika kila eneo, ukijenga kanisa jenga kanisa kubwa, ukiombea watu fanya miujiza mikubwa, ukiomba mamombi toa maombi makubwa, ukitoa sadaka toa sadaka kubwa, ukiwa na uhusiano na mungu uwe na uhusiano mkubwa, fanya kila kitu kikubwa utashangaza watu hata watu wa Mungu watakushangaa.
Wana wa Reuben na Gadi na Manase walijenga
madhabahu kubwa, kila mtu ni lazima adhamirie kufanya mambo makubwa na mara zote
unapokusudia kutenda mambo makubwa watu watachanganyikiwa, watatoa maneno ya kipuuzi, bila kuchunguza
kuwa nini kinachofanyika
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni