Andiko:Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.”
Utangulizi.
Injili ya Yohana ni injili inayokazia kuhusu
kumuamini kumuamini Yesu, kusudi kubwa la mkuandikwa kwa injili hii ni ili watu
wapate kumuamini Yesu kuwa ni mwana wa Mungu Yohana
20:30 -31 Biblia inasema “Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya
wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili
mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe
na uzima kwa jina lake”
Katika andiko la msingi tunaona Yesu akiwatia
moyo wanafunzi wake kwamba wasifadhaike mioyoni mwaoa na kuwa wanapaswa
kumuamini yeye kama wanavyomuamini Mungu, kwa nini Yesu anasema swala hili kwa
sababu alikwisha kuwaambia wazi kuwa Yuda atamsaliti Yohana 13:21, Petro
atamkana mara tatu, Yohana 13:38, na
pia kuwa na pia Yeye anakaribia kuondoka tena kupitia mauti, kwa ujumla hii
ilikuwa hali ngumu kwa wanafunzi wa Bwana ambao walikuwa wameacha vyote ili
kumfuata Yesu, Jambo hili liliwakatisha tamaa.
Mara kwa mara katika maisha yetu tunaweza tukawa
na nyakati ngumu na za kukatisha tamaa katika maisha, tunaweza kukutana na hali
zilizo ngumu na hata tukayaona maisha yetu kuwa giza mbele, tunaweza kujawa na
hofu, kwamba mambo yatakuwaje Biblia inatoa jibu kuwa tumamini Yesu, Yesu
anasema mnamwamini Mungu, niaminini na mimi, hii maana yake ni kuwa kumuamini
Mungu ni sawa kabisa na kumuamini Yesu, Yesu ni Mungu na hivyo tunapaswa
kumwamini na kumtegemea yeye, naye atatutokea na kutupa uzima
Mfano.
Kulikuwa na mkwea milima mmoja maarufu sana
ambaye alikuwa na tabia ya kupanda milima mirefu duniani, siku moja mpanda
milima huyu alichelewa kushuka mlimani, hivyo giza kuu lilimkuta akiwa juu,
hakukuwa na mbara mwezi wala nyota na ilikuwa ngumu sana kuweza kuona
anakokwenda kwa vile kulikuwa na wingu zito na giza nene
Mpanda milima huyu alijaribu kushuka kutokakatika
mlima lakini kwa bahati mbaya aliteleza na akaanza kuanguka akiwa hewani kwa
kasi ya ajabu, alikuwa akiona vitu vyeusi tu alipokuwa anakwenda chini kwa
kasi, ilikuwa hali ya kutisha sana akajua kuwa ni kaburi tu ndilo linalomsubiri
Aliendelea kuanguka kuelekea chini akiwa na hofu
kubwa sana akawaza kuwa sasa anakaribia kufa ghafla alisikia kamba ikiwa
imekamata kiuno chake kwa nguvu sana na mara mwili wake ulianza kuning’inia
alihisi kuwa kama imekamata bara bara kiuno chake na ikimshika kwa nguvu lakini
alikuwa bado yuko hewani ananinginia, naye aliishikilia kwa nguvu zake zote,
lakini alikumbuka kuliitia jina la Yesu na kuomba ee bwana Yesu nakuomba
uniokoe na mauti hii
Mara moja alisikia sauti ikimwambia kutoka
mbinguni Je unataka nikufanyie nini? Alisema uniokoe ee Mungu wangu, Yesu
alimwambia unaamini kuwa naweza kukuokoa? Akasema ndio bwana nakuamini Yesu
akamwambie kata kamba yako iliyokushika kiunoni uende zako
Baada ya sauti hiyo kulikuwa kimya kwa muda, na
muda ukazidi kwenda mpanda milima yule aliendelea kushikilia kamba yake huku
akinin’ginia na hakukubali kuiachia kamba aliishikilia kwa nguvu zake zote
Asubuhi waokoaji walimkuta mpanda milima akiwa
amekufa huku akiwa ameshikilia kamba yake kwa nguvu kubwa sana watu
walisikitika sana na kulia kwani ilikuwa ni futi moja tu kutoka ardhini
Wengi tumefungwa na vitu vidogo tu vinavyotuzuia
kumuamini Mungu, ni lazima tuachie kama hiyo na kumtegemea Mungu mwokozi wetu,
kamwe tusimuachie Mungu
Sijui unapitia hali gani katika maisha yako
lakini najua jambo moja tu kuwa Mungu ataweka kila kitu sawa katika maisha yako
kwa wakati mkamilifu, wakati mwingine unaweza kuchanganyikiwa na wakati
mwingine unaweza kukosa faraja, lakini Mungu anabaki kuwa mwaminifu katika
kututendea mema, kumbuka maneno ya bwana Yesu Usifadhaike, Unamwamini mungu
muamini nay eye, usiogope, wakati wote nenola Mungu linatutaka tumwamini Mungu
2Nyakati
20:20 “Wakaamka
asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa
wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa
Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini
manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.”
Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni