A. Mwandishi wa Kitabu cha Habakuki
-
Aliyeandika kitabu hiki
anajitambulisha kama Nabii Habakuk i(1:1
; 3: 1). Hakuna maelezo mengine ya ziada kuhusu maisha ya binafsi au ya
familia ya huyu mwandishi yaliyopo po pote katika Maandiko. Alikuwa nabii wa
Yuda na inajulikana kutokana na zaburi yake (sura ya tatu) na kwenye maelekezo kwa mkuu wa waimbaji (3:19) kwamba alikuwa wa kabila la
Lawi, mmoja wa waimbaji wa hekaluni. Habakuki maana yake “Kumbatia”
-
.Kitabu cha Habakuki kimeandikwa
kwa mtindo wa mazungumzo kati ya Mungu na Nabii.
-
Habakuki aliona
kwamba viongozi wa Yuda walikuwa wanawaonea maskini, kwa hiyo aliuliza swali
kwamba ni kwa nini Mungu anawaruhusu watu hawa waovu kustawi.
-
Mungu
alipomwambia kwamba Wakaldayo wangekuja kuwaadhibu Yuda, Habakuki aliumia
zaidi. Hakuelewa ni kwa jinsi gani Mungu angeweza kuwatumia Wakaldayo ambao
walikuwa waovu kuliko Wayahudi waovu, ili kutekeleza hukumu dhidi ya watu
walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu. Jibu la Mungu lilikuwa kwamba wenye haki wangeishi kwa imani kwa
Mungu na kwamba walikuwa na uhakika kwamba Mungu alikuwa anafanya lililo
sahihi. Mungu alimwambia Habakuki kwamba punde si punde Wakaldayo wangehukumiwa
na kwamba hatimaye haki ingeshinda kwa ajili ya watu wa Mungu. Habakuki
anamalizia kitabu kwa zaburi ya sifa.
-
Mungu anavyotumia
waovu kuadhibu watu wake wanapotenda uovu kwa nia ya kuwarudisha ili wamrudie,
lakini hao waovu wakiisha kutimiza kusudi la Mungu, wao huadhibiwa zaidi.
-
Yuda walitenda
dhambi ikiwa ni pamoja na kuabudu sanamu, lakini Mungu anatumia Wakaldayo walio
waovu zaidi kuwaadhibu na hatimaye Mungu anawaadhibu Wakaldayo.
-
Ilimshangaza Habakuki kuona waovu wakistawi
huku wakiendelea kutenda dhambi nyingi wala Mungu hawaadhibu upesi! Habakuki
anaelezea imani yake katika mamlaka ya Mungu na katika uhakika kwamba Mungu ana
haki katika njia Zake zote.
-
Ufunuo wa Mungu kwa wenye haki na nia Yake ya
kuiangamiza Babeli iliyokuwa ovu iliamsha wimbo wa sifa wa kinabii na ahadi
kuhusuwokovu katika Sayuni (3:1-19)
C.
Kusudi
-
Kuonyesha kwamba
bado Mungu anaitawala dunia hata kama tunaona kwamba uovu unashamiri na ya
kwamba iko siku Mungu atauhukumu na kuadhibu huo uovu hatimye kuuangamiza
kabisa usiwepo tena.
D.
Wahusika Wakuu
-
Habakuki,
Wababeli.
E.
Tarehe
-
Kitabu hiki
hakikuwekewa tarehe, lakini bila shaka kilikuwa kipindi cha Wakaldayo.
-
1.Hekalu bado limesimama (2 :20) na huduma ya
uimbaji inafanyika (3 :19),
-
2. Kuinuka kwa
Wakaldayo kuwa dola inayotisha miongoni mwa mataifa kunatokea wakati wa kizazi
hicho (1 :5,6) na kuchinjwa kwa
mataifa na Wakaldayo tayari kulishaanza
-
(1 :6,7).Wakaldayo walijulikana
na Wayahudi muda mrefu kwa kuyashinda mataifa mengine hadi kuongoza katika dola
za ulimwengu wakati wa kuanguka kwa Ninawi 612 K.K. au 606 K.K. na kwa ushindi
wao juu ya Wamisri huko Kerkemishi mwaka 605 K.K.
F.
Mgawanyo
-
Swali la Habakuki
na jibu la Mungu. (1 :1-11)
-
Swali la pili la
Habakuki na jibu la Mungu. (1 :12-2 :20)
-
Maombi ya
Habakuki. (3 :1-19)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni