Mithali 12:24 “Mkono
wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.”
Moja
ya kusudi kubwa la kuumbwa kwetu sisi kama wanadamu ni ili tuweze kufanya kazi,
hii ndio ulikuwa mpango mkuu wa Mungu kabla ya anguko la mwanadamu Mwanzo 2:15 “BWANA
Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.”
Agano jipya linakazia zaidi kuwa yeye asiyetaka kufanya kazi kula na asile 2Wathesalonike 3:10 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno
hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.” Unaona
biblia inatia moyo kufanya kazi kwa bidii, kufanya kazi kwa bidii ni ibada ya
kwanza kabisa ambayo Mungu alikuwa amewakusudia wanadamu waifanye, Biblia iko
kinyume sana na uvivu.Zaburi 128:2 “Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa
heri, na kwako kwema” unaonyesha kuwa Baraka za Mungu zinakaa katika kazi za
mikono yetu.
Ujumbe.
Kulikuwa
na mzee mmoja ambaye alikuwa na watoto wane wa kiume, hata hivyo kwa bahati
mbaya watoto hao walikuwa wavivu.
Siku
moja mzee huyu alianza kuugua sana na siku zake za kufa zikakaribia, alikuwa na
hofu sana kuhusu maendeleo ya baadaye ya watoto wake kwani walikuwa wavivu na
waliamini kuwa wana bahati kwa sababu ya mali ya baba yao.
Hali
ya afya ya baba yao iliendelea kuwa mbaya siku hadi siku, na mwishoe mzee huyu
aliamua kuwaita watoto wake na kuzungumza nao kuhusu maendeleo yao, lakini
watoto wake hawakumsikiliza, Hatimaye mzee yule alipata wazo na akataka watoto
wake watambue umuhimu wa kufanya kazi, aliwaita na kuwaambia kuwa alikuwa na
box moja lenya mali za thamani kubwa sana la dhahabu na fedha na madini
mengineyo ambalo alikuwa amewahifadhia na alikuwa anataka wagawame sawasaw.
Vijana walifurahi
sana waliposikia kuwa baba yao ana mali nyingi kiasi kile kwaajili yao, Mzee
aliendelea kueleza kuwa Tatizo kubwa sikumbuki ni wapi nilipoweka box hilo la
thamani kwani alilizika kwenye ardhi yao shambani lakini amesahau kabisa
aliliweka upande gani.
Hata hivyo vijana
wavivu waliendelea kufurahia habari hiyo, ingawa walihuzunika tu kuwa mzee wao
amesahau ni wapi alikoliweka, baada ya siku chache Mzee wao alifariki dunia,
baada ya maziko vijana waliamua kulitafuta boxi la thamani, walifanya kazi kwa
bidii wakichimba kila sehemu ya shamba lao, walichimba na kulima na kukata
misitu na kujaribu kuchimbua kila mahali wakitafuta mali, hawakutaka kukodisha
mtu kwani walijua wanaweza kuliona boxi na kuondoka nalo, hivyo walifanya
wenyewe lakini hawakufanikiwa kuona kitu.
Hatimaye waliamu
kuchimba shimo kila pembe ya shamba lao na kwa bahati shimo moja walilolichimba
lilitoa maji na chemichemi ikawa inabubujisha maji, Mtu mmoja alipita karibu na
shamba lao na kuwapongeza kwa kugundua maji aliwashauri kulimba mboga mboga na
kutumia maji hayo kumwagilia, vijana waliamua kulima mboga mboga na
kumwagilia na kuuza kwa watu mablimbali
na walianza kupata fedha nyingi sana na wakawa matajiri wakubwa.
Hawakuweza kuliona
boxi alilowaambia baba yao lakini hatimaye waligundua kuwa baba yao alikuwa
amemaanisha wafanye kazi kwa bidii na kwamba kufanya kazi kwa bidii kunalipa.
Walitambua kuwa kufanya kazi kwa bidii kuliwapa utajiri mkubwa.
Ndgu yangu Mungu anatutaka tufanye kazi kwa
bidii, Mungu anataka kila tunalotia mkono wetu kufanya tulifenye kwa bidii,
kusoma kwa bidii, kuomba kwa bidii, kazi, kwa bidii, kusali kwa bidii, kuabudu
kwa bidii.
Kama tutafanya kila kitu kwa bidii Biblia inasema
tutasimama mbele ya wafalme Mithali 22:29 “Je! Wamwona
mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama
mbele ya watu wasio na cheo.”
Na. Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni