HAGGAI:
MTIA MOYO WA UJENZI WA HEKALU
A.
Mwandishi
-
Hagai ni moja ya vitabu vitatu
vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya uhamisho ambavyo ni
Hagai, Zekaria na Malaki.
-
Hagai anatajwa kwa jina mara
mbili katika kitabu cha Ezra (Ezr
5:1,6:14) kama “mjumbe wa Bwana” (1:
13). Inawezekana alikuwa mmoja wa wale waliorudi kutoka uhamishoni
waliorudi Yerusalemu, walioweza kulikumbuka hekalu la Solomoni lilivyokuwa
kabla halijaharibiwa na majeshi ya Nebukadneza mwaka 586 K.K. (2:3). Hagai na Zekaria ndio
waliowatia moyo wale watu waliorudi kutoka uhamishoni kujenga upya hekalu.
-
Ilikuwa ni mnamo
mwaka 538 K.K., miaka kumi na minane ilikuwa imepita tangu Dario alipopitisha
amri kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni. Watu walikuwa
bado wanashughulika kujenga nyumba zao, hivyo ujenzi wa hekalu la Mungu ulikuwa
bado haujakamilika.
-
Kundi la kwanza la Wayahudi
lililorudi Yerusalemu liliweka msingi wa hekalu jipya.mnamo mwaka 536
K.K.wakiwa na furaha na matumaini makubwa (Ezr 3:8-10).
-
Hata hivyo Wasamaria na
majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa
wafanya kazi hata ikafanya ujenzi huo usimame mwaka 534 K.K..
-
Watu waliacha ujenzi wa
hekalu, wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Ujumbe wa Hagai ulikuwa kwamba
ni wakati wa kujenga nyumba ya Mungu. Hagai akiwa amefuatana na Zekaria
(taz.utangulizi wa kitabu cha Zekaria), yeye alianza kumhimiza Zerubabeli na
watu wote kuanza tena kujenga nyumba ya BWANA. Chini ya uongozi wa Zerubabeli
mtawala na Yoshua kuhani mkuu na kule kuhimiza kwa Nabii Hagai hekalu
lilijengwa mnamo 520 K.K. Miaka minane baadaye hekalu lilimalizika kujengwa na
kuwekwa wakfu (ling.Ezr 4-6).
B.
Kiini cha ujumbe wa Haggai
- Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu Wake ndani yake.
-
Kuwahimiza watu
kujenga upya hekalu la BWANA na kuwahamasiaha kuyatengeneza maisha yao upya na
Mungu ili waweze kupata baraka Zake.
C.
Historia ya nyuma ya mambo
-
Hekalu la
Yerusalemu lilibomolewa mnamo mwaka 586 K.K. Mwaka wa 538 K.K,
-
Mfalme Koreshi wa
Uajemi alitoa amri Wayahudi warudi ili kujenga upya mji wa Yerusalemu na
hekalu.Mwaka 536 K.K.walianza kujenga hekalu lakini ilikuwa vigumu kumalizia
kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwa Wasamaria na mataifa ya jirani.
-
Kupitia huduma ya
Hagai Zekaria na Yoshua, mwaka 520 K.K., walianza kujenga tena hekalu.Miaka
minane baadaye kazi hiyo ya ujenzi wa hekalu ilimalizika.
Mabaki
ya ikulu ya Mfalme Dario Mmedi /Mmuajemi ni katika utawala wake ndipo Nabii
Haggai aliandika kitabu chake cha kuhamasisha ujenzi wa Nyumba ya bwana makazi
haya ya iliyokuwa ikulu yako mahali paitwapo Persepolis Nyakati za Leo Picha na
maelezo kwa hisani ya Maktaba ya mwalimu Innocent KamoteMchungaji.
D.
Tarehe ya uandishi
-
Tarehe ya
kuandikwa kwa kitabu kwa hiki ni ya uhakika, yaani, mwaka wa pili wa Mfalme
Dario wa Uajemi (mwaka 520 K.K. (1:1).
-
Mpangilio wa
kihistoria ni wa muhimu sana ili kuuelewa ujumbe wa kitabu hiki. Mnamo mwaka
538 K.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi alitoa amri ikiwaruhusu Wayahudi waaliokuwa
uhamishoni kurudi nchini mwao ili kuujenga upya Yerusalemu na hekalu katika
kutimiza unabii wa Isaya na wa Yeremia (Isa45:1,3; Yer 25:11-12; 29:10-14) na
maombezi ya Danieli (Dan 9).
E.
Wahusika Wakuu
-
Hagai, Zerubabel,
Yoshua.
F.
Mgawanyo
-
Wito wa kujenga
hekalu. (1:1-15)
-
Matumaini ya
hekalu jipya. (2:1-9)
-
Baraka
zilizoahidiwa. (2:10-19)
-
Ushindi wa mwisho
wa Mungu. (2:20-23)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni