Nabii wa Kuanguka kwa Ninawi yaani Ashuru (Syria)
Hali ya Syria leo!
Mwandishi wa kitabu cha Nahumu
-
Nahumu maana yake ni mwenye kufariji
-
Hakuna linalofahamika kuhusu wazazi wake au
historia yake wala mafunzo yake lakini ukweli unabaki kuwa kwa kuwa ujumbe wake
unahusu hukumu ni wazi kuwa ulitolewa
wakati mfupi kabla ya Uamsho mkubwa
uliokuja wakati wa Yosia 627-621
-
Nahumu anajulikana kama Nabii wa kisasi au Nabii wa
kuanguka kwa Ninawi kinakisiwa kuwa
kiliandikwa 621 K.K. katika mwaka wa 18
wa Yosia mfalme wa Yuda na kabla ya anguko la Ninawi la mwaka 612 K.K
-
Nahumu anajiita mwekloshi 1;1 na Ekloshi yenyewe Haijulikani
iko upane gani ila kuna wanaodhani kuwa
ni kijiji kidogo mashariki ya mto Tigrisi sio mbali kutoka Ninawi na
wengine wanafikiri kuwa ni kijiji kidogo huko Galilaya karibu na Kapernaumu
jina Kapernaumu maana yake ni kijiji cha Nahumu
B.
Kiini cha kitabu
-
Kiini cha ujumbe wa kitabu hiki ni anguko la Ninawi
katika Septuagint kitabu hiki kimewekwa mara tu baada ya kitabu cha Yona ikifikiriwa kuwa ni ukamilisho wa kitabu cha
Yona
C.
Historia ya nyuma ya mambo
-
Ninawi ulikuwa ni mji mkuu wa waashuru
-
Kwa karne nyingi waashuru waliwaonea sana watu wa
mashariki ya kati na kumuka ukatili waliokuwa nao katika kitabu cha Yona na
angalia Isaya 37
-
Lakini kwa huruma zake Mungu alimtumia Yona Ninawi
na watu walitubu na kuokolewa hata hivyo baada ya Muda watu walirudi katika
njia zao za uovu vilevile
D.
Mistari ya msingi
-
1;3 -
Bwana si mwepesi wa hasira lakini ana nguvu
-
2;13 – Niko kinyume nawe asema Bwana
-
1;7 – Bwana ni mwema kimbilio wakati wa Taabu
-
1;15 – Angalia huko milimani miguu yake yeye
aletaye habari njema
E.
Uchanganuzi
-
Hasira ya Bwana 1;1-8 Kuna Maneno sita ya nguvu
katika Nahumu yanayoelezea hisia za
Mungu na majibu yake kwa waninawi Wivu,
Kisasi, Hasira, Ukali, Ghadhabu, Kumwagwa
Nahumu 1;6. Ingawa nahumu amesema wazi kuwa mungu ni mwingi wa huruma
1;7 na hivyo rehema zake na upendo wake humfanya asihukumu kwa haraka dhidi yao
wamtendao mabaya lakini wakati unakuja
ambapo hulazimika kuadhibu maovu
-
Hasira ya Mungu ni Tofauti na ya wanadamu ya
wanadamu huchanganyika chuki kwa waliomuuzi na mwanadamu hawezi kujizuia katika
hasira yake yenye ubinafsi, Hasira ya
mungu haina haraka wala ubinafsi, au
isiyozuilika kama ya wanadamu 1;3, haki yake na kisasi chake kiko katika kanini
ya kupenda na kuvuna wanadamu na mataifa yote yatavuna kile walichokipanda.
-
Wivu wa mungu ni wa haki unasukumwa na upendo wake
kwa watu na unakusudia kuwalinda kutoka
kwao wanapojaribu kuwapeleka watu wake mbali na yeye na furaha aliyoikusudia
kwao kumbuka alivyomwambia “Sauli Mbaona waniudhi”
-
Kabla ya hasira za mungu milima ilitetemeka na vilima viliyeyuka na nchi ilitetemeka 1;6
F.
Upekee wa kitabu cha Nahumu na ujumbe wake
-
Nahumu ndiye Nabii pekee anayeuita ujumbe wake
kitabu 1;1
-
Nahumu kama Yona na Obadia wanashughulika na mataifa adui
waliozionea Israel na Yuda
-
Yona aliwahubiri waninawi huko ninawi lakini Nahumu
aliizungumzia Ninawi kwa Yuda hivyo ujumbe wake ulikuwa ni faraja kwa Yuda juu
ya ukombozi toka kwa adui zao na watesi wao na hakuna mashitaka kuhusu yuda
wala wito wa toba
-
Nahumu kinasisitiza Anguko la Ninawi na kinakazia
juu ya Hasira takatifu ya Mungu dhidi ya dhambi
-
Kumbuka kuwa ujumbe wa Ninawi kwa Yuda haukutokana
na chuki binafsi za Nahumu kwa adui zao Lakini mungu alimpa ili kuthibitisha
agano lake dhidi ya Yuda na kuwakumbusha kuwa Mungu atawapigania dhidi ya adui zao
Kumbukumbu 28;1,7.
G.
Mgawanyo
-
1 Anguko la
Ninawi linatangazwa sura ya 11;1-15
-
2 Anguko la Ninawi lina changanuliwa sura ya 2;1-13
-
3 Anguko la ninawi
linathibitishwa Sura ya 3;1-19
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni