Mstari wa Msingi: Warumi 12:11 “kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika
roho zenu; mkimtumikia Bwana;”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa kila
tunalolifanya duniani Mungu anataka tulifanye kwa bidii, kufanya kazi ya Mungu kwa
bidii, kuabudu, kwa bidii, kuomba kwa bidii, kusoma kwa bidii, kufanya kazi za
kawaida, kwa bidii Mungu anataka tuwe na bidii, tuwe na Juhudi, katika kila
jambo, Haya ni mapenzi ya Mungu kabisa ni kanuni ya mafanikio. Kama mtu anataka
kufanikiwa katika kila jambo basi ni muhimu jambo analolifanya likafanyika kwa
bidii, Neno la Mungu linaunga mkono utendaji wa kazi kwa bidii na linaeleza
faida za kuwa na bidii katika kila jambo.
Kwa kuanzia na Mstari wa msingi
Warumi 12:11 SUV, Inasema kwa bidii, si walegevu, mkiwa na juhudi
Romans 12:11 NIV, Never be lacking in Zeal, but keep your spiritual
fervor
Romans 12:11 KJV, Not slothful in business; fervent in spirit;
Neno hilo Kwa bidii, kwa juhudi katika Biblia ya kiyunani linasomeka
kama AGONIZOMAI ambalo kwa
kiingereza kuna maneno kadhaa yanaingiliana kuhusu neno hilo
- Ardent (11 instances)
- Burning (456 instances)
- Eager (70 instances)
- Earnest (42 instances)
- Fervent (12 instances)
- Fiery (69 instances)
- Hot (69 instances)
- Impassioned (3 instances)
- Zeal, Fight, Effectually.
Kwa ujumla maneno hayo yote yanakazia kufanya kazi kwa bidii, kufanya
kazi kwa juhudi,kwa wivu, kwa moto, kwa muwako, kwa shauku, kwa viwango, kwa
ufundi na kwa njia nyingine zozote lakini hakuna lugha ya kueleza vema katika
Kiswahili zaidi ya kukazia bidii na juhudi, au kwa moyo wako wote.
Mfano Biblia inazungumza kumpenda Mungu kwa Moyo wetu wote
1.
Kumbukumbu 6:5 “Nawe
mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa
nguvu zako zote.” Kwa maana nyingine Biblia inataka tumpende Mungu kwa
moyo, kwa roho na kwa nguvu hii maana yake nini kwa bidii
2.
Yakobo 5:16 “Ungameni
dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye
haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.”Kumbe hata katika kuomba Biblia
inatutaka tuombe kwa bidii unaona
3.
Matendo 12:5 “Basi
Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili
yake.” Maombi yaliyomtoa Petro gerezani yalikuwa ni maombi yaliyofanyika
kwa juhudi
4.
Matendo 18:24-25 “Basi
Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika
Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia
ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha
kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.” Apolo
alikuwa hodari yaani alikuwa na juhudi na hata alipoanza kuhubiri alikuwa na
“zeal” yaani alikuwa anawakwa anahubiri kuhusu Yesu kwa nguvu.
5.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa
na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao;”Biblia inatutia Moyo vilevile ikitakam bidii katika kuwa na amani na
watu wote, kumbe kila kitu kinahitaji bidii
6.
Mithali 8:17 “Nawapenda
wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.” Biblia inatia
moyo kwamba tumtafute Mungu kwa bidii, bidii inahitajika katika kila eneo
Kwa msingi huo basi kama kila kitu kitafanyika kwa bidii maana yake
mafanikio ni lazima, ni lazima kila mwanafunzi ajifunze kusoma kwa bidii,
wanaofanya kazi wafanye kwa bidii, “USITAMANI KUTEMBEA IKIWA UNAUWEZO WA
KURUKA” “do not desire to walk when you have wings to fly”
Mfano:
Wakati fulani kulikuwa na Mfalme aliyekuwa mkarimu sana na mwenye moyo
Mzuri, lakini pia alikuwa rafiki wa wanyama na ndege, aliwapenda kiasi ambacho
hakufurahi hata kuona mnyama akichinjwa
Kutokana na ukarimu wake kwa wanyama na ndege siku moja mfanya biashara
mmoja alimpatia zawadi ya mwewe wawili “Falcon” Mfalme alifurahi sana na
kumuomba kiongozi wa wa mifugo kuwatunza mwewe hao wawili na kuhakikisha kuwa wanaishi
kwa fuaha na faraja lakini wakiwa na uwezo na mpaka wawe na uwezo wa kuruka,
kwani walikuwa hawawezi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na wakati wa
ukamatwaji walipunguzwa baadhi ya manyoya ili wasiruke
Baada ya Muda Mfalme alitamani kuwaona
mwewe wale wakiruka, lakini kiongozi wa mifugo alimueleza kuwa ni mwewe mmoja
tu ndiye aliyeweza kuruka kwa kasi na huwa anarejea kwa kasi ya ajabu lakini
mwingine hajawahi kuruka hata siku moja,
Mfalme
alishangaa sana na alitoa zawadi kwa mtunzaji wa mifugo kutokana na kuruka kwa
mwewe wa kwanza, hata hivyo alisisitiza kuwa ni lazima ahakikishe kuwa na mwewe
wa pili anaruka. Lakini hata hivyo mwewe wa pili hakuweza kuruka bali alikaa tu
kwa upole katika tawi la mti na kutulia alijaribu kila mbinu lakini ndege yule
hakuweza kuruka.
Mfalme
alimwambia usisikitike nitaita mtu mmoja atakayeweza kumfanya mwewe aweze
kuruka mfalme alitangaza kama yuko mtu anayeweza kumfanya mwewe yule aweze
kuruka ajitokeze na atapewa zawadi
Baada
ya kusikia tangazo hilo Mzee mmoja wa miaka alijitokeza na kufika ikulu na
kumuhakikishia mfalme kuwa yeye anaweza kumfanya mwewe kuruka, Mfalm,e
alimuagiza mkuu wa wanyama kumchukua Mzee yule na kumpeleka kwenye eneo la
mifugo na ndege na kuifanya hiyo kazi na kuwa yeye atatembelea siku inayofuata
kuona itakavyokua na kama kuna mabadiliko.
Siku
ya pili Mfalme alishangaa sana kuona kweli mwewe ameruka kwa mara ya
kwanza na akaenda mbali sana kwa spidi
ya ajabu na kurejea, Mfalme alifurahi sana na kumpa zawadi mzee yule, kisha akamuuliza
Mzee umewezaje kumfanya ndege huyu kuruka Mzee alicheka na kujibu Nilikata tawi
alilokuwa analitegemea kwa kukaa.
Wengi
wetu tuna mbawa za kurukia, tunajua kuruka na tunajua wapi kwa kurukia lakini
tumekaa bila sababu na hatufanyi lolote na tunabakia duni.
Kila
mmoja anaweza kufanya jambo kwa bidii, kila mwanafunzi anaweza kujisomea kwa
bidii watu wengi na wanafunzi wengi wanao uwezo, wanauwezo wa kupata hata maxi
kubwa zaidi ya hizi wanazozipata lakini kuna mahali wamekaa,
Mithali 10: 4
“Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali
mkono wake aliye na bidii hutajirisha.” Ndugu hakuna muujiza wa
mafanikio unaokuja kwa kuambiwa pokea! Pokea! Mafanikio yoyote yanakuja kwa
kufanya kazi kwa bidii, Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo mkuu wa
wajenzi anawaambia wasomaji wake.
Na
mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni