Kumbukumbu 31:3-6
“Bwana Mungu
wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe
utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena. Na Bwana
atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na
nchi yao, ambao aliwaharibu. Naye Bwana
atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru.
Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana,
Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.”
Utangulizi.
Hivi karibuni sasa tunaelekea ukingoni au mwishoni
kabisa mwa mwaka 2017, kila mara unapofika wakati kama huu unakuwa ni wakati wa
wanafunzi kukabiliwa na mitihani yao ya mwisho, mitihani hii ni moja wapo ya
changamoto kwa wanafunzi wote, kwa kidato cha pilina cha nne watakuwa na
mitihani yao ya mwisho, hali kadhalika na mitihani ya kitaifa, na madarasa
mengine watakuwa na mitihani ya aina mbalimbali ya mwisho kwaajili ya kuwapima
ili wavukekuingia darasa lingine, katika wakati kama huu wanafunzi wengi hata
wale wenye uwezo huanza kuinhgia hofu kwa vile hawajui mtihani utaamua nini
katika maisha yao.
Wakati huu ni wakati wa muhimu sana kwao na kwetu
pia sisi walimu na shule kwa ujumla hivyo katika majira kama haya ni muhimu
kila mmoja akiutafuta uso wa Mungu na kujisomea kwa bidii sana lakini hali
kadhalika kuwa na neno la ushindi litakaloongoza maisha yetu wakati huu
unapokaribia.
Kumbukumbu 31:3-6 Mungu anataka kututia moyo
kupitia torati ya Musa kwa wana wa Israel, kuna maswala kadhaa ambayo Musa
alikuwa akiwaambia Israel kama siri ya ushindi wao
1.
Bwana Mungu wako ndiye atakayevuka
mbele yako,
Kuna uwezekano wa kuwa umesoma kwa bidii,
umekuwa na ratiba yako ya kujisomea na umetumia akili yako yote na hekima yako
yote kujiandaa ilivyo jambo hjilo ni jema lakini inawezekana pamoja na
maandalizi hayo ukawa unaogopa Biblia inatupa njia ya ushindi kwamba ni lazima
tumuombe Mungu aweze kwenda pamoja nasi na kututangulia Kutoka 33:14-15
“Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami
nitakupa raha. Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue
kutoka hapa.” Musa alimweleza Mungu kuwa hawezi kwenda bila uso wa
Mungu neno uso wa Mungu maana yake ni uwepo wa Mungu maana yake ni Kumpa Roho
wa Mungu nafasi ya kukuongoza katika masomo yako na maandalizi ya mitihani yako
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho
wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri
lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha
habari yake.”
2.
Iweni hodari na moyo wa ushujaa,
msiogope wala msiwahofu,
Neno la Mungu hapa linatutaka tusiogope
linatutaka tuendelee kuwa na imani na kuweka hofu mbali Israel waliahidiwa
inchi ya kanaani ambayo ndani yake ilikuwa ikikaliwa na majitu hodari, lakini
Israel walipaswa kutokuwaogopa na kuwakabili na kuwashinda, wanafunzi
mnaokabiliwa na mitihani, huu ni wakatoi muhimu sana kwenu, mitihani Inasimama
kama majitu inasimama kama tishio la kufanikiwa katika masomo yako, Lakini
unapaswa kuishinda na kufanikiwa kabisa kwaajili ya Maendeleo yako mbeleni
Joshua 1:5-9 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza
kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa,
ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. Uwe hodari
na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii
niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi,
uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu;
usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila
uendako.Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa
humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala
usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”
3.
Tamka Neno la Mungu.
Tamka neno la Mungu kwa kuliamini na kwa
ujasiri Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima,
mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima”
kumbuka kuwa hofu ni roho hivyo ili kuishinda unapaswa kuwa na ujasiri na hivyo
ni muhimu kwako kuliangalia neno na kulitamka hata ndani ya moyo wako kwa
ujasiri Matendo 4:29 “Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa
wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,”
4.
Uwe na Moyo wa Ushujaa (Imani).
Tendo lolote lile lisilotokana na imani ni dhambi,
Warumi 14:23 “Lakini aliye na shaka, kama akila,
amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo
lisilotoka katika imani ni dhambi” mara tunaporuhusu mashaka
katika maisha yetu ndipo ytunapoanza kuzama Mathayo 14:30-31 “Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga
yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika,
akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?” Ni muhimu kwetu tukimuamini Mungu kwa yasiyowezekana, Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.”
Kila mwanafunzi
anayetarajia kufanya Mitihani hivi karibuni tafadhali omba Maombi haya pamoja
na Mkuuwa wajenzi.
Mungu wa Rehema ni wewe utakayevuka mbele
yangu katika nyakati hizi za mitihani, ni wewe utakayetengeneza future yangu
kupitia ushindi wakati wa mitihani yangu nya mwisho na mitihani ya kitaifa
najiweka katika mikono yako nikikutegemea wewe, niweke mbali na hofu zote maana
wewe hukutupa roho ya woga, Nisaidie kwa Roho wako Mtakatifu na uwepo wako
ukawe pamoja name katika mitihani yangu sawasawa na Mapenzi yako Katika jina la
Yesu amen!
Nakutabiria ushindi, nakutabiria mafanikio makubwa katika mitihani yako, natabiri ufaulu wa kupita kawaida katika mitihani yako ya mwaka huu katika jina la Yesu amen!
Na
mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni