Mstari
wa Msingi: Warumi
12:4-5 “Kwa kuwa kama vile katika mwili
mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na
sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa
mwenzake.”
Ndege wa ajabu aliyekuwa na vichwa viwili
Utangulizi.
Neno
la Mungu linatufundisha kuwa na ushirika wenye mshikamano wa kipekee kama vile
ulivyo mwili wa mwanadamu,tutakuwa tunafikiri vema na kwa unyenyekevu kama
tutakuwa tunatambua kuwa sisi ni sehemu tu ya huo mwili wa Kristo, yaani sisi
ni kiungo kimojawapo katika mwili wa Kristo, kwa sababu hiyo kila tutendapo
jambo lolote ni muhimu kulitenda kwa kuzingatia na wengine pia, kwa kuzingatia
kuwa hatuko peke yetu, kwa kuzingatia kuwa kila mmoja ni wa muhimu, kwa
kuzingatia kuwa hakuna wa kupuuzwa, hii sio katika kanisa peke yake lakini na
katika ndoa pia na katika mashirika pia, na katika sehemu yoyote ambapo watu
hufanya kazi kwa pamoja kwa kusudi moja kanuni ya kuheshimiana itatusaidia kuwa
na mafanikio makubwa sana na ufanisi.
Kwa mujibu wa Mwana theolojia Gene Getz
wMwandishi wa kitabu kiitwachoi Kujengana, kwa kiingereza (Building Up One
Another [Victor Books, 1976]) anaeleza kuwa Neno kila mmoja na mwenzake
limetajwa katika Agano jipya nje ya Injili mara 58 ili kukazia kujaliaana
kwenye nia ya viwango vya juu sana na ametaja mara 12 neno KILA MTU NA MWENZAKE
LINAVYOJITOKEZA KATIKA AYA KADHAA ZA BIBLIA YA KIYUNANI. Nazinukuu:-
1. Tu
viungo kila mmoja na mwenzake Warumi 12:5
2. Tupendane
kila mmoja na mwenzake Warumi 12:10
3. Tuheshimiana
kila mmoja na mwenzake Warumi 12:10
4. Kunai
mamoja kila mmoja na mwenzake Warumi 15:5
5. Kukaribishana
kila moja na mwenzake Warumi 15:7
6. Kuonyana
kila mmoja na mwenzake Warumi 15:14
7. Kusalimiana
kila mmoja na mwenzake Warumi 16:3-16
8. Tumikianeni
kila mmoja na mwenzake ninyi ni ndugu Wagalatia
5:13
9. Mchukuliane
mizigo kila mmoja na mwenzake Wagalatia 6:2-3
10. Kwa
kuvumilina na kuchukuliana katika upendo kila mmoja na mwenzake Waefeso 4:2-4
11. Kwa
kunyenyekeeana kila mmoja na mwenzake Waefeso 5:11
12. Kwa
kutiana moyo kila mmoja na mwenzake 1Wathesalonike
5:11
Aya
zote hizi hapo juu zinakazia ukweli kwamba Mungu anataka tuwe na ushirikiano
usiokuwa wa kawaida na kwamba ni muhimu kila mmoja akajifunza kuwa mbali na
ubinafsi na kuwajali wengine hasa kama tumeungwa katika imani moja.
Mfano:-
Wakati
fulani katika hali ye kushangaza sana aliwahi kutokea ndege mmoja ambaye
alikuwa na vichwa viwili kimoa kiliangalia kulia na kingine kiliangalia kushoto,
Hata hivyo ndege huyu mwenye mwili mmoja vichwa viwili, vichwa vyao havikuwa na
maelewano mazuri na mara kwa mara waligombana na kubishana, hata kwa mambo
ambayo yalkikuwa rahisi sana ingawa kumbka walikuwa wanamwili mmoja.
Ndege
huyu wa ajabu aliishi katika mti mmoja mkubwa uliokuwa kando ya mto
Siku
moja alipokuwa akiruka kuvuka nga’mbo ya mto kichwa cha kushoto kiliona mti
mzuri sana uliokuwa na tunda zuri, kichwa cha kushoto kilitamani kula tunda
lile na hivyo alitua kwaajili ya kula tunda kichwa cha kushoto kilikula tunda
hilo ambalo lilikuwa linanukia vizuri sana, wakati kicha cha kushoto kinakula
kichwa cha kulia kiliuliza ndugu unaweza kuniachia na mimi nijaribu ladha la
hilo tunda?
Kichwa
cha kushoto kikajibu “ Ndugu una wasiwasi gani tuna tumo moja tu kwa hiyo hata
kama mimi nitakula kwa mdomo wangu vitaelekea kwenye tumbo letu tu” “ lakini
nataka kuonja tu utamu wa hilo tunda tafadhali naomba na mimi” kilijibu kichwa
cha kulia.
Kichwa
cha kushoto kilijibu kwa kupuuzia bwana ee tuna tumbo moja tu kwa hiyo hata
nikila mimi vitaelekea kwenye tumbo letu nina haki nya kula hata bila
kukushirikisha kikala chenyewe!
Kichwa
cha kulia kilijisikia vibaya na kikanyamaza kimya.
Siku chache
baadaye wakati ndege alipokuwa katika safari zake kichwa cha kulia kiliona tuna
la rangi ya manjano katika mojawapo ya mti hivyo ndege alitua na kujaribu
kulichuma tunda hilo
Ndege wengine
wanaoishi karibu na mti huo walisema kwa sauti USILE USILE tafadhali tunda hilo
lina sumu kali litakuua.
Kichwa cha kushoto
kiliposikia kiasema USILE, USILE Bwana!
Hata hivyo kichwa
cha kulia hakikusikiliza yanayosemwa na kichwa cha kushoto, Kichwa cha kulia
kilijibu kuwa Nina haki ya kula hata bila kukushirikisha kwa hiyo huna haki ya
kunizuia
Kichwa cha kushoto
kilipiga kelele tafadhali usile tutakufaa!
Kichwa cha kulia
kilijibu kwa kuwa nimeliona nina haki ya kula bila kukushirikisha, kichwa cha
kulia kilikuwa kinalipa kisasi kwa kichwa cha kushoto kutokaa na choyo chake
dhidi ya lile tunda la kwanza
Hatimaye kichwa
cha kulia kilikula lile tunda lenye sumu na baada ya sekunde chache ndege huyu
wa ajabu mwenye vichwa viwili alifariki dunia.
Ndugu zangu hakuna
sumu kali, kama mafarakano, mafarakano katika taifa, katikafamilia, katika
mashirika, katika kazi, katika kanisa, katika misikiti yanaharibu ustawi na
maendeleo ya kila mmoja wetu
Ni muhimu
kuzingatia kama mafundisho ya biblia yanavyokazia umoja na mshikamano sisi nasi
tukaendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kila Nyanja ya maisha yetu,
tusikubali watu wakatugawanga, tusikubalia mafarakanano ya sisi kwa sisi ni
sumu na itaua na kuharibu umoja na mshikamano na ustawi wetu, kiungo kimoja
kikiumia vyote huumia hivyo kama sisi ni mwili mmoja basi tuheshimiane.
.
Na mkuu wa wajenzi
mwenye Hekima.
Rev. Innocent
Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni